Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live

Mwizi Ajisalimisha Polisi Baada ya Mzigo Alioiba Kumnasa

0
0
Mwizi Ajisalimisha Polisi Baada ya Mzigo Alioiba Kumnasa
KIJANA Frank Japhet (23), mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam, amelazimika kujisalimisha katika Kituo cha Polisi Mlandizi, Kibaha, Pwani, baada ya mzigo wa mahindi unaokadiriwa kuwa na uzito wa kilogramu 20, anaodaiwa kuuiba kung’ang’ania mabegani.



Wakati akihojiwa kituoni hapo, mtuhumuwa huyo amesema mzigo huo, uliofungwa kwenye kiroba aliuiba kwa mama mmoja eneo la Mtaa wa Nyambwiro, Mlandizi, Kibaha, mkoani Pwani majira ya saa 7.00 usiku wa kuamkia leo Mei 3, 2018, akaongeza kwamba aliondoka na mzigo huo hadi eneo la Stendi ya Mlandizi alipokuwa auache kwa mwenzake ili arudie mzigo mwingine, ambapo mzigo huo uling’ang’ania kichwani.


Ameendelea kusema kwamba alijitahidi kufanya kila aliloweza ili mzigo huo utoke kichwani ikiwa ni pamoja na kulala ili akinyanyuka ubaki chini lakini aliponyanyuka, alinyanyuka nao kichwani! Baada ya kuzunguka nao kwa muda mrefu, alidai alichoka hivyo akalazimika kujisalimisha polisi ili asije akauawa na raia wenye hasira watakapobaini kuwa ni mwizi.


Japhet mpaka sasa yuko Kituo cha Polisi Mlandizi na mzigo wake kichwani akisubiri mwenye mali aliyoiiba na Jeshi la Polisi Mlandizi tayari limemuita afike kituoni hapo. Tutawaletea taarifa zaidi za tukio hilo.

Mtandao wa www.globalpublishers.co.tz umempigia Mkuu wa Kituo cha polisi kuzungumzia tukio hili na haya ndiyo yalikuwa majibu yake:

“Mimi siyo mzemaji wa Jeshi la Polisi, mtafute Kamanda wa Polisi (RPC) atakueleza kila kitu, kama atakosa mtafute hata msaidizi wake.”

Baada ya kumtafuta Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwanai, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shanna alisema:

“Ni kweli tukio hilo limetokea usiku wa kuamia leo, na hapa nipo kwenye kikao nikitoka tu nitafanya press (mkutano na wanahabari) kuhusu tukio hilo saa 7:30 mchana,” alisema Kamanda huyo.

Hivi Ndivyo Mbunge wa Chadema Alivyommwagia Sifa Rais Magufuli

0
0
Hivi Ndivyo Mbunge wa Chadema Alivyommwagia Sifa Rais Magufuli
Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amefagilia Rais  John Magufuli kwa juhudi zake za kuimarisha miundombinu ya uchumi ikiwemo miradi ya barabara na maji bila kujali majimbo yanayokaliwa na vyama vya upinzani.





“Msigwa amesema hayo jana Mei 2, 2018 baada ya uzinduzi wa barabara ya Ipogolo mkoani humo na kuongeza kuwa Rais Magufuli habagui vyama kama ambavyo huwa anasema kwamba ‘Maendeleo hayana vyama’. Mbunge huyo alienda mbele zaidi na kufafanua mambo ambayo Rais ameyafanya kwa Mkoa wa Iringa tangu aingie madarakani mwaka 2015.



“Mhe. Rais umekuwa ukisisitiza katika hotuba zako kuwa wewe hujali mambo ya vyama, na hii imedhirika kuwa kweli hujali vyama, umesaidia sana, hela za kutoka kwako zimekuja nyingi. Kama alivyosema Mhe. Mahiga, kuna barabara nzuri katika kipindi chako ambacho umekuwa Rais, umejenga barabara ya lami kutoka Mlandege mpaka kwa Mkuu wa Wilaya karibu Shilingi Bilioni 3.5.

“Tuna stendi nzuri ipo Ipogolo ya karibu Shilingi Bilioni 3, tuna maji, kwa hiyo kuna vitu vimefanyika kwa kweli Mhe. Rais hupendelei, hela zinakuja hata sisi ambao ni wa CHADEMA unaleta hela, kwa hiyo tunakupongeza sana,”  alisisitiza mbunge huyo.

Davido Aonyesha Jeuri ya Pesa Akataa Dili la Milioni 60 la Mpenzi Wake

0
0
Davido Aonyesha Jeuri ya Pesa Akataa Dili la Milioni 60 la Mpenzi Wake



Staa wa muziki kutokea Nigeria Davido ameweka hadharani kuwa hataki mpenzi wake Chioma apewe ubalozi kwenye kampuni yoyote kwa shillingi Milioni 60 atakubali tu kama deal hilo litakuwa la Milioni 100 na labda atafikiria kuhusiana na hilo.

Davido ameyasema hayo kupitia account yake ya twitter ambapo ameandika “Nimepata offer ya Milioni 60 za mradi wa mpenzi wangu lakini nimewaambia walete milioni 100 labda atafikiria”



Davido na Chioma inasemekana kuwa wamekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa miaka mitano na pia kitu ambacho kilibeba headlines  kwenye mitandao ya kijamii ni kuhusu Davido kumzawadia Chioma gari aina ya porshe lenye gharama zaidi ya shillingi milioni 200 kwenye birthday yake.

Utani wa Barnaba kwa Billnass “Nakuogopa Labda Uje Mikono Umekata”

0
0
Utani wa Barnaba kwa Billnass “Nakuogopa Labda Uje Mikono Umekata”
Leo May 3,2018 kutana na comment ya staa wa muziki wa Bongo Fleva Barnaba akimjibu Billnas kupitia ukurasa wake wa instagram ambapo amepost video ya msichana ambaye inasemekana ndiye mpenzi wake wa sasa wakiwa pamoja studio .

Billnass baada ya kuona post hiyo aliamua kuandikia comment inayosema >>>“Kaka upo nae studio hapo? nataka nije kurecord kaka ile ngoma yetu classic ndio muda wake” na baada ya muda Barnaba alionekana kumjibu Billnass na kusema “studio nimefunga mdogo wangu kwa muda nakuogopa sana mdogo wangu labda uje mikono umekata”
Kutokana na comment hiyo ya Barnaba mashabiki wengi wameihusisha na video ya Billnass na Nandy iliyovuja na kuzua gumzo kwenye mitandao ya kijamii ikiwaonyesha wakiwa mapenzini siku kadhaa zilizopita.

Yanga Yaagizwa Kumuonya Obrey Chirwa

0
0
Yanga Yaagizwa Kumuonya Obrey Chirwa
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa) katika kikao chake cha Mei 1, 2018 chini ya Mwenyekiti wake Bw. Clement Sanga ilipitia matukio mbalimbali ya Ligi Kuu ya Vodacom, na malalamiko ya klabu za Yanga na Arusha FC na kuyafanyia uamuzi.


Kwa vile mchezaji Obrey Chirwa wa Yanga alionywa kwa kadi ya njano kwa kosa la kumsukuma mchezaji wa Mbeya City ingawa kwenye picha za televisheni inaonekana kama alipiga kiwiko, Kamati haikutoa adhabu nyingine kwa vile tayari ameadhibiwa.


Hata hivyo, klabu ya Yanga imeandikiwa barua kuhusu kumuonya mchezaji huyo kwa vile kumbukumbu zinaonyesha ameshafanya matukio ya utovu wa nidhamu mara kadhaa akiwa uwanjani.

Okoa Ndoa yako Sasa...Umepungukiwa na Nguvu za Kiume na Unashindwa Kupanda Mlima Vizuri

0
0
OKOA NDOA YAKO SASA : JE UMEPUNGUKIWA NA NGUVU ZA KIUME AU UUME WAKO MDOGO AU MPENZI WAKO HAKUTIMIZII UTAKACHO:


Acha kujiona mpweke pale ukutanapo na mpenzi au mke wako kwa sababu ya kutokuwa na nguvu za kiume au Uume wako mdogo

Dawa YA MAPRO POWERA ndio dawa sahihi na tiba tosha kwa sasa Kutibu tatizo na kuponesha kabisa tatizo LA KUWAI KUFIKA KILELENI KABLA MWENZI WAKO BADO AJAKOJOA

KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOA NA MWILI KUCHOKA

UUME KUSINYAA NA KUWA LEGELEGE

KUUMWA NA TUMBO WAKATI UNAPOMALIZA KUFANYA TENDO

Dawa hii utumiwa ata na wazee wenye umri mkubwa na haina madhara yoyote

MAKAKANUA HII NI dawa ya maumbili madogo urefusha na kunenepesha saizi upendayo saiz 5-6-7-8 na unene sm 3-4-5 kwa mini huabiki kwa kuwa na UUME mdogo wai sasa upate tiba sahihi kabisa na ni tofauti na ulizowai kutumia :

Tunarudisha mke au mpenzi ndani ya masaa matatu tu zipo dawa za presha kisukali vidonda vya tumbo korodani iliyovimba dawa za uzazi tunapunguza matiti makubwa kitambi na mwili mkubwa dawa zipo FIKA OFISINI KWANGU MBAGALA ZAKHEMU KWA WATEJA AMBAO AMTAKUWA NA NAFASI YA KUJA OFISINI AU MLIO MKOANI MTALETEWA p

Piga simu 0743362017 au 0789234653

DR AGU

Staili ya Ushangiliaji ya Haji Manara ya Ushangiliaji Yamtokea Puani Apewa Onyo Kali na Kamati ya Ulinzi

0
0
Staili ya Ushangiliaji ya Haji Manara ya Ushangiliaji Yamtokea Puani Apewa Onyo Kali na Kamati ya Ulinzi
Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani wake Yanga mwishoni mwa wiki.

Furaha hiyo ilimfanya msemaji wao kuingia uwanjani kumalizia shangwe na mashabiki wao.

Lakini Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa) katika kikao chake cha Mei Mosi, 2018 chini ya Mwenyekiti wake, Clement Sanga ilipitia matukio mbalimbali ya Ligi Kuu ya Vodacom, na malalamiko ya klabu za Yanga na Arusha FC na kuyafanyia uamuzi.


Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amepewa Onyo Kali kwa kuingia uwanjani kushangilia ushindi wa timu yake baada ya mchezo kumalizika.

Kitendo chake ni ukiukwaji wa Kanuni ya 14 (11) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo, na adhabu dhidi yake imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Mlinga Aomba Radhi Watanzania Baada ya Kujigeuza Daktari Kumchoma Sindano Mwanafunzi

0
0
Mlinga Aomba Radhi Watanzania Baada ya Kujigeuza Daktari Kumchoma Sindano Mwanafunzi
Mbunge wa Ulanga (CCM) Goodluck Mlinga amewaomba radhi Watanzania kwa tukio alilolifanya la 'kujigeuza daktari.'

Akizungumza na MCL Digital katika viwanja vya Bunge leo Mei 3, 2018, amesema aliitwa kuhudhuria uzinduzi wa chanjo na wala yeye si mtaalamu wa afya.

"Kitaalamu mimi ni mtawala si daktari, nilifanya nilivyoelekezwa na sikufahamu madhara yake wanasema kitabibu huruhusiwi kushika hata sindano," amesema Mlinga na kuongeza:

"Kuomba msamaha si woga, sisi tulioendelea nasema kunradhi."

 Mlinga amesema hayo baada ya picha yake kuzagaa katika mitandao ya kijamii ikimuonesha anamdunga sindano binti wakati wa uzinduzi wa chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana jimboni mwake.

 Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alizungumzia suala hilo bungeni na kusema ingawa viongozi hao hawakuwachoma sindano lakini ni makosa kushika hata sindano.

Kitale Alipua Steve Nyerere Asema Sio Mchekeshaji

0
0
Kitale Alipua Steve Nyerere Asema Sio Mchekeshaji
Mchekeshaji Mkude Simba amejibu hoja za Steve Nyerere kuhusu tuzo za za Sinema Zetu International Film Festival Awards (SZIFF), huku akidai yeye si mchekeshaji.

Hapo awali Steve Nyere alihoji ni kwanini Ray, JB, Rich, Roams, Aunt Ezekiel, Shamsa Ford, Duma, Weru, Hemedi, Tausi Mndengela, Mainda, Johari, Uwoya, Marian Ismail na Batuli hakushiriki tuzo hizo.

“Ambao movie tunazimiliki hatujauza haki zetu kwa muhindi ndio tuliweza kushiriki katika tuzo zile, lakini haimaamishi kwa wachekeshaji hote wawepo,” Mkude Simba ameiambia Bongo5.

“Hapana si hivyo, sijajua kuhusudio lake Steve Nyerere lakini huwa naamini mimi bado mchanga, bado najifunza kila siku. Mtu akiniambia mimi si mchekeshaji huwa nakubali na kweli mimi sio mchekeshaji ila nyuma yangu ndio kuna Bwakyila na Mkude Simba,” amesisitiza.


Tuzo za za Sinema Zetu International Film Festival Awards (SZIFF), zilitolewa April 01, 2018 ambapo muigizaji Gabo aliibuka na tuzo tano huku Wema Sepetu akishinda tuzo mbili.

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa Simba Said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

0
0

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo..

anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.


Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Issa simba said Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto.

Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA.

Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

+255 622588038 au 0679119679 au
+255 764318107

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Serikali imetoa kondomu 3,000 kwa waathirika 6,000 wa mafuriko

0
0

KENYA: Serikali imetoa kondomu 3,000 kwa waathirika 6,000 wa mafuriko waliopiga kambi katika Shule ya Garashi

Kwa mujibu wa Waziri wa Afya Dkt. Anisa Omari amesema pia wameongeza huduma za afya kwa waathirika wote katika kambi hiyo

Waathirika hao waliokuwa wakiishi katika eneo la Malindi waliomba kusambaziwa mipira hiyo ili kujikinga na magonjwa mbalimbali ikiwamo UKIMWI

Mmoja ya waliohojiwa amesema katika kambi hiyo kuna vijana ambao bado damu zinachemka hivyo kuna uwezekani kati yao wakaanza kufanya mapenzi na kusambaza magonjwa

Serikali inapanga kuwapelekea kondomu nyingi zaidi.

Mzigo Wang'ang'ania Kichwani Kwa Mwizi Baada ya Kuuiba...Ajipeleka Polisi

0
0

MLANDIZI, PWANI: Kijana Frank Japhet(23) alazimika kujisalimisha Kituo cha Polisi baada ya mzigo wa Mahindi(Kg 20) anaodaiwa kuuiba kung'ang'ania kichwani

Kijana huyo ameeleza kuwa mzigo huo aliuiba kwa Mama mmoja eneo la mtaa wa Nyambwiro, Mlandizi, Pwani

Ameongeza alipoondoka na mzigo huo hadi eneo la stendi ya Mlandizi ili auache kwa mwenzake kisha arudie mzigo mwingine, mzigo huo uling'ang'ania kichwani

Baada ya jitihada nyingi za kuutoa kichwani pamoja na kuzunguka nao kwa muda mrefu, amedai kuwa alichoka hivyo akalazimika kujisalimisha Polisi ili asije akauawa na raia wenye hasira watakapobaini kuwa ni mwizi.

TRA Yapewa Onyo na Serikali

0
0
TRA Yapewa Onyo na Serikali
Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutotumia lugha ya kuudhi au kutumia nguvu pindi wanapokusanya kodi kwa wafanyabiashara.



Badala yake amewataka kuwaelimisha wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kulipa kodi na kuwaeleza ni kwa kiasi gani kodi hiyo imefikia.

Waziri Mkuu amesema hayo, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Tunduma, Frank Mwakajoka aliyehoji kuhusu kauli ya Serikali juu ya usumbufu unaoletwa na TRA kwa wafanyabiashara wakati wa kukusanya kodi.

“Serikali imeunda chombo cha kusikiliza kero za wananchi ndani ya TRA lakini kama hawatasikilizwa wanauwezo wa kupeleka kero zao Wizara ya Fedha au kwa kiongozi yoyote mkubwa katika eneo lake kama vile Mkuu wa Mkoa au Wilaya,” alisema Waziri Mkuu.

“Wafanyabiashara wote kwanza wawe na amani katika kufanyabiashara zao nchini na wawekezaji wote waendelee kuwekeza na kuongeza mtaji zaidi ili kuekeza zaidi kwa sababu serikali imedhamiria kufungua milango ya uwekezaji nchini. Tunajua kwamba kodi ni wajibu wa kila mmoja kadiri ya shughuli zake zinazomletea mapato ilivyo kwa ukubwa wake. Kwa hiyo tumeielekeza TRA ihakikishe inapokwenda kukusanya kodi haitumii lugha ya kuudhi wala nguvu”, amesema Majaliwa.

Aidha ameitaka Mamlaka hiyo kufanya kazi kwa weledi na kuwa na mazungumzo na wafanyabiara. Pia tathmini ya kodi isiwe kiwango kikubwa kuliko mtaji wa mfanyabiashara.

Hata hivyo amesema hatua zitachukuliwa kwa yeyote ambaye hatatumia utaratibu mzuri wa kukusanya kodi na amewataka wafanyabiashara kufanya biashara kwa amani.

Rais JPM Aomba Msaada Serikali ya Denmark

0
0
Rais JPM Aomba Msaada Serikali ya Denmark
Rais John Magufuli ameiomba Serikali ya Denmark kusaidia ujenzi wa kipande cha barabara ya kilomita 11 katika Mkoa wa Iringa ili kuwezesha malori kutopita katikati ya mji huo ikiwa ni pamoja na kupunguza ajali zinazotokea.


Rais Magufuli ombi hilo wakati akizindua barabara ya Iyovi – Iringa – Mafinga yenye urefu wa kilomita 218 iliyojengwa kwa mkopo nafuu kutoka serikali ya Denmark na kugharimu Sh283 bilioni.

Akitoa maelezo wakati akiomba msaada huo Dk. Magufuli amesema mpango huo ulikuwepo tangu alipokuwa wizara ya ujenzi na kufafanua kwamba malori yanayopita katikati ya mji wa Iringa yamekuwa yakisababisha ajali ndani ya mji wa huo.

“Nakuomba Balozi, hili mlichukue kama la urgent, mkitusaidia kama mkopo sisi tuko tayari, mkitupa kama msaada tutashukuru zaidi. Kwa hiyo tunaomba utufikishie hili, ikiwezekana barabara hiyo tutaiita Pamela Road,” amesema

Mbali na hayo Rais ameweka wazi kwamba "Ujenzi wa barabara hii umegharimu bilioni 283.71 nimekopa kutoka Denmark, mbali na kufadhili mradi huu ilisaidia kukarabati barabara za Chalinze - Mlandizi, Chalinze - Segera, kwa niaba ya watanzania natumia fursa hii kutoa shukrani zangu".

Alikiba Naomba Wahurumie - Ommy Dimpoz

0
0
Alikiba naomba wahurumie - Ommy Dimpoz
Msanii Omari Nyembo a.k.a. Ommy Dimpoz ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Yanje' ambao ameshirikiana  msanii Seyi Shay kutoka nchini Nigeria, amemuomba msanii Alikiba awahurumie.


Ommy Dimpoz alisema hayo baada ya Alikiba kutangaza rasmi kuwa wimbo huo mpya wa Ommy Dimpoz ukifikisha watazamaji milioni tatu Youtube basi na yeye ataamsha dude na kuachia wimbo wake mpya baada ya 'Seduce Me' ambayo iliachiwa mwaka jana mwezi Agosti.

Baada ya ahadi hiyo ya Alikiba ndipo alipokuja Ommy Dimpoz na kumuuliza Alikiba kama atatoa ngoma zote tano kwa wakati mmoja au ataanza kuachia moja moja, hii ni ishara kwamba tayari kuna nyimbo zaidi ya tano kutoka wa Alikiba ambazo zipo tayari kwa ajili ya kuachiwa.

Aidha Msanii Alikiba akijibu moja ya swali kutoka kwa shabiki yake kupitia mtandao wa jamii ambaye alitaka kufahamu kuwa hilo dude ataliamsha lini ndipo alipojibu kuwa anawapa siku 10 tu baada ya hapo anaweza kuachia wimbo wake huo mpya.

Rais Magufuli Ahani Msiba Wa Marehemu Mzee Abbas Kandoro Mjini Iringa Leo

0
0
Rais Magufuli Ahani Msiba Wa Marehemu Mzee Abbas Kandoro Mjini Iringa Leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo wakati yeye na mkewe Mama Janeth Magufuli walipokwenda kuhani msiba wa Mkuu wa Mkoa Mstaafu Marehemu Mzee Abbas Kandoro eneo la Ihema nje kidogo ya mji wa Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa pole kwa wafiwa walipokwenda kuhani msiba wa Mkuu wa Mkoa Mstaafu Marehemu Mzee Abbas Kandoro eneo la Ihema nje kidogo ya mji wa Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitambulishwa kwa watoto wa marehemu walipokwenda kuhani msiba wa Mkuu wa Mkoa Mstaafu Marehemu Mzee Abbas Kandoro eneo la Ihema nje kidogo ya mji wa Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018.

Jerry Muro na Haji Manara kupamba mechi ya Uwesu Cup

0
0
Baada ya mechi ya Simba SC na Yanga SC iliyochezwa weekend iliyopita na vijana wa Msimbazi kuondoka na ushindi wa goli moja, burudani imehamia wilayani Pangani ambapo Mbunge wa Jimbo hilo, Juma Uweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, ameandaa kombe la Uwesu Cub ambalo litafunguliwa kwa mechi ya mashabiki wa Simba na Yanga.

Mchezo huo inatarajiwa kuwa na msisimko wa aina yake kutokana na msemaji wa Simba, Haji Manara pamoja aliyekuwa msemaji wa Yanga Jerry Muro kuthibisha kuwepo siku hiyo.

Mgeni rasmi wa tukio hilo anatarajiwa kuwa Naibu Waziri Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza.

Akiongea na waandishi wa habari mapema jana, Mwenyekiti wa Uzalendo kwanza, Steve amesema Jumamosi watakuwa wilayani humo kwaajili ya kuwaelimisha vijana juu ya kujitambua, kutumia fursa walizonazo mkoani humo, kama kutumia vipaji walivyonavyo ili kufanikisha malengo yao ya kimaisha.

Amesema kuwa vijana wengi huvunjika moyo kutokana na changamoto wanazozipitia bila ya kujua watazitatua vipi, hivyo kupitia kampeni yao ya Amka Kijana wataweza kuwapa elimu mbalimbali.

Mbali na elimu hiyo pia amesema siku hiyo kutakuwa na mtanange wa soka baina ya mashabiki wa timu ya Simba na Yanga na baadaye watatembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vilivyomo wilayani humo.

Amesema wasanii mbalimbali kama, Aunt Ezekiel, Flora Mvungi, Jaqueline Wolper, Duma, Johari, JB na wengine wengi. Tamasha hilo litakuwa la wazi na halitakuwa na kiingilio.

Ole Nasha: Wabunge, Wahadhiri Acheni Ukware Waacheni Wanafunzi Wasome

0
0
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha ametoa wito kwa wabunge kutojihusisha na vitendo vya kingono na wafunzi wa vyuo vikuu na wawaache wasome.

Pia ametoa rai kwa wanafunzi na wananchi kwa ujumla kutoa taarifa kwa mamlaka husika pindi wanapopata taarifa za walimu na wahadhiri wa vyuo vikuu kuwafelisha wanafunzi kwa kutaka rushwa ya ngono.

Kauli hiyo ya OleNasha imekuja baada ya Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM) kusema kuwa baadhi ya wahadhiri wanajifanya ni vidume vya mbegu katika kuwafelisha wanafunzi hao.

Aidha, Naibu Waziri huyo amesema serikali imelipokea suala hilo na haina uvumilivu kwa vitendo hivyo.

“Pia mwanafunzi hadi ahesabike kuwa amefeli haitokani na mtazamo wa mwalimu mmoja tu, kuna taratibu zimeweka kupitia ‘marks’ (alama) ambazo amepata kutokana na kazi zake ili kuamua amefaulu au amefeli. Hata kama ilitokea mwalimu mmoja amefanya vitendo hivi, hii haiwezi ikaathiri ufaulu kwa vitendo hivi.

“Vyuo vikuu ikiwamo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), vina taratibu maalumu ya kushughulikia masuala haya ya unyanyasaji wa kijinsia lakini wanafunzi wengi hawatumii msaada huu. Tunawasihi kama watapata matatizo kama haya waende kwa mshauri wa wanafunzi (dean of student),” amesema.

Mke wa P Funk Aapa Kupambana na Kajala Anayetaka Kuvunja Ndoa yao

0
0
MKE WA prodyuza maarufu Bongo, Paul Matthysse ‘P Funk’, Samira amefunguka kuwa licha ya kukutana na mitihani mingi ndani ya ndoa yake lakini kamwe hatokubali kuondoka nyumbani kwake na kumuachia nyumba muigizaji Kajala Masanja ambaye ni mzazi mwenziye na mume wake, kama alivyokuwa amepanga awali na atapambana naye.

 Akizungumza kwa uchungu sana, Samira alisema kila uchwao anakutana na kashfa nyingi zinazomhusisha mumewe na Kajala lakini ameaua kukomaa na ndoa yake.

“Yaani mateso ninayokutana nayo kwenye ndoa yangu ni Mungu pekee ndio anajua tena kwenye hali hii ya ujauzito niliyo nayo, awali nilipanga niondoke nimuachie nyumba lakini nimeona nikomae hadi kieleweke,” alisema Samira.



Mara nyingi Kajala alipokuwa akiulizwa kuhusiana na kuingilia ndoa hii ya mzazi mwenzie amekuwa akikana mara na kusema kuwa kuwa P Funk ni baba wa mtoto wake na si vinginevyo ingawa video mbalimbali zinavuja zikiashiria ni wapenzi.

"Watu Wasiojulikana" Waibua Mjadala Bungeni

0
0
Matukio ya utekaji  na kupotea kwa watu yameibua mvutano baina ya wabunge, bungeni leo.

 Mvutano huo ulianza wakati mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM), Almas Maige akichangia bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya mwaka 2018/19 ya Sh945.5 bilioni.

Katika mchango wake, Maige amegusia suala la matukio ya watu wasiojulikana akisema;

 “Watu wasiojulikana hawa wanaosemwa na wenzetu wa upinzani na huenda watu wasiojulikana wanasema wanafanya kazi upande wa upinzani tu hapana. Mimi nina orodha ya wana CCM waliofanyiwa na watu wasiojulikana.”

Kauli hiyo haikupita hivi hivi, kwani mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara alisimama kumpa taarifa Maige akisema idadi ya watu waliotendewa uhalifu na watu wasiojulikana ni wengi, “Kuna utekaji, uonevu katika nchi hii.”

Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga akamuuliza Maige, “Unapokea taarifa hiyo ya mheshimiwa Waitara.”

Kabla hajajibu, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba akasimama na kusema jeshi la polisi halijateka watu; “Mheshimiwa Maige anaongelea watu wasiojulikana.”

Hoja haikuishia hapo, Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia naye akasimama na kusema, “Suala la uhalifu, halilinganishwi kwa vyama vya siasa, sisi sote ni Watanzania na jeshi la polisi linalinda usalama wa raia wote.”

Hapo ndipo Maige akapewa fursa na Mwenyekiti Giga kuendelea kuchangia akisema;

 “Mimi siongelei uhalifu, naongelea watu kufanya matukio na hawakamatwi. Mimi nasema watu wanaofanya matukio wakamatwe.”

Bado mvutano uliendelea kwani, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Kunti Yusuph akasimama kumpa taarifa Maige kwa kusema;

 “Suala la kusema matukio yaliyofanyika upande wa upinzani na CCM hayafanani, inadhihirisha kwamba Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake imebariki mfumo na matukio haya ili waje waseme Chadema ni wachache na CCM ni wengi. Asante amedhihirisha.”

Akihitimisha mchango wake kwa eneo hilo, Maige amesema, “Mimi nashangaa upande ule (wa upinzani) wanakurupuka, mimi naongelea ombi langu kwa Serikali ili kuweza kuwakamata watu wasojulikana.”
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live




Latest Images