Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104755 articles
Browse latest View live

Yanga Kumalizia Hasira Kimataifa Yatangaza Kihama

$
0
0
Yanga Kumalizia Hasira Kimataifa Yatangaza Kihama
Klabu ya Mabingwa Watetezi Ligii Kuu Tanzania Bara na wawakilishi pekee nchini Tanzania katika mashindano ya kimataifa Yanga, wanatarajia 'kukwea pipa' kesho Mei 3, 2018 kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wao wa kwanza hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho dhidi ya wenyeji U.S.M Algers


Hayo yamethibitishwa na taarifa zilizotolewa na Meneja wa timu kupitia ukurasa maalum wa Yanga, Hafidh Saleh na kusema kwamba matayarisho ya mchezo huo yanakwenda vizuri hadi sasa

"Tuko sawa tumejiandaa, tunahitaji kupata matokeo mazuri, ili kujenga ari mpya katika adhma yetu ya kufanya vizuri kimataifa, hatua ya makundi ni ngumu kwa sababu kila mchezo unakutana na timu ngumu. Nia yetu msimu huu tufike mbali zaidi kuliko miaka yote iliyopita", amesema Saleh.

Yanga ilifanikiwa kutinga hatua ya makundi baada ya kuitoa Wolayta Dicha ya Ethiopia kwa jumla ya ushindi wa mabao 2-1. Mechi za hatua ya makundi zinatarajiwa kuanza Mei 4 na 6.

Real Madril Yatinga Fainal Ligi ya Mabingwa

$
0
0
Real Madril Yatinga Fainal Ligi ya Mabingwa
WABABE wa soka la Ulaya, Real Madrid wametinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya tatu mfululizo na ni mara ya nne ndani ya misimu mitano iliyopita baada ya kuiondoa Bayern Munich katika nusu fainali.



Real Madrid imetimiza lengo hilo licha ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Bayern, usiku wa jana ambapo jumla wanakuwa wametinga fainali kwa mabao 4-3 kutokana na kushinda 2-1 katika mchezo wa kwanza uliochezwa Munich, Ujerumani, wiki iliyopita.


Bayern ambayo iliuanza mchezo huo kwa kasi na kupata bao la haraka dakika ya sita kupitia kwa Joshua Kimmich, ilijikuta ikikosa nafasi kadhaa za wazi na hivyo kuwafanya wenyeji waliokuwa ndani ya Uwanja wa Santiago Bernabeu kutulia na kuanza kumiliki mpira.


Dakika ya 11, Karim Benzema alifunga bao la kichwa akipokea krosi ya Marcelo na kufanya mchezo kuwa mgumu kwa Bayern ambao ni mabingwa wa Bundesliga.



Kosa lililofanywa na kipa wa Bayern, Sven Ulreich aliporudishiwa mpira na kuteleza, kulimfanya Benzema kuwa na kazi nyepesi ya kufunga bao la pili katika dakika ya 46 na hivyo kuwamaliza nguvu Bayern.


Akiichezea Bayern kwa mkopo kutoka Real Madrid, James Rodriguez alifunga bao la kusawazisha kwa shuti kali dakika ya 63 kufanya matokeo kuwa 2-2 lakini hakushangilia bao lake hilo, matokeo ambayo yalidumu hadi mwisho wa mchezo huku staa wa Madrid, Cristiano Ronaldo akitoka bila bao kwa mechi ya pili mfululizo licha ya kuwa yeye ndiye kinara wa mabao kwenye michuano hiyo.


Hivyo, sasa Real Madrid ambayo imeshatwaa kombe hilo mara 12 inasubiri mshindi wa mchezo wa Roma dhidi ya bingwa mara tano wa kombe hilo, Liverpool, ambazo zinatarajiwa kukutana leo katika nusu fainali ya pili, Liverpool ikiwa mbele kwa mabao 5-2. Fainali ya mwaka huu itapigwa kwenye Uwanja wa NSC Olimpiyskiy jijini Kiev, Ukraine Jumamosi ya Mei 26

REAL MADRID (4-4-2):

Navas 9; Vazquez 6, Varane 6, Sergio Ramos 6, Marcelo 7; Kovacic (Casemiro 73min, 6), Kroos 6, Modric 7, Asensio 6 (Nacho 88); Benzema 7 (Bale 72, 6), Ronaldo 6

Subs not used: Casilla, Ceballos Fernandez, Hernandez, Mayoral

Goals: Benzema 11, 46

Bookings: Modric, Lucas, Casemiro, Varane

Manager: Zinedine Zidane 7

BAYERN MUNICH (4-2-3-1):

Ulreich 5; Kimmich 7, Hummels 7, Sule 6, Alaba 7; Tolisso 6 (Wagner 76), Thiago 6; Muller 6, Rodriguez 8 (Javi Martinez 84), Ribery 6; Lewandowski 6

Subs not used: Starke, Rafinha, Mai, Dorsch, Rudy

Goals: Kimmich 3, Rodriguez 63

Booked: None

Manager: Jupp Heynckes 6

Referee: Cuneyt Cakir (Turkey) 7

Baada ya Ommy Dimpozi Kuachia Ngoma Alikiba Atoa Ahadi Hii "Ngoma Hii Ikifika Views Milioni 3 Naliamsha Dude"

$
0
0
Baada ya Ommy Dimpozi Kuachia Ngoma Alikiba Atoa Ahadi Hii "Ngoma Hii Ikifika Views Milioni 3 Naliamsha Dude"
Unatamani kuisikia ngoma mpya kutoka kwa Alikiba? Basi msanii huyo amahidi kufanya hivyo lakini kwa sharti moja tu.

Alikiba kupitia mtandao wake wa Instagram ameahidi kuachia ngoma mpya endapo video ya wimbo mpya wa Ommy Dimpoz aliomshirikisha Seyi Shay wa Nigeria ikivikisha views milioni 3

“Hii nyimbo Ya @ommydimpoz ikifika milioni 3 YOUTUBE Naliamsha DUDE 🤙🏾 (I PROMISE U) #SupportedByKiba #KingKiba,” ameandika Kiba.

Ngoma ya mwisho ya alikiba ilikuwa ni Seduce Me ambayo aliachia August 25, 2017 ukiachana na Maumivu Per Day ambayo aliachia Novemba 29 mwaka jana ambapo hata hivyo haikuwa rasmi.

Familia Yasheherekea Birthiday ya Sugu kwa Namna Hii

$
0
0
Familia Yasheherekea Birthiday ya Sugu kwa  Namna Hii
Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu amesherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa gerezani huku familia yake ikiisherehekea kwa kula chakula pamoja na watoto yatima wanaolelewa katika Kituo cha Nuru, Uyole jijini Mbeya.

Sugu ambaye anafikisha umri wa miaka 46, alisherehekea siku hiyo akiwa gerezani ambako anatumikia kifungo cha miezi mitano.

Keki ya mbunge huyo ilipambwa kwa kuchorwa pingu, mnyororo na taswira ya chumba cha Magereza.

Sugu alihukumiwa kifungo cha miezi mitano baada ya kukutwa na hatia ya kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli, Februari 26.

Mwingine aliyehukumiwa kifungo hicho ni Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga ambao wote wanatumikia kifungo cha miezi mitano jela katika Gereza Kuu la Ruanda jijini hapa.

Jana, uongozi wa Hoteli ya Desderia inayomikiliwa na Sugu ulisherehekea siku hiyo pamoja na watoto yatima wa Kituo cha Nuru na kula nao chakula cha pamoja.

Hilo ni agizo la Sugu kuendelea kuwa karibu na jamii ya wakazi wa Mbeya.

Akizungumza na Mwananchi jana, mke wa Sugu, Happiness Msonga alisema mumewe ndiye aliyeagiza siku ya kuzaliwa kwake iadhimishwe pamoja na watoto yatima kwa kula nao chakula.

“Sugu amesema anawapenda sana watoto na yupo pamoja nao licha ya kuwa yupo gerezani, lakini kiroho yupo nao daima. Ameagiza jana kwa kuwa pia ni Mei mosi, ni vyema tukashiriki sherehe hiyo na watoto yatima,” alisema.

Happiness alisema Sugu kupitia uongozi wa hoteli yake wameanzisha mpango maalumu wa kutembelea na kujumuika na vituo vya watoto yatima vilivyopo jijini Mbeya kila mwisho wa mwezi kwa kuwapelekea chakula na misaada mingine.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Yatima cha Nuru-Uyole, Jarson Fihavango alimshukuru mbunge huyo na uongozi mzima wa hoteli yake kwa kuwapelekea chakula na misaada mingine watoto wanaowalea kituoni hapo.

“Tunajua mbunge wetu alipatwa na matatizo, lakini pamoja na kwamba yupo gerezani, lakini bado anawakumbuka wananchi wake. Sisi tunashukuru sana kwa hiki alichotufanyia,” alisema Fihavango.

“Tunasema aendelee na moyo huohuo na sisi tunamuombea. Hiki alichokifanya kina baraka kubwa mbele za Mwenyezi Mungu, tunajua namna anavyoweza kumlipa.”

Odinga Awasihi Wafuasi Wake Kumaliza Mgomo

$
0
0
Odinga Awasihi Wafuasi Wake Kumaliza Mgomo
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga amewasihi  wafuasi wake wasitishe kampeni ya kususia bidhaa na biashara za kampuni zilizohusishwa kuwa na uhusiano na chama tawala cha Jubilee cha rais Uhuru Kenyatta.


Bwana Odinga ametoa tamko hilo leo katika sikuukuu ya Mei mosi zilizofanyika katika mji mkuu wa Kenya jijini Nairobi.

"Tulikuwa na hasira nyingi kwa yale makampuni yaliokuwa yanaunga mkono serikali ya Jubilee. Tulisema ni makampuni ambayo yanatesa watu wetu, ambayo yamekataa kukubali uamuzi wa wananchi na tukasema watu wetu wote wasusie bidhaa za kampuni hizo. Sasa tumeshikana mkono na Uhuru, tumekubaliana kufanya kazi pamoja tusulishe mambo, na tumeweka sasa kamati ya ushauri ya kuleta suluhu ya kudumu" amesema Odinga.

Ameongeza "Kwa hiyo leo hii tunatangaza tunatoa ile amri ya kususia.

Tangazo la kususia bidhaa za wanaotajwa kuwa washirika wa chama tawala lilitolewa Novemba mwaka jana baada ya uchaguzi mkuu ambao ulibatilishwa na Mahakama ya juu nchini humo kwa madai kuwa ulikuwa na dosari.

Facebook Kuongeza Faragha kwa Watumiaji Wake

$
0
0
Facebook Kuongeza Faragha kwa Watumiaji Wake
Kampuni ya facebook inaongeza faragha kwa watumiaji wake kwa kuweka sehemu ya kufuta historia ya ulichokitafuta katika mtandao huo wa kijamii.

Hivi karibuni kampuni hiyo ilikumbwa na kashfa ya kutothamini faragha za watumiaje wake huku watumiaji zaidi ya millioni hamsini walidukuliwa katika kipindi cha uchaguzi wa Marekani.

Facebook imekua katika sakata la faragha ya watumiaje hivi karibuni, mamilioni ya taarifa za watumiaji zilichukuliwa bila ridhaa na kampuni ya Cambridge Analytical kwa matumizi ya wanasiasa.

Mark Zuckerberg amesema kuwa atahakikisha suala kama hilo halitajitokeza tena, kwa kutengeneza ulinzi zaidi wa mtandao huo.

''Kilichotokea kwa Cambridge Analytica ilikua uvunjifu wa uaminifu wa hali ya juu, walichukua data za watu na kuziuza, hivyo tunatakiwa kuhakikisha kuwa suala hili halitokei tena, kwanza tunaweka vizuizi kwa data ambapo mtu atakua anaombwa kwa ridhaa yake, na pili tunahakikisha tunazijua program mbaya zote zilizo'' alisema Zuckerberg.

Katika mkutano wa mwaka wa kampuni hiyo ya mjini California, Zuckerberg emeongeza pia wanaimarisha faragha ambapo itamruhusu mtumiaji kufuta historia ya kitu alichotafuta.

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo

$
0
0

Kutana na Mtaalam Sharif Hamad Kalala Mchambuzi wa Nyota za Binadamu na Tiba Asili

$
0
0

KUTANA NA SHARIF HAMAD KALALA NI
SHARIFU MCHAMBUZI WA
NYOTA ZA BINAADAMU NA NI MWENYE UPEO MKUBWA KUTAFITI MATATIZO YAKO KABLA YA KUTOA USHAURI WAKE WA TIBA AlJALISHI MBALI ULIKO TIBA YAKE UMFIKIA YEYOTE MWENYE UITAJI POPOTE
DUNIANI.

 SHARIF HAMAD KALALA NI TABIBU MWENYE KUBRI TOKA KWA ALAH ANATIBU KWA NJIA YA VITABU VYA QUR-AN, DAWA ZA ASILI ZA MITI SHAMBA PAMOJA NA DAWA ZA KIARABU.
ANATIBU KWA NJIA YA SIMU KWA KUTOA
MAELEKEZO NAMNA YA MATUMIZI YA DAWA UKIWA NCHI YOYOTE MKOA WOWOTE KWA MATATIZO YAFUATAYO:-

 KUFANIKISHA NDOA KWA UNAYE MPENDA KWA HARAKA. KUMRUDISHA MPEZI NDANI YA MASAA 12 TU.
 ULIJALI (NGUVU ZA KIUME) NDANI YA /IKI MMOJA TU
MIGUU KUWAKA MOTO KUTAFSIRI NDOTO MFARAKANO WA WANANDOA MFARAKANO KAZINIKUPANDISHWA CHEO NDANI YA SIKU SABA 7 TU.
KUTOA PETE YA BAHATI KUTOA MAJINI MACHAFU IKIWA NI KWENYE MWILI WA BINADAMU MAJUMBANI NA KWENYE BIASHARA. KUPATA MAFANIKIO YA MALI BILA YA MASHARTI. KUPANDIKIZANYOTA YA KUBASHIRI KUFUNGUA UZAZI KWA WALIYO FUNGWA KWA NJIA YA USHIRIKINA KUTOA VIFUNGO VYOTE VILIVYO FUNGWA KWENYE BIASHARA. ANA UWEZO MKUBWA WA KUPANDIKIZA NYOTA YA KUMPATA YEYOTE UMPENDAYE KWA KUMUOA AU KUWA NAYE. ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIYE MBALI PIA ALIYE CHUKULIWA
KWA NJIA YAMSUKULE
NAO UWEZO WA KUUA KESI SUGU NA MPYA NDANI SIKU 7 TU.
MENGINEYO MENGI ZAID YALIYO KUWA SUGU PIGA KWA WALE WALIYO ANGAIKA SEHEMU MBALI MBALI SHARIF HAMAD KALALA NI SULUISHO. ENDAPO UTAMSIKILIZA KWA YALE ATAKAYO KUSHAURI NA KUKUPA
ELEKEZI.
 TIBA NI KWA DINI ZOTE POPOTE ULIPO NJE NA NDANI YA NCHI.

MOBILE +255 -673 025 376
WhatsApp +255-757 069 066

Kiswahili Chaenda Mbali Laliga Wakitumua Kwenye Mitandao Yake ya Kijamii

$
0
0
Kiswahili Chaenda Mbali Laliga Wakitumua Kwenye Mitandao Yake ya Kijamii
Ukiambiwa kiswahili ndio lugha ya kwanza ya asili barani Afrika ambayo inapendwa zaidi Ughaibuni bila shaka utakubaliana na kauli hiyo, Kwani tayari lugha hiyo imeanza kutumika hata katika mazingira ambayo watu wengi wasingeweza kudhania.





Nchini Uhispania ukurasa rasmi wa Instagram  wa Ligi Kuu Soka nchini humo La Liga umetumia lugha ya kiswahili kwenye Insta Stories ambapo uliweka picha zaidi ya tatu zote zikiwa zimewekwa picha zilizosindikizwa na maelezo ya kiswahili.

Posti ya kwanza kwenye Insta Stories La Liga waliweka picha ya mshambuliaji wa Atletico Madrid, Atonio Griezman na kuandika “Mambo vipi? La Liga inaongea kiswahili“.



Posti ya pili waliweka picha ya staa wa Barcelona, Lionel  Messi na kuandika “Barceolena wametwaa wa 25 katika historia ya La Liga“.



Posti nyingine iliyofuata ilikuwa ni ya mshambuliaji wa Villareal, Carlos Bacca ambapo waliandika “Carlos Bacca (@goleador70) amefunga Hat-Trick yake ya kwanza na Villareal”



Na posti ya mwisho waliweka picha ya mchezaji wa Real Betis na kuandika Caption ndefu iliyosomeka “Real Betis wanaweza kucheza tena kwenye Europa baada ya kutocheza kwa miaka mitano”



Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa Lugha ya kiswahili kutumika kwenye kurasa za mitandao ya kijamii kwenye Ligi kubwa barani Ulaya kama La Liga.

Harmonize Amefunguka Sababu ya Kutompa Mkono Alikiba Katika Msiba wa Masogange

$
0
0
Harmonize Amefunguka Sababu ya Kutompa Mkono Alikiba Katika Msiba wa Masogange
Msanii wa muziki Bongo, Harmonize amefunguka sababu ya kutompa mkono Alikiba pindi walipokutana katika msiba wa Agness Masogange.

Muimbaji huyo anayefanya vizuri na ngoma ‘Kwa Ngwaru’ ameiambia The Playlist ya Times FM kuwa mambo yote yanayozungumzwa si ya kweli, bali walisalimiana ila si kwa kushikana mikono.

“Unajua asilimia kubwa ya watu wanaozungumza hawakuwa pole, unajua unapomzungumzia Alikiba ni mtu ambaye amefanya muziki wetu upate heshima kwa namna moja au nyingine kama msanii namuheshimu siwezi nikakutana na mtu halafu nisimsalimie, sio kweli,” amesema.

“Kilichofanyika ni kwamba Diamond kamsalimia kwa mkono, wamesamiliana kwa mkono. Mimi nimekuja nimezunguka nikaona kwa kuwa Diamond kamsalimia kwa mkono, kamgeuzia kiganja mimi nikamsalimia kwa sauti tu, tukakaa pale tukaendelea,” amesisitiza Harmonize.

Soma Pia; Sijawahi kutamani kufanya kolabo na Alikiba – Harmonize

Diamond na Alikiba walikutana April 22, 2018 katika viwanja vya Leaders Dar es Salaam ambapo palikuwa panafanyika misa ya kuuaga mwili wa aliyekuwa video vixen Bongo, Agness Gerald ‘Masogange’ ambaye alifariki April 20, 2018 katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, Dar es Salaam.

Baada ya Erasto Nyoni Kufunga Goli Hii Hapa Kauli ya Samatta "Kumbe Umri ni Namba Tu"

$
0
0
Baada ya Erasto Nyoni Kufunga Goli Hii Hapa Kauli ya Samatta "Kumbe Umri ni Namba Tu"
Nyota wa Tanzania anayekipiga kwenye klabu ya soka ya KRC Genk inayoshiriki ligi kuu ya Ubeligji, Mbwana Samatta amefunguka kuhusu suala la umri kwa wachezaji na kusema kumbe ni namba tu.


Samatta ametumia mtandao wa Twitter kueleza hilo wakati akionesha kuridhishwa na kiwango cha mchezaji mkongwe wa Tanzania Erasto Nyoni, ambaye Jumapili alifunga bao pekee kwenye mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga.

Samatta aliandika ''Erasto Nyoni (umri ni namba tu kumbe)'',. Hatua hiyo imechukuliwa kama sehemu ya nyota huyo kutambua kiwango cha kiraka huyo wa Simba ambaye amecheza kwa misimu mingi katika kiwango cha juu.



Erasto Nyoni aliifungia Simba bao lililowapa alama tatu kwenye mchezo wa ligi kuu Jumapili iliyopita dhidi ya Yanga. Bao hilo alifunga dakika ya 37 kipindi cha kwanza.

Nyoni ameshawahi kuzichezea klabu tofauti tofauti hapa nchini na nje ikiwemno A.F.C Arusha, Azam FC na sasa Simba huku nje akiichezea Vital'O ya Burundi.

Lechantre: Erasto Nyoni Ndiye Mchezaji Bora Katika Kikosini Changu

$
0
0
Lechantre:  Erasto Nyoni Ndiye Mchezaji Bora Katika Kikosini Changu
ACHANA na bao alilolifunga dhidi ya Yanga, Kocha wa Simba, Pierre Lechantre amemtangaza beki wake kiraka Erasto Nyoni kuwa ndiye mchezaji wake bora kikosini mwake.



Nyoni katika mechi iliyopita dhidi ya Yanga, alifunga bao pekee lililoipa ushindi Simba wa bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.



Beki huyo mkongwe hivi sasa ni tegemeo katika kikosi cha Simba ambacho amejiunga nacho msimu huu akitokea Azam FC am­bako alimaliza mkataba wake.



Akizungumza na Cham­pioni Jumatano, Lechan­tre alisema ana kila saba­bu ya kumwagia sifa Nyoni kutokana na mchango mkubwa anaoutoa katika timu yake inayoongoza ligi ikiwa na pointi 62.



Lechantre alisema, beki huyo anatimiza vizuri majukumu yake katika ku­zuia na kupunguza hatari langoni, hivyo anastaili sifa za kuwa mchezaji bora na beki bora wa timu yake.



“Nyoni amekuwa katika kikosi cha kwanza cha timu yangu kutokana na jinsi anavyoweza kutimiza majukumu yake, ni ngumu kwangu kumuweka nje.



“Wachezaji wa aina ya Nyoni ndiyo ninaowahitaji katika timu yangu na hata ukiniuliza mchezaji gani bora wa mechi ya watani wa jadi kati ya Simba na Yanga nitamtaja yeye tofauti na bao lake alilolif­unga.



“Nyoni ndiye anayeion­goza safu ya ulinzi vizuri kwa kuwapanga mabeki wenzake na kuwakum­busha majukumu yao,” alisema Lechantre.


Kisa Ndoa Mwanaheri Apigwa Stop Kucheza Filamu

$
0
0
Kisa Ndoa Mwanaheri Apigwa Stop Kucheza Filamu
LICHA ya madai kwamba amepigwa stop kuendelea kucheza filamu na mumewe, Khamis baada ya kuolewa hivi karibuni, mrembo wa filamu za Kibongo, Mwanaheri Ahmed ‘Mwana’ ameibuka na kueleza ukweli.

Za Motomoto News ilizungumza na Mwana ambaye alifunguka kuwa, amekuwa akiyasikia madai hayo, lakini ukweli ni kwamba hata iweje, kamwe hawezi kuachana na kazi yake ya filamu kwani ni fani anayoipenda licha ya kuwa ana elimu kubwa, lakini aliachana na kuajiriwa na kufanya kile alichokuwa anakipenda na mumewe anaheshimu hilo.

“Mume wangu anaiheshimu na anaipenda sana kazi yangu hivyo hawezi kunizuia kuigiza, bado ninaendelea na sanaa kama kawaida maana ndoa hainizuii chochote,” alisema Mwana.

TUCTA Kuijadili Kauli ya Rais Magufuli

$
0
0
TUCTA Kuijadili Kauli ya Rais Magufuli
Katibu Mkuu wa chama cha Wafanyakazi nchini (TUCTA) Yahaya Msigwa, amezungumzia kauli ya Rais Magufuli juu ya kutoongeza mshahara kwa wafanyakazi, jambo ambalo limeonekana kuibua hisia hasi kwa watu wengi wakiwemo wanasiasa wenza na wafanyakazi wenyewe.


Akizungumza na www.eatv.tv. Bwana Msigwa amesema wao kama wawakilishi wa wafanyakazi, wanakusudia kufanya kikao maalum kujadili suala hilo, na kisha kulijadili na seriali kuangalia njia mbadala na muafaka.

“Mambo ya mishahara ni mambo ya utatu yaani wafanyakazi, waajiri na serikali, na mambo haya yanahitaji kujadili kwenye bodi, wafanyakazi wangependa kila mwaka kama inawezekana wawe wanapandishiwa mshahara, kwa hiyo hilo tutalijadili kama wafanyakazi halafu badaye tutajadiliana nao serikali”, amesema Yahaya Msigwa.

Hapo jana kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Me Mosi yaliyofanyika mkoani Iringa kitaifa, Rais Magufuli amesema hatoongeza mshahara wa wafanyakazi kwa sasa kutokan na serikali kijukita kwenye uboreshaji wa miundo mbinu.

Hiki Ndicho Alichokisema Wema Sepetu Kuhusu Ngoma Mpya ya Ommy Dimpoz

$
0
0
Hiki Ndicho Alichokisema Wema Sepetu Kuhusu Ngoma Mpya ya Ommy Dimpoz
Kimya kingi kina mshindo – Malkia wa filamu Bongo, Wema Sepetu ameshindwa kuzuia hisia zake kwenye wimbo mpya’Yanje’ wa Ommy Dimpoz ambao amemshirikisha Seyi Shay kutoka Nigeria.



Madam Sepenga amefunguka kuwa muziki wa aina hiyo ndio muziki anaoupenda na kumwambia msanii huyo kwa sasa anaimba muziki wa kikubwa.



Kupitia mtandao huo Wema ameadika:

Wanasemaga Kimya Kingi kina MSHINDO mkubwa… Ngoma Imenibamba Hatare… Sijui kwasababu ndo aina ya Mziki ninaopenda… Forever Bae Umemaliza wallahy… This One Is Just Amazing… 😍😍😍
.
.
.
Alafu kama naona GROWTH… Yaani Mziki unaoimba now kama wa Kikubwa zaidi… Keep it Up kipenzi… Umeua… Yaani Ni Balaa… Kazi Nzuri umefanya kummezesha Seyi Shai Swahili… 👏🏼👏🏼👏🏼
.
.
.
WellDone… You outdid yourself… Proud of You… Ladies & Gentlemen ebu tufanye kutembelea Bio yake @ommydimpoz tukaicheck hii video na tusikilize hii track… Ni Moto wallahy… .
.
.
Naona hii ulituliza kichwa kweli kweli… Wen you talk about Mziki Mzuri sasa ndo huu apa… 🙌🏼🙌🏼🙌🏼 cc @ommydimpoz @ommydimpoz @ommydimpoz @ommydimpoz

Aunty Ezekiel: Mchango wa Moze Kwangu ni Zaidi ya Pesa

$
0
0
Aunty Ezekiel: Mchango wa Moze Kwangu ni Zaidi ya Pesa
MSANII nyota wa filamu nchini, Aunty Ezekiel, amesema changamoto alizokutana nazo kwenye chumba cha kujifungulia ndio sababu ya kutunga na kuandaa filamu ya 'Mama' ambayo itazinduliwa Mei 13, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Slaam jana, Aunty Ezekiel, alisema  ameamua kuandaa filamu hiyo ili kuonyesha thamani ya mama na amepanga kuizindua kwenye Ukumbi wa Mlimani City.

Alisema lengo la filamu hiyo ni kuwafanya watu na jamii kwa ujumla kuona thamani ya mama na kuwaheshimu.

“Wakati nasubiri kujifungua nikiwa kwenye kile chumba nilipitia magumu ambayo najua mama yangu aliyapitia na baada ya hapo ndipo nikajua thamani ya mama, nilifikiria nimpatie zawadi gani, lakini nikaona ni bora nitengeneze filamu ili nionyeshe thamani ya mama,” alisema

Aidha, alisema mama mara zote amekuwa na mchango mkubwa katika jamii huku akipambana zaidi na familia ikilinganishwa na kina baba.

“Naweza nikasema mama ni muhimu kuliko baba na sisi tumekuwa haturudishi upendo kwa mama zetu kuhusiana na yale waliyotutendea, nikiwa kama msanii nimeona nije na kitu ambacho kitawarudishia thamani yao,” alisema.

Alisema katika movie hiyo ambayo ameifanyia katika Kijiji cha Kisarawe mkoani Pwani, ameshirikiana na mtoto wake (Cookie) na hakutaka kumshirikisha mumewe (Mose Iobo) kwa kuwa fani yake ni mnenguaji.

“Katika kazi zetu hatuingiliani hata siku moja hawezi kuniambia leo nikawe mnenguaji, hilo siliwezi na mimi siwezi nikamuambia aje kwenye movie kwa sababu hawezi ila kwa msaada ananipatia yaani ana msaada mkubwa sana kwangu zaidi hata ya pesa,” alisema..

Okoa Ndoa yako Sasa...Umepungukiwa na Nguvu za Kiume na Unashindwa Kupanda Mlima Vizuri

$
0
0
OKOA NDOA YAKO SASA : JE UMEPUNGUKIWA NA NGUVU ZA KIUME AU UUME WAKO MDOGO AU MPENZI WAKO HAKUTIMIZII UTAKACHO:


Acha kujiona mpweke pale ukutanapo na mpenzi au mke wako kwa sababu ya kutokuwa na nguvu za kiume au Uume wako mdogo

Dawa YA MAPRO POWERA ndio dawa sahihi na tiba tosha kwa sasa Kutibu tatizo na kuponesha kabisa tatizo LA KUWAI KUFIKA KILELENI KABLA MWENZI WAKO BADO AJAKOJOA

KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOA NA MWILI KUCHOKA

UUME KUSINYAA NA KUWA LEGELEGE

KUUMWA NA TUMBO WAKATI UNAPOMALIZA KUFANYA TENDO

Dawa hii utumiwa ata na wazee wenye umri mkubwa na haina madhara yoyote

MAKAKANUA HII NI dawa ya maumbili madogo urefusha na kunenepesha saizi upendayo saiz 5-6-7-8 na unene sm 3-4-5 kwa mini huabiki kwa kuwa na UUME mdogo wai sasa upate tiba sahihi kabisa na ni tofauti na ulizowai kutumia :

Tunarudisha mke au mpenzi ndani ya masaa matatu tu zipo dawa za presha kisukali vidonda vya tumbo korodani iliyovimba dawa za uzazi tunapunguza matiti makubwa kitambi na mwili mkubwa dawa zipo FIKA OFISINI KWANGU MBAGALA ZAKHEMU KWA WATEJA AMBAO AMTAKUWA NA NAFASI YA KUJA OFISINI AU MLIO MKOANI MTALETEWA p

Piga simu 0743362017 au 0789234653

DR AGU

Haji Manara Afunguka Kuondoka Simba

$
0
0
Haji Manara Afunguka Kuondoka Simba
Hatimae Msemaji wa Club ya soka ya Simba Haji Manara ameongea kuhusu taarifa za yeye kuacha kufanya kazi na Club hiyo ambayo juzi ilipata ushindi wa 1-0 vs Yanga uwanja wa Taifa.

Maneno ya Manara leo ni haya >>> “Siondoki Simba na naomba muelewe hvyo..ninafanya kazi sehemu sahihi na wakati sahihi….rafiki zangu na washabiki wa klabu muelewe hvyo..walichokitangaza ni uzushi…nawezaje kuwaacha simba kipindi hiki muhimu?”

Joyce Kiria: Siwezi Kuvumilia Ukatili na Machungu ya Ndoa Yangu

$
0
0
Joyce Kiria: Siwezi Kuvumilia Ukatili na Machungu ya Ndoa Yangu
Mwanaharakati na mtangazaji wa kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria amedai kuwa anapokea matusi na lugha za kebehi kutoka kwa watu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutamka wazi miezi mitatu iliyopita kuwa ananyanyaswa na mumewe kwenye ndoa yake.

Joyce amesema kuwa matusi hayo na lugha za kebehi kwake anaona ni jambo la kawaida na ni afadhali kwake lakini sio kuvumilia maumivu aliyokuwa akiyapata kwenye ndoa yake na mumewe Henry Kilewo.

“Nachotaka kusema ni kwamba kwa vile nilichangua hii kazi  ya kuwa sauti za wanawake najua gharama zipo, na gharama kubwa kabisa ni kutukanwa lakini sio kwamba mimi sioni hayo matusi nayaona lakini navumilia. Kwahiyo sio kwamba siumii naumia!! na kuna wengine wananikosesha dili za matangazo kwenye kipindi changu kwa kuona nimejiharibia na mambo ya kisiasa.“amesema Joyce Kiria kwenye kipindi chake cha Wanawake Live na kufafanua.

“Pamoja na machungu yote ninayoyapitia ya kutukanwa na kukosa wadhamini kwenye kipindi changu nikilinganisha na maumivu ya kwenye ndoa ni bora nitukanwe na jamii  lakini sio kuvumilia ukatili na machungu ya ndoa yangu.“amesema Joyce Kiria.

Mwezi Januari, Joyce Kiria aliutangazia umma kuwa yeye na mumewe hawapo sawa kwenye ndoa yao kwani amekuwa akipigwa na kuachiwa majukumu yote ya kifamilia.

Mwakyembe Amteua Frowin Nyoni Kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu

$
0
0
Mwakyembe Amteua Frowin Nyoni Kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amefanya uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Tanzania.

Viewing all 104755 articles
Browse latest View live




Latest Images