Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live

Trump Kukutana na Rais wa Korea Kusini Mei 22

$
0
0
Trump Kukutana na Rais wa Korea Kusini Mei 22
Rais Donald Trump anatarajia kukutana na rais wa Korea Kusini Moon Jae In ifikapo 22 Mei.

Viongozi hao wawili watakutana katika ikulu ya White House nchini Marekani.

Msemaji wa White House Sarah Sanders ametoa maelezo kuhusu mkutano huo na kusema kuwa Korea Kusini ina uhusiano mzuri na Marekani.

Trump ambae natarajia kukutana na Moon kwa mara ya tatu sasa,anaamini mkutano huo utasaidia katika kudumisha mahusiano kati ya mataifa hayo amwili.

Trump vilevile anatarajia kukutana na Kim Jong Un hivi karibuni.

Msuva Aanza Vizuri Hatua Ya makundi

$
0
0
Msuva Aanza Vizuri Hatua Ya makundi
Winga wa zamani wa Yanga Simon Msuva, ambaye kwasasa anachezea klabu ya soka ya Difaa El-Jadida ya Morocco ameanza vizuri hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Africa baada ya kutoa sare ugenini.


Difaa El-Jadida jana usiku ilicheza mchezo wake wa kwanza katika hatua ya makundi dhidi ya Mouloudia Club D'Alger ya Algeria na kutoa sare ya 1-1 kitu ambacho kinaiweka katika hali nzuri ya kufanya vyema katika michezo ya nyumbani.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Julai 5, 1962 jijini Algiers, Msuva alicheza dakika 87 na kutoa mchango mkubwa katika sare hiyo na sasa watasubiri katika mchezo wao wa nyumbani ili kufanya vizuri.



Msuva ameifungia mabao 5, Difaa El-Jadida katika michuano hii. Timu hiyo imepangwa Kundi B pamoja na timu za Mouloudia Club D'Alger, E. S. Setifienne ya Algeria na TP Mazembe ya DRC.

Kisiwa Kikubwa cha Hawaii Kimepigwa na Kimbunga Kikali na Volkano

$
0
0
Kisiwa Kikubwa cha Hawaii Kimepigwa na Kimbunga Kikali na Volcano
Kisiwa kikubwa cha Hawaii kimepigwa na kimbunga kinachotajwa kuwa kikali taangu mwaka 1975.

Kimbunga hicho cha kipimo cha ritcha 6.8 kimewafanya watu kuondoka majumbani mwao, pia kikiharibu miundombinu ya umeme na maji.

Kimbunga hicho kinatajwa kuanzia kwenye mlima wa volcano uitwao Kilauea. Kwa mujibu wa mashuhuda, tetemeko hilo liliambatana na upepo mkali ambao uliharibu vitu mbalimbali.

Mamia ya wakaazi wa eneo hilo tayari wametafuta hifadhi kutoka maeoe ambayo hayajaathirika.

Maija Stenback, shuhuda wa kimbunga hicho

Tunaishi eneo la mashambani Leilani, karibu vitalu sita vilisambaratishiwa mbali na mlipuko.tuliondolewa eneo hilo saa kadhaa zilizopita na sasa tumejihifadhi kwa marafikiu.

Nusu saa baada ya kimbunga hicho , nilishangaa kukuta mitandao mingi imeandika juu ya tukio hilo , kwa hiyo mimi na binti yangu tukatoka kwenda kujionea kwa macho yetu kwakweli unaweza kusikia na kuhisi mlipuko ukiwa umbali wa nusu maili na kadiri unavyokaribia eneo la tukio ndivyo unavyozidi kulihisi .Ilikuwa kama wakati mtu anavyopiga gitaa la besi kwakweli nzito, na unaweza kuhisi kweli nguvu ya uji wa volkano, rangi nayo sasa ilikuwa ya kustaajabisha na sauti ya volkano hiyo kwakweli ni maajabu makubwa .

Diwani Adai Kimbiji Kuna Simba Watatu

$
0
0
Diwani Adai Kimbiji Kuna Simba Watatu
Wakati habari za simba kuonekana katika baadhi ya maeneo ya vijiji vilivyopakana na mbuga za wanyama zikiendelea kusikika, diwani wa Kimbiji wilayani Kigamboni, Bunaya Sanya amedai kuwa uwapo wa wanyama hao katika kata hiyo kunatishia usalama wa wananchi wake.

Akizungumza jana katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kigamboni, alisema simba hao ambao wapo watatu walianza kuonekana mwaka 2017 katika mitaa ya Minondo na Ngobanja.

Kikao hicho kilikuwa na ajenda mbalimbali ikiwamo kupokea taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kutoka kata tisa za halmashauri hiyo.

“Wafugaji ndiyo waliwaona simba hawa, mwaka jana walikula mbuzi sita waliokuwa katika banda na mwaka huu wameonekana wakila nguruwe pori. Hii ni hatari tunaomba wataalamu idara ya wanyama pori washirikiane na manispaa kufanya uchunguzi ili kuwaibani,” alisema Sanya.

Alifafanua kuwa uchunguzi huo utasaidia kwa kiasi kukamatwa kwa simba hao ambao watapelekwa maeneo husika kwa ajili ya kufugwa.

Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Stephen Katemba alisema watalifuatilia suala hilo kwa kushirikiana na mamlaka husika na kuwataka wakazi wa maeneo hayo wakiwaona watoe taarifa haraka.

Akizungumzia miradi ya maendeleo, Katemba alisema manispaa hiyo ipo katika hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa kituo cha kisasa cha afya kitakachogharimu Sh500 milioni.

“Kituo hiki kinatarajiwa kukamilika mwezi huu na kitakuwa na huduma zote zikiwamo za X-ray na chumba cha kuhifadhi maiti nane kwa wakati mmoja,” alisema Katemba.

Meya wa Kigamboni, Maabadi Hoja aliwashukuru watendaji na madiwani wa manispaa hiyo kwa kufanya kazi kwa ushirikiano.

Masikini! Zari Azidi Kuteswa na Kifo cha Ivan Don Amuandikia Ujumbe Huu

$
0
0
Masikini! Zari Azidi Kuteswa na Kifo cha Ivan Don Amuandikia Ujumbe Huu
Aliyekuwa Baby Mama wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady ameonyesha ni kiasi gani anamkumbuka aliyekuwa mume wake, Ivan Ssemwanga ‘Ivan Don’ ambaye ni Marehemu kwa sasa.

Zari ameshare picha ya zamani katika mtandao wa Instagram ikimuonyesha Don akiwa na mwanaye, Pinto ambaye ni mkubwa kwa sasa na kuandika;

Ni vigumu kuamia ni takribani mwaka mmoja sasa tangu Mungu alipokuita, naona ni kama jana. Hakuna siku inayopita bila kukuombea pamoja mama yako. Roho zenu ziendelee kupumzika kwa amani.

Hakika sisi huja kutoka mbali. Hapa Don anaonekana amembeba Pinto (ambaye ni mkubwa sasa), alianza naye kutoka mbali.


Can’t believe its almost a year since God called you, it seems like yesterday. No day passes that i don’t pray for you and mom. May your souls continue resting in peace.
We surely come from far. Here Don is seen carrying Pinto ( who is a giant now), started from the botton right? Your missed🌹#RandomPost

Ivan alifariki May 25, 2017, alijipatia umaarufu mkubwa tangu nchini mwake Uganda hadi Afrika Kusini ambako ameacha utajiri mkubwa uliomfanya kuwa mmoja ya watu matajiri nchini humo kabla ya kufikwa na mauti.

Kikosi cha Simba Chawafanyia Zoezi la Mwisho Ndanda Kwaajili ya Mechi ya Kesho

$
0
0
Kikosi cha Simba Cawafanyia Zoezi la Mwisho Ndanda Kwaajili ya Mechi ya Kesho
Kikosi cha Simba kinafanya mazoezi yake ya mwisho kuelekea mchezo wa ligi dhidi ya Ndanda utakaopigwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kesho Jumapili.

Simba inafanya mazoezi hayo kwenye Uwanja wa Boko Veterani uliopo pembezoni kidogo mwa jiji la Dar es Salaam.

Taarifa kutoka kambini zinasema kuwa hali ya wachezaji kiafya iko vizuri na hakuna aliye majeruhi hivi sasa.

Simba itakuwa inaingia kukabiliana na Ndanda ikiwa na kumbukumbu ya ushindi dhidi ya Yanga wa bao 1-0 Jumapili ya wiki jana.

Mke wa Sugu Alivyobuni Keki ya Picha ya Gereza Kwenye Birthiday ya Mumewe

$
0
0
Mke wa Sugu Alivyobuni Keki ya Picha ya Gereza Kwenye Birthiday ya Mumewe
Utamaduni wa sherehe ya kuzaliwa ulianza bara la Ulaya miaka mingi iliyopita. Ilikuwa ikiogopewa kwamba mashetani walivutiwa zaidi kwa watu katika siku zao za kuzaliwa, ili kuwalinda na madhara.

Ndugu na marafiki hujumuika kwa mwenye kusherehekea siku ya kuzaliwa wakiwa na maneno yenye faraja na matumaini na pia maombi.

Pia, sherehe hizo hupambwa kwa zawadi zenye lengo la kuleta furaha, uchangamfu na zaidi ya hapo zimelenga kuwafukuza mashetani hao. Sherehe za kuzaliwa zilienea hadi katika nchi za Afrika na siku ya Mei Mosi, mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ alikuwa akisherehekea siku yake.

Siku hiyo alikuwa akitimiza miaka 46. Hata hivyo, aliisherehekea siku hiyo akiwa kifungoni katika gereza la Ruanda jijini Mbeya anakotumikia kifungo cha miezi mitano.

Sugu alihukumiwa kifungo hicho pamoja na katibu wa Chadema wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga Februari 26 baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mbeya kuwakuta na hatia ya kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli. Waslidaiwa kufanya kosa hilo Desemba 30 mwaka jana.

INAENDELEA UK 22

INATOKA UK 21

Sherehe ya Sugu nayo haikukosa zawadi. Kwanza kuliandaliwa keki aliyopelekewa gerezani kama zawadi maalumu kwake, na akasherehekea siku yake muhimu kwa kula chakula pamoja na watoto yatima wa kituo cha Nuru kilichopo Uyole pamoja na kutoa msaada wa maziwa ya watoto na nguo.

Familia ya Sugu, ikiongozwa na mke wake, Happines Msonga, ilimfanyia jambo hilo kwa kumshtukiza. Pia waliambatana na wafanyakazi wa Hotel ya Desderia inayomilikiwa na Sugu pamoja na wafuasi wa Chadema

Keki ilichorwa pingu, mnyororo na taswira ya chumba cha gereza na picha yake ikimuonesha yupo ndani ya chumba hicho na mtu anamuona kupitia nondo za chumba.

Pia ilikuwa na ua aina ya waridi kuashiria mahaba ya mke kwa mume.

Baadaye, familia ya Sugu ilisherekea siku hiyo kwa kwenda kula chakula pamoja na watoto wa kituo hicho cha Nuru kama walivyoagizwa na Sugu kwa uongozi wa hoteli hiyo.

Kwanini watoto yatima?

Pengine swali linaweza kuwa kwa nini kituo cha Nuru na kwa nini iwe kituo cha watoto yatima.

Akizungumza na Mwananchi, Happines alisema mumewe ndiye aliyeagiza kwamba siku ya kuzaliwa kwake iadhimishwe pamoja na watoto yatima kwa kula nao chakula cha pamoja.

Alisema aliamua kufanya hivyo ili kuendelea kuwa karibu na wananchi wake katika shughuli za kijamii hata kama yupo gerezani kwa kuwa anao ajibu wa kuwatumikia wananchi wake.

“Sote tunajua yupo gerezani lakini amesema anawapenda sana watoto na wananchi wa jimbo lake kwa ujumla na kiroho yupo nao daima,” alisema Happiness.

“Alisema kwa kuwa siku yake ya kuzaliwa ni Mei Mosi, ni vyema tukashiriki sherehe hiyo na watoto yatima.”

Anasema kufanya hivyo ni mwendelezo wa Sugu kuwatumikia watoto yatima kama anavyofanya kwa kutumia mfuko wake wa kuwasomesha watoto yatima katika shule za sekondari zilizopo ndani ya jimbo la Mbeya Mjini.

“Sote tunajua kuwa Sugu ana mfuko ule wa kusomesha watoto kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. Hivyo uongozi wa Hotel Desderia ambayo anaimiiliki imeanzisha mpango maalumu wa kuwatembelea na kujumuika na watoto wanaolelewa kwenye vituo vyote vilivyopo jijini hapa kila mwisho wa mwezi kwa kuwapelekea chakula na misaada mingine,” alisema.

Keki ilivyopambwa

Happiness anasema alibuni umbo la keki hiyo kwa lengo la kuonyesha mume wake anasherekea siku yake ya kuzaliwa akiwa gerezani, hivyo ilikuwa ni ishara kwamba bado yupo ndani lakini familia yake na wananchi wa jimbo lake wanamkumbuka na kuendelea kumpenda.

“Wazo la kutengeneza keki ikiwa na muonekano ule lilikuwa langu mwenyewe,” alisema.

“Lakini kubwa zaidi ile ilikuwa ni Surprise kutoka kwangu maana sikumuambia kuwa nitamuandalia chochote. Hivyo siku ile nilipompelekea na kufungua boksi, hakuamini kabisa na hasa alipoona pingu, mnyororo na picha yake inayomuonyesha yupo kwenye chumba cha gereza chenye nondo.”

“Hata siku akitoka gerezani, nitamuandalia keki ambayo itakuwa imechorwa ikionyesha zile pingu zimekatika na milango ya gereza imefunguliwa na hii yote ni kuonyesha kwamba sasa yupo huru na amerejea nyumbani kuungana na familia yake pamoja na wananchi wake wa jimbo la Mbeya Mjini.”

Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha Nuru, Jarson Fihavango alimshukuru Sugu na uongozi mzima wa hoteli yake kwa kuwapelekea chakula na misaada mingine watoto wanaolelewa kituoni hapo.

“Tunajua mbunge wetu alipatwa na matatizo, lakini pamoja na kwamba yupo mahali ambapo si nzuri sana ila bado anawakumba wananchi wake. Na sisi tunashukuru sana kwa hiki alichotufanyia,” alisema.

“Tunasema aendelee na moyo huohuo na sisi tunamuombea. Hiki alichokifanya kina Baraka kubwa mbele za mwenyezi Mungu, tunajua namna anavyoweza kumlipa’.

Fihavango anasema sio kazi rahisi kwa mtu ambaye yupo kwenye matatizo, lakini akawa na roho ya kuwakumbuka watu wake wa walio nje na kuwatumikia kama kawaida.

Katibu wa mbunge

Tangu alipofungwa Sugu amekuwa akiwatumikia wananchi wake wa Mbeya Mjini kupitia kwa wawakilishi wake akiwamo katibu wake, Gideon Siame.

Siame anasema pamoja na bosi kuwa gerezani amekuwa akitekeleza majukumu kwa wananchi wa jimbo hilo kama kawaida huku akiwa anapelekewa taarifa zote na kutoa maelekezo pale inapobidi.

“Kinachoendelea ofisini ni zile shughuli tu za kawaida ambazo hata yeye (Sugu) akiwa Dodoma au nje ya jimbo, huwa tunakuwa tunaendelea nazo. Kuna mambo ambayo huwa yanahitaji tumshirikishe kwa ajili ya mawazo yake au maelekezo huwa tunafanya hivyo,” alisema katibu huyo.

“Na hivi sasa yupo gerezani pale tunapopata nafasi ya kumuona huwa tunamueleza kinachofanyika na yeye anatupa mawazo na maelekezo yake.”

Anasema kila wanapopata muda wa kumuona gerezani, Sugu amekuwa akiwasisitiza kuendeleza harakati za kulikomboa taifa na akiwataka wasiteteleke kwa kuona viongozi wa kisiasa wanafunguliwa kesi na kufungwa kama yeye, bali iwe chachu ya kupigania ukombozi.

Rais John Magufuli Atoa Milioni 5 kwa Ajili ya Kuchangia Ujenzi wa Shule Morogoro

$
0
0
Rais John Magufuli Atoa Milioni 5  kwa Ajili ya Kuchangia Ujenzi wa Shule Morogoro
Rais John Magufuli ametoa Sh 5 milioni  kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa shule katika kijiji cha Mkula mkoani Morogoro.

Rais Magufuli ametoa fedha hizo leo Mei 5 akiwa njiani kuelekea Kilombero kwa ajili ya kuzindua daraja.

Magufuli alisimama katika kijiji hicho baada ya kusimamishwa na wanakijiji wa eneo hilo wakati msafara wake ukielekea katika uzinduzi wa daraja hilo.

Wanakijiji hao wamemueleza Rais Magufuli kuwa wameanza ujenzi wa shule lakini unakwenda kwa kusuasua.

Pia wananchi hao wamelalamika ukosefu wa kituo cha afya katika kijiji hicho.

Rais Magufuli aliwakabidhi fedha hizo Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkula(Chadema) na Mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo.

"Nimewakabidhi wote kwa sababu maendeleo hayana chama, nendeni mkazitumie kwa malengo yaliyopangwa, nataka watoto wetu waende shule,” amesema

"Ole wenu mtumie vibaya, Mimi kutumbua kuko palepale, tunachotaka ni maendeleo naomba tushikamane kwa ajili ya maendeleo.” ameongeza


Aisee Bongo Movie Bado Sana Tusubiri miaka 1000..Ona Huyu Mdada Anayelipwa Bilioni 5 Kwa Kila Episode ya Series

$
0
0
Kwa wale watazamaji wa series ya game of thrones kuna mwanadada anajulikana kama Daenarys Targaryen ambaye jina lake halisi ni Emilia Isabelle Euphemia Rose Clarke, raia wa Uingereza kazaliwa mwaka 1986.

Huyu dada analipwa Euro milion 2 kwa kila epsode anayoshiriki ambazo kwa pesa yetu ya madafu ni sawa na bilion 5.45. KIla series ya game of thrones inakuwa na epsodes nane ina maana akionekana kwenye epsodes zote kitu ambacho mara nyingi uwa inakuwa hivyo anakuwa kavuta bilion kama 50 za kibongo.

Mpaka Mbongo movie ije kufika hapa ni miaka 1000 ijayo.
Malipo hayo ni kwa mtu mmoja sasa jiulize GOT ilivyo na characters wengi sijui budget yake itakuwa kiasi gani.

Lakini ela itakuwa inarudi maana ndiyo series ambayo kila season ikitoka inavunja rekodi ambayo uwa inaiweka yenyewe yani GOT ndiyo series inayofuatiliwa zaidi na imekuwa kuwa ikivunja rekodi yake yenyewe kwa kuongoza watazamaji kila season yani toka ianze kutoka kila season watazamaji wanaongezeka badala ya kupungua na pia ndiyo series inayovunja rekodi kwa kudownloadiwa kiwizi wizi.

SOMA Pia: Job Opportunities at Fastjet Tanzania, Cabin Crew

Kuna Tofauti Kubwa ya Uchekeshaji na Ufanyaji Ujinga, Mdau Amchana Live Idriss Sultan Adai ni Mfanyaji Ujinga

$
0
0

Mdau mmoja Kutoka JF Ameamua Kumtolea uvivu Mchekeshaji Idriss Sultan na Kudai sio mchekeshaji, Jisomee Mwenyewe Mdau Alivyofunguka:

"Ninaomba ieleweke wazi sina bifu na Idris Sultan wala sijawahi kuwa na bifu naye ,ila penye ukweli lazima pasemwe huyu bwana mdogo ni mfanya ujinga na mambo ya kitoto toto ambayo yeye binafsi anadhani anatuchekesha kumbe tunamuona ni punguani tu asiye jielewa.

Mbali na yeye wengine wanaomfuatia kwa kufanya ujinga huku wakidhani wanatuchekesha ni Mkali wao na Dullvani wote hawa ni wafanya ujinga na mambo ya kipuuzi puuzi yasiyoeleweka.

Kwa ambao mpo karibu na Idris Sultan mwambieni tumechoka kuona mambo yake ya kipuuzi abadilike anatuboa " By Hance Mtanashati

Snura Majanga Anaswa Kwa Sangoma ( Mganga wa Jadi ) Akiwa Amebebeshwa Vibuyu...

$
0
0
Msanii mkongwe nchini maarufu kwa jina la Snura Mushi au Snura Majanga amenaswa live akiwa kwa sangoma ( mganga wa jadi ) akisafisha nyota yake kwa lengo la kujiongezea mashabiki……


Tazama ushuhuda wa picha hapo chini….


Hii Hapa Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo ya Uume

$
0
0
Tatizo hili limekuwa likiwaadhiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baada ya kujiona wapo tofauti sana na wengine kwa kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi 6-8 kwanza upungufu wa vichocheo hivi huchochea ukuaji wa uume chongo ambalo hushambulia nerve ambayo uharibu kabisa ukuaji wa uume, ngiri, punyeto, ambayo huathili misuli ya uume, ngiri huleta maumivu, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, korodani moja kuvimba, kutopata choo vizuri, sababu hizi hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na mara nyingi hata nguvu za kiume ( hamu ya tendo la ndoa) hupungua na kwisha kabisa

GEMBE :Ni dawa inayozalisha na kukufanya uume kukua na kuongezeka
NGEMO : Ni dawa bora ya kuongeza nguvu za kiume

Hukutia hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi mara4 nne bila kukinai au kuchoka pia itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk30-45 kwa mtumiaji pia tunatibu kisukari, bp, ngiri, miguu
kuwaka moto KAMA HUNAMDA WA KUFIKA OFISINI KWETU UTALETEWA POPOTE TUPO MBAGALA RANGI

0753471612/ 0715249530
0623 386 305

Rais Magufuli Ampa Mtoto Shujaa Milioni 3 na Kumpatia Ulinzi

$
0
0
Rais Magufuli Ampa  Mtoto Shujaa Milioni 3  na Kumpatia Ulinzi
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli akiwa ziarani mkoani Morogoro amepata fursa ya kuzungumza na wakazi wa Kijiji cha Mang’ula ambao wamemwelezea kero na changamoto zinazowakwamisha katika maendelo ambapo ameahidi kuzishughulikia huku nyingine akizitatua papo hapo.



Akizungumza na wakazi wa kijiji hicho, Rais aliuliza iwapo kuna shule ya sekondari, wanakiji wakajibu ipo, kuhsu matatizo ya shule hiyo, aliomba mwalimu mmoja ajitokeze kuyasema na kwa vile hakukuwa na mwalimu aliyejitokeza, ndipo akajitokeza mtoto Msangi wa kidato cha kwanza katika shule hiyo ambaye alimueleza rais kwamba shule yao haina vyoo hivyo akamuomba awasaidie.



Baada ya hapo Rais alitoa pesa taslimu kiasi cha Tsh. Milioni 3 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyoo katika shule hiyo na akiwataka wazazi na wananchi wa kijiji hicho kujitoa na kuchangia ili kusaidia ujenzi huo.



Rais Magufuli yupo ziarani mkoani Morogoro akielekea wilayani Kilombero, ambapo atazindua daraja la Mto Kilombero.

Yanga Yafunguka Sababu ya Ajibu, Shishimbi na Chirwa Kutokwenada Algeria

$
0
0
Yanga Yafunguka Sababu ya Ajibu, Shishimbi na Chirwa Kutokwenada Algeria
Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa ametoa ufafanuzi juu ya wachezaji wake muhimu, Kelvin Yondani, Obrey Chirwa, Ibrahim Ajib na Papy Kabamba Tshimbi kutojumuika na kikosi kilichosafiri juzi kuelekea nchini Algeria kwaajili ya mchezo wao wa hatua ya makundi dhidi ya USM Alger.



Mkwasa amesema kuwa wachezaji wote waliyoshindwa kujiunga na Yanga kwenye safari hiyo walikuwa na sababu zao muhimu nawala siyo mambo mengine kama yanavyoelezwa.

Kunasababu mbalimbali kwa wachezaji kupelekea wao kutokusafari, rabda nikianza na Kelvin Yondani yeye alipata majeraha wakati wa mechi na Simba na alipoomba atoke tukashindwa mkutoa kwasababu mechi ilikuwa tayari ilishamalizika.

Mchezaji wa pili ni Obrey Chirwa alikuwa na Maleria na baada ya mechi ikaongezeka kwahiyo ikashindikana kusafiri.

Mchezaji wa tatu ni Ajib, yeye yupo fiti ila anamatatizo ya kifamilia Mkewake anatarajia kujifungua muda wowote na hivyo kunahitaji uwangalizi wa hali ya juu kwahiyo anahitajika awe karibu ndiyo maana hakuweza kusafiri.

Papy Kabamba Tshimbi alikuwa pia amepata majeraha kutoka Ethiopia na hata mechi na Simba alikuwa amecheza na akaomba atoke kwakuwa majeraha yalikuwa yameongezeka kwahiyo hakuna kitukingine chochote kimetokea kama watu wanavyodai mtaani kwakuonyesha kuwa kuna kitu chochote huo ndiyo ukweli uliyokuwepo kwahiyo niaombe wanachama wawe na utulivu katika kipindi hiki na tuwe na umoja ili tuhakikishe tunapata matokeo mazuri ugenini kwakuwa ni mechi ya kwanza isituvunje nguvu na watambue kuwa vijana waliyokwenda wanaaminika na wana uweledi mzuri.

Yanga itashuka dimbani siku ya Jumapili kuanza kutupa karata yao ya kwanza kwenyemchezo huo wa kwanza wa hatua ya makundi wakiwa ugenini dhidi ya USM Alger ya nchini Algeria.

Ndalichako Kuwasaka Wanaoichafua Serikali

$
0
0
Ndalichako Kuwasaka Wanaoichafua Serikali
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwasaka wale wote wanaoichafua serikali kwa kughushi vitabu na kuvitupia mtandaoni.

Prof. Ndalichako amesema kuwa katika mkutano unaoendelea jijini Dodoma unaojadili mapendekezo ya bajeti ya mapato na matumizi ya wizara mbalimbali kwa mwaka 2018/19 ambapo amesema huo ni uhalifu.

“Na mimi nimepata nafasi ya kuona kitabu cha Kiingereza cha darasa la tatu nikitabu kilichokuwa kina makosa ambayo yamekwisha kufanyiwa marekebisho na wahusika tayari wamekwisha kuchukuliwa hatua lakini pia kipo kitabu kinachosambaa ambacho kinaonyesha mwili wa binadamu na kwa kweli mishale ya yule binadamu imeenda ovyo ovyo , kitabu hicho hakijawahi kuwa sehemu ya vitabu vinavyotolewa na serikali na ninasikitishwa sana kwamba watu wameamua kutunga vitu vyenye lengo la kuichafua serikali na kufanya hilo ni kosa la jinai,” amesema Ndalichako.

“Nina furaha kwamba leo vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vipo hapa naviagiza mara moja vitafute watu ambao wanatengeneza vitu ambavyo vinaichafua serikali na kughushi na kuchafua serikali ili wachukuliwe hatua kwasababu wao ni wahalifu.”

Tafrani Baada ya Dawa za Kikohozi Kukutwa na ‘Dawa ya Kulevya’ Nigeria

$
0
0
Tafrani baada ya dawa za kikohozi kukutwa na ‘dawa ya kulevya’ Nigeria
Kampuni nne za dawa nchini Nigeria zimevamiwa kutokana na kuhusika na kuuza dawa za kikohozi ambazo zina dawa ya kulevya aina ya codeine.

Kuvamiwa kwa kampuni hizo kunatokana na uchunguzi uliofanywa na Shirika la Utangazaji la BBC na kugundua kuwa dawa hizo zina kilevi hicho cha codeine na kufanya vijana kuzinywa kwa wingi kama dawa wanavyotumia dawa za kulevya.

Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini humo imeeleza kuwa kampuni hizo ziko kwenye miji ya Lagos, Ilorin na Kano nchini humo. Serikali ya nchi hiyo zimepiga marufuku uzalishwaji na uingizwaji wa dawa hizo kutoka nje ya nchi.

Imegundulika kuwa dawa hizo zimekuwa zikiuzwa kihalifu ili vijana wazitumie kama kilevi

Baada ya Kimya cha Mudaa Mrefu Nicki Minaj Aachia Ngoma Mbili kwa Mpigo

$
0
0
Baada ya Kimya cha Mudaa Mrefu Nick Minaj Aachia Ngoma Mbili kwa Mpigo
STAA wa kike wa Muziki wa Hip Hop, Onika Tanya Maraj ‘Nicki Minaj’ Baada ya kupita miezi minne bila ya kuachia ngoma mpya, mekuja kwa hasira kwa kuachia video mbili kwa mpigo.

Rapper huyo ameachia video ya wimbo wake ‘Chun-Li’ na ‘Barbie Tingz’. Wimbo wake wa mwisho ulikuwa ni Motorsport ambao aliimba na Migos pamoja na Cardi B.

Mpaka sasa video ya Chun-Li imeshatazamwa zaidi ya milioni tano kwenye mtandao wa YouTube, wakati ‘Barbie Tingz’ ikiwa imetazamwa zaidi ya mara milioni tatu. Tazama hapa chini video zote mbili.

Msuva Ajiunga na Wenzake Algeria

$
0
0
Msuva Ajiunga na Wenzake Algeria
Mtanzania Simon Msuva anayecheza soka la kimataifa nchini Morocco katika klabu ya Difaa El Jadidi, leo amekutana na wachezaji wa kikosi cha Yanga mjini Algiers, Algeria.

Msuva amepataa wasaa wa kuwatembelea wachezaji hao kwa madhumuni ya kuwajulia hali wakiwa wanasubiria mechi ya mkondo wa kwanza ya Kombe la Shrikisho Afrika dhidi ya USM Alger itakayopigwa kesho.




Msuva alikuwa Algiers na kikosi cha Difaa El Jadidi kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo timu yake jana ilikuwa na kibarua dhidi ya MC Alger katika mtananage ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Winga huyo aliwahi kuichezea Yanga kabla ya kutimkia Uarabuni kujiunga na Difaa ambayo anaitumikia kwa sasa.

Kikosi cha Yanga kesho kitakuwa kinashuka dimbani kwa ajili ya kukipiga na USM Alger, mechi ikitarajiwa kuanza majira ya saa 4 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Rais JPM Azindua Dalaja la Magufuli Kilombero

$
0
0
Rais JPM Azindua Dalaja la Magufuli Kilombero
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo Mei 5, 2018 amezindua Rasmi Darala la Magufuli lililopo Kilombero mkoani humo.


Wachimbaji wa Madini Wanne Wafariki Dunia Baada ya Kufukiwa Mgodini

$
0
0
Wachimbaji wa Madini Wanne Wafariki Dunia Baada ya Kufukiwa Mgodini
Kutoka nchini Afrika Kusini, wachimbaji wa madini wanne wanaripotiwa kufariki dunia baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi wakiwa machimboni, na kufunikwa na mgodi.

Wachimbaji hao ni miangoni mwa wachimbaji wengine 10 waliookolewa katika mgodi huo wa dhahabu ulioko Magharibi jijini Johannesburg.

Inaelezwa kuwa wachimbaji watatu bado wamenasa katika mgodi huo.

Afrika Kusini ni nchi inayoongoza kwa uzalishaji wa madini ya dhahabu lakini imekuwa ikituhumiwa kwa kuwa na rekodi ya usalama dhaifu.
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live




Latest Images