Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104762 articles
Browse latest View live

Aina 10 ya Wanawake Wanaopendwa na Wanaume

$
0
0


1. WENYE MSIMAMO

Wanawake daraja la kwanza wanaopendwa zaidi na wanaume ni wale wenye msimamo, uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, wako makini kwenye matendo yao na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio.

2. WAPENDA USAWA

Aina ya pili inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi ni wanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu ya kifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamii kwa asilimia 50 kwa 50.

3. WANAOJUA MAPENZI

Wanawake wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa ni uwezo wa kutosheleza katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonyesha kuwa wanaume hupenda sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwa sita. Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaume bila kujali sifa zao za nje au za ndani.

4. MARAFIKI

Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume. Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida na raha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, waungwana na wapenda amani.

5. WA WAZI

Aina nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo na uwazi. Si wepesi wa kuburuzwa katika maamuzi ya msingi kwa kisingizio cha wao ni wanawake. Utafiti unaonesha wanawake wa aina hii wamekuwa muhimu hasa kwa wanaume wenye tabia za ubabe na udhaifu katika uelewa wa mambo.

6. WANAOJITEGEMEA 

Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina naomba vocha kila siku. Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wa leo hawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza starehe za upande mmoja.

7. WASIO NA PRESHA

Nikisema wanawake wasiokuwa na presha namaanisha wasiolazimisha vitu vitokee haraka haraka. Wao siku zote huacha mambo yatokee yenyewe na kazi yao kuwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi.

8. MARIDADI 

Kundi lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafi na kujiremba. Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje. Lakini pia ni welewa wa mazingira, si wasamba. Wanapendeza kwa muonekano.

9. WANAORIDHIKA

Wanawake ambao hulidhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwa wanaume, hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzi kwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutoka juu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke.

10. WA MMOJA

Wanawake wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kila aina ya vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziada zaidi ya waliowachagua mwanzo wanahitajika sana. “Niliye naye ananitosheleza kwa kila kitu sitaki mtu mwingine.” Kundi la wanawake wa aina hii ni adimu na muhimu sana.


Fahamu Namna ya Kuishi na Mpenzi Anayependa Fedha

$
0
0


HAPA tunazungumza kuhusu mapenzi kama kawaida yetu. Leo nimekuja na mada ambayo naamini itawagusa wengi. Marafiki zangu, kusaidia katika mapenzi ni jambo zuri tena lenye mantiki sana.
Suala la kusaidiana si la upande mmoja. Linaweza kuwa kwa wote, kwa mwanaume au mwanamke. Ni kati ya nguzo muhimu katika mapenzi, lakini kwa bahati mbaya kuna wale ambao
wamekuwa na tabia ya kupenda sana fedha!

Unajua wenzi wanajuana kulingana na wanavyoishi, hivyo ni rahisi sana kumgundua mwenzako kama anapenda sana fedha au ni kweli ana tatizo linalohitaji msaada wako. Hii ni kasoro, lakini haimaanishi kwamba ndiyo sababu ya kuachana.

Katika mada hii ipo dawa ya namna ya kudumu katika mapenzi motomoto na mwenzi wa aina hii. Imekuwa ni kawaida kumsikia msichana akitamba mbele ya wasichana wenzake kwa kusema: “Mimi nina kibuzi changu bwana kila ninachotaka kinanipa, kinajua kisiponipa nakitosa tu, yaani nakichuna kama sina akili nzuri.”

Umewahi kukutana na maneno ya aina hii? Bila shaka jibu ni ndiyo. Si hivyo tu, wapo wanaume pia ambao ni kero kwa wapenzi wao, yaani wamegeuka wanaume kama mabinti kwa tabia zao za kutegemea kupewa kila kitu na wapenzi wao hata kama wanao uwezo wa kuvipata vitu hivyo kama watajishughulisha.

Ninachotaka kusema leo ni kwamba, mapenzi ya kweli hayana uhusiano wowote na fedha, ukiona mpenzi wako anaweka fedha mbele na ukishindwa kumpatilizia anachokitaka anakasirika, jua penzi lake lina walakini, hakupendi bali anataka kukutumia kisha kukuacha.

Katika mapenzi hatukatai suala la kusaidiana, mpenzi wako akiwa na shida fulani akaomba umsaidie, kama unao uwezo msaidie na kama huna mueleze ukweli kisha muangalie namna nyingine ya kumsaidia.

Itakuwa siyo busara kama utakuwa na tatizo lakini ukaona kwamba ukimweleza mpenzi wako ataona unamchuna. Wapenzi wanaopendana kwa dhati hawachunani bali wanasaidiana na hili ni kwa pande zote mbili.

Kinachokera ni kutoishiwa na matatizo na wakati mwingine unakuta kuchuna kwingine ni kwa mambo ya starehe. Yaani sasa hivi umemuomba mpenzi wako vocha, hajakaa vizuri umemtaka akija akuletee chipsi mayai, baadaye unataka akutoe ‘out’, bila kujali kwamba wakati huo mpenzi wako ana fedha au laah.

Katika mazingira hayo unadhani mpenzi wako atashindwa kukuchoka? Akikuacha kwa sababu hiyo utamlaumu? Kimsingi ukiwa na mpenzi mwenye tabia ya kutaka kukuomba fedha kila wakati tena katika matumizi mengine ambayo siyo ya msingi, mbinu zifuatazo ni muhimu kuzifuata. Twende tukaone.

MWELEZE UKWELI

Kama huna fedha wakati mpenzi wako anakuomba, mueleze wazi kuwa huna na kamwe usijaribu kutoa ahadi ambazo huenda ukashindwa kuzitimiza. Usiwe mtu wa kutoa ahadi za uongo, mara nitakununulia hiki na kile.
Mwanaume hatakiwi afahamike siku ana fedha au hana. Maana kuna wenzangu ambao siku za mishahara wanabadilisha hadi kutembea! Mwanamke akijua hilo naye ataongeza ‘mizinga’ ili afaidi.

JENGENI KUSAIDIANA
Jambo la muhimu ambalo wanaume wengi wanalisahau ni kutokuwafundisha wapenzi wao wajibu wa kutoa. Utakuta kila kitu ananunua yeye, hata nauli ya basi analipa, wakati mpenzi wake ana kazi yake.
Ifike wakati kwa makusudi, mwanaume ampe majukumu ya kufanya mpenzi wake, hiyo itamsaidia mwanamke kujua namna fedha zinavyokuwa hazitoshi na ataweza kubana matumizi.

ACHA UFUJALI
Kuna wanaume wengine tangu wanatongoza wanakuwa ni wafujaji wakubwa wa fedha kwa kutoa ofa na zawadi kibao. Hii inaweza kumjengea imani mpenzi wako kuwa unazo!

Unachotakiwa ni kudhibiti mapema matumizi yako hata kama fedha itakuwepo. Ifahamike kuwa kutoa hakushibishi uhitaji, kadiri unavyotoa ndivyo unavyoongeza mahitaji. Weka maisha yako katikati usijidai tajiri kumbe ni kapuku tu.

BAKI NA HILI
Katika kumalizia niseme tu kwamba, mapenzi si kukomoana, bali kusaidiana. Jenga tabia ya kumsaidia mwenzako ili siku na wewe ukiwa na tatizo akusaidie.

Kitu unachotakiwa kukiepuka ni kuwa tegemezi hadi unakuwa kero. Kumbuka kumpiga mizinga mpenzi wako kila mara kunapunguza mapenzi hivyo epukana na tabia hiyo.

Haya Ndiyo Mambo Yanayoweza Kukuvunjia Heshima

$
0
0

HAKUNA kitu kibaya maishani kama kuonekana upo katika daraja la chini na mtu wa kudharaulika kwenye jamii unayoishi. Kisaikolojia kuna madhara makubwa.

Ni imani yangu kuwa kila mwanadamu timamu anapenda kuheshimiwa lakini wengi wetu tunashindwa kupata heshima tunayoitaka kwa sababu hatufahamu jinsi ya kuishi mbele ya wenzetu.

Kitaalamu, hakuna jambo ambalo hutokea maishani bila sababu maalumu hivyo hata kudharauliwa kwako au kwetu ndani ya jamii tunayoishi kunatokana na jinsi tunavyoenenda.

Mwalimu wangu wa somo la maisha na saikolojia, Eric Shigongo, aliwahi kuniambia ‘Nothing happens in the sky, but the elements should be there,’  akimaanisha kuwa hakuna kitokeacho angani pasipo kuwa na dalili au sababu zake.

Naomba nianze kutoa njia za kukusaidia kurejesha heshima yako kwa kuperuzi na wewe baadhi ya dokezo muhimu zinazoweza kukusaidia kujitambua na kuweza kuyaepuka maisha ya kudharauliwa.

MUONEKANO
Kwanza kabisa ni jinsi unavyoonekana. Muonekano ninaouzungumzia hapa ni usafi wa mavazi na mwili kwa ujumla. Hata siku moja hakuna mchafu anayeheshimika katika jamii anayoishi hata kama ana kipaji kikubwa kiasi gani.
Kwa hiyo uchafu wa mavazi na mwili huchangia mtu kudharauliwa katika jamii anayoishi. Linaweza kuwa jambo dogo sana lakini ni moja kati ya sababu kubwa inayochangia kuporomoka kwa thamani yako mbele ya wenzako.

Mazungumzo
Hapa naomba nieleweke kuwa unachokizungumza kinaweza kukujengea heshima au kukubomolea heshima. Kauli zisizo na busara zitakufanya udharaulike kwa kila mtu. Uropokaji usiokuwa na mantiki huchangia kuporomosha heshima yako hasa kama utakuwa muongeaji zaidi. Biblia inasema penye wingi wa maneno hapakosi uovu.

UTENDAKAZI WAKO
Ndugu zangu, siku zote heshima ya mtu ni kazi. Watu wengi hawapendi kufanya kazi kwa bidii huku wengine wakijiendekeza kwa tabia ya kuombaomba, jambo hilo halifai kwa vile huchangia kubomoa heshima yako mbele ya jamii. Fanya kazi usiishi bila kujishughulisha.

KUTOTIMIZA AHADI
Kama una tabia za kuahidi mambo halafu unashindwa kuyatekeleza, basi unajiweka katika nafasi mbaya ya kutunza heshima yako katika jamii unayoishi. Bora ukwepe kutoa ahadi kuliko kuahidi na kutotimiza.

SIFA ZISIZO NA MAANA
Nakumbuka msemo mmoja kutoka kwa mwandishi mwandamizi aliyekuwa mtaalamu wa falsafa za maisha, marehemu Adolf Balingilaki, ambao unasema kwamba:

“Ukitafuta heshima kwa gharama ya juu, basi utalipwa dharau kwa bei nafuu.”
Msemo huu unamaanisha nini? Siku zote ukiwa unafanya mambo yako kwa ajili ya kusifiwa au mazungumzo yako kuwa ya kujiinua, watu watakudharau.

KUTOKUWA MWAMINIFU
Suala la uaminifu ni pana, kuna uaminifu wa fedha, siri, dhamana na mambo kama hayo, hivyo ni vema kila unachoaminiwa lazima ukitunze kwani ukiwa mtu wa kuvunja uaminifu fahamu kuwa utashusha heshima yako.

Lwandamina Aikimbia Yanga..Aondoka Bila Kuaga

$
0
0
KOCHA Mzambia, George Lwandamina ameondoka leo kwenda Zambia na habari zinasema anarejea Zesco United ya kwao na atatambulishwa Alhamisi.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amsema leo kwamba Lwandamina hajatokea mazoezini leo asubuhi bila sababu na wanamtafuta hapatikani.

“Mimi sijui kaenda wapi, kwa sababu hajaniaga. Hizo hizo habari (za kwenda Zambia) wewe ndiyo unaniambia,”amesema Mkwasa baada ya kuulizwa na Bin Zubeiry Sports – Online juu ya kocha huyo kurejea kwao, Zambia.

Habari zinasema kwamba Zesco United imeamua kumrejesha kocha wake huyo baada ya mafanikio yake Tanzania ndani ya miaka miwili, akiiwezesha kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita na sasa inakaeribia kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga SC imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kwenda hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wolaita Ditcha ya Ethiopia katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kuingia hatua hiyo Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ushindi huo uliotokana na mabao ya Raphael Daudi kipindi cha kwanza na Emmanuel Martin kipindi cha pili, unamaanisha Yanga SC watahitaji kwenda kulazimisha sare ugenini wiki ijayo, au kutofungwa zaidi ya tofauti ya bao moja ili kwenda hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho kwa mara ya pili baada ya mwaka 2016.

Na Lwandamina ambaye mkataba wake unamalizika Juni mwaka huu, anaondoka Yanga siku moja kabla ya kuteremka uwanjani kumenyana na Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Lwandamina alijiunga na Yanga Novemba mwaka 2016 akichukua nafasi ya Mholanzi, Hans van der Pluijm na katika kipindi hicho ameiongoza timu katika michezo 77 ya mashindano yote akitoa sare 18, kushinda 45 kati ya hizo mbili kwa penalti baada ya sare ndani ya muda wa kawaida na kufungwa 14, tano kwa penalti baada ya sare katika muda wa kawaida.

Punguza Unene Unaokusumbua Katika Mwili Kwa Kutumia Bidhaa za Edmark

$
0
0
Tumia Dawa za Edmark za Kupunguza uzito uliozidi Mwilini Mwako, Edmark ni Vurutubisho na Chakula Mbadala na Zimehakikiwa na TFDA...

Ni uhakika kwa afya yako,👉 kupunguza uzito na sumu mwilini, Mafuta Sehemu Mbaya, Kitambi na nyama uzembe na kutibu MAGONJWA Mbalimbali kwa msaada wako mfuate instagram: @afyayanguutajiriwangu @afyayanguutajiriwangu


Au Mtafute WhatsApp Huyu Dada kwa kutumia Namba +255783 566844

Pia Dawa za Edmark Zinaweza kupa Fursa ya Biashara Uweze pata Kipato Kirahisi kwa Kuwasaidia watu Kuimarisha Afya zao

Nape Aliamsha Dude..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya April 11

$
0
0


Nape Aliamsha Dude..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya April 11

Dada Amtaja Edward Lowassa Kumtelekeza...... Mtoto Mkubwa wa Lowassa Apangua Hoja

$
0
0
Mtoto mkubwa wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Fred Lowassa, ameshangaa mwanamke aliyejitokeza na kudai kuwa ni binti wa mwanasiasa huyo.

Aidha, amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutumia vizuri mamlaka yake.

Kauli hiyo ya Fred imekuja  baada ya mwanamke mmoja mkazi wa Kigamboni, Fatuma Lowassa (31), kujitokeza katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, jana Jumanne Aprili 10, akidai kutelekezwa na baba yake ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.

Akiwa Monduli mkoani Arusha, Fred ametoa tamko akisema; “Nimesikia mwanamama mmoja akiongea kuwa yeye ni ndugu yetu kule Dar es Salaam.

“Kwa taarifa tu sisi watu wa Monduli kwetu watoto ni baraka na neema, nimeshangaa ametukosa ukoo mzima kujitambulisha.

“Namwambia Paul Makonda, nimetoka naye mbali sana, nasikitika sana anavyotumia nafasi yake vibaya kwa manufaa anayoyajua. Makonda nimekulea.” Ameandika Fred.

Mwanamke huyo amejitokeza jana katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ikiwa ni mwendelezo wa Makonda kuonana na wanawake waliotelekezwa na watoto na waume zao.

Mwanamke huyo amesema yuko tayari kupima kipimo cha DNA na Lowasa kuthibitisha kama kweli ni baba yake huku akijinasibu kumtafuta baba yake huyo kwa muda mrefu bila mafanikio.

“Nilipeleka barua Ikulu kuomba kuonana na baba kipindi akiwa Waziri Mkuu lakini niliitwa mimi na mama katika Klabu ya Mamba iliyopo Kinondoni, alikuja mwanamume akiwa kwenye gari lenye ‘tinted’ akatuhoji mimi na mama akaondoka hakutupa majibu yoyote hadi leo,” amesema Fatuma.

Aidha, amesema aliwahi kukutana na Fred na akamuahidi kumsaidia lakini hadi sasa amekuwa kimya


VIDEO:

SOMA PIA:Job Opportunity at East African Community, Internal Auditor

Waziri azungumzia maandamano ya Mange Kimambi bungeni

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama amefunguka na kutoa ushauri kuhusu suala la maandamano na kusema kuwa mtu yoyote ambaye ana ratibu maandamano lazima afuate sheria hata kama maandamano yanatambulika kikatiba.

Jenista Mhagama amesema hayo bungeni na kudai kama kila mtu ataamua kuandamana kwa kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaruhusu hilo litakuwa jambo ambalo si sawa hivyo amevitaka vyama vya siasa kufuata sheria za nchi na si kuvunja sheria za nchi.

"Suala la maandamano katika nchi yetu ya Tanzania linaratibiwa na sheria za usalama ndani ya nchi chini ya vyombo vya usalama hasa polisi na Katiba haiwezi kuchukuliwa kwamba ni kigezo cha kuviruhusu vyama kufanya maandamano bila kuzingatia taratibu na sheria zilizowekwa.

"Ninaomba sana Watanzania wote na niviombe vyama vyote vya siasa katika nchi yetu ya Tanzania wahakikishe wanazingatia sheria. 

"Katiba yetu imeruhusu maandamano lakini maandamano yameratibiwa kisheria na kama yameratibiwa kisheria lazima tuhakikishe kwamba tunazingatia sheria katika kuratibu maandamano nchini kwetu Tanzania"

Jenista Mhagama aliendelea kutoa maelezo kuhusu masuala ya maandamano

"Labda niulize swali moja tukiamka hapa siku moja asubuhi na kila mtu ameamua kuandamana wakulima, wafanyakazi yaani kila mtu aamue tu kuandamana kwa sababu tu Katiba imesema nadhani itakuwa siyo sawa na nichukue nafasi hii kuviomba vyama vya siasa kuheshimu Katiba na sheria katika kutekeleza wajibu wao na siyo kuvunja sheria za nchi yetu Tanzania"

SOMA PIA:  Job Opportunity at East African Community, Security Officer

Naibu Waziri wa Afya amkosoa RC Makonda sakata la wanawake waliotelekezwa

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile amekemea udhalilishwaji wa watoto ‘waliotelekezwa’ na baba zao ambao tangu jana picha zao zimekuwa zikisambazwa katika mitandao ya kijamii baada ya kufika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakiwa na mama zao.

Tangu jana wanawake waliotelekezwa na waume zao wamefika katika ofisi hizo zilizopo Ilala jijini hapa, kuanza kusikilizwa.

Katika ujumbe aliouandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter akijibu maoni ya wachangiaji, Dk Ndugulile alivionya vyombo vya habari kwa kushiriki kuonyesha picha za watoto katika mikusanyiko hiyo, huku akitaka utaratibu ufuatwe katika kusikiliza mashauri ya walalamikaji ikiwa ni pamoja na usiri.

“Ni kosa kisheria kwa chombo cha habari au mitandao ya jamii kuonyesha picha zenye kumdhalilisha mtoto kwa mujibu wa sheria ya mtoto Namba 21 ya 2009. Navikumbusha vyombo vya habari kulinda haki za watoto na kutokuwa washirika katika kudhalilisha haki za watoto,” alisema Dk Ndugulile kupitia ujumbe wa Twitter.

“Ushauri wangu kama Wizara inayosimamia haki za watoto, suala kama hili linapaswa kufanyika kwa faragha, kwa sababu una deal na watu na litakuwa endelevu,” amesema Dk Ndugulile.

“Anachokifanya Makonda ni jambo zuri, lakini linahitaji uangalifu na tufuate mifumo sahihi. Nitoe rai kwa wananchi wote kufuata taasisi zinazohusika.”

Alipoulizwa sababu ya wananchi wengi kujitokeza kwa mkuu wa mkoa kama ishara ya kuzidiwa kwa idara ya Ustawi wa Jamii, Dk Ndugulile alikanusha ,

“Si kwamba Ustawi wa Jamii umezidiwa, inawezekana wananchi hawana taarifa za kutosha kwa hiyo kupitia mikutano kama hiyo watapata taarifa. Tufuate mifumo rasmi inayokubalika kisheria,” amesema.

SOMA PIA:  4 Job Opportunities at IMA World Health (IMA)

Vijue vyakula ambavyo wanaume hawapaswi kula mara kwa mara

$
0
0
Watalamu mbalimbali wa masula ya afya wameeleza ya kwamba ipo haja kubwa sana kwa wanaume kuacha kula baadhi ya vyakula ili kuweza kuyazuia madhara ambayo nimeyaeleza katika Makala haya, kwani endapo utaendekeza kula vyakula vya aina hii, kuna uwezekano mkubwa afya yako kuwa matatani.

1.Chumvi ya mezani
Chumvi ya mezani ile ya unga nyeupe haifai kwa mwanaume. Kila mmoja amesikia chumvi hii husababisha shinikizo la juu la damu na pamoja na hayo bado sehemu kubwa ya watu wanatumia chumvi hii.

Chumvi ya mezani husafishwa kwa kuondoa madini madini na hupitishwa katika joto la nyuzi joto 1093. Kwa hiyo uliyonayo sasa ni asilimia 40 ya sodiamu na asilimia 60 ya kloridi, na kisha kemikali kama vile [aluminium silicatea]huongezwa ili kuifanya isishikane na hivyo kubaki katika hali ya unga. Aluminium silicate ni sumu kali inayoharibu mfumo wetu wa fahamu. Inatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazosababisha ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijapita kiwandani (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi kwa afya ya mwanaume.

2. Popcorn
Popcorn au bisi ni chakula kingine mwanaume hatakiwi kula, hupikwa kwa kutumia mafuta yasiyo na afya, sodiamu nyingi na ni chanzo cha baadhi ya kansa. Kuna kitu kinaitwa ‘Diacetyl’ kinachopatikana kwenye popcorn ambacho kinahusika na kusababisha kansa na kuna kingine kiitwacho ‘Perfluorochemicals’ ambacho huathiri tezi ya thyroid na ugonjwa wakati huo huo husababisha ugonjwa wa kupungukiwa umakini ujulikanao kwa kiingereza kama ‘Attention-deficit/hyperactivity disorder (ADHD)‘. Hivyo ni vizuri kuacha kula popcorn

5. Mkate mweupe
Mkate mweupe una wanga mwingi zaidi usio na faida. Kwenye hatua za kutengeneza mkate mweupe vitamini zote za kundi B hupotea, hupotea pia nyuzinyuzi (fiber). Siyo hivyo tu mkate mweupe umesemekana kuwa ni sababu ya ugonjwa wa kisukari na kuongeza uzito zaidi mwilini wakati huo huo ukisababisha tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana.

Vingine vinavyofanana na na hilo ni ugali wa sembe, tambi nyeupe, chai ya rangi na kahawa.
Kula mkate ambao ngano yake haikukobolewa (brown bread), kula ugali wa dona na chai unaweza kutumia tangawizi au mdalasini badala ya majani ya chai.

SOMA PIA: Nafasi za ajira zilizotangazwa Leo

Waziri Mkuu: Ujenzi Wa Ukuta Mererani Umeokoa Mamilioni, Mapato Yamepanda Kutoka Sh. Milioni 147 Hadi Sh. Milioni 714

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kukamilika kwa ujenzi wa ukuta kuzunguka mgodi wa Mererani kutasaidia kuongeza mapato ya Serikali ikiwa ni pamoja na kudhibiti vitendo vya wizi na utoroshaji wa madini ya Tanzanite.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Aprili 10, 2018) Bungeni mjini Dodoma kwenye mkutano wa 11 wa Bunge, wakati akihitimisha mjadala wa mapitio ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa mwaka 2017/2018 na mwelekeo wa kazi za Serikali kwa mwaka 2018/2019.

Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa ujenzi wa ukuta huo uliozinduliwa Aprili 6, mwaka huu Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kutasaidia pia kudhibiti ulanguzi na biashara ya magendo pamoja na kuimarisha usalama kwenye mgodi, kwa wafanyakazi na wafanyabiashara wa Tanzanite.

“Kukamilika kwa ujenzi huo pia kutasaidia kuongeza mapato ambapo katika kipindi cha Januari hadi Machi 2018, Serikali imekusanya takriban shilingi milioni 714 ikilinganishwa na makusanyo ya shilingi milioni 147.1 kwa mwaka mzima wa 2017,” alisema.

Waziri Mkuu alisema kabla ya ujenzi huo, inakadiriwa kuwa asilimia 40 ya madini ya Tanzanite yaliyokuwa yanazalishwa kila mwaka, yalitoroshwa kwa njia za panya na Serikali yetu haikuambulia chochote. “Hii ni kutokana na kukosekana udhibiti wa kutosha wa madini ya tanzanite kuanzia kwenye uzalishaji hadi kwa wauzaji,” alisema.

Alisema mbali na kuwepo kwa eneo la wachimbaji ndani ya ukuta wa Mererani, pia kutajengwa maduka ya Tanzanite na viwanda vya kuongeza thamani, hususan vya ukataji, uchongaji na ung’arishaji. Vilevile, kutakuwa na maeneo ya burudani ambayo yatastawisha zaidi biashara ya Tanzanite na kuwavuta watalii wengi kwenda kutembelea eneo hilo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa (Standard Gauge) itakayokuwa na urefu wa km. 1,219 utarahisisha usafiri wa mizigo na abiria na kuongeza itaongeza biashara hapa nchini pamoja na nchi za jirani.

Waziri Mkuu alisema mradi huo utakapokamilika, unatarajiwa kusafirisha tani milioni 17 kwa mwaka, ikilinganishwa na tani milioni tano za sasa na kwamba utaongeza mapato kwa Serikali ikiwa ni pamoja na kutunza barabara ambazo zimekuwa zikiharibika mapema kutokana na kusafirisha mizigo mizito.

“Reli hii ya kisasa itakuwa na uwezo wa kubeba mzigo wa takriban tani 10,000 kwa mara moja, ambayo ni sawa na malori (semi trailers) 500 yenye uwezo wa kubeba tani 20 kila moja. Hii, itasaidia sio tu kutunza barabara zetu bali pia kupunguza gharama za kukarabati barabara hizo mara kwa mara,” alisisitiza.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

EXCLUSIVE: Shamsa Ford Kamfungukia Faiza Ally “Ni Mkurupukaji”

$
0
0
Jana April 10,2018 muigizaji Shamsa Ford amezungumza kwenye Exclusive interview na Ayo Tv na kufunguka kuhusu Faiza Ally kwa kile ambacho alikisema juu yake kuhusu madili makubwa wanayopata wanawake wa nje ndani ya Tanzania .

VIDEO:

Yanga yafunguka Kuhusu Kuondoka kwa Lwandamina

$
0
0
Baada ya kuenea kwa uvumi kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina, amerejea kwao Zambia kujiunga na timu yake ya zamani, Zesco United, uongozi Yanga umekiri uwepo wa taarifa hizo.

Kupitia Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu ya Yanga, Salum Mkemi, amesema kuwa ni kweli taarifa hizo zimesambaa mitandaoni lakini hawana uhakika kama Lwandamina aeshajiunga na Zesco United.

Licha ya uwepo wa taarifa hizo, Kupitia Radio EFM (E Sports), Mkemi amwemwelezea Kocha Lwandamina kama Mwalimu aliyekuwa anakuza vipaji vya vijana na kuwatengeneza kuwa mhimili wa timu.

Taarifa zilitoka hivi punde kutoka Zesco United, zimethibitisha kuwa Lwandamina ameshajiunga tayari na miamba hao wa Zambia.

Lwandamina ameondoka Yanga ikiwa inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida United utakaopigwa kesho katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Download Upya Application Yetu ya UDAKU SPECIAL .....Ile Ya Zamani Tutaifuta

$
0
0
Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Upya Application yetu ya UDAKU SPECIAL Maana ile ya Zamani Tutaifuta.

Kuna Marekebisho Makubwa tumeyafanya ikiwa na tatizo la Notification kutatuliwa

NB: App mpya ina Icon Nyekundu

 Bonyeza Hapa Chini

==>>Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>>  
  

Miaka 9 Katika Ndoa - Simuelewi Mume Wangu Ajanigusa Miezi Sita Sasa Naomba Ushauri

$
0
0
Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 33 mume wangu ana umri wa miaka 41. Sote ni wasomi na wafanyakazi. Tumefunga ndoa miaka tisa iliyopita tuna mtoto mmoja ana umri wa miaka 7.Wakati tunafunga ndoa wote tulikua mabikra. Mimi nilikua sijawahi kuwa na mpenzi na mume wangu akuwahi kua na mpenzi..

Tulianza kushiriki tendo la ndoa siku ile tulipofunga ndoa. Kwa kweli kwa ujumla maisha yetu ya ndoa ni ya furaha kwa mambo yote lakini sio ya kiunyumba.

Mimi na mume wangu atujawahi kuwa mbali kikazi. Maisha yote hadi leo tuko Dar es salaam pamoja. Tulipofunga ndoa miaka ya mwanzoni tulikua tunaweza kukutana kimwili hata mara tatu kwa mwezi, miaka ilivyokua inazidi kwenda ikawa kukutana kimwili inakua mara moja kila baada ya miezi miwili na tukikutana ni bao moja tu.

Sasa hali imezidi kua mbaya kwani sasa imepita miezi sita tunalala kitanda kimoja mume wangu ajanigusa, hali hii inanisononesha kwani natamani mtoto wa pili. Kwakweli atuna ugomvi wowote. Mimi na mume wangu wote ni wacha Mungu.

Mume wangu ni mchapakazi sana tukitoka kazini tuko wote na sio mtu anaependa kwenda kutembea bila familia. Jumamosi na Jumapili mara nyingi tunatoka out tukirudi home akuna kinachoendelea, anageuka ukutani analala kama mtoto hadi asubuhi, wala hata anigusi nikimsogelea hata ashtuki.

Na asubuhi tukiamka tunaenda ofisini na akifika ofisini lazima anitumie message, mke wangu nakupenda sana. Simuelewi na nashindwa kumuuliza maana mimi kama mwanamke naona aibu.

Kwakweli mawazo ya kutoka nje ayapo kabisa kichwani mwangu maana simjui mwanaume mwingine zaidi yake pia namuogopa Mungu siwezi kucheat.Ila kwa hali ilipofikia naona bora nitengane nae niishi maisha yangu maana bila unyumba amna maana ya ndoa na nataka sana mtoto.

Yule Mtaalam wa Dua na Dawa za Kiarabu na za Kiasili Sharifu Lukumani Sasa Yupo Hewani

$
0
0

YULE MTAHALAM WA DUA NA DAWA ZA KIARABU NA ZA KIASILI YANI MITI SHAMBA SHARIFU LUKUMANI SASA YUPO HEWANI

WENYE SHIDA ZITUATAZO:
CHEO KAZINI, KUONGEZEWA MSHAHARA KAZINI, MWENYE TATIZO LA NGUVU ZA KIUME, ALIEPOTELEWA NA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA, MWENYE KIFAFA, KISUKARI, FANGASI SEHEMU ZA SIRI KWA WALE WENYE MIILI MINENE MTOTO WA JICHO PAMOJA NA WALE WAKINA MAMA WANAOSUMBULIA NA CHANGO LA UZAZI PUMU YA MUDA MREFU WANAWAKE KUJAA MAJI SEHEMU ZA SIRI, MWANAUME KUWAI KUFIKA KILELENI AU KUTOA MANII MFANO WA MAJIMAJI YAKIWA MEPESI AUTOWEZA KUMPA MKEO UJAUZITO JAMBO HILI LINAWASUMBUA WANAUME WALIO WENGI DUNIANI KWA KAWAIDA WANAUME ASIE NA TATIZO HILI UTOA MANII MAZITO NDIO YENYEUWEZO WA KUMPA MWANAMKE MIMBA.

MWANAUME KUPATA MPENZI KWA ULAISI PASIPO NA GHARAMA YOYOTE YANI KWA WALE MADOMO ZEGE KUWA NA UWEZO WA KUSIKILIZWA HATAKAMA RAIA WA INCHI GANI NA UWEZO WA KURUDISHA MPENZI ALIE POTEA NA KUMFANYA AWE WAKO KWA WALE WASIO TAKA MITALA PIA UFANYA KAZI YA KUNG'ALISHA NYOTA SASA MATATIZO YAKO YAMEPATA SULUHISHO ANAPATIKA KWA MASAA ISHIRINI NA NNE

WASILIANA NAE KWA NAMBA 0762899488-0656145170-WhatsApp namba +255620665635

Kikosi cha Simba Kipo Tayari kwa Kufa na Kupona Dhidi ya Mbeya City

$
0
0
Kikosi cha Simba Kipo Tayari kwa Kufa na Kupona Dhidi ya Mbeya CityKikosi cha klabu ya Simba kimeanza rasmi mazoezi yake hii leo kwenye uwanja wa Boko Veteran jijiini Dar es Salaam kujiandaa kuwakabili Mbeya City.

Simba SC imeanza mazoezi hayo kwaajili ya kujiwinda na mchezo wao dhidi ya Mbeya City utakao pigwa tarehe 12.04.2018.

Simba inaongoza kwenye msimamo wa ligi kwa kuwa na jumla ya pointi 52 dhidi ya 46 za Yanga SC anaeshika nafasi ya pili.

Klabu hiyo ya soka yenye maskani yake mitaa ya k/koo inapamba kufa na kupona ili kujihakikishia inafanikiwa kutwaa taji la ligi kuu soka Tanzania Bara ambalo wamelikosa kwa miaka mitano sasa huku likiwa linatetewa na mahasimu wao Yanga SC waliyochukua mara tatu mfululizo.

Serikali Yafunguka Kuhusu Uhalali wa Nembo ya Taifa

$
0
0
Serikali Yafunguka Kuhusu Uhalali wa Nembo ya Taifa
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde amelieleza bunge kuhusu tuhuma za baadhi ya wabunge kuhoji uhalali wa Serikali kutumia nembo ya taifa ambayo picha zilizopo haziakisi uhalisia wa mwanamke wa kitanzania.

Mavunde amesema…>>>“Yamesemwa maneno kwamba nembo yetu haiakisi muonekano wa kitanzania kwamadai kwamba mwanamke aliyepo amevaa wigi, sio kweli kwamba haiakisi nah ii ni moja ya alama ya taifa”

Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza Auwawa Kikatili Baada ya Kubainika Kubaka Kisha KumnyongaBinti wa Miaka 12

$
0
0
Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza Auwawa Kikatili Baada ya Kubainika Kubaka Kisha KumnyongaBinti wa Miaka 12Mwanafunzi wa kiume mwenye umri wa miaka 15 ambaye alikuwa anasoma kidato cha kwanza shule ya sekondari Gituto katika kaunti ya Murang'a nchini Kenya, ameuawa na wananchi wenye hasira kali, baada ya kubainika kumbaka binti mwenye umri wa miaka 12 na kisha kumnyonga.

Dada wa binti aliyeuawa Grace Kabura, amesema alimuacha mdogo wake nyumbani, na aliporudi hakumkuta.
“Nilirudi nyumbani sikumkuta Wambui, nikawauliza watoto waliokuwa wakicheza jirani wakaniambia ameondoka na Duncan Wakahiu”, amesema dada wa binti huyo aliyeuawa.
Grace ameendelea kwa kueleza kwamba baada ya hapo aliwaomba watoto wamuonyeshe nyumbani kwa kijana huyo na kuwakuta wazazi wake, kisha akawaeleza kuwa anamtafuta mdogo wake ambaye ameonekana kuelekea hapo.
Baada ya hapo wazazi wa kijana wakamuita mtoto wao na kumuuliza mahali alipo mwenzake, akawaambia amemtuma dukani na hajarudi.
Grace ameendelea kueleza kuwa wazazi wake waliingiwa na mashaka na kuamua kupekua ndani ya chumba cha kijana wao, na kukuta mwili wa Wambui ukiwa uvunguni na kijana huyo kukimbia.
Hata hivyo wananchi waliamua kumsaka kijana huyo na walipompata walimshushia kipigo na kumuua.

Majaliwa Awaonya Wabunge Wanaopotosha Muungano

$
0
0
Majaliwa Awaonya Wabunge Wanaopotosha Muungano
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waulinde Muungano baina ya Tanzania Bara na Zanzibar na akawaonya wasitumie Bunge hilo kuupotosha.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Aprili 10, 2018) Bungeni mjini Dodoma kwenye mkutano wa 11 wa Bunge, wakati akihitimisha mjadala wa mapitio ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa mwaka 2017/2018 na mwelekeo wa kazi za Serikali kwa mwaka 2018/2019.
Waziri Mkuu amesema mjadala ulioibuka jana kuhusu suala la Muungano haukuwa na afya na kwamba hatarajii kuona hali hiyo ikijirudia tena Bungeni kuhusiana na suala la Muungano.
“Mjadala wa jana sijaupenda kabisa na wala haukuwa na afya, ulikuwa ni malumbano baina waheshimiwa wabunge wawili. Hatuzuii Mhe. Mbunge kuuliza jambo ili apate ufafanuzi lakini pia haturuhusu mtu na mtu watumie Bunge kupotosha ukweli wa mambo,” amesema
Waziri Mkuu amelieleza Bunge kwamba kuna maboresho ambayo yanafanywa hivi sasa na Serikali za pande zote mbili lakini akatumia fursa hiyo kulihakikishia Bunge kwamba majadiliano bado yanaendelea kwenye vikao halali vya SMT na SMZ ambavyo vinaongozwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Akitoa ufafanuzi kuhusu chanzo cha malumbano hayo, Waziri Mkuu alisema kiini cha malumbano hayo ni suala la uagizaji sukari kutoka nje ya nchi ili kufidia upungufu wa sukari uliopo nchini (gap sugar). Alisema katika kutimiza azma hiyo, Serikali haiangalii kama muagizaji ametoka Tanzania Bara au Tanzania Zanzibar.
Akitoa mfano, Waziri Mkuu alisema katika mwaka 2016, upungufu uliojitokeza ulikuwa tani 140,000 lakini waagizaji waliopewa vibali walikuwa wawili kutoka Zanzibar, watatu kutoka Bara na kiwanda cha sukari cha Mahonda kilipewa kibali cha kuagiza tani 390.
“Katika mwaka 2017, gap sugar ilikuwa tani 140,000 na waliopewa vibali walikuwa ni wawili kutoka Zanzibar na wawili kutoka Bara, lakini kwa mwaka huu (2018) gap sugar ni tani 135,000. Tofauti na miaka ya nyuma, safari hii tumewapa vibali wenye viwanda ndiyo waagize sukari kutoka nje. Kwa hiyo, jambo hili la sukari lisivuruge Muungano wetu,” amesisitiza.
Waziri Mkuu alisema nia ya Serikali ni kuzalisha sukari ya kutosha hapa nchini ili nchi ijitegemee na kawataka Mawaziri wa Biashara wa Zanzibar na Tanzania wawe makini ili sukari inayoagizwa nje isije kufurika soko la ndani kwa sababu gharama za uzalishaji sukari ya ndani ni kubwa.
Viewing all 104762 articles
Browse latest View live




Latest Images