Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104743 articles
Browse latest View live

Maaskofu wa Kanisa Katoliki Wamtaka Rais Buhari Kujiuzulu

$
0
0
Maaskofu wa Kanisa Katoliki Wamtaka Rais Buhari Kujiuzulu
Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Nigeria wamemtolea wito Rais Muhammadu Buhari kujiuzulu baada ya makasisi wawili na wafanyakazi wengine kuuawa Jumanne alfajiri.

Buhari ameitwa na wabunge ili waweze kujadili hali ya usalama katika Jimbo la Benue. Pia wabunge hao Jumatano walipitisha kura ya kutokuwa na imani na wakuu wa masuala ya usalama.

Maaskofu wa Kikatoliki wanamshutumu rais kwa kupuuza wito wa mara kwa mara wa kumtaka kutupia macho tatizo la usalama wenye upogo na mbinu dhaifu za kudhibiti mapigano kati ya Wakristo ambao ni wakulima na Waislamu ambao ni wafugaji.

Hali hii ya kushindwa iwe ni kutokana na utendaji dhaifu au ukosefu wa utashi wa kisiasa, ni wakati wake sasa kuchagua njia ya heshima na kufikiria kujiuzulu kuliokoa taifa hilo ili lisididimie kabisa.

“Kwa kuwa rais ambaye anawateua wakuu wa usalama amekataa kuwaita na kuwapa amri, tunachoweza ni kuhitimisha kwamba wanatekeleza majukumu yaliyoandikwa ambayo yeye ameridhia,” imesomeka taarifa ya maaskofu hao.

Taarifa hiyo imekwenda mbali hadi kusema kwamba rais amepoteza kuaminika kwake kwa wananchi kutokana na kushindwa kwake kuiweka nchi kuwa salama.

“Kushindwa huku kuwa ni kutokana na uwezo wake mdogo kiutendaji au ukosefu wa utashi wa kisiasa, wakati umefika kwa yeye kuamua njia ya heshima na kufikiria kukaa kando ili kuliokoa taifa lisiangamie kabisa”.


Rick Ross Kupiga Bonge la Shoo Leo Kenya

$
0
0
Rick Ross Kupiga Bonge la Shoo Leo Kenya
RAPA Mmarekani, Rick Ross, aliwasili jana jijini Nairobi, nchini Kenya kwa ajili ya kufanya shoo ambayo itafanyika leo (Jumamosi) katika viwanja vya Carnivore. Msanii huyo ambaye ni maarufu kwa kufanya shoo akiwa kifua wazi, alionekana kupungua kidogo umbo lake ambalo mashabiki wake wamelizoea.



Muda mfupi baada ya kuongea na vyombo vya habari alipotua uwanja wa ndege, mwanamuziki huyo aliondoka na msafara wake hadi katika hoteli iliyoandaliwa kwa ajili yake. Kwa mujibu wa kituo cha Radio NGR, Ross ambaye ni maarufu kwa jina la Boss, atatumbuiza na wasanii maarufu wa Kenya kina Khaligraph Jones, Camp Mullah na Nyashinski.


Hii itakuwa ziara ya kwanza ya Rick Ross katika Kenya licha ya kupiga kolabo na mwanamuziki Diamond Platnumz wa Tanzania katika wimbo wa Waka Waka.

Video:Hivi Ndivyo Ilivyokuwa Katika Send Off ya Mchumba Wake Stamina

$
0
0
Video:Hivi Ndivyo Ilivyokuwa Katika Send Off ya Mchumba Wake Stamina
RAPA maarufu Bongo anayeunda Kundi la Rostam, Stamina na mchumba wake, Veronica wamefanya Send Off ya aina yake nyumbani kwao na staa huyo mkoani Morogoro usiku wa kuamkia leo.

Stamina na Veronica ambao wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni, katika hafla hiyo walihudhuria baadhi ya mastaa akiwemo swahiba wa Stamnina, rapa Roma Mkatoliki na wengine.


Albert Msando Kuongoza Kamati ya Makonda ya Kutafuta Haki ya Watoto

$
0
0
Albert Msando Kuongoza Kamati ya Makonda ya Kutafuta Haki ya Watoto
Wakili Albert Msando ataongoza kamati iliyounda na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda kwa ajili ya kushughulikia kesi zote na changamoto zilizojitokeza katika zoezi la kutafuta haki za watoto waliotelekezwa na wazazi wao.

Zoezi hilo lilifungwa hapo jana April 27, 2018 ambapo wananchi 17,000 walijitokeza, kati yao 7,184 walisikilizwa, huku 270 wakipimwa DNA.

RC Makonda ameunda Kamati ya Wataalamu 15 wakiwemo Wanasheria, Maafisa Ustawi wa Jamii, Jeshi la Polisi Dawati la jinsia na Asasi za kiraia itakayofanya kazi ya kupitia mapungufu ya kisheria na Changamoto zilizojitokeza.

Kamati hiyo ambayo itaanza kazi rasmi May 05, 2018 chini ya Wakili Albert Msando ambaye ndiye Mwenyekiti wake itatoa mapendekezo kwaajili ya kufikishwa kwa mamlaka husika ili kufanyiwa maboresho.

Utakumbuka December 20, 2017 Wakili Albert Msando aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli katika tume itakayokuwa na jukumu la kufuatilia mali za Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kabla ya kuteuliwa na Rais Magufuli, September 26, 2017 Wakili Msando aliteuliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrion Mwakyembe kuwa Mjumbe wa kamati ya kupitia sheria ya Hakimiliki za kazi za wasanii.

Kikwete Afunguka Haya Baada ya Kuuliwa kwa Mdogo wa Heche "Jeshi Letu Limetengenezwa kulinda watu na si Kuua Wasio na Hatia"

$
0
0
Kikwete Afunguka Haya Baada ya Kuuliwa kwa Mdogo wa Heche "Jeshi Letu Limetengenezwa kulinda watu na si Kuua Wasio na Hatia"
Mbunge wa jimbo la Chalinze (CCM) Ridhiwani Kikwete amefunguka kuhusu kitendo cha mdogo wa Mbunge  Heche wa Tarime aliyeuawa na polisi aliyetajwa kwa jina la William Marwa kuwa kimemsikitisha sana.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Ridhiwani ameandika “Kitendo kilichotokea sio tu kimesikitisha ukoo wa Bwana Heche lakini kwangu binafsi. Jeshi letu limetengenezwa kulinda watu na mali zao sio kuumiza wasio na hatia“
“Ni imani yangu Serikali itasimamia haki kwa familia ya Heche. Poleni sana kwa msiba. Mungu awape subira John Heche” -Ridhiwani Kikwete
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya, Henry Mwaibambe amesema tayari wanamshilia askari wake mwenye namba E1156 Koplo William Marwa kwa tuhuma za kusababisha kifo cha kijana Suguta Chacha mwenye umri wa miaka 26.

Baada ya Gigy Money Kupata Mtoto Amber Lulu Afunguka Haya

$
0
0
Baada ya Gigy Money Kupata Mtoto Amber Lulu Afunguka Haya
Msanii wa muziki Bongo na Video Vixen, Amber Lulu amefunguka mipango yake ya kuitwa mama.

Muimbaji huyo anayefanya vizuri na ngoma ‘Jini Kisirani’ ameiambia XXL ya Clouds FM kuwa bado anajipanga kwa ajili ya suala hilo ila kwa sasa hana mpango.

“Kwa kweli kwa sasa hivi sijatarajia bado, vitu vyangu vingi bado sijakamilisha,” amesema.

“Sio Gigy Money amepata mtoto na mimi nipate, no! unajua unapopata mtoto kuwe na maandalizi yake. Labda yeye rafiki yangu kajiandaa mtoto lazima aje kwenye mazingira mazuri,” ameongeza.

Gigy Money ambaye yupo katika mahusiano na Mtangazaji wa Choice FM, M o J alijifungua mtoto wa kike usiku wa kuamkia jana April 27, 2017 na amempa mwanae jina Mayra.

John Heche Afunguka Mazito Baada ya Mdogo Wake Kuuwawa Kikatili na Polisi

$
0
0
John Heche Afunguka Mazito Baada ya Mdogo Wake Kuuwawa Kikatili na Polisi
Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amefunguka kuwa mpaka sasa haelewi ni kwa vipi mtu anaweza kuuwawa na polisi kwa kuchomwa kisu tena akiwa amefungwa pingu huku akikumbushia tukio la mdogo wake mwingine kujeruhiwa vibaya na polisi ambapo alisababishiwa ulemavu mwaka jana.


Mbunge Heche amesema kwamba mtu kuchomwa kisu mgongoni ni kudhamiria kuua kwasababu mtu huyo hakuwa anapambana.

"Nilijua mikononi mwa polisi ni sehemu salama, wiki mbili zilizopita kijana Allen alikufa katika mazingira tata kule Mbeya, Mwanza mama aliyekamatwa na kunyimwa dhamana mtoto wake mchanga alikufa. Leo ni kwangu mdogo wangu ameuwawa kikatili sana mikononi mwa polisi. Maisha yangu yote nimeyatoa kupigania haki ili watu wasionewe, mtuhumiwa asifanywe mkosaji na kuhukumiwa kabla ya vyombo vya sheria kumhukumu,"  Heche.

Ameongeza " Mwaka jana mdogo wangu mwingine aliumizwa vibaya sana na polisi. IGP Mangu na RPC waliokuwa Tarime walilipa uzito suala hilo lakini walipoondolewa, suala liligeuzwa kisiasa na wale vijana waliokua wamemjeruhi mdogo wangu ambaye mpaka sasa sikio moja halisikii,wakarudishwa kazini kinyemera na kuhamishwa Tarime kama kunikomoa. Mimi nimewahi kutishiwa kuuwawa kituo cha polisi, najisikia maumivu makubwa mno lazima Watanzania wakatae hali hii".

Pamoja na hayo Mbunge huyo amehoji juu ya ukimya wa Waziri na kuongeza kwamba ni watu wangapi wanakufa na kuumizwa mikononi mwa polisi bila matukio kujulikana wala kutangazwa na kuweka wazi kwamba atazungumza muda ukifika.

Waziri Shonza Afunguka Kuhusu Kufungiwa kwa 'Mwanaume Mashine'

$
0
0
Waziri Shonza Afunguka Kuhusu Kufungiwa kwa 'Mwanaume Mashine'
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesema wimbo wa Mwanaume Mashine haujafungiwa.

Ametoa kauli hiyo leo jioni Aprili 27, 2018 baada ya leo mchana Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu kuhoji sababu za kufungiwa kwa wimbo huo.

Shonza ametoa kauli hiyo wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha bajeti ya wizara hiyo mwaka 2018/19 baada ya Zungu kutaka kupewa jibu kuhusu ‘Mwanaume Mashine’ kutokana na maelezo ya Shonza na Waziri wa wizara hiyo, Dk Harrison Mwakyembe wakati wanajibu hoja za wabunge kuhusu bajeti hiyo kutoeleza sababu za kufungiwa kwa wimbo huo.

Mchana Zungu alihoji kufungiwa kwa wimbo huo wakati unamtaja mchezaji mahiri wa Simba.

Bunge limepitisha Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mwaka 2018/19

Kutana na Mtaalam wa Matabibu ya nyota za Binadam na Bingwa wa Tiba za Asili Afrika Mashariki.

$
0
0
Je Wewe ni Mwanasiasi, Mfanyabiashara , Msani, ama mwanafunzi tunazo dawa na pete za bahati zenye uwezo mkubwa wakuyabadilisha maisha yako nakukupatia mafanikio makubwa ndani ya mda mfupi tu.

Kutana na SHABA WA SHABA kutoka Tanga,
Yeye ni mtaalam na mtabibu wa nyota za binadam na bingwa wa tiba za asili Afrika mashariki.
Wasiliana na mtaalam huyu kwani yeye ufaulu pale wote waliko shindwa na pia humaliza kazi zilizo shindikana ama zilizo achwa ndani ya siku1 tu. Sasa amezianza ziyara zake za mikoani na atayatembeleye maeneo mbali mbali ndani na inje ya nchi.

Anatibu magonjwa sugu yanaojulikana nasiojulikana kwakutumia maji, Kioo na mitishamba.
Anazo dawa za mapenzi, kumrudisha alipoteya, kutoa Mikosi, Kutatuwa shida za chumaulete, mvuto wa biashara na sehem za kazi, kusafisha nyota, kurudisha mali zilizo ibiwa, zilizpotea, ama zilizodhulumiwa, kushika wezi na wachawi, kutoa ndagu , Kutoa kinga ya mwili, nyumba, Biashara, kufukuza majini wabaya, Kuuza kwa haraka ( shamba, nyumba, Gari,...), Kesi mahakamani, Kuweka Zindiko ya mwili, nyumba, shamba, Gari, kupata Kazi na kupandishwa cheo, mali na utajiri bila masharti na mengine mengi ya Siri...

Kwa tiba na ushauri wasiliana na ofisi kwa nambari ya simu :
+255 785 358 267 ,
+255 785 358 267

Miss World University Afrika 2017 Akutana na Waziri Mwakyembe

$
0
0
Miss World University Afrika 2017 Akutana na Waziri Mwakyembe
Mshindi wa Miss World University Afrika 2017, Mtanzania Queen Elizabeth Makune, jana April 27 alifika Bungeni Jijini Dodoma na kufanya mazungumzo na viongozi mbali mbali wa serikali wanaosimamia sanaa akiwemo Waziri Harrison Mwakyembe na Naibu wake Juliana Shonza.



Mshindi huyo ambaye alishinda taji hili katika mshindano yaliyofanyika nchini Korea Kusini na warembo kutoka mataifa 53 walishiriki, alihudhuria Dodoma ikiwa ni siku ya kusomwa kwa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.



Niyonzima: Simba Itapata Matokeo Mazuri Mechi ya Yanga

$
0
0
Niyonzima: Simba Itapata Matokeo Mazuri Mechi ya Yanga
KIUNGO mchezeshaji wa Simba, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda ameweka wazi kuwa anaamini klabu yake itapata matokeo mazuri mbele ya wapinzani wao, Yanga licha ya yeye kutokuwepo katika kikosi cha timu hiyo kutokana na kupata msiba wa dada yake nchini kwao.



Niyonzima alisafiri usiku wa juzi Jumatano kwa ajili ya kuelekea kwao Rwanda kwa ajili ya kuwahi msiba wa dada yake ambapo ataukosa mchezo huo wa Simba dhidi ya Yanga ambao utafanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.



Kwenye mchezo wa kwanza ambao kiungo huyo alikuwepo timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1. Mechi iliyopigwa Oktoba 28, mwaka jana katika Dimba la Uhuru.


Akizungumza na Championi Ijumaa, kiungo huyo ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’ alisema kuwa mashabiki wa Simba wasiwe na wasiwasi juu ya kutokuwepo kwake kwa sababu anawaamini wachezaji wenzake watapata matokeo mazuri kwenye mechi hiyo ya Kariakoo Dabi.



“Mashabiki wao wanatakiwa kutuliza roho zao kwani licha ya mimi kutokuwepo katika mchezo huu lakini Simba ina kikosi kipana na wachezaji waliobaki wanaweza kuifanya kazi ya kupata matokeo mazuri mbele ya wenzetu na pia ninawaombea,” alisema.

Babu Mwenye Uzito KG 181 Akiri Kumuua Mjukuu kwa Kumkandamiza

$
0
0
Babu mwenye uzito KG 181 akiri kumuua mjukuu kwa kumkandamiza
Mwanaume mmoja ambaye anatajwa kuwa uzito wa kg 181 nchini Marekani amekiri kumuua bila kukusudia ‘mjuu wake wa kufikia’ (mjukuu wa mkewe) wa miaka 11 kwa kumkalia, tukio ambalo lilitokea mwaka jana.

Mwanaume huyo ajulikanaye kama Donald Martin, 58, ameeleza kuwa alikuwa anajaribu kumdhibiti mtoto huyo aliyekuwa anataka ‘kupigana’ na bibi yake.

Mdogo wa Mbunge John Heche asababishiwa kifo kwa kuchomwa kisu

Anasema katika kuamua ugomvi huo alimkandamiza kwa bahati mbaya mtoto huyo Dylan Davis kwenye kochi jambo lililosababisha kifo chake.

Bunge Lakanusha Kumtimua Cyprian Musiba Bungeni

$
0
0
Bunge Lakanusha Kumtimua Cyprian Musiba  Bungeni
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekanusha taarifa zilizodai kuwa Mkurugenzi wa CZI, Cyprian Musiba amefukuzwa Bungeni.

Taarifa hizo ziliibuka mara baada ya kuwepo picha mtandaoni ikimuonyesha Musiba ‘akizozona’ na baadhi ya watumishi wa Bunge. Kupitia ukurasa wa Twitter wa Bunge wamefafanua kuhusiana na hilo;

Picha zinazosambaa kwenye mitandao zikidai kuwa Mkurugenzi wa CZI Ndg. Cyprian Musiba amefukuzwa Bungeni si kweli. Musiba amekidhi vigezo vya kusajiliwa kuripoti habari za Bunge na kwamba alikuwa akihamishwa kwenda katika jukwaa mahsusi ambalo Waandishi hukaa wawapo Bungeni.


Musiba ni Mhariri wa Gazeti la Tanzanite na Mwanasheria, hivi karibuni alifunguliwa kesi na Mjasiriamali/Mwanahabari na Mkurugenzi wa Compass Communications, Maria Sarungi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa madai ya kumkashifu na kuchafua jina lake kupitia mkutano wake na Waandishi wa Habari uliyofanyika February 25, 2018.

Tukio la Kuuawa Watoto 140 kwa Wakati Mmoja Kama Sadaka Lagundulika

$
0
0
Tukio la kuuawa watoto 140 wakati mmoja kama sadaka lagundulika
Hivi karibuni wataalamu wamegundua kinachofikiriwa kuwa tukio kubwa zaidi la mauaji dhidi ya watoto kwenye historia ya dunia.

Imegundulika kwamba zaidi ya watoto 140 waliuawa kama sadaka kwa wakati mmoja katika moja ya miji ya Pwani ya Kaskazini ya nchini Peru, takribani miaka 550 iliyopita.

Inaelezwa pia sadaka ya watoto hao ilitolewa pamoja na aina ya miti ambayo ilikuwa michanga iliyojulikana kama Ilama siku hiyo hiyo waliouawa watoto.

Mdogo wa Mbunge John Heche asababishiwa kifo kwa kuchomwa kisu

Watoto hao 140 wanaelezwa kuwa walikuwa na umri wa kuanzia miaka mitano hadi 14 japokuwa wengi wao walikuwa kati ya miaka 8 hadi 12

Waziri Majaliwa Avihasa Vyama vya Siasa

$
0
0
Waziri Majaliwa Avihasa Vyama vya Siasa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa vyama vya siasa wajitahidi kuwa makini na namna wanavyoendesha vyama vyao kwa sababu wananchi wanaowaongoza ni wa vyama vyote.


Majaliwa ameyasema hayo leo  wakati akizungumza na Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa katika ukumbi wa mikutano wa Waziri Mkuu ulioko Mlimwa jijini Dodoma.

"Viongozi wa vyama vya siasa wanatakiwa wajitahidi kuwa makini na namna ambavyo wanaendesha siasa katika vyama vyao, wananchi wanaowaongoza ni wa vyama vyote hivyo tupeleke ujumbe ambao utawaongoza kujileta maendeleo,” Majaliwa.

Aidha Kiongozi huyo amewataka pia viongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa waendelee kushikamana ili waweze kulifikisha Taifa mahali ambapo Watanzania wanapatarajia ikiwa ni pamoja na kupunguza umaskini.

Waziri Mkuu amesema kuwa mazungumzo yaliyofanyika leo baina ya Serikali na viongozi hao yameonesha nia ya pamoja ya kuendeleza ushirikiano na kwamba wana wajibu wa kuendeleza historia nzuri kwani siasa ni moja ya nyenzo zinazochochea  maendeleo.

Akijibu ombi la viongozi hao kuhusu changamoto ya upatikanaji wa fedha za kuendesha shughuli za baraza hilo ikiwemo mikutano, Waziri Mkuu ameahidi kuwa Serikali  itafanyia kazi maombi hayo ili waweze kutimiza majukumu yao kama ilivyokusudiwa.


Waliopandikizwa Figo Muhimbili Waruhusiwa

$
0
0
Waliopandikizwa Figo Muhimbili  Waruhusiwa
Wagonjwa wawili kati ya wanne waliopandikizwa figo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wameruhusiwa leo baada ya afya zao kuimarika.

Akizungumza leo Aprili 28, Mkuu wa Kitengo cha Figo, Dk Jackline Shoo amesema upandikizaji huo ni hatua kubwa na imedhihirisha kuwa madaktari wa Tanzania wanaweza.

Dk Shoo amesema wagonjwa wote waliopandikizwa wanaendelea vizuri ila wamewaruhusu wawili huku wakiendelea kuwafuatilia waliosalia.

"Tunashukuru serikali kwa kutuwezesha tunaomba iendelee kutuona ili wigo wa huduma zetu upanuke, tuwahudumie hata watu kutoka nje ya nchi," amesema

Amesema ni matamanio yake kuona kitengo  cha figo, kinakuwa na uwezo wa kuwahudumia watu wengi zaidi kutoka ndani na nje ya nchi.



Ajali ya Gari Yaua Wanafunzi Bukoba

$
0
0
Ajali ya Gari Yaua Wanafunzi Bukoba
Watoto wawili ambao ni wanafunzi wamefariki dunia leo kwa kugongwa na basi la Kampuni ya Frester basi lenye namba za usajili T720 DEV katika eneo la Katongo Luranda Bukoba mkoani Kagera na kisha gari hilo kupinduka.


Akiongea na www.eatv Kamanda wa Polisi mkoani humo Agustine Olomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, ambapo amesema watoto hao wawili walikuwa wanaelekea shule ndipo wakagongwa na basi hilo na kudai kuwa wamefanikiwa kumkamata dereva wa basi hilo.

Aidha Kamanda Olomi amesema kuwa majeruhi zaidi wa 20 ambao walikuwa kwenye basi hilo wamepelekwa hospitali kwa ajili ya kufanyiwa matibabu zaidi kutokana na majeraha waliyoyapata.

Lema Anena Maneno Mazito kwa Jeshi la Polisi

$
0
0
Lema Anena Maneno Mazito kwa Jeshi la Polisi
Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameandika katika ukurasa wake wa Twitter “Kazi ya Polisi ni kazi zenye heshima ni kazi ya kujitolea kwa ajili ya wengine,”

“Sura hii imepotea na kuna chuki kubwa ambayo ni hatari kwa ustawi wa nchi. Matukio dhidi ya raia yanaleta wasi wasi katika nchi. Kiongozi anayejali nchi hapaswi kuwa kipofu na asiweze kuona mambo haya” -ameandika Lema

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya April 29

$
0
0

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya April 29

Yanga yawapa ilani waamuzi watakaochezesha Mechi ya kesho dhidi ya Simba

$
0
0
Uongozi wa klabu ya Yanga umewataka Waamuzi watakaochezesha mchezo wa kesho dhidi ya Simba kufuata sheria 17 za mchezo wa soka.

Kauli hiyo imetolewa na Yanga kupitia Afisa Habari wa timu hiyo, Dismas Teni, ambapo kikosi chao kitakuwa mgeni dhidi ya Simba.

Teni ameeleza kuwa timu zimewekeza kwenye mpira hivyo haitopendeza kuona Waamuzi wanaharibu ladha ya mpira na ksuhindwa kutafsiri sheria 17 za mchezo wa soka.

Timu hizo zinakutana kesho ikiwa ni katika mzunguko wa pili wa ligi, baada ya ule wa kwanza kwenda sare ya bao 1-1.

Viewing all 104743 articles
Browse latest View live




Latest Images