Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104705 articles
Browse latest View live

Familia Yatangaza Ratiba ya Mazishi ya Mdogo wa John Heche

$
0
0
Familia Yatangaza Ratiba ya Mazishi ya Mdogo wa John Heche
Serikali mkoani Mara pamoja na familia ya Chacha Suguta aliyefariki dunia akiwa mikononi mwa polisi juzi, wanatarajia kukutana na waandishi wa habari leo mchana kwa ajili ya kutangaza taratibu na ratiba ya mazishi ya  kijana huyo.

Kikao cha familia pamoja na uongozi wa Serikali kinafanyika baada ya pande hizo mbili kukutana jana na kufikia makubaliano yatakayotangazwa rasmi kwa umma baadaye mchana.

Mbunge wa Tarime, John Heche amesema familia hiyo pia inatarajia kutangaza msimamo wake kuhusu hatua za kisheria zilizochukuliwa dhidi ya askari William Marwa (50) anayedaiwa kumuua Chacha.

Soma: Familia ya Heche yasubiri kikao na polisi kumzika ndugu aliyeuawa

Askari huyo hata hivyo alifikishwa katika mahakama ya wilaya ya Tarime jana na kusomewa shtaka la mauaji.

Tukio hilo lilitokea Aprili 27 mwaka huu baada ya Suguta kukamatwa na polisi usiku akiwa katika baa ya Kasablanca na kupelekwa mahabusu.

Hata hivyo asubuhi ndugu zake walipokwenda kumuangalia, waliambiwa ameshafariki na mwili upo mochwari.  Kesi hiyo itatajwa tena Mei 15 mwaka huu.


Davido Amunulia Gari Mpenzi Wake Aina ya Porsche SUV

$
0
0
Davido Amunulia Gari Mpenzi Wake Aina ya Porsche SUV
Davido sasa ameamua kuweka wazi mahusiano yake na Chioma. Msanii huyo ameweka weka wazi hilo usiku wa jana katika sherehe ya kuzaliwa ya mrembo huyo ambaye ametimiza miaka 23.



Mara kadhaa Davido amekuwa akikataa kuwa na mahusiano na mrembo huyo. Katika sherehe hiyo Davido amemzawadia gari aina ya Porsche SUV yenye thamani ya kiasi cha dola 125k ambapo ni zaidi ya shilini milioni 285 za Kitanzania.

Lakini kubwa zaidi hit maker huyo wa Fall, kupitia Instagram, ameweka video ya gari hilo wakati akimkabidhi mrembo huyo na kuandika ujumbe wa kuthibitisha kuwa wao ni wapenzi.



“I give my baby ASSURANCE!!! I love you baby!! WE IN THIS 4 LIFE!! ❤❤❤❤😍😍😍 @thechefchi !! HAPPY BIRTHDAY CHIOM CHIOM !! FROM ME TO YOU!! I BOUGHT MY BABY A PORSCHE!! 🔥🔥🔥,” ameandika Davido.


Rais wa TFF Atoa Onyo kali kwa Klabu za Bongo Kisa Serengeti Boys

$
0
0
Rais wa TFF Atoa Onyo kali kwa Klabu za Bongo Kisa Serengeti Boys
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Wallace Karia amezitaka klabu zote zitakazo wachukua wachezaji wa Serengeti Boys kuhakikisha wanapata nafasi ya kucheza kwenye timu zao huku akitarajia kuweka sheria kali kwa wale watakao shindwa kuwachezesha.



Karia ameyasema hayo wakati wa mapokezi wa mabingwa hao wapya wa michuano ya kombe la CECAFA  baada ya kuichapa timu ya taiafa ya Somalia kwa jumla ya mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainali Aprili 29, 2018 mjini Bujumbura nchini Burundi.

Mama Kanumba Amlilia Mwakyembe "Mimi ni Staa Nisiye na Fedha Kazi za Mwanangu Naziona tu Mtaani"

$
0
0
Mama Kanumba Amlilia Mwakyembe "Mimi ni Staa Nisiye na Fedha Kazi za Mwanangu Naziona tu Mtaani"
Mama Mzazi wa Muigizaji Steven Kanumba ameupongeza uamuzi wa serikali wa kupitia mikataba ya wasanii ambayo inaonekana kuwa na dalili za unyonyaji.

Amesema kuwa hatua hiyo ni nzuri na muhimu kwake kwani amekuwa akiona kazi za mwanae kila siku mitaani lakini yeye hakuna anachonufaika nacho.

“Kwangu mimi ni faraja, namshukuru Waziri Mwakyembe kwa kuliona hilo. Kwa mfano mwanangu Steven Kanumba, movie zake naziona lakini mama yake ni masikini wanaofaidi ni wengine, sasa kupitia hilo tamko la serikali nasema asante Mungu,” amesema.

“Mimi ni staa nisiye na hela, kazi za mwanangu naziona tu mtaani lakini mimi ni maskini,” Mama Kanumba ameiambia Clouds TV.

Wiki iyopitia Bungeni wakati wa mjadala wa bajeti ya wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2018/19, Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe alisema ameunda kamati ya wanasheria ya kuchunguza mikataba ya kibiashara waliyoingia marehemu Steven Kanumba na Mzee Majuto.

Hatimaye Mzee Majuto Kupelekwa India kwa Matibabu Leo

$
0
0
Hatimaye Mzee Majuto Kupelekwa India kwa Matibabu Leo
Msanii wa filamu bongo Mzee Majuto leo Mei 1, 2018 anatarajiwa kusafiri na kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi kufuatia matatizo aliyopata siku kadhaa zilizopita.


Steve Nyerere ambaye amehusika kwa namna moja au nyingine katika kusaidia kuratibu zoezi la kumuwezesha Mzee Majuto kwenda nchini India kwa matibabu zaidi amefunguka na kusema kuwa leo Mzee huyo atakwenda kwa matibabu zaidi nchini India na kuwataja watu ambao wamehusika katika kufanikisha jambo hilo na kusema ni pamoja na Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri wa Habari Dkt. Harrison Mwakyembe.

"Niseme ahsante sana Mhe. Rais John Pombe Magufuli, Mhe. Mwakyembe, Ummy Mwalimu na wadau pamoja na wasanii mbalimbali kwa kujitoa kwenu, Mzee wetu King Majuto Mungu akipenda leo atakuwa njiani kwenda India kwa matibabu zaidi"

Steve Nyerere hakuishia hapo alikwenda mbali zaidi na kuwataka wasanii wajifunze kupitia kwa Mzee Majuto kuwa kuna ulazima mkubwa wao kuwa na bima ya afya na kusema ni mkombozi kwao, anadai haiwezekani miaka nenda rudi wakawa ni watu wa kuombaomba kila wakati pindi wanapopata matatizo ili hali wanapata pesa za kutosha.

"Tuna kuombea kwa namna moja ama nyingine ,Baba naamini kwa maombi ya Watanzania utarudi katika kazi za ujenzi wa Taifa lako,Kuinua sanaa yetu,Kupeperusha bendera ya mkoa wako ,Baba kuumwa kwako kuna mafunzo mengi kwa wasanii na Watanzania kwa ujumla wake, Wasanii wenzangu bima ya afya ni kitu muhimu kwako na kwa familia yako, Bima ya Afya ni mwokozi kwetu. Sidhani kama miaka nenda rudi tutakuwa watu wa kuomba msaada ,tujiulize tunafanya mapart, tunakunywa na kusaza ,tunajinadi kwenye mitandao nguo zetu kuanzia milioni 3 mpaka 4 tukiulizwa umejipangaje kwa kesho amna kitu, ni muda wa kuamka sasa ,naamini majukumu hayakimbiliki bali tunayakabili" alisisitiza Steve Nyererere

Real Madrid na Bayarn Munich Mmoja Kutinga Fainali Leo

$
0
0
Real Madrid na Bayarn Munich Mmoja Kutinga Fainali Leo
Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya inaendelea leo katika mchezo wa marudiano kati ya Real Madrid watakaokuwa nyumbani kuikaribisha Bayern Munich.

Madrid watakuwa nyumbani Santiago Bernabeu wakiwa na faida na bao moja kufuatia ushindi wa 2-1 ugenini kwenye mechi ya mkondo wa kwanza.

Mechi hiyo itakayoanza majira ya saa 3 na dakika 45 kwa saa za Afrika mashariki utatoa mshindi atakayetangulia kwenye hatua ya fainali ya mashindano hayo.

Mshindi wa pili atasubiriwa kesho ambapo majogoo wa Anfield, Liverpool watakuwa wageni dhidi ya AS Roma huko Italy.

Video:Maskini! Irene Uwoya Azidi Kuwalilia Masogange na Ndikumana

$
0
0
Video:Maskini! Irene Uwoya Azidi Kuwalilia Masogange na Ndikumana
Muigizaji Irene Uwoya amezidi kuonyesha jinsi alivyopata pigo kubwa kuhusiana na kifo cha rafiki yake wa karibu Marehemu Agnes Masogange aliyefariki April 20,2018 na pia kifo cha aliyekuwa mume wake Marehemu Hamad Ndikumana aliyefariki November 15,2017 na walibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume ambaye ni Krish.

Irene Uwoya amepost video itliyoambatanisha picha za Marehemu Agnes Masogange na Marehemu Hamad Ndikumana na kupost kwenye instagrma page yake.

Download Hapa Application Mpya ya Udaku Special Uweze Soma Vimbwanga na Udaku Mtaani Kila Siku

$
0
0
Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Upya Application yetu ya UDAKU SPECIAL Maana ile ya Zamani Tutaifuta.

Kuna Marekebisho Makubwa tumeyafanya ikiwa na tatizo la Notification kutatuliwa

NB: App mpya ina Icon Nyekundu

 Bonyeza Hapa Chini Kuinstall Upya:


==>>Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>> 

Maelfu Waandamana ili Rais Ajiuzulu

$
0
0

Maelfu ya raia wa Malawi mwishoni mwa wiki wameandamana kuipinga serikali katika maandamano ya kwanza tangu mwaka 2011.


Maandamo hayo yaliyoandaliwa na mashirika ya kiraia yamefanyika katika miji sita nchini humo kupinga vitendo vya ufisadi na utawala mbovu chini ya Rais Peter Mutharika, ambaye ameiongoza nchi hiyo tangu 2014.

Katika maandamano ya July 2011 dhidi ya serikali, polisi walifyatua risasi na kuwaua raia 20, mauaji yaliyoishtua nchi hiyo na kusababisha nchi wafadhili kusitisha misaada yao.

Rais wa zamani wa Malawi, Joyce Banda, alirejea nchini humo, Jumamosi iliyopita baada ya kuishi uhamishoni kwa miaka minne, licha kitisho cha kukamatwa kwa tuhuma za Rushwa.

Samatta Awaonya Serengeti Boys " Tulizeni Vichwa Madogo Tusije Kusikia Mmeanza Kuoa"

$
0
0
Samatta Awaonya Serengeti Boys " Tulizeni Vichwa Madogo Tusije Kusikia Mmeanza Kuoa"
Nahodha wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Ally Samatta amewapongeza vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kwa kutwaa ubingwa wa CECAFA Challenge U-17 nchini Burundi.


Serengeti Boys Jumapili ilifanikitwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge U-17) kwa kuwafunga vijana wa Somalia, mabao 2-0 yaliyofungwa na Edson Jeremiah dakika ya 25 na Jaffar Mtoo dakika ya 66.

“Hongereni sana 'Serengeti' (U17) kwa ubingwa wa CECAFA kwa umri wa chini ya miaka 17. Tunaamini TFF ina mipango mikubwa juu yenu. Tulizeni vichwa madogo, tusianze kusikia mmeanza kuoa sasa (utani). Hongereni sana,”. Samatta ameandika kupitia 'Twitter'.



Serengeti Boys imerejea nchini Alfajiri ya leo na kupokewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe ambaye amewapongeza vijana kwa ushindi huo.


Okoa Ndoa yako Sasa...Umepungukiwa na Nguvu za Kiume na Unashindwa Kupanda Mlima Vizuri

$
0
0
OKOA NDOA YAKO SASA : JE UMEPUNGUKIWA NA NGUVU ZA KIUME AU UUME WAKO MDOGO AU MPENZI WAKO HAKUTIMIZII UTAKACHO:


Acha kujiona mpweke pale ukutanapo na mpenzi au mke wako kwa sababu ya kutokuwa na nguvu za kiume au Uume wako mdogo

Dawa YA MAPRO POWERA ndio dawa sahihi na tiba tosha kwa sasa Kutibu tatizo na kuponesha kabisa tatizo LA KUWAI KUFIKA KILELENI KABLA MWENZI WAKO BADO AJAKOJOA

KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOA NA MWILI KUCHOKA

UUME KUSINYAA NA KUWA LEGELEGE

KUUMWA NA TUMBO WAKATI UNAPOMALIZA KUFANYA TENDO

Dawa hii utumiwa ata na wazee wenye umri mkubwa na haina madhara yoyote

MAKAKANUA HII NI dawa ya maumbili madogo urefusha na kunenepesha saizi upendayo saiz 5-6-7-8 na unene sm 3-4-5 kwa mini huabiki kwa kuwa na UUME mdogo wai sasa upate tiba sahihi kabisa na ni tofauti na ulizowai kutumia :

Tunarudisha mke au mpenzi ndani ya masaa matatu tu zipo dawa za presha kisukali vidonda vya tumbo korodani iliyovimba dawa za uzazi tunapunguza matiti makubwa kitambi na mwili mkubwa dawa zipo FIKA OFISINI KWANGU MBAGALA ZAKHEMU KWA WATEJA AMBAO AMTAKUWA NA NAFASI YA KUJA OFISINI AU MLIO MKOANI MTALETEWA p

Piga simu 0743362017 au 0789234653

DR AGU

Waziri Mahiga Aomba Radhi kwa Rais Magufuli Kisa Hiki Hapa

$
0
0
Waziri Mahiga Aomba Radhi kwa Rais Magufuli Kisa Hiki Hapa
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Augustino Maiga ameomba radhi kwa Rais Magufuli kwa niaba ya watu wa Iringa kwa kukosa kura 25 za udhamini kipindi cha kampeni za uchaguzi 2015.

Balozi Maiga ameomba radhi hiyo leo kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambayo kitaifa inafanyika katika uwanja wa Samora mkoani Iringa.

“Nakumbuka Mhe. Rais ulipata shida kidogo kupata wadhamini hapa Iringa Mjini ikabidi utoke nje ya mji ndiyo ukapata ila wadhamini 25 kwa hapa mjini kura hazikupatikani tunakuomba radhi sana Mhe. Rais kwa kukosa busara hiyo. Lakini ulipokuwa hapa ulitoa ahadi kwa wana Iringa na umezitimiza ahadi ya kwanza ulisema Iringa itakuwa Makao Makuu ya Utalii ya mikoa ya kusini hilo tumeshalifanya, Mkuu wa mkoa aliitisha vikao na watu wa mikoa mingine lakini hasa wewe umeshafanya maamuzi kuwa Uwanja wa ndege wa Iringa wa Nduli utarekebishwa na kuweza kuchukua ndege kubwa zaidi kama zile za Bombidier,” alisema Dkt. Mahiga.

Beki wa Liverpool Akunywa na Wacha Waoane ya Daimond na Chege Ajirekodi Akicheza

$
0
0
Beki wa Liverpool Akunywa na Wacha Waoane ya Daimond na Chege Ajirekodi Akicheza
Ngoma ya Chege aliyomshiriksha Diamond Platnumz ‘Waache Waoane’ bado ipo kwenye headlines zake za kiburudani.

Hii ni baada ya beki wa Liverpool, Dejan Lovren ku-share video mtandaoni akisikiliza na kucheza wimbo huo.


Ngoma Waache Waoane ilitoka Augost 4, 2016, wimbo huo uliotayarishwa Wasafi Records hadi sasa una views Milioni 8.3 katika mtandao wa YouTube.

Rais JPM Atoa Agizo Hili kwa Waziri Majaliwa

$
0
0
Rais JPM Atoa Agizo Hili kwa Waziri Majaliwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemwagiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kuwashughulikia viongozi wanaowahamisha watumishi wa Umma bila kuwalipa stahiki zao.


Akiongea leo kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi), mkoani Iringa Rais Magufuli amesema jambo la kuhamisha wafanyakazi bila kuwalipa ameshapiga marufuku hivyo kama kuna kiongozi bado anafanya hivyo ni lazima ashugulikiwe.

''Kama patakuwepo na Mkurugenzi ama kiongozi yoyote anamuhamisha mfanyakazi, awe mwalimu au mtumishi yoyote bila kumlipa posho yake ya uhamisho na wawe bado wanaendelea kufanyakazi, Mh. Waziri Mkuu lisimamie hilo wao wahame moja kwa moja kwenye kazi zao'', amesema.

Awali Risala ya Chama Cha Wafanyakazi nchini TUCTA ilieleza pamoja na kuwepo kwa zuio hilo la Rais, lakini bado wafanyakazi wanahamishwa bila kulipwa stahiki zao jambo ambalo ni kinyume na taratibu za kazi.

Aidha Rais Magufuli amesisitiza kuwa ikitokea kiongozi anamuhamisha mfanyakazi lazima amlipe stahiki zake kwanza vinginevyo huyo kiongozi ni jeuri na dawa yake ni kumuondoa hivyo Mawaziri wanaohusika walifanyie kazi hilo.

Mtanzania Akwapua Tuzo ya Uongozi bora Marekani

$
0
0
Mtanzania Akwapua Tuzo ya Uongozi bora Marekani
Leo May 1, 2018 kunayo hii ya kuifahamu ni Chuo Kikuu cha Minnesotan nchini Marekani kimetoa tuzo ya uongozi bora kuhusu kuhudumia watu wenye ulemavu kupitia michezo kwa Mtanzania N’nyapule Madai.

Mtanzania huyo ambaye ni Kamishna mstaafu Msaidizi Ustawi wa Jamii, amepewa tuzo hiyo April 26, 2018 ikiwa ni sehemu ya kutambulika kwa mchango wake hasa wa kuwahudumia watu wenye ulemavu.

“Tuzo hii ni heshima kwetu Special Olympics lakini pia kwa Watanzania kwa ujumla, kikubwa ni serikali na wadau kutuunga mkono ili tuwasaidie watu wenye ulemavu,”amesema Madai

Pia mstaafu Madai ameihasa jamii kutowaficha watu wenye ulemavu kwani wana uwezo wa kubadilisha maisha yao kupitia michezo na kukuza uchumi wa nchi.

“Wapo walemavu tuliowasaidia ambapo wengine wamefanikiwa hadi kuoa, sasa ukimficha mtu kama huyo inakuwa haipendezi,” -Madai

Marekani: Makubaliano ya Nyuklia na Iran ni ya 'Uongo'

$
0
0
Marekani: makubaliano ya nyuklia na Iran ni ya 'uongo'
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo anasema makubaliano muhimu na Iran ya nyuklia 'yalitokana na uongo', baada ya Israel kudai kwamba ina ushahidi kuhusu mpango wa siri wa nyuklia wa Iran.

Amesema inadhihirisha kuwa makubaliano hayo ya Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani ya mwaka 2015, yalitokana na uongo na sio nia njema.

Rais Trump ameashiria kwa muda mrefu azma yake ya kujitoa katika makubaliano hayo na anatarajiwa kutoa uamuzi katika wiki zijazo.

Mataifa yenye nguvu yanasema Iran imeshinikiza makubaliano hayo na yanapaswa kuendelezwa.

Kwa pamoja Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zimeitaka Iran kuheshimu makubaliano hayo
Iran inashutumiwa nini?

Waziri wa wa Israeli Benjamin Netanyahu siku ya Jumatatu ameishutumu Iran kwa kuendeleza mpango wa kuunda zana za nyuklia - mradi uliopewa jina 'Project Amad', na amesema kuwa nchi hiyo imeendelea kupata elimu kuhusu kuunda silaha za nyuklia baada ya mradi huo kuzimwa mnamo 2003.

Hilo lilifuata ufichuzi mnamo 2002 wa kundi la upinzani linaloishi uhamishoni lililosema kwamba Iran inaunda maenoe ya siri ya urutubisha nyuklia kinyume na makubaliano ya nyuklia ambayo Iran ilitia saini kuyatii.


Daima Iran imekana kuunda zana za nyuklia, na ilikubali miaka mitatu iliyopita kusitisha mpango wake wa kuunda nishati ya nyuklia ili kwa upande wake iondolewe vikwazo.


"Nyaraka zilizopatikana na Israel kutoka ndani ya Iran zinaonyesha pasi na shaka kuwa utawala wa Iran ulikuwa hausemi ukweli. Pompeo alisema katika taarifa yake.

"Tumekagua kwamba nyaraka tulizoziona ni za kweli, "alisema akiongeza: "Iran ilificha mpango kubwa wa nyuklia dhidi ya dunia na shirika la kimataifa la nishati ya atomiki (IAEA) - mpaka leo."


Pompeo pia alionya kwamba Marekani sasa "inakagua ufichuzi huo wa nyaraka za siri wa Iran una maana gani kwa siku zijazo".

Trump, ambaye alizungumza wazi kuhusu upinzani wake wa makubalian hayo na Iran yalifikiwa wakati wa utawala wa Obama, amesema ametizama sehemu ya aliyowasilisha Netanyahu na kueleza kuwa hali hiyo 'haikubaliki'.


Kwa upande wake, Iran imekataa madai ya Israel kuhusu kuwepo kwa nyaraka za siri kutoka Tehran zinazothibitisha kuwa bado wanaendelea na mpango wao wa Nyuklia.

Akizungumza na wafanyakazi mjini Tehran kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei alikanusha madai hayo na kusema kuwa nchi yake itajibu kama Marekani itafanya maamuzi yoyote ya kuwaumiza.

Aunt Ezekieli Kuigawa Bure Filamu yake Mpya

$
0
0
Aunt Ezekieli Kuigawa Bure Filamu yake Mpya
Mwigizaji wa filamu, Aunty Ezekiel amesema anakusudia kuwagawia bure filamu yake mpya Mama ni Mungu wa Dunia atakayoizindua Mei 13 mwaka huu, wageni wote watakaofika siku hiyo.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Aunty amesema lengo la kufanya hivyo ni kuwafikishia ujumbe alioukusudia watu wengi ziadi.

Amesema alipata wazo la kuufikisha ujumbe uliobebwa katika filamu hiyo baada ya kuwa mama. Aunty ni mama wa mtoto mmoja wa kike aitwaye Cookie.

“Nilipoingia leba niliona mateso ambayo wanawake wanapitia katika kupata mtoto nikaona hamna shukrani nyingine ambayo naweza kuitoa kwa mama zaidi ya kutengeneza filamu,” anasema.

Pia, amesema maisha ya kutokuwa na mama yalimuongezea ari ya kutaka kutengeneza filamu hiyo kwa mama yake ambaye alifariki wakati yeye akiwa na miaka minane tu.

“Yaani pamoja na kwamba sasa hivi ni mama, kuna wakati unakumbana na mambo mazito ambayo unatamani mama yako angekuwepo ili umshirikishe lakini ndio hivyo haiwezekani, hivyo filamu hii inatoa mafunzo kwa watu kuona thamani ya mama', amesema.

Akielezea sababu ya kumshirikisha mtoto wake, amesema ni katika kuleta uhalisia zaidi na aliamini kuwa itampa hisia zaidi wakati wa kuigiza tofauti na ambavyo angecheza na mtoto asiye wake.

Filamu hiyo itazinduliwa Mei 13 mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani City na kwamba hana mpango wa kuisambaza zaidi ya watu kuionea kwenye mtandao wa Youtube.

Rais JPM Aagiza Aliyemlilia Apimwe Kizazi

$
0
0
Rais JPM Aagiza Aliyemlilia Apimwe Kizazi
Rais John Pombe Magufuli ametoa agizo kwa Mkuu wa Mkoa Iringa pamoja na RPC mkoani humo kumpatia msaada mwanamama Salmakoni Sanga ikiwa ni pamoja na kumpima kama kweli ametolewa kizazi baada ya kudai kushambuliwa na kijana aliyemtaja kwa jina la Mussa.


Rais Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kumaliza kuhutubia katika sherehe za Mei Mosi mkoani Iringa ambapo mama huyo alijitokeza na kumlilia Rais Magufuli ampatie msaada kutokana na kunyimwa haki yake mahakamani.

Mama huyo amesema kwamba tukio lake la kushambuliwa na Bw. Mussa lilifanyika mwaka jana ambapo shambulio lilimfanya apoteze kiumbe kilichopo tumboni hali iliyompelekea kutolewa kizazi.

Hata hivyo mama huyo amesema kwamba pamoja na maumivu aliyosababishiwa na kijana huyo, bado mahakama ilimuachia huru mtu huyo na yeye akiamini kwamba alidhulumiwa haki yake na mahakama ya mkoa huo.

Akitoa maagizo, Rais Magufuli amemtaka RPC Iringa Juma Bwire na Mkuu wa Mkoa Bi. Amina Masenza kumtafuta kijana huyo na kumfungulia mashtaka upya hata kama alishinda kesi.

Barakah The Prince Afunguka Ishu ya Kusaini WCB

$
0
0
Barakah The Prince Afunguka Ishu ya Kusaini WCB
Msanii wa muziki Bongo, Barakah The Prince amefunguka kuhusu tetesi za kujiunga na label wa WCB.

Muimbaji huyo ameiambia Rick Media kuwa WCB ni kama familia yake ila suala la kujiunga na label hiyo halina ukweli wowote.

“Hapana, WCB ni kama familia yangu, mara nyingi hata mameneja wa WCB ndio wanakuwa wananiongoza na kunielekeza nifanye nini,” amesema Barakah.

“Kwa hiyo tumeamua kuwa kama familia na kuna wasanii wengi wanafanya vizuri, lakini sio kwamba nipo chini ya WCB, no siyo kweli,” amesisitiza.

April 25, 2018 Dj wa Diamond Platnumz ‘Romy Jones/Rj The Dj’ aliachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Bora Iwe akiwa amemshirikisha Baraka The Prince.

Utakumbuka July 21, 2017 Baraka The Prince alitangaza kuondoka katika label ya Rockstar4000 kwa kile alichodai kuna mambo hayapo sawa kati yake na menejimenti hiyo.

Rais Magufuli Agoma Kupandisha Mishahara, Sababu Hizi Hapa

$
0
0

Katika Sherehe za Mei Mosi zilizofanyika Iringa leo Mei Mosi 2018, Rais Magufuli amesema hawezi kupandisha mishahara kwa sasa kama ilivyoombwa na Wafanyakazi kupitia TUCTA kwa sababu fedha zote zinatumika katika kufanya mambo makubwa.

Miongoni mwa mambo hayo ni ulipaji wa madeni mbalimbali, kuajiri watumishi wapya, kutoa elimu bure, kuongezwa kwa bajeti ya afya, mradi wa umeme wa maji wa Stiegler's gorge, Reli ya SGR na ujenzi wa viwanda mbalimbali.

Rais amesema "Kwangu mimi naona hizi hela ni bora kuziweka kwenye miradi kuliko kujiongezea mishahara. Mkitaka hii miradi yote tulioianzisha tuifute ili tujipandishie mishahara mimi sina tatizo hata kujilipa milioni mbilimbili. Kupanga ni kuchagua.

Tukitekeleza hii miradi yote haitachukua muda mrefu mishahara yetu bila kuiongeza na hii si lazima Mei Mosi.

Ningekuwa na hela kwenye chungu zimebaki pale leo ningetamka tu lakini nikitamka nitazitoa wapi? Nina mpango wa kuajiri wafanyakazi 52 elfu, ntawalipa nini? Dhamira yangu inanituma kwamba kusubiri ni kitu kizuri. Hebu tujenge miundo mbinu na kuajiri hawa 52,000"

Rais Magufuli amesema kuwa atawapa nyongeza ya mishahara ya kila mwaka na kwamba nyongeza kubwa itakuwepo kabla ya utawala wake kumalizika.
Viewing all 104705 articles
Browse latest View live


Latest Images