Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Yanga Yaondoka Dar Leo Idadi ya Wachezaji Waliobaki Yaongezeka

$
0
0
Yanga Yaondoka Dar Leo Idadi ya Wachezaji Waliobaki Yaongezeka
Kikosi cha Yanga kimeondoka leo kuelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa kesho Alhamis.

Yanga imeondoka mapema leo asubuhi kuelekea jijini humo huku ikielezwa kuwa kipa namba moja wa Yanga, Youthe Rostand ni miongoni mwa wachezaji waliosalia Dar es Salaam.

Haijajulikana sababu za mchezaji huyo kubaki Dar es Salaam na uongozi haujataja idadi rasmi ya wachezaji ambao wamesafiri kwa ajili ya mechi hiyo dhidi ya Tanzania Prisons.

Mbali na Rostand, wapo baadhi waliosalia Dar es Salaam wakiungana na baadhi ya walioshindwa kusafiri na timu kuelekea Algeria kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger.

Yanga itakuwa mgeni kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ambapo mchezo huo utaanza majira ya saa 10 kamili jioni.

Mama wa Jay-Z: Nilimwambia Mwanangu Nina Mpenzi wa Jinsia Moja

$
0
0
Mama wa Jay-Z: Nilimwambia Mwanangu Nina Mpenzi wa Jinsia Moja
Mama yake mwanamuziki maarufu nchini Marekani na duniani, Jay- Z amezungumza namna ambavyo mtoto wake amekuwa akimpa moyo alipomwambia kuwa amekuwa akijihusisha na mapenzi ya jinsia moja

Gloria Carter aliiambia hadhira katika tuzo za GLAAD kuwa ni mara ya kwanza kuzungumza na mtu kuhusu ukweli wake

Mama wa watoto wanne alitunukiwa tuzo akitambuliwa kwa mchango wake kwenye wimbo uitwao Smile uliotolewa mwaka jana.

Alisema: ''Smile imekuwa halisia kwa sababu nilimshirikisha mtoto wangu nikimweleza mimi ni nani.''

''Mtoto wangu alilia na akasema: 'lazima maisha yalikuwa mabaya sana kuishi namna hiyo kwa muda mrefu.''

''Maisha yangu hayakuwa mabaya,''aliongeza.

''Nilichagua kuilinda familia yangu.Nilikuwa na furaha japo sikuwa huru

Ommy Dimpoz Ashushwa na Nandy

$
0
0
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Nandy ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Ninogeshe' amemshusha chini kwa nafasi moja katika mtandao wa Youtube msanii Ommy Dimpoz ambaye naye anafanya vyema na wimbo wake wa 'Yanje'.

Nandy sasa kwa upande wa Tanzania video yake imeshika nafasi ya kwanza katika mtandao huo wa YouTube na kumshusha Ommy Dimpoz ambaye alikuwa ana trend na kushika nafasi hiyo ya kwanza toka Mei 2, 2018 na sasa kushika nafasi ya pili chini ya Nandy.

Hata hivyo mapokeo ya video hiyo ya Nandy yamekuwa ni makubwa sana kwani video yake ndani ya siku sita toka ilipotoka Mei 3, 2018 imeshafikisha watazamaji zaidi ya Laki sita huku wengine wengi wakisema kuwa kupitia wimbo wake huo mpya na video yake hiyo imewafanya wasahau ujinga wake aliofanya wiki kadhaa zilizopita baada ya video yake akiwa faragha na Bill Nas kusambaaa kwenye mitandao ya kijamii.

Mnyika na Bulaya Watolewa Bungeni

$
0
0
Naibu Spika Tulia Ackson ameagiza Mbunge wa Kibamba Mhe. John Mnyika na Ester Bulaya kutolewa nje ya ukumbi wa Bunge kwa kile alichodai kutoheshimu kiti cha Spika.

Naibu Spika ametoa maamuzi hayo jioni ya leo Mei 9, 2018 katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji mwaka 2018/19 ambapo Mbunge John Mnyika alisimama akitumia kanuni ya 69(1), kutaka kuahirishwa kuhitimishwa kwa hoja ya wizara ya Maji na Umwagiliaji ili apewe nafasi ya kutoa hoja yake ya kwanini bajeti ya wizara hiyo isipitishwe na Bunge.

Mara baada ya kauli hiyo, Dk Tulia alisimama akitumia kanuni ya 69(2), kusema kama Spika atakuwa na maoni kwamba kuwasilishwa kwa hoja hiyo ni kinyume cha uendeshaji bora wa shughuli za Bunge, atakataa kuitoa ili ijadiliwe.

Mbali na Mnyika Naibu Spika Dk. Tulia Ackson amemtoa pia ndani ya Ukumbi wa Bunge, Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema) kwa kutoheshimu kiti cha Spika.

Ishu ya Mafuta ya Kula imemfanya Zitto Kabwe Kumshauri Spika Ndugai

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Ruyagwa Kabwe amemshauri Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai kuwa anapaswa kuwa na msimamo katika kuisimamia serikali kama alivyofanya katika suala la mafuta na kudai hii itamfanya aweke ‘legacy’

Zitto Kabwe amesema hayo baada Spika wa Bunge kumtaka Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kuja na maelezo ya kutosha kuhusu tatizo la sukari na mafuta nchini.

“Namna ambavyo Spika Ndugai amesimamia suala la majibu ya Serikali kuhusu kadhia ya Sukari na Mafuta ya Uto (kula) inanikumbusha bunge la tisa. Ndugai sasa ameanza kuweka ‘legacy’ yake. Aendelee hivi hivi ila jambo la muhimu zaidi suala la mafuta litazamwe kwa muktadha wa Wakulima wa Mawese na Alizeti” ameandika Zitto Kabwe

Mtanzania Abdi Banda Ametwaa Tuzo Katika Club yake Afrika Kusini

$
0
0
Beki wa kati wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa katika club ya Baroka FC ya Afrika Kusini Abdi Banda leo amerudi tena kwenye headlines baada ya kufanikiwa kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi April wa club ya Baroka FC.

Banda leo amefanikiwa kutangazwa mchezaji bora wa Baroka FC ambapo hivi karibuni aliifungiwa magoli mawili timu yake katika mchezo dhidi ya Bloemfontein Celtic, Banda ametangazwa mshindi wa tuzo hiyo na kupewa hundi ya rand 5000 ambazo ni zaidi ya Tsh laki tisa.

Kama hufahamu Banda amekuwa na wakati mzuri na Baroka FC kutokana na kufanikiwa kucheza jumla ya mechi 31, 27 za Ligi na nne za mashindano mengine na kati ya game 31 alizocheza ni mechi moja pekee dhidi ya Free State February 3 2018 ndio alicheza kwa dakika 63 ila game nyingine zote alicheza kwa dakika zote 90, hadi sasa ameoneshwa jumla ya kadi tatu za njano.

Breaking News: Mbunge Sugu Aachiwa Huru Atoka Gerezani

$
0
0
Breaking News: Mbunge Sugu Aachiwa Huru Atoka Gerezani
Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chadema, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ameachiwa huru kutoka gereza la Ruanda, Mbeya alipokuwa akitumikia kifungo cha miezi mitano.

Sugu ameachia huru pamoja na katibu wa Chadema kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, mbunge wa Viti Maalumu, Sophia Mwakagenda na viongozi wengine wa chama hicho walifika gerezani hapo kuwapokea na tayari wamefika nyumbani kwa Sugu.

Wengine waliofika gerezani ni Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi na madiwani.

Sugu na Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela February 26, 2018 kwa kutoa lugha ya fedhea dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desember 30, 2017 katika uwanja wa shule ya msingi Mwenge, Mbeya.

Hatimaye Dogo Janja Ajichora Tattoo Kwapani Yenye Jina la Mke Wake

$
0
0

Finally msanii wa bongo flava, Dogo Janja amepost kupitia ukurasa wake wa Instagram picha inayomuonyesha akiwa amelala na mkono wake wa kulia upande wa chini ikionyesha tattoo yenye jina la mpenzi wake Irene Uwoya.

Hivi Ndivyo Zali Alivyozima Mbwebwe za Daimond

$
0
0
Hivi Ndivyo Zali Alivyozima Mbwebwe za Daimond
Dunia inakwenda spidi sana! Miezi kadhaa baada ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kumwagwa na mama watoto wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, bado mambo ni moto huku mwanamama huyo akidaiwa kuzima ngebe au mbwembwe za jamaa huyo, Risasi Mchanganyiko limedokezwa.

Wakati Diamond akibadili rangi ya lile gari lake aina ya BMW X6 kutoka nyeusi kwenda bluu bahari, Zari yeye alijibu mapigo kwa kununua gari la kifahari aina ya Range Rover Spot lenye rangi nyeupe na kuibua gumzo kubwa kwa mashabiki wao.

Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kwamba, Diamond aliamua kulibadili gari hilo rangi kwani lilikuwa limezoeleka mitaani jijini Dar tangu alipopewa kama zawadi siku ya bethidei yake mwaka 2014 alipokuwa akitimiza umri wa miaka 25. Mbali na kubadili rangi ya gari hiyo, pia alibadilisha ‘rim’ za matairi yake na kuweka nyingine kali zaidi ya zile za awali.
Watu walioko karibu na Zari walidokeza kuwa, mfanyabiashara huyo alivuta ndinga hilo wikiendi iliyopita na kuthibitisha kwamba, yeye ni Boss Lady wa ukweli ambaye anaweza kufanya makubwa hata bila kuwa na mwanaume, tofauti na wengi walivyodhani kwamba kummwaga Diamond ndiyo utakuwa mwisho wake. Vyanzo vilikwenda mbali zaidi na kutaja thamani ya gari hilo la Zari kuwa ni zaidi ya shilingi milioni 171 huku lile la Diamond likiwa na thamani ya shilingi milioni 150.

Zari alitangaza mpango wake wa kununua gari hilo wiki chache zilizopita na hatimaye wikiendi hii alilianika gari hilo jipya na kuliweka kwenye mitandao ya kijamii. Zari alitimiza azma yake hiyo kama alivyoahidi mapema mwaka huu kwamba, kuna mambo alipanga kuyafanya ndani ya Mwaka 2018 ikiwemo kulimiliki gari hilo.

Hata hivyo, mara baada ya kuliweka gari hilo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika; ‘Come through baby girl’, baadhi ya watu walidai kwamba, gari hilo amenunuliwa na mwanaume wake mpya ambaye ni mfanyabiashara maarufu jijini Dar (uchunguzi wetu ukikamilika tutamwanika).

Kufuatia madai hayo, Zari alikanusha kupitia ukurasa wake wa Snapchat ambapo aliweka wazi kuwa amelinunua kwa fedha zake mwenyewe. Mbali na gari hilo, mwaka huu, Zari pia aliahidi kuanzisha migahawa mikubwa kama KFC au McDonalds.

Ili kusikia maoni yake juu ya kufuru za Zari ambazo zimelenga kumkata ngebe, katika harakati za kumsaka Diamond gazeti hili lilifika kwenye ofisi mpya za Wasafi zilizopo Kwazena, Mbezi-Beach ambapo lilijuzwa kuwa jamaa huyo alikuwa nchini Uingereza kikazi.

Alipotafutwa kwa njia ya WhatsApp, Diamond hakujibu ‘chatting’ hivyo jitihada zinaendelea ili kupata maoni yake. Hata hivyo, mmoja wa watu waliokutwa ofisini kwake alisema hawezi kuzungumzia masuala binafsi badala yake aulizwe mambo ya kazi yake ya muziki.

Zari, mbali na gari hilo, pia alishaanika umiliki wake wa magari ya kifahari kama Mercedez Benz, Audi, Hammer, Ferrari na mengineyo huku Diamond akimiliki magari mengine kama Toyota Prado, Toyota Land Cruiser V8 na mengine madogomadogo.

Yanga Yaipigia Saluti Simba “Kwa Hali Ilivyo Simba Ndiyo Mabingwa"

$
0
0
Yanga Yaipigia Saluti Simba “Kwa Hali Ilivyo  Simba Ndiyo Mabingwa"
HATIMAYE benchi la ufundi la Klabu ya Yanga limeamua kukubali kuwa wapinzani wao Simba kwa msimu huu ndiyo mabingwa huku wao sasa wakijipanga kuelekeza nguvu zao katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.



Yanga ndiyo mabingwa watetezi wa ligi kuu baada ya kuutwaa msimu uliopita wakiwazidi Simba kwa mabao ya kufunga lakini kwa msimu huu hadi sasa wanakamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wakiwa na pointi 48 ambazo ni pointi 17 nyuma ya Simba wanaongoza ligi wakiwa na pointi 65.



Akizungumza na Championi Jumatano, muda mfupi baada ya kurejea kutoka nchini Algeruia, Kocha Mkuu wa Yanga, Mkongomani Zahera Mwinyi alisema kwa sasa wamekubali kuwa wapinzani wao ndiyo mabingwa wa ligi huku wao wakielekeza nguvu sasa katika michuano ya kimataifa ambayo wanashiriki.



“Kwa hali ilivyo kwa sasa Simba ndiyo mabingwa wa ligi kwa msimu huu huku sisi tumepanga kwa sasa kuelekea nguvu zetu katika michuano ya kimataifa ambapo tunashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.


“Tunaelekeza nguvu huko kwa sababu hapa Tanzania hatuwezi kuwa mabingwa lakini pia Kombe la FA tumeshatolewa,” alisema Zahera.

Akizungumzia juu ya mwanzo mbaya wa kikosi hicho katika mchezo wake wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika, Mkongomani huyo alisema:



“Tulienda na wachezaji ambao hawana uzofu na michuano hii na ndiyo sababu iliyochangia kwetu kufungwa mabao 4-0 mbele ya wapinzani wetu, licha ya kwamba walifuata maelekezo ya kile ambacho niliwaambia.



“Wachezaji wale muhimu tuliwaacha hapa Dar, utaona jinsi jambo hilo lilivyoweza kuchangia sisi kupoteza mechi yetu ya huko. Nimepanga kuongea na uongozi ikiwezekana kwamba kuwe na timu mbili ambapo moja itaenda Mbeya kucheza na Mbeya City (kesho Alhamisi) halafu ikimaliza iende pia Morogoro kucheza na Mtibwa.



“Wakati huohuo pia kuwe na timu ambayo nitabaki nayo hapa Dar ambayo itajumuisha wale wachezaji ambao hawakwenda Algeria ambao nitakaa nao na kuzungumza, hii timu nitawapa mafunzo kuhakikisha kwamba inafanya vyema kwenye mchezo wetu dhidi ya Rayon Sport.



“Nafanya hivyo kwa sababu nataka nguvu zetu nyingi tuelekeze huko kwenye michuano ya kimataifa kwani ndiyo nafasi pekee ambayo imebaki kwetu kuona tunashiriki michuano ya Afrika kwa msimu ujao, kwani hakuna sehemu nyingine zaidi ya huku hivyo yatupasa kuweka nguvu zaidi,” alisema Mkongomani huyo.

Kuna Wasanii Wanatoa Nyimbo Mbaya wanabaki Wanakomaa na Ma- interview tu- Ommy Dimpoz

$
0
0
Kuna Wasanii Wanatoa Nyimbo Mbaya wanabaki Wanakomaa na Ma- interview tu- Ommy Dimpoz
Wasanii wa muziki Bongo, Ommy Dimpoz amesema kuna baadhi ya wasanii ‘wanatoa’ nyimbo mbaya ila wasanii wanzao wanaogopa kuwaambia.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Yanje’ hilo linatokana wale wanaosema ukweli kuchukiwa siku zote.

“Kuna nyimbo za wasanii wenzangu na nyingine unaona huu wimbo gani na unaona mwana anakomaa na ma-intervie,” amesema.

Amesema ni vigumu kumwambia ukweli msanii mwenzako kwamba wimbo wako si kiwango hicho kutokana tayari ameshawekeza.

“Na siku zote wasema ukweli wanachukiwa, kuna siku niko na washikaji jamaa anamwambia mwana lakini ule wimbo wenu mnaenda ku-shoot video?, mbona ngoma mbaya, nikasema unatoa wapi ujasiri wa kumwambia mtu hivyo,” Dimpoz ameiambia Magic FM.

Utakumbuka kipindi cha nyuma Barakah The Prince aliingia kwenye headlines mara baada ya kudai wimbo wa Ben Pol ‘Tatu’ ni mbaya, hata Godzill aliwahi kufanya kitu kama hicho kwa Nay wa Mitego.

Ebitoke Ashindwa Kumuelewa Shilole " Mi najua ni Mpishi Tu"

$
0
0
Ebitoke Ashindwa Kumuelewa Shilole " Mi najua ni Mpishi Tu"
Mchekeshaji maarufu wa kike nchini Tanzania, Ebitoke ameshindwa kuelewa kama Shilole ni msanii wa muziki au muigizaji kwani hafahamu hata kazi moja ya sanaa ambayo mrembo huyo alishawahi kuifanya zaidi ya kazi yake ya mama ntilie anayoifanya kwa sasa.

Ebitoke amesema hayo leo kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV, alipotakiwa na moja ya wafuatiliaji wa kipindi hicho ataje wimbo japo mmoja wa msanii huyo wa Bongo Fleva na kuuimba.

“Labda unitajie nyimbo zake mimi sizijui kazi zake, mimi najuaga yeye ni mpishi tu ila kwenye nyimbo hapa mtanisamehe sijui nyimbo zake.. Nisiwe muongo naongea ukweli na sio kiki kama mlivyozoea mambo ya kiki siku hizi nimeacha.“amesema Ebitoke.

Kwa upande mwingine Ebitoke amesema kuwa watu wengi wanamuona mchekeshaji lakini hiyo sio kazi anayoipenda katika maisha yake anapenda kuwa muigizaji na ndoto yake kubwa ni kuja kushinda tuzo ya Oscar ili kuitangaza zaidi Tanzania .

Shilole ni muigizaji wa kwanza kuacha fani hiyo na kukimbilia kwenye muziki ambapo tangu aingie ametoa nyimbo kibao kama Nakomaa na jiji, Kigori, Lawama, chuna buzi na nyingine nyingi.

Alichokisema Mbowe Baada ya Sugu Kuachiwa

$
0
0
Alichokisema Mbowe Baada ya Sugu Kuachiwa
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe amesema kwamba baada ya Sugu kuachiwa hatakwenda Bungeni moja kwa moja licha ya kwamba Bunge linaendelea, ila watamuacha arekebishe masuala yake ya kifamilia kwanza.


Mbowe ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza na East Africa Radio, na kusema kwamba haitakuwa vyema kwa Mbunge huyo ambaye alikuwa akitumikia kifungo chake kumruhusu kwenda Bungeni mara moja, kwani ana mambo ya muhimu ya kushughulikia kwanza.

Sambamba na hayo Mbowe amesema alifika kwenye Gereza la Ruanda kumpokea Sugu akiwa na baadhi ya wanafamilia na viongozi wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, wakisubiria kukamilika kwa utaratibu wa kuachiwa huru kwa watu hao.

“Kwa vyovyote kwa mtu aliyekaa gerezani kwa siku zote hizi si rahisi kumtoa leo na kumpeleka Bungeni kesho, ila kwanza lazima mambo yake ya kifamilia yakitulia na mambo mengine akishayamaliza ndio tutaweza kujua ratiba ya Bunge inakuwaje, lakini ataweza kwenda Bungeni, hivi ninavyozungumza nipo mbele ya Gereza la Ruanda hapa Mbeyea, niko na kundi kubwa tu la viongozi Kanda ya Nyasa, wanafamilia na wanachama wa Chadema ambao wamekuja kuwapokea”, amesema Mbowe.

Sugu na Emmanuel Masonga walihukumiwa kifungo cha miezi mitano jela Februari 26, 2018, kwa kosa la kutoa lugha za kashfa.

Al-Shabab Wampiga Hadi Kifo Mwanamke Aliyedaiwa Kuolewa Mara 11 Somalia

$
0
0
Al-Shabab Wampiga Hadi Kifo Mwanamke Aliyedaiwa Kuolewa Mara 11 Somalia
Mwanamke mmoja amepigwa na mawe mpaka kifo nchini Somalia baada ya mahakama moja inayoendeshwa na kundi la wanamgambo wa kiislamu, al-Shabab kumkuta na hatia ya kuolewa na wanaume wengi.

Shukri Abdullahi Warsame alishutumiwa kuolewa mara 11 bila kutalikiwa na waume zake waliopita.

Sehemu ya kiwiliwili chake kilifukiwa ardhini kichwa kikiachwa juu kisha akapigwa mawe na wanamgambo mjini Sablale mpaka umauti.


Mwaka 2014,wapiganaji wa al-Shabab walimpiga mwanamke mmoja na mawe baada ya kumshutumu kuolewa na wanaume wanne kwa siri, wilaya ya Barawe nchini humo.

Wema Sepetu Alamba Shavu Ubalozi Tatu Mzuka

$
0
0
Wema Sepetu Alamba Shavu Ubalozi Tatu Mzuka
Kampuni ya ‘The Network‘ kupitia mchezo wake namba moja wa bahati nasibu nchini Tanzania wa ‘Tatu Mzuka‘leo May 9 2018 imetangza rasmi kushirikiana kibiashara na Muigizaji maarufu Wema sepetu.

Akizungumza na waandisi wa habari Wema Sepetu amesema anafurahi kushirikiana na Tatu Mzuka ambapo fursa hiyo haitamgusa yeye tu bali pia kwa mashabikki zake na Tanzania kwa ujumla kwa kujitengenezea fursa na kuboresha maisha yao.

Ebitoke: Sijaumia Bikira Yangu Kuondolewa, Dunia ya Kujivunia Bikira Imepita

$
0
0
Ebitoke: Sijaumia Bikira Yangu Kuondolewa, Dunia ya Kujivunia Bikira Imepita
Mchekeshaji kutoka Timamu, Ebitoke amedai bikira yake kuondolewa na muimbaji Ben Pol sio ishu kwenye maisha yake kwani kipindi cha mwanamke kujivunia bikira kimeshapita.

Akiongea akiwa Kikaangoni ya EATV, Ebitoke amedai kilichotokea katika maisha yake juu ya mahusiano na Ben Pol sio kitu kibaya, kwani wakati yupo naye mapenzi yalikuwa moto moto hivyo aliitendea haki nafsi yake.

“Kweli bikira yangu imetoka lakini sijaumia hata kidogo, maisha ya sasa yamebadilika, sasa hivi sio kama zamani bila bikira hauolewi,” alisema Ebitoke “Yote niliyopitia nikiwa na Ben Pol ni sehemu ya maisha yangu, sijawahi kujuta kwa sababu najua nimpata mwanaume mwingine,”

Katika hatua nyingine amewataka mashabiki wa vichekesho vyake kukaa mkao wa kula kwaajili ya filamu yake mpya itakayotoka mwakani.

Wasiliana na Dr Mabula Anatibu Upungufu wa Nguvu za Kiume, Busha na Matatizo ya Maumbile Madogo kwa Mwanaume

$
0
0
TUNATIBU NA KUPONESHA KABISA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME UUME MDOGO BUSHA BILA KUPASUA PRESHA VIDONDA VYA TUMBO
Asilimia kubwa ya wanadamu wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali na wapo waliongahika sehemu mbalimbali bira MAFANIKIO MABULA CLINIC ni kituo cha tiba asilia kilichopo mbagara zakhemu njia kuu ya JESHINI JE HUNAUPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME AU UUME WAKO MDOGO NA MWEMBAMBA?

MAPRO PAWER NO 2 ndio Tiba kwa sasa utibu matatizo matatu kwa pamoja 1hitakufanya uchelewe kufika kilekeni dikika 15-20 kwa tendo la kwanza 2 uhimalisha misuli iliyoregea na kusinyaa hasa kwa wale walio hasirika na upigaji punyeto 3 itakufanya upate amu ya kurudia tendo zaidi ya Mara tatu

KWA NINI UJIONE MPWEKE PALE UKUTANAPO NA MPENZI AU MKE WAKO kisa unawai kukojoa au unakomea bao moja tu na huku dawa zipo MAKAKANUA mix ni dawa iliyochanganywa na miti Shamba 9 na Kuwa na uwezo wa kuongeza uume saizi upendayo inchi 5-8 Kwa Urefu na unene sentimita 1-5 dawa hizi hazina madhara yoyote kwa mtumiaji ata wazee wenye umri mkubwa wanapona? zipo dawa za mvuto wa mpenzi mme au mke Kwa masaa matatu tu na kukupigia simu yeye mwenyewe mvuto wa biashara kutengeneza mwonekano mzuri wa mwili kwa wanawake yani shepu tunatibu ngiri miguu mgongo na kiuno kuumwa kupunguza kitambi minyama uzembe matiti na mwili mkubwa

TIBA NA USHAULI MUONE DR MABULA AU PIGA SIMU NO 0752348593 UDUMA ZANGU UTAZIPATA POPOTE ULIPO KAMA UWEZI KUFIKA OFISINI

Sijui Kilichonifanya Niachiwe Kwani Nilijua Nitaachiwa Huru Mwezi wa 6- Mbunge Sugu

$
0
0
Sijui Kilichonifanya Niachiwe Kwani Nilijua Nitaachiwa Huru Mwezi wa 6- Mbunge Sugu
Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu ambaye ameachiwa huru leo kutoka gerezani alikofungwa akiwa na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga, amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kutoka jela.


Akizungumza na East Africa Radio, Sugu amesema hakuwa anajua kama anaachiwa mpaka pale alipofuatwa na polisi kuambiwa ajiandae, na hajui imekuwaje mpaka akaachiwa sasa kwani ilijulikana ataachiwa huru mwezi wa 6.

“Watu wote walikuwa wanatarajia nitoke mwezi wa 6, lakini ghafla hapo jana niliambiwa nijiandae kwamba kesho asubuhi natakiwa niachiwe, kutoka nje nikakuta askari wengi na nikaelekezwa kuingia kwenye gari la RCO mimin a mwenzangu Masonga, tukasindikizwa na maafisa magereza watano wakatupeleka mpaka nyumbani na kutukabidhi kwa familia”, amesema Sugu.

Sugu ameendelea kusema kwamba..."watu wanauliza imekuwaje lakini mimi nawaambia sijui kwa sababu haikuwa kazi yangu kufanya hesabu za magereza, hiyo ni kazi ya magereza, kwa sababu mimi kama mimi ninachoamini sikutakiwa kuwa magereza in the first place, utumishi uko pale pale kwa level ile ile tulikuwa na exposure sasa hivi tumeongeza experience”.

Wawili hao wameachiwa huru leo kutoka gereza kuu la Ruanda mkoani Mbeya walikokuwa akitumikia kifungo chao cha miezi mitano, jambo ambalo limewashtua wengi kwani inaaminiwa muda wake ulikuwa bado haujaisha.

Wadau: Spika Amesimamia Haki na Kuonyesha Wajibu kwa Wabunge

$
0
0
Wadau: Spika Amesimamia Haki na Kuonyesha Wajibu kwa Wabunge
Wadau wamempongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kwa kuonesha nguvu ya Bunge katika kusimamia maslahi ya Taifa, nakubainisha hatua hiyo itaweza kujenga imani kwa wananchi juu ya Bunge lao.


Akizungumza kwenye kipindi cha Easta afrika BreakFast kinachorushwa na East Afrika Radio, mtaalamu wa siasa za kikanda, Amini Mgeni amesema Spika wa bunge la Tanzania amesimamia haki na kuonesha wajibu wa wabunge katika kusimamia maslahi ya wananchi, jambo ambalo linapaswa kuigwa na wabunge wote.

"Hivi ndivyo bunge linavyopaswa kuwa ni mhimili unaojitegemea na unapaswa kuikosoa serikali nakutetea wananchi maana wao ni wakilishi wa watanzania wengi waliowapa dhamana, Spika Ndugai ataheshimika daima kama ataendelea na msimamo wake huu bila kuangalia chama", amesema Amini.

Mei 8, 2018 Spika Ndugai aliyakataa maelezo ya Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Charles Mwijage nakumtaka atoe majibu yakueleweka kuhusu uhaba wa mafuta nchini, jambo ambalo Waziri Mwijage aliahidi atalitolea ufafanuzi saa 11 jioni ya siku hiyo hata hivyo ilishindikana na hatimaye jana Mei 9, 2018 akaweza kutolea ufafanuzi.

Msimamo wa Spika uliwakosha pia baadhi ya wabunge wa upinzani akiwemo kiongozi wa chama cha ACT wazalendo, Zitto Kabwe ambaye aliweza kuelezea hisia zake na kumtaka Spika Ndugai aendelee kuwa kiongozi imara wa bunge kwa kuikosoa serikali pale inapoenda kinyume na maslahi ya wananchi.

Zitto Kabwe Agoma Kumpa Pole Sugu Baada ya Kutoka Gerezani "Siwapi Pole Maana Wapinzani Wote Wafungwa Watarajiwa"

$
0
0
Maneno ya Zitto Kabwe Baada ya Sugu Kuachiwa Huru "Siwapi Pole Maana Wapinzani Wote Wafungwa Watarajiwa"
Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe amesema kuwa amefurahi kuona Mbunge mwenzake wa Mbeya Mjini kupitia tiketi ya CHADEMA, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu pamoja na mwenzie Emmanuel Masonga wakitoka gerezani lakini amekataa kuwapa pole kwa kile alichodai kuwa viongozi wote wa upinzani kwa sasa ni wafungwa watarajiwa.

Zitto amesema kuwa anaamini kukaa kwao gerezani kumewaongezea zaidi ari ya kupambania Demokrasia pana ya nchi yetu.

“Nafurahi kuwa Mbunge Mbeya Mjini Ndg. Joseph Mbilinyi (Sugu) na mdogo wangu Emmanuel Masonga wametoka Gerezani! siwapi pole, maana katika nyakati za Udikteta wapinzani wote ni wafungwa watarajiwa. Naamini kukaa kwao gerezani kumewaongezea zaidi ari ya kupambania Demokrasia pana ya Nchi yetu.Watawala mjue sasa kuwa vifungo vya Uonevu, kututishia Maisha na hata kutupiga risasi havita turudisha nyuma kwenye kupigania demokrasi ya nchi yetu.“ameandika Zitto Kabwe kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Mhe. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ameachiwa huru leo Mei 10, 2018 kutoka gereza la Ruanda, Mbeya alipokuwa akitumikia kifungo cha miezi mitano kwa makosa ya uchochezi.
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images