Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Download Hapa Application ya Udaku Special Uweze Soma Vimbwanga na Udaku Mtaani Kila Siku

$
0
0
Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Upya Application yetu ya UDAKU SPECIAL Maana ile ya Zamani Tutaifuta.

Kuna Marekebisho Makubwa tumeyafanya ikiwa na tatizo la Notification kutatuliwa

NB: App mpya ina Icon Nyekundu

 Bonyeza Hapa Chini

==>>Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>>
  

Diamond, Mobeto Wamerudiana au kiki?

$
0
0
MEVUJA! Video inayomuonyesha msanii maarufu wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Paltnumz’ na mzazi mwenzake, Hamisa Mobetto imesambaa mitandaoni ikiwaonyesha wawili hao wakipeana mahaba mazito kitandani.

Hii imetokea ikiwa ni wiki mbili tangu wawili hao walipokutana live kwenye Tuzo za SZIFF pale Mliamni City Dar ambapo Diamond alimkumbatia mwanamama huyo na kupigana mabusu motomoto mbele ya umati uliofika kushuhudia tukio la tuzo hizo.

Katika video inayosambaa inawaonyesha wawili hao wakiwa kitandani wakijiachia, huku mashabiki mitandaoni wakieleza kwamba huenda wamerudiana ili kulea mtoto wao.

" CCM Wamemtelekeza Mzee Makamba" January Afunguka

$
0
0
JANUARY Makamba, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira ametoa madai mazito kwa chama chake, kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemtelekeza baba yake Mzee Yusuph Makamba akiwa mgonjwa.

Makamba ameandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook, akielezea hali ya baba yake kiafya na kusema pamoja na kupitia hali hiyo lakini CCM hakimpi stahiki zake kama mstaafu wa chama hicho.

Mzee Makamba ameshika nafasi mbalimbali katika chama lakini kikubwa zaidi ni kuwa Katibu Mkuu cha chama hicho, pamoja na nafasi mbalimbali serikalini ikiwemo Mkuu wa mikoa mbalimbali ukiwemo Dar es Salaam.


Katika taarifa hiyo ya January pia imeeleza tuhuma za wanasiasa aliowalea Mzee Makamba ambao mmoja wao kwa sasa anasema maneno mabaya dhidi ya mzee huyo.

Soma andiko la January hapa chini:

Majuzi nilienda kumjulia hali Mzee Makamba ambaye anaumwa. Mazungumzo yake yalihusu watoto wake aliowalea kisiasa, ambapo mmoja wapo, pamoja na kumhifadhi na kumfariji wakati kasahaulika, sasa anasema maneno mabaya dhidi yake.

Tukazungumzia subira na uvumilivu kwenye siasa. Akaamua kunipa kisa kifuatacho:

Mwaka 1980, baada ya kutoka vitani, alipangwa kuwa Katibu Msaidizi wa CCM Dodoma. Mwaka 1982, wakati wa kuadhimisha miaka 5 ya kuzaliwa kwa CCM kimkoa kule Mvumi, alitumwa mnadani Mwitikira kununua kitoweo (ng’ombe na mbuzi) kwa ajili ya sherehe.

Baada ya muda, akiwa kahamishiwa Monduli, akapewa barua ya kusimamishwa utumishi na uongozi (u-NEC) wa CCM kwa tuhuma kwamba wale ng’ombe na mbuzi wa sherehe aliwaswaga kwetu Bumbuli badala ya kuwapeleka Mvumi.

Tukafungasha mizigo na kurudi kijijini. Wakati Mzee anaendelea kutafuta maisha kijijini alikuwa anaandika barua kila siku Ikulu kwa Mwalimu Nyerere kueleza kwamba ameonewa. Baada ya barua kadhaa, Mwalimu akaagiza aitwe kwenye kikao cha Kamati Kuu Chamwino Dodoma. Mzee aliwasili Dodoma akiwa kachoka sana, amebeba makabrasha yake kwenye mfuko wa rambo.Makambazzz

Kikao kilipoanza, Mwalimu akampa nafasi Mzee Makamba ya kujieleza. Mzee akaanza kwa kusema ana hoja nyingi kuonyesha kaonewa lakini angependa kuanza na swali dogo: “Kwenye ile sherehe, Ndugu Moses Nnauye alikuwa mgeni rasmi na alikula ubwabwa. Ndugu Mwenyekiti, naomba aulizwe iwapo ubwabwa ule aliokula ulikuwa na nyama au la.” Mwalimu akamgeukia Nnauye na kumuuliza “Moses, Yusuf anauliza iwapo ubwabwa uliokula ulikuwa na nyama.” Nnauye akasimama na kujibu “Mwenyekiti, ubwabwa ulikuwa na nyama.” Mzee akaendelea “iwapo niliswaga ng’ombe kijijini kwetu, hiyo nyama kwenye ubwabwa ilitoka wapi?” Mwalimu akawageukia watendaji waliotengeneza mashtaka ili watoe majibu. Kukawa hakuna jibu. Baada ya Mzee kujieleza tena kwa kifupi ikadhihirika wazi kabisa kwamba kulikuwa na uonevu mkubwa. Akarudishwa kazini.

Wakati Mzee ananipa kisa hiki, alikuwa anajichoma sindano ya “insulin” kudhibiti kisukari, huku akigusa jicho lake moja ambalo linakaribia kuwa pofu. Amegoma kabisa kutibu jicho akisema “hata likiacha kuona, sio tatizo kabisa; limeshaona mengi humu duniani”

Kwa sasa Mzee hali yake kiafya sio nzuri chama cha mapinduzi hakimpi stahiki zake kama mstaafu.
Source:Mwanahalisi

Kufuli la Nandy Lilivyoacha Gumzo Mitandaoni Wiki Nzima

$
0
0
KEJELI na vijembe vimetawala wikiendi iliyopita baada ya kuvuja kwa video ya wasanii wa Bongo Fleva, Faustine Charles ‘Nandy’ na William Nicholas Limo ‘Billnas’ wakiwa kwenye mahaba mazito huku nguo ya ndani ‘kufuli’ ya mwanadada huyo ikiwa ndiyo gumzo kila kona mitandaoni.

Kufuli hilo la rangi ya pinki liligeuka ishu baada ya baadhi ya watu na wachekeshaji kuwa wanaliigiza kutokana na ukubwa wake.

 Wapo baadhi ya mastaa wakubwa Bongo hasa wale wa vichekesho ambao walitupia mitandaoni aina mbali-mbali za nguo hizo, lakini zenyewe zikiwa ni kubwa kupitia kiasi huku wengine wakiacha bila kuweka neno lolote.

Katika sakata hilo, Nandy amekwishajisalimisha Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) na kuomba radhi kufuatia skendo hiyo.

IMELDA MTEMA

SOMA Nafasi za Ajira Nyingi Zilizotangazwa Leo Jumatatu

Okoa Ndoa yako Sasa...Umepungukiwa na Nguvu za Kiume na Unashindwa Kupanda Mlima Vizuri

$
0
0
OKOA NDOA YAKO SASA : JE UMEPUNGUKIWA NA NGUVU ZA KIUME AU UUME WAKO MDOGO AU MPENZI WAKO HAKUTIMIZII UTAKACHO:


Acha kujiona mpweke pale ukutanapo na mpenzi au mke wako kwa sababu ya kutokuwa na nguvu za kiume au Uume wako mdogo

Dawa YA MAPRO POWERA ndio dawa sahihi na tiba tosha kwa sasa Kutibu tatizo na kuponesha kabisa tatizo LA KUWAI KUFIKA KILELENI KABLA MWENZI WAKO BADO AJAKOJOA

KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOA NA MWILI KUCHOKA

UUME KUSINYAA NA KUWA LEGELEGE

KUUMWA NA TUMBO WAKATI UNAPOMALIZA KUFANYA TENDO

Dawa hii utumiwa ata na wazee wenye umri mkubwa na haina madhara yoyote

MAKAKANUA HII NI dawa ya maumbili madogo urefusha na kunenepesha saizi upendayo saiz 5-6-7-8 na unene sm 3-4-5 kwa mini huabiki kwa kuwa na UUME mdogo wai sasa upate tiba sahihi kabisa na ni tofauti na ulizowai kutumia :

Tunarudisha mke au mpenzi ndani ya masaa matatu tu zipo dawa za presha kisukali vidonda vya tumbo korodani iliyovimba dawa za uzazi tunapunguza matiti makubwa kitambi na mwili mkubwa dawa zipo FIKA OFISINI KWANGU MBAGALA ZAKHEMU KWA WATEJA AMBAO AMTAKUWA NA NAFASI YA KUJA OFISINI AU MLIO MKOANI MTALETEWA p

Piga simu 0743362017 au 0789234653

DR AGU

Julio 'Simba Ikimfunga Yanga Inachukua Ubingwa'

$
0
0
KOCHA Mkuu wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, amesema kama Simba itafanikiwa kushinda mechi zake mbili zijazo ikiwemo ya Yanga basi itakuwa imeshatwaa ubingwa wa msimu huu kutokana na kasi waliyonayo.

 Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 55, nyuma ya Yanga inay­oshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 47. Azam kabla ya mechi ya jana ilikuwa na pointi 45 katika nafasi ya tatu.

Tayari Simba imebakiza mechi saba ambazo sawa na pointi 21 wakati Yanga ikiwa ina mechi nane sawa 24.

Akizungumza na Cham­pioni Jumatatu, Julio alisema: “Unajua kila kitu mipango, Simba sasa hivi ni wakati wao, wapo vizuri na wanastahili kuendelea kushin­da kwa sababu kikosi chao kipo vizuri, kama wakiendelea na kasi hii kwa kushinda mechi mbili zijazo ikiwemo ya Yanga basi wa­takuwa mabingwa na hilo halina mjadala.

 “Nadhani Yanga kwa sasa ingeachana na suala la ubingwa na kuendelea kuijenga timu yao kwa sababu imenifurahisha falsafa yao kutoa nafasi kwa vijana ambao naamini watakuja kuwa tishio katika msimu ujao kama ilivyofanya Simba miaka iliopita.”

 Ibrahim Mussa, Dar es Salaam

Huwa Napata Shida sana Nikikutana na Wanawake Wenye Hii Tabia

$
0
0
Huwa napata shida sana nikikutana na Wanawake wenye hii tabia...Unampenda Mwanamke kabisa from ur heart,unajipanga unampiga saundi..anakujibu,''How old are you kaka'' unamwambia am 29 years..utamsikia,''Oh my Ghosh,ur still a kid,mi nadate guys who are 45 years above...Wanajua kupenda,they are so caring, yaani nyie vijana mnasumbua sana''.Sio tunasumbua,anajua kabisa miaka 29 bado ndo unasaka hela, ndo umeanza maisha huna cha kumhonga, ukijitahidi sanaaa utampeleka shopping Karume na hiyo hela itakuuma kishenzi!

Anakuita Kid bila aibu wakati yeye ana miaka 23 tu halafu eti ana mahaba na jitu la miaka 47..Uongo mtupu!Ina maana mtu hawezi kupenda na kucare hadi afike miaka 45?? Nyie semeni tu mnawalia timing coz mnajua mtu mwenye miaka 45 anakuwa ameshajipanga, amefanya kazi ana hela, unajifanya unampenda kumbe Parasite tu unataka kumnyonyoa mafao yake ya uzeeni,hamna hata aibu..

Mnapenda sana vitu ready made,tengenezeni vya kwenu,ukiona mtu ana miaka 45 jua kuna Mwanamke mwenzio amefanya kazi kumfikisha hapo alipo,we unakuja unadandia tu

Kama kweli una mahaba tafuta mwanaume wako,panda nae daladala za Buguruni mrukie wote dirishani, msotee maisha kwa kutembelea TZ 11 hadi siku apate gari mfaidi wote halafu akifika miaka 45 uone kimwanamke cha IFM kinamsogelea eti he is caring uone inavyouma, utatamani umpige patasi ya kisogo...Gold diggers, waone kwanza, msione gesi mtwara mshaanza kuandamana 45years guy waiting for u student of 23 years, ina maana miaka yote hiyo alikuwa Stevie Wonder au??

Jipange Dada Usidhani Ndoa ni Kama Kupiga Picha Huku Umejibinua Makalio

$
0
0
Umepata bwana, umempenda kweli kweli na umemlalamikia sana eti kwanini hakupeleki kwa wazazi wake kukutambulisha, jamaa akagoma sana mwishowe akaona isiwe kesi akakupeleka.

Wewe badala hata utake hiyo advantage umefika tu siku ya kwanza umeshinda unachati, siku ya pili umeshinda unachati tena ndio unajisifia kwenye groups upo ukweni kumbe wao wanakutazama tu na kukupimia wala hawakwambii kitu.

Siku ya tatu wanakwambia leo ni zamu yako kupika, unaingia jikoni unaona kila kitu kigeni vya huku unaweka kule, vya kule unaweka huku (yaani hujui kupika chochote)

Sufuria unashika kama umeshika power bank, unapika na lipstick, mdomo mwekundu utafikiri mtoto wa jini katoka kufundishwa kunyonya damu tena huku umevaa saa, umevaa culture zimejaa nusu ya mkono, umevaa mini skirt kama wafanyakazi wa Emirates.

Msosi wa wakwe huwezi kupika. Ukiambiwa hufai kuolewa unavuta mdomo utafikiri umenyimwa USB cable ubust smartphone yako.

Unaanza kulalamika wakwe hawakupendi, unalalamika wee, unashindwa kuelewa kuwa wewe ndo tatizo.

Usitake kuolewa ukidhani mumeo atakula chips na wewe utakuwa utakula pizza kila siku, jifunze hata kuchemsha chai basi au unadhani google wataleta app ambayo unaweka USB kwenye simu yako alafu unaielekezea kwenye sahani inaproduce msosi.

#Jipange dada usidhani ndoa ni kama kupiga picha huku umejibinua makalio

Polisi Wawashikilia Wanafunzi Tisa wa Chuo Kikuu kwa Kuhamasisha Maandamaono

$
0
0
Polisi Wawashikilia Wanafunzi Tisa wa Chuo Kikuu kwa Kuhamasisha Maandamaono
Wanafunzi tisa wa Chuo Kikuu cha Stella Maris na Daktari wa Hospitali ya Mission Nanyamba wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara kwa tuhuma za kumkashifu Rais John Magufuli na kuhamasisha maandamano ya April 26.



Kamanda wa Polisi mkoani humo, Lucas Mkondya akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki alisema watuhumiwa hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakitumia mtandao wa kijamii wa WhatsApp na Telegram kumkashifu Rais na kuhamasisha maandamano hayo.

Kamanda Mkondya bila kutaja majina ya watuhumiwa hao kwa madai ya sababu za kiupelelezi, alisema daktari huyo ni kutoka Halmashauri ya mji wa Nanyamba.

“Ninatoa onyo watu wajiepusha kutumia mitandao ya kijamii vibaya na kusababisha uvunjifu wa sheria za nchi. Watuhumiwa wote tunawashikilia kwa upelelezi zaidi,” alisema.

Katika tukio lingine, Kamanda Mkondya alisema wanawashikilia wahamiaji haramu 23 waliokutwa katika nyumba ya kulala wageni eneo la Chikongola, Wilaya ya Mtwara.

Mke wa Rommy Jones Afunguka Mazito Mumewe Kumtongoza Naj

$
0
0
Mke wa Rommy Jones Afunguka Mazito Mumewe Kumtongoza Naj
WIKIENDI iliyopita, mume wa mtu, Romeo Jones ‘Rommy’ ambaye ni kaka na DJ wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alichafuka kufuatia meseji zake akimtongoza msanii wa Bongo Fleva, Najma Dattan ‘Naj’ kuvuja ambapo ilisemekana kuwa, mkewe Kahuye Jord almaarufu Kay Jord alimaindi na kusababisha ndoa yao kutikisika.


Kwenye meseji hizo, Rommy anamtaka kimapenzi Naj ambaye ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Baraka Andrew ‘Barakah The Prince’ ambapo zilionesha akimponda na kudai Barakah anamshusha nyota yake.

Kufuatia skendo hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta mke wa Rommy na kumuuliza analichukuliaje suala hilo ambapo alifunguka kwa mara ya kwanza tangu kuzagaa kwa tuhuma hizo nzito dhidi ya mumewe.

Kay Jord alifunguka kuwa, kwenye meseji hizo zilizodaiwa kwamba mumewe alikuwa akimtongoza Najma, haziendani na ukweli kwani asilimia kubwa zilionekana ulikuwa ni utani.

“Nimesikia na watu wamesema mengi kuwa mimi nimeondoka nyumbani, kisa hizo meseji, jambo ambalo siyo kweli kabisa.

“Hakuna ukweli kwenye jambo hilo ndiyo maana niliamua kukaa kimya,” alisema mke huyo wa Rommy.

Mwanamama huyo alisema kuwa, yuko vizuri kwenye ndoa yake kama kawaida na hakuna ambacho kimetetereka.



Kwa upande wake, Rommy alilieleza Ijumaa Wikienda kuwa, yeye ni mfanyabiashara na Najma wanafahamiana vizuri.

Alisema kuwa, kuhusiana na hizo meseji anazodai kumtongoza Naj ilikuwa ni utani wa kawaida tu.

Rommy na Barakah waliingia kwenye mgogoro mzito baada ya Barakah kuonesha meseji hizo kwenye mitandao ya kijamii huku akimtukana na kudai kuwa, Rommy alikuwa akimtongoza mpenzi wake huyo.

Zanzibar Yafungiwa Michuano ya CECAFA

$
0
0
Zanzibar Yafungiwa Michuano ya CECAFA
Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Zanzibar (Karume Boys), imefungiwa mwaka mmoja kushiriki michuano ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Cup U17.


Mbali na kifungo hicho lakini pia timu hiyo  imepigwa  faini ya dola za Kimarekani 15,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 30, kwa kosa la kupeleka wachezaji waliozidi umri.

Michuano ya CECAFA Challenge Cup U17 inaendelea nchini Burundi na Zanzibar inadaiwa kuorodhesha wachezaji waliozaliwa kabla ya Januari 1 mwaka 2002, ambao wazi wamezidi umri unaotakiwa wa miaka 17.

Kwa kifungo hicho ni wazi Karume Boys watalazimika kusubiri hadi mwaka 2020 endapo watafuzu kucheza fainali hizo kutokana na michuano hiyo kuchezwa kila baada ya miaka miwili na kifungo hicho kinafanyakazi pale timu inapofuzu.



Kwa upande wa ndugu zao vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Tanzania Bara, Serengeti Boys jana wamecheza na Uagnda na kutoa sare ya 1-1 katika mechi yake kwanza ya michuano hiyo.

Koffi Olomida Aalikwa Kenya Kufanya Shoo

$
0
0
Koffi Olomida Aalikwa Kenya Kufanya Shoo
Mwanamuziki Koffi Olomide ametangaza kuwa na onyesho la muziki mwezi huu tarehe 24 nchini Kenya.

Onyesho hili litakuwa la kwanza nchini Kenya tangu alivyokataliwa kuingia nchini humo Julai 2016 baada ya kumdhalilisha mmoja wa wanenguaji wake .

Koffi amesema hayo katika ujumbe wa video kwamba amealikwa kufanya onyesho katika mkutano wa taifa la Kenya ambao utajumuisha viongozi 47 wa nchi hiyo ambao ni mjumuisho wa rais na viongozi wa juu wa serikali.

Mshairi kufungwa jela kwa kuhamasisha umoja Somalia
Mwanamuziki huyo Koffi Olomide anayefanya muziki wa lingala mwenye umri wa miaka 61, aliomba radhi mara kadhaa kutokana na utovu wa nidhamu aliouonyesha nchini Kenya kwa kumpiga mnenguaji wake.

Katika tangazo la video lilowekwa kwenye mtandao wa Youtube inayotambulisha ziara yake mpya ya muziki,Koffi ameonekana akiwaambia mashabiki wake wa Kenya kuwa anawapenda sana na anawakumbuka sana

Tukio lililomtia utatani lilirekodiwa katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta ambako alikuwa amewasili kwa tamasha lilopangwa kufanyika nchini Kenya.

Wengi wa Wakenya walimkashifu vikali kitendo hicho huku maoni katika mitandao ya kijamii, kutpita mada ya #KickKoffiOlomideBackToCongo kwenye Twitter walipendekeza afurushwe kutoka Kenya.

Olomide aliwahi kujitetea kwa kusema kuwa alikuwa akijaribu kumtetea mwanamke huyo kwani mmoja wa maafisa wa kike katika uwanja huo wa ndege alikuwa akiwasumbua wasichana hao wachezaji ngoma aliokuwa wakiandamana naye.

Makonda Awatahadharisha Wakazi wa Dar

$
0
0
Makonda Awatahadharisha Wakazi wa Dar
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa tahadhari kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kuchukua tahadhari kwa mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo na kuwataka kukaa maeneo salama kwa ajili ya usalama wao na mali zao kwa ujumla.


Akizungumza na waandishi wa habari, Makonda amesema kuwa utabiri wa hali ya hewa unaonyesha kuwa leo Aprili 16, 2018 mvua hizo zitakua kubwa zaidi hivyo wananchi hawana budi kuchukua tahadhari mapema zaidi.

"Katika mvua hizo zilizonyesha kwa muda wa siku mbili mfululizo zimeshaleta madhara kadhaa katika baadhi ya maeneo hivyo ili madhara zaidi yasiweze kujitokeza wakazi wa Mkoa huo wa Dar es Salaam hawanabudi kuchukua tahadhari mapema zaidi", amesema Makonda.

Mbowe Ampongeza Fatuma Karume kwa Kuchaguliwa Rais wa TLS

$
0
0
Mbowe Ampongeza Fatuma Karume kwa Kuchaguliwa Rais wa TLS
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe amempongeza Fatma Karume baada ya kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa TLS.



Soma taarifa kamili;

Rais wa Ufaransa Amtaka Trump Asiondoe Vikosi vya Askari Syria

$
0
0
Rais wa Ufaransa Amtaka Trump Asiondoe Vikosi vya Askari Syria
Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amesema amemshamwishi Rais wa Marekani Donald Trump, asiviondoe vikosi vya askari wa Marekani vilivyoko nchini Syria.

Mapema mwezi huu, Rais Trump alisema kwamba ataviondoa vikosi vya askari wake vipatavyo elfu mbili ambavyo vilitumwa nchini Syria hivi karibuni.

Ingawa Rais wa Macron amewaambia waandishi habari nchini kwamba amezungumza na rais Trump kabla ya shambulizi la anga lililotekelezwa mwisho mwa juma lililopita na kumtaka ashiriki kutafuta suluhu ya mgogoro huo kwa muda mrefu zaidi.

Akitolea ufafanuzi juu ya shambulio hilo la anga lililotekelezwa kwa pamoja baina ya Marekani, Ufaransa na Uingereza kwamba lilikuwa la halali.

Uda-rt Yafunga Barabara ya Jangwani

$
0
0
Uda-rt Yafunga Barabara ya Jangwani
Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (Uda-rt), imelazimika kusitisha huduma kwa baadhi ya njia.

Taarifa ya Uda-rt imesema huduma za mabasi hayo kwa baadhi ya njia zimesitishwa kuanzia saa 11:00 alfajiri leo Jumatatu Aprili 16, 2018 kutokana na kufungwa Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani.

Barabara hiyo imefungwa kwa sababu ya mafuriko yaliyosababisha maji kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi.

“Kwa sasa huduma zinatolewa kwa njia za Mbezi – Kimara; Kimara – Morocco; Kimara - Magomeni Mapipa; Kivukoni – Muhimbili; Gerezani – Kivukoni; na Gerezani – Muhimbili,” inasema taarifa ya Uda-rt iliyotolewa na mkuu wa kitengo cha mawasiliano, Deus Bugaywa.

Kampuni hiyo inasema huduma kamili zitarejea baada ya barabara kufunguliwa.

Mama Mobeto Ataka Hamisa Aolewe na Mwanaume Huyu

$
0
0
Mama Mobeto Ataka Hamisa Aolewe na Mwanaume Huyu
Mama wa mwanamitindo, Hamisa Mobeto, Shufaa Rutiginga amesema katika maisha yake alikuwa anamuombea  mtoto wake huyo aolewe na mzungu.

Akizungumza na MCL Digital, Shufaa amesema sababu ya kutaka aolewe na mtu wa aina hiyo ni kutokana na wanaume wa kiafrika kutokuwa na mapenzi ya kweli.

“Unajua mtoto wangu ni mzuri, mrefu ana  shingo  nzuri nataka mwanaume atakayemuoa amuangalie kama malaika, kama malkia kwa kuwa ni mwanamke mwenye misimamo yake na ametulia sio muhuni kama watu wanavyomfikia.

“Wazungu hawana ‘stress’ wanajua namna ya kujali mwanamke, hawanaga mambo ya longolongo linapokuja suala zima la mapenzi tofauti na wanaume wetu wa kiafrika,”amesema.

Kuhusu suala la kuzaa na wanaume tofauti, mama Hamisa amesema hilo kwake halimpi shida na angependa amletee wajukuu wengi zaidi kwa kuwa yeye alijaliwa kumzaa peke yake na kudai kwamba hao ndio ndugu zake.

Ni kutokana na hilo, amesema anatamani amzalie watoto sita, kwa kuwa sasa hivi ana nguvu za kulea wajukuu zake na siku hayupo duniani hao ndio watakuwa ndugu zake na kuweza kumsaidia.

Mpaka sasa Hamisa ana watoto wawili.

Ikulu Yakanusha Taarifa ya Tuzo ya Inayodaiwa Kushinda Magufuli

$
0
0
Ikulu Yakanusha Taarifa ya Tuzo ya Inayodaiwa Kushinda Magufuli
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, nchini Bwana Gerson Msigwa, amesema haiana taarifa juu ya tuzo aliyoshinda Rais Magufuli nchini Ghana, kama kiongozi bora barani Afrika.


Akizungumza na www.eatv.tv Msigwa amesema kuwa utaratibu wa tuzo yoyote lazima mtu anayepewa apewe taarifa rasmi, lakini mpaka sasa hawajapokea taarifa yoyote kutoka kwa waandaaji wa tuzo hizo, hivyo hawajui lolote kama ni kweli ama la.

“Hatuna taarifa ya tuzo hiyo, tunavyojua ni kwamba mtu yeyote anayepewa tuzo lazima apewe taarifa rasmi kutoka kwa watoaji, sasa hatujapata taarifa yoyote mpaka sasa, nasikia ndio tuzo ambazo kina Monalisa wameshinda, lakini hatujapokea taarifa rasmi kuhusu tuzo hiyo, hivyo siwezi nikaizungumzia”, amesema Msigwa.

Tuzo hiyo ambayo imetajwa kuwa ameshinda Rais Magufuli, imetolewa Aprili 15, 2018 jijini Accra nchini Ghana, ambapo pia Watanzania wengine katika tasnia ya filamu waliibuka washindi akiwemo Monalisa (Yvone Chery) na Ray Kigosi.

Naibu Spika: Hakuna Dhambi Kujadili Ripoti ya CAG

$
0
0
Naibu Spika:Hakuna Dhambi Kujadili Ripoti ya CAG
Wakati mjadala ukiendelea kuhusu mawaziri kujibu hoja zilizoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), viongozi hao wameendelea kutoa ufafanuzi.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina na wa Kilimo, Dk Charles Tizeba leo Jumatatu Aprili 16, 2018 wametoa ufafanuzi wa hoja kuhusu wizara zao mjini Dodoma.

Kabla ya Mpina na Dk Tizeba kutoa ufafanuzi; Waziri wa Habari, Dk Harrison Mwakyembe alisema sheria ya ukaguzi wa hesabu haimzuii waziri kueleza kilichoainishwa katika ripoti ya CAG.

“Hakuna dhambi kutoa maelezo maana ukaguzi wake ni wa mwaka 2016/17. Hivi tangu wakati huo mpaka sasa ina maana wizara haijafanya chochote kuhusu kilichoelezwa,” amehoji Dk Mwakyembe.

Amesema wanamuunga mkono CAG na kupongeza ripoti yake ndiyo maana kila mwaka wanazidi kufanya vizuri.

“Hati chafu zilikuwa nyingi miaka ya nyuma lakini safari hii hati chafu zipo tatu tu na wote wenye hati chafu wameshughulikiwa,” amesema Dk Mwakyembe.

Amesema wana wajibu kama Serikali kuwapa wananchi taarifa kwa mambo yanayowahusu.

Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson alisema kujadili taarifa ya ukaguzi ya CAG si dhambi, ila kwa mawaziri wanapaswa kutoa majibu katika kamati za Bunge na wanachokifanya sasa ni kutoa maoni binafsi.

Dk Tulia ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Aprili 16, 2018 alipojibu mwongozo wa wabunge Stanslaus Mabula (Nyamagana) na Goodluck Mlinga (Ulanga) waliohoji kama ni sahihi mawaziri kujibu taarifa ya CAG kwa maelezo kuwa majibu yao yanawachanganya wananchi.

Katika ufafanuzi, Dk Tulia amesema kinachofanywa na mawaziri ni sahihi lakini hayo ni maoni yao binafsi, kwa kuwa kwa mujibu wa sheria ya ukaguzi, wanapaswa kutoa majibu katika vikao vya kamati za Bunge.

“Sheria kama ambavyo haimkatazi CAG kuzungumza na vyombo vya habari kwa namna hiyohiyo haimkatazi mtu yeyote kuzungumzia taarifa ya CAG, haijasema CAG azungumze na vyombo vya habari na pia haijamkataza mtu yeyote kuzungumzia taarifa hii,” amesema Dk Tulia.

Amesema, “Ndiyo maana vyama vya siasa vingine vimeshaeleza kile vinachoona inafaa. Sheria hizi mkizipitia waheshimiwa wabunge majibu huwa hayatolewi kwa mdomo. Waziri anatoa mawazo yake.”

Amesema anayepeleka taarifa ya CAG bungeni ni waziri, kwamba CAG hana mahali pa kupeleka hiyo taarifa isipokuwa kupitia kwa waziri.

“Kwa hivyo waziri anavyotoa maelezo si kwamba amejibu hoja za CAG, hoja za CAG zinajibiwa kwenye kamati kwa mujibu wa sheria, anayejibu kwenye kamati ni ofisa masuhuli husika,” amesema.

“Msitake kuliweka jambo hili kuonyesha hakuna utawala wa sheria nchini. Sheria zipo na mzisome vizuri kuliko kutoa maelezo ya kuchanganya umma,” amesema Dk Tulia.

Amesema, “Sheria ipo wazi kwamba ikishaletwa taarifa ya CAG hapa bungeni mtu yeyote ana ruhusa kuizungumzia. Hiki kinachojibiwa na mawaziri ni maoni yao.”
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images