Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live

Lionel Messi na Mohamed Salah vita yao bado ngumu

0
0
Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona na Timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi na mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah bado wapo kwenye vita kali ya kufukuzia kiatu cha dhahabu barani Ulaya.
 
Messi kwenye mchezo wa jana alishinda goli 3 kati ya magoli 4-2 waliyoshinda dhidi ya klabu ya Deportivo La Coruna.

Kwa ushindi huo Messi anafikisha idadi ya magoli (32) ya La Liga akiwa amemtangulia Mohamed Salah kwa goli moja (31).

Ingawaje Messi anamuongoza Salah lakini bado pia ana mechi nne mkononi za Ligi wakati Mohamed Salah yeye amebakiza mechi mbili za EPL.

Hata hivyo, wakati macho ya wapenzi wengi wa soka duniani wakiangalia mchuano huo wa watu wawili kwa msimu huu, bado kuna wachezaji wengine hatari zaidi ambao wanaweza wakaushangaza ulimwengu wa soka kwa msimu huu nao ni Ciro Immobile kutoka klabu ya SS Lazio na Robert Lewandowski wa Bayern Munich.

Immobile mpaka sasa ametupia magoli 29 na bado ana mechi nne mkononi huku Lewandowski akiwa na magoli 28 na mechi mbili mkononi.

Msimu uliopita 2016/17 kiatu cha dhahabu barani Ulaya kilichukuliwa na Messi ambapo alitupia magoli 37 kati ya mechi 29 alizocheza La Liga .

Kiatu cha dhahabu barani Ulaya kinatolewa kwa mchezaji mwenye magoli mengi zaidi kuliko mchezaji yoyote kwenye Ligi zote za mpira wa miguu barani humo.

Je, unadhani mwaka huu kiatu hicho kitachukuliwa nani?

Amuuwa Mpenzi wake kwa Kumnyonga shingo, Mwanza

0
0

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia kijana aliyefahamika kwa jina la Nicholas Light (25) mkazi wa Mtaa wa Mahama Ilemela kwa kunyonga mpenzi wake Victoria Swai (26).


Inadaiwa kijana huyo alifanya mauaji hayo kwa kumkaba shingo mpenzi wake huyo hali iliyopelekea kukosa hewa na baadae kufariki dunia.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kudai tukio hilo limetokea katika jengo la Ekacliff ofisi ya Kilimanjaro Avitaion.

Katika tukio hilo polisi walifanya uchunguzi katika nyumba alipokuwa akiishi marehemu na mpenzi wake na kumkuta mtuhumiwa akiwa amejificha juu ya dari ya nyumba.

Chanzo cha mauaji hayo kinadaiwa kuwa ni  wivu wa kimapenzi ambapo mtuhumiwa huyo  alikuwa akimtuhumu marehemu kuwa alikuwa akimsaliti kimapenzi ambapo  mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi, pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.

Pedeshee Jack Pemba Asusa Magari yake

0
0
BAADA ya kufunguliwa kesi na tajiri mwenzake, Godfrey Kirumira wa nchini Uganda, Pedeshee Jack Marshal Pemba, ametikisa baada ya kuibuka kwa stori kwamba kumbe aliyasusa magari yake matatu ya kifahari yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.2 za Uganda.


 Kufuatia habari hizo na nyinginezo huku Jack akihusishwa na video za ngono zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Ijumaa Wikien da lilimtafuta mmoja wa ndugu za tajiri huyo anayejulikana kwa kufanya kufuru ya fedha, Eliudi Pemba ambaye alifunguka kila kitu juu ya sakata hilo.


 Eliudi aliliambia gazeti hili kuwa, ni kweli kwamba, Jack Pemba ambaye anaishi nchini Uganda alimkopa Kirumira kiasi cha dola laki 2 za Kimarekani (zaidi ya shilingi milioni 450 za Kibongo) ambazo mahakama imeamuru kaka yake azilipe, lakini mwenyewe amekataa kwa sababu mdai alivunja makubaliano yao.


 Kufuatia msigano huo, wiki iliyopita mahakama iliagiza kukamatwa kwa Jack Pemba ili amlipe Kirumira shilingi bilioni 1 za Uganda kutokana na kukaa na deni lake kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa Eliudi, Jack Pemba alikopa kiasi hicho cha fedha kutoka kwa Kirumira ambapo alimpa magari yake matatu ya kifahari yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1 za Kitanzania.

Magari yenyewe ni Range Rover lenye pleti namba ya jina la ONLY 1 JP (ikimaanisha kuna Jack Pemba mmoja tu).

Gari hilo linatajwa kuwa na gharama ya dola za Kimarekani 140,000 (zaidi ya shilingi milioni 300 za Kitanzania).

Gari lingine ni Land Cruiser ZX la mwaka 2017 lenye pleti namba ya jina la MR PEMBA ambalo jamaa huyo alilinunua kwa gharama ya dola za Kimarekani 175,000 (karibia shilingi milioni 400 za Kitanzania).

Lingine la kifahari ni Hummer H3 lenye thamani ya dola za Kimarekani 35,000 (zaidi ya shilingi milioni 80 za Kibongo).

Eliudi alisema kuwa, kwa fedha za Uganda, jumla ya magari hayo yana gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 1.2 za Uganda.

“Walikubaliana yale magari yawekwe hadi atakaporejesha mkopo, lakini alishangaa kuyaona yanatumiwa na jamaa huyo na watoto wake kwa ajili ya matanuzi na kuyakodisha kwa maharusi.

“Alichokisema Jack ni kwamba Kirumira alivunja makubaliano na magari yake yamechakaa hivyo akamsusia,” alisema Eliudi na kuongeza:

“Baada ya hapo ndipo jamaa akaanza figisufigisu za kumchafua Jack kwa kusambaza video za ngono na msichana wa zamani wa Jack ili ionekane kaka yangu ndiye amefanya hivyo.

“Kiukweli sisi kama familia limetuchukiza na kitendo cha kuchafuliwa kwa ndugu yetu na video za ngono maana Jack ana mke hivyo ilikuwa ni kama kumharibia tu na ameapa hatayachukua hayo magari wala kulipa kiasi hicho cha fedha.”

Mrisho Ngassa Amtetea Yondani Kitendo Cha Kumtemea Mate Mchezaji wa Simba

0
0
Nyota wa zamani wa klabu ya Yanga ambaye kwasasa anachezea Ndanda SC, Mrisho Ngassa, amesema kitendo alichofanya mlinzi wa Yanga Kevin Yondani cha kumtemea mate mlinzi wa kushoto wa Simba Asante Kwasi sio kizuri lakini kilitokana na ukubwa wa mchezo.


Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa 'Instagram' Ngassa ametoa uchambuzi wa baadhi ya matukio ambayo yalitokea katika mchezo huo na kueleza kuwa tukio la Yondani lilitokana na ukubwa wa mchezo ambapo wachezaji hujikuta wakifanya vitu ambavyo hawakutegemea.

''Kweli kitendo ambacho kafanya Yondani sio kizuri lakini angalia mechi ilikuwa ya uzito kiasi gani, hayo katika mpira yapo, haswa mpira wa ushindani kama wa jana'', ameandika.

Kwa upande mwingine Ngassa amezungumzia tukio la Emmanuel Okwi kukabiliana na mlinda mlango wa Yanga Youthe Rostand, kuwa halikuwa la kiungwana kwani alimuumiza golikipa.

''Ukija kwa Okwi kampiga kipa ambae kadaka mpira mfano angemvunja mguu lakini yote ile ni mbinu zakuogopwa uwanjani hicho ndio kiliwapa Simba ushindi kwani kipa alishagongwa akawa anaogopa kwenda'' ameongeza.

Aidha Ngassa amewataka mashabiki kutambua kuwa wao hubaki wanaongea tu kishabiki lakini kwa wachezaji hukutana na kuombana radhi. Pia amewapa hongera Simba kwa ushindi huku akimpa pole Asante Kwasi.

Kutana na Mtaalam wa Matabibu ya nyota za Binadam na Bingwa wa Tiba za Asili Afrika Mashariki.

0
0


Je Wewe ni Mwanasiasi, Mfanyabiashara , Msani, ama mwanafunzi tunazo dawa na pete za bahati zenye uwezo mkubwa wakuyabadilisha maisha yako nakukupatia mafanikio makubwa ndani ya mda mfupi tu.

Kutana na SHABA WA SHABA kutoka Tanga,
Yeye ni mtaalam na mtabibu wa nyota za binadam na bingwa wa tiba za asili Afrika mashariki.
Wasiliana na mtaalam huyu kwani yeye ufaulu pale wote waliko shindwa na pia humaliza kazi zilizo shindikana ama zilizo achwa ndani ya siku1 tu. Sasa amezianza ziyara zake za mikoani na atayatembeleye maeneo mbali mbali ndani na inje ya nchi.

Anatibu magonjwa sugu yanaojulikana nasiojulikana kwakutumia maji, Kioo na mitishamba.
Anazo dawa za mapenzi, kumrudisha alipoteya, kutoa Mikosi, Kutatuwa shida za chumaulete, mvuto wa biashara na sehem za kazi, kusafisha nyota, kurudisha mali zilizo ibiwa, zilizpotea, ama zilizodhulumiwa, kushika wezi na wachawi, kutoa ndagu , Kutoa kinga ya mwili, nyumba, Biashara, kufukuza majini wabaya, Kuuza kwa haraka ( shamba, nyumba, Gari,...), Kesi mahakamani, Kuweka Zindiko ya mwili, nyumba, shamba, Gari, kupata Kazi na kupandishwa cheo, mali na utajiri bila masharti na mengine mengi ya Siri...

Kwa tiba na ushauri wasiliana na ofisi kwa nambari ya simu :
+255 785 358 267 ,
+255 785 358 267

Lissu 'Nimesahau Kutembea', Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya May 1

0
0

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya May 1

Kamati ya Bunge yaipinga serikali kuhamisha walimu

0
0
Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imekosoa utaratibu wa Serikali kuhamisha baadhi ya walimu wa shule za sekondari kufundisha shule za msingi kwa maelezo kuwa kila ngazi ya ualimu ina miongozo na mafunzo yake mahsusi.

Akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kuhusu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mwaka 2018/19 kwa niaba ya mwenyekiti, Peter Serukamba, mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe amesema Serikali inatakiwa kuliangalia suala hilo kwa jicho la pekee.

“Kamati inatambua na kuelewa tatizo la ukosefu wa walimu hasa katika shule za msingi hapa nchini, ila kuchukua walimu wa sekondari kwenda kufundisha shule za msingi si sawa,” amesema Bashe.

Mbunge huyo ameyasema hayo leo Aprili 30 bungeni mjini Dodoma.

“Kumchukua mwalimu wa sekondari kwenda kufundisha shule ya msingi kumepokelewa kwa hisia tofauti miongoni mwa jamii na walimu wenyewe ikiwemo kuhisi kuadhibiwa hivyo kushusha morali ya kufanya kazi.”

Amesema Serikali inapaswa kutazama uamuzi huo kwa jicho la pekee na kufanya uamuzi ulio sahihi kwa mustakabali mzuri wa elimu nchini.

Pia, amesema kamati hiyo ina taarifa kuwa mahitaji ya walimu kwa shule za msingi ni 273,454 lakini walimu waliopo ni 175,946 na hivyo kuwa na upungufu wa walimu 97,508 sawa na asilimia 35.

“Kwa shule za sekondari hasa masomo ya sayansi, mahitaji ni walimu 35,136 lakini waliopo ni 19,285 na hivyo kuwa na upungufu wa walimu 15,851 sawa na asilimia 45.1,” amesema Bashe.

Waziri Kairuki Ataka Bilioni 30 sekta ya Madini, Mafuta zichunguzwe zilipo

0
0
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Leo tarehe 30 Aprili, 2018 Waziri wa Madini, Angellah Kairuki amezindua ripoti ya Nane ya ulinganishi wa mapato ya Serikali na malipo ya kampuni za madini, mafuta na gesi asilia kwa mwaka wa fedha 2015/16 iliyoandaliwa chini ya Mpango wa Uhamasishaji Uwazi katika Mapato ya Madini, Gesi Asilia na Mafuta Tanzania (TEITI) kwa  kushirikiana na Mtaalam Mwelekezi, Boas & Associates na MM Attoneys.

Akizungumza katika uzinduzi wa ripoti hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam na kukutanisha  wawakilishi kutoka Kamati ya TEITI, Wizara ya Madini, makampuni ya mafuta na gesi, Waziri Kairuki amepongeza  Kamati ya TEITI na Sekretarieti kwa mchango wake katika uandaaji wa ripoti hiyo.

Mbali na  Pongezi hizo, Kairuki ameiagiza Kamati ya  TEITI kuongeza nguvu katika kuhakikisha wananchi wanakuwa na uelewa mpana wa umuhimu na wajibu  wa TEITI kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na warsha mbalimbali pamoja na vipindi vya redio na  televisheni.

Amesisitiza kuwa,  kipaumbele kiwekwe kwenye maeneo  yaliyozungukwa na shughuli za utafutaji na uzalishaji wa madini, mafuta na gesi asilia na kupata taarifa ndani ya kipindi cha miezi sita.

Awali akielezea ripoti hiyo,  Kairuki amesema kuwa ripoti hiyo  inahusu tathmini ya mapato ya madini katika kipindi cha kuanzia tarehe 1 Julai, 2015 hadi tarehe 30 Juni, 2016 na kufafanua kuwa jumla ya shilingi 434,627,874,380 zilipokelewa serikalini  kutoka kwenye kampuni 55 za madini, mafuta na gesi asilia zilizoshiriki zoezi la ulinganishi.

Hata hiyo amesema taarifa inaonesha kuwa kampuni zililipa kiasi cha shilingi 465,164,747,725 za kitanzania serikalini na kusababisha tofauti kati ya malipo kuwa ni pungufu ya shilingi 30,536,873,345 za kitanzania chini ya kiasi ambacho Serikali imekiri kupokea.

“ Ni lazima tufahamu ni vipi imejitokeza tofauti hii na ninachukua fursa hii kuelekeza taarifa hii kupelekwa kwa Mkaguzi Mkuu  wa Hesabu za Serikali kwa ajiili ya uchunguzi kama kifungu 18(1) cha Sheria ya TEITI ya mwaka 2015 kinavyotaka,” alisema Waziri Kairuki.

Katika hatua nyingine,  Waziri Kairuki amefafanua kuwa ripoti  imeonesha kuwa sekta ya madini imechangia zaidi kwa asilimia 85 na sekta  ya mafuta na gesi ikionyesha kuchangia asilimia 15 ya mapato ya Serikali chini ya Sekta ya Madini kwa mwaka 2015/16

Akielezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano katika sekta ya madini, Kairuki amesema kuwa ili kuhakikisha madini yanakuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi, Serikali imeanza kuchukua hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kufanya mabadiliko ya Sheria ya Madini pamoja na kanuni zake.

Ametaja hatua nyingine ambayo ni endelevu kuwa ni kufanya tathmini ya jinsi gani nchi  inapata mapato yake kwenye sekta ya madini kutokana na hatua mbalimbali zinazochukuliwa.

Ameendelea kusema kuwa jukumu linafanywa na taasisi mbalimbali  za Serikali lakini TEITI nayo inatekeleza jukumu husika kwa kuhakikisha taarifa za mapato ya madini zinatolewa kwa uwazi kwa wananchi na wadau mbalimbali katika Serikali,  Sekta Binafsi na Mashirika yasiyo ya Kiserikali.

Wakati huo huo akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila amesema kuwa mara baada ya ripoti kuzinduliwa na kukabidhiwa kwa Kamati ya TEITI hatua inayofuatia ni kamati ya TEITI kuwasilisha ripoti hiyo kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili achukue hatua kwenye hoja zilizotokana na ripoti hiyo.

Profesa Msanjila amezitaka kampuni nyingine ambazo hazikushiriki katika kipindi cha ukaguzi kujitokeza katika ukaguzi unaofuata ili  takwimu halisi za mapato zifahamike.

Aidha, ametumia fursa hiyo kukaribisha kampuni nyingine zenye nia ya kuwekeza kwenye sekta ya madini kujitokeza kwa wingi  ili sekta ya madini iwe na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi.

Mbunge Alalamika Kuminywa na Kiti Bungeni

0
0
Katika hatua isiyo ya kawaida leo Bungeni Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ametoa mwongozo akitaka viti vya bungeni kukarabatiwa kwa kuwa viti hivyo ni vibovu na vinawapa shida wabunge.

Salasini ameyasema hayo kwenye kipindi cha Maswali na majibu huku mwongozo wake ukiitaka serikali itoe majibu ni lini viti hivyo vitakarabatiwa ili kuwaondolea adha wabunge wakati wa vikao.

''Mh. Spika viti hivi tunavyokalia havipo kwenye hali nzuri kabisa, vimechakaa na havifanyiwi marekebisho na leo kiti changu kimenifinya makalio. Je ni lini vitafanyiwa ukarabati ?,'' amesema Selasini.

Baada ya kuomba muongozo huo Spika wa Bunge Mh. Job Ngudai amesema kuwa suala hilo limepokelewa na litatolewa ufafanuzi.

Joyce Kiria Alalamika Hadharani Kunyimwa "Dyudyu" Baada ya Kumshauri Mumewe Kuhamia CCM

0
0
Joyce Kiria amefunguka mengi kuhusu mume wake Henry Kileo kupitia Ukurasa wake wa Instagram Baadhi ya mambo aliyosema nimekuwekea hapa chini:



Tazama VIDEO nzima Akifunguka:


Diamond Kama Unataka ndoa, Muoe Hamisa Mobetto

0
0
Vigezo vya Hamisa:
1. Ana umri mzuri kwako.

2. Anakupenda na wala hakupendei hela, coz wenye hela kukuzidi wapo wengi lakini kaamua kuwa na wewe kitambo.

3. Ni mzuri na ana mvuto.

4. Ni mama mwenye malengo ya familia, coz angekuwa mcharuko angetoa mimba, lakini kakubali kulea bila kujali carrier yake ya uanamitindo.

Ushauri wa bure bwana mdogo Diamond.

By Ntemintale

Imefahamika Kumbe Alikiba ni Partner Kwenye Kinywaji cha Mofaya na Sio Balozi

0
0

Jana Palikuwa na Mjadala mkubwa mitandaoni kuhusu Ali Kiba na Kinywaji cha Mofaya alichokizindua tarehe 29 April siku ya Harusi yake Tanzania, Wengi walikuwa wakisema kuwa kinywaji hicho sio cha kwake bali ni cha DJ Mmoja huko South Afrika, lakini ukweli umebainika kuwa ni kweli kinywaji hicho mwanzilishi wake ni DJ Djsbulive kutoka South Afrika lakini kwa sasa amemkaribisha Ali Kiba kuwa Mwenza (Partner) Katika hiyo Biashara ikiwa na maana kuwa amepewa umiliki fulani

DJ Djsbulive Amefunguka haya:

Kutana na Mabingwa wa Tiba Asilia na Tiba Mbadala Wakutatulie Tatizo lako Popote Ulipo

0
0


KUTANA NA MABINGWA HAWA WA TIBA ASILIA NA TIBA MBADALA WAKUTATULIE TATIZO LAKO POPOTE ULIPO AFRICA,ASIA, AMERICA, FALUME ZAKIARABU HUDUMA ZETU ZITAKUFIKIA..... Bi khajat ni mtaalamu wa mambo yamahusiano (MAPENZI) kama umeachwa namume, mpenzi, mchumba, mke, au hajatulia unataka kumtuliza mpenzi wako akupende asikusaliti asitoke nje ya ndoa.... Bi khajati atakurudishia mahusiano yako yaliyo vunjika nakuyafunga yasiteteleke tena... Bi khajati anauwezo wakukupandishia nyota zako hata kama huna bahati yakupendwa kusaminiwa, utaanza kupendwa nawatu wenye pesa matajiri nawatakujali nakukupenda nakutimiziwa ndoto zako.... MAALIMU JUMAA NIBINGWA WA TIBA ASILIA,,, acha kuusononesha moyo wako kw sababu ya ugumu wa maisha.... Jipatie dawa za ngekewa kwenye biashara yako, pete za bahati mvuto wa biashara.. Kupata kazi, ajira nk.... Kama unahisi nyota yako haiko sawa maalimu jumaa atakupandisha nyota yako itang'ala na itafanikisha mambo yako....

PIA TUNATOA UTAJIRI WA MAJINI KWA YEYOTE ANAEHITAJI, Kama unataka utajiri wa pete, au wamajini bila masharti wasiliana nasi kw simu hizo muda wowote popote ulipo ,usisite kupiga simu hata Kama unamambo yako binafsi shida binafsi, maradh, kesi, kazi, biashara, nk. Piga simu ushauli ni bure karibuni sna.... +255 678 857 642 na +255 754 661 565 ...

yote yanawekena inn shaa laaah......

Baada ya Kuachwa na Mkewe Aamua Kujiua

0
0
Baada ya Kuachwa na Mkewe Aamua Kujiua
MWANAMUME mmoja mkazi wa Katoro mkoani Geita aliyetambulika kwa jina la Maganiko Nunda amejiua kwa kunywa sumu kufuatia mgogoro ulioibuka baina yake na mke wake siku hivi karibuni huku chanzo cha mgogoro huo kikidaiwa kuwa ni unywaji wa pombe kupindukia uliosababisha mkewe kumkimbia.



Akisimulia tukio hilo, mtoto wa marehemu amesema baada ya kwenda kumsalimia baba yake (marehemu) alimkuta ameshafariki huku akitokwa na povu mdomoni na puani.

Marehemu aliacha ujumbe wa barua wenye maneno yasemayo kuwa “…Kwa kuwa nimekuwa kero kwa familia yangu nimeamua kujiua…”



Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kutokea kwa kifo hicho japo hakueleza ni aina gani ya sumu ambayo marehemu alitumia kujiua. Jeshi hilo linaendelea na upelelezi wa tukio hilo kabla ya kutoa taarifa kamili kwa umma.





Serengeti Boys Yatua Dar na Kombe Yapewa Mapokezi Makubwa

0
0
Serengeti Boys Yatua Dar na Kombe Yapowa Mapokezi Makubwa
Timu ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys, alfajiri ya May 1 2018 iliwasili Tanzania ikitokea Burundi ilipokuwa inashiriki michuano ya CECAFA U-17 kwa mwaka 2018

Serengeti Boys ambao wametwaa taji la michuano hiyo kwa kuifunga Somalia kwa magoli 2-0 na kutwaa taji hilo, walipokelewa na watu mbalimbali akiwemo waziri wa habari, utamaduni na michezo Dr Harrison Mwakyembe nae alijitokeza kuwapokea.

Sakata la Nondo Kusimamishwa Masomo Latinga Bungeni Wabunge Wacharuka

0
0
Sakata la Nondo Kusimamishwa Masomo Latinga Bungeni Wabunge Wacharuka
Mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali amesema uamuzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) kumsimamisha masomo mwanafunzi wake wa mwaka wa tatu, Abdul Nondo unakitia aibu chuo hicho na ni kinyume na haki za binadamu.

Akizungumza leo Jumatatu Aprili 30, 2018 wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mwaka 2018/19, Bobali amesema sheria iliyotumika kumsimamisha masomo inatakiwa kufutwa.

“Hivi ni wanafunzi wangapi ambao wameshtakiwa na kesi zao zipo mahakamani lakini wanaendelea na masomo. Hili suala la Nondo linakitia aibu chuo pengine watueleze tu kwamba jambo hili ni la kisiasa,” amesema Bobali.

Wakati Bobali akitoa maelezo hayo, mbunge wa Magogoni (CUF), Dk Ally Yusuf Suleiman aliomba taarifa kwa Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge na kubainisha kuwa hata wabunge wapo walioshtakiwa, wengine kufungwa lakini mpaka sasa bado wanaendelea na ubunge wao.

“Napenda kumpa taarifa mzungumzaji (Bobali) kuwa hata wabunge wapo walioshtakiwa lakini mpaka kufungwa lakini bado ni wabunge hadi sasa,”amesema Suleiman.

Nondo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) amesimamishwa masomo kuanzia Machi 26, 2018 kwa barua iliyoandikwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Anangisye, aliyeeleza kuwa amesimamishwa kwa mujibu wa taratibu za chuo hicho.

Nondo alijikuta kwenye misukosuko na vyombo vya dola tangu alipotoweka katika kile kilichoelezwa kuwa ni katika mazingira ya kutatanisha Machi 6 na kuonekana Machi 7 wilayani Mufindi, Iringa.



Mwigizaji wa Filamu za Ngono Amshtaki Trump

0
0
Mwigizaji wa Filamu za Ngono Amshtaki Trump
Mwigizaji wa filamu za ngono Stormy Daniels amemshtaki Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu ujumbe wa Twitter anaodai ni wa kumharibia jina, wakili wake amesema.

Bi Daniels, ambaye jina lake halisi ni Stephanie Clifford, anasema alitishiwa na mwanamume mmoja katika maegesho ya magari mjini Las Vegas na kutakiwa kuacha kuendelea na madai yake kwamba aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Bw Trump.

Rais huyo wa Marekani alipakia kwenye Twitter mchoro wa mwanamume mshukiwa na kisha kuandika "hii ni kazi ya utapeli kabisa".

Wakili wa Bi Daniel aliandika kwenye Twitter kwamba Bw Trump "anafahamu vyema kabisa yaliyotokea".

"Bw Trump alitumia fursa ya mamilioni ya watu katika taifa hili na kimataifa (wanaomfuatilia katika mtandao huo wa kijamii) kutoa taarifa ya uongo yenye lengo la kumshushia hadhi na kumshambulia Bi Clifford," kesi iliyowasilishwa katika mahakama ya dola mjini New York inasema.

Kesi hiyo inasema ujumbe huo wa rais ulikuwa wa kumharibia mtu jina kwani ulimtuhumu Bi Daniels kwa "kutekeleza kosa kubwa" - hususan, la kumtuhumu mtu mwingine kwamba alimtishia.

Bw Trump alikuwa amepakia mtandaoni mapema mwezi huu picha ya mchoro wa mshukiwa huyo na kumweleza kuwa "mwanamume asiyekuwepo".

Mwanamke huyo aliambia kipindi cha CBS News kwamba baada ya kutamatika kwa uhusiano wao, mwanamume mmoja alifika alipokuwa yeye na binti yake katika maegesho hayo ya magari Las Vegas na kumwambia "sahau taarifa hiyo, mwache Donald Trump".


Trump amekana kuwa na ufahamu wowote kumhusu Cohen ambaye hapa anaonekana akiingia mahakamani
Kesi hiyo hata hivyo ilisitishwa kwa siku 90, huku jaji akisema kwamba haki za Bw Cohen zingekuwa hatarini iwapo kesi hiyo ingeendelea akiwa bado anachunguzwa.
Mashtaka Maalum Robert Mueller kuhusu tuhuma kwamba Urusi iliingilia uchaguzi wa urais wa mwaka 2016 na kwamba taifa hilo lilishirikiana na maafisa wa kampeni wa Rais Trump.

Msigwa Awataka Chadema Wasivae Jezi Uwanjani

0
0
Msigwa Awataka Chadema Wasivae Jezi Uwanjani
Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kuwakaribisha wageni wote katika kusherehekea siku ya Mei Mosi ambayo kitaifa inafanyika mkoani Iringa leo na kuwaomba wanachama na wafuasi wa UKAWA wasivae jezi zozote zile uwanjani.


Msigwa amesema hayo leo Mei 1, 2018 na kusema kuwa watu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameichukulia siku hiyo ya wafanyakazi dunia kufanya siasa na kusema wameng'oa bendera za CHADEMA na kuweka bendera za CCM hata kwenye nguzo za umeme kinyume na utaratibu.

"Wenzetu wanatumia sherehe hizi kisiasa kwa kung'oa bendera za CHADEMA na kuweka bendera za CCM hata kwenye nguzo za umeme! Kinyume cha utaratibu, Utadhani ni sherehe ya kuzaliwa kwa CCM. Mji ungepambwa kwa bendera za taifa ingeleta mshikamano na umoja wa Taifa. Kwa bahati mbaya wameashindwa kuona hili. Hata hivyo niwaase wapenzi na wanachama wa CHADEMA na UKAWA! Wasije uwanjani na nembo au bendera za vyama. Tuonyeshe ukomavu na uelewa wa kisiasa" alisema Msigwa

Aidha Mbunge Msigwa amewaomba watu wa Iringa waweze kuwapokea na kuwakarimu vizuri wageni hao ili watamani kurudi tena Iringa ili wakuze uchumi wa Manispaaa hiyo ya Iringa.

Mbali na hilo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ndiye mgeni rasmi katika sherehe hizo hivyo anatarajiwa kuhotubia taifa kutokea Iringa

Polisi Yatoa Ufafanuzi Ripoti ya Uchunguzi wa Kifo cha Masogange

0
0
Polisi Yatoa Ufafanuzi Ripoti ya Uchunguzi wa Kifo cha Masogange
WAKATI kukiwa na shauku kubwa ya kujua sababu za mwili wa marehemu Agness Gerald ‘Masogange’ kufanyiwa uchunguzi wa kipolisi wakati ukiwa Mochwari ya Hospitali ya Muhimbili, Jeshi hilo limefunguka na kutoa ufafanuzi, huku likiwataka Watanzania kuelewa kuwa kufanyia maiti uchunguzi wa kipolisi ni jambo la kawaida.

UCHUNGUZI WA MUHIMBILI

Masogange (28) alifariki dunia Aprili 21, mwaka huu katika Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar na mwili wake kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kuhifadhiwa.

Baadaye Polisi walifika hospitalini hapo na kuufanyia uchunguzi mwili huo hivyo baadhi ya watu waliowasiliana na gazeti hili walikuwa na shauku ya kupata ripoti ya uchunguzi huo.

KIFO CHENYE UTATA?

Kitendo cha Polisi kuufanyia uchunguzi mwili huo kilizua gumzo kwa baadhi ya watu waliofika hospitalini hapo, huku wengi wakihoji mantiki yake, wakiamini kuwa uchunguzi wa maiti hufanyika kwa watu waliokufa vifo vyenye utata.

“Inakuwaje Polisi wanachunguza mwili wa mtu aliyefariki dunia katika mazingira ya kawaida kabisa na hata ripoti za madaktari zinaeleza kuwa kifo hicho hakina utata?” Walisikika baadhi ya watu wakihojiana wenyewe kwa wenyewe.

Hata hivyo, ikiwa sasa zimekatika takribani siku kumi tangu kifo hicho, Polisi ilikuwa haijaweka wazi matokeo ya uchunguzi huo, jambo ambalo limekuwa likiendelea kuzua mjadala mitaani kiasi cha baadhi ya watu kuanza kuhusisha tukio la kupimwa maiti yake na maisha ya marehemu enzi za uhai wake.

KAMANDA ATOA UFAFANUZI

Kufuatia sakata hilo, Ijumaa Wikienda liliamua kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Muliro Jumanne na kumwomba atolee ufafanuzi suala hilo ambapo mazungumzo hayo yalikuwa hivi;

Ijumaa Wikienda: Kamanda habari za kazi? Wakati mwili wa marehemu Masogange ukiwa Muhimbili, kulizuka taharuki baada ya Polisi kuuchukua mwili huo na kwenda kuufanyia uchunguzi. Watu walikuwa wakitamani kujua kwa nini ilikuwa lazima afanyiwe uchunguzi wakati tayari madaktari walieleza kuwa kifo chake ni cha kawaida?

Kamanda Muliro: Mimi naendelea vizuri. Lakini kwa nini iwe ni kifo cha Masogange, wakati suala la kufanyia uchunguzi maiti hufanywa kwa kila mtu? Ukienda pale Muhimbili wakati wote utakuta Polisi wapo wanafanya uchunguzi wa maiti.

Ijumaa Wikienda: Watu wanahoji kwa Masogange kwa sababu wanaamini kuwa kifo chake hakikuwa cha utata. Madaktari walishasema kuwa alikufa kifo cha kawaida, kwa nini afanyiwe tena uchunguzi wakati ripoti ya kifo chake ipo?

Kamanda Muliro: Nasema hiyo ni kazi ya Polisi siku zote. Kifo chochote kinatakiwa kufanyiwa uchunguzi, lakini sasa ninyi (Waandishi) macho yenu yako kwa mastaa tu. Polisi tunafanya uchunguzi hata kwenye vifo ambavyo tunajua kuwa kimetokana na nini.

“Tunachunguza hata waliokufa kwa ajali za pikipiki. Ni utendaji wa kawaida wa Polisi.

Ijumaa Wikienda: Sawa Kamanda nimekuelewa. Lakini sasa matokeo ya vipimo vya uchunguzi wa Masogange yameonesha nini?

Kamanda Muliro: Wewe chukua haya niliyokueleza kama ndiyo habari yako, kuhusu matokeo ya Masogange, hilo achana nalo. Natamani watu wangeelimishwa kwamba Polisi kuchunguza maiti ni suala la kawaida.

TUJIKUMBUSHE

Masogange aliyefariki dunia Aprili 21, mwaka huu katika Hospitali ya Mama Ngoma jijini Dar, aliagwa katika Viwanja vya Leaders vilivyoko Kinondoni Aprili 23 na kuzikwa nyumbani kwao katika Wilaya ya Mbalizi mkoani Mbeya Aprili 24.

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo

0
0
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live




Latest Images