Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Irene Uwoya Ahofia Kutokewa na Mzuka wa Masogange

$
0
0
 Irene Uwoya Ahofia Kutokewa na Mzuka wa Masogange
Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amesema tangu rafiki yake Agnes Gerald ‘Masogange’ atangulie mbele ya haki amekuwa akihofia kutokewa na mzuka wake.

Uwoya ambaye alikuwa na ukaribu mkubwa na rafiki yake marehemu Msasogange amekiri kuwa tangu msiba huo amekuwa na hofu hata ya kukaa mwenyewe.

Kwenye mahojiano aliyofanya  hivi karibuni na Global Publishers , Uwoya alisema, kwa jinsi walivyokuwa karibu na Masogange, amekuwa akiwaza mengi na ndiyo maana ameshindwa kabisa kuishi katika nyumba ile waliyokuwa wanaishi jirani na mrembo huyo, maeneo ya Makongo Juu jijini Dar.

"Nahofia kweli jamani kutokewa na Masogange. Kwa sasa imenibidi niwe mtu wa kujichanganya sana ili nisiwe namkumbuka Masogange”.

Masogange aliaga dunia wiki chache zilizopita baada ya Kuugua na kulazwa katika hospitali ya Mama Ngoma na kisha baadae kuzikwa kijijini kwao  Mbeya.

Kenya Kutimiza Ndoto Yao ya Kisayansi Leo Kuzindua Satelaiti Katika Anga ya Juu

$
0
0
Kenya Kutimiza Ndoto Yao ya Kisayansi Leo Kuzindua Satelaiti Katika Anga ya Juu
Kenya inajiandaa kutimiza ndoto kubwa ya kisayansi leo Ijumaa. Chombo cha Satelaiti kilichoundwa nchini humo kitarushwa katika anga za juu hii leo kutoka nchini Japan.

Chombo hicho kilibuniwa na wanasayansi kutoka Chuo

Wanasayansi wa anga za juu kutoka Kenya waliokiunda chombo hicho tayari wako katika makao ya Uchunguzi wa Sayansi ya Anga za juu nchini Japan, (JAXA) ambapo chombo hicho kitarushwa kutoka huko.

Nchini Kenya kwenyewe raia wataweza kufuatilia shughuli hiyo moja kwa moja kwenye mtandao wa You Tube, na sherehe maalumu ya kushuhudia imeandaliwa katika chuo kikuu cha Nairobi.

Satelaiti hiyo ndogo ni ya thamani ya dola milioni moja - gharama inayoonekana kuwa ndogo kifedha kwa kiwango cha sayansi ya anga za juu.

Tanzania Prisons Yawafanyia Mbaya Yanga Yawavua Ubingwa Peupe

$
0
0
Tanzania Prisons Yawafanyia Mbaya Yanga Yawavua Ubingwa Peupe
Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga imekubali kipigo cha mabao 2 – 0 dhidi ya TZ Prisons kwenye dimba la Sokoine jijini Mbeya.

Kukubali kipigo cha mabao hayo 2 – 0 dhidi ya TZ Prisons kinaifanya Yanga kuvuliwa ubingwa rasmi wa ligi kuu Tanzania Bara.

Yanga yenye pointi 48 ilihitaji kushinda michezo yote sita huku akiiyombea dua baya hasimu wake Simba kupoteza walau mechi moja ili kujihakikishia kutwaa ubingwa huo kwa mara ya nne mfululizo lakini hali imekuwa tofauti hii leo baada ya kukubali kipigo hicho mbele ya Prisons.

Mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba mpaka sasa inajumla ya pointi 65 huku ikisaliwa na michezo mitatu mkononi kabla ya kumaliza msimu huu wa mwaka 2017/18.

Waliopeleka kilio mitaa ya Jangwani hii leo ni wachezaji, Eliuter Mpepo katika dakika ya 58 na Salum Bosco kunako dakika ya 85 ya mchezo.


Haji Manara Akataa Kuitwa Msemaji wa Simba " Niite Msemaji wa Mabingwa wa Nchi"

$
0
0
Haji Manara Akataa Kuitwa Msemaji wa Simba " Niite Msemaji wa Mabingwa wa Nchi"
Alhamisi ya May 10 2018 Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara club ya Dar es Salaam Young Africans walikuwa Sokoine Mbeya kucheza mchezo wao wa 25 wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Tanzania Prisons.

Yanga wakiwa Mbeya wamekubali kupoteza mchezo mbele ya Tanzania Prisons kwa magoli 2-0, hivyo kipigo hicho kimeifanya Simba kutangazwa Bingwa wa VPL msimu wa 2017/2018 wakiwa na point 65 na michezo mitatu mkononi.

Samatta Aikoa Timu Yake na Kipigo Atandika Goli Moja

$
0
0
Samatta Aikoa Timu Yake na Kipigo Atandika Goli Moja
Kikosi cha KRC Genk jana anachocheza Mtanzania, Mbwana Samatta, jana kilikwenda sare ya bao 1-1 dhidi ya KAA Gent katika mchezo wa Play Offs kwenye ligi ya Ubelgiji.

Samatta aliingia Uwanjani dakika ya 54 ya mchezo akitokea benchi kuchukua nafasi ya Mgiriki Nikolaos Karelia wakati timu yake ikiwa nyuma kwa bao 1-0.

Baada ya Samatta kuingia Uwanjani, ilimchukua takribani dakika 12 kuisawazishia Genk katika dakika ya 66 ya mchezo na mechi hiyo mpaka inamalizika matokeo yalikuwa ni 1-1.

Matokeo hayo yameifanya Genk kufikia jumla ya pointi 32 ikiwa imecheza jumla ya mechi 8 ikikamata nafasi ya 6.

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Siku ya Leo

$
0
0

Dawa Bora za Nguvu za Kiume na Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa

$
0
0
DAWA BORA ZA NGUVU ZA KIUME NA KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA
Baada ya utafiti wa muda mrefu juu ya matatinzo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurundia tendo kwa haraka Sasa inakuletea suluhisho juu ya matatizo haya kwa kutumia dawa za FULL POWER

Full Power dawa asili yenye vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume dawa hii inamchanganyiko wa kutosha kuzalisha vichocheo vingi vya hernone za gestro gen zikiwemo vitamin b6 na b1 vitamin e pamoja na madini aina ya zinc

Itakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wakufanya tendo la ndoa zaidi hatua nne au zaidi na kuchelewa kufika kileleni zaidi ya dakika 20/30 ZAT 50

Inarundisha maumbile ya uume yaani kurefusha na kunenepesha nchi 3/7 na upana cm 3/4 standard.kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukitumia maumbile yatabaki kuwa hivyo siku zote pia anatibu matatizo mengine kama presha kisukari ngiri chango la tumbo kujaa gesi kutopata choo vizuri minguu kuwaka moto matatizo ya uzazi bawasili na magonjwa ya zinaa kama kisonono na kaswende

Tunapatikana Dar es Salaam  na mikoan wasiliana na DR Oshinda no 0755505099 au 0714126118  Karibuni kwa hunduma bora

Nina Nyumba Mombassa kwa Sasa Nikaenda Nafikia Nyumbani- Alikiba

$
0
0
Nina Nyumba Mombassa kwa Sasa Nikaenda Nafikia Nyumbani- Alikiba
Msanii wa muziki kutoka RockStar4000, Alikiba amethibitisha kuwa na nyumba yake ya kuishi Mombasa nchini Kenya.


Muimbaji huyo ambaye amezindua kinywaji chake cha Mofaya siku ya sherehe ya harusi yake, amesema kwa sasa akienda Mombasa nafikia nyumbani kwake kwani tayari ana nyumba.

“Mombana nina nyumba tayari, sasa hivi nikienda nafikia nyumbani,” Alikiba alikiambia kipindi cha 360 cha Clouds TV baada ya kuulizwa na mtangazaji kama ana mpango wa kujenga nyumba au kununua.

Katika hatua nyingine muimbaji huyo amesema kinywaji chache cha Mofaya kitaingia sokoni rasmi ya siku kuu ya Eid el Fitri mapema mwezi ujao huku akishindwa kuweka wazi bei ya kinywaji hicho.

Alisema kwa sasa wametangaza deal kwa makampuni mbalimbali ambayo yatapenda kuwa mawakala wa kusambaza kinyaji hicho ambazo kimeonekana kuwa muaarufu kwa siku za karibuni.


Ningekuwa wa Ajabu Kama Ningeondoka Simba Bila ya Kupata Ubingwa- Haji Manara

$
0
0
Ningekuwa wa Ajabu Kama Ningeondoka Simba Bila ya Kupata Ubingwa- Haji Manara
Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Mabingwa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC, Haji Manara amefunguka na kudai angekuwa mtu wa ajabu kama angeondoka wekundu wa Msimbazi bila ya kupata ubingwa wowote wa ligi kuu.


Manara ametoa kauli hiyo muda mchache klabu ya Mabingwa Watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kukabidhi rasmi ubingwa kwa watani wao wa Jadi, Simba SC baada ya kuchapwa bao 2-0 na wenyeji wao Tanzania Prisons 'wajela jela' mchezo ulichezwa katika dimba la Sokoine Jijini Mbeya jioni ya Mei 10, 2018.

"Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma, ametusikia na kutupa malipo tuliyokuwa tunastahili, tumepambana lakini niwashukuru sana wachezaji wetu wa Simba kwa kutambua dhamira yetu ya kupata ubingwa. Lakini niwaambie tu kwamba bado hatujaridhika kwasababu tunataka tumalize ligi hii bila ya kufungwa", amesema Manara.

Pamoja na hayo, Manara ameendelea kwa kusema "hakuna mwanasimba yeyote mwenye furaha kama niliyo kuwa nayo mimi maana nimeumia sana ndani ya miaka minne hii, nimetukanwa, nimedhalilishwa na kufedheheshwa sana lakini Mwenyezi Mungu amenilipia. Ningekuwa mtu wa ajabu sana kama ningeondoka Simba bila ya kupata ubingwa wa ligi kuu".

Kwa upande mwingine, Manara amewakataza watu wasimuite msemaji wa mabingwa wa Tanzania bali aitwe msemaji wa mabingwa wa nchi.

Shirika Linalotetea Watu Wanaotaka Kufa Limetangaza Kifo cha Mwanasansi David Goodal Aliyejiua kwa Sumu

$
0
0
Shirika Linalotetea Watu Wanaotaka Kufa Limetangaza Kifo cha Mwanasansi David Goodal Aliyejiua kwa Sumu
Mwanasayansi David Goodall mwenye miaka 104, aliyesafiri kutoka Australia hadi Uswizi ili kujitoa uhai amefariki May 10, 2018 usiku katika kliniki moja nchini Uswizi, shirika linalotetea haki za watu wanaotaka kufa limetangaza.

Mwanaikolojia huyo ambaye pia alikuwa mtaalamu wa mimea hakuwa anaugua lakini alisema kuwa aliamua kujitoa uhai kutokana na kudhoofika kwa ‘ubora wa maisha yake’.

Uswizi, ni nchi pekee iliyo na vituo vinavyotoa huduma hiyo kwa raia wa mataifa mengine, huduma ambayo inaruhusu watu kujitoa uhai.

Trump Atangaza Tarehe Atakayokutana na Kim Jong Un

$
0
0
Trump Atangaza Tarehe Atakayokutana na Kim Jong Un
Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kwamba atakutana na kiongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK), Kim Jong Un, nchini Singapore tarehe 12 mwezi Juni.

Trump aliushangaza ulimwengu April alipotangaza kwamba amekubali mwaliko wa kukutana moja kwa moja na Kim.

Trump alitangaza uamuzi wake saa chache baada ya kuwakaribisha nyumbani Wamarekani watatu ambao wamekuwa wakizuiliwa na Korea Kaskazini ambao waliachiliwa huru na kuruhusiwa kurejea nyumbani.

Alikiba Afunguka Namna Alivyokutana Mrembo Mombasa Hadi Kuwa Mkewe

$
0
0
Alikiba Afunguka Namna Alivyokutana Mrembo Mombasa Hadi Kuwa Mkewe
Msanii wa muziki wa Bongo, Alikiba amefunguka namna alivyokutana na mkewe kutokea Mombosa, Kenya na sababu ya usiri katika mambo yake mengi anayofanya.

Muimbaji huyo katika kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV amesema kutokana na safari zake za mara kwa mara nchini Kenya aliweza kukutana naye, pia Gavana wa Mombasa, Hassan Ali Joho alihusika kufanikisha hilo.

“Yeah Joho ni mtu ambaye aliniongoza sana kwenye maswala ya msingi, kama nilivyokuwambia kwenye masuala ya dini, mimi na mke wangu tulikutana Nairobi, tukajuana tukaanza kuwasiliana,” amesema.

“Tulivyokuwa marafiki na Hassan nikamwambia kaka kuna msichana anakaa hapa, akaniambia kama ni kuoa basi process zifuatwe nilipoonja Mo Faya tu!, nikaoa hapo hapo,” amesema Alikiba.

Katika hatua nyingine amesema sababu ya kufanya siri baadhi ya mambo yake kama alivyofanya katika ujio wa kinywaji chake, Mo Faya ni kutokana na kutengeneza shauka ya kutaka kujua zaidi na pia ndio tabia yake.

“Kwa sababu muamko unakuwa mkubwa zaidi wanakuwa hawategemei ni kitu gani Alikiba anaweza akafanya, kwa hiyo kama ni kitu kizuri watu wanakuwa wanafurahi zaidi,” amesema.

Alikiba alioa April 19, 2018 Mombasa nchini Kenya na sherehe ya pili iliyofanyika April 29, Dar es Salaam, Tanzania ndipo alitambulisha rasmi bidhaa yake ya energy drink, Mo Faya.

Video: Shangwe, Vurugu za Wachezaji wa Simba Baada ya Kuwa Mabingwa

$
0
0
Video: Shangwe, Vurugu za Wachezaji wa Simba Baada ya Kuwa Mabingwa
Simba wanakabidhiwa ubingwa wakiwa mjini Singida hata kabla ya kuivaa Singida katika mechi yao ya Ligi Kuu Bara, kesho Jumamosi. Hii inatokana na waliokuwa mabingwa watetezi, Yanga kufungwa kwa mabao 2-0 dhidi ya Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Kufungwa kwa Yanga kuinaifanya ibaki na pointi 48 katika nafasi ya tatu, Azam FC katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 49 na Simba sasa wanachukua ubingwa wakiwa na pointi 65. Simba wanachukua ubingwa wakiwa na pointi tatu mkononi.

Rosa Ree Ajikwamua Kuja na Mini Supermarket Yake Yenye Thamani ya Zaidi ya Milioni 30

$
0
0
Mwanamuziki wa Bongo fleva Rose Kimario maarufu kama Rosa Ree ameingia Kwenye ulimwengu wa kibiashara baada ya kufungua mini supermarket yake mpya aliyoipa jina la Rosa Ree Mini Supermarket.

Risa Ree alitumia ukurasa wake wa Instagram kutangaza habari hiyo njema.

Rosa Ree amefanya Interview na Millard Ayo Tv na ameweka wazi kuwa imemgharimu zaidi ya milioni 30 kuwekeza Kwenye biashara ile

"Ile ni Supermarket yangu na ninategemea kuifungua rasmi wiki ijayo hivi sasa tupo Kwenye maandalizi ya mwisho ni kitu ambacho nilipanga kufanya kwa muda mrefu sasa.

"Kusema ukweli nimewekeza pesa nyingi lakini kwa haraka haraka nimewekeza zaidi ya milioni 30 na nina mpango wa kufungua supermarket kubwa zaidi ya ile”.

TAZAMA VIDEO:

Nigeria Yaimarisha Ulinzi Yapima Ebora Airport

$
0
0
Nigeria Yaimarisha Ulinzi Yapima Ebora Airport
Kutoka nchini Nigeria, vyombo vya ulinzi vimeimarisha ulinzi kwenye viwanja vya ndege, bandari na mipaka ya nchi hiyo kwa kupima abiria, baada ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kutangaza kuingia kwa ugonjwa wa Ebola nchini kwao wiki hii.

Waziri wa Afya wa Nigeria Isaac Adewole ameliambia Shirika la Utangazaji la CNN kwamba wamegundua watu takriban 17 waliokuwa wakisafiri wanakisiwa kufariki kwa virusi hivyo vya homa ya Ebola.

Inaelezwa kuwa miili ya watu hao itafanyiwa uchunguzi wa halijoto katika mipaka ya nchi hiyo.

“Tunaimarisha ulinzi, na wanaotokea DRC watakaguliwa na kusimamiwa na mamlaka husika baada ya kuondoka kwenye viwanja hivyo vya ndege, bandari na mipakani.” – Isaac Adewole

Nimegundua Wanaume Wengi Kwa Sasa Upendelea Kuao Wadada Wenye Tabia Hizi

$
0
0
Katika pitapita zangu, na kujionea maisha ya wanaume wenzangu, nimegundua kuwa wanaume wengi hupenda kuoa wanawake wapole ambaye akijadiliana nae jambo hapandi juu kama kifuu cha Nazi ya moto, vile vile mwenye uchumi mdogo asimzidi yeye na zaidi awe na hofu na Mungu na kumshauri mwanaume anapokosea pia Mwenye Mawazo ya Kimaisha.

Wale Wapenda Starehe Ambao ni Wengi kwa Kipindi Hichi Tunawapenda tu kwa Starehe za Muda ila Kuoa na Kuweka Ndani ni Nadra Sana..Je Utafiti wangu ni Sawa ?

Breaking News: Mbunge Viti Maalumu wa Singida Ambaye Mke wa Kafulila Apata Ajali

$
0
0
Breaking News: Mbunge wa Singida Ambaye Mke wa Kafulila Apata Ajali
Mbunge wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Singida kupitia CHADEMA, Jesca Kishoa, amepata ajali leo Mei 11, 2018 majira ya saa nne asubuhi Jijini Dodoma.


Mume wake David Kafulila amethibitisha na sasa amefikishwa katika Hospitali ya Bunge.

“Nimeshtuka sana kupokea taarifa za ajali hiyo, kama mnavyoona kwenye picha ajali ilikuwa mbaya sana na gari limeharibika vibaya. Baada ya ajali hiyo yeye alipatwa na mshituko wa moyo, lakini mpaka sasa anaendelea vizuri, kwa sasa nipo njiani naelekea huko Dodoma huko hospitali,” amesema Kafulila.



Mwanamke Ahukumiwa Kifo kwa Kumuua Mumewe Aliyembaka

$
0
0
Mwanamke Ahukumiwa Kifo kwa Kumuua Mumewe Aliyembaka
Mahakama moja nchini Sudan imemhukumu kifo mwanamke mwenye umri wa miaka 19 kwa kumuua mumewe aliyembaka.

Jaji wa mahakama hiyo iliopo Omdurman alithibitisha hukumu hiyo ya kifo baada ya familia ya mumewe mwanamke huyo kukataa kufidiwa kifedha.

Wakati alipokuwa na umri wa miaka 16 , Nourra Hussein alilazimishwa kuingia katika ndoa na familia yake.

Hakuwa na raha hatua iliomlazimu kutoroka na kujificha katika nyumba ya shangazi yake.

Lakini miaka mitatu baadaye , anasema kuwa alidanganywa arudi nyumbani na familia yake ambayo ilimrudisha tena kwa mumewe.

Huwa Napata Shida sana Nikikutana na Wanawake Wenye Hii Tabia

$
0
0
Huwa napata shida sana nikikutana na Wanawake wenye hii tabia...Unampenda Mwanamke kabisa from ur heart,unajipanga unampiga saundi..anakujibu,''How old are you kaka'' unamwambia am 29 years..utamsikia,''Oh my Ghosh,ur still a kid,mi nadate guys who are 45 years above...Wanajua kupenda,they are so caring,yaani nyie vijana mnasumbua sana''.Sio tunasumbua,anajua kabisa miaka 29 bado ndo unasaka hela,ndo umeanza maisha huna cha kumhonga,ukijitahidi sanaaa utampeleka shopping Karume na hiyo hela itakuuma kishenzi!

Anakuita Kid bila aibu wakati yeye ana miaka 23 tu halafu eti ana mahaba na jitu la miaka 47..Uongo mtupu!Ina maana mtu hawezi kupenda na kucare hadi afike miaka 45??Nyie semeni tu mnawalia timing coz mnajua mtu mwenye miaka 45 anakuwa ameshajipanga,amefanya kazi ana hela,unajifanya unampenda kumbe Parasite tu unataka kumnyonyoa mafao yake ya uzeeni,hamna hata aibu..Mnapenda sana vitu ready made,tengenezeni vya kwenu,ukiona mtu ana miaka 45 jua kuna Mwanamke mwenzio amefanya kazi kumfikisha hapo alipo,we unakuja unadandia tu,,,Kama kweli una mahaba tafuta mwanaume wako,panda nae daladala za Buguruni mrukie wote dirishani,msotee maisha kwa kutembelea TZ 11 hadi siku apate gari mfaidi wote halafu akifika miaka 45 uone kimwanamke cha IFM kinamsogelea eti hes caring uone inavyouma,utatamani umpige patasi ya kisogo...Gold diggers,waone kwanza,msione gesi mtwara mshaanza kuandamana!45years guy waiting for u student of 23 years,ina maana miaka yote hiyo alikuwa Stevie Wonder au??

By  Seth De Jesus Giovanni

Anashinda Whatsapp Masaa Yote, Ila Nashindwa Kumbwaga

$
0
0
Huyu dada nimemfahamu miaka mitatu iliyopita.

Ni mwanasheria kwenye firm fulani jijini Dar, nilikuwa nina mpango wa kumuoa haraka, ila mmoja wa marafiki zake wa karibu aliniambia nijitahidi kumfahamu kwanza kabla sijaamua kumuoa nadhani alihisi kitu.

Kufahamiana naye kwa muda tukaishia kupata mtoto mmoja wa kike ambaye sasa ana miaka miwili.

Ni mwanamke mzuri sana, ni gumzo kila anapopita au kufanya kazi, hata nilitaka nitoane macho na patina mmoja wa firm yake.

Kwa kweli anaita kila jicho ana mengi mazuri, lakini pia ana mapungufu yaliyonipigisha breki kali juu ya tope.

Kwa sasa anaishi na wazazi wake, lakini mara nyingi saba tunalala kwangu. Nafahamika kwao kama mzazi mwenza, kwetu pia kaskazini wanamtambua.

Amekuwa ni mwepesi sana wa kupata marafiki wa kiume, ana hasira za karibu, kujiachiachia sana kwa wanaume imekuwa sehemu ya maisha yake, yeye anadai si wapenzi wake. Wanataniana tu hii ni moja ya sababu iliyonizuia kumuoa.

Nilihisi kama hajiheshimu.hayuko tayari kuishi kama mke wa mtu nikadhani nimwache kwanza ale maisha wakati nami nakula taratibu ingawa nahofu ya magonjwa.

Simu zake sijawahi ziona hata mara moja zikiita kwa sauti toka nimfahamu.anashinda watsapp 24/7.

Facebook kwake ni kama oxgen, kila siku anaongeza wanaume, viber anatumiwa mioyo na mikisi ya wanaume, linkedin pia hayuko mbali.

Nahisi kweli atakuwa ananipenda, lakini kwa hayo nashindwa kuji commit, ila bahati mbaya nashindwa hata kumuacha, hasa ukizingatia nina mtoto naye.

Yaani sijui nifanyeje, nimbwage.

Naona sio waifu matirio.

Ataniua jamani.

By Kelly
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live


Latest Images