Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Timu Tatu England Zamtaka Mbwana Samatta

$
0
0
NEEMA imezidi kumfungikia mshambuliaji Mtanzania, Mbwana Samatta anayekipiga katika Klabu ya KRC Genk ya Ubelegiji baada ya klabu tatu za England kumuwania.

 Samatta aliyewahi kuichezea TP Mazembe ya DR Congo alijiunga na Genk mwaka 2015 baada ya mkataba wake kumalizika ambaye wakati wowote huenda akatimkia England.

Akizungumza katika Kipindi cha Spoti Hausi kupitia Global TV Online, baba mzazi wa Samatta, Mzee Ally Samata alisema tayari klabu tatu kutoka England na nyingine za Hispania na Ufaransa zinamtaka.

Mzee Samata alisema, usajili wake huo hivi sasa upo chini ya wakala wake ambaye yupo kwenye mazungumzo na klabu hizo ambazo majina yake ameyaficha.

“Ninataka kumuona akicheza soka England, ninaamini atafanikiwa kwani tayari malengo hayo naona yameanza kutimia baada ya klabu tatu kutoka England kuvutiwa naye.

“Nimemwambia akubali kujiunga na timu hizo bila kujali nafasi zake katika ligi kuu kwani nina imani atazitumia kama njia ya kufika mbali zaidi.

“Ninaamini mwanangu atafanikiwa na ninataka kumuona akiichezea timu yangu ninayoipenda mimi na yeye mwenyewe ambayo ni Manchester United.

 “Lakini akikosa kuichezea Man United, basi aichezee timu yoyote ya England ikiwemo Arsenal licha ya kutoipenda timu hiyo kwani ligi ya nchini huko ndiyo inapendwa zaidi duniani,” alisema Mzee Samata.

Yanga yadondokea timu za Africa Mashariki

$
0
0
Klabu ya soka ya Yanga imepangwa na timu mbili kutoka nchi za Africa Mashariki kwenye kundi D, la michuano ya Kombe la Shirikisho barani Africa, kwenye droo iliyochezeshwa jijini Cairo leo mchana.

Yanga imepangwa na timu za Rayon Sports kutoka Rwanda ambayo katika hatua ya mtoano imewatoa mabingwa wa Africa mwaka 2016 Mamelodi Sondowns ya Africa Kusini.

Pia katika kundi hilo kuna timu ya Gor Mahia ya nchini Kenya ambayo nayo imetinga katika hatua ya makundi baada ya kuitoa Supersports United pia ya Africa Kusini. Gor Mahia pia iliibuka bingwa wa michuano ya Sportpesa msimu uliopita.

Timu ya nne katika kundi hilo ni U.S.M Alger ambayo inatokea nchini Algeria ikiwa imefuzu hatua ya makundi kwa kuitoa Maniema Union ya DR Congo.

Yanga yenyewe imetinga hatua ya Makundi baada ya kuitoa Wolayta Dicha ya Ethiopia kwa jumla ya ushindi wa mabao 2-1. Mechi za hatua ya makundi zinatarajiwa kuanza Mei 4 na 6.

Download Hapa Application Mpya ya Udaku Special Uweze Soma Vimbwanga na Udaku Mtaani Kila Siku

$
0
0
Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Upya Application yetu ya UDAKU SPECIAL Maana ile ya Zamani Tutaifuta.

Kuna Marekebisho Makubwa tumeyafanya ikiwa na tatizo la Notification kutatuliwa

NB: App mpya ina Icon Nyekundu

 Bonyeza Hapa Chini

==>>Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>> 

Wimbo wa Jason Derulo na Diamond kwa ajili ya Kombe la Dunia umetoka, usikilize hapa

$
0
0
Hatimaye wimbo wa Jason Derule na Diamond Platnumz ‘Colours’ kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia 2018 umetoka. Usikilize hapa.

VIDEO:

Alinipenda Sana Kabla Hajapata Kazi, Sasa Kapata Kazi Ananiona Bwege

$
0
0
Najuta ni kiherehere cha moyo wangu kukupenda,kukuthamini na jukujali.

Naombeni msaada,ni mpenzi wangu yapata 1&half year katika mahusiano ni binti ambaye tulifahamiana nae siku moja alipokuja na mama yake mdogo ofisini kwangu kupata huduma,

huyu mama yake mdogo ni mtu ninaefahamiana nae hivyo basi akaona haina budi kunitambulisha kwa mwanae nami nikaona ni vizuri kuanzia hapo binti yule alianza kunizoea na kuonesha dalili zote za kunitaka hata baadhi ya siku hufunga safari na kuja kunisalimia.

nami sikua na hiyana huwa sipendi kumkwaza mtu nikawa nampa ushirikiano tu mzur.

kutokana na ubize wa kazi yangu muda wa story huwa sina nikamwambia kama hutojali uwe unakuja saa 12jioni muda ambao nipo off ila sijui kama mama yako mdogo atakubali akasema hilo halina shida nikimwambia nakuja kwako hawezi kunikatalia kiukweli hilo jibu lake lilinipa ulakini!!

Basi jioni tukawa tunaenda sehemu ya utulivu tunapiga story sana tunapata chakula then tunaondoka tuliendelea hivyo kwa muda mrefu huwa anakuwa kama na kitu cha kutaka kuniambia lakini anashindwa kila usiku lazima anipigie simu na asubuhi lazima aniulize umeamkaje.

kutokana na tabia zake nzuri alizozionesha kwangu nikaona pengine Mungu ndo kanionesha mke mwema nikamtongoza japo sikutumia nguvu hata kidogo alitabasam na kufurahi nakumbuka alinikumbatia na kunipiga busu hadi nilihisi kuwewesuka kwa joto lake.

Nikawa namhudumia kila alichokitaka nilimpatia na alinipenda na kuniheshimu kama mume wake.

Nakumbuka aligombana na mama yake mdogo akawa kahamia kwa dada yake ni mbali kidogo huko nadhani maisha yalikuwa ya shida,alikuwa akinipigia simu "leo baby sijala"nikawa namsaidia akiugua namtumia pesa za matibabu,

SASA basi miezi miwili imepita kapata kazi basi ni dharau mwanzo mwisho simu hapigi,text hanitumii hata nikimtext baada ya masaa mawili ndo anareply tena shortly wiki tatu zimepita kanipigia simu anaumwa bila hiyana nikaenda kumuona na nilimpa kila kitu anachohitaji mgonjwa sikutaka maongezi nikaondoka zangu hadi leo sijawasiliana nae sababu ninahasira nae sana na ninataka nimfanyie kitu ambacho hatakisahau ili iwe fundisho au nyie wanajamvi mnanishauri nini?

Okoa Ndoa yako Sasa...Umepungukiwa na Nguvu za Kiume na Unashindwa Kupanda Mlima Vizuri

$
0
0
OKOA NDOA YAKO SASA : JE UMEPUNGUKIWA NA NGUVU ZA KIUME AU UUME WAKO MDOGO AU MPENZI WAKO HAKUTIMIZII UTAKACHO:


Acha kujiona mpweke pale ukutanapo na mpenzi au mke wako kwa sababu ya kutokuwa na nguvu za kiume au Uume wako mdogo

Dawa YA MAPRO POWERA ndio dawa sahihi na tiba tosha kwa sasa Kutibu tatizo na kuponesha kabisa tatizo LA KUWAI KUFIKA KILELENI KABLA MWENZI WAKO BADO AJAKOJOA

KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOA NA MWILI KUCHOKA

UUME KUSINYAA NA KUWA LEGELEGE

KUUMWA NA TUMBO WAKATI UNAPOMALIZA KUFANYA TENDO

Dawa hii utumiwa ata na wazee wenye umri mkubwa na haina madhara yoyote

MAKAKANUA HII NI dawa ya maumbili madogo urefusha na kunenepesha saizi upendayo saiz 5-6-7-8 na unene sm 3-4-5 kwa mini huabiki kwa kuwa na UUME mdogo wai sasa upate tiba sahihi kabisa na ni tofauti na ulizowai kutumia :

Tunarudisha mke au mpenzi ndani ya masaa matatu tu zipo dawa za presha kisukali vidonda vya tumbo korodani iliyovimba dawa za uzazi tunapunguza matiti makubwa kitambi na mwili mkubwa dawa zipo FIKA OFISINI KWANGU MBAGALA ZAKHEMU KWA WATEJA AMBAO AMTAKUWA NA NAFASI YA KUJA OFISINI AU MLIO MKOANI MTALETEWA p

Piga simu 0743362017 au 0789234653

DR AGU

"Binadamu Asiyekuwa na Akiba ni Waajabu"- Spika

$
0
0

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amefunguka na kudai kuna baadhi ya wananchi hususani wanaoishi mijini hawana desturi ya kuhifadhi chakula cha akiba majumbani mwao jambo ambalo ni baya linaweza kuhatarisha maisha yao kwani hata panya na mchwa huwa wanahifadhi


Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo Aprili 21, 2018 wakati alipokuwa anatoa salamu za kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma waliojitokeza kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa mradi maghala na vihenge vya kisasa kwa ajili ya kuhifadhia chakula lenye uwezo wa kubeba tani elfu 20.

"Binadamu asiyekuwa na akiba ya chakula atakuwa waajabu sana, kama mchwa na panya wanaweka akiba ya vyakula je itakuja kuwa binadamu ?. Sisi watu wa mijini tukikaguliwa nyumba zetu hata debe ndani la mahindi hukuti wala nusu debe ya maharage kazi ni kwenda sokoni kila siku", amesema Ndugai.

Kwa upande mwingine, Spika wa Bunge Job Ndugai amempongeza Rais wa awamu ya tano Dkt. John Magufuli pamoja na wasaidizi wake akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kuweza kutekeleza ahadi zilizopo kwenye Chama cha Mapinduzi (CCM).

Hii ndio Chanzo Uharibifu Mlima K’njaro

$
0
0
WANANCHI wanaozunguka Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), wamedaiwa kusababisha migogoro kati yao na hifadhi hiyo kutokana na kutofuata sheria na kanuni za hifadhi.

Akizungumza hivi karibuni na Nipashe, Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Pascal Shelutete, alisema chanzo cha migogoro ya mipaka husababishwa tafsiri zinazopingana kati ya wataalamu na wananchi kuhusu matangazo ya serikali yanayoanzisha hifadhi.

Shelutete alisema matatizo hayo yanaweza kuvuruga uhusiano kati ya wananchi na shirika na kutishia rasilimali zilizopo ndani ya hifadhi kupotea.

Alisema wamekuwa wakisisitiza wananchi umuhimu wa kuheshimu sheria ya mipaka za hifadhi za taifa, lakini ni changamoto kwa kuwa wananchi hawana uelewa wa kutosha.

Alisema watu wachache wenye nia mbaya wasipokemewa, madhara yatakuwa makubwa ikiwamo kupoteza uoto wa asili ambao ni chanzo cha utalii ndani ya hifadhi.

Hata hivyo, alisema TANAPA imeweka bikoni zenye viwango katika mipaka ya  hifadhi kwa  asilimia 80 na mwananchi atakayeingia eneo la hifadhi kwa kufanya shughuli za kibinadamu atachukuliwa hatua za kisheria.

Mkurugenzi wa TANAPA, Mtango Mtahiko, alisema migogoro mingi ya ardhi husababishwa na idadi ya watu kuongezeka huku akibainisha wakati wa uhuru kulikuwa na watu milioni nane na sasa wameongezeka hadi kufikia milioni 58.

“Tanzania ni miongoni mwa nchi chache zenye rasilimali za asili kama uoto wa asili, na maeneo ya kuzalisha mali yamepungua wakati binadamu wanaongezeka,” alisema Mtahiko.

Mhifadhi Mkuu KINAPA, Betrita Loibooki, alisema kutokana na uelewa mdogo wa wananchi wanaozunguka mlima Kilimanjaro, wanaona hakuna umuhimu wa kutunza misitu hivyo kulazimisha kuachiwa maeneo kwa ajili ya shughuli zao jambo ambalo ni hatari.

Alisema wananchi wanatakiwa kufuata sheria na kanuni zilizowekwa kwa kuwa faida zitokanazo na hifadhi hizo zinamfikia kila mwananchi na taifa.

Sheria ya TANAPA hairuhusu matumizi ya aina yoyote kasoro utalii wa kuangalia na kupiga picha, elimu na utafiti katika hifadhi za taifa.

Mimi Mars Afunguka Kuhusu Kolabo

$
0
0
MWANADADA kiwango kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Marriane Mdee ‘Mimi Mars’, amefunguka kuwa miongoni mwa vitu anavyopenda kwenye muziki ni kufanya kazi kwa kushirikiana na wanamuziki wengine kwani ushirikiano ni kitu kizuri.

Akipiga stori na Mikito Nusu Nusu, Mimi ambaye hivi karibuni amepiga kolabo na Frankie Maston na Yeyo Leslie, wa ngoma iitwayo Mi Nawe, amesema kushirikiana kwenye muziki ni kitu kizuri na ikitokea akihitajika na mtu.

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

$
0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?

Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?

Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU.

Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Issa simba said Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili, ZINDIKO za Nyumba.

MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA.

Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI.

Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

WASILIANA NAE:

+255 622588038
0679119679
+255 764318107

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Humphrey Pole Pole "Ukimtuhumu Rais Amelisababishia Hasara Taifa"

$
0
0

Leo April 22, 2018 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, Humphrey Polepole amewataka baadhi ya watu wanaokaa kutuhumu kuwa Rais amelisababishia Taifa hasara kuacha kwani wakiomba wathibitishe wengi usema ulikuwa ni mjadala Twitter.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Polepole ameandika “Ukimtuhumu Rais amelisababishia hasara Taifa ukaombwa uthibitishe utaweza au utasema yalikuwa tu majadiliano ya twita baada ya chakula cha mchana?”

“Huko barabarani defamation ni kosa kubwa, lakini mbona mnataka viongozi wetu wadhalilishwe kisha tukae kimya, kaanze kumtukana babako” -Polepole

Rais Magufuli atuma salamu za pole kwa Familia ya Masogange

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za pole kwa familia ya Agness Gerald Waya kufuatia kifo cha mtoto wao Agness alimaarufu kama Masogange kilichotokea Ijumaa.

Rais Magufuli ametuma salamu hizo kupitia kwa Mwenyekiti Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Bw. Kheri James na kusema kuwa amesikitishwa sana na kifo cha binti huyo kwani kifo chake kinapunguza idadi ya vijana ambao ndiyo jeshi na watu ambao wanaweza kufikisha mbali taifa.

"Kupitia jukwaa hili naomba nitoa salamu za Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye leo amewasilisi mjini Dodoma lakini ameomba niwasilishe kwenu salamu za pole kwa kuondokewa na kijana mwenzetu, Mwenyekiti anafahamu nchii hii sisi vijana ndiyo warithi wa taifa hili sisi ndiyo tumebebe dira ya kulifikisha taifa ambapo tunadhani linafaa kufika hivyo anasikitishwa sana kuona katika jeshi kubwa kama hili la vijana tunapungukiwa na vijana wenzetu wanaondoka na kupunguza idadi ya askari wetu , naomba mpokee salamu za Mwenyekiti wetu" alisema Kheri James

Mwili wa Agness Masogange utazikwa jijini Mbeya nyumbani kwa wazazi wake Mbalizi

Mdogo wa Ali Kiba Amua Kufuata Nyayo za Kaka yake Kwa Kuvuta jiko

$
0
0

Alikiba ambaye siku ya alhamisi ya tarehe 19, April, 2018 alifunga ndoa na binti Aminah Rikesh kutoka nchini Kenya katika mji wa Mombasa ambapo inatarajiwa Alikiba kuirudisha sherehe hiyo nyumbani Tanzania tarehe 29. Siku hiyo Alikiba aliweka wazi mdogo wake Abdukiba kuwa ataoa karibuni.

Hatimaye ahadi hiyo ya Alikiba kuhusu mdogo wake imetimia kwani msanii huyo ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake ya 'Jeraha' amefunga ndoa pia na moja ya mtu wake wa karibu na kufanikiwa kuongeza idadi ya wanawake katika familia yao kama ambavyo mdogo wake wa kike Zabibu anavyosema kuwa mwanzo walikuwa wawili tu yeye na mama yake lakini ameongezeka mke wa Kiba na kudai anatarajia kuongezeka mwingine wa nne karibuni ambae ndiye mke wa Abdukiba.

Kupitia mtandao wa Instagram msanii H Baba ambaye ni mtu wa karibu na kina Alikiba ameweka wazi kuwa Abdukiba leo amefunguka ndoa na kumtakia kheri kwenye siku yake hiyo muhimu katika maisha yake.

"Hongera sana Abdukiba kwakuchukua jiko lako Allah akulindie ndoa yako, jambo la kheri uja na kheri zake karibu chama la waliompendeza Mungu kwani kuoa nijambo la kheri" alisema H Baba

Alikiba na Abdukiba wanadhaniwa kuwa huenda wanaweza kufanya sherehe ya pamoja April 29, 2018 jijini Dar es Salaaam ili kufurahi na watu wao wa karibu kufuatia zoezi la wao kufunga ndoa.

Diamond Platnumz na Ali Kiba Wapeana Mikono...Bifu Limekwisha?

$
0
0

MATUKIO KWA PICHA :
@officialalikiba na @diamondplatnumz wakipeana mikono katika Tukio la Kuaga mwili wa marehemu Agnes Masogange... Hakika Duniani Tunapita.... Hii ni Ishara Ya Amani kati Ya wawili hawa.

DROP COMMENT YAKO HAPA TAFADHALI.

Msanii wa Bongo fleva Jebby, afariki dunia

$
0
0

Msanii wa bongo fleva anayefahamika kwa jina la Jebby ambaye amewahi kufanya vyema na wimbo kama Swahiba amefariki dunia leo April 22, 2018 mjini Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu.


Watu wa karibu na msanii Jebby wamesema kuwa msanii huyo alikuwa anaumwa na mpaka umauti umemkuta Dodoma alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya bandama na ndiyo yaliyosababisha kifo chake.


Msanii Afande Sele pia amethibitisha hilo na kusema kuwa Jebby alikuwa anasumbuliwa na matatizo hayo ya bandama na kuwa leo ndiyo amefariki dunia.


"Hayupo tena duniani swahiba...pumzika kwa amani mdogo wangu wa haki Jebby.Tukimaliza kazi tutavalishwa taji" alisema Afande Selle

Polepole: CCM Haijamkosoa CAG, CHADEMA Ndo Waliomkosoa

$
0
0

Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi ya CCM, Humphrey PolePole amefunguka na kusema kuwa wao kama Chama Cha Mapinduzi na serikali hakuna mtu kati yao aliyemjibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Assad bali CHADEMA ndiyo wamemjibu.


Polepole amesema hayo leo April 22, 2018 kupitia mtandao wake wa twitter na kudai kuwa wao waliipokea ripoti hiyo na kumpongeza CAG na kuitaka serikali iendelee kuchukua hatua katika yale ambayo CAG ameyabaini.


"Kimsingi kwa CCM au Serikali yake hakuna hata mtu mmoja ambaye amemjibu CAG, sisi tulipokea, tulipongeza na tukaelekeza Serikali iendelee kuchukua hatua. Ambaye amejitokeza kujibu hadharani ni CHADEMA ndio pekee wamemjibu na kumkosoa CAG. Ila naona watu wachache pamba masikioni" alisisitiza Polepole


Polepole anasema yeye alipowaita waandishi wa habari hakumjibu CAG bali amedai kuwa alifanya ufafanuzi wa hoja mbalimbali ikiwepo ile ya Trilioni 1.5 ambayo kwenye ruipoti ya CAG inaonekana haina maelezo.


"Kuna tofauti kati ya kumjibu CAG na kufafanua hoja ambazo amezitoa kwa CCM na kuulaani vikali upotoshaji wa Zitto Kabwe juu ya taarifa ya CAG" 

Baba Mzazi wa Agness Masogange Asimulia Alivyoagana na Mwanaye Muda Mfupi Kabla ya Mauti kumkuta

$
0
0

Gerald Waya, ambaye ni baba mzazi wa Agnes (Masogange), amesema mwanaye alikuwa nguzo katika maisha yake, hivyo ni pigo kubwa kwake na familia nzima.


Akizungumza nyumbani kwake Mbalizi II wilayani Mbeya, leo Aprili 22, 2018 Mzee Waya amesema Masogange ni mtoto wanne katika familia yake ya watoto sita, wa kike wakiwa watano.


Amesema Masogange alisoma Shule ya Msingi Utengule-Mbalizi na sekondari ya Sangu alikoishia kidato cha pili.


Waya amesema Masogange alipata matatizo hivyo akalazimika kuacha shule. Hata hivyo amesema hataki kuzungumzia mambo mabaya wakati huu anapoomboleza kifo cha mwanaye.


 “Aliishia form two (kidato cha pili), akapata matatizo ikabidi aache shule. Tulikosana kidogo lakini tukayamaliza yeye akaenda Dar es Salaam,” amesema.


Waya amesema, “Mwanangu alikuwa nguvu kwangu, alikarabati nyumba hii ninayoishi kwa sasa na nilikuwa nafarijika sana, lakini leo kusikia msiba huu kwa kweli inaniuma sana.”


Amesema Masogange alimpigia simu, “Tukaongea naye akaniambia ‘mimi baba ninaumwa’. Nikamuuliza nini tatizo akasema, “aah!   baba niombee tu kwa Mungu’. Na Jumamosi iliyopita nilimpigia simu wakati yupo hospitali kujua maendeleo yake lakini akaniambia ‘baba byee’.  Nikaanza kulia, na hapo sikuwasiliana naye tena hadi nilipopata taarifa za kifo chake,” amesema.

Serengeti Boys watinga Nusu Fainali CECAFA U17

$
0
0

TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imepata ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Sudan katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA U17 inayoendelea nchini Burundi.

Kwa matokeo hayo, Serengeti Boys inakwenda Nusu Fainali ya michuano hiyo kutoka Kundi B, ikiungana na Uganda, zote zikiwa na pointi nne kila moja, wakati Sudan inaaga baada ya kupoteza mechi zote mbili.

Zanzibar ni timu nyingine iliyopangwa katika kundi hilo, lakini iliondolewa kwa kuwasili na wachezaji waliozidi umri.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Muyinga mjini Bujumbura, mabao ya Serengeti Boys yamefungwa na Alphonce Msanga mawili dakika za nne na 59, Mustapha Nankunku dakika ya 27, Edson Mshirakandi dakika ya 28, Jaffar Mtoo dakika ya 78 na Kelvin Paul dakika ya 83.

Mechi yake ya kwanza, Aprili 15, mwaka huu Serengeti Boys ilitoa sare ya 1-1 na Uganda.

Matumaini ya Yanga Kutetea Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara yazidi kuwa Haba

$
0
0

MATUMAINI ya Yanga SC kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara yamezidi kuwa haba baada ya leo kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Mbeya City Uwanja wa Sokoine.

Matokeo hayo yanaiongezea Yanga SC pointi nyingine moja, wakifikisha 48 katika mechi 23, wakizidiwa pointi 11 na vinara, Simba SC wenye pointi 59 za mechi 25 na wababe hao watakutana Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na marefa, Shomari Lawi wa Kigoma aliyesaidiwa na Omari Juma wa Dodoma na Godfrey Kihwili wa Arusha, Yanga ilitangulia kupata bao lake kipindi chake cha kwanza, kupitia kwa Raphael Daudi Loth kabla ya MCC kusawazisha kipindi cha pili kupitia kwa Iddi Suleiman Nado.

Mbeya City walianza kulitia misukosuko lango la Yanga dakika ya nne tu, baada ya mshambuliaji wake tegemeo, Frank Ikobela kupiga shuti lililozuiwa na beki Juma Abdul na kuwa kona ambayo iliokolewa. Yanga SC ilijibu shambulizi hilo dakika ya 14 baada kiungo Pius Buswita kutia krosi nzuri iliyopanguliwa na kipa Owen Chaima na mpira kumkuta kiungo Raphael Daudi ambaye alipojaribu kuurudisha ukaokolewa na kipa huyo Mmalawi.

Chaima akafanya kazi nzuri tena dakika ya 16 kwa kuokoa mpira uliopigwa na mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa aliyepokea pasi nzuri ya kiungo mzawa, Yussuf Mhilu

Mbeya City wakazinduka dakika ya 20 baada ya mshambuliaji wao, Eliud Ambokile kupiga mpira wa juu kiufundi kufuatia pasi ya kiungo Mohammed Samatta ukagonga mwamba na kurudi uwanjani kabla ya beki wa kushoto, Gardiel Michael kuondosha kwenye hatari.

Kipa wa Yanga, Mcameroon Youthe Rostand akafanya kazi nzuri ya kudaka mpira uliogongwa kwa kifua na Victor Hangaya dakika ya 34 kufuatia krosi ya mwasapili ambapo kipa anadaka.

Kaimu Nahodha wa Yanga SC, Kevin Patrick Yondan alishindwa kuendelea na mchezo baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza, nafasi yake ikichukuliwa na Nahodha Mkuu, mkongwe Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

Yanga ikaanza kufunguka zaidi kipindi cha pili kwa kupeleka mashambulizi ya moja kwa moja hususan baada ya mabadiliko mengine yaliyofanywa akitolewa kiungo Emmanuel Martin na nafasi yake kuchukuliwa na Juma Mahadhi.

Hiyo iliiwasaidia wana Jangwani hao kupata bao dakika ya 58, kiungo Raphael Daudi Loth akiiadhibu timu yake ya zamani kwa shuti kali baada ya kuanzishiwa mpira wa adhabu na beki wa kulia, Juma Abdul kufuatia Mahadhi kuangushwa.

Baada ya bao hilo, mashabiki wa Mbeya City wakaanza kufanya fujo wakitupa mawe uwanjani na moja likamgonga kiichwani kipa wa Yanga, Youthe Rostand.

Mchezo ukaendelea baada ya dakika mbili, lakini dakika ya 65 beki wa Mbeya City Ramadhani Malima akatolewa kwa kadi nyekundu, baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kumfuatia kumchezea rafu kiungo wa Yanga, Yussuf Mhilu.

Vurugu zikaibuka tena Uwanja wa Sokoine masabiki wakipiga mawe na Polisi wakalazimika kutumia gesi za machozi kutuliza vurugu, kabla ya mchezo huo kuendelea tena dakika tano baadaye kufuatia ulinzi kuimarishwa kwa gari lingine la aksari wa kupambana na Ghasia kuingia uwanjani.

Mchezo wa kujihami kulinda bao dakika za mwishoni uliwagharimu Yanga kuwapa wenyeji bao la kusawazisha, lililofungwa na Iddi Suleiman Nado dakika ya 90 kwa kichwa akimalizia krosi ya Kenny Kunambi.

Bao hilo liliwachanganya Yanga na kuwaruhusu Mbeya City kutawala mchezo zaidi kuelekea filimbi ya mwisho.

Kikosi cha Mbeya City kilikuwa: Owen Chaima, Kenny Kunambi, Hassan Mwasapili, Haruna Shamte, Ramadhan Malima, Majaliwa Mbaga, Eliud Ambokile/Danny Joram dk90+7, Medson Mwakatundu, Victor Hangaya/Iddi Suleiman dk75, Mohamed Samata na Frank Ikobela.

Yanga SC: Youthe Rostand, Juma Abdul, Gardiel Michael, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Kelvin Yondan/ Nadir haroub ‘Cannavaro’ dk46, Said Juma ‘Makapu’, Yussuf Mhilu, Pius Buswita, Obrey Chilwa, Raphael Daudi na Emmanuel Martin/Juma Mahadhi dk51.

Mwigazaji Irene Paul Akerwa na Picha ya Mwombolezaji Aliyezimia huku Ameshika Vitu vyake visipotee mazishi ya Masogange

$
0
0

Mwigazaji Irene Paul Naye Akerwa na Picha ya Mwombolezaji Aliyezimia huku Ameshika Vitu vyake visipotee mazishi ya Masogange
_
Regrann from @irenepaul001 - Maskini pamoja na kuzimia/kuishiwa nguvu lakini aliweza kuwa na nguvu ya kushika vitu vyake... wote tumeguswa lakini pia tusifanye msiba ya wenzetu kama sehemu ya kupata kiki zetu!! TUIHESHIMU kama kweli tuna malengo mema ya kumsindikiza mwenzetu kwa upendo, na zaidi tujue kutofaufisha kati ya LOCATION ZA FILAMU na DUNIA YA UKWELI.

Kuna vitu havikeri ila VINACHEFUA!! I am sorry to say umenichefua leo.. na bora ungekuwa Jinsia yetu angalau!! Ningelala na hili ningekabwa!! Pumzika kwa Amani AGNES!!(BONGO MOVIE WENGI UZURI TUNAJUANA NA HAPA TUMEELEWANA). - #regrann
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images