Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104687 articles
Browse latest View live

Mwanamke Haya Hapa Mambo yatayomfanya Mumeo Akupende zaidi

$
0
0
Wapo baadhi ya wanawake hudiliki hata kutumia dumba hii yote ikiwa kuwafanya wanaume zao wawapende, lakini wengi wao wamesahau ya kwamba kufanya hivo sio chachu ya kufanya mahusiano hayo yakue bali ni kuyadidimiza.

Lakini ukweli kwamba mambo ya libwata yamepitwa na wakati katika karne hii hivyo ili mumeo akupende zaidi katika mahusiano yenu unatakiwa kufanya yafautayo;

1. Muamini mmeo au mchumba wako.

2. Usimkatishe tamaa katika maono yake.

3. Usimlazimishe kupenda mambo unayoyapenda.

4. Kila wakati kila unapo tatizo ni vyema ukamwambia kuliko kusema kwa wengine.

5. Usidhani kwamba hawezi kutambua uwepo na uzuri wa wanawake wengine hivyo mfanye awe karibu nawe ilia one thamani yaw ewe pekeee..

6. Usilazimishe kuwajibika juu ya mambo yako: Kama vile kwenda saluni, umeme, vocha na mambo mengine hasa kama bado mko katika mchakato wa uchumba, kama atafanya hivyo mwache afanye mwenyewe msimlazimishe eti kwa sababu shosti wako huwa anafanyiwa hivyo na wewe unataka, ladies huo ni utoto.

Uingereza Nayo Yawatahadharisha Raia Wake wanaoelekea Tanzania Aprili 26

$
0
0
Uingereza Nayo  Yawatahadharisha Raia Wake wanaoelekea Tanzania Aprili 26
Iwapo wewe ni raia wa Uingereza na unapanga kusafiri kuelekea Tanzania wiki hii unatakiwa kuwa mwangalifu ili kuhakikisha kuwa haujipati katika maandamano ya kisiasa yanayopangwa kufanyika tarehe 26 Aprili .

Katika tahadhari ya usafiri iliotolewa na ubalozi wa Uingereza, wasafiri wameonywa kwamba ijapokuwa safari za kuelekea taifa hilo hazina matatizo yoyote, wageni wanaoingia nchini humo siku hiyo wanafaa kuwa makini kwani iwapo kutakuwa na maandano kunaweza kuwa na 'maafa'.

Kulingana na gazeti la The Citizen Tanzania, tahadhari hiyo ilitolewa kufuatia wito wa kufanyika kwa maandano dhidi ya serikali na mwanaharakati wa mtandaoni anayeishi nchini Marekani Mange Kimambi.

Jaji aamuru barua za uhusiano wa Madonna na Tupac kupigwa mnada
Mtu wa kwanza kupandikizwa uume duniani
Mchumba mpya wa Zuma alazimishwa kujiuzulu ajira yake
Anadai kwamba maandamano hayo ni ya kupinga ukandamizaji wa uhuru wa kisiasa na unyanyasaji wa haki za kibinaadamu.


Barua ilioandikwa na ubalozi wa Uingereza kwa vyombo vya habari nchini Tanzania
Serikali tayari imepinga madai hayo na kusema kuwa maandamano hayo yatakuwa kinyume na sheria.

Rais John Magufuli amesisitiza kuwa maafisa wa usalama watakabiliana na wale watakaoshiriki katika maandamano hayo.

''Kutokana na uzoefu wa hapo mbeleniu balozi wa Uingereza nchini Tanzania umeonya kwamba maafisa wa usalama nchini Tanzania huenda wakatumia vitoa machozi na hata risasi kukabiliana na mandamano yoyote haramu''.

''Kuweni makini mulipo na epukeni makundi makubwa ya watu ama maandamano ya umma'', ilisema taarifa hiyo.

Takriban raia 75,000 wa Uingereza hutembelea Tanzania kila mwaka.

Nafasi za Ajira zilizotangazwa Leo

$
0
0

Sakata la Tiketi za Mwendokasi: Kampuni ya Maxcom Yaishtaki UDA-RT

$
0
0

Sakata la Tiketi za Mwendokasi: Kampuni ya Maxcom Yaishtaki UDA-RT
Kampuni ya Maxcom Africa PLC imeeleza kuwa, imefungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu ya Tanzania dhidi ya Kampuni ya UDA-RT inayotoa huduma ya usafiri wa Mabasi ya Mwendokasi, kutokana na kampuni hiyo kushindwa kulipa gharama za uendeshaji, uwekezaji na stahiki za wafanyakazi.

Binti wa Miaka Ishirini Amuua Mdogo Wake wa Miaka Miwili na Kumtupa Uvunguni

$
0
0
Binti wa Miaka Ishirini Amuua Mdogo Wake wa Miaka Miwili na Kumtupa Uvunguni
Mtoto wa miaka miwili amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali kitovuni na kuwekwa uvunguni mwa kitanda nyumbani kwao Kigamboni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Lukula amezungumza na Mcl Digital leo Aprili, 25 na kuthibitisha tukio hilo.

Kamanda Lukula amesema kuwa tukio hilo limetokea juzi Jumatatu ambapo inadaiwa kuwa binti wa miaka (20) alimchoma mtoto huyo kwenye kitovu kwa kutumia kitu chenye ncha kali na kumficha uvunguni.

“Ni kweli tukio hilo limetokea juzi, aliyefanya hilo tukio ni binti wa miaka 20 ambaye ni ndugu wa mama wa marehemu. Si mfanyakazi wa ndani kama wengine wanavyodai, alimchoma huyo mtoto na kumlaza kifudifudi uvunguni kisha akaondoka,’’ ameeleza Kamanda Lukula na kuongeza:

“Sijapata majina sahihi maana nilielekeza niletewe na bado sijaletewa lakini tukio hilo ni la kweli.’’

Kamanda Lukula amesema baada ya huyo binti kufanya tukio hilo aliondoka nyumbani hapo.

“Huyo binti baada ya kufanya hilo tukio alikwenda kwa mwanaume anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na baada ya mama wa mtoto kurudi kazini hakumkuta nyumbani,’’amesema

Baada ya uchunguzi wa polisi, binti huyo alikamatwa na alikwenda kuwaonyesha alipomuweka mtoto uvunguni mwa kitanda.

Kamanda Lukula amesema kwa sasa taratibu nyingine za kisheria zinaendelea baada ya mtuhumiwa kukamatwa.

Yanga Yawatahadharisha Simba " Msibweteke Mechi ya Jpili"

$
0
0
Yanga Yawatahadharisha Simba " Msibweteke  Mechi ya Jpili"
Makamu Mwenyekiti wa Tawi la Umoja la Klabu ya Mabingwa Watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, Waziri Jitu amedai timu yake kushindwa kupata alama tatu kwa baadhi ya michezo waliyocheza kuwa Simba isijipe imani kwamba itaweza kuwafunga.


Waziri Jitu ametoa kauli hiyo zikiwa zimesalia takribani siku 4 kuelekea mpambano wa jadi ambao unatolewa macho na kila mpenda soka nchini kujua ni nani atakuwa mshindi kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili Aprili 29, 2018.

"Yanga kushindwa kuchukua pointi tatu kwa baadhi ya michezo Simba isijipe imani kwamba inaweza ikatufunga, mimi nitakupa mfano hai, mzunguko wa kwanza ilikuwa hivyo hivyo walikuwa wanasema Yanga mbovu. Simba imefanya usajili wa Bilioni 1.5 lakini hatima yake dakika 90 ndio zimemaliza mchezo, tumekwenda patapata yaani moja moja, siku zote katika historia ya Simba na Yanga ni kwamba mwenye timu nzuri ndio huwa anapata adhabu na wasimba wa zamani wanalijua hili", amesema Waziri.

Pamoja na hayo, Waziri ameendelea kwa kusema "sasa mimi niwaombe Simba wasibweteke mechi ya Jumapili. Yanga yupo vizuri na asipige hesabu kwamba anaenda kumfunga Yanga mpira dakika 90, Yanga anaenda kumpiga Simba Jumapili".

Kwa upande mwiingine, Waziri amesema anaamini kabisa kuwa hamasa waliyopata wachezaji kuelekea katika mchezo huo na michezo iliyobakia ya Ligi inatosha kuonyesha kiwango chao katika mchezo wao dhidi ya mahasimu na wanaamini wachezaji wote hawatakubali kufungwa na Simba.

Watoto wa Miaka 14 na 15 Waoana kwa Idhini ya Mahakama ya Dini

$
0
0
Watoto wa Miaka 14 na 15 Waoana kwa Idhini ya Mahakama ya Dini
Kutoka nchini Indonesia, watoto wawili, mvulana akiwa na miaka 15 na msichana miaka 14 jana April 24, 2018 wamefunga ndoa baada ya kupewa ruhusa kisheria kufanya hivyo.

Inaelezwa kuwa watoto hao walikwenda kutafuta ruhusa kwenye mahakama ya kidini ambapo inaelezwa kuwa serikali huwa haitoi ruhusa ya watoto kuoana mpaka mahakama ya kidini itoe ruhusa.

Walichoandika mastaa baada ya Meek Mill kuachiwa

Kesi ya watoto hiyo imekabiliwa na upinzani mkubwa ndani na nje ya nchi hiyo huku serikali ikipanga kufanya mabadiliko ya sheria.
Indonesia ni nchi yenye idadi kubwa ya Waislamu na wasichana wake wengi wadogo wameolewa.

Ushauri wa Halima Bulembo kwa Wapinzani “hawana hoja”

Sheria ya nchi hiyo kuhusu ndoa ni kwamba, msichana kuanzia miaka 16 na mvulana miaka 19 na kuendelea wanaweza kuoana lakini wanaweza kuoana hata chini ya umri huo kama mahakama ya kidini itaidhinisha.

YouTube Yaongeza Vigezo Vipya kwa Watakaohitaji Kuwezesha Akaunti Zao Kulipa ‘Monetization’

$
0
0
YouTube Yaongeza Vigezo Vipya kwa Watakaohitaji Kuwezesha Akaunti Zao Kulipa ‘Monetization’
Kama wewe ni Vlogger, Bloger, mtangazaji au Muandishi wa Habari na una lengo la kuanza kutumia mtandao wa YouTube ili uweze kujiingizia kipato basi kuna vigezo vipya vimeongezwa.

Kwa sasa Mtandao huo utahitaji mtumiaji awe amefikisha masaa 4,000 yaani dakika 240,000 ya kutazamwa kwenye akaunti yako kwa miezi 12 iliyopita ili uweze kuiwezesha akaunti yake ya YouTube kulipa ‘Monetization’ .

Licha ya kigezo hicho, pia vigezo vya awali vya kuwa na angalau Subscribers 1,000 na watazamaji (views) 10,000 bado vitaendelea kutumika kama vigezo vya msingi vya kuwezesha akaunti yako kuanza kulipa ‘Monetization’ .

Masharti hayo yameanza kufanya kazi mwezi wa Februari kwa nchi ya Marekani na kwa nchi nyingine yameanza kufanya kazi mwezi Marchi ambapo masharti hayo hayatahusisha akaunti ambazo tayari zilianza kulipwa kwa masharti ya awali. Hii ni kwa mujibu wa Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo, Paul Muret .

Chanzo: Mtandao wa Tech Crunch

Kombe la Dunia Lamaliza ‘Bifu’ la Diamond, Nahreel

$
0
0
Kombe la Dunia Lamaliza ‘Bifu’ la Diamond, Nahreel
Chumba cha habari Dar. Fainali za Kombe la Dunia ambazo zitatimua vumbi nchini Urusi mwezi Juni mwaka huu  zimewakutanisha mahasimu wawili, Diamond Platnumz na mtayarishaji Nahreel waliotofautiana baada ya kufanya kazi pamoja miaka mitatu iliyopita.

Daimond alitofautiana na Nahreel baada ya kuondoa utambulisho wa mtayarishaji huyo katika wimbo Nana aliomshirikisha Mr Flavour wa Nigeria.

Nahreel aliyetengeneza wimbo huo alikasirishwa na kitendo cha Diamond kuondoa utambulisho wake maarufu “Nahreel on the beat” katika video.

Ilichukua muda mrefu mashabiki kujua mtayarishaji wa wimbo huo kabla ya Nahreel kulalamikia hatua ya utambulisho wake kuondolewa na ndipo Diamond alipojitokeza kujitetea kwamba hakufanya hivyo kwa makusudi.

Katika utetezi wake alisema Nahreel alimpa wimbo ambao hauna utambulisho, hivyo baada ya kumaliza kurekodi video ilishindikana kuweka kipande kingine na kwamba hakufanya makusudi.

Hata hivyo, Coca Cola nchini imewakutanisha tena kutengeneza kipande cha wimbo Colors maalumu kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia.

Kipande cha Diamond kilichounganishwa na wimbo huo kimetengenezwa na Nahreel ambao kwa mara ya kwanza uliimbwa na mwanamuziki wa Marekani, Jason Derulo.

Joyce Banda Apanga Kurejea Malawi Huku Polisi Wakimsubiri

$
0
0
Joyce Banda Apanga Kurejea Malawi Huku Polisi Wakimsubiri
Rais wa zamani wa Malawi Joyce Banda anatarajiwa kurejea nyumbani Jumamosi baada ya kukimbilia uhamishoni alikoishi kwa zaidi ya miaka mitatu kwa sababu ya madai ya kuhusika katika rushwa, amesema msemaji wa chama chake.

Kashfa iliyofahamika kama Cashgate ni ufisadi ulioibuliwa ukiwahusisha maofisa wa ngazi ya juu kwamba walijichotea mamilioni ya dola kutoka hazina ya serikali na ulifichuka mwaka 2013 wakati akiwa rais.

Wahisani waliamua kukata misaada hali iliyozuia ukuaji wa maendeleo nchini Malawi, moja ya nchi masikini zinazotegemea sana misaada ya kigeni.

Banda, rais wa kwanza mwanamke nchini Malawi, aliangushwa katika uchaguzi mwaka 2014 na Rais Peter Mutharika aliyeshinda. Baada ya kuanza kushutumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka na utakatishaji fedha madai ambayo alikanusha, aliondoka nchini na hajarudi tangu hapo.

“Naweza kuthibitisha kwamba kama chama tumepokea mawasiliano kutoka ofisi ya rais wa zamani kwamba anarejea nchini Malawi Jumamosi,” alisema naibu msemaji wa chama cha PP, Ackson Kaliyile.

Julai mwaka jana polisi walitoa hati ya kumkamata Banda, wakisema shutuma za makosa yake ni sehemu ya Cashgate. Lakini mapema mwaka huu Taasisi ya Kupambana na Rushwa ilisema haikuwa na ushahidi wa kutosha kuusimamia dhidi yake, kwa namna fulani kama ikimsafisha mwanamama huyo.

Polisi hawajasema hadharani ikiwa mashtaka dhidi yake yametupwa. Msemaji wa polisi alisema Jumatatu kwamba polisi hawatatoa maoni yoyote kwa suala lolote hadi Banda awe amerejea nchini.

Mwaka 2016 Banda alitangaza akiwa uhamishoni kwamba atawania urais katika uchaguzi mkuu mwaka 2019, na chama kimesema anarudi kwa maandalizi hayo.

Wolper Anyosha Mikono Juu “R.I.P Bongo Movie Acha Nipambane Zangu “

$
0
0
Wolper Anyosha Mikono Juu “R.I.P Bongo Movie Acha Nipambane Zangu “
Msanii wa Bongo movie Jacqueline Wolper ameonesha kukubali kushindwa kwenye upande wa filamu na hatimaye kuamua kuwekeza nguvu zake nyingi kwenye upande ushonaji ambao amekuwa akifanya kama sehemu yake nyingine yakujitafutia kipato.

Wolper ambaye ameamua kupost kwenye ukurasa wake wa Instagram ameandika kuwa…..>>>“Natamani Bongo movie Tupendane saana yani saaaaana, kiukweli na siyo kinafki kiasi kwamba hata mtu akitokea akamuongelea bongo movie vibaya basi wote tusimame nae paka ajute kwanini kafanya hlo tukio, lakini maskin ya Mungu mchawi wetu kafa atujui kaburi lake tukamuombe radhi atusamehe tuwe huru..

“Yani Mtu akikosea ndio kwanza tunakandamiza na kuonyesha wasioliona lile kosa ichi ni kilio na ni msiba mkubwa R.i.p Bongo movie. Acha nipambane na cherehani zangu niangalie ni jinsi gani nakomboa mafundi cherehani na Tuheshimike Tanzania hope Mafundi cherehani amtoniangusha na amtokua wanafki 🙏.” – Jacqueline Wolper

Watu 18 Wauawa Kikatiliu Wakiwa Katika Ibada Nigeria

$
0
0
Watu 18 Wauawa Kikatiliu Wakiwa Katika Ibada Nigeria
Kutoka nchini Nigeria, watu 18 wameuawa kikatili jana April 24, 2018 wakiwa kanisani jambo ambalo Rais Muhammadu Buhari amelilaani na kusema ni la ‘kishetani‘.

Kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi Benue katika mji wa Makurdi, Fatai Owoseni, takribani wanaume 30 ambao ni wachunga mifugo walivamia na kuwaua watu hao 18, wawili kati yao wakiwa viongozi wa kanisa.

 Wauaji hao wanaripotiwa kuvamia eneo hilo la kanisa ambapo kulikuwa na misa ya mazishi ilikuwa ikiendelea na kuanza kuwashambulia watu pamoja na wachungaji hao ambao walikuwa wanaongoza misa hiyo.

Mrisho Mpoto "Wanawake Bongo Wanafikiria Kukaa Uchi Ndio Wataolewa"

$
0
0

Mijadala mingi iliibuka baada ya wasanii AY na Ali Kiba kuamua kuoa wake zao ambao sio watanzania sasa Mrisho Mpoto atoa somo kwa wasichana wa kitanzania na kuwaambia.


" Wasifikirie kukaa utupu ndio wanaweza kuolewa bali ni nidhamu, heshima, kujitunza na kujiheshimu pia akaongeza kwa kuwashauri wajiangalie wapi walipokosea na wajisahihishe."

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

$
0
0

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?

Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?

Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU.

Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Issa simba said Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili, ZINDIKO za Nyumba.

MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA.

Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI.

Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

WASILIANA NAE:

+255 622588038
0679119679
+255 764318107

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Wema Awatolea Povu Wanaomsema "Mi ndo Tz Sweetheart Bana Mpende Msipende ndo Nshakuwa Sasa"

$
0
0
Wema Awatolea Povu Wanaomsema "Mi ndo Tz Sweetheart Bana  Mpende Msipende ndo Nshakuwa Sasa"
Mwanadada maarufu nchini Tanzania  ambaye ni muigizaji wa movie za kibongo Wema Sepetu leo ameamua kumwaga povu kwa watu ambao wamekuwa wakimsema na kuwaambia kuwa yeye ni Tz Sweetheart  hata wakimsema na bado anawapenda tu.

 Kupitia accaunt yake ya Instagram ameanika "mi nawapenda tu ... mi ndo sweetheart bana .... mpende msipende nshakuwa sasa... ila ndo hivyo nshakuwa sweetheart ..sasa wewe seeeeeeeemaaaa, pondaaaaa.... ila Tz sweeheart ndo mie.... sema mnazungumziaje moto... kuchoma moto vepeee...?  ila nyie watu nyie... mnajua kuchoma moto ni process eeh... leo mmenipa mpya .... ntapambana na moto wenu... naahidi ntapambana nao .... ngoja nirudie .... NAWAPENDA tu.... nyie wangu tu.... ila sio kwa wenu ... "

Wakili: Puto Lililopo Tumbo mwa Sethi Linaweza Pasuka Muda Wowote na Kuhatarisha Maisha Yake

$
0
0
Wakili: Puto Lililopo Tumbo mwa Sethi Linaweza Pasuka Muda Wowote na Kuhatarisha Maisha Yake
Upande wa utetezi, umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Puto (Balloon) lililopo tumboni mwa mmiliki wa IPTL, Harbinder Sethi linaweza kupasuka muda wowote kuanzia sasa na kuhatarisha maisha yake.

Hayo yameelezwa na wakili wa utetezi, Hajra Mungula mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai kueleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilka.

Wakili Mungula amedai kuwa April 11,2018 mahakama iliamuru Seth apelekwe Hospitali ya Taifa Muhimbili kupatiwa matibabu lakini aliishia kupata vipimo, huku akishindwa kupatiwa matibabu wala majibu yake.

“Mshtakiwa hajapatiwa majibu wala matibabu ni wiki ya pili sasa, hali yake ni mbaya, pia Puto lake linaweza kupasuka muda wowote na kuhatarisha maisha yake,” ameeleza Mungula.

Baada ya kueleza hayo, wakili Swai amedai kuwa Seth alishaonana na jopo la madaktari na ameambiwa majibu yake atapatiwa April 26,2018.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Shaidi amesema amefurahi kuona mshtakiwa amepelekwa hospitali, lakini anasisitiza kuwa apatiwe matibabu.

Pia ameutaka upande wa mashtaka kuhakikisha unakamilisha upelelezi kwa wakati ili kesi iishe, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi May 10,2018.

Mbali ya Sethi, mshtakiwa mwingine ni mfanyabiashara James Rugemarila ambapo kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Shilingi Bilioni 309.

Alichokisema Mange Kimambi Baada ya Idriss Kuandika Hivi Kuhusu Maandamano ya April 26 "Maandamano ya Amani Juu ya Jambo Fulani Yanahaki ya Kupewa Sapport"

$
0
0
Alichokisema Mange Kimambi Baada ya Idriss Kuandika Hivi Kuhusu Maandamano ya April 26 "Maandamano ya Amani  Juu ya Jambo Fulani Yanahaki ya Kupewa Sapport"
Idriss Sultani ameonekana kuwa upande ambao umemfurahisha mwanaharakati mange Kimambi kuhusu kuweka msimamo wake juu ya maandamano yaliopangwa kufanyika siku ya kesho april 26 huku muandaaji mkubwa wa maandamano hayo akiwa mwanadada mange Kimambi.

 Kupitia Ukrasa wake wa instagram Idriss aliandika "Maandamano yoyote yernye amani na ni kwaajili  ya kuweka awereness  juu ya jambo flani bila vita wala ugomvi wa aina yoyote  yana haki ya kupewa sapport  kama yamekugusa. Inaitwa the Democratic Republic on Tanzania. Let's  act like our name. Kuwa mzalendo kwa kuepuka maandamano ya shari tu Rismillah itangulie#mzalendo"

Baada ya Mange Kimambi kuona post ya Idriss naye aliandika hivi " Idriss uwezi kuelewa uzito wa post hii sababu watanzania wanahitaji  sapoti kama hii kutoka kwa nyinyi mastaa ni wewe pekee umejirisk  kwaajili yao. watanzania wanaweza  wasikulipe ila mungu atakulipa. Ulichokifanya leo  kina uzito wake. Idriss naomba usikae nyumbani siku ya leo........ Heshima yangu kwako is waaaaaay up there! salute!!!!!!"

Polisi Yatoa Onyo Kali kwa Watakaoandamana Kesho " Tumejipanga Hakuna Maandamano Yatakayofanyika Kesho"

$
0
0
Polisi Yatoa Onyo Kali kwa Watakaoandamana Kesho " Tumejipanga Hakuna Maandamano Yatakayofanyika Kesho"
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewataka wananchi wote kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwa kuwa maandamano yanayozungumzwa hayapo na ni batili.

Akizungumza leo Jumatano Aprili 25 na shirikisho la waendesha bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, ACP Sweethbert Njwele amesema jeshi la polisi limejipanga kuhakikisha kila mtu anafanya shughuli zake kama kawaida bila uvunjifu wowote wa amani.

"Niwahakikishie jeshi la polisi tumejipanga na mkoa wetu utaendelea kubaki salama hakuna maandamano yatakayofanyika hivyo kila mtu aendelee na shughuli zake kama kawaida," amesema Njwele.

Amesema waendesha bodaboda ni kundi kubwa ila kuna baadhi yao si waaminifu na kutaka wajiepushe na watu watakaowashawishi kuvunja sheria za nchi.

Kwa upande wake, Msemaji wa Shirikisho hilo Adamu Kyando amesema uvumi unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Aprili 26 bodaboda watashiriki si kweli kwani hakuna bodaboda yeyote atakayeshiriki maandamano hayo.

"Kuna taarifa zinazosambaa kwenye mitandao yakijamii ikihamasisha bodaboda kushiriki maandamano taarifa hizi si za kweli na ni batili," amesema Kyando.

Amesema kwa yeyote atakayeshiriki maandamano hayo uongozi hautahusika kwani taarifa zinazosambazwa hazitoki kwenye shirikisho hilo.

Shaidi Atema Cheche Mahakamani Kesi ya Bilionea Msuya...... Afunguka Siri Nzito Kuhusu Simu, Laini na Pikipiki Zilizotumika Katika Mipango ya Mauaji

$
0
0
Shaidi  Atema Cheche Mahakamani Kesi ya Bilionea Msuya...... Afunguka Siri Nzito Kuhusu Simu, Laini na Pikipiki Zilizotumika Katika Mipango ya Mauaji
Mahakama Kuu imeelezwa kuwa simu, laini na pikipiki zilizotumika katika mipango ya mauaji ya bilionea Erasto Msuya, zilinunuliwa kwa maelekezo ya mshtakiwa wa kwanza, Sharifu Mohamed.

Pia, mahakama chini ya Jaji Salma Maghimbi anayesikiliza kesi hiyo, ilielezwa kuwa baada ya kumkamata Sharifu aliwataja watu wengine wawili ambao ni Shaibu Mredii (mshtakiwa wa pili) na Joseph Chussa (sio miongoni mwa washtakiwa wa kesi hiyo kwa sasa).

Hayo yamo katika ushahidi wa shahidi wa 27 wa upande wa mashtaka, mkaguzi wa Polisi, Damian Chilumba, aliyedai ujumbe wa mwisho (SMS) uliotumwa kwenye simu ya marehemu, saa chache kabla ya kuuawa Agosti 7, 2013 uliwasaidia makachero kuwanasa watuhumiwa.

Shahidi huyo wa Serikali, jana alipata fursa ya kusoma maelezo ya mashahidi watatu, Hamisa Kassim, Evelyne Munis na Shaaban Mahmoud ambao wametoweka na hawajulikani walipo.

Chilumba ambaye alikuwa kiongozi wa timu ya mawasiliano ya kimtandao (Cyber), alidai mahakamani jana kuwa timu yake ndiyo iliyobaini uwapo wa namba ya mwisho iliyowasiliana na marehemu.

Akiongozwa na wakili mwandamizi wa Serikali, Abdallah Chavulla kutoa ushahidi wake, shahidi huyo alidai baada ya kufanikiwa kuondoa neno la siri katika simu za marehemu, walikuta SMS mbili.

Kwa mujibu wa shahidi huyo, baada ya kufungua simu mojawapo ya marehemu, walikuta SMS hizo zikiwa zimetumwa kupitia namba ya mtandao wa Airtel siku moja kabla ya mauaji na siku ya mauaji.

“Ujumbe wa kwanza ulitumwa tarehe 6/8/2013 ukimjulisha (marehemu) kuwa ‘nina riziki’ na ujumbe wa tarehe 7/8/2013 saa nne au saa tano hivi ulisema niko Kia nakusubiri hapa,” alidai shahidi huyo na kuongeza:

“Tulianza kufuatilia ujumbe huo (wa tarehe 7/8.2013) ambao ndiyo ulikuwa wa mwisho kwenye simu ya marehemu na saa chache baadaye akauawa. Tuliandika barua Airtel kupata taarifa zake.”

Katika barua hiyo, shahidi huyo alidai waliiomba kampuni ya Airtel kuwapa taarifa mmiliki wa laini hiyo ya simu, ilikosajiliwa na kwa wakati huo ilikuwa ikisomeka eneo gani.

Alidai kuwa majibu ya Airtel yalionyesha kuwa laini hiyo ilikuwa imesajiliwa Arusha Agosti 3, 2013 kwa jina la Motii Mongululu lakini wakati huo haikuwa tena hewani.

“Walituambia baada ya kusajiliwa, laini hiyo ilifanya mawasiliano na namba nne tu na wakatuambia iliwahi kuchomekwa kwenye handset (simu) ambayo inatumia namba nyingine,” alidai na kuongeza:

“Tulifanikiwa kumkamata dada mmoja pale Arusha kituo kikuu cha mabasi anaitwa Hamisa (Kassim), ambaye ndiye mwenye hiyo namba, ambaye alikumbuka kusajili line kwa jina la Motii Mongululu.”

Hata hivyo, shahidi huyo alidai katika mahojiano, Hamisa aliwaeleza kuwa alisajili laini hiyo kwa maelekezo ya wakala mwenzake aliyemtaja kuwa ni Aneth Shija ambaye naye alikamatwa.

“Aneth alikiri ndiye aliyempa maelekezo Hamisa kusajili hiyo laini na nyingine mbili na kwamba, alizisajili kwa maelekezo ya mtu aliyemtaja kuwa ni Adam ambaye ni kijana wa kimasai,” alieleza.

Shahidi huyo alidai kupitia kwa Aneth walifanikiwa kupata namba ya Adam ambaye alikamatwa Mirerani, lakini naye akadai aliagizwa na mshtakiwa wa tatu, Mussa Mangu kusajili laini hizo.

Mkaguzi huyo wa polisi aliieleza mahakama kuwa baada ya Mangu kukamatwa na kuhojiwa, alikiri kusajili laini hizo za simu lakini naye akadai kuwa alitumwa na mshtakiwa wa kwanza, Sharifu.

“Alituambia maelekezo ya kusajili laini na kununua simu alipewa na bosi wake aliyemtaja kuwa ni Sharifu Mohamed. Alitueleza kuwa kwa ufahamu wake, yote yalikuwa ni maandalizi ya mauaji.

“Siku hiyo hiyo tulimkamata Sharifu nyumbani kwake na katika mahojiano ya awali alimtambua Mussa kama mfanyakazi wake na kukiri vitu vyote vilivyonunuliwa naye vilikuwa maelekezo yake,” alieleza.

Alivyomtaja Chusa

Shahidi huyo ambaye sasa yuko Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, alitaja vitu ambavyo Sharifu aliwaelekeza Mangu na Adamu wavinunue ni simu mpya, laini za simu na pikipiki mbili mpya.

“Kutoka kwa Sharifu akatuongezea watu wengine wawili ambao ni Shaibu Mredii (mshtakiwa wa pili) na Joseph Chussa (si miongoni mwa washtakiwa wa kesi hiyo kwa sasa),” alidai shahidi huyo.

Chussa alikuwa miongoni mwa washtakiwa katika kesi hiyo kwenye hatua za awali, lakini mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP) kwa kutumia mamlaka yake, alimfutia mashtaka hayo Aprili 17, 2014.

Shahidi huyo alieleza kuwa Mredii alikamatwa na polisi akiwa Mirerani na kazi ya kuwatafuta washtakiwa wengine katika kesi hiyo iliendelea na alikamatwa mshtakiwa wa nne, Jalila Zuberi.

Aliieleza mahakama kuwa timu mbalimbali za upelelezi ziliendelea na kazi ya kuwasaka watuhumiwa na kufanikiwa kuwakamata washtakiwa Karim Kihundwa, Sadick Jabir na Ally Majeshi.

Mkaguzi huyo wa polisi alidai baada ya kukamatwa kwa Karim na Sadick wilayani Kaliua mkoani Tabora, Sadick anadaiwa kuelekeza mahali alipoficha bunduki iliyotumika katika mauaji hayo.

Timu ya makachero ikiongozwa na mkuu wa upelelezi (RCO) Mkoa Kilimanjaro, Ramdhan Ng’anzi walikwenda Sanya Juu wilayani Siha na kufanikiwa kuipata bunduki hiyo.

Shahidi huyo alidai ndiye aliyewapeleka washtakiwa Karim na Sadick ofisi ya mkemia mkuu wa Serikali Arusha kwa ajili ya kuchukuliwa sampuli za vinasaba (DNA) na jaketi lililopatikana eneo la tukio.

Pia, shahidi huyo aliieleza mahakama kuwa yeye na shahidi wa nane, mkaguzi msaidizi wa polisi, Herman Mutungi, ndio waliopeleka bunduki hiyo kwa mtaalamu wa milipuko jijini Dar es Salaam.

Akingozwa na Chavulla ambaye kwa jana alisaidiana na Ignas Mwinuka, shahidi huyo alidai ndiye aliyeandika maelezo ya mashahidi watatu ambao hawapatikani.

Shahidi huyo aliiomba mahakama ipokee maelezo ya mashahidi hao, Hamisa Kassim, Evelyne Munis na Shaaban Mahmoud, ombi ambalo lilikubaliwa na mahakama na akapata fursa ya kuyasoma.

Maelezo ya Hamisa

Katika maelezo yake, Hamisa aliyekuwa wakala wa kusajili laini za simu, alieleza kuwa rafiki yake aitwaye Aneth Shija, alimweleza kuwa kuna kijana wa kimasai aitwaye Adam anamtaka kimapenzi.

“Huyo Aneth mara nyingi anasajili laini zake bila kufuata utaratibu, mara ya mwisho alisajili laini tatu yaani tarehe 5/8/2013 na 6/8/2013. Mtu anayetaka kusajili laini lazima awe na kitambulisho.

“Nakumbuka 5/8/2013 alikuja Adam akiwa na mwenzake wakiongea lugha ya kimasai lakini Aneth hakuwapo na alikuwa amemwachia ofisi yake dada mmoja anaitwa Eva (Evelyne Munisi),” anaeleza.

Kulingana na maelezo hayo, Hamisa anadai alimuona Eva anajaza fomu kwa ajili ya kumsajilia laini huyo Adam, lakini hakukuwa na kitambulisho ila hazikupokea vocha.

“Kutokana na matatizo hayo, huyo Eva alikuja kwangu nikawaambia ni tatizo tu la mtandao. Waliondoka na siku iliyofuata walikuja tena na kupewa zile laini zikiwa zinafanya kazi,” alidai.

Maelezo ya Evelyne

Akisoma maelezo ya Evelyne, shahidi huyo alimnukuu akisema alifahamiana na Aneth alipokwenda siku moja kusajili laini yake ya Tigo katika kituo hicho cha mabasi Arusha na wakawa marafiki.

“Siku moja tarehe 3/8/2013 nikiwa Moshi niliona simu ya Aneth akinipigia nikamwambia niko njiani nakwenda Arusha. Nilipofika Arusha aliniomba nimsaidie kubaki kwenye ofisi yake,” anaeleza.

Evelyne ambaye alikuwa mwanafunzi wa Chuo cha Nairobi Institute cha jijini Arusha, anadai siku moja Aneth alimpigia simu na kumweleza kuna kijana atakuja amsajilie simu kwa jina la Motii Mongululu.

“Nilimpelekea Hamisa anisaidie kumsajilia hizo laini. Alikuja Adam na kuchukua hizo laini mbili nilizozisajili kwa jina la Motii Mongululu, ingawa niliona alishasajili tena kwa jina la Motii Ndoole.

“Tarehe 6/8/2013, Aneth alinipigia tena simu akaniambia nichukue laini nisajili kwa jina la John Francis. Nilimpelekea Hamisa nikamwambia Aneth kasema Adam atakuja kuichukua,” alieleza.

Katika maelezo ya shahidi mwingine, Shaaban Mohamed, alinukuliwa akisema siku asiyoifahamu Agosti 2013, alifika nyumbani kwake eneo la Bomang’ombe, mtu aliyemtaja kwa jina la Said Jabir.

Shaaban anadai Said alikuja na pikipiki mpya aina ya King Lion nyeusi na alipomuuliza kama amenunua, alimweleza ni ya kaka yake ambaye ni mshtakiwa wa sita, Sadik Jabir.

Hata hivyo, anadai baada ya siku kadhaa kupita, Said alikuja na makachero wa Polisi wakiitaka pikipiki hiyo na alimweleza akaichukue mahali alipokuwa ameipaki ndani ya nyumba yake.

Mkaguzi huyo wa polisi katika ushahidi wake, alidai yeye ndiye aliyekabidhiwa pikipiki hiyo na kurudi nayo Moshi, alimkabidhi Inspekta Samwel Maimu aliyekuwa mtunza vielelezo.

Kesi hiyo itaendelea leo kwa jopo la mawakili wa utetezi linaloundwa na Hudson Ndusyepo, Majura Magafu, Emmanuel Safari na John Lundu, watakapopata nafasi ya kumdodosa shahidi huyo.

Mgogoro Udart, Maxmalipo Watua Bunge

$
0
0
Mgogoro Udart, Maxmalipo Watua Bunge
Mgogoro kati ya Kampuni ya Usafiri wa Mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (Udart) na Kampuni ya Maxicom Tanzania (Maxmalipo) umetua bungeni leo baada ya Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson kumuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kuutolea maelezo wakati akihitimisha hoja ya bajeti ya wizara yake.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia (CCM), kuomba mwongozo kwa Naibu Spika kuwa serikali itoe maelezo kuhusu mgogoro huo uliozua usumbufu kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kwa muda wa siku tatu sasa.

“Mgogoro huo umesababisha abiria wanaotumia usafiri huo Dar es Salaam kutoka sehemu mbalimbali za jiji kupata usumbufu kwa kukosekana kwa mashine za eletroniki za kutolea tiketi ambayo imesababisha usumbufu lakini pia kuna upotevu wa fedha kwenye upatikanaji wa tiketi hizo jambo lililosababishwa na mgogoro huo wenye harufu ya ufisadi,” amesema.

Hoja hiyo ya Mtulia iliungwa mkono na Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema) ambaye aliomba mwongozo kwa Naibu Spika kuwa bunge litumie kanuni ya 47 kusitisha shughuli za bunge na kujadili mgogoro huo kwa dharura.

Akijibu miongozo hiyo Dk. Tulia amesema kwa kuwa miongozo hiyo inahusiana na hoja ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi inayohitimishwa leo, waziri husika alitolee maelezo.

“Waziri wakati unahitimisha hoja yako bunge linakuagiza ulitolee maelezo suala hili. Lakini pia haliwezi kusitisha shughuli zake na kulijadili kwa dharura kwa sababu waziri utalitolea maelezo leo baadaye,” amesema Naibu Spika.
Viewing all 104687 articles
Browse latest View live




Latest Images