Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Alikiba Nashukuru kwa Kunialika Nawatakia Maisha Mema- Waziri Ummy Mwalimu

$
0
0
Alikiba Nashukuru kwa Kunialika Nawatakia Maisha Mema- Waziri Ummy Mwalimu
Waziri Ummy amewatakia maisha mema yenye heri, furaha, baraka na maelewano pamoja na wake zao.

“Asanteni sana @OfficialAliKiba na Abdu Kiba kwa kunialika kushiriki nanyi katika Siku yenu. Ninawatakia maisha ya ndoa yenye heri, furaha, baraka na maelewano pamoja na wake zenu Amina na Ruwayda. Hongereni sana🌺,“ ameandika Ummy leo April,30 kupitia mtandao wake wa Kijamii.


Prezzo Amaliza Beef Lake na Jaguar

$
0
0
Prezzo Amaliza Beef Lake na Jaguar
Msanii maarufu kutokea +254 Kenya Prezzo amethibitisha kumaliza beef lake na msanii mwenzake ambaye kwa sasa ni Mbunge katika jimbo la Starehe  Charles Njagua maarufu kama “Jaguar “ na kulithibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

“Kama wengi mnavojua mimi na ndugu yangu @jaguarkenya tulkuwa na friction miaka nenda, miaka rudi ila Mungu alitupatanisha tukaamua kusahau yalio pita na focus kwa ya lio mbele. Iam glad we burried the hatchet now lets put in work my brother Bless up #Rapcellency“

Aslay Afunguka Kifo cha Masogange Kilivyozima Ngoma Yake

$
0
0
Aslay Afunguka Kifo cha Masogange Kilivyozima Ngoma Yake
Msanii wa muziki Bongo, Aslay amesema ngoma yake ya mwisho kutoa ‘Kwa Raha’ licha kuendelea kufanya vizuri imekumbana na misukosuko.

Muimbaji huyo amesema ngoma hiyo aliitoa kama zawadi kwa mashabiki wake kwani ngoma yake ya mwisho kutoa rasmi ni Nibebe mara baada ya kubadilisha mfumo wake wa kutoa ngoma.

“Kwa Raha nilitoa kama zawadi kwa sababu kuna ngoma inakuja kuitoa tena baadaye ila nasema ni ngoma yangu naipenda na namshukuru Mwenyenzi Mungu imeenda japo kuwa hapa kati imekutana misukosuko, Agness amefariki, kuna vitu kibao vimetokea lakini nashukuru ngoma hivyo hivyo inaenda,” Aslay ameiambia Bongo5.

Ngoma ya Kwa Raha, Aslay aliitoa April 17, 2018, ngoma hiyo ambayo ni ya pili kwa yeye kutoa kwa mwaka huu hadi sasa ina views 481,993 katika mtandao wa YouTube.

John Heche Afunguka Kuhusu Mazishi ya Mdogo Wake

$
0
0
John Heche Afunguka Kuhusu Mazishi ya Mdogo Wake
Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche ambaye pia ni kaka wa marehemu Chacha Heche Suguta, amesema kwamba mpaka sasa hawajaamua juu ya mazishi ya mdogo wao, ambaye aliuawa na Polisi .
Akizungumza na www.eatv.tv. Mheshimiwa Heche amesema kwa sasa wapo kwenye kikao cha familia wakijadili juu ya suala hilo, na watakapopata suluhu ya kuzika ama la, wataujulisha umma.

Chacha Suguta aliuawa Ijumaa ya April 27 kwa kuchomwa kisu na polisi wa kituo cha Sirari, waliokuwa wamemkamata baada ya kumkuta bar akinywa pombe.

Haji Manara Atoa Kali Amkaribisha Msemaji wa Yanga Mjini "Njoo Nikupe Elimu Hii"

$
0
0
Haji Manara Atoa Kali Amkaribisha Msemaji wa Yanga Mjini "Njoo Nikupe Elimu Hii"
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji Manara amemkaribisha mjini Msemaji wa  Klabu ya  Young Africans, (Yanga)  Dismas Ten  kwa kumwambia anamkaribisha kumpatia elimu juu ya kazi anayoifanya.


Manara  ametoa kauli hiyo ya kumkaribiisha mjini Msemaji huyo wa Yanga baada ya Klabu yake kuifunga Yanga siku ya jana ambapo amesema alimuweka kiporo siku nyingi na kwamba alikuwa akisubiri siku ya kumpa majibu kutoka na kile achokiita mafumbo kutoka kwa Ten.

"Bro wewe bado sana..unatumia lugha za mafumbo ambazo haziisaidii klabu..huna hamasa na hutoi taarifa kiweledi na kwa matakwa ya sasa ya soka na soko..njoo nikupe elimu hii" Manara.



Ameongeza "Jumatatu iliopita ulisema Yanga lazma watashinda..haya kiko wapi? leo nimeweka picha yako na nakutag ili walau watu wakujue kidogo....Hii ndio Simba bro...okey karibu town".

Askari Aliyemuua Mdogo wa John Heche Apandishwa Kizimbani

$
0
0
Askari Aliyemuua Mdogo wa John Heche Apandishwa Kizimbani
Askari polisi E. 1156 William Marwa amefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu mkazi wilaya ya Tarime, akikabiliwa na shtaka la mauaji ya Suguta Chacha ambaye ni mdogo wa Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

Mshtakiwa huyo amesomewa kesi ya mauaji namba, PI 76/2018 mbele ya Hakimu A.R. Kahimba leo Aprili 30.

Askari huyo anayedaiwa kutenda kosa hilo Aprili 27 hakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Serikali Yapiga Marufuku Makanisa Yanayofanya Maombi Usiku

$
0
0
Serikali Yapiga Marufuku Makanisa Yanayofanya Maombi Usiku
Makanisa ambayo yanatoa huduma ya maombi nyakati za usiku yamepigwa marufuku na serikali nchini Kenya kufanya hivyo.



Serikali katika Kaunti ya Narok imesema kuwa maombi hayo yanapelekea mimba za utotoni kuongezeka wengi wao wakiwa ni wanafunzi.

Amri hiyo imetolewa na Kamishna wa Kaunti ya Narok, George Natembeya Ijumaa ya wiki iliyopota. Ambapo amesema kwa mujibu wa takwimu za Kaunti hiyo zinaonesha wastani wa wanafunzi 15 wanapata mimba kwenye kila shule katika kaunti hiyo.

Natembeya amesema kuanzia mwezi Machi hadi Aprili tayari wanafunzi 17 wamepata ujauzito katika shule ya wasichana ya Suswa, hii ni kwa mujibu wa taratibu za kuwapima mimba kila baada ya miezi miwili.

Kichuya Amtolea Povu Zito Yondani Baada ya Kumtemea Mate Asante Kwasi

$
0
0
Kichuya Amtolea Povu Zito Yondani Baada ya Kumtemea Mate Asante Kwasi
Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Shiza Kichuya, amezungumzia kitendo cha beki wa Yanga, kelvin Yondani kumtemea mate mchezaji wa Simba Asante Kwasi akieleza kuwa ni cha kukemewa.

Kichuya ameandika ujumbe mfupi kupitia Instagram unaoonesha kuchukizwa na kitendo hicho alichokifaya Yondani jana katika mchezo wa ligi ambao Simba walishinda kwa bao 1-0.

Kichuya ameandika kuwa tabia hiyo kwa wacheza haipendezi na ni ya kishamba hivyo inapaswa isiendelee kufanyika kwasbabu kuna maisha baada ya mpira.

"Mpira siyo vita, kumtemea mwenziyo mate ni kukosa ustaarabu na utu, tukemee hii tabia na tuache ushamba, kuna maisha baada ya mpira" ameandika Kichuya.


Alikiba Akaribishwa Rasmi Katika Umiliki wa Kinywaji cha Mofaya

$
0
0
Alikiba Akaribishwa Rasmi Katika Umiliki wa Kinywaji cha Mafaya
Siku ya April 29, 2018 msanii Alikiba alitambulisha kinywaji kipya ambacho ni energy Drink walichokipa jina la Mofaya Energy Drink katika sherehe ya harusi yake na mdogo wake Abdukiba katika ukumbi wa Serena Hotel iliyopo Jijini Dar Es Salaam.

Sasa baada ya Alikiba kukitambulisha kinywaji hicho, leo April 30, 2018 kupitia ukurasa wa Instagram wa kinywaji hicho cha Mofaya energy Drink wamepost picha ikimuonesha Alikiba akikaribishwa rasmi katika umiliki wa kinywaji hicho huku wakiambatanisha na ujumbe huu..

..>>>“We welcome our new boss to the winning team @officialalikiba . Welcome sir we are honored to have you on board. We welcome our new owner Mr @officialalikiba who joins us as a new shareholder and will be heading the East African team.” – Mofaya

Prof Tibaijuka- Hata Sisi Tuliosingiziwa Kuna Siku Watakuja Kujua Ukweli

$
0
0
Prof Tibaijuka- Hata Sisi Tuliosingiziwa Kuna Siku Watakuja Kujua Ukweli
Ikiwa zimepita siku kadhaa tangu kufariki kwa aliyewahi kuwa mke wa Raisi wa kwanza wa Afrika Kusini Winnie Mandela, Mbunge wa Muleba kusini Prof Anna Tibaijuka  ameonesha kukerwa na baadhi baadhi na tuhuma alizowahi kupewa mwanaharakati huyo ikiwemo kuua.

“Sasa hivi Winnie Mandela ndio anatambuliwa kwamba aliweka mchango mkubwa, kwanini wakati wa uhai wake alifanyiwa kila hila na kusingiziwa? Mimi kusingiziwa nakujua…! wanasema aisifiaye mvua imemnyea”

“Winnie Mandela alisingiziwa mambo makubwa kwamba aliua mototo lakini leo wanasema ilikuwa dili tu kumchafua Yule mama. Hii inatupa moyo hata sisi ambao tumesingiziwa mambo kwamba kuna siku watu watakuja kujua ukweli uko wapi na watabaki kushangaa ” –Prof Anna Tibaijuka

Mbunge Ataka Walimu Wapenda Ngono Kulipuliwa Bungeni

$
0
0
Mbunge Ataka Walimu Wapenda Ngono Kulipuliwa Bungeni
Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga amelitaarifu bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, juu ya vitendo vinavyofanywa na baadhi ya walimu wa vyuo vikuu hapa nchini, vya kufelisha wanafunzi wa kike kwa makusudi.


Akichangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Elimu na , Goodluck Mlinga amesema walimu hao ambao wanajifanya ni vidume vya mbegu, hufelisha wanafunzi wa kike ili wawape rushwa ya ngono, kuweza kuwawekea maksi za ufaulu.

“Kumekuwa na tatizo la vyo vikuu, wanafunzi wetu wa kike wanapata shida mno, katika vyuo vyetu vikuu kuna walimu wanajulikana kabisa kuwa hawa walimu ni madume ya mbegu, wanafelisha wanafunzi wa kike, wanataka wawape rushwa za mapenzi ndio wawafaulishe”, amesema Goodluck Mlinga

Pia Mheshimiwa Mlinga amesema yupo tayari kupeleka majina ya walimu hao ambao wapo vyuo vyote nchini kwa Waziri wa Elimu, ili waweze kuchukuliwa hatua stahiki.

“Mheshimiwa Waziri nitashirikiana na wewe kama utapenda unipe ushirikiano, nitakuletea majina ya vyuo vikuu vyote Tanzania, ya walimu ambao madume ya mbegu kazi yao ni kufelisha wanafunzi na kutaka rushwa za ngono”, amesema Mheshimiwa Mlinga.

Mambo ni Hivi Chidd Benzi Aamua Kuokoka..... Hivi Ndivyo Alivyosheherekea Birthday Yake Kanisani

$
0
0
Mambo ni Hivi Chidd Benzi Aamua Kuokoka..... Hivi Ndivyo Alivyosheherekea Birthday Yake Kanisani
Mwanamuziki wa hip hop bongo mwenye sauti ya kipee Rashid Makwilo maarufu kama Chid Benz, amefunguka juu ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kanisani, na kuwepo kwa tetesi za kuokoa.

Akizungumza na www.eatv.tv Chid Benz amesema kwamba alihudhuria kanisani hapo kwa sababu alialikwa, na sio kuokoka kama wengi wanavyodhani.

“Imani ni kitu fulani chepesi sana ingawa ni kigumu sana, mimi nilialikwa pale kama mgeni rasmi, kulikuwa kuna wabunge, wajumbe wa serikali,  lakini mimi nilialikwa nisingeweza kukataa, tena nikaona ni bahati ni siku yangu ya kuzaliwa, nikaona kwa nini nisende nikasikiliza nikaungana nao, mimi ni Rashid Abdala Makwilo, sijachange wala sijaongea kwamba  nimeokoka”, amesema Chid Benz

Chid ameendelea kwa kusema kwamba....”sina mpango huo wa kuokoka,  naishi katika misingi ambayo nawezakufuata imani yoyote jinsi inayonituma na kuheshimu dini nyingine, sio vibaya”.

Licha ya kuhudhuria kanisani hivi karibuni Chid Benz alionekana akiwa jukwaani na wanamuziki wa nyimbo za Injili, akiwemo Bony Mwaitege.

Kimenuka Yanga Wataka Uchaguzi wa Viongozi Ufanyike

$
0
0
Kimenuka Yanga Wataka Uchaguzi wa Viongozi Ufanyike
Mara baada ya jana Yanga kupoteza mchezo wake kwa kufungwa bao 1-0 na wapinzani wao Simba SC, Uongozi wa Tawi la Umoja ya timu hiyo wameomba kufanyike uchaguzi wa haraka ili kuweza kuwa na viongozi ambao wataweza kuipeleka Yanga kufanya vizuri katika mashindano yaliyopo mbele yao.


Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Tawi la Umoja la Klabu ya Mabingwa Watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, Waziri Jitu na kusema kwa sasa hawana viongozi kwa mujibu wa katiba na wanasikitishwa na hali halisi iliyo ndani ya klabu hiyo kwani hawana imani na viongozi waliomadarakani kwa sasa kwani hata matokeo ya jana Aprili 29, 2018 yamechangiwa na wao.

"Viongozi waliopo madarakani bado hawawezi kufanya uchaguzi, sasa sisi tunachoomba ni kwamba viongozi waliopo madarakani hapa huu ndio uwezo wao na wanayanga tutulie kwa sababu sisi tunadai uchaguzi na serikali wanajua kwamba Yanga haina viongozi kwa mujibu wa katiba yetu, tunadai uchaguzi", amesema Waziri Jitu.

Aidha, Jitu amewaomba wanachama kuendelea kutulia ili kutokuwachanganya wachezaji ambao wapo katika maandalizi mazito ya mashindano ya kimataifa kwa sasa.

Kwa upande mwingine, Jitu amesema endapo viongozi waliopo madarakani wangekubali kufanya uchaguzi mapema basi katika mechi ya jana wangekuwa na uwezo wa kuwafunga Simba kutokana na Mwenyekiti wanaomuhitaji kuwa na mapenzi ya dhati na klabu.

Chadema Yakanusha Haya Kuhusu Tundu Lissu

$
0
0
Chadema Yakanusha Haya Kuhusu Tundu Lissu
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kimekanusha taarifa zinazoendelea mitandaoni kuhusu uwezekano wa kurejea nchini kwa Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho, Tundu Lissu kutokea Ubelgiji alipokuwa akipatiwa matibabu tangu mapema Januari mwaka huu.

Kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano CHADEMA, Ndg. Tumaini Makene amesema kwamba kupitia mitandaoni mapema leo kumekuwa na taarifa za kwamba Lissu anatarajiwa kurejea nyumbani Tanzania wakati wowote kuanzia juzi, kwamba amemaliza matibabu yake kitu ambacho sicho cha kweli na kimezua taharuki.

Katika taarifa yake Ndg. Makene amesema kwamba Mwanasheria huyo ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, hajazungumza na mwandishi wa habari yeyote juu ya kurejea kwake nyumbani kwa sababu zilizo wazi kabisa kuwa bado hajapona na anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mwingine mwisho wiki hii au wiki ijayo.

Hata hivyo chama hicho kimetoa wito kwa na wanachama na Watanzania wote wenye mapenzi mema kutokana na kuguswa na uzito wa masahibu yaliyompata Lissu wameendelea kuguswa na kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya matibabu na hali ya afya yake kupuuza taarifa hizo.

Tundu Lissu yupo nchini Ubelgiji akipatiwa awamu ya tatu ya matibabu baada ya kumaliza matibabu nchini Kenya mwezi Januari ambapo alikuwepo huko kwa takribani miezi minne ambapo alikuwa akiuguza majeraha ya risasi.

Mbunge huyo machachari alipigwa risasi zilizokadiriwa 37 nje ya makazi yake huko Jijini Dodoma majira ya saa 7 mchana na watu wasiojulikana wakati alipokuwa akitoka kwenye majukumu yake ya kibunge.

Download Hapa Application Mpya ya Udaku Special Uweze Soma Vimbwanga na Udaku Mtaani Kila Siku

$
0
0
Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Upya Application yetu ya UDAKU SPECIAL Maana ile ya Zamani Tutaifuta.

Kuna Marekebisho Makubwa tumeyafanya ikiwa na tatizo la Notification kutatuliwa

NB: App mpya ina Icon Nyekundu

 Bonyeza Hapa Chini Kuinstall Upya:


==>>Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>> 

MKE Alininyanyasa Sana Nilipofukuzwa Kazi, MUNGU Ameniona, Sasa Yamegeuka

$
0
0
Siku moja nisiyopenda kuikumbuka nilitwa ofisini kwa bosi wangu na kukabidhiwa barua ya kufukuzwa kazi
Hiyo ilikua ni baada ya uchunguzi wa miezi kdhaa wa kosa nililokua nimelifanya bahati mbaya. Miezi mitatu nyuma nilimuingizia pesa mteja kimakosa kwenye akaunti yake kiasi cha million mia tatu na hamsini ambazo alitakiwa kuwekewa Mteja mwingine halali kupata pesa hizo.

Kama humu ndani Kuna banker ataelewa nachokisema, kwamba makosa kama haya benki ni kawaida sana. Ukigundua kosa kama hili unawahi una reverse hiyo entry una m-credit anaetakiwa shida ni kama uliemwekea kimakosa akawahi kuzichukua ndipo yanakukuta yaliyonikuta mimi.

Baada ya kufukuzwa kazi mke wangu alibadilika kabisa
Nilishuhudia yafuatayo:-

(1) Alitamka mimi ni mjinga ndio maana nimefukuzwa kazi.

(2) Chake kikawa chake tu.

(3) Akawa anawaambia wazi watoto kuwa kitu fulani kimenunuliwa na yeye na sio mimi.

(4) Muda wa kurudi home ukabadilika sasa anarudi usiku mwingi, nampa kipigo cha nguvu anazira na kukimbilia kwao, kwenye usuluhishi anawaambia wasuluhishi kwamba mimi namuonea wivu kwa kuwa ana kazi mimi sina.

(5) Niliuza Gari zangu mbili ili nipate mtaji wa kufanya biashara hivyo nikawa sina Gari nilijua maadam wife ana Gari tutatumia wote maana hata yeye wakati hana Gari alikua akitumia magari yangu.

Kinyume na matarajio hakutaka kabisa niguse Gari lake mimi nikawa mtu wa miguu.Majirani wakawa wanashangaa mfumo wetu wa maisha.

(6) Life yetu ya bedroom ikawa imekufa no intimacy no love making nothing. Alianza kidogo kidogo leo mara aseme anaumwa, kesho kachoka, hadi mwezi unaisha. Nikaamua isiwe tabu nikaacha kuulizia tena, nae akawa amepotezea moja kwa moja.

Hata wazazi wangu aliwa mistreat sana wakawa hawaji tena kwangu, mama yangu akawa ananitumia vitu kwa njia basi kutoka nyumbani kama mchele, maharage, unga na kadhalika ili na mm nionekane nachangia.Wakuu siku ya kufa nyani miti yote huteleza. Kila nilichojaribu kukifanya ili nijinasue kinakwama, nakuta mtaji wote unakata naanza moja.Ilikatika miaka minne nikiwa kwenye hali hii maana nilipata matatizo 2010. Mwaka Jana kuna Dada mmoja tulisoma wote primary school akaamua kunisaidia, huyu dada tulikutana Posta accidentally tukapeana contact
mimi nilishamsahau ila yeye alinikumbuka.

Baadae akaniunganisha na mumewe ambae ni HR manager kwenye shirika fulani, nikamwelezea ukweli wote na akaniingiza kaziniWife sikumwambia kuwa nimepata kazi akaanza kuona nakuja na mahitaji ndani, nikawa naondoka zangu alfajiri narudi usiku mwingi. Nikaita mafundi wakabomoa ukuta wote wa fensi uliokua umeoza waliiba sana cement wakati wa ujenzi ukajengwa upya, vitu vyote vilivyochoka ndani nikabadilisha. Wife alishangaa sana ila akashindwa kuniuliza maana hadi hapo tulikua hatuongeleshani zaidi ya salam za asubuhi na jioni tu basi.

Wana jf siwezi kuwaficha sehemu niliyopata naingiza hela Mara kumi ya ile kazi yangu ya benki, hii sikutokana na mshahara bali njia mbali mbali katikati ya mwezi kitengo chetu tupo wanne,hali ikiwa nzuri huwa tunagawana hadi laki mbili kila siku, kama hali ni mbaya tunagawana laki moja kwa siku hii ni mbali na ile tunayogawana mwisho wa mwezi kama million 3 each person mshahara ni mdogo tu ni laki saba tu kwa mwezi.Maana mshikaji alisema anaweza kuniingiza kazini ila kama mfanyakazi wa kawaida kwa kuwa benki nilifukuzwa hakukua na reference wala background check so nikaamua kufuta kwenye CV kuwa nilifanya bank.

Nimeanza mchakato wa talaka kupitia mwanasheria mmoja rafiki yangu, mwezi January mwaka huu amemwandikia barua ya kumtaarifu uamuzi huo na copy Ustawi wa jamii pia, baadae tutafungua shauri la talaka.Kinyume na matarajio yangu wife kwa kuwa alishañichoka na hakuna kinachoendelea kati yetu nilijua angekubali tu. Cha ajabu hivi sasa kupitia wazee wake wameniita kikao zaidi ya Mara 6 sasa ili tusuluhishe tofauti zetuKawa mpole sana, alidhan nitaendelea kuteseka milele

Wakuu sasa sipo nyumbani kwa hasira ya mambo aliyonitendea hivi sasa sipo nyumbani nimepanga upande wa nyumba nimeanza ujenzi ili nihamie. Kila siku lazima nipite kwa watoto niwaone ndo niondoke. Nimesimama njia panda, mm binafsi nilishaamua simtaki tena huyu mwanamke ila wazee na viongozi wa dini tunakoabudu wanasema turudiane juzi mke wangu alinipigia magoti tukiwa kikaoni kwamba nimsamehe, nifute kusudio la kuomba talaka mahakamani. Wazazi wangu hawataki kusikia kabisa neno msamahakwa matendo aliyotufanyia.


NB: Nimetaja kipato ili kuwapa mwanga na uelewa wa tatizo isichukuliwe vinginevyo

Nimesikia amepata matatizo kazini ila sina uhakika na taarifa hizo

Naomba ushauri wenu

By Christo devries

Kwanini Mabinti wa Kitanga Wanagombaniwa?

$
0
0
Jamani hivi Tanga Kunani? Toka Nimekua na Kubalaa nasikia tu kuwa ukipata Mwanamke wa Kitanga Unasuki na wengine wanasema eti Mwanaume Ukienda Tanga Hauwezi rudi Siku hiyo hiyo lazima ulale ...Najiuliza Hivi Mabinti wa Kitanga wana nini ? Huku Mtaani kwetu wanagombaniwa kama Njungu.....Tufahamisheni jamani Wanaojua

“Sijafurahishwa na ushindi wa goli moja” Mgosi alitaka Yanga wafungwe ngapi?

$
0
0
Wanasema ushindi ni ushindi haijalihi ni wa aina gani lakini legendary wa Simba Mussa Hassan Mgosi kwa upande wake anasema hajafurahia Simba kupata ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya Yanga.

Mgosi ambaye amewahi kuitumikia Simba kwa nyakati tofauti kama mchezaji na baadae akiwa meneja anasema, ni jambo jema Simba imepata pointi tatu lakini anaamini timu yake ilikuwa na uwezo wa kufunga goli zaidi ya moja.

“Yanga walitakiwa wapigwe goli sita na kuendea kwa sababu walikuja kutafuta sare wakawa wanaupoza mchezo lakini Simba wangecheza kwa speed yao ileile tulikuwa tunawafunga nyingi”-Mussa Mgosi.

Chid Benz Azikana Taarifa za kuokoka, ‘Nilialikwa Kama Mgeni Rasmi’

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo, Chid Benz amefunguka ukweli wa taarifa zilizodai kuwa ameamua kuokoka.

Taarifa hizo zimeibuka mara baada ya kuoneka katika moja ya makanisa, pia akiwa na muimbaji wa nyimbo za Injili, Bony Mwaitege.

Rapper huyo akizungumza na EATV amesema alialikwa kanisani hapo kama mgeni rasmi wa shughuli iliyokuwa ikiendelea na hakuna zaidi ya hapo.

“Nilialikwa pale kama mgeni rasmi, kulikuwa kuna wabunge, wajumbe wa serikali, lakini mimi nilialikwa nisingeweza kukataa, tena nikaona ni bahati ni siku yangu ya kuzaliwa, nikaona kwa nini nisende nikasikiliza nikaungana nao, mimi ni Rashid Abdala Makwilo, sijabadilisha,” amesema Chidi Benz.

Tangu July, 2017 Chidi Benz alipotoa ngoma inayokwenda kwa jina Muda ambayo alimshirikisha Q Chillah hajatoa ngoma yoyote zaidi ya kugonga vichwa vya habari kwa matukio mbali mbali.

Mambo Ambayo Wanaume Wanakosea Wakati wa Kutongoza Mwanamke

$
0
0
1.PAPARA
wanaume wengi tumekuwa na haraka sana tunapokuwa tukitaka kuaproach hali inayomfanya mwanamke akuwekee ugumu.mfano umekutana na dada mzuri mmesalimiana hapo hapo unamuomba namba yake.mjomba hata akikupa ujue utasumbuka sana kumpata coz atakufikiria sana juu ya uharaka wako.
2.KUJIFAKE
wanaume wengi tumekuwa tukijipandisha au kujionyesha tofauti na hali zetu.ukiwa unaaproach jaribu kuwa real.huwezi kumwambia mdada unafanya kazi benki afu uko na techno
3.KUTOSOMA MOOD YA MWANAMKE
unapomuaproach mwanamke lazma usome mood yake coz sometime unaweza kutoswa coz hujamsoma mwanamke.unamtongozaje mwanamke asubuhi?,,
4.KUMPONDA UR EX LOVER
mwanamke anakuuliza kwanini uko single,unaanza kumponda ex wako kwa maneno ya kashfa hali kama hii inaweza kumtisha kisaikolojia umtongozae.
5.KULALAMIKA
Unamtongoza mwanamke huku unalalamika juu ya mapenzi oooh mara sijawahi kupendwa.mjomba hapo unaonyesha udhaifu wako.UKITULIA NA KUMTONGOZA MWANAMKE BILA KUYATENDA HAYA MBNA UTAMPATA KILA UMTAKAE
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images