Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Kutana na Mtaalam wa Matabibu ya nyota za Binadam na Bingwa wa Tiba za Asili Afrika Mashariki.

$
0
0
Je Wewe ni Mwanasiasi, Mfanyabiashara , Msani, ama mwanafunzi tunazo dawa na pete za bahati zenye uwezo mkubwa wakuyabadilisha maisha yako nakukupatia mafanikio makubwa ndani ya mda mfupi tu.

Kutana na SHABA WA SHABA kutoka Tanga,
Yeye ni mtaalam na mtabibu wa nyota za binadam na bingwa wa tiba za asili Afrika mashariki.
Wasiliana na mtaalam huyu kwani yeye ufaulu pale wote waliko shindwa na pia humaliza kazi zilizo shindikana ama zilizo achwa ndani ya siku1 tu. Sasa amezianza ziyara zake za mikoani na atayatembeleye maeneo mbali mbali ndani na inje ya nchi.

Anatibu magonjwa sugu yanaojulikana nasiojulikana kwakutumia maji, Kioo na mitishamba.
Anazo dawa za mapenzi, kumrudisha alipoteya, kutoa Mikosi, Kutatuwa shida za chumaulete, mvuto wa biashara na sehem za kazi, kusafisha nyota, kurudisha mali zilizo ibiwa, zilizpotea, ama zilizodhulumiwa, kushika wezi na wachawi, kutoa ndagu , Kutoa kinga ya mwili, nyumba, Biashara, kufukuza majini wabaya, Kuuza kwa haraka ( shamba, nyumba, Gari,...), Kesi mahakamani, Kuweka Zindiko ya mwili, nyumba, shamba, Gari, kupata Kazi na kupandishwa cheo, mali na utajiri bila masharti na mengine mengi ya Siri...

Kwa tiba na ushauri wasiliana na ofisi kwa nambari ya simu :
+255 785 358 267 ,
+255 785 358 267

Irene Uwoya Afunguka Sababu ya Kuchora Tatuu ya Masogange " Haikuniuma Hata Kidogo Tofauti na Tatuu Nyingine

$
0
0
Irene Uwoya Afunguka Sababu ya Kuchola Tatuu ya Masogange " Haikunimuma Hata Kidogo Tofauti na Tatuu Nyingine
STAA mkali wa filamu Bongo, Irene Uwoya amefunguka kuwa ‘tatuu’ aliyoichora kama kumbukumbu kwa rafiki yake kipenzi, video queen maarufu Bongo, Agness Gerald ‘Masogange’ haikumuuma hata kidogo tofauti na tatuu nyingine alizozichora mwilini mwake.



Akizungumza na Amani, Uwoya alisema kuwa kuchora tatuu hiyo mkononi mwake kunaonesha wazi Agness anaendelea kuishi ndani ya moyo wake siku zote na atamkumbuka sana kipindi chote cha urafiki wao wakati wa enzi za uhai wake.


“Nimechora tatuu ya Masogange sikuhisi maumivu kama niliyosikia nilipochora tatuu nyingine mwilini mwangu, nafikiri ni kutokana na uchungu mkali niliokuwa nao na kingine ni kwamba nimechora jina hili mkononi mwangu najua kila nikiliangalia nitapata amani ya moyo,” alisema Uwoya

Steve Nyerere Kuwachangisha Wasanii Kumsafirisha Mzee Majuto Kwaajili ya Matibabu India

$
0
0
Steve Nyerere Kuwachangisha Wasanii Kumsafirisha Mzee Majuto Kwaajili ya Matibabu India
Wasanii wa filamu nchini Tanzania wakiwakilishwa na Steve Nyerere pamoja na Aunt Ezekiel Jumatano hii wamemtembela muigizaji mkongwe nchini, King Majuto, ambaye amelazwa katika Hospitali ya Tumaini iliyopo Upanga Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kumjulia hali hospitalini hapo Mwenyekiti wa Wasanii, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’, amesema kutakuwa hakuna haja ya wasanii hao kutoa michango mikubwa mara tu, mzee Majuto atakapopoteza maisha, kwahiyo wamejipanga na kumtafutia tiketi mbili ili aweze kwenda India kupata matibabu.

TID Awapa Makavu Wasanii Wanaotangaza Ndoa

$
0
0
TID Awapa Makavu Wasanii Wanaotangaza Ndoa
Mkongwe wa BongoFleva Khalid Mohamed maarufu kwa jina la TID au Mzee Kigogo amesema hayupo tayari kuoa kwa sasa kama wasanii wenzake wanavyofanya kwa madai wengi wao wanatumia ndoa kama kutengeneza kiki katika mitandao ya kijamii na sehemu zinginezo.


TID ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kupita takribani siku 24 tokea msanii huyo kutangaza wazi kuwa yupo katika mahusiano na mwanadada mmoja ambae alikuwa nae nchini Germany jambo ambalo wengi wao walitarajia kuoa ndoa ikifuata katika siku za usoni.

"Sijasema kama ninaoa mwezi wa sita (Juni) ila tulikuwa tunajifurahisha mimi na rafiki yangu usingizi katika 'comment' instagram ilikuwa utani tu sijafikilia kuwa hivyo. Unajua sasa hivi watu wanataka kutengenezea kama kiki kitendo cha kuoa, kwa hiyo mimi sio mtu kutafuta kiki kwa kutumia ndoa", amesema TID.

Mbali na hilo, TID hakusita kutoa siri za swahiba wake wa miaka mingi Q-Chief kwamba alishawahi kutangaza kutaka kuoa lakini mpaka sasa hakuna chochote alichokifanya.

Mbeya City Yamponza Kocha wa Simba, Yanga

$
0
0
Mbeya City Yamponza Kocha wa Simba, Yanga
WAKATI homa ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga ikizidi kupamba moto, uongozi wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) kwa kushirikiana na Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) umekumbana na changamoto kubwa kuhusiana na mwamuzi atakayechezesha mechi ya watani hao wa jadi itakayofanyika Aprili 29, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Changamoto hiyo inatokana na mwamuzi aliyekuwa amepangwa kuchezesha mchezo huo hapo awali kukumbana na kashfa ya kuboronga katika mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Mbeya City na Yanga iliyofanyika hivi karibuni kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.



Mwamuzi wa mechi hiyo alikuwa ni Shomary Lawi kutoka Kigoma ambaye anadaiwa kushindwa kuumudu mchezo huo kutokana na kukosa umakini baada ya kuruhusu mchezaji aliyekuwa amefanyiwa mabadiliko kuingia tena uwanjani na kuendelea na mchezo.


Habari za kuaminika ambazo Championi Jumatano limezipata kutoka ndani ya TFF zimedai kutokana na Lawi kuboronga kwake katika mchezo wa Mbeya City na Yanga, uongozi wa Bodi ya Ligi pamoja na Kamati ya Waamuzi ya TFF, unaangalia ni cha kufanya kuhusiana na mwamuzi huyo, kama ataachwa achezeshe mechi hiyo au aondolewe na nafasi yake ichukuliwe na mwamuzi mwingine.

Alipotafutwa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura ili aweze kuzungumzia hilo hakupatikana.

Hapa Ndipo Atakapozikwa Obama?

$
0
0
Hapa Ndipo Atakapozikwa Obama?
Marais saba wa Marekani na wake zao wamezikwa katika maeneo ya maktaba na makumbusho zilizobeba kazi zao za tangu ujanani hadi katika uongozi wa Taifa hilo.

Pia marais wote wa Taifa hilo wana utamaduni wa kutaja eneo watakalozikwa, kwa kuwa utangazaji hufanyika mara tu waingiapo Ikulu au wawapo katika mbio za kuwania kuingia Ikulu.

Hatua hiyo hufanyika ili kutoliweka Taifa katika sintofahamu pindi wanapoondoka duniani ghafla. Kwa sasa Marekani haina sheria ya eneo maalumu la mazishi ya viongozi kama zilivyo baadhi ya nchi zilizoendelea kutokana na kila mmoja kuwa na wosia wake tangu anapoanza maisha ya kujitegemea.

Hata hivyo, wakati huo ukiwa utamaduni wa kawaida wa marais hao kuwa na mahala wanapochagua kuzikwa washindapo uchaguzi kwa mara ya kwanza, Rais wa 44 wa Taifa hilo, Barack Obama hakufanya na hajafanya hivyo hadi sasa.

Maeneo walikozikwa marais wa Marekani yapo katika majimbo 23 ikiwemo District of Columbia. Marais 45 wameitawala nchi hiyo tangu mwaka 1789. Kati yao, 38 wamefariki dunia.

Jimbo lenye makaburi mengi walikozikwa marais ni Virginia walikozikwa saba. Tangu 1789, Wamarekani 49 wamehudumu kama makamu wa rais, kati yao 41 walishafariki dunia. Jimbo lenye makaburi mengi ya makamu wa rais ni New York walipozikwa 10.

Kizungumkuti cha Obama

Kwa upande wa Obama, inaelezwa kwamba hadi mwisho wa utawala wake ulioanza 2009 hadi 2017 hakueleza atazikwa wapi, iwe kwa maandishi au mdomo kwa wasaidizi wake.

Kwa wasaidizi na watu wake wa karibu ilibaki kuwa iwapo ingetokea akafariki dunia ghafla, basi angezikwa katika Jimbo la Chicago mahali ambako nyota yake ya kisiasa ilianzia kung’ara.

Hata hivyo, ikiwa ni zaidi ya miaka miwili sasa tangu astaafu, Obama yuko ‘bize’ na ujenzi wa makumbusho ya kazi zake ambayo pia itatumika kama maktaba katika eneo la Jackson Park, Chicago, mahala ambapo pia wengi wanadhani kaburi lake litajengwa hata kabla hajafa. Pia ni katika eneo hilo anapojenga makumbusho panatajwa kuwa ndipo mkewe, Michelle atakapozikwa. Marais saba wa Marekani na wake zao wamezikwa kwenye makumbusho au maktaba walizoanzisha, utaratibu ulioasisiwa mwaka 1945 baada ya kifo cha rais wa 32, Franklin Roosevelt.

Roosevelt alizikwa katika Makumbusho ya Taifa ya Historia ya Franklin Roosevelt iliyopo Hyde Park, New York.

Swali lililopo vichwani mwa wengi na ni Obama pekee mwenye jibu,

INAENDELEA UK 18

INATOKA UK 17

ni lile la mwanasiasa huyo aliyeondoka madarakani akiwa na miaka 55 atazikwa katika Jackson Park au wapi?

Taarifa za ndani zinadai makumbusho hiyo inayojengwa katika eneo la kati ya eka 23 hadi 24 haionyeshi kuwapo ramani ya kaburi au makaburi ya familia yake, ingawa kwa thamani ya ‘mjengo’ na ardhi vinavyofikia zaidi ya Dola 300 milioni za Marekani (zaidi ya Sh700 bilioni) lolote linaweza kufanyika iwe sasa au baadaye.

Baadhi ya wadadisi wa mambo wanasema utamaduni wa viongozi wa Taifa hilo kuzikwa katika makumbusho au maktaba zao umepitwa na wakati na kwamba, ni vyema kukawa na eneo maalumu la kihistoria litakalotumika kama sehemu ya makaburi ya marais walioitawala Marekani.

Hata hivyo, wanaopinga wana hoja kuwa makumbusho au maktaba zao kutengewa maeneo ya makaburi ni jambo jema na linavutia makumi kwa maelfu ya watu kuzitembelea ili kujionea vitu mbalimbali vilivyotunzwa.

“Palipo na kaburi kwenye maktaba ya rais, hilo ni jambo jema maana linavuta hisia za watu kufika na kujionea vitu vilivyomo,” anasema Benjamin Hufbauer, Profesa wa Chuo Kikuu cha Louisville ambaye pia ni mwandishi wa kitabu cha Presidential Temples: How Memorials and Libraries Shape Public Memory.

Profesa Hufbauer anasema, hata hivyo ni vyema Obama na familia yake wakazingatia kwamba kuweka eneo watakapozikwa katika maktaba hiyo ni jambo muhimu kwa sababu ya sifa tofauti alizonazo.

“Kwanza Obama alikuwa rais mweusi wa kwanza na pili, kizazi chake kina mchanganyiko wa uhamiaji na ukazi (wa Marekani) hivyo itakuwa vizuri zaidi akiwa na eneo hilo ambalo pia litawavuta mamilioni ya Waafrika na Wazungu kulitembelea,” anasema.

Marekani kuna maktaba na makumbusho 13 za marais, lakini ile ya Obama itakuwa chini ya Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka cha Taifa, ingawa kutokana na baadhi ya nyaraka alizotumia kama rais kuhifadhiwa maeneo tofauti haitapata fungu la fedha la kujiendesha kutoka kituo hicho. Kituo hicho ni idara ya Serikali.

Ingawa hadi sasa atakapozikwa Obama hapajafahamika, marais wanaoondoka madarakani wanatakiwa kiutaratibu kueleza watakapozikwa kwa mkuu majeshi kupitia kitengo cha huduma za wastaafu na zaidi ya hilo wanapaswa kupata ushauri wa kitalaamu, na hasa inapotokea kuwa sehemu hizo zinakuwa na masilahi mengi ya nchi.

Familia itaamua atakapozikwa

Kigingi kingine kinachoweza kuikabili makumbusho ya Obama ni kile cha iwapo ataamua kuwa eneo la makaburi liwepo ndani yake, sheria za Illinois zinataka kibali mpaka kitolewe baada ya usanifu mpya kuwasilishwa. Kwa sasa si Obama, taasisi yake wala makumbusho anayoijenga iliyowasilisha ombi hilo.

Licha ya kwamba rais huyo mstaafu hajafanya lolote mpaka sasa, na ukweli kwamba kifo hakipigi hodi, wanafamilia wataamua wapi watamfanyia maziko iwapo atafariki dunia kabla hajaamua atakapozikwa lakini vyovyote iwavyo mwili wake hautazikwa nje ya Chicago mahali ambako alikulia na kupatia umaarufu wake kisiasa.

Kwa mujibu wa watu wa karibu wa Obama, makumbusho yake inayotarajiwa kuzinduliwa miaka minne ijayo, itakuwa ya kisasa na yenye hadhi ya juu zaidi ikizingatiwa kwamba ndiye rais wa saba bora zaidi nchini humo (kwa mujibu wa utafiti wa mashirika makubwa matano ya habari nchini Marekani).

Marais 10 bora wa Marekani na ubora wao kwa mujibu wa mashirika hayo kwa kufuatia mtiririko ni Abraham Lincoln, George Washington, Franklin Roosevelt, Theodore Roosevelt, Thomas Jefferson, Harry Truman, Dwight Eisenhower, Obama, Ronald Reagan na Lyndon Johnson.

“Kama kutakuwa na eneo la makaburi nadhani litakuwa linatembelewa na watu wengi wakiwamo watalii kuona atapokuwa ‘amelala’ mmoja wa viongozi bora zaidi wa Marekani,” anasema mmoja wa wasaidizi wa Obama.

Mtendaji mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Makumbusho Afrika na Marekani iliyopo Charleston, Michael Boulware anasema utembeleaji wa maeneo ya kihistoria unamfanya mtu aguswe na historia husika.

“Unaweza kusikia hadithi popote, unaweza kuisoma kwenye vitabu viwili au vitatu, lakini kuwa katika eneo husika kunaongeza uwezo wa akili kujihisi ni sehemu ya historia,” anasema.

“Sidhani kama kuna swali kwamba Rais Obama hatakufa, lakini kama rais mwenye rekodi (zilizotukuka) na historia ya aina yake, anastahili kuenziwa na kadri muda unavyokwenda ataendelea kuonekana bora zaidi kihistoria.”

Obama pia anaweza kuamua kuzikwa katika Jimbo la Hawaii, huko ndiko alikozaliwa na kutumia muda mwingi wa ujana akilelewa na mama yake, Ann Dunham. Pia, Hawaii ndilo eneo maarufu kwa familia yake analolitembelea kila mara na pia Obama anaweza kuwa rais wa kwanza wa Marekani kwa mabaki ya mwili wake kuchomwa moto, utamaduni ambao unafanywa na jamii kubwa ya Kiasia nchini humo.

Walivyozikwa baadhi ya marais

Harry Truman alizikwa kwenye maktaba na makumbusho yake iliyopo eneo la Independence, Mo; Ronald Reagan alizikwa katika maktaba na makumbusho yake, Simi Valley, California; Herbert Hoover alizikwa kwenye maktaba na makumbusho yake West Branch na Dwight Eisenhower kwenye eneo la shughuli zake la Abilene lililopo Kansas.

Wengine ni Richard Nixon aliyezikwa kwenye viwanja vya maktaba ya rais vya Yorba Linda huko California na Gerald Ford aliyezikwa kwenye makumbusho yake ya Grand Rapids iliyopo Michigan.

Hata hivyo, John F. Kennedy na Lyndon Johnson hawakuzikwa kwenye maktaba na makumbusho zao zilizopo Boston na Austin. Kennedy aliyeuawa kwa risasi jijini Dallas, Texas, Novemba 22, 1963 alizikwa katika makaburi ya Arlington, ilhali Lyndon alizikwa kwenye ranchi ya familia iliyopo Texas.

Kati ya marais watano wa zamani wanaoishi, Jimmy Carter amekuwa akizungumza mara kwa mara juu ya mahala atakapozikwa akisisitiza kuwa lazima iwe katika mji aliozaliwa wa Plains uliopo Georgia. Maktaba na makumbusho yake ya kirais ipo Atlanta, mji ambao upo mbali na Georgia.

Oktoba, 2017 mtangulizi wa Obama, George W. Bush alitangaza kuwa yeye na mkewe Laura watazikwa kwenye makaburi ya Taifa ya Texas yaliyopo Austin. Baba yake, George H.W. Bush na mkewe Barbara wana eneo lao ndani ya maktaba na makumbusho ya kirais iliyopo Texas A&M University na tayari mkewe Barbara amezikwa katika eneo hilo Aprili 21 mwaka huu.

Kwa upande wa Bill Clinton na mkewe Hillary pia hawajatangaza watakapozikwa, lakini zipo fununu juu ya Washington kuwa ndio mji watakapozikwa na hawajakanusha taarifa hiyo.

Kauli za mabosi wa makumbusho

Mkurugenzi mtendaji wa maktaba na makumbusho ya Harry Truman, Kurt Graham anasema ukweli kwamba eneo hilo lina kumbukumbu nyingi za rais huyo wa zamani, lakini pia kuzikwa kwake hapo kunaamsha hisia zaidi za wageni wanaopatembelea, linaongeza umakini na tafakuri ambayo huwezi kuipata katika maonyesho yoyote duniani.

Truman alizikwa pembeni mwa kaburi la mkewe, Bess ndani ya maktaba hiyo na bintiye na mjukuu wake waliozikwa kando kidogo ya wawili hao.

Katika maktaba na makumbusho za akina Nixon na Reagan, wageni huyachukulia makaburi yao kama maeneo fulani ya matambiko, kukiwa na ukimya mkubwa wawapo sehemu hizo.

Msemaji wa Taasisi ya Reagan, Melissa Giller anasema: “ Sidhani kama wageni hawahisi hisia za ajabu kwa kuwa Rais Reagan na mkewe walizikwa hapa. Hapa wageni siku zote wako kwenye makaburi yao wakitoa heshima na baadhi yao pia huja na maua na kuyaacha juu ya makaburi haya.

Imekusanywa na Kulwa Magwa kwa msaada wa taarifa mbalimbali

Serengeti Boys Yatinga Fainali Michuano ya CECAFA

$
0
0
Serengeti Boys Yatinga Fainali Michuano ya CECAFA
Vijana wa Serengeti Boys imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya CECAFA chini ya umri wa miaka 17 inayoendelea huko nchini Burundi.

Serengeti Boys wamefanikiwa kutinga kwenye hatua hiyo baada ya kuifunga Kenya kwa mabao 2-1 kwenye mchezo huo ambao umechezwa kwenye uwanja wa Muyinga.

Mabao ya Serengeti yamefungwa na Jafar Juma (21) na Kelvin Paul (62).

Professor Jay Alivyoingia na Style ya Kurap Bungeni

$
0
0
Hapa nakukutanisha na Mbunge wa Mikumi Joseph Haule maarufu Professor Jay baada ya kupewa nafasi ya kuchangia mapendekezo yake katika makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambapo akaamua kuingiza style za kurap baada ya kupewa dakika chache za kuchangiua.


VIDEO

Wanawake Wapewa Adhabu ya Kuchimba Kaburi na Kijiji Kisa Hiki Hapa

$
0
0
Wanawake Wapewa Adhabu ya Kuchimba Kaburi na Kijiji Kisa Hiki Hapa
Ni kawaida na ni utamaduni wa sehemu nyingi duniani wanaume kuchimba kaburi na kuwaachia wanawake shughuli nyingine za jikoni wakati wa msiba.

Lakini sivyo ilivyokuwa kwa wanawake wa Mtaa wa Bwihegule wilayani Geita. Wanawake hao wa Kata ya Mtakuja walilazimika kuchimba kaburi, ikiwa ni adhabu iliyotokana na tuhuma kuwa wanahusika na vifo vya ghafla vya wanaume mtaani hapo.

Tukio hilo lililoibua hisia na maoni mchanganyiko kutoka kwa walioshuhudia lilitokea Aprili 24 baada ya mkazi wa mtaa huo, Nkangiko Vigume (57), kufariki dunia ghafla Aprili 23.

Wanaume saba wafariki

Habari kutoka mtaani hapo zinasema amri ya kutaka wanawake kuchimba kaburi na kulala matanga ilitolewa na mtemi, ambaye ni kiongozi wa mila wa jamii ya Wasukuma mtaani hapo, Kahema Nsabilando.

Alitoa amri hiyo baada ya uamuzi kufikiwa kwenye kikao cha dharura kilichojadili matukio ya vifo vya ghafla vya wanaume mtaani hapo.

Wakazi waliitisha kikao hicho kujadili vifo vya ghafla vya wanaume baada ya Vigume kufariki Aprili 23 na kufanya idadi ya waliokufa kufikia saba.

“Hili ni tukio la saba wanaume wanafariki ghafla hapa mtaani kwa kuumwa kichwa. Vikao vya wananzengo vimeshafanyika na kuwaonya akina mama kuacha mambo haya (ya kuhusika na mauaji ya kishirikina ya wanaume), lakini wamerudia tena,” alisema Nsabilando.

“Tumechoshwa na lazima waadhibiwe kwa kuachwa walale matanga na kuchimba kaburi wenyewe kwa mujibu wa mila na desturi.”

Kifo na matukio ya ajabu

Akisimulia yaliyojiri kabla ya kikao kilichotoa uamuzi, Nsabilando alisema baada ya Vigume kufariki dunia, utaratibu wa kuandaa mwili kwa ajili ya mazishi ulifanyika lakini yalitokea matukio aliyodai ni ya ajabu yakiashiria kifo chake hakikuwa cha kawaida.

“Wazee tuliuandaa mwili wa marehemu na kuulaza kitandani mikono ikiwa imenyooshwa, lakini baada ya muda mfupi tuliona mikono imewekwa kifuani,” alidai.

Kiongozi huyo alidai kilichowashtua zaidi hadi kufikia uamuzi wa kutoa adhabu ni mwili huo kukutwa umelala kifudifudi licha ya kuachwa kitandani ukiwa chali.

Kuhusu vifo tata mtani hapo, Mbares Mabula ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya maafa, alisema ndani ya miaka miwili kumekuwa na vifo vyenye utata vya wanaume vinavyosadikiwa kusababishwa na wanawake wanaotuhumiwa kutaka kutaka kurithi mali.

Alidai baadhi ya waliokufa na kuzikwa, wanaonekana mitaani katika mazingira yanayotatanisha, hivyo kuibua hofu ya ushirikina.

Licha ya mwandishi wa Mwananchi kuwashuhudia polisi wanne katika eneo la tukio, wawili kati yao wakiwa na silaha, kamanda wa polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema jana kuwa ofisi yake haina taarifa hizo.

Lakini mkuu wa wilaya, Herman Kapufi alisema uchunguzi wa awali umebaini limesababishwa na imani potofu za kimila na kuahidi hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote waliohusika.

“Hivi ni vitendo vya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake. Serikali haiwezi kuvivumilia, tutafanya uchunguzi na kuchukua hatua dhidi ya walioamuru wanawake kuchimba kaburi ili kuvikomesha,” alisema Kapufi.

Kapufi alisema imani za kishirikiana huchochea mauaji ya watu kwa kukatwa kwa mapanga katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Wanawake walonga

Baadhi ya wanawake waliofanya adhabu hiyo hawakukubaliana na uamuzi huo.

“Hatukubaliani na uamuzi, lakini hatuna la kufanya kutokana na mabavu ya wanaume ambao baadhi hutushurutisha kwa fimbo kuchimba kaburi,” alisema Specaoza Salum, mmoja wa wanawake walioshiriki kuchimba kaburi.

Mwanamke mwingine, Kabula Shija alisema pamoja na kulala matanga na kukamilisha uchimbaji kaburi kabla ya saa 7:00 mchana siku hiyo ya Aprili 24, wanaume hao pia waliwaagiza kuhakikisha wanapika na kuwapa chakula kabla ya muda huo.

Mwanamke mwingine, Suzan Mayala alisema adhabu hiyo haikujali hali zao kiafya wala majukumu ya kifamilia na kijamii kwa sababu ilihusisha wanawake wote wakiwemo wenye watoto wachanga.

Familia haikuweza kuzuia

Hata kama isingekubaliana na adhabu hiyo, familia ya wafiwa haikuwa na uwezo wa kuzuia utekelezaji wake.

Thomas Nzobano, kiongozi wa ukoo wa marehemu Vigume, alisema hawakuwa na uwezo wa kuingilia kati uamuzi wa wananzengo kwa sababu kiutaratibu hawaruhusiwi kujihusisha na masuala ya matanga na mazishi.

“Familia tunatakiwa kusubiri uamuzi na kufuata maagizo ya wananzengo kuhusu masuala yote ya mazishi. Hatujihusishi na kuchimba kaburi kwa kuwa hiyo ni kazi ya wanajamii,” alisema Nzobano.

Mwanafamilia mwingine, Ndakirwa Mkangiko ambaye ni mmoja wa watoto 12 wa Vigume, alisema familia imeshtushwa na kifo cha ghafla cha baba yao aliyeugua kichwa kwa muda mfupi.

Hasira zilizidi nguvu uongozi

Mwenyekiti wa Mtaa ya Bwihegule, Andrea Barnaba alisema hamaki na hasira ya wananchi kuhusu matukio ya vifo na madai ya mwili wa marehemu kugeuzwa ulipolazwa, ziliuzidi nguvu uongozi wa Serikali ya eneo hilo na kulazimika kuwaacha wananchi kuendelea na walichoamua.

“Hakuna mtu wala kiongozi yeyote aliyekuwa akisikilizwa na wananchi zaidi ya viongozi wa kimila wakiongozwa na mtemi. Kama viongozi tuliona ni busara kutotumia mabavu ili kuepuka madhara zaidi kutokana na hamaki waliyokuwa nayo wananchi,” alisema Barnaba.

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Jumamosi

$
0
0

Tanzia: Jay Dee Apata Pigo Afiwa na Mama Yake

$
0
0
Tanzia: Jay Dee Apata Pigo Afiwa na Mama Yake
MAMA mzazi wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, Bi. Martha Mbibo, amefariki dunia alfajiri ya leo Alhamisi Aprili 26, 2018.

Kaka wa Lady Jaydee ambaye pia ni msanii Dabo, amethibitisha taarifa hizo na amesema kwamba mama yao amefariki akiwa nyumbani kwake baada ya kuugua Saratani kwa muda mrefu.

Dabo amesema msiba upo nyumbani kwa marehemu Jet jijini Dar es salaam ambapo familia ya marehemu itatoa utaratibu wa mazishi mara baada ya utaratibu wa kuupeleka mwili hospitali kuhifadhiwa kukamilika.

April 01, 2018 Lady Jaydee kupitia Instagram aliandika;


Bi. Mbibo alianza kuugua tangu mwishoni mwa mwaka 2016 ambapo alipatiwa matibabu hapa nchini na nje ya nchini (India).

Mi Mzima Kabisa na Nikifa Mtapata Habari Zangu Popote Mlipo- Mzee Majuto

$
0
0
Mi Mzima Kabisa na Nikifa Mtapata Habari Zangu Popote Mlipo- Mzee Majuto
Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania, Amri Athuman maarufu Mzee Majuto amefunguka na kuwatoa wasiwasi wapenzi na mashabiki wake kiujumla kuwa yeye ni mzima kabisa na endapo Mungu atamchukua 'kufariki' basi watapata habari popote pale watakapo kuwepo.


Mzee Majuto ametoa kauli hiyo baada ya siku za hivi karibuni kuzushiwa kifo kwa mara nyingine tena baada ya yeye kuzidiwa na kurudishwa hospitalini kwa mara nyingine ili aweze kupatiwa matibabu juu ya ugonjwa unaomsumbua.

"Mimi ni mzima kabisa, watu msiwe na wasiwasi kama nikifa mtapata habari nyote kwamba mimi tayari nimeshaaga dunia na sina wasiwasi kwa sababu wazazi wangu wote hawapo, mtume wangu ninayempenda Mohamed (S.A.W) naye pia hayupo sasa sembuse mimi msihofu sana jamani", amesema Mzee Majuto.

Siku ya Jumatatu Aprili 23, 2018 Mzee Majuto alilazwa katika Hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam, baada ya kuzidiwa. Awali Majuto alilazwa hospitalini hapo mnamo Januari mwaka 2018 na kufanyiwa upasuaji wa ugonjwa wa tezi dume ambao ndio umekuwa ugonjwa wake mkubwa unaomsumbua kila mara.

Serikali Kununua Ndege Kubwa ya Masafa Marefu

$
0
0
Serikali Kununua Ndege Kubwa ya Masafa Marefu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa Serikali inatarajia kununua ndege nyingine kubwa ya saba ya masafa marefu na kueleza kuwa haitakodi kwa sababu kukodi ni gharama kubwa ikilinganishwa na kununua.

Prof. Mbarawa amesema Serikali haikurupuki kununua ndege hizo kwa kuwa inao mpango kazi unaobadilishwa kila mara kulingana na wakati.

Ameendelea kwa kueleza kuwa nia ya serikali ni nzuri kwani huwezi kuwa na viwanja vya ndege kama huna shirika lako la ndege, hivyo serikali imenunua ndege sita ambazo tatu zimetua na zinafanya kazi.

“Mwaka huu tunategemea ndege tatu zitawasilisha ambazo ni Boeng 787 ya masafa marefu yenye uwezo wa kuchukua abiria 262, nyingine mbili zenye uwezo wa kuchukua abiria 132 kila moja ni Bombardier CHCS 300 ambazo zitawasilia na kuanza kufanya kazi,” amesema.

“Kikawaida huwezi kuwa na ndege moja ya masafa marefu ikafanya kazi vizuri hivyo kwenye bajeti hii tumeshapanga kununua ndege nyingine boeng 787 ili tuwe na ndege mbili za masafa marefu ambapo moja ikiwa inatoka Dar es Salaam kwenda Guangzhou na moja inatoka Guangzhou kuja Dar es Salaam. Ndio utaratibu unavyokwenda,” amesema.

Katika hatua nyingine ameongeza kuwa Kampuni ya Ndege (ATCL), inao mpango kazi hivyo si kweli kwamba haina kama wabunge walivyodai ambapo kila baada ya muda inabadilishwa kwani si msahafu hivyo itabadilishwa kutokana na mahitaji ya soko.

Kifo cha Masogange Kimenifunza Niachane na Maisha ya Starehe -Pretty Kindy

$
0
0
MSANII wa muziki na filamu Bongo, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ ameibuka na kueleza kwamba kifo cha mrembo, Agness Gerald ‘Masogange’ kilichotokea wiki iliyopita kimempa funzo kubwa katika maisha yake na kimemsababisha azidi kubadili tabia na mwenendo wake zaidi.

Akizungumza na Za Motomoto News, Pretty Kind alisema kifo hicho kimempa funzo kwani hapishani sana umri na Masogange hivyo kimemwaminisha kwamba kufa kunakuja wakati wowote haijalishi una umri mkubwa au mdogo kwa hiyo amejikuta akizidi kubadilika na kuachana na maisha ya starehe yasiyompendeza Mungu.



“Kifo cha Masogange kimeniumiza sana mpaka niliugua ghafla na kushindwa hata kwenda kuuaga mwili wake pia kimenipa funzo kubwa maana maisha aliyokuwa anaishi ndiyo nilikuwa naishi mimi zamani kabla sijaanza kubadilika, nilikuwa naishi maisha yasiyompendeza Mungu, kujiachia kwa sana lakini kwa sasa nimezidi kubadilika kutokana na kifo hiki muda mwingi natumia kumuomba Mungu na kufanya kazi kwa bidii maana kifo kipo wakati wowote,” alisema Pretty Kind.

DKT. Slaa Afunguka Kuhusu Maandamano Yaliyofanywa na Watanzania Sweden

$
0
0
DKT.S laa Afunguka Kuhusu Maandamano Yaliyofanywa na Watanzania Sweden
Wakati polisi wakitoa tahadhari kwa wananchi kuhusu maandamano yaliyoratibiwa kwenye mitandao ya kijamii na kupangwa kufanyika leo, Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dk Wilbrod Slaa amesema ofisi yake ilipokea barua kutoka polisi wa nchi hiyo kuhusu taarifa za Watanzania waliotaka kuandamana jana.

Hata hivyo, hapa nchini polisi imeonya ikisema maandamano hayo ni batili na atakayeshiriki atashughulikiwa.

Akizungumza na gazeti hili kutoka nchini Sweden, Dk Slaa alisema jana kuwa, polisi walisema wameshawapa kibali waandamanaji na watawapa ulinzi unaostahili.

“Ilipofika saa tatu asubuhi, walifika watu kumi, polisi hawakuwa na kazi kubwa waliwapangia wapi wasimame, walikuja na mabango yao. Lakini hakukuwa na muziki kwa sababu huku hawatakiwi kupiga muziki,” alisema.

Alisema baada ya kuwaona waandamanaji hao wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali, walikubaliana na polisi kuwa waingie ndani ili kujua nini wanachohitaji.

“Walikataa kuingia ndani na wakasema hawana sababu ya kujadiliana. Tukawaambia tunawaomba watupe viongozi wawili ili wawe wawakilishi na viongozi hao waseme nini wanachotaka. Lakini pia walikataa,” alisema.

Dk Slaa alisema Sweden ni moja ya nchi zenye vyama vya Watanzania vilivyosajiliwa kuanzia ngazi ya mkoa na kuendelea na viongozi wa vyama hivyo walipiga simu ubalozini wakimsifu Rais Magufuli.

“Nimepokea simu kutoka sehemu mbalimbali, kwamba wanamuunga mkono Rais John Magufuli. Wanataka Rais asilegeze kamba katika vita dhidi ya rushwa na matumizi mabaya ya mali za umma kwa sababu vita hivyo vinatengeneza maadui ndiyo maana mambo kama haya yanatokea,” alisema.

Kuhusu ujumbe aliosema ni wa upotoshaji ulioandikwa kwenye mabango ya waandamanaji hao, Balozi Slaa alisema unamhukumu Rais kwa mambo ambayo mahakama haijathibitisha.

Polisi nchini yaonya

Akizungumza na waendesha bodaboda jana, kaimu kamanda wa polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Sweetbert Njolike alisema jeshi hilo limejipanga kuhakikisha kila mtu anafanya shughuli zake kama kawaida bila uvunjifu wowote wa amani.

“Niwahakikishie Jeshi la Polisi tumejipanga na mkoa wetu utaendelea kubaki salama hakuna maandamano yatakayofanyika, hivyo kila mtu aendelee na shughuli zake kama kawaida,” alisema.

Wakati hayo yakijiri Dar es Salaam, polisi mkoani Mwanza walifanya onyesho la utayari wa kiutendaji na vifaa vyao kwa kuzunguka mitaa kadhaa jijini humo.

Msafara wa magari zaidi ya 15 yaliyokuwa yamewasha taa na kupiga ving’ora ulihusisha askari wenye sare za kikosi cha kutuliza ghasia (FFU), waliobeba silaha na kujihami kwa zana na vifaa vya kudhibiti na kukabiliana na ghasia. Miongoni mwa magari yaliyozungushwa mitaani ni ya doria ya kila siku, gari la maji ya kuwasha na malori, yote yakiwa na askari.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema wamejiandaa kikamilifu kukabiliana na kuwadhibiti wote watakaothubutu kujitokeza mitaani leo kushiriki maandamano yanayohamasishwa kupitia mitandao ya kijamii.

“Kutakuwa na doria ya askari wenye sare na wasio na sare mitaani na maeneo yote ya Mkoa wa Mwanza, watakaothubutu kuandamana watasimulia wengine kitakachowapata,” alisema.

Mkuu wa mkoa huo, John Mongella aliunga mkono kauli hiyo akisema maandamano hayo ni haramu kisheria kwa sababu hadi leo hakuna taarifa iliyotolewa polisi kwa mujibu wa sheria.

Kutoka Dodoma polisi walipita mitaani baadhi wakiwa kwenye magari na wengine wakikimbia.

Kamanda wa polisi mkoani humo, Gilles Muroto alisema watakaothubutu kuandamana watakabiliwa na jeshi hilo ipasavyo.

Mkoani Mtwara, kamanda wa polisi wa mkoa huo, Lucas Mkondya alisema watu wachache wanaohamasisha maandamano wasithubutu kuandamana kwa kuwa watapambana na nguvu ya dola na madhara yatakayotokea jeshi hilo lisilaumiwe.

Alisema katika kufuatilia wanaochochea, kuyahamasisha na kumkashifu Rais, wanafunzi tisa wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine tawi la Mtwara wanashikiliwa.

“Wawili kati yao upelelezi tumekamilisha na kuwafikisha mahakamani, waliobakia tunaendelea kukamilisha upelelezi,” alisema.

Kwa upande wa Morogoro, mkuu wa mkoa huo, Dk Stephen Kebwe alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama kushirikiana kudhibiti maandamano yasiyo halali yaliyopangwa kufanyika leo.

“Kama kuna watu wanataka kuandamana basi wajifungie chumbani waandamane lakini wakijaribu kuingia barabarani polisi hakikisheni mnawashughulikia,” aliagiza Dk Kebwe.

Kamanda wa polisi mkoani humo, Ulrich Matei alisema kwamba wapo askari na vifaa vya kutosha kukabiliana na maandamano hayo.

Marekani waandamana

Wakati huohuo, baadhi ya Watanzania wanaoishi nchini Marekani waliandamana hadi katika ofisi za ubalozi wa Tanzania mjini Washington kuwasilisha madai yao.

Baadhi ya picha zilizotumwa kwenye mitandao ya kijamii ziliwaonyesha waandamanaji hao wakiwa na mabango wakiwa nje ya ubalozi huo huku wengine wakisikika wakizungumza mambo mbalimbali.

Baadaye watu hao waliokuwa wakizungumza Kiswahili walijipanga kando ya barabara wakiimba na kuendelea kuonyesha mabango yao.

Imeandikwa na Fortune Francis, George Njogopa (Dar), Saada Amiri (Mwanza), Florah Temba (Moshi), Hamida Shariff (Morogoro) na Haika Kimaro (Mtwara).

Michepuko Inasaidia Mjini- Mtulia

$
0
0
Michepuko Inasaidia Mjini- Mtulia
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia, akichangia Mjadala wa ujenzi wa barabara na ATCL, uliopo katika bajeti ya wizara ya ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka 2018/19, iliyosomwa juzi na Waziri wake, Profesa Makame Mbarawa, ameiomba wizara hiyo kuzipandisha hadhi baadhi ya barabara na kuziwekea lami badala ya kuweka vumbi au changarawe kwani kufanya hivyo kuwapelekea vumbi wananchi wa Kinondoni ambao nyumba zao zimesongamana.

Aidha, Mtulia amesema Barabara za ‘Michepuko’, (za mkato) zinaruhusiwa kwa maeneo ya mjini ili kuharakisha usafiri kwa watumiaji na kupunguza misongamano.

Video: Irene Poul Atoboa Siri Nzito Kuzimia kwa Rammy "Alipanga Kufanya Kiki Kwenye Msiba wa Masogange Ushahidi wa Hilo Ninao"

$
0
0
Video: Irene Poul Atoboa Siri Nzito Kuzimia kwa Rammy  "Alipanga Kufanya Kiki Kwenye Msiba wa Masogange Ushahidi wa Hilo Ninao"
Muigizaji Irene Poul amezungumza kwa mara ya kwanza na Ayo Tv toka alipo-post ujumbe kuhusu Rammy ambaye alionekana akibebwa na wasanii wenzake wakati alipopoteza nguvu kwenye msiba wa marehemu Agness Masogange.

Irene Paul amesema kwamba Rammy alipanga kufanya kiki katika msiba wa marehemu Masogange ndio mana akafanya vile alivyofanya siku ya msiba na ushahidi wa hilo anao, Irene kaongezea kwa kusema Rammy alikuwa anafanya msiba kama ni wake kitu ambacho haikikuwa sahihi.

Whatsap Wawapiga Marufuku Watu Hawa Kutumia Mtandao Huo

$
0
0
Whatsap Wawapiga Marufuku Watu Hawa Kutumia Mtandao Huo
Mtandao maarufu wa WhatsApp umezuia watu walio chini ya miaka 16 kutumia mtandao huo, kwenye nchi za Umoja wa Ulaya.


Kabla ya hapo watumiaji walitakiwa kuwa na umri wa miaka 13, lakini sasa watumiaji ni lazima wawe na miaka 16 na kuendelea kulingana na utaratibu mpya wa  kulinda taarifa binafsi nchini humo.

Mtandao huo ambao unamilikiwa na mtandao mkubwa wa facebook, utawauliza watumiaji kuthibitisha umri wao watakapojisajili, kuanzia mwezi ujao mwaka huu.

Kutokana na hilo WhatsApp utakuwa mtandao wa kijamii wa tano kuhitaji umri maalum ili kuweza kuutumia, ikiwemo Facebook, Snapchat, Instagram na YouTube.

Wema Sepetu Agoma Kuigiza na Mama Kanumba "Kamwe Siwezi Kuigiza Naye Filamu Moja"

$
0
0
Kamwe Siwezi Kuigiza Filamu Moja na Mama Kanumba- Wema Sepetu
Msanii wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka na kuweka wazi kuwa kamwe hawezi kuigiza filamu moja na Mama mzazi wa Marehemu Steven Kanumba kwani Mwenyewe hakutaka mama yake ajiingize Kwenye sanaa.

Wema ameanika hayo huku akisisitiza kuwa kipindi wakati Kanumba yuko hai alimweleza Wema ambaye alikuwa mpenzi wake kuwa kamwe hataki mama yake ajiingize kwenye Bongo movie.

Wema alifunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers ambao walimuuliza endapo yupo tayari kucheza filamu na Mama Kanumba ambaye hivi sasa amegeukia sanaa hiyo:

"Hapana, siwezi kwa sababu Kanumba alikuwa hataki mama yake aigize na hata mimi alishaniambia, sasa nitavunja makubaliano yetu mimi na Kanumba”.

Lakini pia Kwenye mahojiano hayo Wema alikataa tuhuma alizorushiwa na Mama Kanumba kuwa alipowenda nyumbani kwa Wema hakufunguliwa geti badala yake aliishia kuchomeshwa mahindi:

"Jamani…kwanza siku hiyo mimi sikuwepo kabisa, niliambiwa tu alikuja na kwa nini nifanye hivyo sasa“.

Download Hapa Application Mpya ya Udaku Special Uweze Soma Vimbwanga na Udaku Mtaani Kila Siku

$
0
0
Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Upya Application yetu ya UDAKU SPECIAL Maana ile ya Zamani Tutaifuta.

Kuna Marekebisho Makubwa tumeyafanya ikiwa na tatizo la Notification kutatuliwa

NB: App mpya ina Icon Nyekundu

 Bonyeza Hapa Chini:

==>>Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>>    
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images