Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Mtangazaji wa Cloud Michael Lukindo aacha kazi ya utangazaji,aamua kufanya muziki...Afuata nyazo za kina Ray C

$
0
0
Kama wewe ni msikilizaji mzuri wa radio hasa Cloud Fm basi utakuwa unamfahamu au kuwahi kumsikia mtangazaji Michael Lukindo.
Habari ni kwamba Michael Lukindo ameamua kuachana na mambo ya utangazaji na kujikita katika masuala ya muziki kwa sababu ameona ana kipaji kizuri cha kuimba.

Michael lukindo ambae alifaamika kwa jina la Mr Infoma aliacha kusikika Cloud Fm tangu mwezi februari mwaka huu.

Maamuzi ya namna kama hiyo yamewahi kufanywa na wasanii Ray C na Vanessa mdee mabao waliacha kazi ya utangazaji na kuamua kujikita kwenye Muziki.

Kwa sasa Michael Lukindo anatamba na wimbo wake mpya aliouachia hivi karibuni unaoitwa "Basi iwe",unaweza kuupata kwenye YouTube channel yake ya Michael Lukindo.


Baba Amnywesha Sumu Mwanae Aliyezaa na Mchepuko Ili Kulinda ndoa

$
0
0
Mtoto wa miezi miwili (jina limehifadhiwa) mkazi wa Manispaa ya Shinyanga amedaiwa kunyeshwa sumu na baba yake mzazi kwa madai ya kutaka kuficha kizazi hicho ili mkewe asijue amezaa nje ya ndoa.

Akielezea makasa huo jana, mama mzazi wa mtoto huyo, Maria Shija (22) alisema lilitokea Machi 24, mwaka huu majira ya saa tatu usiku.

Maria alisema siku hiyo baba wa mtoto huyo, Edson Damian (37) alikwenda nyumbani kwao anapoishi yeye na mama yake kwa ajili ya kumsalimia mtoto huyo, na ndipo akamywesha sumu ya panya kwa lengo la kumuua wakiwa wamekaa nje.

Mzazi huyo alisema kabla ya mzazi mwenzake kufanya kitendo hicho, alikuwa akimtuma maji ya kunywa ndani mara kwa mara kitu ambacho si kawaida yake.

Alisema aliporudisha kikombe ndani mara ya mwishho ndipo akasikia harufu ya sumu ya panya, na aliporudi haraka kwa mtoto akamkuta ameanza kutoa mapovu na mwanaume huyo kukimbia.

“Baada ya kuona mtoto kapewa sumu nikakimbia kwa jirani ambaye ana zizi la ng’ombe, ndipo nikachukua maziwa nikamnywesha na baadae nikachukua bodaboda hadi kituo cha Polisi kupewa RB na kisha kwenda hospitali ya Rufani ya mkoa wa Shinyanga kupatiwa matibabu," alisema Maria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishina Msaidizi Simon Haule alithibisha kutokea kwa kisa hicho na kwamba mtuhumiwa huyo yupo mbaroni.

Alisema upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu shtaka linalomkabili.

Akielezea historia ya mapenzi yao, Maria alisema Damian wakati anamtaka kimapenzi alimwambia hana mke, lakini baada ya mtoto kuzaliwa akasema ana mke, hamtaki kwani atavunja ndoa yake.

Mtu wa karibu na familia ya Maria, Jumanne Kagusa alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi.

Kutana na Mtaalam Sharif Hamad Kalala Mchambuzi wa Nyota za Binadamu na Tiba Asili

$
0
0
KUTANA NA SHARIF HAMAD KALALA NI
SHARIFU MCHAMBUZI WA
NYOTA ZA BINAADAMU NA NI MWENYE UPEO MKUBWA KUTAFITI MATATIZO YAKO KABLA YA KUTOA USHAURI WAKE WA TIBA AlJALISHI MBALI ULIKO TIBA YAKE UMFIKIA YEYOTE MWENYE UITAJI POPOTE
DUNIANI.

 SHARIF HAMAD KALALA NI TABIBU MWENYE KUBRI TOKA KWA ALAH ANATIBU KWA NJIA YA VITABU VYA QUR-AN, DAWA ZA ASILI ZA MITI SHAMBA PAMOJA NA DAWA ZA KIARABU.
ANATIBU KWA NJIA YA SIMU KWA KUTOA
MAELEKEZO NAMNA YA MATUMIZI YA DAWA UKIWA NCHI YOYOTE MKOA WOWOTE KWA MATATIZO YAFUATAYO:-

 KUFANIKISHA NDOA KWA UNAYE MPENDA KWA HARAKA. KUMRUDISHA MPEZI NDANI YA MASAA 12 TU.
 ULIJALI (NGUVU ZA KIUME) NDANI YA /IKI MMOJA TU
MIGUU KUWAKA MOTO KUTAFSIRI NDOTO MFARAKANO WA WANANDOA MFARAKANO KAZINIKUPANDISHWA CHEO NDANI YA SIKU SABA 7 TU.
KUTOA PETE YA BAHATI KUTOA MAJINI MACHAFU IKIWA NI KWENYE MWILI WA BINADAMU MAJUMBANI NA KWENYE BIASHARA. KUPATA MAFANIKIO YA MALI BILA YA MASHARTI. KUPANDIKIZANYOTA YA KUBASHIRI KUFUNGUA UZAZI KWA WALIYO FUNGWA KWA NJIA YA USHIRIKINA KUTOA VIFUNGO VYOTE VILIVYO FUNGWA KWENYE BIASHARA. ANA UWEZO MKUBWA WA KUPANDIKIZA NYOTA YA KUMPATA YEYOTE UMPENDAYE KWA KUMUOA AU KUWA NAYE. ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIYE MBALI PIA ALIYE CHUKULIWA
KWA NJIA YAMSUKULE
NAO UWEZO WA KUUA KESI SUGU NA MPYA NDANI SIKU 7 TU.
MENGINEYO MENGI ZAID YALIYO KUWA SUGU PIGA KWA WALE WALIYO ANGAIKA SEHEMU MBALI MBALI SHARIF HAMAD KALALA NI SULUISHO. ENDAPO UTAMSIKILIZA KWA YALE ATAKAYO KUSHAURI NA KUKUPA
ELEKEZI.
 TIBA NI KWA DINI ZOTE POPOTE ULIPO NJE NA NDANI YA NCHI.
MOBILE +255 -673 025 376
WhatsApp +255-757 069 066

Wanaume 18 Wakubali Kupimwa DNA kwa Makonda

$
0
0
WANAUME 18 kati ya waliofika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuhojiwa kuhusu kutelekeza watoto wamekubali kupimwa vinasaba (DNA) na Mkemia Mkuu wa Serikali, taarifa iliyotolewa jana na Paul Makonda ilisema.

Makonda alisema hatua hiyo imefikiwa na wanasheria na maofisa ustawi wa jamii baada ya kuhoji wanaume waliodaiwa kuwatelekeza watoto, katika malalamiko yanayoendelea kutolewa na wanawake kuanzia Jumatatu katika ofisi hizo, Ilala.

Mkuu wa Mkoa Makonda alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea maendeleo ya zoezi linalomalizika leo.

"Jumla ya wanaume 18 ambao walibisha kuwa watoto sio wao wamekubali kwenda kupimwa DNA kwa Mkemia Mkuu ili kupata uthibitisho wa uhalali wa mzazi na hao ni kati ya wanaume 198 walioitikia wito na kuja ofisini kwangu," alisema Makonda.

Kadhalika, alisema kati ya wanaume 198 waliofika katika ofisi hizo baada ya kuandikiwa barua za wito, 179 walikubaliana na wanawake waliozaa nao mikakati ya kulea watoto husika.

"Familia 179 zimefikia muafaka," alisema Makonda na "haya ni mafanikio makubwa. Kama watu waliokuwa hawahudumii familia na leo hii wamekubali kuhudumia na kurudi nyumbani kwa amani, kazi hii imezaa matunda."

Makonda alisema kati ya wanaume 198 waliofika katika ofisi hizo kutafuta mwafaka, 19 kati yao mashauri yao yamepelekwa mahakamani ili kutafuta suluhu.

"Kazi inaendelea vizuri, tunaona mafanikio kwa sababu wanawake waliojitokeza ni wengi wanaokosa huduma kutoka kwa wanaume zao," alisema. "Wanaume waliopewa barua za wito nao wamekuja wakasilikizwa na mwafaka ukapatikana."

Pia alisema wanawake 1,498 wamejitokeza katika siku tatu kwa ajili ya kutoa malalamiko yao na kupewa msaada wa kisheria.Makonda alisema kutokana na kuwapo kwa idadi hiyo kubwa ya wanawake, wameongeza wanasheria 200 na maofisa ustawi wa jamii 60 na kusababisha kuwapo kwa watoa huduma 378.

"Kwa sababu ya mwitikio mkubwa wa wanawake, tumelazimika kuongeza wanasheria na maofisa ustawi wa jamii ili kazi hii ifanyike kwa haraka," alisema Makonda.

ZAMU YA WANAUMEAidha, Makonda alisema baada ya kusikiliza wanawake waliotelekezwa, kanzia Jumatatu itakuwa zamu ya wanaume ambao wameandikiwa barua za wito.

"Ingawa wapo baadhi ya wanaume ambao wameandikiwa barua za wito na wameshakuja kusikiliza walichoitiwa, kuanzia Jumatatu itakuwa ni siku ya kuwasikiliza baada ya kuwasikiliza wanawake," alisema Makonda.

Alisema wanaume ambao wamepewa wito huo wanatakiwa wajitokeze kusikiliza na endapo watakaidi hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Makonda pia aliwataka wanawake na wanaume wenye matatizo ya kutelekezewa watoto kweli wajitokeze katika ofisi hizo ili wapate msaada wa kisheria bure badala ya kuandika kwenye mitandao ya kijamii.

"Kama kweli mtu ana matatizo ni wajibu wake kuja hapa ili asikilizwe na kupatiwa msaada bure badala ya kuandika kwenye mitandao ya kijamii ambako hakuna majibu," alisema Makonda.

Leo ni siku ya mwisho ya kutoa msaada wa kisheria kwa wanawake ambao walitelekezewa watoto na wanaume waliozaa nao.

Mtoto Azaliwa Baada ya Wazazi Wake Kufariki Miaka Minne Nyuma

$
0
0
Katika hali ambayo imewashangaza watu wengi, inaripotiwa kuwa huko nchini China mtoto amezaliwa baada ya wazazi wake kufariki miaka minne iliyopita.

Hii imewezekana kutokana na mwanamke mmoja kupandikizwa kidaktari mbegu na yai vya wazazi hao ili abebe mimba hiyo.

Mwaka 2013 wazazi hao walitoa mayai hayo yaliyogandishwa kwa matumaini ya kupata mtoto kwa kupitia mfumo wa IVF lakini bahati mbaya walipata ajali kabla ya mayai hayo kutumika.

Kabla ya kufariki wawili hao walitoa ruhusa ya mayai hay

Nandy Aomba Radhi Kanisa Lake Baada ya Kuvuja kwa Video Akiwa Faragha na Bill Nasi

$
0
0
Nandy Aomba Radhi Kanisa Lake  Baada ya Kuvuja kwa Video Akiwa Faragha na Bill Nasi
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nandy ambaye hi leo amekutwa na balaa la kuvuja kwa video yake ya utupu, ameomba radhi kwa watu mbali mbali ikiwemo kanisa lake juu ya video hiyo, inayomuonyesha akiwa faragha na msanii mwenzake Bill Nas.


Akizungumza hilo Nandy amesema video hiyo ni ya mwaka 2016, na haelewi kwa nini mtu aliyeivujisha kaamua kufanya hivyo, lakini ni kitendo kilichomuumiza sana hivyo anaomba msamaha kwa jamii, mashabiki, kanisa na kila mtu ambaye imemgusa kwa namna moja au nyingine wamsamehe, kwani tayari anajutia jambo hilo.

“Nimesikitika sana, hiyo video ni ya ukweli ni ya mwaka 2016, nilikuwa na mahusiano na Bill Nas na tulikubaliana iwe siri, sasa sielewi kwa sababu gani kaamua kuvujisha, nimesikitishwa sana, ni video ambayo ilishutiwa kwa snapchat, sasa sielewi wakati ameipata hiyo video alikuwa nayo au alichukua mwenyewe, sijui niseme nini, naomba radhi sana kwa familia yangu, kanisani kwangu, serikali yangu, mashabiki, naomba radhi sana, adhabu ya maumivu ambayo nayapata imetokana na kumuamini mtu, ilikuwa ni private”, amesema Nandy.

Wawili hawa mara kwa mara walikuwa na skendo ya kuwa na mahusiano lakini wamekuwa wakikanusha, na watu kuanza kuibua hisia upya baada ya Nandy kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa Bill Nas kwa kupost picha inayomuonyesha akiwa kifuani kwake.

Yanga Mambo Magumu Mabosi Wakutana Usiku Kumjadili Lwandamina

$
0
0
KAMATI ya Utendaji ya Yanga, juzi usiku ilikutana haraka kujadili suala kuondoka kwa kocha wao Mzambia, George Lwandamina aliyejiunga na Klabu ya Zesco United ya nchini huko.

Taarifa zilizotolewa jana na Zesco ni kwamba wamemalizana na kocha huyo ambaye anachukua mikoba ya kocha wa muda, Tenant Chembo aliyejiuzulu Jumapili iliyopita.

Kocha huyo aliondoka juzi Jumanne na kurudi nyumbani kwao kwa ajili ya kusaini mkataba mpya wa kukinoa kikosi hicho.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili ya Yanga, Hussein Nyika alisema wajumbe wa kamati ya utendaji wote walikutana juzi baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida United uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.


“Ni mapema kuanza kulizungumzia suala la Lwandamina kwa sasa kwa sababu jana (juzi) kamati ya utendaji ilikutana kujadili ili kulipatia ufumbuzi suala hilo. “Hivyo, katika kikao hicho baadhi ya mambo tumejadili na kufi kia muafaka mzuri, hivyo ningepewa muda kidogo na baada ya kufi kia muafaka mzuri tutalitolea ufafanuzi,” alisema Nyika.

Aidha, imeelezwa kuwa kamati hiyo imekubaliana kumpitisha kocha wa viungo Noel Mwandila kusaidiana na Shadrack Nsajigwa katika kipindi hiki cha mpito.

Kulikua na Haja gani ya Kuhojiwa Uraia wa Nondo Ana Umaarufu Gani, Mnachafua Serikali tu- Ahmed Shabiby

$
0
0
Kulikua na Haja gani ya Kuhojiwa Uraia wa Nondo Ana Umaarufu Gani, Mnachafua Serikali tu- Ahmed Shabiby
Mbunge wa Gairo (CCM), Ahmed Shabiby, amesema hakuna umuhimu mamlaka za serikali kutumia vyombo vya habari kuwaita baadhi ya watu kwa ajili ya kuwahoji kutokana na tuhuma wanazokabiliwa nazo.

Shabiby amesema hayo Bungeni Mjini Dodoma jana Aprili 12, 2018  huku akitolea mfano tukio la Mwenyekiti wa TSNP ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu (UDSM), Abdul Nondo, ambaye aliitwa na Mamlaka ya Uhamiaji kwa ajili ya kuhojiwa uraia wake, na kusema kwamba vitendo hivyo vinaichafua serikali kwa kiasi kikubwa.

“Sasa hivi kuna watu kwenye Utumishi ambao wanafanya mambo ya kuichafua Serikali ya CCM, kulikuwa na haja gani ya kumita yule kijana Abdul Nondo kumhoji sijui alete cheti cha kuzaliwa cha bibi cheti cha mjomba, cheti cha babu? Mamlaka inashindwaje kufanya investigations zake (uchunguzi) ili kubaini ukweli mapaka iite wanahabari?

“Tunawapa watu umaarufu wakati kesi ipo polisi, ipo mahakamani, kuna watu wengine watatumia hiyo kitu kusema Serikali ya CCM ikimtaka mtu inamuomba uraia wake, sidhani kama Serikali ina haja na mtu mdogo kama yule ambaye hata hana madhara yoyote,” alisema Shabiby.

Familia ya Shehe Yahya Yagombea Maiti

$
0
0
Familia ya Shehe Yahya Yagombea Maiti

Hali ya sintofahamu imeibuka katika familia ya marehemu Shehe Yahya Hussein na familia ya Idarusi, baada ya kujikuta wakigombea maiti ya mume wa binti wa Shehe Yahya aitwaye Mariam Yahaya Husein, baada ya ndugu wa mumewe huyo kumuwekea ngumu kushiriki mazishi.



Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika ambaye yupo karibu na familia hiyo (hakupenda jina lake liandikwe gazetini), sakata hilo limefika pabaya kiasi kwamba mwili wa marehemu imebidi ushikiliwe na polisi mpaka pale watakapokubaliana nani azike.“Marehemu shehe Yahya ana binti aitwaye Mariam ni maarufu kwa jina la Mamu. Huyu alikuwa na mumewe aitwaye Idarusi na kwa pamoja wana watoto wawili.

“Huyo bwana kiukweli alikuwa na uwezo mzuri wa kifedha kwani aliwahi kufanya kazi Umoja wa Mataifa kama mtaalamu wa lugha na baada ya kustaafu alikuwa analipwa malipo mazuri tu ya kiinua mgongo.“Sasa kwa muda mrefu takribani miezi tisa huyo mumewe alikuwa anaumwa na Mariam, alikwenda naye India kwa ajili ya matibabu.“Huko, Mariam kahangaika naye kwelikweli lakini mwisho huyo mwanamme wiki iliyopita Aprili 5, alifariki dunia,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kiliendelea kueleza kwamba baada ya mumewe kufariki dunia, Mariam alirudi nchini na maiti ya mumewe kwa ajili ya taratibu za mazishi. Lakini alipofika shemeji zake walimwambia hatakiwi kufikia msibani badala yake anatakiwa kufikia hotelini, kwa hiyo akafikia Lamada.

Chanzo hicho kiliendelea kueleza kwamba akiwa hotelini hapo, ndugu wa marehemu walitaka kumzunguka ili waweze kuuchukua mwili na kuusafirisha mpaka Arusha kwa ajili ya mazishi.

“Si unajua tena mali za mirathi, mwenye cheti cha mazishi ndiye anaweza kufungua jalada la mirathi. Sasa michakato ya kubeba mwili kimyakimya ikiendelea na Mariam alitonywa.“Ikabidi aende uwanja wa ndege na kuzuia taratibu za kuchukua mwili kuendelea na kudai yeye ndiye ana haki ya kumzika mumewe kwani ndiye kamtoa India na amepata naye shida na si mtu mwingine.

“Hapo ndipo soo lilipoanzia na kutinga kwenye kituo cha polisi cha uwanjani hapo. Baadaye ndugu nao wakaamua kuibua suala lingine kwamba hawakubaliani na taarifa za msiba wa ndugu yao na wanahitaji mwili ufanyiwe uchunguzi, mwili ukachukuliwa na kupelekwa Muhimbili,” kilisema chanzo hicho.

Amani lilitinga nyumbani kwao Mariam, lakini pia halikuweza kumpata zaidi ya kukutana na kaka yake Mtabiri Maarufu nchini, Maalim Hassan Yahya Hussen ambaye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.“Ni kweli mlichosikia. Mariam ni mdogo wangu baba mmoja na mumewe huyo Idarusi ninamfahamu maana alimuoa kwa ndoa miaka takribani sita na wameishi muda mrefu nyumbani kwetu Magomeni.

“Wana watoto wawili na wiki iliyopita huyo mumewe alifariki dunia. Sasa familia ya mwanaume inaonekana ilikuwa haina mazungumzo mazuri na huyu mdogo wangu, ndipo kizaazaa kilipoanzia, kila mmoja anataka amzike marehemu imefikia hatua mpaka upande wa mwanaume wanataka mwili ufanyiwe uchunguzi kwani hawana imani na taarifa za kifo chake.

“Binafsi nimeombwa kuliingilia hili suala, kwa hiyo nitajitahidi marehemu afanyiwe uchunguzi Muhimbili kisha azikwe kwanza halafu mambo mengine kama ni ya mali na nini zifuatwe sheria lakini marehemu akiwa amekwishazikwa,” alisema Maalimu Hassan.Upande wa Idarusi pia hawakupatikana kutoa ushirikiano licha ya kuwapigia simu ndugu zake waitwao Aikal na Hassan, simu zao zilikuwa hazipokelewi.

Afisa mmoja wa Kituo cha Polisi cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambaye hakupenda jina lake kuandikwa gazetini kwa kuwa siyo msemaji alithibitisha kutokea kwa jambo hilo.

DRC Yasusia Mkutano wa Umoja wa Mataifa

$
0
0
DRC yasusia mkutano wa Umoja wa mataifa
Umoja wa mataifa hii leo unafanya mkutano maalum mjini Geneva Uswizi kuchangisha fedha za kukabiliana na janga la kibinaadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Mashirika ya misaada yanasema zaidi ya watu milioni 5 wamelazimika kuyatoroka makaazi yao kwasababu ya mapigano katika sehemu tofauti ya nchi hiyo kubwa.

Lakini serikali ya DRC imekataa kuhudhuria mkutano huo wa ufadhili ikisema kwamba hali inafanywa kuwa mbaya wakati ni kinyume cha hicho.

Mkutano huo umedhamiriwa kuchangisha dola bilioni 1.7 kupunguza uzito wa inachotajwa na Umoja wamataifa kuwa ni janga kubwa la binaadamu nchini Congo.

Mpaka sasa serikali ya DRC haijajibu mualiko wa Umoja wa mataifa ikisema taasisi hiyo kuu imetilia chumvi hali halisi nchini na ukubwa wa tatizo lililopo.

Mashirika ya misaada yanasema watu milioni tano wamelazimika kuyatoroka makaazi yao kutokana na ghasia, mapigano, njaa na ukosefu wa utulivu na kwamba maelfu ya raia wa Congo wamelazimika kutafuta hifadhi magharibi mwa Uganda.

Wanaharakati wa kutetea haki za binaadamu ndani ya DRC wamezusha wasiwasi kutokana na hatua hiyo ya serikali kususia mkutano huo mkuu mjini Geneva.

Wasiwasi wa aina hiyo pia umetolewa na baadhi ya raia wanoasema kwamba wataendelea kuteseka bila ya msaada wa kimataifa.

Je kuna hasara gani wa kwa serikali hiyo kukataa kuhudhuria mkutano wa Geneva?

Mashirika ya misaada yanasema DRC inateseka katika janga kubwa lenye uzito la kibinaadamu lililosahaulika kwa muda mrefu.

Kuna watu milioni 13 wanaohitaji usaidizi: miongoni mwao watoto milioni 2 wanaugua utapia mlo mbaya, na watu milioni 4.5 wamepoteza makaazi yao.

Maafisa hatahivyo wa Umoja wamataifa wanatumai kwamba wanadiplomasia wa Congo watabadili uamuzi wao na wahudhurie mkutano huo leo.

Ni wazi kwamba mkutano wenyewe utaendelea licha ya chochote kile kitachotokea, wanaharakati wanasema maisha ya mamilioni ya watu yamo hatarini.

Bulaya, Mdee Watekeleza Sharti la Dhamana Waripoti Polisi

$
0
0
Bulaya, Mdee Watekeleza Sharti la Dhamana Waripoti Polisi
Mwenyekiti wa BAWACHA na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Ester Bulaya (MB) wamewasili katika Kituo cha Polisi Kati jijini Dar es salaam.

Hatua ya Wabunge hao kuwasili leo Ijumaa, April 13 ni moja ya sharti la dhamana mabapo waliambiwa waripoti.

Viongozi Sita wa CHADEMA akiwemo Halima Mdee waliachiwa huru April 3 baada ya kutimiza masharti ya dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam.

Maneno ya Maua Sama Baada ya Kuvuja kwa Video ya Nandy Akiwa Kwenye Mahaba Mazito na Bill Nass

$
0
0
Maneno ya Maua Sama Baada ya Kuvuja kwa Video ya Nandy Akiwa Kwenye Mahaba Mazito na Bill Nass
Stori kubwa kwa sasa ambayo imechukua headlines za kutosha katika burudani Bongo, ni kusambaa kwa video ya Nandy na Bill Nass ambayo inawaonyesha wakiwa faragha.

Msanii Maua Sama katika mahojiano na 5 Selekt, EATV amesema kitu hicho kinaweza kumtokea mtu yeyote na anaamini video hiyo imesambaa kwa bahati mbaya.

“Nafikiri ile ni bahati mbaya inaweza kumtokea mtu mwingine yeyote japokuwa i cant say much lakini mimi naona kama imetokea bahati mbaya,” amesema Maua Sama.

Utakumbuka hapo jana Nandy aliomba radhi kwa mashabiki wake kwa kile kilichotokea; Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba radhi SANA SANA familia yangu, Ndugu zangu, Mashabiki wangu na Serikali kwa kilochotokea, bado siko sawa.. naomba mniombee uzima.

Chriss Mauki Ajitosa Sakata la Kuvuja Video ya Nandy na Bilinas Amtaka Waziri Mwakyembe Kuwachukulia Hatua

$
0
0
Chriss Mauki Ajitosa Sakata la Kuvuja Video ya Nandy na Bilinas Amtaka Waziri Mwakyembe Kuwachukulia Hatua
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na mshauri wa masuala mbalimbali ya mahusiano Dr. Chris Mauki amefunguka na kutoa maoni yake kuhusu sakata la wasanii Nandy pamoja na Bill Nas kufuatia kuvuja kwa video yao wakiwa faragha.


Mauki ameitaka Wizara inayohusika na masuala ya sanaa ichukue hatua dhidi ya wasanii hao ili kudumisha maadili na nidhamu katika jamii hususani kwa wasanii ambao ni kioo cha jamii na kusewa endapo watafanya hivyo basi litakuwa funzo kwa wasanii wengine na watu wengine katika jamii.

"Mheshimiwa waziri Mwakyembe, Naibu Waziri pamoja na baraza la sanaa chini ya ndugu Mwingereza. Tutaiona nia yenu ya dhati kabisa kwenye kudumisha maadili na nidhamu katika jamii na hususani kwa wasanii ambao wanajiita "kioo cha jamii" pale ambapo hamtoinyamazia hii hali ya kuanikwa mitandaoni matukio ambayo kiuhalisia yalihitaji privacy, ninasimama sehemu ya ndugu zao hao wahusika, sehemu ya wazazi wao, sehemu ya wadogo zao, na wengine wengi ambao waliwaona kama role models wao. Kulikoni majukwaani tuwaone kama vioo vya jamii na huku nyuma mitandaoni mnaiharibu kabisa ile picha mliyoichora machoni pa watanzania"

Aidha Mauki aliendelea kusisitiza kuwa "Kama ilivyoenea katika public basi tujulishwe katika public ni hatua gani za kinidhamu zinafuata na onyo kwa wengine wenye fikra finyu na chafu kama hawa wanaohalalisha tabia za kingono mitandaoni. Masikio ya wenye akili na hekima yanasubiri kusikia kutoka kwenu viongozi wetu wenye mpini" alisisitiza Chris Mauki

Baraka The Prince Rommy Jones na Naj Mambo ni Moto

$
0
0
Baada ya official Dj wa Diamond Platnumz na WCB kwa ujumla, Romyjones Kuanikwa akimtongoza mpenzi wa Baraka The prince huko Instagram unadhani nini kitafata? Je watamalizia tofauti zao kwa kuchambana mitandaoni ama watadeal kiuke kukunjana mashati?

VIDEO:

Okoa Ndoa yako Sasa...Umepungukiwa na Nguvu za Kiume na Unashindwa Kupanda Mlima Vizuri

$
0
0
OKOA NDOA YAKO SASA : JE UMEPUNGUKIWA NA NGUVU ZA KIUME AU UUME WAKO MDOGO AU MPENZI WAKO HAKUTIMIZII UTAKACHO:


Acha kujiona mpweke pale ukutanapo na mpenzi au mke wako kwa sababu ya kutokuwa na nguvu za kiume au Uume wako mdogo

Dawa YA MAPRO POWERA ndio dawa sahihi na tiba tosha kwa sasa Kutibu tatizo na kuponesha kabisa tatizo LA KUWAI KUFIKA KILELENI KABLA MWENZI WAKO BADO AJAKOJOA

KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOA NA MWILI KUCHOKA

UUME KUSINYAA NA KUWA LEGELEGE

KUUMWA NA TUMBO WAKATI UNAPOMALIZA KUFANYA TENDO

Dawa hii utumiwa ata na wazee wenye umri mkubwa na haina madhara yoyote

MAKAKANUA HII NI dawa ya maumbili madogo urefusha na kunenepesha saizi upendayo saiz 5-6-7-8 na unene sm 3-4-5 kwa mini huabiki kwa kuwa na UUME mdogo wai sasa upate tiba sahihi kabisa na ni tofauti na ulizowai kutumia :

Tunarudisha mke au mpenzi ndani ya masaa matatu tu zipo dawa za presha kisukali vidonda vya tumbo korodani iliyovimba dawa za uzazi tunapunguza matiti makubwa kitambi na mwili mkubwa dawa zipo FIKA OFISINI KWANGU MBAGALA ZAKHEMU KWA WATEJA AMBAO AMTAKUWA NA NAFASI YA KUJA OFISINI AU MLIO MKOANI MTALETEWA p

Piga simu 0743362017 au 0789234653

DR AGU

Vanessa Mdee Ampongeza Jux Baada ya Kulamba Dili China

$
0
0
Vanessa Mdee Ampongeza Jux Baada ya Kulamba Dili China
Hapo jana, April 12, 2018 Jux kupitia brand yake ya African Boy alisaini dili nchini China. Sasa mpenzi wake, Vanessa Mdee hajawa nyuma kwenye hilo.

Vanessa Mdee amempongeza Jux kwa hatua hiyo aliyopiga na kuwashukuru watu wote waliokuwa waki-support bidhaa za Jux kupitia African Boy. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Vanessa ameandika;

“We live in a world of endless possibilities. Hongera sana sana sana babe, umepambana sana kuijenga African Boy pamoja na Watanzania wote waliowahi ku-support brand yako ya kijanja, now it’s Money Time. God bless you with more Jux, nakuona mbali babi wewe piga kazi,” amesema Vanessa.

Soma Pia; Jux kupitia African Boy alamba dili China

Jux amesaini dili na kampuni  ya Vendome ya nchini China kwa ajili ya kuzalisha bidhaa zake kupitia brand ya African Boy ambayo ina bidhaa kama tisheti, kofia, viatu, mabegi n.k.

RC Gambo Apata Pigo Afiwa na Mama Yake Mzazi

$
0
0
RC Gambo Apata Pigo Afiwa na Mama Yake Mzazi
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amefiwa na mama yake mzazi usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya The Madras Medical Mission – Chennai nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.

RC Gambo lupitia mtao wake wa Instagram amethibitisha kifo hicho huku akieleza kuwa anahiaji maombi kwasababu huo ni mtihani mzito sana kwake.

Kwa masikitiko na uchungu mkubwa napenda kutangaza kifo Cha Mama yangu Mzazi ( Mama aliyenilea kwa kuuza uji) kilichotokea usiku wa leo kwenye hospitali ya The Madras Medical Mission – Chennai nchini India! Kama mtoto nilijitahidi kufanya kila lililowezekana ikiwa ni pamoja na kumpeleka Afrika Kusini kwa matibabu kabla ya India. Ni Imani yangu kuwa hata Mungu atakubali kuwa kama binadamu nilifanya kila lililowezekana Ila yeye kampenda zaidi! Niombeeni sana maana mtihani huu ni mzito sana kwangu sidhani kama nita uhimili!

Serikali Yafunguka Sababu ya Kukatika kwa Umeme

$
0
0
Serikali Yafunguka Sababu ya Kukatika kwa Umeme
Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Nishati imefunguka na kudai kukatika kwa umeme mara kwa mara kunatokana na sababu nyingi na wala sio kutokuwepo kwa umeme au miundo mbinu pekee yake kama baadhi ya wananchi wanavyokuwa wanafikilia.


Hayo yamebainishwa na Waziri wa Wizara hiyo, Dkt Medard Kalemani leo Aprili kwenye kikao cha tisa mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo linaendelea kufanyika Jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge Temeke (CUF), Mh. Abdallah Mtolea aliyetaka kujua sababu zinazopelekea kukatika kwa umeme jiji la Dar es Salaam kwa ujumla mara kwa mara.

"Kukatika kwa umeme kuna tokana na sababu nyingi, siyo kwa sababu ya kutokuwepo kwa umeme au miundombinu. Wakati mwingine ni kasoro ndogo ndogo, tunakiri kabisa zipo changamoto za maeneo machache za kukatika kwa umeme kwenye baadhi ya nyakati za muda. Tunachokiomba ni kutupa taarifa inapotokea hitilafu ya namna hiyo", amesema Dkt. Kalemani.

Kwa upande mwingine, Dkt. Kalemani amesema katika majuma mawili yaliyopita palikuwepo na tatizo la umeme katika maeneo ya Mbagala Jijini Dar es Salaam lakini kwa sasa wameimarisha tatizo hilo na suala la umeme katika maeneo hayo kuwa vizuri.

Polisi Wamng'ang'ania Ester Bulaya Wampeleka Mahabusu

$
0
0

Polisi Wamng'ang'ania Ester Bulaya Wampeleka Mahabusu
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Katibu wake, Dk. Vincent Mashinji wameondoka katika Kituo Kikuu cha Polisi central baada ya kuripoti, huku Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya ikidaiwa atalala mahabusu kwa ajili ya kufikishwa mahakamani.

Wengine waliondoka kituoni hapo ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Mashinji amesema kuwa wameripoti kituoni hapo kama walivyoamriwa na mahakama, lakini wameambiwa Mbunge Bulaya atabaki mahabusu kwa ajili ya upelelezi.

“Mbunge Bulaya amebaki mahabusu kwa sababu za kiupelelezi lakini tumeambiwa ataunganishwa katika shauri letu,” -Dk.Mashinji.

Khloe Kardashian Apata Mtoto wa Kike

$
0
0
Khloe Kardashian Apata Mtoto wa Kike
Staa maarufu kutokea Marekani Khloe Kardashian ambaye wengi wamemfahamu kupitia kipindi cha “The Kardashians” amebahatika kupata mtoto wa kike April 12,2018 akiwa na umri wa miaka 33 ikiwa baba wa mtoto huyo ni mchezaji wa NBA Tristan Thompson.



Tristan Thompson na Khloe Kardashian wamekuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu hadi kubahatika kupata mtoto wao wa kwanza na siku chache zilizopita Tristan aliingia kwenye headlines katika mitandao ya kijamii baada ya video kusambaa ikimuonyesha akiwa na wanawake wawili na kusemekana kuwa ni wapenzi wake.

Tristan alibahatika kupata mtoto wake wa kwanza na mwanamke mwingine kabla ya kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Khloe Kardashian na hivyo kwa sasa anafurahia kuwa baba mwenye watoto wawili.
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images