Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Ciara Afungua Mashtaka Juu ya Mzazi Mwenzake Future

$
0
0
Ciara Afungua Mashtaka Juu ya Mzazi Mwenzake Future
Staa wa muziki kutokea Marekani Ciara amemfungulia mashtaka mzazi mwenzake Future baada ya kusemekana kuwa hatimizi ahadi zake za kumuona mtoto wao Future Zahir Willburn mwenye umri wa miaka mitatu  na kila ifikapo siku za kumuona basi huvunja siku hiyo kwa majukumu mengine binafsi.

Kupitia chombo cha habari cha TMZ kinadai kuwa Ciara amefungua mashtaka na kudai kuwa asilimia 37 ya muda wa Future haonekani kuwa karibu au kuja kumuona mwanae Furture Zahir na hata mtoto akijaribu kumtembelea baba yake anaishia kushinda nyumbani na bibi yake bila kupata muda na baba yake.



Rappa Future pamoja na Ciara walifanikiwa kuwa katika mahusiano ya kiampenzi kwa muda mrefu na kubahatika kupata mtoto mmoja wa kiume  Future Zahir na kuachana August 2014.

TCAA: Kutua kwa Ndege ya Emirates Kumeipa Kiki Anga ya Tanzania

$
0
0
TCAA: Kutua kwa Ndege ya Emirates Kumeipa Kiki Anga ya Tanzania
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imesema kutua kwa ndege ya Emirates Airbus A380-800 kumewaongezea kujiamini katika biashara ya usafiri wa anga duniani.

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema leo Aprili 27, jijini Dar es salaam kuwa Emirates walichagua uwanja wa JNIA Dar es Salaam kutokana na kuzingatiwa kwa vigezo vya kimataifa vya uwanja huo.

 Dege hilo linalotajwa kuwa moja ya ndege kubwa duniani, lilitua kwa dharura JNIA Aprili 24 kutokana na hali mbaya ya hewa Mauritius, ilikokuwa ikielekea. Hata hivyo ndege hiyo iliondoka Aprili 25 kwenda Mauritius.

Simba Yatangaza Vita na Wanahabari Watakaotumia Neno 'Wahasimu'

$
0
0
Simba Yatangaza Vita na Wanahabari Watakaotumia Neno 'Wahasimu'
Uongozi wa klabu ya Simba kupitia Ofisa Habari wake, Haji Manara, umetangaza vita na Wanahabari watakaotumia neno MAHASIMU badala ya WATANi pindi wanapotangaza na kuziandika klabu hizo.

Manara ameeleza kuwa Simba na Yanga si mahasimu bali ni watani wa jadi, tofauti na baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikiripoti tofauti.

Manara ameyasema hayo leo alipotisha kikao na Waandishi wa Habari kwenye Makao Makuu ya Simba, yaliyopo Kariakoo.

Ofisa huyo wa Habari, amesema neno hilo lina maana mbaya ambayo ni VITA hivyo halipaswi kutumika huku akieleza kuwa wao si Palestina na Israel.

Kufuatia baadhi ya vyombo vya habari kuripoti wakizitaja timu hizo za Kariakoo kuwa ni Mahasimu badala ya watani wa jadi, Manara ametangaza kuwa klabu itaanzisha vita na Mwandishi au Mtangazaji yeyote atakayeripoti kwa kuandika ama kutamka jina la MAHASIMU badala ya watani wa jadi.

Gigy Money Ajifungua Mtoto wa Kike

$
0
0
Gigy Money Ajifungua  Mtoto wa Kike
Mwanadada wa bongo fleva na video Qeen Gigy money amejifungua mtoto wa kike usiku wa kuamkia leo ambaye amezaa na mpenzi wake wa muda mrefu Moj ambaye ni mtangazaji wa choise fm.

Moj na Gigy Money kabla ya kupata mtoto huyo walikuwa wakitaniana kwa kuitana mama Candy na Mama Candy amefunguka na kudai kuwa mtoto wao hawatampa jina hilo bali wataangalia jina lingine la kumwita.

Siri ya Alikiba, Abdukiba na Zabibu Kiba Ndoa zao Kuongozana Hii Hapa

$
0
0
Siri ya Alikiba, Abdukiba na Zabibu Kiba Ndoa zao Kuongozana Hii Hapa
Wengi wamekuwa wakijiuliza sababu ya watoto wa Mzee Salehe Kiba, Ali Salehe Kiba, Abdul Kiba na Zabibu Kiba kuongozana kwenye kuoa na kuolewa lakini hatimaye siri imevuja kuwa, mama yao ndiye aliyechagiza hilo ili kuwapa radhi zake.

Akizungumza na Ijumaa juzikati, mmoja wa wanafamilia ya Kiba aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa, Ali Kiba na Abdu Kiba hawakuwa na mpango wa kuoa katika siku za hivi karibuni lakini mkwara wa mama yao ndiyo uliwasukuma kufanya hivyo.

“Kuna wakati mama yao alikuwa hana furaha kabisa na akiulizwa anasema, anaumia kuona wanaye umri unakwenda lakini hawaoi, wanaishia kuonekana na wasichana na kuzaa nao tu, alikuwa akiumia sana.

“Alitamani sana kuona wanaye wanaingia kwenye ndoa haraka na alikuwa akiwaeleza kila wakati kuhusu hilo. Sasa ili kumfurahisha mama yao ndipo wakaamua kuwa waoe tena kwa kufuatana, ndiyo maana unaona ndoa zao zimeongozana. “Na Zabibu naye siku si nyingi anaolewa, ilikuwa naye aolewe baada ya Abdu kisha wafanye sherehe ya harusi ya pamoja lakini kuna vitu vimekwamisha hilo,” alidai mtoa habari huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.




Katika kile kilichoonekana kuwa, sababu ya ndoa hizo kufuatana ni mkwara wa mzazi, Ijumaa liliwahi kufanya mahojiano na mama wa Kiba ambaye alifungukia hilo la kutamani kuona wanaye hao wanaingia kwenye maisha ya ndoa.

Alisema: “Nitahakikisha mwaka huu (mwaka jana mwishoni) hauishi wanangu watakuwa wameoa, hilo ndilo litanifanya niwe na amani moyoni mwangu.” Gazeti hili lilifanya jitihada za kuwapata Ali na Abdu kwa nyakati tofauti ili kujua kama kuoa kwao kuna msukumo mkubwa kutoka kwa mama yao lakini hawakuweza kupatikana mara moja.

Hata hivyo mwandishi wetu alimtafuta Zabibu kuzungumzia ndoa yake ambapo alipopatikana alisema kuwa, kuhusu yeye kuolewa hilo suala likiwepo Watanzania watajua tu ila kwa sasa ni Ali na Abdu.

TUJIKUMBUSHE

Ali Kiba alioa Aprili 19, mwaka huu nyumbani kwa bibi harusi, Mombasa nchini Kenya huku Abdul Kiba naye akiolea Bongo, Aprili 22. Zabibu Kiba yeye yuko kwenye uchumba na mchezaji wa Timu ya Baroka FC ya Sauzi Afrika, Abdi Banda na inadaiwa siku si nyingi nao wataoana.

Okoa Ndoa yako Sasa...Umepungukiwa na Nguvu za Kiume na Unashindwa Kupanda Mlima Vizuri

$
0
0
OKOA NDOA YAKO SASA : JE UMEPUNGUKIWA NA NGUVU ZA KIUME AU UUME WAKO MDOGO AU MPENZI WAKO HAKUTIMIZII UTAKACHO:


Acha kujiona mpweke pale ukutanapo na mpenzi au mke wako kwa sababu ya kutokuwa na nguvu za kiume au Uume wako mdogo

Dawa YA MAPRO POWERA ndio dawa sahihi na tiba tosha kwa sasa Kutibu tatizo na kuponesha kabisa tatizo LA KUWAI KUFIKA KILELENI KABLA MWENZI WAKO BADO AJAKOJOA

KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOA NA MWILI KUCHOKA

UUME KUSINYAA NA KUWA LEGELEGE

KUUMWA NA TUMBO WAKATI UNAPOMALIZA KUFANYA TENDO

Dawa hii utumiwa ata na wazee wenye umri mkubwa na haina madhara yoyote

MAKAKANUA HII NI dawa ya maumbili madogo urefusha na kunenepesha saizi upendayo saiz 5-6-7-8 na unene sm 3-4-5 kwa mini huabiki kwa kuwa na UUME mdogo wai sasa upate tiba sahihi kabisa na ni tofauti na ulizowai kutumia :

Tunarudisha mke au mpenzi ndani ya masaa matatu tu zipo dawa za presha kisukali vidonda vya tumbo korodani iliyovimba dawa za uzazi tunapunguza matiti makubwa kitambi na mwili mkubwa dawa zipo FIKA OFISINI KWANGU MBAGALA ZAKHEMU KWA WATEJA AMBAO AMTAKUWA NA NAFASI YA KUJA OFISINI AU MLIO MKOANI MTALETEWA p

Piga simu 0743362017 au 0789234653

DR AGU

Afungwa Miaka 32 Jela Kwa Kumpinga Nkuruzinza

$
0
0
Mahakama nchini Burundi imemhukumu mwanaharakati wa haki za binadamu, Germain Rukuki, kifungo cha miaka 32 jela baada ya kukutwa na hatia ya kushiriki katika maandamano dhidi ya Rais Pierre Nkurunzinza, wakati akiwania muhula wa tatu.


Rukuki anatuhumiwa kushiriki katika vuguvugu lililojaribu mapinduzi ya kijeshi na utekelezwaji wa mauaji ya askari polisi Mei 13, 2015, tarehe ambayo kundi la wanajeshi lilijaribu kumpindua Rais Nkurunzinza wakati akiwa nchini Tanzania.

Mwendesha mashtaka alimuongezea mashtaka mapya katika kesi hiyo ikiwemo mauaji, uharibifu wa mali ya umma, jaribio la kupindua utawala uliochaguliwa kidemokrasia makosa ambayo upande wa utetezi haukujulishwa

Baada ya Utata wa Waamuzi Simba Watoa Neno

$
0
0
Klabu ya soka ya Simba kupitia kwa msemaji wake Haji Manara, imewataka waamuzi wa mchezo wao dhidi ya Yanga siku ya jumapili kufanya maamuzi kwa kuzingatia sheria 17 zinazoongoza mchezo wa soka.


Akiongea leo kuelekea mchezo huo utakaopigwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, Manara amesema pamoja na kuwepo kwa utata kwenye suala la waamuzi wa mchezo huo lakini wao kama klabu wanaomba tu wazingatie sheria 17.

''Kwenye suala la waamuzi naomba tuyaache mengine ila niweke wazi tu kuwa, wachezeshe kwa kuzingatia sheria 17 za soka, nasisitiza wachezeshe kwa kuzingatia sheria 17 za soka'', amesema Manara kwa msisitizo.

Kumekuwa na utata baada ya shirikisho la soka nchini TFF kupitia kwa kamati ya waamuzi kumtangaza mwamuzi Emmanuel Mwandembwa kuchezesha mchezo huo huku ikimtambulisha kuwa anatokea Mwanza wakati anatokea Arusha.

Hata hivyo mwenyekiti wa kamati ya waamuzi Salum Chama, amefafanua kuwa wamemtambua Emmanuel Mwandembwa kama mwamuzi anayetokea Mwanza kwasababu yupo kwenye chuo cha michezo Malya mkoani huko kwa masomo yanayochukua miaka mitatu.

Naomba Mkaniombee Labda Nibadilike- Magufuli

$
0
0
Naomba Mkaniombee Labda Nibadilike- Magufuli
Rais John  Magufuli amewaonya viongozi wenye migogoro hususani wilayani Kondoa, kuacha kutofautiana na wakae pamoja ili kuyamaliza matatizo yao na kusisitiza pande zote zenye migogoro kuanza upya na kwamba siyo kila tatizo lazima lifikishwe kwake.

Rais Magufuli amefunguka hayo leo Ijumaa  mjini Kondoa wakati wa ufunguzi wa barabara ya Dodoma hadi Babati yenye urefu wa kilomita 251.

Amesema, Tanzania ni moja na watu wote wanahitaji maendeleo hivyo migogoro ya baadhi ya vingozi inachelewesha maendeleo ya wananchi.

"Viongozi wa Kondoa muache kugomba leo nimeona niwape meseji live muache kugombana niliwateua mimi nitawatoa mimi. Kuna wakati unakuta Hanang na Kondoa wanagombania mipaka utafikiria ni nchi jirani hilo nalo linakaa muda mrefu hata viongozi wanashindwa kulitatua hivyo ifike mahali tumalize migogoro hii" Rais Magufuli.

Ameongeza "Siyo kila mgogoro, lazima uletwe kwa rais. Nitaimaliza mingapi?  Viongozi waliopo washughulikie migogoro ya saizi yao. Tanzania ni kubwa na inachangamoto nyingi, hivyo ninyi ni viongozi mnatakiwa muelewane kwa manufaa ya wananchi wenu.  Nafahamu viongozi hampendi kuzungumzwa hadharani. Mimi nazungumzaga tu ndiyo tatizo langu. Naomba mkaniombee labda nibadilike," amesema rais Magufuli.

Rais Magufuli pia amewasihi watanzania wasikubali kugawanywa kwa misingi ya Itikadi, Ukabila au Dini na vyama kwani amani na umoja wa nchi ndiyo huchangia maendeleo yanayopatikana kila siku.

TFF Yamtanga Makonda Kuwa Mgeni Rasmi Mechi ya Simba, Yanga

$
0
0
Makonda Kuwangoza Mashabiki wa Simba, Yanga Jumapili Taifa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtangaza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara ambao utawakutanisha Simba na Yanga Aprili 29, 2018 katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam.


Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na Afisa habari wa TFF, Cliford Mario Ndimbo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema Mhe. Makonda atawaongoza maelfu ya mashabiki wa mpira wa miguu watakaojitokeza kweye uwanja huo kushuhudia mchezo huo namba 178 utakaoanza saa 10 jioni.

Aidha, Cliford amesema mpaka kufikia sasa tayari tiketi za mchezo huo zinaendelea kuuzwa ambapo VIP A ni shilingi 30,000, VIP B na C 20,000 na mzunguko (Jukwaa la rangi ya Chungwa,Kijani na Bluu) 7,000.

Simba wanaingia uwanjani wakiwa wanaongoza ligi baada ya kujikusanyia pointi 59 ikicheza michezo 25 wakati Yanga wana pointi 48 wakiwa nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 23.

Kamati ya Bunge Yaiponda Serikali Kufungia Nyimbo za Wasanii

$
0
0
Kamati ya Bunge Yaiponda Serikali Kufungia Nyimbo za Wasanii
Kamati ya Bunge ya Huduma za Maendeleo ya Jamii imeuponda utaratibu unaotumika na Serikali wa kufungia nyimbo za wasanii, zisizoendana na maadili ya kitanzania kwa maelezo kuwa unaleta changamoto kwa wasanii.

Akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kuhusu bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mwaka 2018/19 kwa niaba ya mwenyekiti wake Peter Serukamba, mbunge wa Ludewa (CCM), Deogratius Ngalawa amesema vyombo vinavyohusika na usimamizi vinapaswa kuhakikisha vinatimiza majukumu yake kwa kukagua nyimbo zote za wasanii kabla hazijatoka.

“Lengo ni kuhakikisha hakuna wimbo unaotoka kama haujazingatia maadili. Kuangalia nyimbo ambazo ni za kimataifa na kuzipa kibali maalum kwa maana ya muda na mahali pa kuutumia wimbo huo kabla haujaanza kutumiwa na vyombo vya habari.

Baada Kuondoka Arsenal, Wenga Kwenda Kwenye Timu Hii

$
0
0
Baada Kuondoka Arsenal, Wenga Kwenda Kwenye Timu Hii
Siku kadhaa baada ya kupita toka kocha wa Arsenal Arsene Wenger kutangaza kuwa ataondoka Arsenal mara baada ya msimu kumalizika,  leo zimeripotiwa habari mpya kuhusu Arsene Wenger baada ya kocha wa PSG ya Ufaransa Unai Emery kutangaza kuwa nae ataondoka timu hiyo.



Unai Emery mwenye umri wa miaka 46 alitolewa Champions League akiwa hatua ya 16 bora “Nimewaambia wachezaji, mkurugenzi na Rais wa club kuwa huu ndio mwisho wangu, namshukuru kila mmoja na kilichobakia ni fainali ya Kombe la Ufaransa”



Wakati kukiendelea na maswali ya nani atamrithi Wenger katika club ya Arsenal baada ya kudumu kwa miaka 22, tayari Wenger ameanza kuhusishwa na tetesi za kuwa atajiunga na Paris Saint Germain ya Ufaransa kama mbadala wa kocha Unai Emery.

Video: Zungu Amkalia Kooni Mwakyembe Kisa Kufungiwa Wimbo wa Mwanaume Mashine

$
0
0
Video: Zungu Amkalia Kooni Mwakyembe Kisa Kufungiwa Wimbo wa Mwanaume Mashine
Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu amemtaka Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe atakapokuwa akijibu hoja za wabunge zilizotolewa katika mjadala wa bajeti hiyo mwaka 2018/19, kueleza sababu za kuufungia wimbo wa Mwanaume mashine.



Akizungumza bungeni leo Aprili 27, Zungu amesema wimbo wa  Mwanaume mashine unamtaja mcheza soka wa timu ya Simba, Ramadhani Kichuya.



“Wimbo huo unamtaja mchezaji soka wa timu ya Simba, Ramadhan Kichuya, wapenzi wa timu hiyo wangependa kuusikiliza siku ya Jumapili wakati Simba ikipambana na Yanga katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam,” amesema Zungu.

Jamani Naombeni Msinilaumu Kwa Uamuzi Huu Niliouchukua Kwa Mume Wangu

$
0
0
Mimi nimeolewa miaka 15 sasa na tumejaaliwa watoto 4. Ndoa yetu ilipofikisha miaka 4-5 mume wangu alicheat, nikamkamata through sms akapinga sana lakini baadae alikubali akakiri kosa na kuomba msamaha nikamsamehe

Tumeendelea kuishi na nilipopata mtoto wa tatu akanicheat tena, safari hii alikuwa nje ya nchi kimasomo, napo alikiri na kuomba msamaha, nikamsamehe

Wakati niko mjamzito mimba ya mtoto wa nne alinicheat tena, kibaya zaidi alinicheat na house girl wanga akampa ujauzito. kwa hivyo wakati mimi nina mimba na House girl naye mjamzito (japo sikujua kama house girl alikuwa mjamzito kwani aliondoka nyumbani) niligundua baadae kuwa mtoto wa aliyekuwa house Girl wangu ni wa mume wangu

Kama kawaida yake akaomba msamaha safari hii hadi kupiga goti na kulia ili nimsamehe...na mimi kwa kuwa bado nampenda na nimemvumilia kwa mengi nikaamua kumsamehe tena..ila tulikubailana masharti mengi na akakubali masharti yote niliyompa..mwanzoni alibehave vizuri sana akawa muwazi kwangu hanifichi chochote kuhusu huyo mtoto.. na tuliishi maisha ya furaha kwani alinijali mno na alionekana kweli amerigrate.
sasa cha kushangaza siku za karibuni amebadilika sana, amekuwa msiri na hasemi chochote kuhusu huyo mtoto wa nje..siku hizi anatuma hela kwa siri na pia anawasiliana na huyo mama wa mtoto kwa siri haniambii chochote..

Nilipoona mabadiliko niliamua kumuuliza imekuwaje tena mbona siri tena wakati tulikubaliana kila kitu kiwe open? hakunijibu isipokuwa alikuwa mkali na kufoka na kusema hilo swala tumeshamalizana nalo sitaki kulisikiasikia tena..

Nikajaribu tena siku nyingine kumuuliza na majibu ndio hayo hayo, kwa kifupi hataki na anakwepa kuzungumzia hilo suala kabisa...sasa najiuliza kwa nini anafanya siri? kama hakuna jambo lolote baya basi anaficha nini? ina maana kuna kitu zaidi ya mtoto.

Sasa jamani mimi nimeamua kama ifuatavyo:

1. Na mimi nimeamua kuwa na mahusiano nje ya ndoa, jamani msinilaumu nami pia nahitaji kuliwazwa na kufarijiwa kwa kifupi nimechoka na mastress yasiyo kuwa na mwisho, sikuwahi kumcheat mume wangu katika maisha yote ya ndoa. ila sasa atanisamehe tu hata akijua wala sijali, nipo tayari kwa lolote..

2. Sina mpango wa kuondoka kwenye nyumba tuliyojenga pamoja nitaishi hapa hapa kwani sipendi watoto wangu walelwe na mzazi mmoja..watoto hawajui kinachoendelea in fact hata ndugu na jamaa hawajui chochote kwani mimi sijawaambia na wala sijawahi kuwaeleza matatizo ya ndoa yangu..kwa nje tunaonekana familia iliyobarikiwa na ina furaha lkn wenyewe ndio tunaojua ndani kukoje

3. Kwa sababu sisemagi matatizo yangu kwa ndugu na marafiki nimeamua kuweka hapa labda nitapunguza kitu fulani kichwani kwani sometime naona kama nazidiwa mawazo vile

By Qeen Maleo

Msaada Please, Mpenzi Wangu Ananing'ata Tukiwa Sita kwa Sita Mpaka Natoka Damu

$
0
0
Wakuu nifanyeje juu ya sweetie wangu huyu. I really love and Am dying for her ila hili tatizo nahisi ipo siku nitachoka

Tatizo ninapomdinya nashtukia ghafla kaning'ata shingoni, nimebadili style,nikapiga doggy kajipinda hadi kang'ata paja , yaaani huku shingoni nimejaa alama alama , wengine wanasemaga ni love bite ila hii yangu imezidi kipimo , sometimes mpaka damu zinanitoka na kuuguza kidonda..Isije ikawa ndo anachembechembe za uvampire


Wakuu what should I do

By Jackson

Breaking News: Aliyewahi Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abbas Kondoro Afariki Dunia

$
0
0

TANZIA: Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro afariki dunia usiku huu

Kandoro amefariki katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikolazwa kwa matibabu

Mbunge Msukuma Ashangaa Waziri Kufungia Video Zenye Mipasuo...Adai Ndio Starehe Yenyewe

$
0
0

“Kinachofanywa sasa Msanii wa Bongofleva anafanya kazi nzuri kwenye ku-shoot akikosea kidogo kwenye mpasuo Waziri huyo amefunga…”

“Mimi nauliza unafungia Wasanii wa Tanzania kuonyesha mpasuo, embu angalia miziki ya kina Rihanna na ndio mnakaa mnaangalia humu kwenye Youtube kila saa ila ya Tanzania mnataka Wasanii wavae dera” –Mbunge wa Geita Joseph Musukuma

“Hata ngoma za tamaduni za Kitanzania kina Mama hasa Wasukuma na Wagogo wanafunga tu kwenye maziwa hapa, wanafunga na hapa chini.... huku chini inakua kivutio, sasa mbona hii miziki ya sasa hivi mnaleta figisu ambayo hatuwaelewi”

JE UNAUNGA MKONO HOJA YA MSUKUMA AU UNAPINGA???

TOA MAONI YAKO HAPA

Ajali Mbaya Yaua Mwanajeshi na Mtoto wa Mwanajeshi Morogoro

$
0
0

AJALI, MOROGORO: Mwanajeshi mmoja wa JWTZ pamoja na mtoto wa Mwanajeshi mwenzake wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha gari la Polisi aina ya Basi lililogongana na gari dogo aina ya Noah iliyokuwa imebeba Wanajeshi wa JWTZ, maeneo ya Bwawani

Inadaiwa basi hilo la Polisi lilikuwa likitokea Dodoma huku Noah hiyo iliyokuwa na Wanajeshi takribani 6 pamoja na mtoto wa Wanajeshi mmoja wapo ilikuwa ikitokea Morogoro

Majeruhi wote wamepelekwa hospitalini Morogoro

Kanuni Mpya Kudhibiti Matusi na Picha za Uchi Mitandaoni

$
0
0
Serikali imesema kanuni mpya za maudhui kwenye mitandao, runinga na redio zimetungwa kwa lengo la kudhibiti usambazaji wa kauli chafu, matusi, picha za utupu na zenye maudhui yasiyofaa kwa watoto.

Kanuni hizo zimetungwa ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Mawasiliano ya Kiektroniki na Posta ya Mwaka 2010.

Pia imesema itaendelea kuhamasisha utengenezaji na uzalishaji wa maudhui ya ndani yanayozingatia maadili, mila na desturi za Mtanzania huku ikikiri kuwapo kwa mmomonyoko wa maadili kunakoongezeka siku hadi siku, hivyo imejipanga kukabiliana na changamoto hiyo.

Akiwasilisha bungeni mjini hapa jana hotuba ya makadirio ya bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Waziri wa wizara hiyo, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema kanuni hizo zinamtaka kila mtumiaji wa mitandao awe na namba ya siri ili 'wajanja' wasitumie kirahisi chombo chake cha mawasiliano kutenda matendo yanayokwenda kinyume cha sheria.

Alisema kanuni hizo pia zinaweka muda maalumu kwa picha mgando na nyongevu za filamu au muziki wenye maneno yasiyofaa kwa watoto kuonyeshwa kwenye runinga.

"Tuliweka muda huo maalumu kuanzia saa 4:00 usiku hadi saa 11:30 asubuhi, lakini wadau wamekuwa wakali, wanadai picha na nyimbo hizo zirushwe kuanzia saa 6:00 usiku wakati watoto wamelala na mwisho saa 11:00 asubuhi, kabla watoto hawajaamka," alisema Dk. Mwakyembe.

Aliongeza kuwa kanuni hizo zinataka madaraja yawekwe kwa kila filamu, video, wimbo au albamu kutoka ndani au nje ya nchi ndipo kazi hizo zitumike kwenye vyombo vya utangazaji.

"Msingi wa kanuni hizi ni kuhakikisha teknolojia inatutumikia badala ya kututumikisha na kuvuruga mustakabali wa maadili ya taifa letu. Ni kanuni zilizozingatia mazingira yetu halisi kama kila Watanzania," alisema.

Dk. Mwakyembe alisema, mmomonyoko wa maadili ya Kitanzania unaoongezeka siku hadi siku, ni miongoni mwa changamoto zinazoikabili wizara yake.

Alisema wanaendelea kutoa elimu kupitia vyombo vya habari na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuzingatia maadili, mila na desturi za Kitanzania.

Ili kutekeleza majukumu yake kwa mwaka ujao wa fedha, Dk. Mwakyembe aliliomba Bunge kuidhinisha bajeti ya Sh. bilioni 33.3. Kati yake, Sh. bilioni 12.2 ni mishahara, Sh. bilioni 9.3 kwa ajili ya matumizi mengine na Sh. bilioni 8.7 za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya April 28

$
0
0


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya April 28
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images