Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Sakata la Okwi Kuhusu Yanga na Simba, Hili Hapa Tamko la TFF

$
0
0
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana leo (Septemba 7) na kupitia masuala mbalimbali ikiwemo mgogoro wa kimkataba kati ya klabu ya Yanga na mchezaji Emmanuel Okwi.
Mkataba huo ulipitiwa na Kamati ikiwemo kumsikiliza mchezaji mwenyewe pamoja na upande wa Yanga na kuridhika kuwa mkataba kati ya pande hizo umevunjika Ukiwa ni mkataba wa pande mbili Yanga ilikiuka kipengele namba 8 kuhusu malipo ya ada ya usajili.
Yanga ikiwa kama mwajiri haikutekeleza kipengele hicho cha kimkataba hadi kufikia Juni 27 mwaka huu ilipoandika barua TFF kuomba mkataba huo uvunjwe,Kwa maana hiyo Okwi ni mchezaji huru,hivyo yuko huru kujiunga na timu yoyote.


Anti Lulu Asema Mazito 'Nataka Kuzaa na Diamond Platnumz'

$
0
0
MOYO unahifadhi mengi! Msichana wa mjini asiyeishiwa matukio Bongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Anti Lulu’ amefunguka kwamba yupo tayari kuzaa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwani amepata taarifa kwamba anasaka mtoto lakini wanawake anaokuwa nao hawataki kumzalia, Ijumaa Wikienda linakupasha.

BILA KUMUNG’UNYA MANENO
Akizungumza na gazeti hili bora la mastaa Bongo akiwa dukani kwake Kinondoni jijini Dar, wikiendi iliyopita, Anti Lulu bila kumung’unya maneno, alifunguka kwamba hivi karibuni alifuatwa na ndugu wa karibu wa Diamond au Dangote kama anavyopenda kujiita na kumuomba afanye jitihada azae naye.

MAKUBWA!
Alidai aliambiwa kuwa kila Diamond akimpa kibendi mwanamke, huwa mwanamke huyo anakwenda kukitoa bila hata ridhaa yake (Diamond).

“Ndugu wa Diamond alinifuata hapa dukani kwangu akanitaka nizae na Dangote kwani anasaka sana mtoto na kila akimpa mwanamke mimba huwa anaichoropoa bila kuafikiana naye.“Sababu kubwa ya wanawake hao kutoa mimba ni kutokana na mpenzi wa Diamond ambaye ni Wema (Isaac Sepetu) kudaiwa kuloga ili mwanamke yeyote asizae naye na kila akimpa mimba mwanamke inatoka au anakwenda kutoa mwenyewe bila sababu yoyote,” alisema Anti Lulu.

Pamoja na tetesi hizo, Anti Lulu alisema haogopi lolote kwani amejizatiti ndiyo maana amejitokeza hadharani na kutaka kuzaa na Diamond.

Aunt Ezekiel Ampigia Debe Wema Sepetu Asema Anafaa Kuwa Mke Mwema

$
0
0
Stori: Imelda Mtema
FAGIO! Mkali wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amemmwagia sifa shosti yake Wema Sepetu na kudai anafaa kuwa mke kama alivyo yeye.

Akimmwagia sifa mbele ya kinasa sauti chetu, Aunt alisema Wema anajua mapenzi ya dhati, anajali, mcheshi na anajua maisha tofauti na watu wengi wanavyofikiria.

“Siyo kwamba namsifia lakini Wema anafaa kuwekwa ndani, unajua watu wanashindwa kujua tu kwamba Wema nje ya ustaa wake anajua kuhimili maisha, anafaa kuolewa,” alisema Aunt.
Wema na Diamond wapo katika mikakati ya kufunga ndoa.

Kauli ya Wema Sepetu Kuhusu Kajala Masanja Yaleta Utata, Wengi Wasema ilikuwa ni Kejeli Kwa Kajala

$
0
0
Stori: Mayasa Mariwata na Shani Ramadhani
NGOMA nzito! Kauli ya sexy lady wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ kuwa yupo tayari kumtumikia msanii mwenzake Kajala Masanja ‘K’ kwenye kampuni yake ya KAY Entertiment tena bila malipo yoyote, imetafisiriwa kuwa ni kejeli

Hivi karibuni Wema alikaririwa akisema: “Nakubali kwamba Kajala anaweza kuwa na maisha mazuri ya kiasi hicho na akanifanya mfanyakazi wake katika kamusi yake kwa sababu sioni cha kumfanya ashindwe kuwa hivyo, naamini anaweza kuniajiri na wala sina kipingamizi! hahahaa!”

Baada ya kauli hiyo ya Wema, mashabiki wake waliikataa kwa maelezo kuwa alilenga kumkejeli Kajala ambaye awali aliwahi kumwajiri kwenye kampuni yake ya Endless Fame Production.

Zitto Kabwe Atoa ya Moyoni na Kusema Haya Kusuhu Wapambe Kumgombanisha na Mbowe

$
0
0
Kwa ufupi
Zitto (37), ambaye alikuwa naibu katibu mkuu wa Chadema, alisema kuwa hata kuvuliwa nyadhifa zake ndani ya chama kulisababishwa na wapambe hao, lakini akasisitiza kuwa hana kinyongo tena kwa kuwa alishamwomba Mungu na sasa amesamehe kabisa.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ameeleza tofauti yake na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akisema imesababishwa na watu aliowaita wapambe.

Zitto (37), ambaye alikuwa naibu katibu mkuu wa Chadema, alisema kuwa hata kuvuliwa nyadhifa zake ndani ya chama kulisababishwa na wapambe hao, lakini akasisitiza kuwa hana kinyongo tena kwa kuwa alishamwomba Mungu na sasa amesamehe kabisa.

Tofauti za wawili hao hazijawahi kutolewa hadharani licha ya mitandao mbalimbali kuzungumzia kuharibika kwa uhusiano wao ikinukuu habari kutoka vikao vya ndani vya Chadema.

Hata hivyo, mapema mwaka huu, Zitto alirushiwa tuhuma nzito na Chadema kutokana na uhusiano wake na baadhi ya makada wa CCM, lakini mbunge huyo aliyahusisha maneno hayo na mwenyekiti wake na aliandika maneno makali dhidi ya Mbowe kwenye ukurasa wake wa facebook.

Lakini katika mahojiano na Mwananchi yaliyofanyika wiki iliyopita nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam, Zitto alionekana kujutia kuharibika huko kwa uhusiano wao na kusema “wapambe ndiyo wanatugombanisha”.

“Sina shida yoyote na Mbowe, naamini ipo siku tutagundua wapambe walituathiri na ndiyo waliotufikisha hapa,” alisisitiza Zitto bila kutaja ni kina nani hasa.

Zitto alisema yeye na Mbowe wametoka mbali tangu akiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na hafurahii uhusiano wao ukiishia katika hali hiyo.

“Naumia sana, lakini naamini ipo siku ama nikiwa hai au nimekufa watu wataujua ukweli,” alisema mwanasiasa huyo kijana aliyepata umaarufu kutokana na uwezo wake wa kujenga hoja.

Alisema, akiwa mwenyekiti wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu (Daruso) yeye na mwenyekiti wake ndiyo waliokijenga chama wakati huo Mbowe akiwa mbunge wa Hai.

Alisema wakati huo Mbowe alikuwa akienda chumbani kwake kusuka mikakati ya kuiinua Chadema na kwamba walikuwa wakila chips pamoja na wakati mwingine kwenye klabu ya usiku ya Bilicanas inayomilikiwa na Mbowe.

“Wakati mwingine naangalia, naumia sana. Wakati tunafanya hayo yote wengine walikuwa CCM, wengine walikuwa wafanyabiashara, lakini sasa ndiyo wana sauti katika chama,” alisema Zitto.

Zitto alisema kuwa wakati huo walikuwa na kampeni yao waliyoiita ‘Real Madrid’ ambayo ilikuwa na lengo la kuingiza kila mwanasiasa bora katika chama chao.

Real Madrid ni klabu ya soka ya Hispania yenye mafanikio makubwa duniani na sera yake ni kusajili wachezaji nyota duniani kwa gharama zozote.

“Na kweli tulifanikiwa na kuongeza wabunge kutoka watano hadi 48 wa sasa,” alisema.

“I real miss that (nakumbuka sana). Naumia sana, mimi leo sina maelewano na watu ambao tulikuwa nao katika mapambano. Lakini nasononeshwa zaidi na kitu kinachoendelea ndani ya Chadema.

“Nini kimetokea Chadema? Kwa nini tumejikuta tumeondoka katika mstari? Tupo wabunge 48 bungeni sasa, lakini hatusogezi mbele nchi, tumerudi nyuma wakati huo tulikuwa watano lakini tulikuwa tunaenda vizuri sana.”

Akizungumzia jinsi wapambe walivyoharibu uhusiano wao, Zitto alisema kuna siku Mbowe alimtuhumu kuwa ameanzisha chama cha umma, pia akasema ana majina mawili tofauti katika mtandao wa Jamii forums ambayo anayatumia kuwasema viongozi wa Chadema.

“Kukatokea vurugu, baadaye nikasema naondoka. Ile nataka kutoka wabunge wakanizuia mlangoni nisipite, waliponizuia nilikuwa na hasira sana, nikawaambia lazima nitoke. Waliponizuia hasira zikanipanda nikaanguka chini nikalia sana, yaani sana” alisema akionekana mwenye hisia huku machozi yakimlengalenga.

Kwa mujibu wa Zitto, jioni ya siku hiyo walijikuta wamekaa meza moja na Mbowe na baada ya kuzungumza waligundua kuwa walikuwa wamelishwa maneno.

“Tulizungumza na wote tulilia sana. Wakati kama huu nikikumbuka nasikia uchungu kwa sababu ni wapambe wametufikisha hapa,” alisema.

Usagaji Tatizo Linalokua Kwa Kasi Sana Bongo Kwa Wanawake

$
0
0
Uchunguzi Mdogo uliofanywa na Udaku Specially Imebaini tatizo la Usagaji badala ya kupungua sasa limeanza kuwa Sugu miongoni mwa Wasichana wa Kibongo na Sasa kufikia mpaka wanafunzi wadogo wa kike kufanya mambo hayo wakiwa mashuleni, Imebainika kuwa Mitandao hasa Whats app na Facebook imekuwa ndio njia wanazotumia wadada kutongozana wenyewe kwa wenyewe mpaka inafikia kufanya vitendo hivyo vya aibu , Kati ya Wadada tulio wahoji wengi wamesema kuwa Wao wanafagilia zaidi penzi la Jinsia Moja (Usagaji) kuliko na Mwanaume , Wengi wamesema kwa Wanaume Wanafuata PESA tu na si Mapenzi , Mmoja Alisema Hivi "Mimi nikiamua Kufanya Mapenzi na Mwanaume basi Ujue nataka kumchuna tu ila nikiwa nataka kuenjoy basi namtafuta Msichana Mwenzangu tunakula Raha" 

Jamani Sijui nini Kifanyike Hapo ? Wanaume Mmeshindwa Kazi Au ?

Lulu Michael Kwa Picha Hii Aingia Katika List ya Mastaa Malimbukeni Wanapopata Pesa

$
0
0
Kumezuka katabia Kwa Wasanii Mastaa Kuonesha Pesa zao Kwenye Mitandao ya Kijamii Kama Facebook na Instagram wanapozipata kwa Mkupuo , Lulu Michael nae ameingia katika list ya wasanii hao, Juzi Kapost picha hiyo Hapo Juu akionesha zigo la Pesa...Je ni Sawa kwa staa kama Lulu Kufanya Hivyo au ni Ulimbukeni wa Pesa?

Mzoga wa Samaki Aina ya Nyangumi Waibuka Pwani ya Mtwara, Ni Samaki Mkubwa Kuwahi Kuonekana

$
0
0

Mzoga wa samaki aina ya nyangumi umeibuka katika pwani ya Mtwara leo baada ya kukutwa ukielea bahari kuu na wavuvi. Mzoga huo ulivutwa hadi pwani kwa mshangao wa wananchi. Taarifa kamili ya tukio hilo zinatafutwa kwa sasa angalia taswira za mzoga huo.

Hapo akiwa Nchi Kavu baada ya Wavuvi Kumkokota , Wananchi Wakusanyika Kushangaa ni Samaki Mkubwa ambae hajawahi onekana maeneo hayo.

King Mswati Noma Sana Aongeza Mke Mwingine Bikira, Sasa Ana Wake 14 , Angalia Picha

$
0
0



KING Mswati Mfalme wa Swaziland amefikisha wake kumi na nne 14 baada ya juzi jumatatu kumchagua mke mwingine mwenye umri wa miaka 19 masharti ya mwanamke anaetakiwa kuchaguliwa ni sharti awe bikra.

Takribani wasichana 80,000 walipita mbele ya wageni wa heshima 46 ambapo na mfalme alikuwa ameketi mbele akiwa kaketi na malkia aliechaguliwa mwaka jana LaFogiyane Baadhi ya wasichana wanakimbia katika taifa hilo kutokana na sheria hizo.

Wasichana hao hupita wakiwa nusu uchi ndipo mfalme anachagua mke wake kafikisha wake 14 

Spika Sitta Kumpa Nafasi Hamad Rashid ili Amtukane Maalim seif ni Sawa ?

$
0
0
Jana mwisho wa bunge Mheshimiwa Spika alimpa nafasi Hamad Rashid amjibu na kumtukana Maalim Seif kwenye bunge.

ampa dakika za kutosha kumshambulia na kumtukana na kujitangaza kua yeye ni msafi na kutangaza kuwa atagombea wa urais wa Zanzibar.

Ninajiuliza ni sawa kwa mheshimiwa spika kufanya haya?

Kwa nini asiache hayo masuali ya Hamad Rashid wamalizane kwenye vyombo vya habari kama Maalim alivyofanya?

Mtanzania Wameandika Hivi Kuhusu Hilo:
MJUMBE wa Bunge Maalumu la Katiba ambaye pia ni Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), amemshambulia kwa maneno Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Maalim Seif Sharif Hamad, huku akimfananisha na popo.

Mbunge huyo alisema hayo baada ya kupewa nafasi na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta, akisema lengo ni kujibu mashambulizi yaliyoelezwa kwake na Maalim Seif kupitia kituo kimoja cha televisheni.

Baada ya kupewa fursa hiyo, Hamad alisema Maalim Seif hafai kuwa kiongozi kwa kuwa hana msimamo kisiasa jambo ambalo linamfanya awe kama popo ambaye hajulikani kama ni ndege au mnyama.

Ukweli Kuhusu Taarifa zilizo Sambaa Jana Kuwa Babu Seya na Papi Kocha Wameachiwa

$
0
0
Taadhari Uvumi huo si Kweli
Picha inayosambazwa kwenye mitandao ni ya Oktoba 2013 wakati wakitoka Mahakamani pia tetesi hizi si za kweli. 


Kilichosambazwa na blogs nyingi ni mipango yao wakifika uraiani kama watatoka kwa msamaha wa Raisi ikiwa na kichwa cha habari kisichoakisi maelezo ya ndani kuvutia wasomaji


Jeshi la Magereza Limetoa Tamko Lake Hapa:

Hivi sasa kuna taarifa zimesambaa kupitia Ujumbe mfupi wa simu (SMS) na mitandao ya kijamii zikihusisha kuachiliwa huru kwa wafungwa wawili wanaotumikia Kifungo cha Maisha gerezani. Wafungwa hao wanaotajwa ni Nguza Vicking(Maarufu kwa jina Babu Seya) na Johnson Nguza(Maarufu kwa jina la Papii Kocha).

Napenda kuufahamisha Umma wa Watanzania kuwa taarifa hizo zote zilizotolewa kupitia njia hizo ni za Uongo na uzushi mkubwa na zinalenga kuipotosha jamii kwani wafungwa hao wapo gerezani na wanaendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha Maisha gerezani kwa mujibu wa Sheria.

Jeshi la Magereza nchini linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uhalifu huo na linawataka wale wote wanaotumiwa ujumbe wa aina hiyo waepuke kuusambaza ujumbe huo kwa wengine bali waufute, kwani kuendelea kuusambaza ni kosa kisheria.

Aidha, Jeshi la Magereza linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwabaini wanaosambaza ujumbe huo likishirikiana na Vyombo vingine muhimu kwa lengo la kuwakamata wahalifu hao ili mkondo wa Sheria uchukue nafasi yake.

Imetolewa na;

Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza,

Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,

Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,

DAR ES SALAAM.

Septemba 8, 2014.

Ray C Ala Tenda Nono Hospital ya Mwananyamala

$
0
0
Baada ya kupitia kipindi kigumu cha kutumia madawa ya kulevya ‘ unga ’ kisha kunusuriwa, super lady kwenye Bongo Fleva , Rehema Chalamila ‘ Ray C ’ , hatimaye mambo yameanza kumnyookea baada ya kulamba shavu tenda nono ya kulisha Hospitali ya Mwananyamala , Dar . 

Super lady kwenye Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C ’.

Ray C almaarufu Kiuno Bila Mfupa amefungua bonge la ‘ restauranti’ maeneo ya Mwananyamala Hospital, ambapo amepata tenda ya kuwahudumia chakula wafanyakazi wa hospitali hiyo na Idara ya Maji ( Dawasa ) ambapo anafanya kazi hiyo kwa saa ishirini na nne na muda mwingi anakuwepo yeye mwenyewe.

“Bidada sasa hivi yupo njema sana. Kalamba shavu la kulisha Hospitali ya Mwananyamala na Dawasa na hapo ni mchana na usiku so yupo bize kinoma. 

Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, wanahabari wetu waliusaka mgahawa huo na kufanikiwa kuupata ambapo walimkuta Ray C akiwa bize kuhudumia wateja ambapo alisema:

“Namshukuru Mungu kwani nimepata tenda ya kuwapikia chakula wafanyakazi wa Mwananyamala na wale wagonjwa ambao ni waathirika wa madawa ya kulevya. ”

Breaking News: Kaburi la Mmoja Kati ya Waliopata Ajali ya Bus Musoma Lafukuliwa na Watu Wasiojulikana

$
0
0
Kaburi la mmoja kati ya watu waliopoteza maisha katika ajali mbaya iliyohusisha mabasi ya Mwanza Coach na J4 katika eneo la Sabasaba, Musoma, Mara limekutwa likiwa limefukuliwa na watu wasiojulikana leo asubuhi.

Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichofika katika eneo la makaburi ya Musoma Basi, ndugu wa marehemu aliyetajwa kwa jina la Juma Sai walienda asubuhi kuangalia kaburi ikiwa ni siku ya tatu tangu wafanye mazishi, ndipo walipokuta kaburi limefukuliwa na mbao zilizotumika kuhifadhi mwili kwa imani ya dini ya kiislamu zikiwa zimewekwa pembeni.

“Mwili wa marehemu bado uko ndani, watu wengi wako hapa na polisi wameimarisha hali ya usalama. Madaktari wameshafika hapa na wanafanya uchunguzi kuona kama kuna kiungo chochote kilichotolewa kwenye mwili wa marehemu. Inasikitisha sana.” Kimeeleza chanzo chetu cha kuaminika.

Ijumaa iliyopita, kulitokea ajali mbaya iliyohusisha magari matatu, mabasi ya kampuni ya Mwanza Coasch na J4 pamoja na gari dogo aina ya Landcruiser. Watu zaidi ya 40 walifariki na wengine 79 kujeruhiwa.

Diamond Kufanya Show ya bure Stuttgart, Ujerumani September 20 Kuwafidia Mashabiki

$
0
0
Baada ya show ya Diamond Platnumz iliyokuwa ifanyike mjini Stuttgart, Ujerumani kushindwa kufanyika mwishoni mwa mwezi uliopita na kusababisha vurugu kutoka kwa mashabiki waliofika ukumbini kumshuhudia star huyo wa ‘Number 1′, show hiyo inatarajiwa kufanyika September 20, 2014 bila kiingilio.

Kupitia Instagram Diamond amethibitisha kwa kuandika:

“YES!!!! STUTTGART GERMANY!!! on this 20th of September 2014… kiukweli nilisikitishwa sana na kilichotokea last time Stuttgart… lakini baada ya kugundua kuwa pia lilikuwa ni kosa la mtu mwingine na si promotter kama nilivyodhani, yaani Brittis Events… ndipo tulipoamua na kuwaletea Burudani hii Mashabiki zetu pendwa wa Stuttgart….hakikisha ufikapo unapendeza zaidi maana kama ujuavyo safari hii Vyombo vyote vya habari ndani na nje ya nchi vitakuwa pale kwa RedCarpet…. kiingilio ni BUREEEEEE!!!… tafadhariwambie na wenzio wa nchi za karibu…#NORWAY #HOLLAND #SWITZLAND #BELGIUM #SWEEDEN na kadharika!!!!”

Exclusive Pics: Mchumba wa Nay wa Mitego, Siwema ni Mjamzito Tena

$
0
0

Baada ya kuharibika kwa mimba ya kwanza ya mchumba Nay Wa Mitego, Siwema, hatimaye mwanadada huyo anatatarajia kuwa mama tena na anatarajia kujifungua hivi karibuni.

“Umemuona mama kijacho,” Nay alimwambia wa Bongo5 baada ya kutembelewa na mpenzi wake katika uwanja ndege wa Mwanza akijiandaa kuekelea Dar es salam, huku akicheka na kuendelea kumpiga mabusu mpenzi wake huyo anayeishi jijini humo.

Kuna Wadada Wamebariki Makalio, Embu Ona Hii Video Fupi Irene Anachofanya

$
0
0
Kuna Wadada Wamebariki Makalio, Embu Ona Hii Video Fupi Huyu Dada anayejiita Irene Anavyotingisha Wezele Lake Huku Akijiangalia Kwenye Kioo cha Meza ya Kujirembea..Shidaa Tupu:

Kisirani Champonza Lulu Michael…Tajiri Wa Madini Ammwaga

$
0
0
Star wa filamu nchini aliyejaaliwa mvuto wa  kipekee, Lulu Elizabeth Michael anadaiwa  kutodumu na mwanaume sababu ya kuendekeza ubabe na kutaka kum-control mwanaume anayekuwa naye.

Inadaiwa Lulu hataki mchezo, mwanaume akishakuwa nae basi lazima ahakikishe hafurukuti. Taarifa  zinadai  kuwa miezi ya  hivi karibuni alikuwa na jamaa mmoja mdogo kimapenzi akammwaga na baada ya muda akawa anatoka na tajiri mmoja wa madin toka Arusha lakini tajiri huyo alinyoosha mikono juu baada ya Lulu kama kawaida kuruhusu majeshi yake yam-control jamaa huyo. 

Chanzo kimoja kikizungumza  kwa  sharti  la  kutotajwa  jina kimesema:

 ” Lulu ni mtu mwenye kisirani kwa wanaume, hadumu nao, wengie wanaokuwau nae ni wale wavumilivu sana. Nadhani ana matatizo ambayo yanahitaji mtaalam wa saikolijia ya mahusiano, akizinguliwa tu hachelewi kuvunja simu na kurejesha kila kitu alichokuwa amepewa” 

Mwigizaji Mkongwe Nchini Lucy Komba Afunga Ndoa. Tazama Picha za Harusi

$
0
0



Hatimaye yule mwigizaji mkongwe nchini Lucy komba amefunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi aishie nchini Denmark aliyefahamika kwa jina la Stanley,. Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii nchini lucy ameandika

"..Asante Mungu kwa siku hii nzuri na muhimu sana katika maisha yangu, wengi hawakutaka nifikie siku hii, kunawengine walinuna, kunawengine waliniombea mabaya, kuna wengine walichukia na wengine waliambiana wanichunie walifikiri bila wao Mungu hawezi kuifanikisha siku hii, nasema asante Mungu kwa sababu aliifanikisha siku hii kwa nguvu zake wqtu wanaonipenda walisheherekea siku hii vizuri walikunywa na kula na kusaza watu zaidi ya miasita walikuwa ukumbini wakishangilia pamoja nami haleluyaaaaaaaaaaaaaaa anachokiunganisha Mungu binadamu hawezi kukitenganisha hata ieeje.."

Hongera sana lucy. 

Kikwete Asalimu Amri Kwa Ukawa, Wakubaliana Kurekebisha Katiba iliyopo! Katiba Mpya Hadi Baada ya 2015

$
0
0
Cheyo anasema wamekubaliana na Jakaya Kikwete kuwa Bunge lirekebishe Katiba Iliyopo. Aidha, anasema wamekubaliana marekebisho yaruhusu Matokeo ya Urais yaweze kuhojiwa Mahakamani na kuwepo na Mgombea Binafsi uchaguzi 2015

Hivyo basi Mchakato wa Katiba Mpya utaendelea baada ya uchaguzi 2015!

Irene Uwoya: Sipendi Wanaume Wanene au Wenye vitambi maana ni wachovu Kitandani

$
0
0
Star wa filamu za  kibongo, Irene Uwoya anadaiwa hana mzuka kabisa wa kutoka kimapenzi  na wanaume wanene au wenye vitambi kwa madai si lolote kitandani wanaishia kuhema hema tu.
Inadaiwa kuwa Uwoya anapenda wanaume wasio wanene, wenye miili ya kimazoezi na wasio na vitambi kwa madai wako vizuri sana kunako sita kwa sita na mwenyewe huvutiwa nao sana. Chanzo kimoja kutoka kambi ya Uwoya kikizungumza jana kilisema:
  
“Wanaume wengi wakiwemo wenye pesa zao wamekuwa wakimsumbua Uwoya , yeye hana muda nao  maana  sio type yake. Anapenda wanaume wenye vifua vya mazoezi na wasio na vitambi, yeye anaona wenye vitambi na wanene hawawezi gwaride la sita kwa sita”.

Hata hivyo Uwoya hakupatikana kuzungumzia  suala hilo lakini takribani mwezi sasa alipohojiwa na jarida moja linalotoka kwa mwezi mara mbili alisema kuwa hapendi wanaume wanene linapokuja suala la mahausiano ya kimapenzi.
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images