Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Azam FC yapepea kwa ushindi wa 1-0 dhidi Mtibwa Sugar

$
0
0
Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC  imefanikiwa kuchomoza na ushindi mwembamba wa bao 1 – 0 dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

Azam FC imefanikiwa kupata bao lake la mapema kupitia kwa mchezaji wake, Shaban Idd dakika ya 38 akipokea pasi safi kutoka kwa Ramadhan Singano na hivyo kuwafanya matajiri hao wa Jiji la Dar es Salaam kuzidi kujiimarisha nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.

Polisi Abakwa Alipokwenda Kumkamata Mbakaji

$
0
0
Askari Polisi mmoja wa kike huko Yorkshire Kusini, nchini England ameripoti kubakwa na mwanaume ambaye alikwenda kumkamata akiwa na askari mwingine kwa makosa ya jaribio la kubaka.

Mwanaume huyo alikuwa akihisiwa kufanya vitendo hivyo vya kujaribu kubaka watoto wa kike na ndipo askari huyo alipokwenda na mwenzie kumkamata ili afikishwe polisi.

Inaelezwa kuwa mwanamume huyo tayari amekwisha kamatwa na amefungulia mashtaka ya kujaribu kubaka, shambulio, unyanyasaji wa kijinsia na uharibifu wa makosa ya jinai.

Zimbabwe yawa Nchi ya Pili Afrika kugawa Leseni za Kulima Bangi

$
0
0
Wiki hii inayomalizika serikali ya Zimbabwe imetoa ruhusa kisheria bangi kulimwa kama zao jingine la chakula au biashara.

Ruhusa hiyo imetolewa ili zao hilo litumike kwaajili ya sababu za matibabu. Kwa watakaotaka kulima zao hilo, watapewa leseni ya miaka mitano kwaajili ya kumiliki, kusafirisha na kuuza bangi na bidhaa zake zilizokaushwa.

Zimbabwe ndio nchi ya pili Afrika kufanya jambo hili baada ya Lesotho kuwa ya kwanza kugawa leseni za kufanya kilimo hicho mwezi September mwaka 2017.

VIDEO: 'Inasikitisha' Hiki Ndicho Kilichomuua Kandoro'

$
0
0
Mtoto wa  marehemu wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Abbasi Kandoro amefunguka na kueleze sababu iliyopelekea kifo cha babayake.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI

Wanaosema Yanga Mbovu Manara Anamajibu yao

$
0
0
Haji Manara amesema amewasikia baadhi ya mashabiki wa Yanga wakisema timu yao ikiwa mbovu ndio huwa inaifunga Simba, Manara amesema kama wanadhani timu yao ni mbovu wasiipeleke uwanjani kwa sababu hawataki kuifunga timu mbovu.

Anawashangaa mashabiki hao wanao sema Yanga ni mbovu wakati ndio mabingwa watetezi wa VPL wakiwa wameshinda taji hilo mara tatu mfululizo katika misimu iliyopita na kuongeza kuwa hawaidharau.

“Kuna watu nimesikia wanasema Yanga ikiwa mbovu huwa inaifunga Simba, mimi siamini kama Yanga ni mbovu, unasemaje timu mbovu wakati ndiyo bingwa mara tatu mfululizo, wamefuzu hatua ya makundi Afrika. Hata sisi hatutaki kuifunga timu mbovu kama wabovu wasije uwanjani sisi tunataka timu nzuri itupe ushindani watanzania wapate raha.”
“Hatuwadharau Yanga, ni timu bora wamekuwa mabingwa mara tatu mfululizo wameingia hatua ya makundi ya mashindano ya Afrika lakini sisi tunahitaji ushindi. Ushindi wetu utatokana na support ya mashabiki.”

Download Hapa Application Mpya ya Udaku Special Uweze Soma Vimbwanga na Udaku Mtaani Kila Siku

$
0
0

Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Upya Application yetu ya UDAKU SPECIAL Maana ile ya Zamani Tutaifuta.

Kuna Marekebisho Makubwa tumeyafanya ikiwa na tatizo la Notification kutatuliwa

NB: App mpya ina Icon Nyekundu

 Bonyeza Hapa Chini Kuinstall Upya:


==>>Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>>

“Sioni Beki wa Yanga wa Kumkaba Okwi na Bocco

$
0
0

Mchezaji wa zamani wa Simba pia amewahi kuifundisha timu hiyo kwa nyakati tofauti kocha Jamhiri Kihwelu ‘Julio’ anatamani Simba ipate ushindi Yanga siku ya Jumapili Aprili 29, 2018 ili kujihakikishia ubingwa wa ligi msimu huu.

Julio amesema kwa sasa haoni beki wa Yanga ambaye anaweza kuwazuia washambuliaji wa Simba Emanuel Okwi na John Bocco ambao wapo kwenye ubora wao wa kutupia kambani.

“Upande wangu napenda tuwafunge Yanga kwa sababu naamini tukishawafunga tayari tunakuwa mabingwa, lakini kama watatufunga wataanza kutuletea ugumu kwenda kwenye ubingwa.”
“Si dhani kama kuna beki kwa kipindi hiki wa kuweza kumkaba Okwi au John Bocco wengine sitakikuwasema mambo ni mepesi yanaeleweka.”

“Yanga wajipange, tupo vizuri sidhani kama kipindi cha kwanza watamaliza hawajachezea tatu.”


Mzee Majuto na Marehemu Kanumba Waifumbua Macho serikali

$
0
0
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeumizwa vikali na baadhi ya makampuni yanayowatumia vibaya wasanii wa muziki na waigizaji wa filamu kwenye matangazo yao kwa kuingia nao mikataba mibovu ambayo haina faida kwa watu hao.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe juzi bungeni wakati akihitimisha mjadala wa makadirio ya bajeti ya wizara yake.

Waziri Mwakyembe amesema amechukizwa na kitendo cha Mzee Majuto kuomba achangiwe fedha kwa ajili ya matibabu ile hali anaonekana karibia nusu ya mabango yote ya matangazo hapa nchini na kutangaza kiama kwa makampuni na taasisi zinazonyonya wasanii.

“Kwa kweli dhuluma kwa wasanii ilikuwapo kubwa sana kwa kutumia ‘middle men’ (watu wa kati), watu wenye fedha wamechezea sana wasanii wetu. Hili limeanza kubadilika tumeanza kuwa-empower (kuwawezesha) wasanii wetu kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wasitumie middle men,“ameeleza Waziri Mwakyembe.

“Kwa mfano vijana wetu wazuri kama kina Kanumba, amefariki kila mtu anajua ni milionea, hapana.. waliotajirika ni wengine. Leo hii mwanasanaa mzuri mzee majuto anaumwa, anaomba fedha, mimi nachanga kutoka mfuko kwangu, maisha yenyewe unayaelewa waheshimiwa.. lakini nusu ya mabango ya biashara ni ya Mzee Majuto.“amesema Mwakyembe.

Hata hivyo, Waziri Mwakyembe tayari ameshateua kamati maalumu ya wanasheria ambayo itapitia upya mikataba yote ya wasanii na waigizaji kwa kuanzia na Makampuni yaliyowahi kufanya kazi na Mzee Majuto na Marehemu Steven Kanumba.

“Naomba sasa nitumie nafasi hii kueleza kwamba nimeunda Kamati ya wanasheria, tunaanza na kesi ya Mzee Majuto, Mashirika yote na makampuni yote yaliyoingia mikataba na Mzee Majuto tutaipitia upya mikataba hiyo, kama ameonewa ni lazima ilipwe familia yake, tumeshachoka. Na tukishamaliza tunarudi kwa Kanumba na msanii yeyote ambaye anaona aliingia mkataba wa kipumbavu aje atuone.“amemaliza Waziri Mwakyembe.

Familia ya Mzee Majuto Jumatano Aprili 25, 2018 ilijitokeza kuomba msaada wa hali na mali kwa Watanzania ili aweze kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Baada ya P-Square na Diamond, Rick Ross kuwaibukia Sauti Sol

$
0
0
Wakati leo April 28, 2018 msanii kutoka nchini Marekani, Rick Ross akitarajiwa kufanya show nchini Kenya, rapper huyo ana mpango wa kuacha alama katika nchi hiyo.

Akizungumza na NRG Radio Rick Ross amefunguka kuhusu mipango ya kufanya kolabo na kundi la muziki kutoka nchini Kenya, Sauti Sol.

Endapo kolabo hiyo itafanikiwa kutoka Sauti Sol watakuwa wasanii wa watatu Afrika kufanya kolabo na Rick Ross mara baada ya kundi la P Square kutoka Nigeria ambao mwaka 2012 walitoa wimbo uitwao Beautiful Onyinye, mwaka 2017 Diamond alimshirikisha rapper huyo katika ngoma yake ‘Waka’.

Kutana na Mtaalam wa Matabibu ya nyota za Binadam na Bingwa wa Tiba za Asili Afrika Mashariki.

$
0
0
Je Wewe ni Mwanasiasi, Mfanyabiashara , Msani, ama mwanafunzi tunazo dawa na pete za bahati zenye uwezo mkubwa wakuyabadilisha maisha yako nakukupatia mafanikio makubwa ndani ya mda mfupi tu.

Kutana na SHABA WA SHABA kutoka Tanga,
Yeye ni mtaalam na mtabibu wa nyota za binadam na bingwa wa tiba za asili Afrika mashariki.
Wasiliana na mtaalam huyu kwani yeye ufaulu pale wote waliko shindwa na pia humaliza kazi zilizo shindikana ama zilizo achwa ndani ya siku1 tu. Sasa amezianza ziyara zake za mikoani na atayatembeleye maeneo mbali mbali ndani na inje ya nchi.

Anatibu magonjwa sugu yanaojulikana nasiojulikana kwakutumia maji, Kioo na mitishamba.
Anazo dawa za mapenzi, kumrudisha alipoteya, kutoa Mikosi, Kutatuwa shida za chumaulete, mvuto wa biashara na sehem za kazi, kusafisha nyota, kurudisha mali zilizo ibiwa, zilizpotea, ama zilizodhulumiwa, kushika wezi na wachawi, kutoa ndagu , Kutoa kinga ya mwili, nyumba, Biashara, kufukuza majini wabaya, Kuuza kwa haraka ( shamba, nyumba, Gari,...), Kesi mahakamani, Kuweka Zindiko ya mwili, nyumba, shamba, Gari, kupata Kazi na kupandishwa cheo, mali na utajiri bila masharti na mengine mengi ya Siri...

Kwa tiba na ushauri wasiliana na ofisi kwa nambari ya simu :
+255 785 358 267 ,
+255 785 358 267

Ivo Mapunda Akiri Uwepo wa Ushirikina Kambini

$
0
0
Mhemko wa pambano la Simba na Yanga umepanda, presha ni kubwa kila kona. Shaffih Dauda imekutana na mlinda lango wa zamani wa klabu ya Simba Ivo Mapunda na kufanya naye mahojiano kuhusiana na pambano hilo.
Mapunda ameongea mengi ikiwemo suala la ushirikina, imani za kishirikina zimekuwa zikitawala sana katika soka la Tanzania na Afrika kwa ujumla na Ivo amekiri kuwepo kwa imani hizo katika soka la Tanzania.
Ivo amekiri kwamba wakati akiichezea Simba walikiwa wakifanya ushirikina, japokuwa Ivo yeye amekana kushiriki moja kwa moja katika mambo hayo ila amesema kulikuwa na wataalamu ambao walikuwa wanawafuata uwanjani.

“Katika vyumba vya kubadilishia nguo walikuwa wanakuja watu wanatupa vitu vya kuvaa ambavyo ni vya kishirikina, mimi sikuwa nafanya hivyo, mara nyingine nilikuwa natupa chooni au naficha kwenye begi.”

Ivo anasema hakuwa anaamini katika mambo hayo yaliyokuwa yakifanyika Simba (uchawi), kwani kama ni kweli uchawi ungekuwa upo baasi hao waganga wangemsaidoa kwenda kuchukua au kucheza nafasi ya De Gea.

Kuhusu taulo lake ambalo lilikuwa likizua kizaa zaa mara nyingi likizaniwa kuwa na ushirikina, Mapunda amekanusha kuhusu ushirikina katika taulo hilo na kusema hakuwa anatumia taulo jilo katika uchawi bali alikuwa akiandika maneno ya biblia katika taulo hilo.

Ivo amekiri kwamba kuelekea katika mchezo huu Simba wanaonekana kuwa na kikosi kizuri zaidi kwani first eleven yao inaonekana kukamilika sana pamoja na wachezaji wa akiba kuliko kikosi cha Yanga.

Meli zakwama Bandarini Kutokana na Utata wa Kodi

$
0
0
KAMATI ya Bunge, Viwanda, Biashara na Mazingira imesema meli mbili za mafuta ghafi zimekwama katika bandari ya Dar es Salaam kwa zaidi ya wiki mbili sasa kutokana na utata wa kodi inayotakiwa kulipwa.

Kufuatia hali hiyo, Serikali imeagizwa kulitafutia ufumbuzi suala hilo kwa kuwa linaweza kusababisha uhaba wa bidhaa zingine zinazotokana na mafuta hayo.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Suleiman Sadiq Murad, katika semina ya kuwajengea uwezo wabunge kuhusu utendaji kazi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) na Tume ya Ushindani (FCC).

Murad alisema kuna meli mbili zipo bandarini zimeleta mafuta hayo na kwamba Mkemia Mkuu, TBS wametoa cheti) kwamba ni ‘mafuta ghafi, lakini Mamlaka ya Mapato (TRA) imekataa, ikisema sio mafuta ghafi.

“Meli zile zimekaa bandarini, kwa sasa zina zaidi ya wiki mbili, meli moja ina tani 30,000 na nyingine ina tani 31,000,” alisema.

“Sasa katika hali kama hii inapotokea jambo la namna hii hivi kuna mawasiliano gani kati ya TBS na TRA kuhakikisha kwamba mizigo ile ambayo nyinyi wenyewe mmekagua na mnasema mzigo huu ni Crude Oil (mafuta ghafi) wakati TRA inasema Semi-Refined (yaliyosafishwa kidogo)?” alihoji Mwenyekiti huyo.

Alitoa tahadhari kwa serikali kuwa mafuta ya kula yameanza kupanda bei kwa sababu mafuta ghafi yaliyoko nchini yanatumika na viwanda havitakuwa na malighafi tena ya mafuta ghafi.

“Bunge limepitisha crude oil itatozwa asilimia 10 na semi- refined asilimia 25 sasa yule wa TBS anasema hii ni crude ilipiwe asilimia 10, TRA anasema ilipiwe asilimia 25,” alisema.

Mwenyekiti huyo alisema kuna tatizo na lipo bandarini na kumuomba Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Stella Manyanya, aliyekuwapo katika kikao hicho kwenda kulitafutia ufumbuzi.

“Naibu naomba ulichukue na mimi nitakaa na Kamati tuzungumze kwa kina kwa kuwa sisi tuna wajibu wa kushauri na kuisaidia serikali,” alisema.

“Eneo hili lina utata kidogo, tunaomba muangalie mnawezaje kulitatua kwa kuwa meli hizo mbili pale zinashindwa kushusha mafuta kwa sababu wenye viwanda, TBS wanasema ni crude, lakini TRA wanasema ni semi refined, tunaomba serikali isaidie suala hili,” alisisitiza Murad.

Akizungumzia suala hilo, Manyanya alisema suala la uagizaji mafuta lina uhusiano mkubwa sana na masuala ya kiuchumi katika nchi.

“Kwa vyovyote vile inapotokea jambo kama hili ngazi za maamuzi za juu zitakaa pamoja na kufikia muafaka namna gani ya kulishughulikia kwa manufaa mapana ya nchi yetu,” alisema Manyanya.

Awali, akitoa mada Kaimu Mkurugenzi wa TBS, Tumaini Mtitu, alisema shirika hilo linakabiliwa na upungufu wa vifaa vya kupimia bidhaa kwa sababu ya ufinyu wa nafasi ya maabara 24 na gharama ya kuvinunua.

“Pia kuna changamoto ya uelewa mdogo wa umma na jumuiya ya wafanyabiashara kuhusu umuhimu wa viwango katika kulinda afya na usalama wa walaji na kuongeza uwezo wa kuuza bidhaa zetu nje ya nchi kwa maendeleo ya uchumi wa nchi yetu,” alisema.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Dk. John Mduma, alisema Tume imefanikiwa kukamata na kuteketeza bidhaa bandia za aina mbalimbali zenye thamani ya Sh. bilioni 26 na ziliteketezwa kwa kuzingatia sheria husika na kanuni zake pamoja na taratibu za ulinzi na mazingira.

Mbunge Amtaja Diamond kama Nembo ya Taifa

$
0
0
Mbunge amtaja Diamond kama Nembo ya Taifa By Peter Akaro | April 28, 2018 - 5:54 pm
Spread the love
Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja ameitaka Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kuwatumia wasanii hasa Diamond katika kuitangaza nchini.

Ngeleja ameyasema hayo jana Bungeni wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

“Bongo Flava imetutoa, tunamzungumzia msanii kama Diamond, tunaungana na Watanzania wote kumpongeza kwa hatua aliyofikia ya kutambuliwa kwamba awe miongoni mwa watu waliotunga wimbo maalum kwa ajili ya Kombe la Dunia mwaka huu,” amesema.

“Naamini huko atapoenda kutuwakilisha, naamini Wizara ya Maliasili itam-package kwenda kuitangaza nchi yetu Diamond kwa sababu yeye ni nembo ya Taifa, kwa hiyo ni muhimu kuwa na watu kama hawa katika taifa letu,” amesisitiza.

Diamond kwa kushirikiana na msanii kutoka Marekani, Jason Derulo wameimba wimbo unaokwenda kwa jina la Colours ambao ni maalum kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia 2018 inayotarajiwa kuanza June nchini Urusi.

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo

$
0
0

Mtandao wa Telegram Umetoweka Hewani kwa saa Kadhaa kwa Watumiaji Wengi Duniani

$
0
0

Mtandao wa #Telegram umetoweka hewani kwa saa kadhaa kwa watumiaji wengi duniani
-
Mwanzilishi wake Pavel Durov amekiri kuna tatizo katika miundombinu yao (server)
-
Ni siku chache baada ya mtandao huo kufungiwa na serikali ya Urusi baada ya kukataa kushirikiana na shirika la kijasusi la nchi hiyo lakini bado ukaendelea kupatikana kwa watumiaji nchini humo
-
Telegram umekuwa mtandao mwiba kwa serikali nyingi duniani kufuatia kuweka mazingira magumu kiusalama kwa serikali hizo kuweza kupata taarifa za watumiaji wa mtandao huo.

Okoa Ndoa yako Sasa...Umepungukiwa na Nguvu za Kiume na Unashindwa Kupanda Mlima Vizuri

$
0
0

OKOA NDOA YAKO SASA : JE UMEPUNGUKIWA NA NGUVU ZA KIUME AU UUME WAKO MDOGO AU MPENZI WAKO HAKUTIMIZII UTAKACHO:


Acha kujiona mpweke pale ukutanapo na mpenzi au mke wako kwa sababu ya kutokuwa na nguvu za kiume au Uume wako mdogo

Dawa YA MAPRO POWERA ndio dawa sahihi na tiba tosha kwa sasa Kutibu tatizo na kuponesha kabisa tatizo LA KUWAI KUFIKA KILELENI KABLA MWENZI WAKO BADO AJAKOJOA

KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOA NA MWILI KUCHOKA

UUME KUSINYAA NA KUWA LEGELEGE

KUUMWA NA TUMBO WAKATI UNAPOMALIZA KUFANYA TENDO

Dawa hii utumiwa ata na wazee wenye umri mkubwa na haina madhara yoyote

MAKAKANUA HII NI dawa ya maumbili madogo urefusha na kunenepesha saizi upendayo saiz 5-6-7-8 na unene sm 3-4-5 kwa mini huabiki kwa kuwa na UUME mdogo wai sasa upate tiba sahihi kabisa na ni tofauti na ulizowai kutumia :

Tunarudisha mke au mpenzi ndani ya masaa matatu tu zipo dawa za presha kisukali vidonda vya tumbo korodani iliyovimba dawa za uzazi tunapunguza matiti makubwa kitambi na mwili mkubwa dawa zipo FIKA OFISINI KWANGU MBAGALA ZAKHEMU KWA WATEJA AMBAO AMTAKUWA NA NAFASI YA KUJA OFISINI AU MLIO MKOANI MTALETEWA p

Piga simu 0743362017 au 0789234653

DR AGU

Hivi ndio Vikosi vya Simba SC na Yanga SC

$
0
0
Ikiwa ni masaa tu yanasubiriwa kuanza kwa mtanange wa mechi kati ya klabu ya Simba na Yanga kunako dimba la Uwanja wa Taifa, tayari vikosi vya timu zote mbili vimeshatangazwa.



Yanga hao watawakosa wachezaji wao muhimu kama Amis Tambwe na Donald Ngoma ambao wote ni majeruhi huku Simba ikiwa na wachezaji wake wote muhimu ambapo mashambulizi yataongozwa na Emmanuel Okwi na John Bocco.

Serikali yachukizwa na baadhi ya makampuni yanayowatumia vibaya Wasanii

$
0
0
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeumizwa vikali na baadhi ya makampuni yanayowatumia vibaya wasanii wa muziki na waigizaji wa filamu kwenye matangazo yao kwa kuingia nao mikataba mibovu ambayo haina faida kwa watu hao.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe juzi bungeni wakati akihitimisha mjadala wa makadirio ya bajeti ya wizara yake.

Waziri Mwakyembe amesema amechukizwa na kitendo cha Mzee Majuto kuomba achangiwe fedha kwa ajili ya matibabu ile hali anaonekana karibia nusu ya mabango yote ya matangazo hapa nchini na kutangaza kiama kwa makampuni na taasisi zinazonyonya wasanii.

“Kwa kweli dhuluma kwa wasanii ilikuwapo kubwa sana kwa kutumia ‘middle men’ (watu wa kati), watu wenye fedha wamechezea sana wasanii wetu. Hili limeanza kubadilika tumeanza kuwa-empower (kuwawezesha) wasanii wetu kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wasitumie middle men,“ameeleza Waziri Mwakyembe.

“Kwa mfano vijana wetu wazuri kama kina Kanumba, amefariki kila mtu anajua ni milionea, hapana.. waliotajirika ni wengine. Leo hii mwanasanaa mzuri mzee majuto anaumwa, anaomba fedha, mimi nachanga kutoka mfuko kwangu, maisha yenyewe unayaelewa waheshimiwa.. lakini nusu ya mabango ya biashara ni ya Mzee Majuto.“amesema Mwakyembe.

Hata hivyo, Waziri Mwakyembe tayari ameshateua kamati maalumu ya wanasheria ambayo itapitia upya mikataba yote ya wasanii na waigizaji kwa kuanzia na Makampuni yaliyowahi kufanya kazi na Mzee Majuto na Marehemu Steven Kanumba.

“Naomba sasa nitumie nafasi hii kueleza kwamba nimeunda Kamati ya wanasheria, tunaanza na kesi ya Mzee Majuto, Mashirika yote na makampuni yote yaliyoingia mikataba na Mzee Majuto tutaipitia upya mikataba hiyo, kama ameonewa ni lazima ilipwe familia yake, tumeshachoka. Na tukishamaliza tunarudi kwa Kanumba na msanii yeyote ambaye anaona aliingia mkataba wa kipumbavu aje atuone.“amemaliza Waziri Mwakyembe.

Familia ya Mzee Majuto Jumatano Aprili 25, 2018 ilijitokeza kuomba msaada wa hali na mali kwa Watanzania ili aweze kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Ali Kiba Agoma Katu Katu Kumwalika Diamond Kwenye Harusi yake Inayofanyika Dar Leo

$
0
0

Licha ya habari kusema kuwa Diamond yupo tayari kuhudhuria sherehe ya harusi ya Alikiba Jioni Ya leo hii, lakini upande wa Diamond umesema hajaalikwa. Chanzo kilicho karibu na Alikiba kimeiambia GPL ....
.
“Kiba anaonekana bado hayuko poa na Diamond, kamfanyia mwenzake jambo la kushangaza sana maana huwezi amini hadi dakika hii hajamualika kwenye sherehe yake ya harusi, yaani inaonekana Kiba hayuko tayari kushirikiana na mwenzake maana mara nyingi amekuwa akijishusha lakini hampi ushirikiano,” .
.
Nae Aidan Seif ambaye ni meneja wa Alikiba alipoulizwa na GPL kuhusu issue hiyo amesema
.
“Hadi sasa hatujamualika na kwa kweli sijajua kama tutamualika,” .
.
Hata hivyo mastaa tofauti nchini wamealikwa. Tusubiri na tuone.


TOA MAONI YAKO HAPA TAFADHALI

Jakaya Kikwete Ampongeza Rais Magufuli

$
0
0
Mbunge wa Chalinze kupitia CCM, Mh. Ridhiwani Kikwete ameonesha kuridhishwa na kazi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli hususani katika kuboresha miundombinu nchini.

Ridhiwani ameyasema hayo baada ya kujionea ub ora wa daraja la Kelema wilayani Chemba mkoani Dodoma, alipopita eneo hilo ikiwa ni sehemu ya safari yake kuelekea kwenye maadhimisho ya siku ya Muungano yaliyofanyika jijini humo.

Kupitia mtandao wa Twitter Mh. Ridhiwani ameandika, ''Nikiwa na mke wangu, kuangalia uzuri wa nchi yetu. Hakika ni nchi nzuri yenye kuvutia. Hongera sana Rais wangu @MagufuliJP kwa kusimamia Miundombinu, pia Asante @WorldBankAfrica kwa kusaidia maendeleo''.

Aidha katika ujumbe huo wa Ridhiwani pia ameishukuru Benki ya Dunia kwa misaada inayotoa hususani ujenzi wa barabara ambao ndio umekuwa kipaumbele chake katika nchi zinazoendelea ikizisaidia kwa mikopo ya masharti nafuu.

April 27 Rais Magufuli alizindua barabara ya Kondoa-Babati, yenye urefu wa Km 251. Katika uzinduzi huo aliwataka wananchi kutunza miundombinu hiyo, haswa alama za barabarani kwani hiyo ndio barabara kuu kwa upande wa Kaskazini.

Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images