Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Naibu Waziri wa Afya Apiga Stop Upimaji wa DNA

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya  Apiga Stop DNA
SERIKLI kupitia kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile imekataza Mamlaka ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), kuruhusu watu au taasisi zisizo na mamlaka kisheria kuwaamuru kupima sampuli za vinasaba (DNA).
Dkt. Ndugulile aliyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa Bodi Tendaji ya GCLA yenye wajumbe saba kutoka Wizara yake, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Katiba na Sheria na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) huku akiziitaka mamlaka hiyo kutoa elimu kwa jamii kuhusu majukumu ya mamlaka hiyo, ili kuepuka watu au taasisi kutoa maagizo juu kwa mamlaka hiyo kinyume cha sheria na taratibu.
“Tusiamini kila mtu anajua utaratibu. Tunaweza sasa kuja kuvumbua mambo ambayo hayapo. Si kila mtu anaweza kuamrisha Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuchukua vipimo vya DNA, si hivyo kuna taratibu zake,” alisema.
Dkt. Ndugulile alisema lazima wananchi waelezwe taratibu zikoje, nani anawajibika kwenda kupeleka sampuli na nani ana wajibu huo kwa sababu majukumu yake ni ya kisheria huku akieleza katika siku za karibuni suala la kupima vinasaba limezungumziwa sana hali ambayo imezua mkanganyiko kwa jamii, hivyo kuitaka mamlaka hiyo kutimiza wajibu wa kutoa elimu.
Licha ya kutokumtaja mtu aliyetoa amri ya watu kupimwa DNA, hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, aliwaita watu waliodaiwa kutelekeza watoto kujitokeza ambapo baadhi yao walijitokeza, lakini 90 kati ya wanaume hao, waliwakana watoto waliodaiwa kuwa wamewatelekeza na kutaka waende wakapimwe DNA katika maabara ya Mkemia Mkuu ili kumaliza utata huo.
Katika hatua nyingine, Dk. Ndugulile aliitaka taasisi hiyo kuwa na mkaguzi wa kimataifa wa ubora wa sampuli wanazopima, ili zikubalike kitaifa na kimataifa.
“Lazima muwe na mkaguzi wa kimataifa wa kuthibitisha kile mlichopima kwa sababu taasisi hii ina majukumu ya kisheria ya kuamua ukweli kuhusu sampuli iliyopimwa. Mkisema huu ni unga wa mahindi ilhali tunaona ni dawa za kulevya hatuwezi kupinga,” alisema.
Pia aliitaka mamlaka hiyo kutoa majibu kwa wakati, ili kupunguza kesi zilizopo mahakamani zinazosubiri majibu ya maabara hayo.Alisema, ili kutekeleza agizo hilo, amewataka kuandaa mikataba inayoonyesha kazi itakamilika kwa muda gani pindi wanapopokea sampuli.
“Utakumbuka kuna wakati kesi zilirundikana katika mahakama zetu hivyo mnatakiwa kufanya kazi kwa haraka na kwa wakati na muwe na mikataba inayoonyesha kazi itakamilika kwa muda gani,” alisema.
Aidha, aliwataka kuwatambua wale wote wanaojihusisha shughuli za kemikali nchini wakiwamo, wauzaji, wanunuzi na wanaozitumia kwa ajili ya kupunguza matukio ya uhalifu nchini. Kadhalika aliwataka kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi na Mazingira (NEMC) kuthibiti majitaka katika viwanda, ili kuepusha madhara kwa watu.
“Sijawasikia mkipima maji taka yanayotiririka viwandani mmekaa kimya kama si wajibu wenu, hakikisheni mnashirikiana nao na kuchukua sampuli nyie wenyewe mpime na mtoe majibu,” alisema.
Naye Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk. Fidelice Mafumiko, alisema GCLA inakabiliwa na uhaba wa watumishi takribani 200 na pia uchakavu wa mitambo ya kimaabara. Dk. Mafumuko pia alisema fedha za bajeti ya serikali ya mwaka 2017/18 zilizotengwa kwa ajili ya kununua mitambo na vifaa vya maabara hiyo hazijatoka hadi sasa hali ambayo inawafanya kushindwa kutekeleza majukumu yako kikamilifu.
Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Prof. Ester Jason, aliahidi kuisumbua wizara hiyo kuhusu kutekeleza majukumu ya mamlaka ikiwa ni pamoja na kutoa fedha mapema iwezekanayo.

Baraka Da Prince Amtandika Mimba Mchepuko Wake na Kuikataa

$
0
0
Baraka Da Prince Amtandika Mimba Mchepuko Wake na Kuikataa
Mwanamuziki wa Bongo fleva Barakah The Prince amekumbwa na skendo nzito ya kumpachika mimba mwanamke mwingine ambaye ni mchepuko wake na sasa anadaiwa kuikataa mimba hiyo.

Miezi michache iliyopita kuna tetesi zilisambaa kuwa Barakah alionekana mkoani Mwanza na mwanamke mwingine ambaye ilidaiwa ni mchepuko wake wakila bata Kwenye hoteli ya kifahari.

Barakah alikana tetesi hizo na kudai kuwa ana mpenzi mmoja tu ambaye ni Naj na hana mwanamke mwingine na wanaosambaza taarifa hizo wanataka kumuharibia penzi lake na Naj.

Shilawadu wanaripoti kuwa msichana huyo mwenye kibendi cha Barakah anaitwa Naomi na ni mkazi wa Arusha na inasemekana hivi sasa Barakah anakataa mimba hiyo na tayari msichana huyo amesha mtafuta Naj kumuuliza.

Kwenye mahojiano na XXL ya Clouds Fm, Mchepuko huyo wa Barakah The Prince alifunguka haya kuhusiana na taarifa hizo:

"Nina mimba ya Barakah lakini hataki Habari za hiyo mimba na mimi nimeshamwambia mwanamke wake Najma. Mimi ninachotaka huyo barakah afikirie na atoe jibu moja kuhusi hii mimba maana mimi siwezi kutoa hii mimba".

Wema Amtumia Salamu Nzito Haji Manara Kisa Hiki Hapa

$
0
0
Wema Amtumia Salamu Nzito Haji Manara Kisa Hiki Hapa
Msanii Wema Sepetu, ametuma salamu kwa mkuu wa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Haji Manara, na kutamba kwa kusema, klabu ya Yanga ndio timu kubwa na yenye mafanikio hapa nchini na kitendo cha kufungwa na Simba katika mchezo wa April 29 ni sehemu ya mchezo tu.


Akiongea na waandishi wa habari leo Mei 02 wakati wa kutambulishwa kama balozi wa Startimes kueleka kombe la dunia, Wema amesema yeye ni mpenzi mkubwa wa timu Yanga na hata katika kuchukua ubingwa timu hiyo imefanikiwa zaidi kuliko wapizani wao simba.

“Mpelekeeni salamu Haji Manara, anajua kabisa kwamba Yanga tumechukua ligi (kuu bara) mara nyingi sana, kwa hiyo wao (Simba) kutufunga juzi ni changamoto, katika ubingwa huwa tunawachapa kilasiku”, amesema Wema

Haji Manara na msanii Wema Sepetu wamekua na tambo za maneno kuhusu timu za Simba Yanga hususani katika mitandao ya kijamii.

Akiongelea kuhusu nchi wakilishi wa bara la Afrika katika michuano ya kombe la dunia Wema amesema, bado kuna changamoto kubwa kwa nchi hizo kufanya vizuri katika michuano hiyo ukilinganisha na mataifa ya bara la Ulaya.

Bill Nass Afunguka Kuhusu Picha Zake Zinazosambaa Mtandaoni

$
0
0
Bill Nass Afunguka Kuhusu Picha Zake Zinazosambaa Mtandaoni
Rapa Billnass ambaye anatamba na ngoma ya 'Tagi Ubavu' amefunguka na kudai kipindi hiki kigumu anachokipitia kwa watu kuweka picha zake mitandaoni zikiwa zinamzungumzia ndivyo sivyo zinampa nafasi kubwa ya yeye kuwajua watu zaidi jinsi akili zao zilivyo katika kutafakari baadhi ya mambo.


Billnass amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI baada ya kuulizwa swali na muongozaji wa kipindi hicho Elbogast Myaluko kama alipata bahati ya kukutana na picha yake mitandaoni aliyopiga kwenye hafla ya harusi ya Alikiba siku za hivi karibuni iliyokuwa ikisambazwa na mashabiki zake ikiwa na ishara kama anakanda unga hivi.

"Ni kweli nimekutana nayo hiyo picha, lakini haipo kama watu wanavyoizungumzia na kuonekana, ile picha nilipigwa wakati nilikuwa naongea na mtu. Kwa bahati mbaya mimi nikiwa naongea huwa natumia ishara ya vitendo kwa sana, na pale nilipokuwepo palikuwa na kelele sana. Kwa hiyo sijui nilipigwa muda gani lakini watu waliikata nikaanza kuiona twitter", amesema Billnass.

Pamoja na hayo, Billnass ameendelea kwa kusema "kila mtu na akili yake unajua kuna watu wengine wewe unapomaliza kufikilia wao ndio wanaanza kwa hiyo kila mtu ana mpaka wake wa mawazo. Niliona lakini nikaona siwezi kujibizana na kila mtu. Haiwezi kuniumiza ila napata nafasi ya kuwajua watu zaidi jinsi walivyo".

Tukio la Mlinga Kumchoma Sindano Mwanafunzi Lazua Gumzo...... Waziri wa Afya Asema Sio Sahihi

$
0
0
Tukio la Mlinga Kumchoma Sindano Mwanafunzi Lazua Gumzo...... Waziri wa Afya Asema Sio Sahihi
KUFUATIA picha zilizosambaa mitandaoni zikimuonyesha Mbunge wa Ulanga, Morogoro (CCM), Goodluck Mlinga, kuonekana ameshika sindano kama anamchoma mwanafunzi chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi, jambo hilo limeibua hisia tofauti miongoni mwa wadau huku wakihoji kuhusu mtu asiye na taaluma ya afya anapata wapi mamlaka ya kutoa chanjo hiyo.


“Siasa imeingia sehemu mbaya sana, tiba si eneo la mzaha kiasi hiki, hili ni eneo hatari, na mchezo huu kwa afya za watu unaweza kusababisha maumivu hata ulemavu, si kila mtu anaweza kutoa chanjo,” alitoa maoni mmoja wa wadau kupitia mtanda wa Twitter.


Akijibu hoja hiyo kupitia akaunti ya Twitter, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema jambo hilo si sahihi kwani wanaotakiwa kutoa huduma za afya ni watu wataalamu wa tiba na si mtu mwingine huku akimuagiza katibu mkuu wa wizara hiyo kutoa maelekezo kwa waganga.



“Hii si sahihi, tayari nimeshamuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kutoa maelekezo mara moja kwa waganga wakuu wa mikoa na wilaya kusisitiza uzingatiwaji wa Miongozo ya Utoaji wa Huduma za Afya nchini, masuala ya kitaalamu yafanywe na wataalamu,” alisema Ummy.


Kitendo alichokifanya Mlinga kimeelezewa na baadhi ya watu kama kufanya mambo ya afya yawe ya  kisiasa japo haijulikani kama mbunge huyo alikuwa akimchoma kweli mwanafunzi huyo au alishika tu sindano mabegani mwake kama ishara ya uzinduzi wa chanjo na kuhimiza wanafunzi wajitokeze kupata kinga hiyo.


Hivi karibuni, Wizara ya Afya ilizindua chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wa umri wa miaka 14 ambayo inaendelea kutolewa nchi nzima, ili kuwakinga na matatizo hayo ambayo hupoteza idadi kubwa ya akina mama.

Kenyatta Awaomba Radhi Wananchi Wake "Nisameheni Tuungane Kurekebisha Majeraha "

$
0
0
Kenyatta Awaomba Radhi Wananchi Wake "Nisameheni Tuungane Kurekebisha Majeraha "
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewaomba msamaha wananchi wake wakati akilihutubia bunge la nchi hiyo ikiwa kuna jambo baya ambalo alilifanya likawaumiza wananchi wake, kwa njia yoyote ile ikiwa ni pamoja na kushindwa kuwaunganisha kipindi cha uchaguzi.


Kenyatta ameoomba msamaha huo mapema jana wakati akilihutubia bunge la nchi hiyo ikiwa  ni kawaida kwake kulihutubia bunge mara moja kwa mwaka.

"Forgive me. Nisameheni tuungane, tushirikiane kurekebisha majeraha tusahau yaliyopita," amesema Rais Kenyatta ambapo inaaminika alitumia saa moja na dakika 22 katika hotuba yake.

Akizungumzia kuhusu yeye kukutana na Kiongozi wa Muungano wa Upinzani nchi Kenya , Kenyatta amesema kwamba

“Wakati tulipokutana mimi na yeye (Odinga) mapema mwaka jana tulikubaliana kufanya kazi pamoja ili kuijenga nchi yetu hii. Tunaimani kabisa kwamba tutatumia muungano wetu kutatua kero za Wakenya".

Mrithi wa ‘Morgan Tsvangirai’: Mkinichagua Kuwa Rais Nitawafukuza Wachina Wote

$
0
0
Mrithi wa ‘Morgan Tsvangirai’: Mkinichagua Kuwa Rais Nitawafukuza Wachina Wote
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change (MDC) nchini Zimbabwe, Nelson Chamisa amesema kuwa atawafukuza wawekezaji wote kutoka China nchini humo endapo atachaguliwa kuwa Rais kwenye uchaguzi mkuu mwezi Julai mwaka huu.


Chamisa amesema kuwa Wachina wamekuwa wakitorosha rasilimali za nchi hiyo na uwekezaji wao umegubikwa na rushwa hivyo haoni sababu ya kuwaruhusu kufanya kazi nchini humo.

“Wawekezaji kutoka china ni moja ya watu wanaolifilisi taifa letu, wanachukua rasilimali zetu kwa kisingizio cha uwekezaji na wamesaini mikataba ya hovyo na serikali ya Zanu-PF sioni umuhimu wao ni bora tukaacha hizo rasilimali zikatumiwa baadae nawaahidi mkinichagua kuwa rais nitawafukuza wawekezaji wote Wachina na wengine ambao wataonekana na mikataba kama hiyo nitawatimua, tumechoka kunyonywa,“amesema Chamisa juzi Mei 01, 2018 mjini Harare kwenye maadhimisho ya siku yawafanyakazi duniani.

Zimbabwe inatajwa kuwa ni nchi ya nne barani Afrika kuwa na wawekezaji wengi kutoka China, na hoja hiyo inaungwa mkono na wabunge wengi hata wale wa chama tawala cha ZANU-PF.

Uchaguzi huo mkuu utakuwa uchaguzi wa kwanza na wa kihistoia nchini humo tangu utawala wa Robert Mugabe kuangushwa mwezi Januari mwaka huu.

Chamisa alitangazwa kuwa kiongozi wa chama cha MDC mwezi Februari akimrithi aliyekuwa kiongozi wa chama hicho, Morgan Tsvangirai  baada kufariki dunia.

Mpinzani mkubwa wa Chamisa ni Rais wa sasa wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa maarufu kwa jina la ‘Ngwena’ yaani MAMBA .

Mdogo wa John Heche Aliyeuwawa kwa Kuchomwa Visu Kuzikwa Leo

$
0
0
Mdogo wa John Heche Aliyeuwawa kwa Kuchomwa Visu Kuzikwa Leo
Mkazi wa Tarime, Chacha Suguta (27), anayedaiwa kuuawa kwa kuchomwa visu akiwa mikononi mwa polisi, anazikwa leo.

Msemaji wa familia ya Suguta, Wegesa Suguta ameiambia Mwananchi kuwa tayari mwili wa marehemu umewasili kijijini kwao Nyabitocho wilayani Tarime .

Suguta ambaye pia ni mdogo wa mbunge wa Tarime, John Heche, alifariki dunia Aprili 27 baada ya kukamatwa na polisi akiwa baa.

Suguta anazikwa wakati familia yake ikitangaza kuukataa msaada wa chakula uliotolewa na  polisi.

"Familia hatutapokea fidia kutoka kwa mtu wala taasisi yoyote. Lakini tunachoomba hili liwe tukio la mwisho raia kufia mikononi mwa polisi, siyo Tarime pekee, bali nchi nzima," amesema Heche

Tayari askari polisi William Marwa amefikishiwa mahakamani akidaiwa kumuua kwa kumchoma kisu Chacha usiku wa Aprili 27 katika tukio lililotokea eneo la Sirari, mpakani mwa Tanzania na Kenya.


Kutana na Mtaalam Sharif Hamad Kalala Mchambuzi wa Nyota za Binadamu na Tiba Asili

$
0
0
KUTANA NA SHARIF HAMAD KALALA NI
SHARIFU MCHAMBUZI WA
NYOTA ZA BINAADAMU NA NI MWENYE UPEO MKUBWA KUTAFITI MATATIZO YAKO KABLA YA KUTOA USHAURI WAKE WA TIBA AlJALISHI MBALI ULIKO TIBA YAKE UMFIKIA YEYOTE MWENYE UITAJI POPOTE
DUNIANI.

 SHARIF HAMAD KALALA NI TABIBU MWENYE KUBRI TOKA KWA ALAH ANATIBU KWA NJIA YA VITABU VYA QUR-AN, DAWA ZA ASILI ZA MITI SHAMBA PAMOJA NA DAWA ZA KIARABU.
ANATIBU KWA NJIA YA SIMU KWA KUTOA
MAELEKEZO NAMNA YA MATUMIZI YA DAWA UKIWA NCHI YOYOTE MKOA WOWOTE KWA MATATIZO YAFUATAYO:-

 KUFANIKISHA NDOA KWA UNAYE MPENDA KWA HARAKA. KUMRUDISHA MPEZI NDANI YA MASAA 12 TU.
 ULIJALI (NGUVU ZA KIUME) NDANI YA /IKI MMOJA TU
MIGUU KUWAKA MOTO KUTAFSIRI NDOTO MFARAKANO WA WANANDOA MFARAKANO KAZINIKUPANDISHWA CHEO NDANI YA SIKU SABA 7 TU.
KUTOA PETE YA BAHATI KUTOA MAJINI MACHAFU IKIWA NI KWENYE MWILI WA BINADAMU MAJUMBANI NA KWENYE BIASHARA. KUPATA MAFANIKIO YA MALI BILA YA MASHARTI. KUPANDIKIZANYOTA YA KUBASHIRI KUFUNGUA UZAZI KWA WALIYO FUNGWA KWA NJIA YA USHIRIKINA KUTOA VIFUNGO VYOTE VILIVYO FUNGWA KWENYE BIASHARA. ANA UWEZO MKUBWA WA KUPANDIKIZA NYOTA YA KUMPATA YEYOTE UMPENDAYE KWA KUMUOA AU KUWA NAYE. ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIYE MBALI PIA ALIYE CHUKULIWA
KWA NJIA YAMSUKULE
NAO UWEZO WA KUUA KESI SUGU NA MPYA NDANI SIKU 7 TU.
MENGINEYO MENGI ZAID YALIYO KUWA SUGU PIGA KWA WALE WALIYO ANGAIKA SEHEMU MBALI MBALI SHARIF HAMAD KALALA NI SULUISHO. ENDAPO UTAMSIKILIZA KWA YALE ATAKAYO KUSHAURI NA KUKUPA
ELEKEZI.
 TIBA NI KWA DINI ZOTE POPOTE ULIPO NJE NA NDANI YA NCHI.

MOBILE +255 -673 025 376
WhatsApp +255-757 069 066

Wanawake Mbele ya Pesa, Mimba na Ukimwi ni Matokeo tu

$
0
0

Kama ulikuwa huwafamu vizuri baadhi ya Dada zetu mjini,
Usitenge muda kuwafahamu, sababu utaweza kuwa chizi
Pesa wananusa kama sisimizi anavyo nusa sukari ipo wapi
Ukiwa na pesa ya kutosha utaweza kuwachanganya kijiji kizima
ukifulia kijiji kizima wanakuacha, utaanza kuonekana kama kituko

Aliye umba pesa Mr pilato kweli kaziloga. 
Ukiwa na pesa, wanawake wanacho itaji ni pesa yako tu. 
utumie condom, usitumie shauri yako
pesa imewatoa ufahamu kabisaaaaa

Gigy Money Atangaza Rasmi Hana Rafiki, "Hata Nepi tu Zinawashinda Sina Shoga Mjini "

$
0
0
Gigy Money Atangaza Rasmi Hana Rafiki, "Hata Nepi tu Zinawashinda Sina Shoga Mjini "
Mwanadada Gigy Money ametangaza kuwa kwa sasa hana rafiki kwa sababu aliyokuwa akiwategemea kama marafiki zake wameshindwa kujitokeaza hata kumpa nepi katika uzazi wake na kusema kuwa wamesahau kuwa alikuwa akiwasaidia kwa zaidi ya miaka saba mjini lakini leo hii kama vile hawajui kilichotokea kwake.

Katika ukurasa wake wa instagram, Gigy Money ameonekana kukerwa na baaadhi ya rafiki zake wa kike waliojifanya kuwa marafiki lakini sasa hivi wanakuwa hawajui kuwa amejifungua , aliandika

“Thanks aunty missa i love you shoga,jamani wengine mnajifanya mashost , twin boo , bae ila nepi tu zinawashinda natangaza rasmi sina shoga mjini hapa ni washkaji tu byee, #ushoagakazinaujuekujitoa.

Kwa hesabu za haraka haraka marafiki wa karibu wa Gigy money ni pamoja na Amber Lulu pamoja na Tunda ambao walikuwa karibu nae , ingawa madongo haya hayajaweka wazi yamemlenga nani lakini ni marafiki wa karibu wa Gigy money.

Wema Sepetu Abadili Gia Wasafi TV, Atupilia Mbali Kipindi Chake

$
0
0
Wema Abadili Gia Wasafi TV
Baada ya Mrembo Wema Sepetu kuweka wazi anakuja na TV Show yake ndani ya Wasafi TV, amefunguka nini hasa kinaendelea kwa sasa.

Kipya cha kufahamu ni kwamba kipindi hicho cha Wema Sepetu hakitakuwa reality show kama ilivyokuwa mwanzoni kikiruka EATV.

“Kitakuwa ni kipindi cha tofauti tutakuwa wanadada watatu. Sitapenda kuweka wazi zaidi lakini haitakuwa reality show, kama itakuwa ni reality show nitaweka kwenye App yangu,” Wema ameiambia Bongo5.

“Bado hatujaanza ku-shoot kwa sababu sasa hivi bado wanafanya majaribio, kwa hiyo ile process nzima ya vipindi bado haijanza, so content zipo pale pale na tutaanza ku-shoot hivi karibuni,” ameongeza.

Utakumbuka hapo awali Wema Sepetu ndiye alikuwa wa kwanza kuweka wazi kuwa Diamond atakuwa Boss wake kupitia Wasafi Tv.

Msanii Majuto Kuomba Msaada ni Udhalilishaji – Mlela Afunguka

$
0
0
Majuto kuomba msaada ni udhalilishaji – Mlela
Muigizaji wa filamu Bongo Yusuph Mlela, amesema kitendo cha Mzee Majuto kuomba msaada kwa watu mbali mbali ili aweze kwenda kupata matibabu,ni udhalilishaji mkubwa.


Mlela ameyasema hayo kwenye eNewz ya East Africa Television, na kueleza kwamba wao kama wasanii wanatakiwa wajifunze, kwani kitendo cha msanii mkubwa kama yule kukosa matibabu kwa kutokuwa na pesa sio kitu sahihi na inaonesha ni jinsi gani wasanii wako chini kiuchumi, licha ya kazi nyingi na matangazo mbali mbali ambayo amewahi kuyafanya.

“Kiukweli si sahihi inanionesha ni jinsi gani bado tuko chini, kuomba msaada vile ni udhalilishaji, sisi ambao tuko kwenye game na umri unaruhusu tuchukulie kama changamoto tujipange kama binadamu, haya yasiendelee kujitokeza”, amesema Yusuph Mlela.

Kutokana na hilo Yusuph Mlela ameitaka serikali kutia mkono wake na kusimamia haki na kazi za wasanii, ili waweze kuingiza kile ambacho wanakitolea jasho kwa usahihi.

Mabosi wa Kampuni Iliyokuwa na Mkataba na Mzee Majuto Waswekwa Rumande

$
0
0
Mabosi wa Kampuni Iliyokuwa na Mkataba na Mzee Majuto Waswekwa Rumande
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa kuna Kampuni iko Mwanza iliingia Mkataba na King Majuto na Mkataba huo ulikuwa ni wakumlipa Milioni 24 wakatoa check, check hiyo ikawa haina Pesa, Hivyo serikali imewachukulia hatua wahusika.

“Naomba niwaeleze wananchi Nimeunda jopo la wanasheria na tumeshaanza kikao cha kwanza sasa hivi kazi yetu kubwa kwasababu tumeshaanza na suala la Mzee Majuto ni kuangalia kazi zote akizokwisha zifanya na tunawaandikia barua wote waliohusika watupe mikataba wanayoijua wao tutakaa nao tuanza kuchambua mkataba mmoja baada mwingine na tutawataarifu itakavyo fuatia,” amesema Dkt. Mwakyembe
“Kuna kampuni moja ya Mwanza waliingia Mkataba na King Majuto na Mkataba huo ulikuwa ni wakumlipa Milioni 24 wakatoa check, check hiyo ikawa haina Pesa tunashukuru uongozi wa Mwanza kwa kushirikiana nao wahusika wako ndani na tutaendelea kuchukua hatua kali kwa watu ambao wanadhani wanaweza kutumia jasho la wenzao kujinufaisha wenyewe,” alisisitiza.

Je Wajua..Mwanaume Ufikiria Kufanya Mapenzi Kila Baada ya Masaa 48?

$
0
0

 Umewahi kusikia kauli hizi? " Mume wangu hatosheki kitandani..""..Sidhani kufanya mapenzi ndio liwe jambo la msingi lakini huyu mwanaume kaa! Basi tu kila siku mpaka kero.."
Bila shaka ni kilio cha wanawake wachache walioamua kusema. Hivi kweli ni mara ngapi au kiasi gani tuseme inatosha? Je wanaume wanafanya makusudi? Je kuna uwezekano wakabadilika?

Katika mapenzi, suala la kumtaka mwenza kimapenzi hutegemea sababu nyingi, chache ni uwezo wa kiafya, utayari wa kihisia, usalama wa kazini na mengineyo. Japokuwa jinsia zote huwa na kiu ya mapenzi lakini wanaume huwa ni zaidi.

Daktari David Reuben anasema kuwa ".. Wanaume wengi huzungukia ktk mzunguko wa saa 48 yaani huhitaji kukutana kimwili kila baada ya saa 48 ili wawe ktk hali njema ya kimwili na kiakili..."
Nae Daktari na mwandishi Dr Herbert Miles anasema ".. Mwanaume mwenye afya njema mbegu hujaa kila baada ya saa 42 hadi 78 na kuzalisha nguvu kali inayohitaji zitolewe.."

Pia mwanasayansi Alan Frome anasema kuwa '.. Wanaume wanaonekana kuwa na njaa ya kukutana kimwili kwa sababu ya maumbile ambapo prostate gland ina kifuko kidogo kitunzacho mbegu, na kijaapo, mwanaume huhitaji kuzitoa, presha huzidi zaidi na zikitoka hurudi ktk hali yake ya kawaida.."

UPANDE WA WANAWAKE
Wanawake hutofautiana kabisaa na wanaume hali kadhalika na wao kwa wao. Kwa mujibu wa utafiti wa Johnson Masters 2010, kwa wastani 20-25% ya wanawake huwa na mtazamo hasi au vuguvugu ktk kuhitaji kukutana kimwili.
2% hawajali kabisa kuhusu kukutana kimwili.
25% zaidi huhitaji sana, husaka kukutana kimwili na huanzisha hitaji hili hata kabla ya mwanaume kusema.
50% iliyobaki huwa na uhitaji wa wastani tu.
Ifahamike pia hasa kwa wanaume kuwa, hali ya mwanamke hubadilika sana ktk kuhitaji tendo la ndoa ktk kipindi cha mzunguko wa siku zake.
Lakini mwanamke anapofikia miaka 40+ hitaji la kukutana kimwili hulingana karibu na lile la mwanaume

NINI KIFANYIKE
Wanaume ambao hawajaoa wanapaswa wajike sana ktk shughuli za uzalishaji mali zinazochosha mwili au mazoezi na kuepuka mambo yanayochochea hisia za mapenzi hapo wataishinda saa ya 48, Walio ktk ndoa wawe na utaratibu unaokubaliana na hali ya mwanamke na wajenge mazoea ya kufanya romansi sana ili kuendana na mabadiliko ya mwanaume na kuepusha utumwa wa ngono ndani ya ndoa au kukimbilia nje ya ndoa hali inayoleta magonjwa, kutelekeza familia na mengineyo yasiyoleta furaha ya familia

By Himidini

Hii Hapa Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo ya Uume

$
0
0

Tatizo hili limekuwa likiwaadhiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baada ya kujiona wapo tofauti sana na wengine kwa kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi 6-8 kwanza upungufu wa vichocheo hivi huchochea ukuaji wa uume chongo ambalo hushambulia nerve ambayo uharibu kabisa ukuaji wa uume, ngiri, punyeto, ambayo huathili misuli ya uume, ngiri huleta maumivu, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, korodani moja kuvimba, kutopata choo vizuri, sababu hizi hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na mara nyingi hata nguvu za kiume ( hamu ya tendo la ndoa) hupungua na kwisha kabisa

GEMBE :Ni dawa inayozalisha na kukufanya uume kukua na kuongezeka
NGEMO : Ni dawa bora ya kuongeza nguvu za kiume

Hukutia hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi mara4 nne bila kukinai au kuchoka pia itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk30-45 kwa mtumiaji pia tunatibu kisukari, bp, ngiri, miguu kuwaka moto KAMA HUNAMDA WA KUFIKA OFISINI KWETU UTALETEWA POPOTE TUPO MBAGALA RANGI3 0753471612/ 0715249530
0623 386 305

Kwani Kusoma ni Kujua Kiingereza? – Rais Magufuli ahoji

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli amehoji wanafunzi wa chuo cha Mkwawa iwapo  kujua kusoma ni kujua Kiingereza.

Rais Magufuli ameyasema hayo jana , Mei 2 wakati akizungumza na wanafunzi pamoja na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa, kilichopo mkoani Iringa wakati akitoa ufafanuzi wa shule za private na shule za Sekondari.

''Eti mtu amemaliza form four halafu hajui kuandika barua ya Kingereza, kwani kusoma ni kujua Kingereza!? Warusi wanajua Kingereza!? Kwani Wachina wanajua Kingereza !? Mbona wanatengeneza silaha za kila aina" !?

Aidha Rais Magufuli amesema kuwa “Shule za private wanafunzi wake wanachujwa, wakifika form 2 kuingia form 3 wanawachuja tena. Wanabaki na ile cream ili waonekane wanaongoza. Serikali inayowapenda wananchi wake haiwezi ikafanya hivyo.”

==>>Msikilize hapo chini

Rais Magufuli Awajibu Wanaokosoa Mpango wa Walimu wa Sekondari Kupelekwa Shule ya Msingi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewajibu watanzania ambao wanakosoa mpango wa serikali wa kuwapeleka walimu wa sekondari kufundisha shule ya msingi.

Rais Magufuli amesema kuwa kitendo hicho ni cha kawaida kwani hakiadhiri mishahara yao bali kinawapa muda mwingi walimu hao kufanya kazi nyingine za ziada.

“Wakati wa Nyerere walikuwa wanachukuliwa walimu wa UPE kwenda kufundisha shule za msingi. Sasa tunachukua wenye digrii. 

"Kikubwa kinachoangaliwa ni mshahara wake tu.. Kwa sababu mshahara unapimwa si kwa vile unafundisha shule ya msingi, ni kutokana na Qualification zako. 

"Tena kule ni kurahisi tu unaweza kufanya na mambo yako mengine.“alisema Rais Magufuli jana Mei 2, 2018 wakati akizungumza na wafanyakazi na wanafunzi  wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa, kilichopo mkoani Iringa.

Rais Magufuli alitolea mfano wa nchi zinazotumia Maprofesa kufundisha shule ya msingi;  “Ukienda nchi za Scandinavia utakuta maprofesa ndiyo wanafundisha chekechea, na mishahara yao ni mikubwa kuliko wanaofundisha chuo kikuu. Just mind set.”

Mwezi Februari mwaka huu serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ilitangaza kuwa baadhi ya walimu wa masomo ya sanaa kutoka shule za sekondari watapelekwa shule za msingi ili kukidhi mahitaji.

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo

$
0
0

Breaking News: Bodi ya Ligi Yamsimamisha Kelvin Yondani Kuchezea Yanga

$
0
0
Breaking News: Bodi ya Ligi Yamsimamisha Kelvin Yondani Kuchezea Yanga
Bodi ya Ligi Tanzania, imetangaza kumsimamisha beki wa Yanga, Kelvin Yondani kutokana na kuonekana katika video akimtemea mate beki, Asante Kwasi.

Mtendani wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amezungumza hivi punde na kusema suala lake limepelekwa Kamati ya nidhamu baada ya kuonekana haliwezi kusikilizwa na Kamati ya Saa 72 iliyokaa.

"Kwa hiyo sasa tunamsimamisha hadi hapo kamati itakapokaa na kuamua kuhusiana na suala lake," alisema Wambura.

Katika picha ya video ilimuonyesha Yondani akimtemea Kwasi raia wa Ghana katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyowakutanisha watani wa jadi, Yanga na Simba ambao walishinda kwa bao 1-0.

Suala hilo lilizua mjadala mkubwa miongoni mwa wadau, wakiwemo waliomtetea Yondani na walioona haikuwa sahihi.

Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images