Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

MAUMIVU: MC Pilipili awa MC katika harusi ya mpenzi wake wa zamani

$
0
0
Mchekeshaji Emmanuel Mathias maaarufu kama Mc Pilipili ameonyesha maumivu aliyoyapata baada ya kuona aliyekuwa mpenzi wake Nicole Franklyn kuolewa na mwanaume mwingine na kufanywa kuwa Mc katika harusi hiyo.

Mc Pilipili ameyaandika maumivu hayo kupitia instagram account yake kitendo ambacho hakijazoeleka na mashabiki kwa mchekeshaji huyo kuandika maumivu kupitia ukurasa wake wa instagram.

“huyu ni wewe ukinivua koti nilipotoka kuchekesha ukiwa umevaa jezi yangu ya SIMBA MABINGWA Kweli ndo umeamua kuolewa na huyo @mwijaku ambae mimi hanigusi kwa lolote!!??? wigi lako bado liko nyumbani hilo ulilovaa hapo na iyo kanga yako ipo pia USIACHE MBACHAO KWA MSALA UPITAO….UTAJANIKUMBUKA!!



Wasiliana na Mtaalam wa Dua na Dawa za Kiarabu na Asili Dr Sharifu Lukumani

$
0
0

YULE MTAHALAM WA DUA NA DAWA ZA KIARABU NA ZA KIASILI YANI MITI SHAMBA SHARIFU LUKUMANI SASA YUPO HEWANI WENYE SHIDA ZITUATAZO CHEO KAZINI,KUONGEZEWA MSHAHARA KAZINI,MWENYE TATIZO LA NGUVU ZA KIUME,ALIEPOTELEWA NA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA, MWENYE KIFAFA,KISUKARI,FANGASI SEHEMU ZA SIRI KWA WALE WENYE MIILI MINENE MTOTO WA JICHO PAMOJA NA WALE WAKINA MAMA WANAOSUMBULIA NA CHANGO LA UZAZI PUMU YA MUDA MREFU WANAWAKE KUJAA MAJI SEHEMU ZA SIRI MWANAUME KUWAI KUFIKA KILELENI AU KUTOA MANII MFANO WA MAJIMAJI YAKIWA MEPESI AUTOWEZA KUMPA MKEO UJAUZITO JAMBO HILI LINAWASUMBUA WANAUME WALIO WENGI DUNIANI KWA KAWAIDA WANAUME ASIE NA TATIZO HILI UTOA MANII MAZITO NDIO YENYEUWEZO WA KUMPA MWANAMKE MIMBA.MWANAUME KUPATA MPENZI KWA ULAISI PASIPO NA GHARAMA YOYOTE YANI KWA WALE MADOMO ZEGE KUWA NA UWEZO WA KUSIKILIZWA HATAKAMA RAIA WA INCHI GANI NA UWEZO WA KURUDISHA MPENZI ALIE POTEA NA KUMFANYA AWE WAKO KWA WALE WASIO TAKA MITALA PIA UFANYA KAZI YA KUNG'ALISHA NYOTA SASA MATATIZO YAKO YAMEPATA SULUHISHO ANAPATIKA KWA MASAA ISHIRINI NA NNE

WASILIANA NAE KWA NAMBA 0762899488-0656145170

WhatsApp namba +255620665635

Bunge labadili ratiba kuwapa fursa wabunge mfungo wa Ramadhan

$
0
0

Bunge limebadilisha ratiba ili kuruhusu waumini wa dini ya Kiislamu kushiriki kikamilifu mfungo mtukufu wa Ramadhan bila kuathiri shughuli za chombo hicho cha Dola.

Utenguaji wa kanuni hizo umefanywa bungeni leo Jumatano Mei 16, 2018 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama na kuungwa mkono na wabunge.

Kwa mujibu wa Mhagama, ratiba iliyobadilika ni ya kipindi cha mchana ambapo sasa Bunge litaanza saa 10:00 jioni badala ya saa 11.00 jioni na kumalizika saa 12.00 jioni badala ya saa 1.45 usiku.

Amesema mara baada ya kumalizika kwa mfungo huo, ratiba itarudi kama kawaida.

Daktari Kortini kwa kuiba moyo wa marehemu

$
0
0
Mkuu wa zamani wa uchunguzi wa chanzo cha vifo nchini Kenya ameshtakiwa kosa la kuiba moyo kutoka kwenye maiti iliyokuwa inafanyiwa upasuaji.

Dkt. Moses Njue alikanusha shitaka hilo aliposomewa mashitaka yake katika Mahakama ya Hakimu Mkuu Nairobi ambapo alikuwa ameshitakiwa yeye na mwanae pamoja msaidizi wake.

Walidaiwa kuiba moyo wa Timothy Mwandi Muumbo wakifanyia mwili wake upasuaji  Juni 25, 2015 katika chumba cha kuhifadhia maiti cha 'Lee Funeral Home'.

Hakimu Mkuu Francis Andayi aliagiza watuhumiwa wengine wafike Mahakamani na kujibu mashitaka kabla ya kesi kuanza kusikilizwa  Julai 3.

Dkt. Njue alikanusha pia shitaka jingine la kuuharibu moyo ili kuficha ushahidi, akifahamu kwamba ripoti ya uchunguzi wa maiti hiyo ingetumiwa kwenye kesi iliyokuwepo Mahakamani.

Serikali yasema aihusiki na Taasisi inayowatoza fedha Wanawake kupitia jina la Mama Samia

$
0
0

Serikali kupitia Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Muhagama imesema aihusiki na Taasisi inayowatoza wanawake sh. elfu kumi kumi kupitia jina la Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu katika mkoa wa Kigoma.

Akijibu swali la Mbunge wa viti Maalumu Mkoa wa Kigoma,Josephine Gezebuke aliyehoji,

Katika Mkoa wa Kigoma iko NGO’s ambayo imezunguka kwa muda wa wiki mbili katika wilaya zote saba ikiwatoka wanawake sh. elfu 10, 10 na kuwapigisha picha na kuwaahidi kwamba serikali itatoa mikopo kwa kupitia mfuko wa Makamu wa Rais, Mama Samia, Je? ninataka serikali inieleze mpango huo wa kutoa pesa kupitia mfuko wa Mama Samia upo?

“Shughuli zote za uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi katika nchi yetu ya Tanzania zinasimamiwa na sera 2004 na sheria ya uwezeshaji wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004 ambayo inaruhusu uanzishwaji wa Taasisi mbalimbali kisheria, Taarifa kuhusu Taasisi hiyo zilishapatikana ndani ya serikali na ofisi ya Makamu wa Rais ilishatoa tamko la kuikana taasisi hiyo kwamba haihusiki nayo,” amesema Waziri Jenista.

“Ninaomba nichukue nafasi hii kuuagiza uongozi wa Mkoa wa Kigoma kuifuatilia taaisi hiyo na kuikana na kuipa maelekezo kwamba ofisi ya Makamu wa Rais aihusiki na jambo hilo na kama wanaendesha shughuli hizo kwa kutumia sheria taratibu nyingine wanapaswa kujieleza kwa kutumia sheria na taratibu zingine walizozifauta lakini sio ofisi wa Makamu wa Rais.”

Aidha Jenista amesema kuwa kama Taasisi hiyo itaendelea kuwadanganya wananchi kutumia mgongo wa Ofisi ya Makamu wa Rais serikali haitasika kuchukua hatua kali.


“Serikali ya Mizuka, Tutaangukia pua Muda si Mrefu” –Pascal Haonga

$
0
0
Wabunge wameendelea kuchangia mapendekezo yao katika hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa fedha 2018/19 iliyowasilishwa bungeni na Waziri wake Dr Charles Tizeba ambapo miongoni mwa Wabunge waliopata nafasi hiyo ni pamoja na Mbunge wa Mbozi Pascal Haonga aliyeilalamikia Serikali kushindwa kuwasaidia wakulima.

 VIDEO:

Ali Kiba 'Mimi ni Mswahili Hasa Hata Diamond Haoni ndani'

$
0
0
Msanii wa muziki nchini Alikiba amewataka watanzani pamoja na wasanii kujivunia kutumia lugha ya Kiswahili kwasababu ni lugha kubwa na watu wengi Duniani  hutamani kujifunza lugha ya Kiswahili.


Alikiba amesema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na amedai kuwa watanzania wanapaswa kujivunia kuitwa waswahili na wasione aibu na kuongeza kuwa hata katika nyimbo zake amekua akitumia kiswahili kama kuonesha jitihada za kuunga mkono lugha hiyo.

“Lugha yetu ni nzuri lazima tujivunie, najivunia sana kuwa mswahili na kuongea Kiswahili na kutumia kiswahil katika kazi yangu ya kunipatia maisha, kwahiyo kila mtanzania ni lazima ajivunie kuwa mswahili, asikwambie mtu acha uswahili, ni lazima ujivunie sio sifa mbaya” amesema Alikiba

Alikiba aliongeza kwamba hata akiwa anafanya matamasha nje ya nchi watu wengi wamekuwa wanataka kufundishwa lugha ya kiswahili kutokana na matamshi yake kuvutia.

Download Hapa Application Mpya ya Udaku Special Uweze Soma Vimbwanga na Udaku Mtaani Kila Siku

$
0
0
Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Upya Application yetu ya UDAKU SPECIAL Maana ile ya Zamani Tutaifuta.

Kuna Marekebisho Makubwa tumeyafanya ikiwa na tatizo la Notification kutatuliwa

NB: App mpya ina Icon Nyekundu

 Bonyeza Hapa Chini Kuinstall Upya:

==>>Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>>  
   

Dawa Bora za Nguvu za Kiume na Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa

$
0
0
DAWA BORA ZA NGUVU ZA KIUME NA KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA
Baada ya utafiti wa muda mrefu juu ya matatinzo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurundia tendo kwa haraka Sasa inakuletea suluhisho juu ya matatizo haya kwa kutumia dawa za FULL POWER

Full Power dawa asili yenye vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume dawa hii inamchanganyiko wa kutosha kuzalisha vichocheo vingi vya hernone za gestro gen zikiwemo vitamin b6 na b1 vitamin e pamoja na madini aina ya zinc

Itakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wakufanya tendo la ndoa zaidi hatua nne au zaidi na kuchelewa kufika kileleni zaidi ya dakika 20/30 ZAT 50

Inarundisha maumbile ya uume yaani kurefusha na kunenepesha nchi 3/7 na upana cm 3/4 standard.kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukitumia maumbile yatabaki kuwa hivyo siku zote pia anatibu matatizo mengine kama presha kisukari ngiri chango la tumbo kujaa gesi kutopata choo vizuri minguu kuwaka moto matatizo ya uzazi bawasili na magonjwa ya zinaa kama kisonono na kaswende

Tunapatikana Dar es Salaam  na mikoan wasiliana na DR Oshinda no 0755505099 au 0714126118  Karibuni kwa hunduma bora

Sakata la Ngombe Vibudu Waliokutwa Kwenye Lori Wakipelekwa Sokoni Laibuka Bungeni, Serikali yajibu

$
0
0

NA ISMAEL MOHAMED
Zikiwa zimepita siku chache tangu ilipotokea kizazaa cha ng'ombe waliokufa kutaka kuingizwa sokoni, serikali imewaondoa hofu watanzania kuwa nyama inayopatikana nchini ni bora na yenye usalama wa kutosha na kwa namna yoyote hawawezi kula vibudu.


Kauli hiyo imetolewa leo Mei 16, 2018 na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhanga Mpina Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 30 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la Mbunge wa Mbinga mjini Sixtus Mapunda aliyetaka kusikia kauli ya serikali kuhusiana na jaribio la kuuza vibudu katika machinjio ya Tegeta Jijini Dar es Salaam Mei 13, 2018.

Wakati anajibu swali hilo Waziri Mpina amesema katika machinjio ya Tegeta walilikamata lori likiwa na ng'ombe 54 kati ya hao 12 walikuwa ni mizoga ambapo mizoga hiyo minne ilikuwa imeshachunwa na miwili ilikuwa tayari imeshakatwa katwa vipande.

"Vyombo vyetu vya usimamizi, Mkurugenzi wa Mifugo, TFDA (Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini) na Halmashauri tunao usimamizi madhubuti kwenye machinjio na mabucha yetu katika kuzingatia usalama wa walaji hivyo basi watanzania wote wasipewe mashaka wala hofu na mtu yoyote kwasababu nyama za Tanzania ni bora kwa namna yoyote hawawezi kula vibudu", amesema Mpina.

Aidha, Waziri Mpina amewashauri watanzania waendelee kula nyama za mifugo yao kwa kuwa vyombo vya dola vipo na vinawahakikishia usalama wa kutosha katika masuala hayo.

"Kwa jaribio hili tu tayari ameshafungiwa machinjio yake kutokana na jambo hilo kuwa limefanywa kinyume na sheria za nchi hivyo Wizara yangu pamoja na Halmashauri ya Kinondoni tulichukua maamuzi ya kuyafungia machinjio ya tegeta kwa muda usiojulikana, kuiteketeza mizoga 12 na kuifukia pamoja kumkamata dereva wa lori hilo pia bado tunamtafuta mmliki wa machinjio hayo kwa kuwa alikimbia baada ya tukio kutokea", amesisitizia Mpina.

Kwa upande mwingine, Mpina amesema mpaka sasa hivi serikali imewaondoa watumishi wote waliokuwa katika kizuizi cha Kibaha na kupeleka wengine baada ya tukio hilo.

Kumekucha..Tanzania Yaziunganisha Benki Mbili Kuwa Moja

$
0
0

NA ISMAEL MOHAMED
Benki Kuu ya Tanzania BoT, imeridhia uamuzi wa kuiunganisha Benki ya Twiga Bancorp Ltd na ile ya Tanzania Postal Bank Public limited Company (TPB Plc), ili iwe benki moja yenye nguvu ambayo utendaji wake utakuwa chini ya usimamizi na uendeshaji wa TPB Plc, uamuzi ambao utaanza Mei 17, 2018


Hayo yamebainishwa na Naibu Gavana wa Benki Kuu Dkt. Bernard Kibese wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Mei 16, 2018 na kusema benki hiyo ya Twiga Bancorp iliyokuwa chini ya usimamizi wa benki kuu kwa takribani ya miaka miwili, ambapo mali za wateja na madeni ya benki hiyo kwa sasa yatasimamiwa na benki ya Tanzania Postal Bank Public Limited Company.

Dkt. Kabesema amesema uamuzi huu umechukuliwa ili kuboresha uangalizi na utendaji wa benki zinazomilikiwa na serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuuhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha.

Pamoja na hayo, Naibu Gavana Kibese amesema hatua kama hiyo itachukuliwa pia kwa benki nyingine za serikali ambazo ufanisi wake hautokuwa wa kuridhisha, kwani nia ya serikali ni kuwa na benki moja kama sio chache zinazofanya vizuri, malengo ambayo Rais Dkt John Pombe Magufuli amekuwa akisisitiza mara kwa mara.

Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa Bodi ya Bima ya Amana, Bi Rosemery Tenga amewataka walikuwa wateja katika benki ambazo zipo chini ya BOT kufuata mitaji ya benki hiyo kuyumba kwenda katika benki hizo na utaratibu wa malipo utafanyika chini ya usimamizi wa bodi ya Amana.

Uamuzi huo wa BoT umetokana na benki ya Twiga kuwa na upungufu mkubwa wa mtaji ambapo ni kinyume na matwaka ya sheria ya mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake ambapo kwa wakati huo ilihatarisha usalama wa sekta ya fedha.

Time ya Soka ya Watoto wa Kike Yachukua Nafasi ya Pili Kombe la Dunia

$
0
0

Timu ya soka ya Tanzania ya watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu, imefungwa kwa mbinde goli 1-0 na timu ya Brazil katika fainali ya Kombe la Dunia( Street Children World Cup)
-
Kwa matokeo haya timu hiyo imeshika nafasi ya pili katika michuano hiyo iliyoandaliwa na Shirika la Street Child United na kufanyika nchini Urusi
-
Timu hiyo ya Tanzania mpaka inaingia hatua ya fainali ilikuwa haijapoteza mchezo hata mmoja na hivyo mchezo wa fainali waliofungwa ndio mchezo pekee waliopoteza
-
Itakumbukwa kuwa mwaka 2014 nchini Brazil, timu ya wavulana walio kwenye mazingira magumu ilichukua ubingwa kwa kuifunga Burundi.

Zari Aamua Kumshauri Diamond Kutumia Kinga Anapo Chapachapa

$
0
0
KUNA kumlipua mtu, lakini huku kulipua kwingine ni sawa na kurusha bomu la nyuklia kwenye nyumba ya adui yako na kuisambaratisha kiroho mbaya.


NI ZARI

Hicho ndicho amekifanya mwanamama Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kwa aliyekuwa baby-baba wa watoto wake ambaye ni staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Katika mahojiano maalum na vyombo mbalimbali nchini Kenya wikiendi iliyopita, Zari ambaye ni mjasiriamali na mburudishaji mwenye jina kubwa Afrika Mashariki alifunguka makubwa live juu ya kuachana na Diamond, kubwa likiwa ni kumtaka atumie kinga au mipira ya kiume (kondomu) anapofanya usaliti.


KWA WANAUME WASALITI

Kupitia Citizen TV, Zari ambaye ni raia wa Uganda mwenye maskani yake, Pretoria nchini Afrika Kusini alitumia nafasi hiyo kutuma ujumbe kwa wanaume wote wasaliti kutumia kinga ili kutowahatarishia maisha wapenzi wao. Zari alisema hayo wakati akijibu swali aliloulizwa la sababu hasa iliyomfanya kutangaza kummwaga Diamond, ishu aliyoifanya Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day), Februari 14, mwaka huu.


Mama huyo wa watoto watano alieleza kwamba, mwanamke hawezi kumzuia mwanaume kusaliti, lakini kama mwanaume ameshindwa kujizuia na anapaswa au ameamua kufanya hivyo, basi angalau atumie kondomu katika tendo la ndoa.


KUMHATARISHIA MAISHA

Alisema kuwa, kwa kushindwa kutumia kondomu, mwanaume wake huyo (Diamond) angemhatarishia maisha kwa kumweka katika mazingira hatarishi ya kupata magonjwa ya kuambukiza kama Virusi Vya Ukimwi (HIV).

“Kwa wanaume, sisemi kwamba wawe wasaliti kadiri wawezavyo, hapana, lakini kama wanataka kufanya hivyo, wajaribu kutumia kondomu kwa sababu siyo kwamba watapata watoto wasiotarajiwa tu, lakini pia wataishia kupata HIV na magonjwa mengine ya kuambukiza (STD’s).“Siyo hayo tu, lakini pia wasipotumia kondomu watawapelekea magonjwa wengine (wapenzi wao) wanaowasubiria nyumbani,” alisema Zari aliyezaa watoto wawili na Diamond, Tiffah na Nillan.


HESHIMA KWA WAPENZI WAO

Zari pia aliwataka wanaume kufikiri na kuwaza juu ya familia zao na kama wameshindwa kabisa kujizuia na kuamua kusaliti, basi wasifanye mambo hayo hadharani kwani huko ni kuwakosea heshima wapenzi au wazazi wenzao.



“Kama ikitokea wote mkapata magonjwa haya ya kuambukiza ikiwemo HIV (Ukimwi), nani atawahudumia watoto wenu wadogo?“Unaweza ukafanya lolote kwa sababu upo kwenye biashara ya shoo (burudani), lakini vipi kuhusu mwenzako? Je, unafikiri nini juu ya watoto wako wadogo?

 HATUMII KONDOMU!

“Sawa, ni juu yako kujiachia unavyotaka kwa raha zako, sasa kwa nini unalifanya linakuwa jambo la watu wote kwenye jamii? Mbaya zaidi hutumii kondomu na ushahidi upo.“Ushahidi unakuwepo kwa sababu matokeo yake ni watoto kibao,” alifunguka Zari, maelezo ambayo yalitafsiriwa kuwa alimlenga Diamond.


ALIFUATA NINI?

Zari alitua nchini Kenya wikiendi iliyopita kwa ajili ya kampeni ya vita dhidi ya Ugonjwa wa Kansa kisha alihudhuria kwenye pati ya usiku iliyofanyika katika Ukumbi wa Uhuru Gardens jijini Nairobi ambapo akiwa huko alipata mapokezi ya kihistoria kwa namna anavyopendwa.



Juu ya kauli ya Zari akimtaka Diamond kutumia kinga, Risasi Mchanganyiko lilifanya jitihada za kumpata Diamond, lakini ziligonga mwamba hivyo zinaendelea.Kwa mahojiano yenye kusisimua ya Zari, kimbia kurasa za 8&9.

STORI: Mwandishi Wetu, Risasi Mchanganyiko.

Makubaliano yaliyofikiwa baina ya serikali na kampuni ya Tanzanite One

$
0
0
Kampuni ya uchimbaji Madini Tanzanite One imekubali kulipa fidia serikali pamoja na kodi watakayo kubaliana kutokana na dozari zilizokuwepo hapo awali.

Soma taarifa kamili;


Nimekuja Dar kumuona mtoto wangu Alikiba – Yvonne Chaka Chaka (+Video)

$
0
0
Msanii mkongwe Afrika Kusini Yvonne Chaka Chaka ameeleza sababu kubwa ya kuja Tanzania ni kumuangalia mtoto wake Alikiba na pia kuja kuachia rasmi wimbo wao mpya unaoitwa ‘Akili ya Mama’ ambao waliorekodi mwishoni mwa 2016.

VIDEO:

Mume Ashuhudia Mkewe Akiuawa

$
0
0
Jeshi la Polisi katika wilaya ya Gomba nchini Uganda linachunguza tukio la kuuawa kwa mwanamke mjamzito aliyejulikana kwa jina la Amina Nabukeera (19) katika Kijiji cha Bakandula.


Akisimulia tukio hilo mume wa marehemu Bwana Arafat Kabuubi amesema tukio hilo limetokea jana Mei 15, 2018 muda wa saa mbili usiku wakati akiwa na mkewe wakielekea kununua mahitaji ya nyumbani

“Mimi na mke wangu tulikuwa tunaenda moja ya maeneo ya biashara muda wa saa mbili usiku kununua mahitaji ya nyumbani, nilikua nikitembea mbele yake kabla sijasikia purukushani nyuma yangu na nilipogeuka niliona mtu akimshumbulia mke wangu kwa kumpiga na nyundo kichwani, alimkata sikio la upande wa kulia pamoja na taya kwa kutumia panga kabla ya kukimbia. niliogopa sana na nilikosa nguvu za kumpigania mke wangu” amesema bwana Kabuubi

Bwana Kabuubi aliongeza kuwa alijaribu kupiga kelele za kuomba msaada lakini alikua tayari amechelewa kumuokoa mke wake ambae alifariki wakati akitafuta usafiri wa kumpeleka katika kituo kidogo cha afya.

Mkuu wa Polisi katika mkoa wa Katonga Kamanda Joseph Musana amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuomba wananchi kuwa watulivu wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi wa kumbaini mtuhumiwa.

Hilo ni tukio la pili kwa marehemu kushambuliwa ambapo mwezi Machi mwaka huu alishambuliwa akiwa nyumbani kwake lakini alipatiwa matibabu katika kituo kidogo cha afya.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Gomba ukisubiri kufanyiwa uchunguzi wa kidaktari.

Kiboko ya Matatizo ya Nguvu za Kiume, Maumbile Madogo, Mvuto wa Mapenzi na Magonjwa Sugu

$
0
0
KIBOKO YA MATATIZO YA NGUVU ZA KIUME,MAUMBILE MADOGO, MVUTO WA MAPENZI ,MAGONJWA SUGU

Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiasili watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapunguvu katika mwiliwake.

Kunasababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

SUPER CHAN :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

LUGINI 3 POWER:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

MANUS :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

TULIZA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR GALIMBO NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO
PIGA SIMU 0759208637

Mahakama Yaibana Serikali kesi ya mhasibu Takukuru

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetoa siku 14 kwa upande wa mashtaka kuhakikisha wanakamilisha kuchapa maelezo ya washtakiwa wa kesi ya kumiliki mali zisizoendana na kipato, inayomkabili mhasibu mkuu wa Taasisi na Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai na wenzake watatu.

Mbali na Gugai, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasini Katera na wote wanakabiliwa na mashitaka 43 yakiwemo 20 ya utakatishaji wa fedha haramu, kumiliki mali zisizoendana na kipato na kughushi mikataba ya mauziano ya viwanja katika maeneo mbalimbali.

Uamuzi huo umetolewa leo Mei 16, 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya kesi hiyo kuahirishwa kwa zaidi ya mara saba,ikiwa katika hatua ya kuwasomea hoja za awali (PH), washtakiwa hao.

Hatua hiyo, inatokana na upande wa mashtaka kuieleza Mahakama hiyo kuwa wapo katika hatua za mwisho za kuchapa maelezo ya washtakiwa.

Awali, wakili wa Serikali Mkuu, Vitalis Peter amedai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali, lakini walikuwa hawajakamilisha uchapaji wa maelezo ya washtakiwa hao.

“Kesi imekuja kwa ajili ya upande wa Jamhuri kuwasomea maelezo ya awali washtakiwa wote , lakini tunaiomba Mahakama itupe ahirisho la mwisho ili tuweze kukamilisha uchapaji wa maelezo ya washtakiwa,” amedai wakili Peter.

“Tayari maelezo ya washtakiwa tumeshaanda na kilichobaki ni kuchapwa tu, hivyo tunaiomba Mahakama yako itupe ahirisho la mwisho.”

Baada ya maelezo hayo, wakili wa utetezi, Semi Malimi na Alex Mgongolwa wamedai kuwa maelezo ya awali yameahirishwa kusomwa kwa zaidi ya mara saba kuanzia April 4, 2018.

Baada ya kupitia maelezo ya pande zote, hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Mei 30, 2018 na kuutaka upande wa mashtaka kuhakikisha wanakamilisha kuchapa maelezo hayo ili washtakiwa hao waweze kusomewa maelezo ya awali.

Kampuni ya Tanzanite One yakubali kuilipa Serikali fidia

$
0
0
Kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzanite One imekubali kuilipa Serikali fidia pamoja na kodi watakayokubaliana kutokana na dosari zilizokuwepo hapo awali.

Makubaliano hayo yametiwa saini Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli Profesa Palamagamba Kabuni na  Mkurugenzi wa Tanzanite One Bw.Faisal Juma.

Akizungumza mara baada ya kutia saini makubaliano hayo, Mwenyekiti wa  kamati ya majadiliano kwa upande wa Serikali, Prof. Palamagamba Kabudi amesema Tanzanite One imekubali kulipa fidia Serikali kutokana na mambo iliyofanya ambayo yalikuwa kinyume na utaratibu ulioleta hasara kwa Serikali.

Amesema fidia hiyo inatakiwa kulipwa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza italipwa ndani ya wiki mbili kuanzia leo  na haitahusisha Kodi. Pia Kampuni hiyo Tanzanite One italazimika kulipa kodi kama kawaida inazodaiwa na Serikali na tozo nyingine zote zinazodaiwa na Serikali.

Pia  Serikali  imekubaliana na Kampuni ya Tanzanite One kuwa itafuata masharti yote ya sheria ya madini ya mwaka 2010 ambayo inaeleza kuwa ni Watanzania tu ndio wanaoruhusiwa kuchimba madini ya Vito na pale ambapo watanzania hawana uwezo huo ndipo wanapoweza kuingia ubia na wageni.

Aidha Prof. Kabudi amesema kuhusu wachimbaji wadogo wadogo wa Tanzanite katika eneo la Mirerani  utaratibu mpya unawekwa lengo kubwa ikiwa ni kutekeleza sheria ya madini ya mwaka 2010 ambayo inalenga madini ya vito kuwa mikononi mwa Watanzania.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzanite One Faisal Juma amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuunda kamati hiyo ya kizalendo katika kufuatilia rasilimali za madini nchini ambapo wameweza kujadiliana na kufikia muafaka wa kulipa fidia ikiwa ni mbali na malipo yote yaliyotakiwa kulipwa serikali ikiwemo kodi.

Amesema Tanzanite One itahakikisha inafuata taratibu zote za Sheria ya Madini ya mwaka 2010 kwa lengo la kuhakikisha rasilimali ya madini inawanufaisha Watanzania na kwamba uvunjifu wa sheria uliofanywa na kampuni hiyo hautajirudia tena.

“Sisi kama Tanzanite One tunaihakikishia Serikali kuwa uaminifu uliotuonyesha na sisi pia kama Kampuni tutahakikisha tunakuwa waaminifu na kuwa zao hili linanufaisha taifa kutokana na imani aliyotuonyesha Mhe. Rais kama wananchi wake kutupa nafasi na fursa ya kusikilizwa ili kurekebisha makosa tuliyoyatenda” amesema   Faisal.

Faisal amesema Tanzanite One itahakikisha haitafanya makosa iliyofanya mara ya kwanza na hivyo kuwa mfano wa kampuni nyingine za madini kuhakikisha rasilimali za madini zinawanufaisha Watanzania.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi Mawasiliano ya Rais, IKULU.
Dar es Salaam
16 Mei, 2018

Kondakta Atiwa mbaroni kwa kukutwa na vipodozi vilivyopigwa marufuku

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia  kondakta wa kampuni  moja ya mabasi yanayofanya safari kati ya Dar es Salaam na Mbeya,baada ya kumkuta na vipodozi vilivyopigwa marufuku.

Mtuhumiwa huyo mkazi wa Kitunda jijini Dar es Salaam alikutwa akiwa amehifadhi vipodozi hivyo katika mifuko miwili ya plasitiki na kwenye boksi.

Akizungumza leo Jumatano Mei 16, 2018 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa baada ya polisi kusimamisha basi na kulifanyia upekuzi.

Amesema tukio hilo limetokea Mei 15, 2018  saa mbili usiku huko maeneo ya Melela Barabara Kuu ya Iringa-Morogoro.

Matei amesema mtuhumiwa alikutwa na vipodozi katoni 56 vya aina tofauti na kwamba vipodozi hivyo vimepigwa marufuku kuingizwa nchini.

Alivitaja vipondozi hiyo kuwa ni Extra Claire tube katoni 23,Lemon Vert Cream katoni 12, perfect white cream  6, betason 4, carolite 3, beiaton 2, extra cream1, sivop cream 1, dyna Claire 1, lemonvet cream 1, princes tube cream 1, epiderm cream 1, exoplus boksi 1, actilua lotion dazen 11, demon Claire pakti 3, oranvet jelly pakti 3 na Claire for men 11

Katika tukio lingine kamanda Matei amesema polisi wanamshikilia  mkazi wa Kikwalaza tarafa ya Mikumi wilayani Kilosa kwa tuhuma za kukutwa na meno ya tembo yenye uzito wa kilogramu 10 zenye thamani ya Sh34 milioni , akiwa amezipakia kwenye baiskeli.

Kamanda Matei amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa Mei 15, 2018 na polisi wakishilikiana na maofisa wanyamapori.

Amesema alikutwa akiwa amepakia meno hayo katika baiskeli.
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>