Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Mfungwa Apatikana na Simu Mwilini Kenya, Aliziingiza Kupitia Sehemu Nyeti ya Nyuma

$
0
0
Mfungwa mmoja nchini Kenya amewaacha wengi vinywa wazi, baada ya simu tatu za mkononi kutolewa mwilini mwake. Inaarifia aliziingiza simu hizo mwilini mwake kupitia sehemu yake nyeti ya nyuma.
Mfungwa huyo wa gereza la King'ong'o katika jimbo la Nyeri alifanyiwa upasuaji Jumanne kutolewa simu hizo ambazo alikuwa amezificha mwilini mwake kupitia sehemu yake ya nyuma.
Mfungwa ambaye alitolewa simu mwilini kwa kufanyiwa upasuaji
Tatizo la kuingiza bidhaa kimagendo ndani ya magereza ni kero kubwa kwa maafisa wakuu wa magereza.

Wamekuwa kwa miaka mingi wakijaribu kulikomesha tatizo hilo bila mafanikio.Kwa njia yoyote ile wafungwa huingiza bidhaa kama simu katika magereza nchini Kenya kinyume na sheria za magereza.

Maafisa wa magereza wanakiri kwamba wafungwa hawa wakati mwingine hushirikiana na walinzi wa magereza kuingiza bidhaa katika magereza kimagendo.

Wema: Kipilipili Kichwani Kwangu Kinanifanya Ninunue Mawigi

$
0
0
WEMA Sepetu ‘Beatiful Onyinye’ au Madam nyota katika tasnia ya filamu Bongo ametoa siri yake kuwa ni mteja mzuri wa mawigi badala ya kufuga nywele kama vile warembo wengine kutokana na kuwa na nywele za kipilipili.

Staa huyo anasema kuwa amejaribu sana kuzihudumia nywele zale hizo lakini mara nyingi hukatika, hivyo akaamua kunyoa kipara.

“Mara nyingi nikitengeneza nywele ni wiki moja tu nazitoa, siwezi kukaa na nywele muda mrefu kichwani kwangu, nilikuwa napenda kusuka au kutengeneza nywele zangu za asili, lakini sina nywele nzuri zangu ni kipilipili ndio maana natumia sana mawigi,”anasema Wema.

Wema anasema kuwa aliamua kuwa mfuasi wa mawigi baada ya pale alipokuwa akisuka nywele zake kukatika katika na kutumia muda mwingi kuzitibia bila mafanikio na yeye kujigundua kuwa hana nywele ndefu za asili pamoja kama angeamua kutengeneza haikuwezekana.

Irene Paul Aichana Bongo Movie ‘Steve Nyerere Hana Sifa za Kuwa Kiongozi wa Wasani'

$
0
0
UWEZI kuamini! Staa na mtayarishaji wa filamu za Kibongo, Irene Paul amejitoa mhanga na kuanika uozo wa Kundi la Bongo Movie Unity bila woga baada ya kusema halina faida yoyote kwa wasanii wanaounda kundi zaidi ya kuwanufaisha viongozi wake ambao wanalitumia kwa masilahi yao binafsi.

Akiweka woga pembeni tena bila ya kupepesa macho, Irene alisema Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ hana sifa za kuwa kiongozi wa wasanii.

“Nyumba ni baba mwenye busara kwa familia yake na anayemudu kuongoza familia yake, lakini mnakuwaje na kiongozi anayegawa watu kama Steve!

“Anaweza kukununia bila hata sababu, hayo na mengine ya ufisadi wa michango mbalimbali siwezi kuyaongelea, lakini ukweli Bongo Movie haina kiongozi,”anasema Irene.

Jitihada za kumtafuta Steve Nyerere kujibu tuhuma hizi hazikuzaa matunda baada ya kutopokea simu pamoja na kwamba ilikuwa ikiita.

Hata baada ya kupigiwa zaidi ya mara nne, Steve hakupokea simu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno (sms) hakujibu.

Dokii Afichua Siri ya Vigogo Kuwakwepa Mastaa wa Kike Bongo, Skendo Chafu zatajwa

$
0
0
UMMY Wencelaus ‘Dokii’ ametoa maneno mazito ambayo wasanii wa kike wanatakiwa kuyasikiliza kwa umakini mkubwa.

Dokii ambaye ni msanii wa kike anayeonekana kuwa karibu na baadhi ya wanasiasa, alisema viongozi wengi wa kubwa wa serikali ya Tanzania wanaogoa kuwa karibu na waigizaji wengi wa kike kutokana na kuandamwa na kashifa kila kukicha.

Msanii huyo aliongeza kuwa yeye anaweza kuwa karibu na vigogo hao kwa kuwa anajiheshimu na kuheshimu sanaa yake.

“Kati ya wasanii wa kike kumi bora wa Tanzania hakuna mwenye uwezo wa kuomba ahadi ya kuonana na mheshimiwa na kukubaliwa huwezi kumpata hata mmoja kwa sababu wamechafuka kwa kashifa,”anasema Dokii.

Dokii anasema kuwa yeye yupo tofauti na wasanii wenzake kwani anatumia umaarufu wake kufanya biashara na si kutumia mwili wake vibaya kitu kinachowaharibia baadhi ya wasanii wa kike wa Bongo movie.

Baada ya kugundua hilo, Dokii anatoa somo kwa wasanii wa kike hususan chipukizi ambao wanataka kujiunga na sanaa waangalie kazi na siyo mapenzi.

Jaji Warioba: Bunge lisitishwe Katiba Mpya Haiwezi Patikana Ndani ya Wiki Mbili zilizobakia

$
0
0
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amesema ni vyema Bunge Maalumu la Katiba likasitishwa kwani Katiba bora haiwezi kupatikana kwa muda wa wiki mbili.

Kauli hiyo ya Jaji Warioba imekuja siku moja baada ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kumtaka Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, kulisitisha, huku mwenyewe akisema litaendelea na hadi kufikia Oktoba 4 Katiba inayopendekezwa itapatikana.

Jaji Warioba alieleza kushangazwa kwa haraka waliyokuwanayo wajumbe wa Bunge hilo 

wakati wanajua kuwa Katiba haiwezi kupatikana kwa muda uliobaki.

Alisema wiki mbili au tatu zilizobaki ni chache mno na kwamba Katiba mpya haiwezi kupatikana, hivyo ni vyema sasa busara ikatumika kulisitisha.

“Mimi sizungumzii kauli ya Ukawa, lakini natoa maoni yangu kwamba sidhani kama watamaliza kwa kipindi hiki kifupi, kuna mambo hawawezi kupata kwa muda huu mfupi.

“Ninachotaka watumie tu busara waliahirishe… sijui haraka yao hii ni ya nini. Kwanini wanashindwa kuelewa kuwa Katiba ni suala la maridhiano?” alihoji Jaji Warioba.

Mainda: Japo Nimeokoka Kwa Sasa ila Mkorogo ilikuwa Ngumu Kuacha

$
0
0
STAA wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amefunguka kuwa miongoni mwa vitu vilivyokuwa vimeuteka ujana wake ni pamoja na matumizi ya mkorogo ambapo ilikuwa vigumu kuacha baada ya kuokoka.

Akipiga stori na paparazi wetu, Mainda alisema kutokana na starehe za ujana pamoja na kutaka kuonekana mrembo, alitumia vipodozi hatari bila kujua kwamba vina madhara makubwa mwilini mwake.
 “Kusema kweli niliamini mkorogo ni kitu ambacho kingeniongezea mvuto kwa kiasi kikubwa, bila kujua kuwa nilikuwa najisababishia madhara mwilini.

Pia nilikuwa nafanya kitu kisichompendeza Mungu, katika kujitakasa na maovu yangu kwa Bwana ndiyo maana nikaamua kuacha kabisa kujichubua japo haikuwa rahisi,” alisema Mainda.

Wema Sepetu, Diamond, Aunt na Kajala Watajwa Kwenye Michepuko Hatari, Steve Nyerere Aanika Aibu yao

$
0
0
Stori: Shakoor Jongo
Ni tamaa ya ngono au ni nini? Hivyo ndivyo unavyoweza kujiuliza baada ya kubainika kwamba mastaa watatu Bongo, Wema Isaac Sepetu, mpenzi wake Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Aunt Ezekiel Grayson wanatajwa kwenye mchepuko hatari wa kuzungukana kimalovee, Ijumaa lina kila sababu ya kukujuza.

KILA KUKICHA
Ishu hiyo imebumburuka baada ya hivi karibuni mastaa kutengeneza vichwa vya habari kila kukicha kuhusiana na mambo yao hayo.

AUNT NA MOZE IYOBO
Duru za kihabari zinaonesha kwamba hivi karibuni mwigizaji Aunt, bila ya kupepesa macho huku akijua dhahiri kuwa ni mke wa mtu, Sunday Demonte alifungua kinywa na kuapa kuwa hawezi kuachana na mume wa mtu, Moses Peter Iyobo ‘Moze Iyobo’ ambaye ni densa wa Diamond.
Aunt alitamka maneno hayo akijua fika kuwa Moze Iyobo ni mume wa mwanamke aitwaye Mwengy ambapo wanaishi Mbagala jijini Dar, wakiwa wamejaliwa mtoto mmoja.

AUNT KIOO CHA JAMII?
“Dah! Natambua kuwa msanii ni kioo cha jamii lakini si kwa Aunt, hana hadhi ya kuitwa kioo cha jamii kutokana na tabia yake ya kuchepuka wakati ni mwanandoa,” alidai mmoja wa watu wake wa karibu.

Mdau mwingine wa sanaa za nyumbani aliyejitambulisha kwa jina la Said, mkazi wa Mwananyamala jijini Dar, alimshangaa Aunt kukiri hadharani kuwa ana uhusiano usiofaa na Moze Iyobo ambaye ni shemeji wa Wema kwa Diamond na yeye (Aunt) ni shosti wa Wema.

Alisema kwamba, kwa hadhi yake, Aunt hakupaswa kutoa kauli hiyo ili watu waendelee na minong’ono kuhusiana na yeye (Aunt) tofauti na alivyofunguka bila aibu ukizingatia ni mke wa mtu.
“Unajua kwa nini nasema Aunt anajidhalilisha au anawadhalilisha wanawake wenzake ni pale anapokiri kuwa ndoa yake ipo tena bado anampenda mumewe huku anakuja kusema kuwa anampenda Moze Iyobo, huo kama siyo mchepuko ni nini?” alihoji Said.

AUNT AWA MBOGO
Baada ya Steve kutoa dukuduku lake mwigizaji huyo aligeuka mbogo na kumwambia Steve kuwa amuache kwa raha zake kwani anampenda Moze Iyobo hata aseme nini hawezi kumuacha.
“Hata uongee nini Steve, siwezi kumuacha mpenzi wangu, nampenda sana na hayo masharti unayoyasema kuwa ameyatoa Diamond unayajua wewe, niachie nile raha zangu na Moze wangu,” alisema Aunt akimwangushia Moze Iyobo bonge la ‘kisi’.

KUTOKA IJUMAA
Ni kweli wasanii ni kioo cha jamii lakini kwa kuwa wamekuwa ‘vichwa ngumu’ kutenda yale yanayowafanya kuwa vioo vya jamii ni vema jamii yenyewe ikachuja mema na kuyachukua kisha kuwaacha wabaki na hayo machafu yao.

WEMA NA DIAMOND
Uchunguzi ulionesha kwamba, huku wakijua kila kitu waliwaruhusu Ahmed Hashim ‘Petit Man’ (Toto ya Wema) na Esma Platnumz ‘kuchepuka’ huku Petit akiwa ni shemeji wa Diamond kwa Wema.
Pia Diamond alifanya ‘misteki’ kumuacha mdogo wake, Esma ‘kuruka’ na Petit kwa kuwa ni shemeji yake.

KAJALA ANAINGIAJE?
Ilibainika pia kwamba Petit aliwahi kuchepuka na mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’ ambaye ni mke wa mtu, Faraji Agostino aliyeko gerezani na hilo likiwa wazi hata kwa hao akina Wema na Diamond.
“Hebu jaribu kuangalia huo mzunguko na mkanganyiko uliopo hapo. Yaani ni aibu tosha,” alisema mdau mwingine kuhusiana na ishu hiyo.
STEVE NYERERE AANIKA AIBU YAO
Hivi karibuni kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar, Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ aliwavaa mastaa hao na kuanika aibu yao huku akimshutumu Aunt ambaye alifika maeneo hayo akiwa ameongozana na mpenzi wake huyo wa sasa, Moze Iyobo.
Steve alisikika akimwambia Aunt kuwa hamtendei haki Moze Iyobo na anamnyima uhuru mkubwa kutokana na umri wake ambao anaweza hata kumzaa.

“Unajua wewe Aunt unastahili kuwa na mtoto mkubwa mwenye umri usiokuwa tofauti na huyu Moze Iyobo.“Hivi kwa nini unajidhalilisha kiasi hicho kwani wazee wenzako hujawaona hadi kumbemenda mtoto wa watu?” alisika Steve akimpasha Aunt kwa sauti ya juu.

NI SHARTI LA DIAMOND KWA WEMA
Akiendelea kumpasha Aunt, jamaa huyo alikwenda mbali zaidi pale alipomwambia Aunt kwamba anahisi kuwa uhusiano wake na Moze Iyobo ni sharti kutoka kwa Diamond kumpa Wema ili alifanyie kazi na kumwambia kuwa ahakikishe yeye (Aunt) anakuwa na Moze na Petit Man amuoe Esma.

“Unajua hivi karibuni baada ya Diamond kuandika yale maneno katika Mtandao  wa Instagram, nilisikia waliachana sasa naona Diamond alimwambia Wema kama unataka nikurudie ahakikishe kuwa wewe Aunt unakuwa na huyu mtoto (Moze Iyobo) halafu yule dogo mwenye rasta sijui mnamuita Petit Man ahakikishe anamuoa Esma dada yake Diamond,” alisema Steve.
GPL

Wadada Tuweni Makini Sana na Vyumba vya Kujaribia Nguo Madukani, Huyu Alipigwa Picha Bila Kujua Akijaribu Nguo

$
0
0


Wadada Tuweni Makini Sana na Vyumba vya Kujaribia Nguo Madukani, Huyu Alipigwa Picha Bila Kujua Akijaribu Nguo Dukani , Udaku Specially tumepewa siri kuwa huwa kuna kamera za siri zinafichwa kwa baadhi ya Maduka yenye tabia mbaya na kuchukua picha kwa siri..So kuweni Makini Wakina Dada

Niko Out na Mrembo Mmoja Mkali Kavaa Vikuku Miguu Yote Miwili..Inamaanisha Nini?

$
0
0
Wadau hapa niko out na mrembo mmoja tulikutana facebook miezi miwili hivi imepita leo ndio tumeonana live tupo chobingo moja hivi siri yangu tunapata moja moja, kaja  amenivalia kimini na chini amevaa vikuku ama vicheni miguu yote miwili ...eti huwa zina ashiria au kumanisha nini? Huku mtaani midume huwa tuna danganyana sana juu ya hii kitu Wengine husema ukimuona anazo pande zote huyo antoa kotekote, Ebu tupeni ukweli wana dada au ni urembo tu kama heleni....?

Mtazame Diamond Akibonga Kizungu Alipokuwa Akihojiwa na Coke Studio

$
0
0
Join Diamond Platnumz who makes a return to Coke Studio Africa Season II and Yemi Alade as they answer questions from the fans online and tell us more about their musical journey.

Jux Akana Tetesi Kuwa Wimbo Wake Mpya Amemuimbia Vanessa Mdee Ambae Inasemekana ni Wapenzi

$
0
0
Mwanamuziki wa Bongo Flava Jux Amezikana Tetesi kuwa Wimbo wake Mpya 'Sisikii' amemuimbia Vanessa Mdee ambae inasemekana kwa sasa ni Wapenzi ,
Jux Ameambia Udaku Special kuwa Nyimbo zake zote alizowahi kuzitoa sio maalum kwa ajili ya mtu bali amezitunga tu na hazihusiani na Maisha yake,
Ikumbukwe pia wimbo Nitasubiri kulikuwa na Tetesi kuwa Amemuandikia Jack Cliff ambae yupo Jela Huko Makau China

Mike Tyson amporomoshea matusi mtangazaji wa kipindi cha TV kilichoruka LIVE

$
0
0
Bingwa wa zamani wa dunia katika mchezo wa masumbwi Mike Tyson alishindwa kuvumilia swali aliloulizwa na mtangazaji wa Canada wa kipindi cha Television kilichokuwa kinaruka Live na kumporomeshea matusi mfululizo.

Mtangazaji huyo, Nathan Downer alikuwa akifanya mahojiano na Mike na alikuwa kwenye kipengele kuhusu mkutano wake na mgombea wa kiti cha Mayor, Rob Ford anaemuunga mkono.

Baada ya maswali mawili matatu, mtangazaji huyo alimuuliza Mike Tyson swali kuhusu sakata lake la kufungwa kwa kosa la ubakaji na hapo ndipo mambo yalipobadilika.

“Baadhi ya wakosoaji wako wanaweza kusema, ‘hizi ni mbio za kuwania kiti cha mayor, tunajua wewe ni mfungwa wa kesi ya ubakaji, hii inaweza kuiumiza kampeni yake (Rob Ford). Utalijibu vipi hilo?” Aliuliza Downer.

Kwanza Tyson alianza kwa kumwambia kuwa hamjui mtu mwingine anaesema hivyo na kwamba amemsikia yeye peke yake akisema hivyo.

“It’s so interesting because you come across as a nice guy but you’re really a piece of shit…“F*ck you.” Alisikika Tyson.

Baada ya sekunde chache aliongeza tena kwa msisitizo hata baada ya kukumbushwa kuwa yuko kwenye kipindi kinachoruka moja kwa moja, “No because you’re a piece a shit, you really are. F*ck you.”
Mtangazaji alijitahidi kuyapotezea yaliyotokea na kuendelea na maswali mengine lakini mambo hayakuwa sawa kabisa.

Baada ya mahojiano hayo, Downer alitweet kuwaomba radhi watazamaji na kwamba kwa upande wake binafsi hana tatizo na alichofanya Tyson.

“No ill will toward Mike Tyson. He lashed out at me and that's okay. Not taking it personally.” Alitweet.

“I'm okay everybody. Unfortuantlely my question hurt Mike Tyson's feelings. That was not my intentions. My apolgies for the language” Inasomeka tweet nyingine ya Downer.

Tyson yuko Canada kwa ajili ya kufanya onesho lake la ‘Mike Tyson: Undisputed Truth’.

Tapeli Anaetumia Jina la Director Adam JUMA Kutapeli Watu

$
0
0
Baada ya kupata email kutoka kwa Director Adam Juma ambae ni friend na tunafahamiana kuwa ni muhimu sana, ikabidi kuamua kuijibu instantly kuona ni tatizo gani naweza kumsaidia lakini e mail iliyofuata ambayo sio kawaida ya ADAM kabisa ni kama ifuatavyo…….

Thanks for your reply, am in Istanbul,Turkey right now for a short business trip and am short of cash right here, i tried to access my account from the cash machines here and its not working, i went to the bank to withdraw and was informed that i cant withdraw from my account in some countries, am wondering if i could get a quick loan of $2,950 USD from you or anything you can afford to loan me to clear my Hotel bills here and also take a cab to the airport i promise to refund it as soon as i get back home. Please i have limited access and time here and you are the only help i have. Any amount at the moment will go a long way if not all. Let me know what you can do so I can tell you how to get the money to me.

Waiting to read from you.


Adam M Juma

Producer / Director
Visual lab: Next Level
——————————–

mob: +255753074823

e-mail: mtupah@yahoo.com

Huu ni utapeli wa hali ya juu sababu niliweza kuwasiliana na Mr Juma himself na kusema kuwa e mail accoubt yake imekuwa “Hacked” kwa hiyo wewe rafiki au fan wa Director/Producer Adam Juma kuwa makini sana na Tapeli huyu maana hautakuwa unamsaidia Adam ila unamfaidisha Cyber Tapeli.

Ex-Wife wa Prezzo Afunguka kuhusu Prezzo, Kumbe Prezzo si Lolote wala Chochote, Jisomee Hapa

$
0
0
Mwanamama mmoja ajulikanaye kama DAISY KIPLAGAT ambae amejitambulisha kuwa yeye ni Baby Mama wa rapper kutoka nchini Kenya Prezidaa PREZZO, aliingia kwenye group hilo na kuanza kumwaga radhi kuhusiana na msanii huyo kuwa hana ushirikiano kabisa katika kulea mtoto ambae amezaa na mwanamama huyo. Daisy aliongeza kuwa hataki chochote kutoka kwa rapper huyo ila kinachomboa ni pale jinsi msanii huyo ambae hajawasiliana na mtoto wao huyo wa kike tokea akiwa na miaka 2 lakini anaendelea kujitamba kuwa ana mtoto wakati hajawahi kutoa hata senti moja kusaidia kulea mtoto huyo.

“He goes around on TV and since he is able to hold a mic or have fake written interviews he is always claiming to be taking his daughter to the best school in Kenya and that she is her princess spoils her rotten. He has never paid her fees never paid any dime for her up keep all this is my sweat and my blessed parents and family support. I don’t need to communicate with him but I wanted to have this space to let you all know that this guy instead chooses to go around with women and lie to them how rich he is and yet he doesn’t have anything and stays at his mum’s house. So when you all hear how he does and loves his daughter please don’t be fooled,” – Daisy Kiplagat.


Steve Nyerere ajiuzulu uenyekiti Bongo Movies, Majungu na Kupigwa Vita na Wenzake Vyachangia

$
0
0
Muigizaji wa filamu za Kiswahili, Steve Nyerere aliyekuwa mwenyekiti wa Bongo Movies ameamua kujiuzulu nafasi hiyo.

Steve ameeleza uamuzi wake kupitia Instagram bila kutoa sababu zilizopelekea kujiuzulu kwake.

“Napenda kuwashkulu ndugu zangu wote wasaniii wenzangu kaka zangu mama zangu rafiki zangu mimi pamoja na family yangu nimeamua kujiuzuru uongozi wa bongo move nabaki kuwa mwanachama wa kawaida naimani tulifurahi pamoja tukauzunika pamoja na daima tutakuwa pamoja.”

Uamuzi wa Steve Nyerere umepokelewa kwa hisia tofauti na wapenzi wa filamu za kitanzania ambao wengine wamemtaka kutofanya hivyo huku wakitaja ‘majungu’ na kusemwa kama chanzo cha yote.

“Khaaaaaaa asa @stevenyerere2 kujihuzur sio suluhisho la tatizo kaanza willy umefata ww sasa c kamat nzima itajiuzur!?? Why mnashindwa kukaa km wasanii mkasuluhisha penye makosa mambo yakaendelea? Majungu yapo kila sehem kusemwa kupo kila sehem @stevenyerere2 mnapoelekea bongomovie kila mtu atakaa mwenyewe wallah.” Ameandika shabiki anaetumia jina la Neyjd.

Oscar Pistorius Akutwa na Hatia ya Kuua Bila Kukusudia

$
0
0
Mwanariadha Oscar Pistorius amekutwa na hatia ya kuumuua bila kukusudia mpenzi wake Reeva Steenkamp ikiwa ni siku moja baada ya kutopatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia.

Akisoma hukumu ya Oscar muda mfupi uliopita, Jaji Thokozile Masipa ameeleza kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa aliua kwa kukusudia.

Mahakama imemkuta na hatia pia katika kesi ya kutumia silaha vibaya.

Kutokana na kukutwa na hatia hiyo, Pistorius anaweza kukabiliwa na kifungo cha hadi miaka 15 jela.

Hata hivyo hukumu ya idadi ya miaka ya kifungo hicho inategemea sana maamuzi ya Jaji kutokana na sababu na utetezi wa mtuhumiwa.  

Bado hakimu anaendelea kusoma hukumu ya Oscar Pistorius huku dunia ikishuhudia moja kwa moja kwenye runinga muenendo wa kesi hiyo.

Queen Darleen Akanusha Kumtafutia Mademu Diamond

$
0
0
Queen Darleen amekanusha tuhuma kuwa ana mtindo wa kumtafutia mademu kaka yake Diamond Platnumz.

Queen amesema kwa heshima aliyonayo kwake, sio rahisi kumpa kazi hiyo.

“Unajua Naseeb miye ananiheshimu sana hata akiwa na wenzake kama alikuwa anaongea ujinga nikiwepo haongei kwakuwa anajua miye ni mkubwa wake,” Queen ameiambia Bongo5. “Na pia naweza kukaa hata miezi mitatu hatujaonana sasa nashangaa naambiwa namtafutia wanawake. Anajua sasa hivi yeye yupo juu na anafanya vizuri kwahiyo watu wanaongea tu vitu ambavyo hawavielewi. Siwezi kufanya hivyo hata siku moja kwani yeye ana maisha yake na uhuru wake na miye pia hivyo hivyo. Basi nisiwe na marafiki wazuri nitaambiwa namuunganishia mdogo wangu! Kwahiyo niwe sasa na marafiki vijuso sasa? Lazima watu wajue kuwa Diamond ni mdogo sana kwangu na tunaheshimiana sana siwezi kumpangia masuala ya mahusiano miye yeyote nitakayeletewa na yeye kwangu sawa ili mradi kampenda mwenyewe mie sina tatizo,” ameongeza.

Kwa upande mwingine muimbaji huyo amesema anatarajia kutoa wimbo aliomshirikisha mdogo wake huyo.

“Nipo busy sana na kazi zingine si unajua tena ila mashabiki wangu wasijali natoa wimbo mpya soon ambao nimemshirikisha mdogo wangu Naseeb aka Diamond Platnumz. Wimbo umefanyika kwa Tudd Thomas. Jina la wimbo bado sijajua. Sitowaangusha mashabiki wangu kama kawaida.”

Halima Mdee Ashinda Kwa Kishindo Kiti cha Mwenyekiti Mpya Bawacha

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Kawe Mheshimiwa Halima James Mdee, ameshinda kiti cha Uenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) baada ya kupata kura 165 huku mtu aliyemfuatia kwa karibu akipata kura 35. Akiongea na ITV mara baada ya kupata matokeo hayo, mbunge huyo amesema matokeo hayo yamedhihirisha ni kwa jinsi gani anakubalika kwa wakinamama ndani ya chama hicho.

Taarifa ya Kuungua Tena Kwa Mara ya Pili Msikiti wa Mtambani wa Dar es salaam

$
0
0
Hii ni mara ya pili kutokea hitilafu ya umeme ambayo imesababisha moto kwenye msikiti wa Mtambani uliopo Kinondoni Manyanya baada ya mara ya kwanza ambapo uliungua tena August 13 mwaka huu.
Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa eneo la tukio wamesema kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme,Kikosi cha zimamoto na uokoaji kilifika na kufanikiwa kuuzima moto huo kabla haujaleta madhara zaidi.

Mtoto Aliyezamia Ndege Kutoka Dar es Salaam Mpaka Zanzibar Utata Mtupu

$
0
0
Dar es Salaam. Polisi Zanzibar wameanza uchunguzi kubaini mazingira ya safari tata ya mtoto Karine Godfrey aliyesafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar kwa ndege bila tiketi wala kugundulika.

Mtoto huyo, Karine au Jenipher Godfrey anayesoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi Jitihada, Dar es Salaam alionekana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Septemba Mosi saa 11.30 jioni, akieleza kuwa aliingia Zanzibar kwa ndege ambayo hata hivyo, haikufahamika mara moja ni ya shirika gani.

Alikutwa uwanjani hapo akijiandaa kuondoka kwenda mahali asipopajua.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis alisema mbali ya kushangazwa na mazingira ya safari ya mtoto huyo, polisi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar wanalifanyia kazi suala hilo.

“Ni jambo la kushangaza. Tunajiuliza, huyu mtoto alifikaje katika ndege bila ya kuwa na tiketi wala taarifa zozote kuelezea safari yake na je, huko Dar es Salaam aliondokaje hadi kuingia katika ndege bila ya hivyo vitu, sielewi ilikuwaje.

“Ina maana hakufanyiwa hata ukaguzi kama ilivyo kawaida kwa wasafiri. Tunalichunguza hili, huu ni uzembe wa hali ya juu ulioonyeshwa na wahusika wote wa viwanja vya ndege,” alisema.

Alivyogundulika

Kamanda Khamis alisema kuwa ilikuwa saa 11.30 jioni, mtoto huyo alipogundulika baada ya dereva wa teksi, Kassim Gharib kumwona akiwa nje ya uwanja huo kwa muda mrefu na kuanza kumhoji.

Katika mahojiano hayo, mtoto huyo alisema alishuka katika ndege kutoka Dar es Salaam na kwamba anaishi Kitunda pia, Dar es Salaam. Hata hivyo, alikataa kusema alipanda ndege ya shirika gani.

Alisema lengo la kwenda kwake Zanzibar ni kumtembelea baba yake mzazi ambaye alimtaja kwa jina moja la Godfrey na kuongeza kuwa ni askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), lakini bila ya kueleza yupo kambi gani. Baada ya hapo dereva huyo alimpeleka Kituo cha Polisi Mazizini.
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images