Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live

Thea Atoa Pongezi Zake kwa Makonda ....... Ni Baada ya Kampeni ya Kusaidia Wanawake

$
0
0
Msanii wa bongo movies Ndumbagwe Misayo maarufu kama Thea ameandika ujumbe mrefu kwa ajili ya kumpongeza Mh Paul Makonda baada ya kuanzisha kampeni ya kusaidia wanawake ambao wametelekezwa na wanaume zao na kuwaachia watoto kulea peke yao.

Thea aliandika hivi kuhusu kampeni hiyo ya Mh Paul:
"Kwanza nimpogeze mheshimiwa paul makonda kwa kujitolea na kulikumbuka kundi hili la wanawake waliojitokezwa, kwakweli tatizo hili ni kubwa sana  na kumuachia Mh Makonda peke yake haitwezekana kwa sababu tatizo sio kwa dar peke yake bali ni Tanzania nzima.

"Niombe wadau wa maendeleo ya wanawake tanznia kutafuta suluhu ambayo ni endelevu kwa tatizo hili.upo ukatili unaotokea kama ajali lakini ukatili huu mwingi kwa wanawak na wasichana utokana na umaskini.

"Wanawake hawa waliojitokeza leo inamaanisha kuwa hawajaweza kumudu mahitaji ya msingi, nitoe wito kwa wanawake na wadau wengine kumuunga mkono Mh Paul Makonda ili kuweza pia kuwakwamua wanawake hawa kiuchumi.

"Tuwasaidie wanawake hawa kuwa na uchumi imara kwa sababu sio wanaume wote wanakataa kutoa matunzo kwa makusudi, wengine wamekuwa wakiyumba.

Hata hivyo kutokana na kampeni hii kila mtu amekuwa na muonekano tofauti kwa sababu wapo wanaosapoti na pia wapo wanaosema zoezi haliwezi kumaliza tatizo.

Mtanzania Aliyezalishwa na Kutelekezwana Mchina Awa Gumzo Mitandaoni

$
0
0
Mtanzania Aliyezalishwa na Kutelekezwana Mchina Awa Gumzo MitandaoniKambi  ya siku tano inayoendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwatafuta wanaume waliotelekeza watoto wao imempa umaarufu mitandaoni msichana aliyejitambulisha kwa jina moja la Safina.

Picha za msichana huyo ambaye ni mkazi wa Dar es Salaam, zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii tangu alipoonekana nje ya ofisi za Mkuu wa Mkoa juzi asubuhi akiwa na mtoto wake anayefanana na Mchina.

Mwanamke huyo alipigwa picha akiwa amekaa kwenye ofisi hizo na mtoto wake huyo akisubiri foleni ya kupata msaada kutoka kwa wanasheria, maofisa ustawi wa jamii na polisi kutoka Dawati la Jinsia.

Baada ya picha hiyo kusambaa iliibuka mijadala kwenye mitandao hiyo wengi wakihoji kama kweli baba wa mtoto huyo atakuwa Mtanzania.

Baada ya muda kupita, ujumbe wa video iliyomrekodi msichana huyo ulisambaa akielezea alivyokutana na Mchina huyo na kuanzisha uhusiano ambao hatimaye ulisababisha kupatikana kwa mtoto huyo.

Kwenye ujumbe huo, msichana huyo alisema alikutana kwa mara ya kwanza na mchina huyo mwaka 2013 alipokuwa akifanyakazi kwenye kampuni ya ujenzi ya Hainan kutoka China.

Alisema wakati huo kampuni hiyo ilikuwa ikijenga majengo maeneo ya Gongolamboto jijini Dar es salaam na baadaye walihamia mkoani Dodoma na kuendelea na maisha.

"Nilikaa na baba yake huyu mtoto miaka mitatu mkoani Dodoma hadi alipopata matatizo na kuamua kurudi kwao China.... aliniambia atarudi na atanitafuta kwa njia ya simu lakini hadi leo sina mawasiliano naye," alisema.

Safina alisema anamlea mtoto huyo katika mazingira magumu bila msaada kwa kuwa mtoto huyo hana ndugu yeyote wa upande wa baba hapa nchini.

Safina alikuwa akizungumza huku akionyesha picha mbalimbali zinazoonyesha hatua za mahusiano yao, ikiwemo inayomwonyesha mzazi mwenzake akiwa amembeba mtoto huyo alipokuwa mchanga huko mkoani Dodoma.

Pia alikuwa akiwaonyesha waandishi wa habari vibali vya muda vya ukaazi alivyokuwa akitumia raia huyo wa China alipokuwa akifanyakazi nchini ambavyo vimeisha muda wake.

Msichana mwingine ambaye ujumbe wake wa video umesambaa ni Mwajuma Mohamed ambaye alisema kuwa ametelekezwa na mzazi mwenzake hivyo utaratibu ulioanzishwa na Mkuu wa Mkoa ni ukombozi kwao.

Alisema kwa sasa maisha ni magumu na kwamba ingawa yuko hai lakini anashindwa kuyamudu na kuhoji kuwa itakuwaje kama ikitokea akafariki na kumwacha mtoto wake bila baba.

Anahofu anaweza kuwa mtoto wa mitaani, alisema zaidi.

"Nawaambia wanaume huko waliko waache kutubebesha mimba na kututelekeza, huyu mtoto sijazaa na mzazi wangu nimezaa na wewe mwanaume uliyenikimbia, yaani nina dukuduku natamani nimkamate huyo mwanaume nimkamue ili aone uchungu wa maisha," alisema Mwajuma.

Awali, kambi hiyo ilipangwa kufanyika kwa siku tatu lakini kutokana na wingi wa wanawake waliojitokeza Makonda alitangaza iendelee kwa siku tano mfululizo ili kuhudumia wengi zaidi.

Wanawake hao wanapewa msaada wa kisheria na wanasheria mbalimbali, polisi na maofisa wa ustawi wa ajamii.

Mambo ni Hivi Naye Dance wa Daimond Ang'ang'aniwa kwa Makonda Sakata la Kutelekeza Mtoto

$
0
0
Mambo ni Hivi Naye Dance wa Daimond Ang'ang'aniwa kwa Makonda Sakata la Kutelekeza Mtoto
Dansa kutoka WCB ambaye ni mchezo shoo wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zungu amekumbwa na skendo ya kuwa mmoja kati ya wanaume waliotelekeza watoto wao Dar.

Siku ya jumatatu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda aliwakusanya wanawake wote ambao wametelekezwa na wanaume ambao wamezaa nao ambapo hawawahudumii watoto wao.

Mmoja kati ya Wanawake waliojitokeza ni mwanamke ambaye alijitambilisha kama mzazi mwenza wa Dansa wa  Diamond anayejulikana kama Zungu ambapo alidai alimtelekeza yeye pamoja na mtoto wake baada ta kuachana ambapo amekuwa hataki kumtunza mtoto wake.

Baada ya tuhuma hizo Zungu alitafutwa na Timamu Tv ambapo amefunguka na kusema yule mwanamke ana matatizo ya akili pia ni mkorofi na amedai kuwa hajawahi kumkataa mtoto wake na amesema yupo tayari hata leo kwenda kwa Makonda na kujielezea na kama ikitokea anatakiwa amchukue mtoto wake amesema yupo tayari kumlea mwanaye mwenyewe.

Watu 36 Wahukumiwa Kifo kwa Kushambulia Makanisa

$
0
0
Watu 36 Wahukumiwa Kifo  kwa Kushambulia MakanisaMahakama ya kijeshi huko Misri imewahukumu watu thelathini na sita adhabu ya kifo kutokana na makosa ya mashambulizi dhidi ya makanisa ya Coptic.
Watu sabini walikufa kutokana na shambulizi la bomu katika kanisa kuu la ki Coptic mjini Cairo mwishoni mwa mwaka 2016, na makanisa ya Alexandria na Tanta yaliripuliwa siku kama hiyo mwezi wa nne mwaka uliofuata.
Tayari kundi la wanamgambo wa kiislamu wenye msiamamo mkali wamekiri kuhusika na mashambulizi hayo matatu. Wameendelea kukiri kuwa kazi yao kubwa ilikuwa kuwashambulia wakristo wachache, pamoja na mamlaka ya kijeshi.

Misri inahitaji mahakama kupeleka kesi za namna hiyo kwa Mufti mkuu nchini humo kwa kuzingatia adhabu ya kifo kabla ya hukumu ya mwisho.

Mmiliki wa Facebook Akiri Kampuni Yake Inakabiliana na Urusi

$
0
0
Mmiliki wa Facebook Akiri Kampuni Yake Inakabiliana na Urusi
Mmiliki wa Facebook amewaambia maseneta wa Marekani kuwa kampuni yake imekuwa ikipambana na watumiaji wa Warusi wanaotaka kuutumia vibaya mtandao huo wa kijamii
" Haya ni makabiliano ya kijeshi. Watarekebika ,"alisema he said.
Bw Zuckerberg alikua akijibu maswali kuhusiana na sakata ya matumizi mabaya ya data za kibinafsi maarufu kama Cambridge Analytica.
Pia amefichua kuwa Robert Mueller, kutoka baraza maalum linalochunguza madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani wa Mwaka 2016 aliwahoji wafanyakazi wa Facebook.

Lakini aliongeza kuwa : "kazi yetu na baraza maalum ni ya siri na ninataka kuhakikisha kwamba katika kikao cha wazi sifichui chochcote juu ya taarifa za siri.
Mwezi Februari, Ofisi ya Bw Mueller ilishtakiwa na Warusi 13 kwa kudukua taarifa za uchaguzi wa mwaka 2016, pamoja na makampuni matatu ya Urusi.
utokana na hojaji hiyo hisa za mtandao wa Facebook jana ziliongezeka mpaka kufikia asilimia nne

Kutokana na kuhojiwa kwa Bw Zuckerberg na seneti ya Marekani hisa za mtandao wa Facebook jana ziliongezeka hadi kufikia asilimia nne
Bw Zuckerberg amesema kuwa kampuni yake sasa imetengeneza nyenzo za kubaini akaunti gushi.
Awali Mtendaji mkuu wa mtandao wa kijamii Facebook, Mark Zuckerberg ameomba msamaha kwa kamati ya Seneti ya Marekani kwa kuruhusu makampuni kadhaa kutumia vibaya data binafsi za jukwaa hilo kisiasa.
Mark Zuckerberg alijitetea kwa muda wa saa tano katika jopo la wasikilizaji kutoka bunge la seneti la Marekani linalohusika na masuala ya biashara na kamati ya mahakama.

Kwamba wakati wote kutakuwa na kitengo kisicholipiwa cha Facebook, kunachoweza kulipiwa , kitengo ambacho hakina matangazo ya biashara cha mtandao wa kijamii
Kukabiliana na kauli za uchochezi wa chuki " una kiwango cha juu cha makosa kuliko vile ninavyotaka "
Binafsi alihofia juu ya uwezekano wa upendeleo wa kisiasa kwneye kampuni yake

Kinyume na matarajio ya ulimwengu, wakati wa kikao dhidi yake badala ya kuvaa fulana kama alivyozoeleka, Bw Zuckerberg alikuwa maevalia nadhifu suti nyeusi
Kutokana na hojaji hiyo hisa za mtandao wa Facebook jana ziliongezeka mpaka kufikia asilimia nne , nao wanasheria nchini Uingereza na Marekani wameanzisha mashtaka dhidi ya Facebook, Cambridge Analytica, na makampuni mengine mawili yanayounganishwa na kesi hiyo.
Na baada ya utetezi wake Mark ameelezea hisia zake kutokana na mtandao wa Facebook hapa ulipofikia na yanayojiri hafurahishwi na chochote.
Utetezi wa Mark Zuckerberg, umepokelewa vyema na masoko ya hisa na hivyo kuifaidia Facebook kwa ongezeko la hisa asilimia nne unusu.

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo

$
0
0

Wastara Aibuka na Kutoboa Siri Ya Kuolewa na Kuachika Mara 3

$
0
0
Wastara Aibuka na Kutoboa Siri Ya Kuolewa na Kuachika Mara 3
BAADA ya kuolewa mara tatu na ndoa hizo kuvunjika, staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma ameibuka na kueleza siri za kuachika.
Akizungumza katika Tamasha la Single Mothers lililoandaliwa na msanii mwenzake, Faiza Ally na kufanyika katika Hoteli ya De Mag iliyopo Mwananyamala, Dar, Wastara alisema kuwa, siri kubwa ya ndoa zake kuvunjika ni kutokana na kukosekana kwa maelewano ndani ya nyumba na siyo kwamba huwa anapenda kuachika.
“Unajua kuna vitu ambavyo ningevikubali kuvifanya nilipokuwa ndani ya ndoa, ungekuta sasa hivi nimeshakufa hivyo kuolewa n
a kuachika siyo kupenda, bali nilishindwa kukubaliana na mambo ambayo nilikuwa ninalazimishwa kuyafanya,” alisema Wastara wakati akizungumza na wamama hao ambao wanawalea watoto bila baba zao.
Hata hivyo, aliwataka wamama hao kuwa na ujasiri wa kufanya kazi kwa bidii na wasinyong’onyee kwa sababu ya kuwa wanawalea watoto peke yao baada ya kuzalishwa na wanaume kuwakimbia au kuachika katika ndoa.

Wolper Ashindwa Kuvumilia Afunguka Mahusiano ya Nisher na Brown " Nisha Hana Vigezo vya Kutembea na Brown"

$
0
0
Wolper Ashindwa Kuvumilia Afunguka Mahusiano ya Nisher na Brown " Nisha Hana Vigezo vya Kutembea na Brown"
STAA wa Bongo Movie, Jackline Wolper amepinga kwa nguvu zote stori zinazosambaa mitandaoni kuwa X-wake ambaye ni mwanamitindo, Brown ana uhusiano wa kimapenzi na muigizaji mwenziye, Salma Jabu ‘Nisha’.

Wolper amesema Nisha ni mchekeshaji hivyo haamini kabisa kama anaweza kutoka na mwanamitindo huyo na pia anazijua taype za wanawake wanaoweza kutembea na Brown haifanani kabisa na Nisha.

Aidha, amesema Project yao mpya ya kijana amka itawasaidia vijana wengi waliokata tamaa ili waweze kuamka na kujikwamua kimaisha kupitia vipaji vyao hata kama ni vipaji vya wanavyodharaulika.

Tundu Lissu Kufanyiwa Upasuaji wa Mguu Afunguka Haya

$
0
0
Tundu Lissu Kufanyiwa Upasuaji wa Mguu Afunguka Haya
MBUNGE wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema kwa amara nyingine tena, leo Aprili 11, 2018 ataingia kwenye chumba cha upasuaji kwa ajili ya kufanyiwa oparesheni ya mguu wake wa kulia ambao bado una matatizo kutokana na risasi alizopigwa Septemba 7 mwaka jana nyumbani kwake, Area D, Dodoma.

Upasuaji huu utakuwa ni wa 20 tangu alipoanza kutibiwa, baada ya kushambuliwa kwa risasi mwaka jana.

Lissu ambaye yupo nchini Ubelgiji kwa matibabu amesema kwamba oparesheni hiyo ni sehemu ya tiba ya mguu huo huku akieleza kuwa kwenye mikono yuko salama kitabibu.

Mama Samia Azindua Chanjo ya Kinga ya Saratani ya Mlango wa Kizazi

$
0
0
Mama Samia Azindua Chanjo ya Kinga ya Saratani ya Mlango wa Kizazi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, jana Jumanne, Aprili 10, amezindua chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi (HPV Vaccine), kwenye viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam.

Kinga hiyo itakuwa ni kwa wasichana kuanzia umri wa miaka 14 ambapo amesema itatolewa bila malipo na kwa mwaka huu itatolewa kwa wasichana 616,734.

"Mume Wangu Akitaka Kuoa Mke wa Pili Anipe Talaka " Shamsa Ford

$
0
0
"Mume Wangu Akitaka Kuoa Mke wa Pili Anipe Talaka " Shamsa Ford
Msanii wa fila
mu, Shamsa Ford akiwa anasherekea miaka miwili ya ndoa yake , ameibuka kwa kudai kwamba ikitokea mume wake anataka kuoa mke wa pili basi ataomba talaka. Mwigizaji huyo amedai hawezi kuishi mbali na mume wake huyo kwa madai ana wivu uliopitiliza.

Lwandamina Aikimbia Yanga Akimbilia Kwao Ajiunga Rasmi na Zesco United

$
0
0


George Lwandamina Aikimbia  Yanga Ajiunga Rasmi na Zesco United
Hatimae yametimia, aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga, George Lwandamina amerejea kwao Zambia na kutangazwa rasmi kujiunga na timu yake ya zamani ya  Zesco United ambayo alikuwa akiifundisha kabla ya kuja nchini kujiunga na miamba hiyo ya Jangwani.
Taarifa rasmi kutoka ndani ya klabu ya Zesco United iliyotolewa hapo jana aprili 10 imemtambulisha rasmi Lwandamina kuwa kocha mkuu akichukua mikoba ya Tenant Chembo.

Aprili 8 mwaka 2018 Zesco United ilitangaza kuachana na aliyekuwa kocha wake Chembo baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Nkana FC.

Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa kupitia mahojiano yake amewahi kusema kuwa hajui lolote kuhusu taarifa hiyo, kama Lwandamina ameondoka basi hajamuaga.

Sakata la Wanawake Waliotelekezwa na Watoto na Wabunge Lamfikia Ndugai Ataka Wapeleke Vyeti Kupima DNA

$
0
0
Sakata la Wanawake Waliotelekezwa na Watoto na Wabunge Lamfikia Ndugai Ataka Wapeleke Vyeti Kupima DNASpika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema zoezi linaloendelea katika Mkoa wa Dar es Salaam linaloongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda, la kuwatafutia haki wanawake waliowatelekezewaa watoto na wanaume waliozaa nao bila kuwahudumia na halikadhalika wanawake waliowakimbia wanaume zao na kuwaacha na watoto limemtikisa.

Spika Ndugai amesema baada ya Makonda kukutana na akina mama hao ambapo inadaiwa wapo baadhi ya Wabunge waliotajwa kutelekeza watoto.

Ndugai amesema (kwa utani) amesikia wapo na wanaume walitelekezewa watoto na akina mama ambao ni wabunge huku
akiwaomba wamuandikie barua na wamletee cheti kinachoonyesha na kuthibitisha Kipimo cha Vinasaba vya uzazi ‘DNA’.

Majaji Wawili wa Mahakama Wajihudhuru Nafasi Zao

$
0
0

Majaji Wawili wa Mahakama Wajihudhuru Nafasi Zao
Majaji wawili wa Mahakama ya Katiba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamejiuzulu kwenye nafasi zao, na kusalia majaji sita badala ya tisa katika Mahakama hiyo.
Jaji mmoja alifariki dunia siku ya Jumapili na wengine wawili wamejiuzulu bila hata  kutoa maelezo au sababu ya kujuzulu kwao.
Majaji hao ambao ni  Jean-Louis Esambo na Banyaku Luape wamedaiwa kutoripoti katika Mahakama ya Katiba, Mnamo Oktoba 17, 2016, ambayo ingetoa uamuzi muhimu kuhusu hatma ya DRC.
Imeelezwa kwamba Tangazo hilo limeishangaza serikali ya DRC kwa uamuzi  huo ingawa majaji hao wawili walionesha zaidi ya mara moja maoni tofauti na rais wa mahakama hiyo.

Msigwa Ajibu Tuhuma za Kutelekeza mtoto

$
0
0

Msigwa Ajibu Tuhuma za Kutelekeza mtoto
Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa amejibu tuhuma za kutelekeza mtoto, baada ya picha kuzagaa kwenye mitandao ikimuonyesha mtoto ambaye amefanana naye akitajwa kumtelekeza.
Akizungumza na www.eatv.tv, Peter Msigwa amesema kwamba alichokiandika kwenye mitandao ya kijamii anamaanisha hivyo anamtaka mwanamke huyo ambaye ametajwa kuwa miongoni mwa walioenda kwa mkuu wa mkoa wa Dar e salaam Paul Makonda kwa kutelekezwa, asiishie hapo tu bali aende hata Bungeni.
“Ilikoanzia imeanzia kwa Jerry Muro ndiye kasambaza hizi habari, kitu ambacho nakijibu hapa amekianzisha Jerry Muro, sasa mimi nasema kama huyo mtu yupo, nimetoa namba zangu na kama sipatikani aje hapa Bungeni”, amesema Peter Msigwa.
Hapo jana Peter Msigwa ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa facebook akisema kwamba iwapo kweli mwanamke huyo yupo na akithibitisha ni kweli amemtelekeza, basi yupo tayari kujiuzulu ubunge wake alionao.

Rais Asaini Sheria ya Pedi Bure kwa Wanafunzi

$
0
0

Rais asaini sheria ya pedi bure kwa wanafunzi
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesaini muswada wa sheria ambao sasa utakuwa kamili, inayoitaka serikali kugawa pedi bure kwa wanafunzi wa kike nchini humo.
Rais Kenyatta amesaini sheria hiyo jana Aprili 10, ambayo pia inaitaka serikali kuweka mazingira salama kwa wanafunzi hao kuweza kuhifadhi pedi zao.
“Sheria ya Marekebisho ya Elimu ya Msingi, kuweka wajibu wa kutoa taulo za usafi (pedi) za kutosha na za ubora kwa kila mtoto msichana aliyesajiliwa na kujiandikisha katika taasisi ya elimu ya msingi ya umma na kufikia ujira, kwa serikali”, imesema taarifa iliyotolewa na serikali ya Kenya kwa vyombo vya habari.
Ripoti ya UNESCO ya mwaka 2016 imeeleza kwamba binti mmoja kati ya 10 kwenye nchi zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara, anakosekana shuleni kwa siku ambazo yupo kwenye hedhi, kutokana na kukosa pedi za kujistiri.

Kutana na Mtaalam Sharif Hamad Kalala Mchambuzi wa Nyota za Binadamu na Tiba Asili

$
0
0

KUTANA NA SHARIF HAMAD KALALA NI
SHARIFU MCHAMBUZI WA
NYOTA ZA BINAADAMU NA NI MWENYE UPEO MKUBWA KUTAFITI MATATIZO YAKO KABLA YA KUTOA USHAURI WAKE WA TIBA AlJALISHI MBALI ULIKO TIBA YAKE UMFIKIA YEYOTE MWENYE UITAJI POPOTE
DUNIANI.

 SHARIF HAMAD KALALA NI TABIBU MWENYE KUBRI TOKA KWA ALAH ANATIBU KWA NJIA YA VITABU VYA QUR-AN, DAWA ZA ASILI ZA MITI SHAMBA PAMOJA NA DAWA ZA KIARABU.
ANATIBU KWA NJIA YA SIMU KWA KUTOA
MAELEKEZO NAMNA YA MATUMIZI YA DAWA UKIWA NCHI YOYOTE MKOA WOWOTE KWA MATATIZO YAFUATAYO:-

 KUFANIKISHA NDOA KWA UNAYE MPENDA KWA HARAKA. KUMRUDISHA MPEZI NDANI YA MASAA 12 TU.
 ULIJALI (NGUVU ZA KIUME) NDANI YA /IKI MMOJA TU 
MIGUU KUWAKA MOTO KUTAFSIRI NDOTO MFARAKANO WA WANANDOA MFARAKANO KAZINIKUPANDISHWA CHEO NDANI YA SIKU SABA 7 TU. 
KUTOA PETE YA BAHATI KUTOA MAJINI MACHAFU IKIWA NI KWENYE MWILI WA BINADAMU MAJUMBANI NA KWENYE BIASHARA. KUPATA MAFANIKIO YA MALI BILA YA MASHARTI. KUPANDIKIZANYOTA YA KUBASHIRI KUFUNGUA UZAZI KWA WALIYO FUNGWA KWA NJIA YA USHIRIKINA KUTOA VIFUNGO VYOTE VILIVYO FUNGWA KWENYE BIASHARA. ANA UWEZO MKUBWA WA KUPANDIKIZA NYOTA YA KUMPATA YEYOTE UMPENDAYE KWA KUMUOA AU KUWA NAYE. ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIYE MBALI PIA ALIYE CHUKULIWA
KWA NJIA YAMSUKULE
NAO UWEZO WA KUUA KESI SUGU NA MPYA NDANI SIKU 7 TU.
MENGINEYO MENGI ZAID YALIYO KUWA SUGU PIGA KWA WALE WALIYO ANGAIKA SEHEMU MBALI MBALI SHARIF HAMAD KALALA NI SULUISHO. ENDAPO UTAMSIKILIZA KWA YALE ATAKAYO KUSHAURI NA KUKUPA
ELEKEZI.
 TIBA NI KWA DINI ZOTE POPOTE ULIPO NJE NA NDANI YA NCHI.
MOBILE +255 -673 025 376
WhatsApp +255-757 069 066

Spika Job Ndugai Acharuka' Sitaki Wabunge Waingie Bungeni na Power Bank'

$
0
0

BUNGENI: Spika Job Ndugai amesema ameagiza Wabunge wasiingie na 'power bank' wala chaja za simu ndani ya ukumbi wa Bunge.

Hii ni kutokana na mlipuko uliotokea wakati wa kikao cha Bunge baada ya 'power bank' ya Mbunge wa Nsimbo, Richard Mbogo kupata hitilafu hali iliyopelekea kikao hicho cha Bunge kuahirishwa

Aidha Wabunge wamesisitiza Katibu wa Bunge afikirie kumpongeza Askari aliyejitoa mhanga na kuitoa nje 'power bank' iliyokuwa ikiwaka moto kwani alionesha ujasiri mkubwa .

Mwanamke Akamatwa na Kufungiwa Kwa Kosa la Kuwapa Wanawake Wenzake Mimba za Bandia

$
0
0

GUINEA: Mwanamke mmoja(N'na Camara) ambaye aliuza dawa za kienyeji kwa wagumba, akiwaambia kuwa wangepata mimba, amefungiwa miaka mitano kufanya kazi hiyo
-
N'na Fanta Camara anadaiwa kuwalaghai zaidi ya wanawake 700 kwa kutengeneza dawa ya kienyeji ambayo ilisababisha matumbo yao kufura na kuonekana kuwa ni wajawazito
-
Camara, alipatwa na hatia ya kuwapatia wanawake hao dawa zilizowadhuru na zilizoweka maisha yao hatarini. Aliagizwa kulipa fidia ya dola za Marekani 165,000
-
Mwaka 2006 shirika la afya duniani lilisema kuwa asilimia 80 ya waafrika walitumia matibabu ya kienyeji.

Baada ya Kumalizana na Twanga Pepeta Ally Choki Aamua Kupumzika na Familia Yake

$
0
0
Baada ya Kumalizana na Twanga Pepeta Ally Choki Aamua Kupumzika na Familia Yake
BAADA ya kumaliza mkataba na Bendi ya The African ‘Twanga Pepeta’, mwanamuziki Ally Choki amefunguka kuwa, hana mpango wa kuanzisha bendi kama alivyosema mwanzoni, bali anapumzika na kuangalia familia yake huku akiwa anafanya kazi na bendi nyingine.



Akibonga na Risasi Vibes, Choki alisema kuwa, anafanya kazi na Bendi ya The Mafiki huku muda mwingi akiutumia kwa ajili ya kuangalia familia zaidi na kuhofia kuanzisha bendi yake kutokana na hali halisi ya sasa, kwamba, muziki huo haulipi na bendi alishakuwa nayo, ikafa.



“Mwanzoni nilitamani kuirudisha bendi yangu ya Extra Bongo, lakini nimekuja kutafakari nikaamua niachane nayo tu maana nitaumia zaidi kwani kuwa na bendi kuna changamoto kubwa sana hivyo nitaendelea kufanya kazi na bendi za watu na kutulia na familia zaidi,” alisema.
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live




Latest Images