Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Siku ya Leo


Breaking News: Mdogo Wa John Heche Auawa Kikatili kwa Kumchomwa Kisu Mgongoni

$
0
0
Polisi Wadaiwa Kumuua Mdogo Wa John Heche kwa Kumchoma Kisu Mgongoni
Mdogo wa Mbunge wa John Heche anayejulikana kwa jina la Suguta, ameuawa kwa kuchomwa kisu.


Kwa mujibu wa John Heche mdogo wake amechomwa kisu na polisi wa kituo cha Sirari waliomkamata baada ya kumkuta bar akinywa pombe, huku akiwa na pingu mkononi.

"Ni kweli kwamba mdogo wangu ameuawa na polisi, na ameuawa akiwa mikononi mwa polisi, jana usiku polisi walimkamata akiwa kwenye bar alikuwa na wenzake wanakunywa pombe, sasa wakamkamata, wameenda naye mpaka kituo cha polisi akiwa mzima wamemfunga pingu, askari mmoja akatoa kisu akamchoma eneo la mgongo kikaenda mpaka kikagusa chembe ya moyo, wamemchoma kisu akiwa wamemfunga pingu tena akiwa kituo cha polisi", amesema John Heche.


Daimond, Nandi Watinga Bungeni Waibua Shangwe kwa Wabunge

$
0
0
Daimond, Nandi Watinga Bungeni Waibua Shangwe kwa Wabunge
Wanamuziki Diamond, Nandy na Mwenyekiti wa CUF anayetambulika na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba ni miongoni mwa wageni waliohudhuria kikao cha Bunge leo,  Aprili 27,  mjini Dodoma.

Wanamuziki hao pamoja na Lipumba walishangiliwa na wabunge baada ya kutambulishwa na mwenyekiti wa Bunge, Musa Azzan Zungu.

Mbali na wasanii hao na Lipumba, wngine waliotambuliwa ni mwanamuziki Mrisho Mpoto na msanii wa filamu Monalisa.

Zungu amesema wote ni wageni wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo. Bajeti ya wizara hiyo mwaka 2018/19 inasomwa leo.

Heshima ya Ndoa Ilikuwa Inanipa Stress - Tundaman

$
0
0
Heshima ya Ndoa Ilikuwa Inanipa Stress - Tundaman
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tunda Man, amesema sababu iliyomfanya awe kimya baada ya kuoa ni kutafuta heshima ya ndoa, ambayo alihisi asingeipata kwa mapema angedhalilika.


Akizungumza na eNewz ya East Africa Television, Tunda Man amesema kwamba kitendo cha kutokuwa na mtoto baada ya kuoa kilikuwa kinamnyima raha, hivyo aliamua aache vingine vyote ili kutafuta heshima ya ndoa, lakini sasa anarudi kwenye game rasmi kwani ameshapata alichokuwa akikitafuta.

“Kitu kikubwa ni kwamba sasa niko huru, mwanzo ilikuwa heshima ya ndoa lazima mtoto, kitu kama hiko kilikuwa kinanitia stress kinoma yani, kwa hiyo nimeoa kama miaka miwili iliyopita, na nilikuwa nimekaa kimya ka muda mrefu kutafuta heshima ya ndoa, mnielewe wananchi, nafikiri heshima imekuja tayari, nina mtoto anaitwa Itsal, kwa hiyo kitu kikubwa sasa hvi nadeal na ngoma zangu”, amesema Tunda Man.

Msanii huyo amesema wiki ijayo anatarajia kuachia kazi mpya tatu kwa pamoja, ikiwemo ambayo ametunga baada ya kushuhudia machungu aliyopitia mke wake wakati wa ujauzito.

Inasikitisha Vilio Vyatanda Kuagwa Kwa Mwili Wa Mtoto Aliyechomwa Kisu Na Dada Yake na Kufichwa Uvunguni

$
0
0
Mtotro Joshua Michael (2) aliyeuawa na dada yake Delta Kalambo (19) kwa kuchomwa kisu kwenye kitovu na mwili wake kufichwa uvunguni unazikwa leo Sengerema mkoani Mwanza.

Simanzi ilitawala watu waliojitokeza kuuaga mwili wa mtoto huyo nyumbani kwao Kigamboni jana huku baadhi wakieleza kuumizwa na unyama uliofanyika kwa mtoto huyo.

Tukio la kuuliwa kwa mtoto huyo lilitokea Jumatatu katika eneo la Tungi Mwembepoa, Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati mama wa mtoto ambaye ni muuguzi wa Hospitali ya Mkuranga, Magreth Kasedi, akiwa kazini.

Msemaji wa familia ambaye ni baba mkubwa wa marehemu, Deus Philipo, jana alisema marehemu huyo atazikwa leo mkoani Mwanza.

Alisema mazishi yatafanyika katika kijiji cha Nyabila endapo wasingekutana na changamoto barabarani.

"Nashindwa kusema tutazika kesho (leo) kwa sababu hatujui huko njiani safari itakuwaje ila tukifika mapema tutazika," alisema.

Kasedi alisema  juzi kuwa Jumatatu aliamka asubuhi kama kawaida na kumuacha mtoto wake na Delta ambaye ni mtoto wa dada yake.

Alisema aliporudi alishangaa kukuta mwanawe wala Delta hawapo nyumbani na ndipo "Nikaingaika kumtafuta mtoto... kila sehemu".

"Kwa majirani... hayupo. Nikahangaika kupiga simu yake haipatikani, lakini wakati nipo kazini nilipata ujumbe mfupi kutoka kwa Delta kuwa nimpigie mtu fulani lakini ujumbe huo sikuuelewa anamaanisha nini."

Alisema kuwa alimpeleka Delta kwenye mafunzo ya ufundi cherehani hivyo alipoona msichana huyo na mtoto hawaonekani nyumbani aliamua kumpigia simu fundi mwalimu wake kujua kama amemuachia mtoto wake.

"Nilimuuliza kama kaachiwa mtoto wangu akaniambia Delta kaja majira ya saa tatu asubuhi bila mtoto," alisema na kueleza zaidi:

"Lakini nilipofika nyumbani kuingia ndani nikakuta ndoo ya bafuni iko sebleni ikiwa na brashi ndani. Nikaenda mezani nikakuta ujumbe mrefu sana.

"Sehemu ya ujumbe huo ulisema mama naomba unisamehe mimi nimekuwa mkaidi, umenionya mara nyingi sana kwa hiyo naomba unisamehe... naenda nyumbani.

"Yaani kaandika mengi nikashindwa kuendelea, nikaamua kutoka nje kumtafuta mtoto kwa majirani kwa kudhani kuwa huenda atakuwa kamuacha kwasababu kaandika anataka kwenda kwao."

Kasedi alisema alihangaika kwa majirani lakini hakuweza kumpata mtoto na ndipo waliposhauriana na majirani waende kutoa taarifa kituo polisi.

Alisema baada ya kutoka polisi walikwenda Stendi ya Steven, eneo la Kisiwani kwa ajili ya kumtafuta kijana anayejulikana kwa jina la Chasii Manyanya ambaye ana mahusiano ya kimapenzi na msichana huyo.

"Huyu kijana alikuwa akipigiwa simu anapokea na kuiacha hewani, ndipo tulipoenda kuhangaika kumtafuta hadi tukafanikiwa kuonyeshwa nyumba anayoishi," alisema mama huyo katika mazungumzo.

"Nilikaa hapo mpaka saa 4:45 usiku ndipo alipokuja huyo kijana, nikamuambia mimi ninachotaka ni mtoto wangu, sina haja na huyo msichana. Akaniambia mama sijaletewa mtoto."

Aliendelea kusimulia kuwa baada ya kuona hivyo alilazimika kutoa taarifa polisi na kijana huyo kushikiliwa huku wakifanya jitihada mbalimbali za kumtafuta Delta ili aeleze mtoto alipo.

Alisema ilipofika asubuhi ya Jumanne aliwahi kituo cha polisi wakasema wanamuangalia kwenye mitandao wajue alipo na ilivyofika saa nne aliiwasha simu ikiwa inaonyesha yupo eneo la Mikadi, Kigamboni.

"Kumbe mimi nahangaika kutafuta mtoto kumbe yuko chini ya uvungu wangu wa kitanda, yaani hakuna damu iliyomwagika," alisema mzazi huyo. "Baada ya kumchoma kisu kwenye kitovu akamlaza kifudifudi na kumfunika vizuri (uvunguni)."

Aidha, alisema mtuhumiwa huyo baada ya kuwasha simu yake majira ya nne aliwasiliana na fundi cherehani ambapo alipomuuliza alipo mtoto alimjibu kuwa amemuacha chumbani.

"Fundi aliwasiliana naye akamuelekeza alipo na kumuambia hataki mtu ajue ndipo fundi akachukua bodaboda kumfuata ili amuelekeze sehemu mtoto alipo," alisema.

"Na mimi nikamtumia ujumbe kwenye simu nikamuambia Delta sijawahi kukufanyia ubaya wowote katika maisha yako, naomba uniambie mtoto wangu alipo.

"Akanijubu kuwa Joshua yupo uvunguni."

Alisema alipopata huo ujumbe alimjulisha baba wa mtoto ausome kwa kuwa yeye alikuwa ameshindwa kuuelewa na ndipo walipofuatilia na kukuta mtoto yuko uvunguni mwa kitanda.

"Polisi walikuja na kuuchukua mwili wa mtoto lakini niliomba nimuangalie nijue... ndipo nikaona kamchoma na kisu kwenye kitovu na utumbo ulikuwa unatoka," alisema Kasedi.

"Hakuna jirani ambaye alisikia kelele za kulia kwa huyo mtoto, nasikia alifungulia mziki sauti kubwa."

Aliendelea kusimulia kuwa Delta alikamatwa baada ya mpenzi wake kuambiwa ampigie simu wakutane kwa ajili ya kumtafutia sehemu ya kuishi, kwasababu ametoroka nyumbani.

"Basi akamjibu yule kijana yuko tayari akamuelekeza alipo na ndipo polisi walipoongozana naye na kumkamata na kwa sasa yuko polisi."

Aidha, alisema hakuweza kuamini kama mtoto huyo ambaye alikuwa akimchukulia kama wake wa kwanza angeweza kufanya tukio hilo.

Alisema hakuwahi kugombana naye na kikubwa alikuwa akimuonya kitendo cha kumuingiza mpenzi wake ndani kwake kwani ni ukosefu wa maadili.

"Huyo mwanaume wake nimemfumania ndani kwangu mara mbili, nikamuonya maana huyu ni kama mwanangu... mtoto wa dada yako hana tofauti na mtoto wako."

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Lukula, alithibitisha kutokea kwa tukio na kueleza kuwa wanamshikilia msichana huyo kwa ajili ya mahojiano ili sheria ichukue mkondo wake.

"Huyu msichana baada ya kufanya huu unyama aliuweka mwili chini ya uvungu wa kitanda na kwenda kujificha na tulipofanikiwa kumkamata tulimuambia atuonyeshe alipo mtoto akasema yuko chini ya uvungu wa kitanda wanapolala wazazi wa mtoto," alisema Kamanda Lukula.

Kuelekea Mechi ya Watani wa Jadi Mzee Ashusha Dua Nzito kwa Yanga

$
0
0
Kuelekea Mechi ya Watani wa Jadi Mzee Ashusha Dua Nzito kwa Yanga
Katibu wa Baraza la Wazee wa klabu ya Yanga, Ibrahimu Akilimali amesema kuwa kuelekea mchezo wao dhidi ya watani zao Simba SC kunahaja ya kutupilia mbali tofauti zao na kumuomba Mungu katika kuhakikisha wanachomoza na ushindi siku hiyo ya Aprili 29.

Wakati zimesalia siku mbili pekee kabla ya kukutana kwa watani hao wajadi Simba SC dhidi ya Yanga SC kwenye dimba la Taifa siku ya Jumapili hii, Mzee Akilimali ametumia muda wake kuiyombea timu yake kuhakikisha inachomoza na ushindi siku hiyo.

Tunalengo la kuwashinda wapinzani wetu, siyo rahisi lakini lazima ujiandae kwa hayo wazee tunatoa baraka zote kwa vijana kwakuwa hatuna kinyongo.

Isipokuwa mimi naomba tu Yaarabbi Yaarabbi nakuomba turudishie hali yetu ileile ya umoja na mshikamano wetu kwa kila hali, tushikamane kwaajili ya kuwasapato vijana wetu na tumuombe Mwenyezi Mungu kila mmoja kwa dua yake na imani yake ili tupate ushindi siku hiyo ya Jumapili.

Nawaomba wana Yanga wenzangu tuwe wamoja tuwache tofauti zetu twende katika mchezo maana ni mgumu sana.

Kocha mpya ameingia na viongozi wetu wamefanya mambo haraka haraka sasa hivi yupo kazini, Msimbazi ubingwa bado isipokuwa tu mtu hawezi kukata tamaa ila hali bado. Amenitambuka mechi chache tu na yeye atarajie kufanya vibaya kwenye mechi hizo alizo nazo.

Wazee hatuna ahadi yoyote kwa vijana kwakuwa hayo yanatamkwa na viongozi.

Simba ambayo inaongoza kwenye msimamo wa ligi kwakuwa na jumla ya pointi 59 nyuma ya hasimu wake Yanga wenye alama 48 zinatarajia kukutana siku ya Jumapili ya Aprili 29 kwenye dimba la Taifa Jijini Dar es salaam.

Afande Sele Akubari Yaishe kwa Mzozo wa Jina la Simba ....Amtumia Salamu za Heri Daimond

$
0
0
Afande Sele Akubari Yaishe kwa Mzozo wa Jina la Simba ....Amtumia Salamu za Heri Daimond
Baada ya mzozo mkubwa wa kipindi cha nyuma wa kugombea uhalali wa umiliki wa jina la Simba kati ya mkongwe wa muziki wa Hip Hop, Afande Sele na msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz. Hatimaye Afande Sele ameonekana kukubali yaishe kwani amemtakia kila la kheri Diamond kwenye uwakilishi wake kwenye Kombe la Dunia.

Afande Sele amesema kuwa maendeleo hayana u-team hivyo anaamini kuwa kitendo cha Diamond kushiriki kwenye wimbo rasmi wa Kombe la Dunia ni jambo la kupongezwa na kila mtu.

“Maendeleo hayana timu, kutoka Tandale hadi Rusia, Kinesi Cup hadi World Cup. Hongera sana mdogo wangu baba yake Tipha…Lion Never loose..💪…All the best Nasib/Tanzania.“ameandika Afande Sele kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Soma zaidi – Afande Sele kumaliza kesi ya neno ‘Simba’ kati ya Diamond na Mr Blue kwa style hii

Salamu hizo za Afande Sele zimekuja ikiwa ni siku tano zimepita tangu wimbo rasmi wa Kombe la dunia ‘Colours’ uliowakutanisha Jason Derulo na Diamond Platnumz.

Tunda: Mimi Sipigi Picha za Utupu Huu ni Mtindo Wangu wa Maisha

$
0
0
Tunda: Mimi Sipigi Picha za Utupu Huu ni Mtindo Wangu wa Maisha
Video vixen Bongo, Tunda amedai yeye huwa hapigi picha za utupu bali watu wanavyomuona ndio mtindo wake wa maisha.

Tunda amesema picha za utupu ni pale mtu anapoenda studio na kupiga picha lakini zile anazopiga akiwa nyumbani kwake ni zinapaswa kueleweka ni picha za kawaida.

“Unajua kuna picha za utupu kwamba ile mtu unaenda studio unaamua kuwa wazi na kupiga picha, na kuna jinsi mtu anavyovaa kama ni nguo fupi yaani kawaida ya yeye kuvaa yapo si utupu kuna tofauti, mimi sipigi picha za utupu, no!,” amesema.

Tunda anametokea kwenye video za wasanii kama Young Dee, Chege na Temba na wengineo. Kwa sasa mrembo huyo katika mahusiano na mtangazaji wa Clouds TV, Casto Dickson.

Download Hapa Application Mpya ya Udaku Special Uweze Soma Vimbwanga na Udaku Mtaani Kila Siku

$
0
0
Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Upya Application yetu ya UDAKU SPECIAL Maana ile ya Zamani Tutaifuta.

Kuna Marekebisho Makubwa tumeyafanya ikiwa na tatizo la Notification kutatuliwa

NB: App mpya ina Icon Nyekundu

 Bonyeza Hapa Chini Kuinstall Upya:


==>>Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>>   

Sijawahi Kutamani Kufanya Kolabo na Alikiba- Harmonize

$
0
0
Sijawahi Kutamani Kufanya Kolabo na Alikiba- Harmonize
Msanii kutoka label ya WCB, Harmonize amefunguka iwapo yupo tayari kufanya kolabo na Alikiba.

Muimbaji huyo amesema hajawahi kutamani kufanya kolabo na msanii huyo na si Alikiba pekee bali na wasanii wengi.

“Lengo la Watanzania wote ni kuona ni kiasi gani tunaweza ku-push muziki wetu na kuupeleka mbali. Sijawahi kutamani kufanya kolabo na Alikiba, sijawahi kutamani kufanya kolabo na msanii yeyote lakini ikitokea kipindi tunafanya,” amesema.

“Vitu vingine lazima viwepo ili game izidi kupamba moto, so mimi sidhani kama kuna kitu cha ajabu sana,” Harmonize ameiambia Radio Five.

Kwa sasa Harmonize anafanya vizuri na kolabo aliyofanya na Diamond inayokwenda kwa jina la Kwa Ngwaru, huu ni wimbo wa pili kufanya pamoja baada ya ule wa Bado uliotoka mwaka 2016.

Hivi Ndivyo Wanawake Waliozaa na Alikiba Walivyomwaga Chozi Siku ya Harusi

$
0
0
Hivi Ndivyo Wanawake Waliozaa na Alikiba Walivyomwaga Chozi Siku ya Harusi
NDOA ya mwana-muziki wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’ na mwanadada kutoka Mombasa nchini Kenya, Amina Khali nayo huwezi kuiacha nyuma miongoni mwa matukio yaliyotrend.

Ndoa hii ambayo ilizimwa na vifo vya mastaa, Agness Masogange, Jebby, Mama Cheni na Dalila ilitrendi kwenye mitandao ya kijamii kwa mambo mengi, kama ifuatavyo;

Vilio

Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Alikiba, aliyetupenyezea habari alieleza kwamba ndoa hii iliacha vilio vingi kwa wanawake ambao walitembea na Kiba kabla. Alisema; “Kama unavyojua Kiba alishazaa watoto wanne, wale watoto kila mmoja ana mama yake. Sasa mama zao wanalia maana nao walikuwa wana matarajio ya kuolewa.”

Ukiachana na wanawake hao waliozaa na mkali huyo wa Wimbo wa Seduce Me, kundi lingine lililoachwa na majonzi ni mastaa wanaodaiwa kutoka nao kimapenzi. Mrembo Jokate Mwegelo naye alikuwa mmoja kati ya mastaa waliopitia kipindi kigumu kwani alikutana na mashuti ya kutosha kutoka kwa mashabiki ambao walikuwa wakichukia uhusiano wake pindi yupo na Kiba. Ndoa kurushwa ‘live’

Mbali na vilio suala lingine ilikuwa ni ndoa yenyewe kuoneshwa ‘live’, na kituo kimoja cha televisheni ambapo watu wengi hawakukubali kuikosa.

Gumzo kubwa lilikuwa mitaani hasa katika ‘vibanda umiza’ ambapo walikuwa wakiionesha tukio live kwa kulipisha kiingilio.

Neno (Naumia) Wakati wa Tendo la Ndoa Kutoka Kwa Mwanamke Lanitatiza

$
0
0

Kwakifupi ni hivi:-
Kila tufanyapo tendo la ndoa, mwenzangu hutoa kilio pasipo machozi, huku ameikunja sura yake na wakatihuo hutamka neno Naumia... Hii kitu imekua inanipa wakati mgumu na kunifanya nimuonee huruma mpenzi wangu na kumuuliza, nitoke? chakushangazi yeye hukataa na Kuniambia usitoe na huku anuonyesha kufurahia tendo.

Maswali:-
Je, hulia kwa kupata maumivu?
Je, hulia kwa kuhisi raha?
Je, nawengine wanaliaga kama wangu?
Je, hutoa kilio kwa mbwembwe tu?

Naombeni ushauri wenu wakuu

BREAKING NEWS: Mdogo wa John Heche auawa kwa kuchomwa na Kisu

$
0
0

Mdogo wa Mbunge wa John Heche anayejulikana kwa jina la Suguta, ameuawa kwa kuchomwa kisu.

Kwa mujibu wa John Heche mdogo wake amechomwa kisu na polisi wa kituo cha Sirari waliomkamata baada ya kumkuta bar akinywa pombe, huku akiwa na pingu mkononi.

"Ni kweli kwamba mdogo wangu ameuawa na polisi, na ameuawa akiwa mikononi mwa polisi, jana usiku polisi walimkamata akiwa kwenye bar alikuwa na wenzake wanakunywa pombe, sasa wakamkamata, wameenda naye mpaka kituo cha polisi akiwa mzima wamemfunga pingu, askari mmoja akatoa kisu akamchoma eneo la mgongo kikaenda mpaka kikagusa chembe ya moyo, wamemchoma kisu akiwa wamemfunga pingu tena akiwa kituo cha polisi", amesema John Heche.

Breaking News: Lema Akamatwa na Polisi Nje ya Mahakama

$
0
0
Breaking News: Lema Akamatwa na Polisi Nje ya Mahakama
Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Godbless Lema leo April 27, 2018 amekamatwa na polisi na kufunguliwa kesi mpya kuhusu uchochezi kwa ndoto aliyowahi kuota kuhusu Rais Dkt. John Pombe Magufuli miaka miwili iliyopita.


Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amethibitisha hilo na kusema kuwa Lema leo alihudhuria Mahakamani kwa ajili ya kesi iliyokuwa ikimkabili kuhusiana na ndoto alizoota miaka miwili iliyopita.

"Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limemkamata Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kwa kile kinachodaiwa "uchochezi". Dhidi ya Mh Rais kuhusiana na ndoto aliyowahi kuota. Lema alihudhuria Mahakamani siku ya leo kwa ajili ya kesi iliyokua ikimkabili kuhusiana na ndoto alizoota miaka 2 iliyopita. Baada ya Mahakama kufuta kesi hiyo leo na kuachiwa...Polisi walimkamata tena na kumfungulia kesi upya kwa mashtaka yale yale" alisema John Mrema

Kesi hii ni mwendelezo wa kesi iliyokua ikimkabili Mh Godbless Lema na ambayo ilimsotesha Mahabusu (Magereza) kwa zaidi ya miezi 4 mwaka juzi kabla ya kuachiwa kwa dhamana mapema mwaka jana.

Mrembo Pretty Kindy Aliyefungiwa kwa Kuvaa Nguo Nusu Utupu Anyooka..Afunguka Haya

$
0
0

Mrembo Pretty Kindy Aliyefungiwa kwa Kuvaa Nguo Nusu Utupu Anyooka..Afunguka Haya:
_
Regrann from #official_prettykind - Nimependeza sana wallah kumbe nguo ndevu zinanipendeza hivi 😅😅 with my brothers Dodoma Ashukuriwe Kiongozi nimekuwa kabinti kenye maadili muonekano mzuri 👏

J Cole : Album yangu ya KOD inanipa Kumbukumbu ya Tanzania, Zanzibar

$
0
0
Tarehe 20/ April 2018 Msanii wa Hip Hop na producer Jermaine Lamar Cole almaarufu J Cole anatokea kwny viunga vya Fayettevile, North Carolina, Marekani. Alitoa Album yake ya tano iitwao KOD yenye kirefu cha Kids On Drugs, Kill Our Demons au King Overdose.

Ndani ya Album hii KOD amezugumzia kuhusu tatizo la madawa ya kulevya na jinsi ya kuhandle maumivu ya maisha bila kutumia njia hatarishi km za Madawa au kujiigiza starehe zisizostahili km Xanny.

Kupitia account yake ya Twitter J Cole wakati anajibu ni swali la shabiki mmoja kuhusu ipi ni kumbukumbu nzuri kwako wakati una record Album ameitaja Tanzania, Zanzibar na pia amethibitisha kuwa aliipata jina la Album KOD kipindi yupo Tanzania, Zanzibar.

Pia amezitaja nyimbo 4 kati ya 12 alizifanya akiwa Tanzania, Zanzibar nyimbo alizo ziandika akiwa Tanzania ni The Cut off, Kevin's Heart, FRIENDS na Window Pain. Nyimbo zingine zinazopatikana kwenye Album hii ni Photograph, 1985, Moti8, BRACKETS, ATM, Once an Addict na Intro

Kwa wale walioisikiliza hii Album mtakubaliana nami ndie Album bora kutoka kwa J. Cole ukisikiliza nyimbo zote pamoja na ujumbe uliopo kwny izo nyimbo haina ubishi hii Album bora ikifatiwa na 2014 Forest Hill Drive halafu Born Sinner, 4 Your Eyez Only then Cole World :The Sideline Story.


Mwanamuziki Amwaga Chozi Hadharani Baada ya Kumbusu Mwanafunzi

$
0
0
Mwanamuziki Amwaga Chozi Hadharani Baada ya Kumbusu Mwanafunzi
Kutoka nchini Japan, mwanamziki wa bendi moja maarufu nchini humo iitwayo Tokio ameomba msamaha kupitia vyombo vya habari kwa kumbusu msichana ambaye anaelezwa kuwa wa shule ya sekondari.

Mwanamziki huyo Tatsuya Yamaguchi ambaye ana umri wa miaka 46 anadaiwa kumpeleka binti huyo nyumbani kwake na kumbusu na baada ya wiki mbili alipigiwa simu na polisi kuitwa kituo cha polisi kujibu tuhuma hizo.

Rais Kim amevuka mstari wa vita kuingia Korea Kusini

Akiomba msamaha huo huku akitokwa machozi, anaeleza kuwa siku ya tukio alikuwa amelewa na hakujua kilichoendelea hadi alipopigiwa simu na polisi na kuelezwa madai ya binti huyo.

RPC Athibitisha Mdogo Wake Heche Kuuawa na Polisi

$
0
0
RPC Athibitisha Mdogo Wake Heche Kuuawa na Polisi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya Henry Mwaibambe amethibitisha kuuawa kwa Bwana Chacha Heche Suguta ambaye ni mdogo wa Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche, kwa kuchomwa kisu na Polisi.


Akizungumza na www.eatv.tv Kamanda Mwaibambe amesema marehemu alikuwa na mgogoro na mmoja ya askari waliokuwa wamemkamata, na kufikia hatua ya kutaka kushikana (kupigana) ndipo askari aliposhindwa kujizuia na kumchoma kisu.

“Tukio ni la kweli limetokea na huyo askari tunamshikilia, huyo kijana alikamatwa usiku sasa wakati wapo kwenye gari wakielekea kituo cha polisi, ukatokea mzozo kati ya huyu askari na huyu marehemu, mzozo kama wanataka kupigana, mwenzake akaingilia kuamua, lakini ni kweli askari amemjeruhi huyu mgongoni, mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi leo saa 6 mbele ya ndugu zake, kweli umekutwa na jeraha la hicho kisu mgongoni na mtuhumiwa alikuwa hajavalishwa pingu, ila hatujui nini waliambiana mpaka kufikia hivyo”, amesema Kamanda Mwaibambe.

Sambamba na hilo Kamanda Mwaibambe amesema hali ya kituoni hapo kwa sasa imetulia baada ya wananchi kufurika kulalamikia mauaji hayo, na kwamba amezungumza na ndugu wa familia kuwaeleza jinsi tukio lilivyokuwa.

Pia Kamanda Mwaibambe amewataka watu kutochukulia tukio hilo kisiasa, isipokuwa ni kama tukio lingine la mauaji, ingawa sio jambo zuri kwa mtu yeyote.

JPM Amtwisha Mzigo Mkuu wa Mkoa Dodoma

$
0
0
JPM amtwisha mzigo mkuu wa Mkoa Dodoma
Rais John Magufuli amemtaka Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isaac Kamwelwe na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge kufuatilia ubadhirifu wa fedha za mradi wa maji katika Mkoa wa Dodoma na kuhakikisha wahusika wanakamatwa au maji yanatoka.


Rais Magufuli ameyasema hayo leo Aprili 27, wilayani Kondoa wakati wa hafla ya uzinduzi wa barabara ya Dodoma – Babati yenye urefu wa kilomita 251 ambayo ni sehemu ya barabara kuu inayotoka Capetown, Afrika Kusini mpaka Cairo, Misri.
Ameagiza vyombo vya dola kuwatafuta wahusika wa ubadhirifu wa fedha hizo ambazo amesema ni zaidi ya Sh2 bilioni.

Amesema ni lazima wahusika wachukuliwe hatua kwa sababu hizo ni fedha za wananchi, na ni vyema ziwaletee maendeleo.

“Haiwezekani tukawa tunaimba maji kila siku halafu maji hayatoki. Vyombo vya dola vihakikishe wahusika wote wanakamatwa au maji yanatoka. Tukibembelezana hivi hatutafika, hata hii barabara tusingebana, isingekamilika,” amesema Rais Magufuli.

Awali kabla ya Rais Magufuli kuzungumza, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge alisema kuna ubadhirifu wa Sh1.5 bilioni kwenye mradi wa maji katika wilaya za Kondoa na Chemba ambao mpaka sasa  unasuasa.

Mkuu huyo wa mkoa alisema mradi huo ulitengewa  Sh2.8 bilioni kwa ajili ya wilaya hizo, lakini kulitokea ubadhirifu wa Sh1.5 bilioni.


Amebainisha kwamba vyombo vya dola vinaendelea na uchunguzi wa ubadhirifu huo.

Azamu Yafuata Nyayo za Zimba, Yanga

$
0
0
Azamu Yafuata Nyayo za Zimba, Yanga
Klabu ya soka ya Azam FC imetua mkoani Morogoro kwaajili ya kuweka kambi kuelekea mchezo wake dhidi ya Mtibwa Sugar, utakaopigwa kesho huku pia klabu za SImba na Yanga zikiwa zimeweka kambi mkoani humo.


Azam FC imeondoka jijini Dar es salaam ikiwa tayari imeshafanya maandalizi yote ya mchezo huo na kitakachofanyika katika kambi ya muda mfupi Morogoro ni mazoezi mepesi tu kabla ya mechi.

Jumanne hii Azam FC ilicheza mchezo wa kirafiki na Kombaini ya Jeshi na kushinda mabao 2-0 yaliyofungwa na mshambuliaji Shaaban Idd na winga Enock Atta. Mchezo huo ulikuwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya kesho.

Timu hizo zilipokutana kwenye raundi ya kwanza zilitoka sare ya bao 1-1, Azam FC ikitangulia kufunga kupitia kwa winga Enock Atta kabla ya Kelvin Sabato kusawazisha dakika za mwisho kwa mpira wa moja kwa moja wa adhabu ndogo.

Hadi sasa kwenye msimamo wa ligi, Azam FC inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 46 huku wapinzani wao Mtibwa Sugar ikiwa nafasi ya sita kwa pointi 33. Simba na Yanga nazo zipo Morogoro kumalizia maandalizi ya mchezo wao wa Jumapili.

Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images