Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Ripoti: Tanzania Yaongoza Kulalamikiwa kwa Matumizi Mabaya ya Instagram Duniani

$
0
0
Mtandao wa Instagram unaohusisha uwekaji picha umeendelea kupata mashabiki wengi nchini Tanzania lakini wengi kati ya watumiaji hao wameisababisha kuwa kati ya nchi zinazoongoza kwa matumizi mabaya ya mtandao huo duniani kote.

Ripoti hiyo imetolewa na Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasialiano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy katika mahojiano maalum aliyofanya na Ibrahim Issa wa 100.5 Times Fm.

“Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo zimeongoza kwa watu kulalamika kwamba matumizi yetu hayaendani na makusudio. Na hii inatokana na pale watu ambao wanawafuata watu wa` Tanzania kuona vitu wanavyoweka vitu wanavyoweka, ugomvi, matusi, picha za ajabu…za ngono na nini. Sasa watu huwa wanalalamika.” Amesema Innocent Mungy.

“Wanapolalamika, ule mtandao huwa unaweka record kwamba watu wengi waliolalamika kwenye mtandao huu kuhusu picha za watumiaji ambao wako Tanzania labda ni 20 wakilinganisha na sehemu nyingine ambazo idadi inakuwa ndogo zaidi.” Ameongeza.

Amefafanua kuwa kwenye mitandao yote ya kijamii, wakati wa kujiunga mtumiaji hupewa maelezo ya kurasa kadhaa kuhusu namna ya kutumia mtandao huo ikiwa ni pamoja na makatazo lakini watumiaji wengi wa Tanzania huwa hawayafuatilii/huyapuuza.

Mwisho, Mungy ametoa wito kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini kuitumia mitandao hiyo kwa maendeleo na sio vinginevyo.

“Mitandao hii ya kijamii kama mawasiliano ni maendeleo. Matumizi ya mitandao sio mabaya ila watumiaji ndio wanafanya vitu vibaya. Ningewataka watanzania ambao wanatumia mawasiliano haya vibaya waache. Tuitumie vizuri. Na wale watu ambao unawaona wewe hawaendani na matumizi ambayo yanapendeza, wafute kwenye mtandao wako. Wa-Unlike, wa-Unfriend au wa-delete kabisa ili usione hayo mambo yao ya kipuuzi wanayofanya.”

Usikose kusikiliza kwa undani habari hii katika kipindi cha Mtazamo Wiki Hii cha 100.5 Times Fm, Jumamosi hii kuanzia saa moja kamili asubuhi.

Diamond Apiga Mbili kwa Mpigo, Ashinda Tuzo Australia na Atajwa Kuwania Tuzo ya MTV Europe Music

$
0
0
Neema inazidi kumuangia Diamond Platinumz na leo amepata habari njema baada ya kutajwa kuwania tuzo ya MTV EMAs huku akipokea tuzo kutoka nchini Australia.

Diamond amewapa mashabiki wake habari njema za ushindi wa tuzo ya AAMA ya Australia kupitia tiketi ya collabo ya aliyopewa na Desert Eagle, wimbo unaoitwa ‘Everyday’.

Ningependa niwajulishe kuwa kijana wenu nimepata tunzo nyingine toka Australia ya Collabo bora ya Mwaka toka kwenye tunzo za #AAMMA_Awards kupitia nyimbo niliyoshirikishwa na Desert Eagle iitwayo #EVERYDAY..... (jus wanted to inform you that, your favourite artist @Diamondplatnunz won another award from Australia on #AAMMA_Awards as best Collaboration song of the Year..).” Ameandika.

Wakati huo huo, mtoto wa Tandale ametajwa kuwa moja kati ya wasanii wanaowania MTV Europe Music Awards mwaka huu huku akichuana na wakali wengine kutoka Afrika akiwemo Davido, Toofan (Togo) na Goldfish (Afrika Kusini).

Msanii mwingine wa tano akisubiria kutajwa baada ya mashabiki kumpekeza kutoka kwenye kundi la wasanii sita ambao ni Anselmo Ralph, Gangs of Ballet, Mafikizolo, Sarkodie, Sauti Sol na Tiwa Savage.  

Aidha, majina yote ya wasanii wanaowania tuzo hizo yatatajwa September 16 ambapo upigaji kura utaanza rasmi.

Hongera Diamond Platinumz, Tanzania inazidi kutajwa kwenye majukwaa ya kimataifa.

Sikiliza na Download Another New Hit Single From Jux

$
0
0
Miongoni mwa mastar wa Tanzania wanaofanya Bongo Fleva ambao wana mashabiki wengi wa kike ni pamoja na Jux inawezekana labda aina ya muziki anaoufanya kuwagusa wasichana wengi

Zimesikika zingle zake kadhaa ikiwemo Napata Raha,Nitasubiri ,Uzuri wako na hii iko kwenye list ya single zake ambazo amesema anategemea zitafanya vizuri zaidi,Jux pia ni mmoja kati ya wanaounda kundi la Wakacha akiwepo na Cyril.
Bonyeza play kusikiliza.

Kajala Azuzuliwa na Pesa, Afanya Vituko ,Amwaga Malaki Uwanjani

$
0
0
FEDHA mwanaharamu! Katika hali ya kushangaza, staa wa filamu ambaye fedha imemtembelea kwa sasa, Kajala Masanja ‘K’ amenaswa akimwaga fedha kama amechanganyikiwa mbele ya kadamnasi, Risasi Mchanganyiko linakupa mchapo kamili.

Tukio hilo lililowaacha watu midomo wazi lilitokea hivi karibuni katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar, kulipokuwa na uzinduzi wa filamu ya Mateso Yangu Ughaibuni ambapo muigizaji huyo alionesha jeuri ya fedha baada ya kupagawishwa na sebene la Yamoto Band.

ALIINGIA NA WAPAMBE
Awali, paparazi wetu alimshuhudia Kajala akitinga viwanjani hapo akiwa ameongozana na wapambe takriban 15 na kwenda kukaa katika meza moja ambapo mhudumu aliwasikiliza kujua wanachokunywa.

VINYWAJI VYAAGIZWA NJE
Kutokana na uzinduzi huo kutokuwa na pombe, K aliamuru kila mtu aletewe kile anachokihitaji halafu bili yote apelekewe yeye, Mama la Mama kama wanavyowaita watoto wa mjini.
“Waletee hawa vinywaji wanavyojisikia kunywa pia wasikilize meza ile pale kisha bili niletee mimi,” alisikika Kajala

MINONG’ONO YAMTIA WAZIMU
Baada ya kauli ile wafuatiliaji wa mambo ya watu hasa wakienda shughulini wakaanza kutoa minong’ono kuwa hata iweje bado Kajala hajafikia uchezeaji wa fedha kama alivyokuwa shosti wake wa ‘long time’, Wema Sepetu aliyepewa taito ya Madam kutokana na kujua kuzitumbua fedha.

“Kwani kuagizia watu vinywaji ndiyo kuonyesha kufuru au jeuri ya fedha, angalia wahudumu wanavyogawa vinywaji kwa kusuasua, unafikiri angekuwa Madam (Wema) angekubali hata akae muda wote asiende kutunza thubutu, chezea Madame (Madam) wewe,” alisikika mualikwa mmoja.
YAMOTO BAND WAMWINUA
Ndani ya muda mfupi, Kajala akavunja ukimya baada ya bendi ya Yamoto kupiga wimbo wa Nitajuta ndipo Kajala aliposhindwa kuvumilia na kwenda kuwamwagia fedha huku wapambe wake wakimshangilia.

“Ndiooo mkurugenzi hivyo ndivyo ujana unavyoliwa,” kelele zilisikika kutoka katika meza waliyokuwa wameketi wapambe wake.

KAMA LAKI SITA NA USHEE
Ufukunyuzi wa paparazi wetu kwa harakaharaka, ulizihesabu fedha hizo alizowamwagia watoto hao wa Mkubwa Fella ambapo hesabu zilionesha zilikuwa zaidi ya shilingi laki sita.

AKOSOLEWA
Hata hivyo kuna baadhi ya watu walimkosoa staa huyo kwa kusema kitendo cha yeye kupata fedha kwa sasa kinaonekana kumchanganya kiasi cha kuzimwaga pasipo kuwa na sababu ya msingi.

“Bora angetunza kidogo na nyingine akatumia kwa vitu vya maana likiwemo suala la kumsaidia mume wake ambaye yuko jela kwa kushindwa kulipa faini ya shilingi mil. 200,” alisikika mdau mmoja wa filamu ambaye hakutaka kuanikwa jina gazetini.

UZALENDO WAMSHINDA STEVE NYERERE
Kadri Kajala alivyozidi kumwaga fedha, uzalendo ulimshinda Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ambapo alimfuata Kajala na kutaka na yeye amtunze.
“Hebu kuwa na adabu, mi mkubwa wako na mimi nitunze kwanza mambo mengine yaendelee, haiwezekani uoneshe jeuri ya fedha kiasi hiki wakati mimi mdau nipo hapa hunipozi,” alisikika Steve Nyerere.

AMEZIPATA WAPI FEDHA?
Baada ya vurugu zote zile kufanyika, paparazi wetu alimvaa Kajala na kutaka kujua vyanzo vya fedha hizo na kumuuliza kama amehongwa, akachomoa.

“Mimi sihongwi ukitegemea fedha za mwanaume huwezi kuwa na heshima mjini, nina biashara zangu na kampuni yangu hiki ninachokitumia hapa ni faida tu ya siku mbili tatu mimi mjasiriamali wewe,” alisema Kajala.

TUJIKUMBUSHE
Kumbukumbu zinaonesha, kipindi ambacho Kajala na Wema walikuwa marafiki, Kajala hakuwa na fedha nyingi lakini baada ya kutofautiana, pesa imemtembelea huku mwenzake akidaiwa kuyumba kiuchumi.
GPL


Mauji ya Wanawake Arusha, Mama Fezza Kessy Nae Anusurika Kuuwawa

$
0
0
WAKATI hofu ya mauaji ya wanawake ikiwa bado imetanda mkoani Arusha, mama mzazi wa mshiriki wa shindano la Big Brother Africa, Feza Kessy ameponea chupuchupu baada ya kuvamiwa na majambazi wawili kisha kuporwa fedha.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutoka jijini humo, Feza alisema mama yake aitwaye Rose Kessy alikutwa na masaibu hayo mchana wa saa nane, Jumatano iliyopita akiwa hatua chache kutoka nyumbani kwake, eneo la Boma ya Siara, Moshono.

“Watu wawili wakiwa na pikipiki walimsimamisha akiwa garini anarejea nyumbani, wakamteremsha na kuanza kumsachi, wakachukua pochi yake ambayo ilikuwa na shilingi laki tatu ndani. Wakati wanafanya tukio hilo watu walikuwa wanatazama tu bila kufanya lolote.

“Watu wengine walipita na gari wakataka kusimama, lakini wakaonyeshwa bastola na kupewa ishara ya kuendelea na safari. Yaani walikuwa wanafanya wakiwa hawana wasiwasi utafikiri ni askari vile, hivi hapa ndiyo nimerudi kutoka polisi,” alisema mshiriki huyo ambaye pia aliwahi kushiriki shindano la Miss Tanzania miaka ya nyuma.
GPL

Watu Wengi Sana Hasa Wanawake Wamefanya Whats App Sehemu ya Kujifariji

$
0
0

I hate WhatsApp na Mitandao mingine kama fb from the bottom of my heart (nipo huko kwa sababu kuna some meaningful contacts), lakini acha tu niwepo, maana wakati mwingine hii mitandao inanisaidia kufanya research zangu na Biashara.

Tatizo ni badala ya watu kuitumia kuwasiliana kwa mambo ya maana na kuwa na mipaka ya ni watu gani wapate messages wanazoandika, basi unakuta kwenye STATUS za whatsApp chini ya profile, messages kama vile:

"I luv u dady, can't wait to 've ur f" (Unakuta ni uzushi tu, hakuna chochote, hajaolewa wala nini, kama sio ufuska ni nn?)

"Oh baby, I can't forget that f u gave me last night" (Sijui alikutana na mtu tu akamnyapua, yeye tayari keshaanza kumpublish kama baby)

"We are the real lovers, no one can separate us" (Unakuta ndoa inatemblea drip, ina migogoro balaa)

"luv luv luv u my husband, u know ur a gentleman" (Mkianza kuchat anamdis jamaa)

"This is my beloved son, he was born when his father was going to Europe, so two in one!" (Europe tandika! Hajui hata Airport iliko!)

"Kill them with succes n burry them with Smile" (Unakuta mambo yamemgomea, hasa vitoto vya shule, may be hata amedisco, mafanikio yatakuwa yake!)

"I'm single but this does not mean I'm available" (Hapa amechakazwa, hadi hajijui status yake!)

etc, etc, etc.,

Bado wale wanaojipa matumaini na kujifanya mara wanampenda Mungu sana, sijui Yesu na wakati hata hawamjui! 

Bado picha za uchi - kuonyesha nyonyo, mattako, mara wanapeana kisses,mara wamekumbatiana.

Yaani kuna vimbwenga visivyokuwa vya kawaida na visivyoisha! Wengi wao huwa nadelete namba zao za simu, nikiwavumilia huwa nawablock. Wale ninaowavumilia sana huwa nawaacha tu kama walivyo!

Baada ya kufanya research kuhusu hawa watu hasa wa WhatsApp ndipo nilipogundua yafuatayo:

1. Wanaoandika message kuonyesha wanawapenda wenzi wao, wala hawawapendi - ukiwapa tu nafasi ya kuchat wanaanza kuandika maneno ya usaliti kuhusu wapenzi wao

2. Wanaoandika msgs kujifanya wamewamiss wenzi wao - hawana hata wapenzi wa kusingizia, wanajifariji baada ya kukataliwa, wewe waruhusu tu kidogo waongelee habari ya mapenzi, mbona majanga!

3. Wanaoandika msgs kali kali kuhusu mapenzi e.g. "leave me alone", "Kwani mapenzi/mwanaume kitu gani" - wametendwa baada ya kuwavamia wanaume kichwakichwa

4. Wengine wanaandika msgs kama vile "Sexy me", "love myself", - hawa wanatafuta attention ya wanaume na kujaribu kujipandishia self esteem.

5. Bado wale wanaoweka picha za magari, majumba na kuandika "Hapa ndio kwa hubby", sijui "I'm tired driving this BMW thing, need to change a car!", - hawa wanataka kujionyesha kuwa mambo yao safi hata wasipoolewa maisha yatasonga kwa nguvu ya wallet.

Yaani kuna mengi, mengi .........

Baada ya Kushindwa Mapenzi ya Diva na Chagga Barbie Prezzo Aamua Kutulia Kimapenzi na Mrembo Asiye na Umaarufu

$
0
0
Baada ya drama kutoka kwa Diva, Huddah Monroe na Chagga Barbie, Prezzo ameamua kutulia na msichana asiye na umaarufu wowote.

Rapper huyo kutoka Kenya ameshare picha ya mrembo wake mpya kwenye Instagram na kuandika: “My 1st & only #WCW #Rapcellency #TrulyUnruly.”

Diva Afunguka Tena…Adai Zitto Kabwe ni Mume Wake na Anatambulika Kisheria

$
0
0
Mtangazajiwa Kipindi cha Ala za Roho kinachorushwa kupitia Radio Clouds FM ya jijini Dar, Loveness Malinzi ‘Diva’ kwa mara ya kwanza, amejilipua kuzungumzia uhusiano wake na Zitto Kabwe kwamba walikuwa mke na mume.

Katika mahojiano maalum na mwanahabari wetu jijini Dar juzi, Diva alisema anashangazwa na baadhi ya vyombo vya habari  kumnyima uhuru wa kuongelea suala lake na ‘zilipendwa’ wake huyo wakati kisheria yeye ni mke wake hivyo anapaswa kuzungumzia kutengana kwao.

“Ninyi mnayaongelea mambo ya Zitto na mimi juu kwa juu tu hamjui kama mimi nimeishi naye kama mke na mume nyumbani kwake Masaki (Dar), sasa nini kilisababisha penzi letu kuvunjika watu hawajui, nina ushahidi wa kutosha lakini wanaongeaongea tu,” alisema Diva.Akaongeza: 

“Sasa ninavyojua mimi kwa sheria za nchi, mwanamke na mwanaume wakiishi pamoja kwa zaidi ya miezi sita tayari ni mke na mume. Hawezi kuniacha kirahisirahisi tu.”

Diva alikwenda mbele zaidi kufuatia kauli ya Zitto aliyoitoa hivi karibuni kupitia Kipindi cha Mkasi kinachorushwa hewani na Runinga ya East African Television ‘EATV’ na mtangazaji Salama Jabir.

Zitto aliulizwa ana uhusiano gani na Diva, naye akajibu ni mtu wanayefahamiana tu lakini si mpenzi wake.

Ilidaiwa kwamba, majibu hayo ya Zitto kwa Salama ndiyo yaliyoibua hasira ya Diva hadi kufikia hatua ya kutupia kwenye ukurasa wake wa Instagram, e-mail aliyodai aliwahi kutumiwa na Zitto siku za nyuma akimtaka asiwe anaweka wazi uhusiano wao kwa sababu atachafuka kisiasa.

-mail ilisomeka  hivi:
Unanikosea sana ujue unapoweka mambo yetu hadharani. Ninaonekana siwezi kuwa kiongozi kwa sababu nashindwa ku-handle masuala yangu binafsi.
“Madhara uliyoyafanya ni makubwa sana. Wapinzani wangu wa kisiasa watayatumia sana dhidi yangu.

“Ungekuwa unajua madhara yake usingethubutu kufanya ulivyofanya mara tatu sasa. Sijui nia yako nini, ila ipo siku utajua umenikosea sanasana.”
  
Swali la mwandishi:
Je, Zitto akikubali kufuata huo utaratibu uwe mkewe utamuacha GK ambaye umekuwa ukimtangaza kuwa mpenzi wako?
Diva: Hilo nitakujibu baadaye.

Siku za karibuni, baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti uhusiano wa Diva na Zitto bila kuzama kwa undani.

Kufuatia Diva kutupia madai hayo mtandaoni na kudai yeye ana hadhi ya mke kwa Zitto na kauli ya Zitto kwenye runinga kwamba Diva si mpenzi wake, baadhi ya watu waliozungumza na Amani walionesha kwenda kinyume na mtangazaji huyo.

Wengi walidai kwamba wana kumbukumbu zilizonyooka kwamba Diva amewahi kujinadi kutoka na Mbongo Fleva, Gwamaka Kaihula ‘Crazy GK’.

“Sasa Diva anavyodai ni kama mke wa Zitto mbona anamtangaza mwanaume mwingine?” Alisema mkazi mmoja wa jiji aitwaye Yuda.

Naye Ismail Juma, mkazi wa Kigogo, Dar alisema aliwahi kusoma kwenye vyombo vya habari kwamba Diva anapumzika na mwanamuziki kutoka Kenya, Jackson Makini ‘Prezzo’ kiasi cha kumzalishia bifu na demu wa jamaa huyo, Huddah Monroe.
“Diva awe na aibu basi, asikurupuke wakati yeye mwenyewe si msafi kivile,” alisema Ismail.


Kufuatia madai hayo, kwa muda wa siku saba, Amani limekuwa likimsaka Zitto kwa njia ya simu lakini bila mafanikio.Watu wa karibu naye walipoulizwa alipo, walisema wanachojua ana shughuli zake nchini Zambia.

Esha Buheti Apigwa Vijembe kwa Kuwa na Makalio Madogo

$
0
0
Kitendo cha kutojaaliwa makalio makubwa kwa staa wa filamu za Kibongo, Esha Buheti kimemsababishia anangwe na wasanii wenzake.

Akiongea  na  mwandishi wetu, Esha alisema anafahamu na anawashangaa watu wanaoponda maeneo hayo ya mwili wake kwani kwa upande wake anaamini kuwa mwanamke sura, makalio majaaliwa kwani hata mwanaume aliyemuoa analijua hilo na anampenda jinsi alivyo.

“Kwa kuwa mume wangu ananikubali jinsi nilivyo hainiumizi kichwa kwani mimi naamini sifa ya mwanamke ni tabia na wala siyo shepu kama wengine wanavyofikiria,” alisema Esha.

AJALI: Mwanamke Aanguka Kwenye Bodaboda, Akanyagwa na Lori na Kufariki Dunia Papo Hapo

$
0
0

Mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 amekufa papo hapo baada ya kudondoka kwenye pikipiki aliyokuwa amepanda na kisha kukanyagwa na gari.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura amesema kuwa ajali hiyo ilitokea jana  mchana katika barabara ya Bagamoyo eneo la Tangibovu ambapo gari likiendeshwa na dereva asiyefahamika akitoka kwa Alysykes kuingia barabara ya Bagamoyo, aliigonga pikipiki namba T 505 CTJ Fekon ikiendeshwa na dereva asiyefahamika.
Alisema pikipiki hiyo iliyokuwa ikitokea Mbezi Makonde kwenda Mwenge ilikuwa imempakia mwanamke huyo ambaye baada ya pikipiki kugongwa alianguka chini na kisha kukanyagwa na lori namba T 277 CIL aina ya Tata likiwa na trela namba T 339 CYB lililokuwa katika uelekeo mmoja na pikipiki.

Kamanda alisema mwanamke huyo alikufa papo hapo na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala huku Polisi wakiendelea kuwasaka madereva waliohusika katika ajali hiyo.

Mwigizaji Lulu Michael Amnasa Meneja wa Wema Sepetu

$
0
0
Na Shakoor Jongo
Taarifa ikufikie kwamba sexy lady wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amemnasa aliyekuwa meneja wa Wema Isaac Sepetu, Martin Kadinda ambaye ndiye atakuwa meneja wake kwa sasa.

Akizungumza na Amani kwenye Hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro iliyopo Posta jijini Dar hivi karibuni waliponaswa wamegandana kama ruba, Kadinda alimuwahi mwanahabari wetu na kumsihi kuwa hawana uhusiano wa kimapenzi bali kuna habari mpya.

Kadinda ambaye hivi karibuni alimwaga kibarua kwa Wema, alisema kwamba aliongozana na Lulu hotelini hapo kwa kuwa kulikuwa na Fainali ya Shindano la Miss Ilala, Dar, wakiwa ni mtu na meneja wake kama alivyokuwa kipindi yuko na Wema.

“Kwa sasa ‘nammeneji’ Lulu. Naomba ieleweke hivyo ili baadaye watu wasiseme tunatoka kimapenzi kwa sababu nitakuwa naonekana naye kila mara na kwenye sehemu tofauti,” alisema Kadinda ambaye pia ni mbunifu wa mavazi.

Kwa upande wa Lulu, alionekana kufurahia maneno hayo na kufanikiwa kumpata meneja huyo huku akiongezea kuwa amefarijika kuwa na meneja kama Kadinda.“Huyu ni meneja bora na siyo bora meneja kwa hiyo kama mtu anataka kufanya kazi na mimi, aanze kwa meneja wangu,” alisema Lulu.
Ukaribu wa Lulu na Kadinda ulianza kitambo hata kabla Kadinda hajafahamika kama ilivyo sasa.

IPTL Yamdai Zitto Kabwe Fidia ya sh. Bilioni 500

$
0
0
Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), imefungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, wakimtaka Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe awalipe fidia ya Sh bilioni 500 kutokana na kutoa kashfa dhidi yao.

IPTL, Kampuni ya Pan Africa Power Solutions Tanzania Limited (PAP) na Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni hayo mawili, Harbinder Seth wamefungua kesi dhidi ya Zitto, Mhariri wa gazeti la Raia Mwema, Kampuni ya Raia Mwema na Kampuni ya Flint Graphics.
Washitakiwa wengine wameshitakiwa kwasababu  makala yenye maneno ya kashfa na kuwachafua, iliyochapishwa Agosti 13 mwaka huu katika ukurasa wa 7 na 14 wa gazeti lao, ikiwa na kichwa cha habari  cha “Fedha za IPTL ni Mali ya Umma” na Kampuni ya Flint Graphics kwa kuchapisha gazeti hilo.
Aidha, wanaiomba Mahakama iamuru makala hayo, yalikuwa ya upotoshaji na kuwachafua kwa kudhamiria,  pia wadaiwa waombe radhi kwa kuchapisha habari ya kuomba msamaha kwenye kurasa za mbele katika matoleo mawili mfululizo ya gazeti hilo. 

Wadaiwa hao waliiomba Mahakama, itoe zuio kwa wadaiwa, watumishi wao, wafanyakazi, washirika, wawakilishi au watu wengine wanaofanya kazi chini ya wadaiwa,  kuchapisha au kuandika makala yoyote ya kuwachafua.

Mwigizaji Johari Bado Anateswa na Penzi la Ray..Asema Ipo Siku Lazima Ray Arudi Kwake

$
0
0
Na Rhoda Josiah
MKONGWE katika tasnia ya filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ ameonekana kuendelea kuteseka na penzi la mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ baada ya kunaswa akimzungumzia.

Tukio hilo lilijiri juzikati katika Viwanja vya Leaders Club kwenye uzinduzi wa filamu ya Mateso Yangu Ughaibuni ambapo Johari alikuwa amekaa na kruu yake (huku  wakigonga ulabu) ndipo mmoja kati wenzake hao, akagusia stori za Ray kisha Johari alicheka na kusema ipo siku Ray atarejea katika mikono yake.

“Ipo siku ambayo haijulikani tarehe wala mwaka Ray lazima atarudi katika mikono yangu kwani namfahamu sana Ray kuwa ni mtu wa kuruka lakini kwangu amefika,” alisikika Johari.

Good news! Mtanzania Mwingine Kwenye Headlines… Kapewa Vyeo BET

$
0
0
Kabla ya kuanza kukupa info kuhusu huyu Mtanzania nataka nikukumbushe headlines chache za Watanzania walioingia kwenye headlines za kimataifa hivi karibuni.
Ni CloudsTV International kufungua ofisi Kingston Jamaica ambayo itahudumia ukanda wa Caribbean, Diamond Platnumz kuchaguliwa kushiriki tuzo za MTV Europe, AzamTV kuanza kufanya kazi Uganda kwa kuhudumia mamilioni kupitia king’amuzi chake na power bank za Puku zinazomilikiwa na Mtanzania aishie Marekani.
Sasa hivi vichwa hivyo vya habari vitaongezewa hii kubwa nyingine baada ya Mtanzania Kay Madati kuchaguliwa kuwa makamu wa Rais katika kituo kikubwa cha Television nchini Marekani BET.

Taarifa iliyoandikwa na Mtandao maarufu wa Forbes imesema amechaguliwa ‘Kay Madati as Executive Vice President and Chief Digital Officer. Madati, a Tanzanian citizen who has lived in Africa, the United Kingdom, and the United States’
Nilikua sifahamu kama Madati ambae ni raia wa Tanzania aliyeishi UK, Marekani na Afrika, aliwahi kuwa makamu wa Rais CNN Worldwide… aliwahi pia kufanya kazi na BMW Amerika kaskazini, Octagon Worldwide lakini pia amefanya kazi na Facebook.
‘Madati was most recently the Head of Entertainment and Media on the Global Marketing Solutions team at Facebook Inc‘
Sehemu ya kazi ya Madati BET itakua ni kuziongoza timu za BET kwenye maswala ya digital ‘will oversee BET Digital, the interactive arm of BET Networks whose platforms include BET.com, which encompasses entertainment, music, culture, and news; BET Mobile, which provides apps, ringtones, games and video content for wireless devices; Centric.tv, the online home for the Centric cable channel; and BET Video On Demand, one of the largest VOD services providing African-American content‘

Unawapa Somo Gani Wadada Waliobakiwa na Vitu Vya Kuhongwa na Kuyakosa Mapenzi?

$
0
0

Unawapa somo gani wadada waliobakiwa na magari ya kuhongwa, Simu za gharama za kuhongwa, majumba ya kuhongwa huku wakiyakosa Mapenzi na kusema Watapaki kuwa Single Ladies forever?

Hakuna kitu kinachoumiza moyo kama mapenzi hata kama unamiliki dunia.

Utajikaza tu lakini, maumivu yako pale pale; hata unywe hadi ulewe, uvute hadi uchizike.

Cha muhimu ni kumheshimu akupendae, hasa kama tayari mpo kwenye kiapo cha ndoa. 

Mwaka juzi ilitokea nchini Nigeria; Wanawake zaidi ya 8,000 waliandamana hadi kwa waziri kuitaka serikali iwatafutie wanaume wa kuwaoa, la sivyo watachukua wanaume wa wale wenye ndoa ili wawatumie kwa zamu.

Kunda Mwanamke Ndugu yangu Kabisa Wakati wa Ujana wake Alikuwa Moto wa Kuotea Mbali Uzuri Wake Ulimdatisha Kila Mtu Kiasi Akaapa Hata Olewa na Alikusanyia Mali nyingi sana kutoka kwa Wanaume Wakware..Sasa yupo na Miaka 42 anajuta kwa upweke alionao Japo Anakila Kitu plus Majumba Hakuna anaye mtaka nae zaidi ya vijana Kumchezea na Kusepa.

It is easy to say "i want to be single lady" but it is very difficult to maintain singlelism

Nimeacha Poda na Sijarogwa na Diamond na Ninamkubali Kinoma- Q Chillah

$
0
0
Msanii wa Bongo fleva aliyetamba na hits Song kibao Q chillah amefunguka na kusema kuwa ameacha kweli kutumia madawa ya kulevya na kamwe hawezi kurudia tena maana madawa hayo yalimfanya kuwa na maisha ya ajabu,kama kuona kila mtu ni adui yake,kutokuwa na amani Q Chillah amefunguka hayo leo alipokuwa akichat Live katika ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachofanywa kila siku ya Jumatano kuanzia saa sita mchana.
Q Chillah amesema toka ameeacha kutumia madawa hayo ya kulevya kwa sasa ni mwaka wa tatu hivyo anawashauri vijana kutojaribu wala kushawishika kuingia katika matumizi ya dawa za kulevya hivyo wanapaswa kujitambua na kutambua dhamani yao kama vijana na kujua kuwa taifa linawategemea hivyo wakiingia katika matumizi ya dawa za kulevya watashindwa kutimiza ndoto zao nyingi na kuharibikiwa kimaisha.
Mbali na kuzungumzia juu ya matumiz ya dawa za kulevya pia Q Chillah ameweka wazi mikakati yake ya kurudi tena katika game la Bongo Fleva na kuweza kushika hatamu katika muziki huo kutokana na uwezo wake katika muziki,hivyo amenza kwa kuachia wimbo wake mpya alioufanya na msanii Mb dogy,wimbo huo ambao leo umetambulishwa katika kipindi cha Power Jams ya East Africa Radio unakwenda kwa jina la Nipende Nikupende.
Ni kweli nilikuwa kimya katika muziki kutokana na matatizo ya hapa na pale hivyo sikuacha muziki bali nilianguka kimuziki lakini leo ndio nimerudi rasmi katika game na nimetambulisha wimbo mpya niliofanya na Mb Dogy hivyo mashabiki zangu kaeni mkao wa kula sasa.
SIJAROGWA NA DIAMOND ILA NAMKUBALI
Q Chillah amefunguka na kusema kuwa baadhi ya vyombo vya habari na waandishi walimkariri vibaya ila hajarogwa na msanii yoyote yule na nyota ya msanii Diamond kwa sasa imewaka kwake ndio maana anafanya vizuri maana mwenyezi mungu ndiye kamfungulia njia ya yeye kuweza kuwika na kufanya vizuri kwa sasa na hakuna uchawi kama amabvyo baadhi ya watu wanavyosema.
"Hapana sikweli Diamond hanirogi bali Mungu kamfungulia njia na daima nitasapoti kazi za wenzangu,tukumbuke kuwa mchawi Mungu binaadam njia tu namkubali Diamond kama ambavyo watu wenginewanavyomkubali"
Baadhi ya waandishi wa habari wamekurupuka na hizo habari ila mimi siamini saaana nyota,naamini katika uwezo wa mtu sababu bila uwezo binafsi nyota haiwezi onekana hata kidogo,hivyo hata Diamond ameonyesha uwezo wake binafsi ndio maana ameweza kufungua njia na kufika mbele zaidi kimuziki ila siamini uchawi namwamini mungu.

Mwanaridha Kilema Oscar Pistorius Aponea Kwenda Jela , Jaji Asema Hana Kesi ya Kuua Kwa Kukusudia

$
0
0
Hatimaye Jaji Thokozile Masipa ametoa maamuzi juu ya kesi iliyokuwa inamkabili mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius na kutupilia mbali madai kuwa aliua kwa kukusudia.

Baada ya muda mrefu na mgumu wa muenendo wa kesi hiyo, jaji huyo ameamuru kuwa Pistorious hana hatia katika mashtaka yote yaliyokuwa yanamkabili.

Jaji Masipa ameeleza kuwa upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha kuwa Oscar alimuua mpenzi wake kwa kukusudia baada ya kuwepo ugomvi kati yao.

Hata hivyo, jaji Masipa ameeleza kuwa ameridhishwa na maelezo ya upande wa mashitaka kuwa Oscar Pistorius alikuwa na uwezo wa kutambua mabaya na mema wakati wa tukio hilo.

Huenda mwanariadha huyo akafunguliwa shitaka la kuua bila kukusudia baada ya kuwavuka mashitaka yaliyowasilishwa mahakamani hapo.

Oscar Pistorius alimuua kwa kumpiga risasi mpenzi wake Reeva Steenkamp katika siku ya wapendanao mwaka 2013. Lakini katika utetezi wake aliiambia mahakama kuwa alimpiga risasi kimakosa akidhani ni mtu aliyevamia katika nyumba yao usiku ule.

Kuvaa Shanga Miguu au Vikuku Kwa Mwanamke Kuna Maana Yoyote Mbaya?

$
0
0
Kumekuwa na tetesi nyingi kuhusu urembo huu wa kuvaa cheni za miguuni. Wengi wamekuwa wakisema kuwa cheni hizo zinamaanisha kwamba mvaaji anaonyesha kwamba yeye anaweza mapenzi ya kinyume na maumbile, au analika pande zote tetesi hizi zimeleta mchanganyiko kidogo kwenye urembo huu.

Watu wengine wamediriki hata kukataza kabisa wapenzi wao wasivae urembo huo, mimi binafsi siwezi kuongozana na mtu amevaa kitu kama hicho. Haya sasa kazi kwako mdau, wewe unaonaje ni sawa urembo huo kutumika, na je mwenza wako akivaa urembo huo, utaafiki?

PICHA: Mkazi wa Ilemela jijini Mwanza Ajitundika mtini na Kujinyonga

$
0
0

Mwanaume  mmoja  mkazi  wa  Kiseke, Ilemela  jijini  Mwanza  amekutwa  amekufa  baada ya  kujinyonga  kwa  kamba  juu  ya  mti  huku  mwili  wake  ukiwa  umeharibika  vibaya  na  kuvuja  maji….

Inakadiriwa  kuwa  mtu  huyo  alijinyonga  siku  tatu  zilizopita  na  chanzo  cha  kifo  hicho  bado  hakijafahamika  kutokana  na  mtu  huyo  kutoaacha  ujumbe  wowote  huku  wakazi  wa  eneo  hilo  wakishindwa  kumtambua  vizuri  kutokana  na  mwili  wake  kuharibika.

Kutokana  na  hali  hiyo, maafisa  wa  jeshi  la  polisi  waliokuwepo  eneo  la  tukio  waliamuru  mwili  huo  uzikwe  baada  ya  uchunguzi  wa  awali  wa  daktari  aliyekuwepo  eneo  la  tukio

Mke Wa Mtu Atia Aibu baada ya Kusaula nguo Zote mbele ya Watoto Wakati akicheza Ngoma za Vigodoro

$
0
0
Wakati serikali ikipiga marufuku disko la mitaani maarufu kwa jina la ‘Vigodoro’ bado kuna baadhi ya mikoa inapuuza agizo hilo ambapo mwanamke mmoja ambaye mumewe anafanya kazi kwenye mgahawa uliopo ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Morogoro, aliyetajwa kwa jina la Mama Abdul (pichani), amejitoa fahamu kupitia Kigodoro na kujikuta akisaula nguo hadharani.

Tukio hilo lililoshuhudiwa na Udaku Specially lilijiri juzikati, majira ya mchana kwenye kigodoro mbele ya watoto waliopokea ekaristi takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Monica lililopo maeneo ya Kihonda mkoani hapa.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images