Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Polisi Aliyemkodi Mwenzake ili Amtie Mimba Mkewe, Amfikisha Mahakamani kwa Kushindwa Kumtia Mkewe Mimba

$
0
0

In Dar-es-Salaam, a Tanzanian Court must decide on a honorable intentions in a case where a man hired his neighbor to get his wife pregnant.

It seems that Darius Makambako 50 with his wife Precious 45, really wanted to have a child, but the renowned doctor had told the couple,the husband was sterile. There was no doubt, the couple was tired of being in a 23 year childless marriage.

So Makambako, a member of the Tanzanian Police Force (Traffic Department), after claiming his wife’s protests, hired his neighbor Evans Mastano, 52, a fellow police officer in the country’s commercial city of Dar-es-Salaam to impregnate his wife.

Since Evans was already married and the father of two beautiful daughters, plus he looked very much like Darius to the boot, the plan seemed good.

Makambako paid Mastano 2,000,000 Tanzanian Shillings for the job and for three evenings a week for the next 10 months in 2016.

Evans tried desperately, a total 77 different times to impregnate his friend’s wife Precious, but failed terribly.

Reports say Precious, a nurse at a private clinic had decided to get a three months vacation leave (March to June 2016) to dedicate her time to sleeping with her husband’s best friend and neighbor in order to have her first child, but the man failed to impregnate her despite the husband leaving them in bed the whole day in most times.

And when Precious failed to get pregnant for 10 months, however, Makambako was not understanding and insisted that Evans have a medical examination, which he did in January 2017.

The doctor’s pronouncement that Evans Mastano was also sterile shocked everyone except his (Evan's) wife, who was forced to confess that Evans was not the real father of her two children, but were for his cousin, Edward.

“I was forced to secretly sleep with Edward, his first cousin to have these two children after realizing that my husband could not impregnate me for two years”, Angela told the Dar-es-Salaam Today News.

Now Makamboko is suing Evans for breach of contract in an effort to get his money back, but Evans refuses to give it up because he said he did not guarantee conception, but only that he would give an honest effort.
.

Source: DAR-ES-SALAAM TODAY.

Serikali ya Kenya Yatangaza Ongezeko la Mshahara Kwa Wafanyakazi wa Kima cha Chini

$
0
0

NAIROBI, KENYA: Serikali ya Kenya yatangaza ongezeko la asilimia 5 kwa kima cha chini cha mshahara ili kuwalinda wafanyakazi na mfumuko wa bei uliofikia 4.8% mwaka huu.
-
Ongezeko hilo limetangazwa leo Mei Mosi, 2018 na Waziri wa Ajira na Mafao ya Kijamii, Ukur Yattani akisoma hotuba ya Rais Kenyatta katika viwanja vya Uhuru Park katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani mwaka huu.
-
Pia Serikali imeona upotevu wa masaa ya uzalishaji yaliyofikia milioni 100 kutokana na migomo ambayo imeona ni mbaya kwa taifa linaloendelea kama Kenya na kuona umuhimu wa kufanya mdahalo wa kitaifa na wadau ili kumaliza tatizo hilo.

Rais Magufuli: Kabla Kipindi Changu cha Urais Hakitaisha Bila Kuongeza Mishahara

$
0
0
Rais Magufuli: Kabla Kipindi Changu cha Urais Hakitaisha Bila Kuongeza Mishahara
Katika hotuba yake leo kwenye maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi (Mei Mosi), yaliyofanyika kitaifa Mkoani Iringa, Rais Magufuli ameahidi kupandisha mishahara kwa kiasi kikubwa kabla hajamaliza awamu yake ya uongozi.

''Kipindi changu cha Urais hakitaisha kabla sijapandisha mishahara wafanyakazi. Na mimi nataka niwaeleze kupandisha kwangu kutakuwa si kwa elfu kumi, kutakuwa kupandisha kwelikweli'', amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli ameweka wazi kuwa alitamani sana mwaka huu kupandisha mishahara lakini baada ya kuona changamoto zilizopo ikiwemo kulipa madeni ya nyuma akaona azimalize kwanza kabla ya kupandisha.

Pamoja na hayo Rais Magufuli ameviomba vyama vya wafanyakazi na masharikisho yao, kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano kwasababu inaongozwa na walimu akiwemo yeye mwenyewe na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambao wote wamewahi kuwa walimu.

Pia Rais Magufuli amemshukuru Rais wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi (TUCTA)  Tumaini Nyamhokya, kwa maandalizi mazuri ya sherehe hizo ambazo zimefanyika kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.

Aunt Ezekiel Kuzindua Filamu Yake Mey 13

$
0
0
Aunt Ezekiel Kuzindua Filamu Yake Mey 13
Msanii maarufu wa filamu nchini, Anty Ezekiel, anatarajia kuzindua filamu yake mpya aliyoipa jina la ‘Mama’, siku ya Jumapili Mei 13 mwaka huu yenye maudhui ya kuenzi na kutambua mchango wa mwanamke kama mama kwenye jamii,



Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Anty  amesema kuwa ameamua kuonyesha umuhimu na thamani ya mwanamke katika jamii kutokana na nafasi ya mama.



Uzinduzi huo wa filamu hiyo unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam Mei 13 mwaka huu.

Ewura Yatangaza Kushusha Bei ya Petrol, Dizeli na Mafuta ya Taa

$
0
0
Ewura Yatangaza Kushusha Bei ya Petrol, Dizeli na Mafuta ya Taa
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) imetangaza kushuka kwa bei ya mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa kwa asilimia 0.9 hadi asilimia 3.8 kuanzia kesho, Mei 2.

Taarifa iliyotolewa leo Mei Mosi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Nzingagwa Mchany amesema bei hiyo ni kwa upande wa  Tanzania bara.

Hata hivyo, punguzo hilo ni kwa watumiaji wa mafuta yanayopitia katika bandari ya Dar es Salaam huku watumiaji wa bandari ya Tanga bei ikiongezeka.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ikilinganishwa na tangazo la bei ya mafuta la Aprili 4, bei ya petroli imepungua kwa Sh88 kwa lita (asilimia 3.8) na dizeli Sh61 kwa lita (asilimia 2.75) huku bei ya mafuta ya taa ikiongezeka kwa Sh2 kwa lita sawa na asilimia 0.09.

Kadhalika bei ya wanunuzi wa jumla wa bidhaa za petroli nayo imepungua kwa Sh100.91 kwa lita (asilimia 4.58), dizeli Sh73.71 kwa lita (asilimia 3.52) na mafuta ya taa ni Sh10.49 kwa lita sawa na asilimia 0.51.

Mafuta yanayopita bandari ya Tanga bei yake kwa wanunuzi wa rejareja imeongezeka kwa asilimia 0.14 kwa petroli na asilimia 0.71kwa dizeli lakini wauzaji wa jumla bei imepungua kwa asilimia 0.46 (Sh9.8 kwa lita) kwa petroli na asilimia 0.1 (Sh1.9 kwa lita) kwa dizeli.

“Hakuna uingizaji mpya wa mafuta uliofanyika nchini kupitia bandari ya Tanga lakini kutokana na mabadiliko ya bei ya Ewura lakini kuna mabadiliko ya bidhaa hizo tofauti na ilivyotangazwa Aprili 4. Bei ya petrol itaongezeka kwa sh3 kwa lita huku dizeli ikiongezeka kwa Sh15 kwa lita,” imeeleza taarifa hiyo.

Kutokana na kupungua kwa mafuta ya taa katika bandari, watumiaji wa mafuta ya taa wa mikoa ya nyanda za juu ambao hutumia bandari hiyo, wameshauriwa kuchukua bidhaa hiyo katika bandari ya Dar es Salaam kwa bei elekezi.

Jack Pemba Avujisha Video yake ya Ngono

$
0
0
Aliyewahi kuwa bwana wake Auntie Ezekiel Pedej'ee Jack Pemba ambaye kwasasa anaishi nchini Uganda akifahamika kwamba ni Raia kutoka Kongo, wiki hii ka trend kwenye vyombo vya habari vya nchini humo baada ya video yake akiwa anakula tunda bila chenga kuvuja huku ikidaiwa kaivujisha mwenyewe.

Video hiyo ambayo anaonekana akiwa na mdada ajulikanaye kama Honey Suleman ambaye inasemekana ni rafiki mkubwa wa mke wa Jack Pemba hadi wanaitana ndugu.

Kwenye video hiyo Jack kaficha uso wake huku akimwacha mdada aonekane.
Honey anadai ya kwamba video hiyo waliirekodi wakati wakiwa penzini na Jack Pemba alimtaka ampatie 5,000$ asiivujishe jambo ambalo Honey anasema hakuwa tayari kufanya hivyo akamwambia avujishe tu maana hayuko tayari kuwa blackmailed.

Aliongeza kuwa bado Jack Pemba anazo video nyingine mbili hivyo bora tu aziachie zote maana hatishiki.

Jack Pemba ambaye kwa sasa inadaiwa kafulia hali tia maji tia maji ana madeni mengi mpaka kuweka gari zake rehani imewashangaza wana Uganda kusikia ana nyemelea mpaka ela ndogo kiasi hicho wakati awali alikuwa anaosha gari zake kwa pome za bei ghali.

Kutokana na maadili ya Udaku Special Blog video sitoiweka ila pichani ni Jack Pemba na Honey.
Mitandaoni watu wanamsifia Honey kwa jinsi alivyokuwa anajituma na mauno kama fifi moto wakati wakimponda kuwa kakauka hana maji kabisa.

DFG Universal Music watoa top 10 ya wasanii Bongo,Kiba ashika namba 5 nyuma kidogo ya Aslay

$
0
0
Wakuu kampuni Kubwa ya muziki , AR na burudani Afrika (HQ Johannesburg South Africa and Lagos Nigeria) DFG Universal Music muda mchache uliopita wametoa top 10 ya wasanii wa Tanzania kupitia kituo cha TV cha TRACE,wanadai wameangalia influence kwny s/network, mkwanja,viewship,trending ,hela, shoo na vitu kibao wamevitaja. Utafiti wao uliwafuatilia wasanii kadhaa waliojuu kwa kipindi cha miezi 9 iliyopita.
Hii list wamedai ni ya wasanii wanaofanya mziki wa kuimba (Afropop na RNB). Wakinadada watatu wamepenya kwenye nyavu.
List yao ilikuwa hivi
1.Diamond (nilitegemea)
2.Harmonize
3.Vanessa Mdee
4.Aslay
5.Ali Kiba
6.Baraka Da Prince
7.Rayvan
8.Mavoko
9.Jux
10.walipewa Maua Sama, Ben Pol na Nandy.
Wakuu maoni yenu

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) yatoa Tahadhari ya Mvua Kubwa Mikoa Mitano

$
0
0
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa tahadhari ya kunyesha mvua kubwa juu ya wastani, kwa siku tano zinazoweza kusababisha mafuriko katika maeneo mengi nchini .

Kwa mujibu wa TMA, mvua hizo zitaanza leo Mei Mosi mpaka Mei 5 mwaka huu na zinatarajiwa kunyesha mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Mikoa mingine ni Mara, Mara, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Katavi, Kigoma, Arusha, Kilimanjaro na Manyara.

TMA imesema kiwango cha athari zinazoweza kutokea katika jamii ni pamoja na adha ya usafiri, barabara kubwa kutopitika na maji kujaa au kupita kwa kasi.

Pia imetoa wito kwa wakazi wa maeneo ya mabondeni kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari zitakazotolewa.

Ahadi ya Rais Magufuli Kwa Wafanyakazi Baada ya Kushindwa Kuwapandishia Mishahara Mwaka Huu

$
0
0
Katika hotuba yake leo kwenye maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi (Mei Mosi), yaliyofanyika kitaifa Mkoani Iringa, Rais Magufuli ameahidi kupandisha mishahara kwa kiasi kikubwa kabla hajamaliza awamu yake ya uongozi.

''Kipindi changu cha Urais hakitaisha kabla sijapandisha mishahara wafanyakazi. Na mimi nataka niwaeleze kupandisha kwangu kutakuwa si kwa elfu kumi, kutakuwa kupandisha kwelikweli'', amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli ameweka wazi kuwa alitamani sana mwaka huu kupandisha mishahara lakini baada ya kuona changamoto zilizopo ikiwemo kulipa madeni ya nyuma akaona azimalize kwanza kabla ya kupandisha.

"Natamani mwaka huu kupandisha mishahara kwa wafanyakazi lakini kutokana na changamoto zilizopo za kuajiri wafanyakazi 52,000 nitawalipa nini? nikisema natamka kuongeza mishahara, nitazipata wapi?”amesema Magufuli.

Pamoja na hayo Rais Magufuli ameviomba vyama vya wafanyakazi na masharikisho yao, kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano kwasababu inaongozwa na walimu akiwemo yeye mwenyewe na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambao wote wamewahi kuwa walimu.

Pia Rais Magufuli amemshukuru Rais wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi (TUCTA)  Tumaini Nyamhokya, kwa maandalizi mazuri ya sherehe hizo ambazo zimefanyika kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.

Mwanamke Aangua Kilio Mbele ya Rais Magufuli Iringa....Rais Magufuli Atoa Maagizo

$
0
0
Rais John Pombe Magufuli ametoa agizo kwa Mkuu wa Mkoa Iringa pamoja na RPC mkoani humo kumpatia msaada mwanamama Salmakoni Sanga ikiwa ni pamoja na kumpima kama kweli ametolewa kizazi baada ya kudai kushambuliwa na kijana aliyemtaja kwa jina la Mussa.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kumaliza kuhutubia katika sherehe za Mei Mosi mkoani Iringa ambapo mama huyo alijitokeza na kumlilia Rais Magufuli ampatie msaada kutokana na kunyimwa haki yake mahakamani.

Mama huyo amesema kwamba tukio lake la kushambuliwa na Bw. Mussa lilifanyika mwaka jana ambapo shambulio lilimfanya apoteze kiumbe kilichopo tumboni hali iliyompelekea kutolewa kizazi.

Hata hivyo mama huyo amesema kwamba pamoja na maumivu aliyosababishiwa na kijana huyo, bado mahakama ilimuachia huru mtu huyo na yeye akiamini kwamba alidhulumiwa haki yake na mahakama ya mkoa huo.

Akitoa maagizo, Rais Magufuli amemtaka RPC Iringa Juma Bwire na Mkuu wa Mkoa Bi. Amina Masenza kumtafuta kijana huyo na kumfungulia mashtaka upya hata kama alishinda kesi.

Breaking News: Familia ya heche yakubali kumzika Suguta

$
0
0
Habari zilizotufikia hivi punde nikwamba Familia ya Mbunge John Heche yakubali kumzika ndugu yao Sunguta Chacha.

Baada ya Familia ya Heche kukataa kumzika ndugu yao kutokana na kuuawa na Polisi siku 4 zilizopita leo Familia hiyo imetangaza kuwa imeridhia kumzika ndugu yao.

Nyashinski Atolea Ufafanuzi Ujumbe wake Mbaya wa Twitter kwa Diamond

$
0
0
Unaukumbuka ujumbe wa Twitter ambao ulidaiwa kuwa wa Nyashinski ambapo ulikuwa unasema kuwa Diamond hajui kutengeneza hit song? Basi msanii huyo ameamua kufunguka kuhusu ujumbe huo.

Hilo lilitokea ikiwa ni siku chache zimepite baada ya Diamond kutumia mtandao wake wa Instagram kumpigia debe kwa mashabiki na watu wote Afrika Mashariki tuungane katika kumpigia kura Nyashinski katika tuzo za MTV EMA alizochaguliwa kuwania mwaka jana.

Akiongea na Lil Ommy TV, Shinski amesema ujumbe huo haukuwa wake na wala haukutumwa kupitia akaunti yake ya Twitter. “Wacha niweke very very clear, Twitter account yangu ni Realshinski sio official au Thereal. Ukiangalia hiyo tweet ilitoka kwenye Twitter nyingine,” amesema msanii huyo.

“Unajua unaweza kuwa na watu wengi Twitter wanajiita Nyashinski. So nikaona acha niweke sawa, hiyo tweet ilikuwa inasema Diamond hajui kumake hits, wote tunajua Diamond anajua kumake hits. Hiyo kwanza haikuwa kweli , hiyo haikuwa tweet yangu,” ameongeza.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya May 2

$
0
0


Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya May 2

Msanii Fid Q Aitumia Ombi Hili Serikali

$
0
0
Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q, amewasilisha ombi la kutaka kutambuliwa na kuundiwa sera yake kwa sanaa ya muziki Bongo ili iweze kujitegemea.


Fid Q ametumia siku ya Wafanyakazi kutoa ombi hilo kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ikiwa ni siku moja tu tangu ateuliwe na Chama cha Muziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA), kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Fedha, Mipango na Uchumi.

''SANAA ni sekta rasmi hivi sasa lakini bado haijapewa sera na hiyo ni sawa na kuwa na ofisi isiyokua na KANUNI, TARATIBU wala SHERIA. Kwa ufupi bado tunaongozwa na sera ya utamaduni. Tunayofuraha kubwa ya kuitumia sikukuu hii ya wafanyakazi kwa kuikumbusha WIZARA na SERIKALI kwa ujumla kutuundia sera ili SANAA yetu iweze kuleta tija kwenye jamii. (Na katika hilo tunashauri RASIMU iandaliwe na WASANII wenyewe). ameandika.

Aidha Fid Q ameongeza kwa kusema wasanii wanalipa kodi kwa kazi zao za sanaa lakini kazi zao hazilindwi na serikali, kitu ambacho kinatishia usalama wa wao kuendelea kulipa kodi siku za usoni kwani hawatakuwa wanatengeneza faida.

Fid Q ameteuliwa hivi karibuni na TUMA kushika nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa kamati ya Fedha, Mipango na Uchumi wa chama hicho, ambapo ameanza kazi rasmi jana April 30.

Mama Salma Amshauri Alikiba Kuhusu UKIMWI

$
0
0
Mke wa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete amefunguka na kumshauri msanii Alikiba na mkewe pamoja na Abdukiba na mkewe kuhusu suala la ugonjwa wa UKIMWI na kuwaambia kuwa wame makini kwani ugonjwa huo ni janga na halina tiba.


Mama Salma alisema hayo usiku wa Jumapili ya wiki hii ambapo wasanii wao walifanya sherehe za kuwatambulisha wake zao hivyo Mama Salma wakati akitoa nasaha zake kwa wasanii hao na wake zao aliwataka kuliogopa janga hilo la UKIMWI.

"Dunia ina maradhi, UKIMWI ni janga, UKIMWI ni hatari hauna kinga wala tiba hivyo ogopeni sana mdudu anayeitwa UKIMWI kuwa mwaminifu kwa mke wako na kuwa mwaminifu mume wako wote, mkiwa waaminifu mtayaepuka haya maradhi ambayo hayana kinga wala tiba, nyinyi wasanii kila mtu anawapenda lakini wapendeni sana wake zenu na nyinyi wapendeni sana waume zenu" alisisitiza Mama Salma Kikwete.

Davido Awajibu Mashabiki Wanaosema Kapenda Ghafla

$
0
0
Staa wa muziki kutoka Nigeria Davido leo akisherehekea Birthday ya mpenzi wake ameamua kuweka wazi kuhusiana na mahusiano yake ya kimapenzi na Chioma ambaye amezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

Davido ambaye amewashtua mashabiki wengi na kuanza kuhoji kuwa kapenda ghafla, baada ya kuamua kumpost mpenzi wake Chioma na kumzawadia gari jipya aina ya Porshe yenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 200 wakidhani kuwa ni mapema sana kufanya hivyo

Davido kupitia twitter account yake amewajibu walihoji kuwa kapenda ghafla kwa kusema kuwa “kama kuwa na mtu katika mahusiano kwa miaka mitano ni kupenda ghafla basi sawa” Kwa sasa Davido ana watoto wawili ambao amezaa na wanawake wawili tofauti ambaye mmoja alizaa na Momodu na mwingine alizaa na Amanda.

VIDEO: HATARI !! Simba Amshambulia Mzee, Hii Usijaribu Kuifanya

$
0
0
Alichofanya huyu Mzee ni kitendo  cha hatari sana na haitakiwi mwingine yeyote aige au ajaribu hata kufikiria kufanya hivyo, tahadhari ni video inayotisha.

VIDEO:

Views wa You Tube Wamkosha Venessa Mdee

$
0
0
Views wa You Tube Wamkosha Venessa Mdee
MWANADADA ambaye kwa sasa anafanya vyema na album iitwayo Money Mondays, Vanessa Mdee ‘Vee Money’, hivi karibuni amechekelea views katika mtandao wa YouTube ambazo wimbo wake namba 9, kwenye album yake uitwao Wet, umepata.

Wimbo huo ambao video yake ilifanywa na prodyuza kutoka Afrika Kusini, Justin Compas, ukiwa na wiki mbili tu umeweza kutazamwa na watu zaidi ya milioni moja jambo ambalo lilimfanya Vee Money kuandika hivi kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram;

“1 Million views in 2 weeks. #Wet. Kwangu mimi ni kitu kikubwa tena sana. (Nimesema kwangu mimi).”

Mbali na maandishi hayo Vee Money aliwashukuru pia mashabiki wake ambao wanampa sapoti katika kazi zake za muziki kila kukicha.

Kanye West: Wamarekani Weusi Walipenda Kuwa Watumwa

$
0
0
Kanye West: Wamarekani Weusi Walipenda Kuwa Watumwa
Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka nchini Marekani Kanye West amesema kuwa utumwa wa Wamarekani weusi uliofanyika zaidi ya miaka 100 iliopita lilikuwa chaguo lao.


Watu weusi walilazimishwa kutoka Afrika na kuelekea Marekani katika karne za 17, 18 na 19 na kuuzwa kama watumwa.

Kanye alinukuliwa na mtandao wa TMZ kwamba, haiwezekani watu wakubali kutawaliwa kwa miaka zaidi ya 400 bila kufanya chochote.

“Unaposikia kwamba utumwa ulifanyika kwa zaidi ya miaka 400.. miaka 400? ni kama walipendelea hilo kufanyika’, alisema katika tovuti ya burudani ya TMZ.

West baadaye alituma ujumbe wa Twitter na kusema kwamba hakueleweka vyema na kwamba alizungumza kuhusu miaka 400 kwa sababu ‘fikra zetu’ haziwezi kufungwa kwa miaka mingine 400.

Katika mahojiano na TMZ West alisema hivi sasa tunachagua kufanywa watumwa swala lililozua hisia kali kutoka kwa mfanyakazi mmoja mweusi katika kampuni hiyo.

Bwana Lathan alisema kuwa matamshi ya msanii huyo yalionekana kutolewa bila kufikiria.

“Una haki ya kuamini chochote unachotaka , lakini ujue kuna ukweli katika dunia ya sasa na athari zake kwa kila kitu ulichosema’, aliongezea huku nyota huyo akisimama na kujikuna kidevu.

“Lazima tukabiliane na ukandamizaji uliotokana na mika 400 ya utumwa ambayo ulisema kuwa watu wetu walipendelea, bwana Lathan aliendelea akiongezea kwamba nimeshangazwa na ndugu yangu nimeumizwa kwa wewe kusema kitu ambacho sio cha kweli.

Katika mahojiano hayo ya TMZ West amemtaja bwana Trump kuwa rafiki yake na kusema kuwa rais huyo ni miongoni mwa watu wake anaowapenda sana.

Matamshi yake yalizua hisia kali katika mitandao ya kijamii huku watumiaji wa mtandao wa twitter wakisema kuwa msanii huyo anafaa kusoma upya vitabu vya historia.

Kanisa Lapiga Marufuku Uvaaji wa Shela la Harusi

$
0
0
Kanisa Lapiga Marufuku Uvaaji wa Shela la Harusi
Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha, limewapiga marufuku wanawake wajawazito kuvaa shela wakati wa kufunga ndoa kwa madai vazi hilo ni alama ya ubikira kwa mwanamke na sio vinginevyo.


Hayo yamesemwa na Paroko Msaidizi wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Theresa, Padre Festus Mangwangi  wakati akiweka mkazo juu ya tamko lililotolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo hilo Isaack Amani, wakati akiadhimisha misa ya shukrani iliyofanyika Jumapili iliyopita, baada ya kuteuliwa kwake na Baba Mtakatifu Francis kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo. Kabla ya uteuzi huo uliotangazwa Desemba 27 mwaka 2017, Askofu Mkuu Amani alikuwa Askofu wa Jimbo la Moshi na kusema haitakiwi kwa mwanamke yeyote ambaye anajijua ni mjamzito kuvaa shela kipindi anafunga ndoa kwa kuwa vazi hilo linavaliwa na mwanamke asiyemjua mwanaume (bikra).

Aidha, Padre Festus Mangwangi amewataka wazazi kuwafundisha watoto wao wa kike kutunza miili yao na kuishi maisha ya kimaadili hadi watakapopata wenza wa kufunga nao ndoa na hapo ndipo alama ya shela itakapoonekana umuhimu wake.

"Tamko la Askofu Mkuu linatekelezwa kwa kuwaeleza maharusi watarajiwa wanapokwenda kupata mafundisho ya ndoa kwa katekista na baadaye padre, kuwa kama ni wajawazito basi wasivae shela na hata wale wanaowajua wanaume pia wanashauriwa wasivae", amesema Padre Festus.

Pamoja na hayo, Padre Festus ameendelea kwa kusema "wanaojitambua kuwa si bikira, hawavai shela, lakini wako wanaojificha na kuvaa shela, hii inakuwa sawa na kudanganya".

Kwa upande mwingine, Padre Festus amesema endapo atatokea mtu akadanganya na kuvaa shela wakati tayari anamjua mwanaume au kuwa mjamzito basi atakuwa anafanya utovu wa nidhamu.

Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images