Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live

Dk Bashiru abadili msimamo Katiba mpya...."Siwezi Kuchambua Tena ,Mnataka Nifukuzwe?"

$
0
0
Katibu Mkuu mpya wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema msimamo wake kuhusu mabadiliko ya Katiba utakuwa tofauti na ule aliokuwa nao awali kabla ya kuingia rasmi kwenye siasa za CCM kwa kuwa sasa ataendana na maelekezo ya chama hicho.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu CCM, Dk Bashiru alionekana kuwa ni mpigania demokrasia na haki wakati akiwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, akishiriki katika midahalo na mahojiano na vituo vya redio na televisheni kuhusu mijadala ya kitaifa.

Mwaka 2014  Dk Bashiru alisema Katiba ya sasa “haiwezi kuwa medani ya muafaka wa kitaifa kwa sababu ilisimamia msingi na muafaka wa kitaifa katika chama kimoja”
 

 “Tangu mwaka 1992 wanasiasa wamekuwa wakidai Katiba mpya kwa hoja hiyo; kwamba tuko katika mazingira mapya ya kisiasa, mahitaji mpya ya kisiasa, tuna hatua mpya matarajio mapya, changamoto mpya, taratibu mpya za kuendesha nchi,” alinukuliwa  Dr Bashiru katika mahojiano enzi hizo kabla hajaingia katika siasa za CCM.

Sasa amebadili msimamo,  na msimamo wake utategemea maamuzi ya Halmashauri Kuu ya CCM.

“Leo nazungumza kama katibu mkuu, yaani swali lako lina majibu humo humo,” alisema Dk Bashiru jana alipoongea na waandishi wa habari kwenye ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijini Dar es Salaam.

“Ukiwa mchambuzi, unachambua kweli kweli. Ukiwa msemaji wa chama, unawasilisha yaliyoamuliwa kwenye vikao.

“Halmashauri Kuu ndio chombo kikuu kilichoniteua na inaweza kunifukuza. Kwenye uchambuzi kule nisingeweza kufukuzwa.

“Hapa kama wewe unanitakia mema, siwezi kuchambua yale ambayo hayajaamuliwa na vikao. Lakini jambo kubwa nchi hii kama tutaheshimu katiba za vyama vyetu na Katiba za Serikali zetu mbili zilizopo, tunaweza kuanzia hapo kujadili namna ya kurekebisha Katiba hii.”

Ferooz Afunguka Mambo Yanayomkwamisha Kuachia Muziki

$
0
0

Msanii mkongwe wa Bongo Flava, Ferooz amesema kuwa kuna wakati anatamani kuacha muziki lakini anashindwa.

Muimbaji huyo ameeleza sababu ya kutaka kufikia uamuzi huo ni kuonekana si kitu wakati ameutoa mbali muziki huo.

“Kikubwa kinachoniumiza nikiangalia game nilipolitoa mpaka lilipofika halafu bado naonekana mimi ndio nimekosea, mkosefu namba moja,” amesema.

“Game linanisahau kwa kifupi, mkapa nafikia fikra za kusema ni quit kufanya muziki, ni quit kufanya game, nitangaze nimeacha muziki. Nataka niache muziki lakini najikuta kwamba nashindwa kwa sababu imeshakuwa kwenye damu,” Ferooz ameiambia Wasafi TV.

Ameongeza kuwa licha ya kufanya muziki kwa takribani miaka 20 sasa amekuwa pia akifanya mambo mengine lakini mwisho wa siku anajikuta amesharudi kwenye muziki. Wimbo wa mwisho kutoa Ferooz unakwenda kwa jina la Najaribu.

Waziri wa Elimu Atoa Tamko Baada ya Kwaya ya Wanafunzi Kutumbuiza Utupu - VIDEO

$
0
0

Kwaya moja ya Wanafunzi wa kike nchini Afrika Kusini imezua gumzo nnchini humo baada ya wanakwaya wake kutumbuiza katika jukwaa la tamasha la EC Choral lililofanyika Jumatatu ya Mei 28, 2018.

Waziri wa Elimu nchini Afrika Kusini, Bi. Angie Motshekga

Wanafunzi hao ambao hata hivyo hawajabainika wanatoka shule gani, na mpaka sasa video yao imezua gumzo nchini humo baada ya kusambaa mitandaoni.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Dispatch limedai kuwa mwalimu wa kwaya hiyo ya wanafunzi ambaye hakujitambulisha jina lake alijivunia kuona wanafunzi hao wakienzi utamaduni na mila za kabila la  Xhosa.

“Hili ni jambo la furaha kwetu sisi kama wa Xhosa, watoto wetu wanakua katika mazingira ya kisasa hadi wanasahau tamaduni zao nadhani sasa tunarudisha utamaduni wetu wa enzi hizo unaoonekana kusahaulika,“ameeleza Mwalimu huyo.

Wasichana hao kwenye video hiyo ambao kifuani wanaonekana kuwa watupu huku kiunoni wakivalia vinguo vifupi. video yao imezua gumzo kiasi  kwamba serikali nchini kupitia Wizara ya Elimu kuingilia kati.

Waziri wa Elimu nchini Afrika Kusini, Angie Motshekga amelaani tukio hilo na kuliagiza Jeshi la Polisi nchini humo kufanya upelelezi juu ya video hiyo ili kuwabaini wahusika hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la habari la AFP.

“Huu ni udhalilishaji wa kijinsia na kinyume cha maadili ya taifa letu, hakuna makosa kupenda tamaduni wako lakini hakukuwa na umuhimu wowote kucheza wakiwa wakiwa utupu”.amesema Bi. Angie Motshekga.

Tazama video ya wanafunzi hao wakitumbuiza (video by Dispatch Live).

TANZIA: Mbunge Bashe Afiwa na Mama Yake

$
0
0

Mbunge wa Nzega, Hussein Bashe amefiwa na Mama yake Mzazi, Zainab Abdi aliyekuwa anapatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es salaam.

Bashe amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kutoa taarifa hiyo.

Ndugu zangu nimeondokewa na mama yangu mpendwa.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un

Naye, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amempa pole Mbunge huyo kwa kuandika “Inna lilah waina ilaih raajiun. Mola akupe subra ndugu yangu @HusseinBashe katika mtihani huu mkubwa wa kufiwa na mama yako mzazi.”

Zitto ameongeza kwa kuandika “Inna lilah waina ilaih raajiun. Mola akupe subra ndugu yangu Hussein Bashe katika mtihani huu mkubwa wa kufiwa na mama yako mzazi. Poleni sana Sheikh Mohammed, Ibrahim Mohamed Bashe, Abubakar, Kauthar na ndugu na jamaa huko Nzega. Tupo pamoja nanyi na Mola awape nguvu.”

Davido kusherehekea sikukuu ya Eid na Watanzania

$
0
0

Hit maker wa IF, Fall , FIA na nyingine nyingi, David Adedeji Adeleke aka Davido anatarajia kufanya show ya nguvu siku ya Sikukuu ya Eid mbele ya wakazi wa Dar es salaam kwa mujibu wa bosi wa King Solomon, Solomon Nasuma.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo, Assurance amekuwa ni mmoja kati ya wasanii wanaofanya vizuri zaidi kwa Afrika baada ya kutajwa katika kinyang’anyiro cha tuzo za BET katika kipengele cha ‘International Act’ akiwa na wakali wengine wa Afrika kama Cassper Nyovest wa South Africa, Fally Ipupa wa DRC, Tiwa Savage wa Nigeria pamoja na Kundi la Distruction Boyz kutoka Afrika Kusini.

Akiongea na wadau waliojitokeza katika uzinduzi wa wimbo ‘Sheba’ ya Kundi la The Mafik uliofanyika Club Next Door wiki hii, bosi huyo aliwataka watu waliohudhuria ukumbini hapo kukaa mkao wa kula kwaajili ya show kubwa ya Davido katikati ya mwezi huu.

Bosi huyo hakuweka wazi kama show hiyo itafanyikia katika ukumbi wa Club Next Door Masaki au katika ukumbi mkubwa ya King Solomon Hall uliopo Namanga jijini Dar es salaam.

Watanzania kwa sasa wanaisubiria kwa hamu show hiyo ya aina yake kutokana na muimbaji huyo kufanya vizuri katika show zake ambazo amekuwa akizifanya nchi mbalimbali kupitia ziara yake ya muziki ya The 30 billion African Tour.


Muimbaji huyo amekuwa na mafanikio makumbwa mwaka 2017/18 baada ya ngoma zake mbili kwa pamoja kufanya vizuri duniani, ambapo ngoma ya ‘IF’ ikifikisha mauzo ya Diamond huku ‘Fall’ ikifikisha mauzo ya Platnumz.

Mwanamke Akikujibu Hivi Achana nae Haraka Sana Ujue Hakuna Kitu Hapo....

$
0
0
Wanawake wa uswahilini wa siku hizi wamekuwa na swagger ya aina moja wanapotongozwa.utasikia "MIMI NAWAOGOPA WANAUME",ukiuliza wewe ni bikra kwani? Atajibu hapana,ukiuliza kwa nini unawaogopa wanaume wakati we sio bikra atakujibu" NISHATENDWA SANA".ndugu yangu nakushauri,kama ukijibiwa hivo basi ondoka fasta ujue hapo hakuna mwanamke kabisa,kwa sababu haiwezekani mtu atendwe yeye tu na kila mwanaume,ujue huyo ana mapungufu ambayo hata wewe hutaweza kuvumilia ,mapungufu ambayo hata wewe utamtenda tu na mwisho wa siku utamuongezea idadi ya wanaume waliomtenda.ila mara nyingi wanawake wanaojibu hivo au wanaotendwa hivo unakuta ni hawajatulia kabisa(vicheche).

Mama Diamond Amkumbuka Zari Aandika Maneno Haya Kwenye Mtandao Wake wa Kijamii

$
0
0

Stori kubwa kwa sasa ni kuhusu Zari kuonekana kwenye video ya wimbo mpya wa Diamond Iyena – Baadhi ya mashabiki wamefurahia hilo lakini wengine wameonekana kukereka.

Sasa kubwa zaidi Mama mzazi wa Diamond, Bi Sandrah kupitia mtandao wa Instagram ameweka picha ya Zari na kuandika ujumbe wa kumsifia zaidi.

“Mama Latiffah mwenye…#IYENA yake Mwanamke usafi gaga kulisugua Mume akirudi sharti viatu kumvua… @diamondplatnumz ft @rayvanny,” ameandika Bi. Sandra kwenye mtandao huo.

Naye Esma Platnumz amemjibu mama yake kwa kucomment kwenye picha hiyo kwa kuandika, “Heee kwenye USAFI SASA mama TEE NAMPONGEZA wallah dada msafi huyu Kwenye Mapishi @wemasepetu unanikomeshaga.”

Video ya wimbo huo wa Iyena, indaiwa umefanyika kati ya mwezi Juni hadi Sepetemba mwaka jana.

Jacqueline Wolper Aibua Mapya, Adai Harmonize Bado Anampenda

$
0
0

Msanii wa filamu, Bongo Jacqueline Wolper ametaja sababu zilizopelekea ex-boyfriend wake, Harmozie kutaja orodha wa wanaume 11 ambao alidai waliwahi kutoka kimapenzi na mrembo huyo.

Muigizaji huyo akizungumza akiwa nchini Kenya na Kiss FM amesema kuwa kilichopelekea Harmonize kufanya hivyo ni maumivu ya mapenzi.

“Binafsi sikuchukia wala sikukasirika kwa sababu niliona amepaniki, you know a guy love me a lot, kwa hiyo niliona amepaniki tu na ni maumivu ya mapenzi na sikumshangaa,” amesema Wolper.

Utakumbuka usiku wa kuamkia May 8, 2018 ndipo Harmonize alitoa orodha hiyo, ni baada ya Wolper kwenye moja ya interview kudai kuwa mpenzi wa Harmonize wa sasa, Sarah ni mlezi wa wana.

Mmiliki wa Jamii Forum Aachiwa Huru na Mahakama

$
0
0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa Jamii Forums, MaxenceMelo na Mwanahisa wa  mtandao huo, Micke William baada ya kuwaona hawana kesi ya kujibu.

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa aliwaachia huru washtakiwa hao leo Juni 1, baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi sita wa upande wa mashtaka na kuona ushahidi huo hauna mashiko.

“Hakukuwa na ushahidi unaoeleza moja kwa moja wa barua hiyo ya kuwataka watoe taarifa za kampuni yao na ushahidi huo una mashaka?” amesema Mwambapa

Katika kesi hiyo Melo na mwenzake wanadaiwa kuzuia uchunguzi wa jeshi la polisi kwa kukataa kutoa taarifa za kampuni yao.

Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa,amedai kuwa baada ya usajili, kampuni hupewa taarifa za siri ambazo huwezesha mtu kuingia katika mtandao huo husika hivyo washtakiwa hao walikuwa na uwezo kuona taarifa kwenye mfumo wao.

Kishenyi amedai kuwa kufuatia jitihada hizo za Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum(ZCO) za kuwataka washtakiwa kutoa taarifa muhimu na wao kukataa walikamatwa na kufikishwa mahakamani.

Waathirika wa Ukimwi Wamshtaki Rais

$
0
0

Banjul, Gambia. Watu watatu walioathirika kutokana na tiba feki ya ugonjwa wa Ukimwi iliyobuniwa na rais wa zamani wa Gambia Yahya Jammeh wamefungua mashtaka wakitaka walipwe fidia hiyo ikiwa ni kesi ya kwanza dhidi yake tangu akimbilie uhamishoni.

Waathirika hao watatu walifungua kesi katika Mahakama Kuu jijini Banjul Alhamisi, ilisema taarifa ya shirika lisilo la kiserikali la AIDS-Free World lenye makao yake Marekani ambalo linawasaidia kukusanya ushahidi.

Jammeh, ambaye utawala wake wa miaka 22 katika nchi hii ndogo ya Afrika Magharibi uligubikwa na shutuma za ukiukwaji wa haki za binadamu, alikimbilia Guinea ya Ikwete mwaka jana baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu.

Ousman Sowe, Lamin Ceesay na Fatou Jatta walikuwa miongoni mwa raia wa mwanzo wa Gambia kujiunga katika programu ya matibabu dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi (HIV) na Ukimwi (AIDS) mwaka 2007 ambapo walitakiwa kuacha kutumia dawa za kufubaza makali ya ugonjwa huo badala yake wanywe dawa ya maji iliyotengenezwa nchini ambayo iliwasababisha kutapika.

 Afya za waathirika

Afya zao zilizidi kuzorota wakati wengine waliokuwa kwenye programu hiyo walifariki dunia.

“Naamini ni wajibu wangu kumwajibisha Jammeh,” alisema Sowe, mhadhiri wa zamani wa chuo kikuu mwenye umri wa miaka 60 hivi.

“Nilijua kwamba siku moja ukweli utafahamika.”

Waathirika hao walisema watu walikuwa wanaogopa kumkosoa rais alipokuwa madarakani na madaktari na wagonjwa walitangaza hadharani kwamba dawa ilikuwa inafanya kazi.

Programu ile ilizorotesha mapambano dhidi ya HIV/AIDS katika nchi ambayo inashika mkia ikilinganishwa na mataifa mengine ya Afrika katika viwango vya utoaji tiba

Source: Mwananchi
 

Benki 10 matatani kwa kupitisha fedha zilizoibwa NYS

$
0
0

Gavana wa Benki Kuu, Dk Patrick Njorog


Nairobi, Kenya. Wakati vigogo kadhaa wanashikiliwa kwa tuhuma za ufisadi, benki 10 za kibiashara zinazotuhumiwa kupitishia fedha za Mfuko wa Taifa wa Huduma ya Vijana Kenya (NYS), ziko matatani.

Hata hivyo, benki hizo zimeonyesha ukimya kuhusiana na ukwapuaji wa fedha hizo, licha ya Serikali kupitia kwa mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, George Kinoti kuzitaka kuwajibika.

Uchunguzi kuhusiana na fedha za NYS unaendelea chini ya Benki Kuu, Ofisi ya Mkurugezi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP), Huduma ya Taifa ya Upelelezi (NIS) na Mamlaka ya Mapato (KRA).

Tayari ofisi ya DCI na Benki Kuu zimeonya kuhusu madhara ambayo benki zilizotumika kuchepusha fedha hizo zinaweza kuyapata ikiwamo kufutiwa leseni za uendeshaji.

Gavana wa Benki Kuu, Dk Patrick Njoroge alisema hivi karibuni kuwa wizi wa fedha za NYS kupitia vocha za kughushi za malipo ulifanikishwa na mabenki ‘kwa makusudi’. “Ni kwa jinsi gani unaweza kufanya kosa katika mambo ambayo unayafahamu?” Alihoji Dk Njoroge.

Alhamisi, mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, George Kinoti pia alizionya benki kuacha kujificha nyuma ya uchunguzi unaoendelea. “Wanapaswa kutoka nje wakiwa wasafi kama mwongozo unavyosena na kusema iwapo taratibu zilikiukwa, lakini waambieni kwamba wamegusa namba mbaya. Sisi na CBK (Benki Kuu) tunawafuata,” alisema.

Licha onyo hilo, hakuna benki kati ya zilizotajwa iliyokuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwa kina isipokuwa Diamond Trust Bank ambayo ilisema inatimiza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na miongozo ya kibenki.

Benki ya Stanbic ilisema maofisa wake “wamefungwa na mahitaji ya kuhifadhi usiri na kwa hiyo taarifa yoyote (juu ya yale waliyofanya wakati pesa ilipoingia) yanaweza kujadiliwa na maofisa walioidhinishwa.”

Benki ya Biashara Kenya (KCB), ambayo pia inafuatiliwa ilikataa kutoa maoni juu ya masuala yoyote yanayochunguzwa ikiwa ni pamoja na yale waliyoyafanya wakati fedha za NYS zilipokwapuliwa.

“Kama unavyojua, suala hili liko chini ya uchunguzi katika mamlaka za uchunguzi na ni suala la kisheria. Kwa hiyo hatutaki kutoa maoni,” ilisema taarifa.

Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Standard Chartered Kenya, Lamin Manjang pia alikataa kutoa maelezo akisema, “hatuwezi kutoa maoni juu ya suala hilo kwa kuwa linafanyiwa uchunguzi na taasisi za Serikali zenye mamlaka.”

Vilevile, Benki ya Barclays Kenya ilisema haitaki kuathiri ubora wa mchakato wa uchunguzi ikisisitiza kuwa, “tunauchukulia kwa umakini na kwa hiyo tunashirikiana kikamilifu na taasisi za uchunguzi.”

 “Tunajua uchunguzi unaoendelea katika NYS. Jambo hili linafuatiliwa na mamlaka za Serikali. Zaidi ya hayo hatuwezi kutoa maoni juu ya jambo hilo, bado ni jambo la uchunguzi.”

Gazeti la Daily Nation, lilipeleka barua za ombi la kupata maoni katika Benki ya Equity, Benki ya Ushirika na Benki Kuu ambazo pia zimetajwa na wachunguzi, lakini wahusika hawakujibu chochote.

Hata hivyo, licha ya onyo la gavana na mkurugenzi wa upelelezi,  benki zinapaswa kuchukulia kwa tahadhari suala hilo ikizingatiwa kwamba hazitakiwi kuchunguza taarifa za wateja wao, kukamata au kuchukua fedha zao.

Vigogo washikiliwa

Vigogo watano ambao ni miongoni mwa watu 24 waliokamatwa kwa tuhuma za ufisadi wa fedha za NYS, wanashikiliwa mahabusu kutokana na amri ya mahakama.

Vigogo hao wenye nyadhifa za juu ni Lilian Omollo (katibu mkuu wa Wizara ya Vijana, Sammy Mbugua (mkaguzi mkuu katika Wizara ya Utumishi wa Umma), Micheal Ojiambo (mkurugenzi wa usimamizi katika wizara hiyo), Clement Murage (mhasibu mkuu wa zamani) na Richard Ndubai (mkurugenzi mkuu wa NYS).

Hii Hapa Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo ya Uume

$
0
0

Tatizo hili limekuwa likiwaadhiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baada ya kujiona wapo tofauti sana na wengine kwa kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi 6-8 kwanza upungufu wa vichocheo hivi huchochea ukuaji wa uume chongo ambalo hushambulia nerve ambayo uharibu kabisa ukuaji wa uume, ngiri, punyeto, ambayo huathili misuli ya uume, ngiri huleta maumivu, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, korodani moja kuvimba, kutopata choo vizuri, sababu hizi hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na mara nyingi hata nguvu za kiume ( hamu ya tendo la ndoa) hupungua na kwisha kabisa

GEMBE :Ni dawa inayozalisha na kukufanya uume kukua na kuongezeka
NGEMO : Ni dawa bora ya kuongeza nguvu za kiume

Hukutia hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi mara4 nne bila kukinai au kuchoka pia itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk30-45 kwa mtumiaji pia tunatibu kisukari, bp, ngiri, miguu kuwaka moto KAMA HUNAMDA WA KUFIKA OFISINI KWETU UTALETEWA POPOTE TUPO MBAGALA RANGI TATU

 0753471612/ 0715249530
0623 386 305

DR KUZENZA

Nina Ugonjwa wa Kupenda Wanawake Naweza Fanya lolote Nimpate Mwanamke...

$
0
0
Hili jambo kipindi cha nyuma sikuona kama ni tatizo lakini sasa naanza kuona ni tatizo. siku nimekaa nikapiga mahesabu ya idadi ya wanawake nliotembea nao ni zaidi ya 500 hao ndio ninawakumbuka. huwa nachanganyikiwa kabisa nikiona mwanamke....sijafaham kama nilirogwa au ni nini. nimetembea mikoa kama 8 hivi tanzania huko nimeacha kilio tu maana nimepiga mahesabu nina watoto wa nje mpaka sasa 17. moja ya tatizo langu kubwa huwa sipendi kabisa kutumia kinga.

naweza nikatumia kinga bao la kwanza ila ujue kuendelea hapo yaani huwa navaa natumia baaaye naichomoa ili nipige issue kavu baada ya saa moja au mawili ndo naweza kumaliza. nikivaa kinga ndo inaweza ikafika kesho. wanawake wameshanijua yaani wakitaka pesa wananionesha tu k zao..wakionesha basi naishiwa nguvu yaani hata nikiwa na hasira vipi nikioneshwa K.U basi naachanganyikiwa nakuwa kama bwege tu.

nakumbuka kuna siku moja nlikuwa na dada mmoja room kwake tunapiga story huku tunaangalia movie..mara ikaja sehem ya movie wanafanya tendo hilo la ndoa.nikajawa na hamu ile mbaya nikaanza kumuomba yule dada...yule dada alinambia hawezi nipa maana sijatulia kabisa. tena mbaya zaidi akanionesha kuwa unaiona hii....huku akifunua na kunionesha hakuwa amevaa nguo ya ndani. akanambia unaiona hii??? sikupi hata kidogo we hujatulia" siku ile nililia sana kulilia anipatie ile issue...nlilia kama masaa matatu hivi na nikamwambia yule dada achukue kadi yangu akachukue pesa zooooote zilizopo kwenye account yangu akirudi anipe... akagoma akasema kama nipo serious basi nimrushie pesa kwenye simu yake. nikaangalia kwenye account nlikuwa na 450,000. nlimrushia ndo akanipa issue. nlipomaliza ndo akili ilinirudia nlijilaumu sana maana nlimpa pesa yangu yooote. mwezi mzima niliteseka.

siku nyingine nliahirisha safari kabisa kumkimbizia dada mmoja ambaye alikuwa anaishi buguruni kwa mnyamani nlimfutatilia toka mwenge wakati mimi nlikuwa naenda mbezi.ilibidi niahirishe safari yangu nimfate mpaka kufika buguruni kwa mnyamani yule mtoto ndo akakubali tukae sehemu tule chips kuku ndo tuwekane sawa.

sasa nawaza nifanyeje jamani pamoja ya kuwa ndo udume wenyewe lakini daaaah mwenzenu napenda sana kukuchi. napenda ,napenda napenda...na nikiona nachanganyikiwa kabisa hata siwezi kufikiri vizuri.

By Brian

Mtanzania ala shavu la kuwa miongoni mwa Blogers 50 duniani walioalikwa na Russia, World Cup

$
0
0
Mwanabloger kutoka Tanzania Krantz Mwantepele kutoka blog ya Mwanaharakati Mzalendo amechaguliwa na serikali ya Russia kuwa miongoni mwa Blogers na social media influencers 50 dunia nzima kwaajili ya kutembelea nchi hiyo kabla michuano hiyo haijaanza mapema Juni 14.


Mtanzania huyo pamoja na wenzake atapara fursa ya kutembelea viwanja vyote 5 ambavyo ni Krestovsky Stadim, Fisht Olympic Stadium, Cosco Arena, pamona na Ekaterinburg Arena.z

Krant ambaye pia ni Katibu wa Tanzania Bloggers Network (TBN), alisema yeye aliomba nafasi hiyo kupitia mitandao ya kijamii baada ya kutumiwa link za marafiki zake.

“Nafurahi kuwa mmoja ya Blogers na social media influencers 50 dunia nzima kualikwa na serikali ya Urusi kufanya Coverage ya kombe la dunia na vivutio mbali mbali vya nchini humo,” alisema Krant.

Krant akikabidhiwa bendera na Mkurungezi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, Devotha Mdachi.

Aliongeza, “Nitakuwa balozi mzuri pia wa utalii wa hapa nchini kwa udhamini mkubwa wa Wonderfultanzania, Nitawakilisha vizuri huko ughaibuni Endelea kufuatilia na koncept_tv na Mwanaharakati Mzalendo Blog nitakupa exclusive zote kupitia huko,”

Mwanabloger huyo pia alipongezwa na wadau mbalimbali ikiwemo serikali pamoja na kukabidhiwa bendera ya Tanzania na Mkurungezi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, Devotha Mdachi.

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Mafupi na Upungufu wa Nguvu za Kiume? Suluhisho Hili Hapa

$
0
0

KWANINI BAADHI YA WANAUME WANA MAUMBILE MAFUPI NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME DR SITTA NDO SULULISHO LAKO tatiza, hili limekuwa likiwaasili watu wengi,sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine, kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo zipo , sababu nyingi zinazosababisha, tatizo hilo baadhi ni (i) upungufu wa vichocheo vya HORMONES ZA CETROGEN ambazo mwanaume, anapobarehe vichocheo hivi, HORMONES hizo, husaidia ukuaji wa uume 

SUPER MIZIZI, ni dawa inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi utakayo na kuzibua mlija iliysinyaa, 

NSHOLA ni dawa bora, ya kurudisha nguvu, za, kiume bari inatibu ,kabisa kutoa tatizo hilo, na kukupa , hamu ya , kurudia tendo, la ndoa zaidi, ya mala nne 4 ,bila kuchoka atakama unaumli ,wa mika 80,! pia ana ,dawa za ,kutibu, presha ya kupanda ,na kushuka, kisukari kuondoa, mafuta , mwilini ,na maumivu ya, mgogo kiuno, dawa zipo, matazo, ya hedhi, kwa ,wanawake hedhi, zisizokuwa na, mpangilio, na kasonono, pia , vidonda ,vya, tumbo ,(STOMACHI UCLENS) IHUSHI ndoji lako. 

NKANYA ni dwa ya mvuto wa kimapenzi ,mchumba mpenzi ariyekuacha, mke mme, atakuludia kwa, mda, wa msaa3 tu , ukishaitumia atarudi ,mwenyewe bila ,ugovi tena, NKOMA ni dawa kuongeza HIPS na mguu wa bia kwa wadada . 

HERBON, ni, dawa, ya kuongeza, CD4, NGAKAMA ,ni dawa ya kutibu ,miguu, kufaganzi, na ,kuwaka moto, huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa! DR SITTA, amebobea, kwa tiba asilia 

DAR ANAPATIKANA MBAGALA, ZAKHEM, SONGEA BOMBAMBILI SHINYANGA, KAHAMA MJINI, KWA MAELEZO ZAIDI , PIGA SIMU 0763172670 au 0715172670 

WOTE MNAKALIBISHWA, KAMA, UTAKUWA NA TATIZOUTAHUDUMIWA,

Wasiliana na Dr Mabula Anatibu Upungufu wa Nguvu za Kiume, Busha na Matatizo ya Maumbile Madogo kwa Mwanaume

$
0
0
 
TUNATIBU NA KUPONESHA KABISA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME UUME MDOGO BUSHA BILA KUPASUA PRESHA VIDONDA VYA TUMBO
Asilimia kubwa ya wanadamu wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali na wapo waliongahika sehemu mbalimbali bira MAFANIKIO MABULA CLINIC ni kituo cha tiba asilia kilichopo mbagara zakhemu njia kuu ya JESHINI JE HUNAUPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME AU UUME WAKO MDOGO NA MWEMBAMBA?

MAPRO PAWER NO 2 ndio Tiba kwa sasa utibu matatizo matatu kwa pamoja 1hitakufanya uchelewe kufika kilekeni dikika 15-20 kwa tendo la kwanza 2 uhimalisha misuli iliyoregea na kusinyaa hasa kwa wale walio hasirika na upigaji punyeto 3 itakufanya upate amu ya kurudia tendo zaidi ya Mara tatu

KWA NINI UJIONE MPWEKE PALE UKUTANAPO NA MPENZI AU MKE WAKO kisa unawai kukojoa au unakomea bao moja tu na huku dawa zipo MAKAKANUA mix ni dawa iliyochanganywa na miti Shamba 9 na Kuwa na uwezo wa kuongeza uume saizi upendayo inchi 5-8 Kwa Urefu na unene sentimita 1-5 dawa hizi hazina madhara yoyote kwa mtumiaji ata wazee wenye umri mkubwa wanapona? zipo dawa za mvuto wa mpenzi mme au mke Kwa masaa matatu tu na kukupigia simu yeye mwenyewe mvuto wa biashara kutengeneza mwonekano mzuri wa mwili kwa wanawake yani shepu tunatibu ngiri miguu mgongo na kiuno kuumwa kupunguza kitambi minyama uzembe matiti na mwili mkubwa

TIBA NA USHAULI MUONE DR MABULA AU PIGA SIMU NO 0752348593 UDUMA ZANGU UTAZIPATA POPOTE ULIPO KAMA UWEZI KUFIKA OFISINI

Taarifa MUHIMU Toka Bungeni Dodoma Leo

$
0
0

Taarifa MUHIMU Toka Bungeni Dodoma Leo

Tazama Hapa Taarifa Muhimu Toka IKULU Leo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dkt. John Magufuli amemteua Prof Andrew Barnabas Pembe kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu kiongozi, Balozi John Kijazi kupitia Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa imesema kuwa uteuzi wa Prof. Pembe umeanza siku ya leo.

Kabla ya uteuzi huo Prof. Pembe alikuwa Mhadhiri  na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hicho anayeshughulikia taaluma, utafiti na ushauri.

Waziri Mkuu: ”Nahitaji maelezo yenu mpaka saa 12 jioni ...Mkishindwa Ondokeni”

$
0
0
SERIKALI imesema hairidhiki na ubia unaoendeshwa kwenye Kiwanda cha Nguo cha Urafiki.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo jioni (Ijumaa, Juni mosi, 2018) wakati akizungumza na mamia ya wafanyakazi wa kiwanda hicho mara baada ya kukagua mitambo mbalimbali kwenye kiwanda hicho.

“Serikali haturidhiki na ubia huu, na huyu mbia aelewe kwamba Serikali haturidhishwi na ubia huu wala kinachoendelea hapa kiwandani,” amesema huku akishangiliwa kwa nguvu na wafanyakazi wa kiwanda hicho.

Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage aongoze kikao baina ya wabia hao na menejimenti ya kiwanda na apewe taarifa hiyo leo saa 12 jioni baada ya kufuturu.

“Ubia wenu hauna tija. Kwa hiyo wewe Msajili wa Hazina na huyo mwekezaji, nikitoka hapa, mbaki mfanye kikao na mnipe majibu leo saa 12 jioni. Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na Mkuu wa Mkoa muongoze mjadala huo na nikitoka kufuturu mniambie maazimio yenu, na kama haiwezekani, mvunje kabisa ubia huo ili tujue hatuna mbia tutafute mbia,” amesema.

Waziri Mkuu amesema wabia wakuu wa kiwanda hicho ni Msajili wa Hazina na kampuni ya Changzhou State owned Textile Assets Operations kutoka China na kwamba Serikali ilipoamua kukaribisha uwekezaji ilitarajia kupata mtaji, teknolojia na ajira za kutosha lakini hali ya sasa ni kinyume kabisa.

“Hatuwezi kuvumilia, tunasema tuna mbia mwenye mtaji, hakuna mtaji; tulisema tunataka mbia mwenye kuleta teknolojia mpya, hakuna teknolojia; tulisema aendeshe shughuli hii kukiwa na ajira endelevu, hizo ajira hakuna; halafu tubaki tunamwangalia tu. Bora atuambie amekwama, aondoke, tutangaze vinginevyo,” amesema.

“Tulikopa mtaji lakini Tanzania hizo hela hazijaja, tunataka majibu ya fedha hizo; kama fedha iliyokopwa kwenye Benki ya Exim ya China ingeletwa nchini tungeweza kuziba mapengo na kusaidia kiwanda kiweze kufanya kazi. Sasa kwa sababu fedha hiyo haijaja nchini, tunataka maelezo fedha hiyo iko wapi?” amesisitiza.

“Mitambo iliyonunuliwa na mwekezaji miaka mitano au sita iliyopita haifanyi kazi tangu ilipoletwa nchini, nataka majibu, je mitambo hii ilinunuliwa ikiwa mizima au vipi; na tena mmeng’oa mashine kwenye ma-godown matatu, nimeambiwa mlikuwa na nia ya kuleta mashine mpya, lakini sasa ni miaka mitano, je mashine zile zote zimeenda wapi, na kama mmeuza ameuziwa nani? Mkae mjadili na leo hii mniletee majibu yote haya,” amesisitiza.

Waziri Mkuu amesema kiwanda hicho ni matokeo ya urafiki wa China na Tanzania na kina historia ndefu na mahusiano ya muda mrefu. “Asiingie mtu akatuharibia, na tunataka mahusiano yetu na China yaendelee. Amesema baada ya kupokea taarifa hiyo, Serikali itakaa na Balozi wa China ili itafutwe suluhisho.

Waziri Mkuu amewataka watumishi wa kiwanda hicho walioko likizo na wale waliopo kazini wawe wavumilivu wakati Serikali ikiendelea kutafuta dawa ya matatizo yao.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amemtaka Meneja Rasilmali Watu na Utawala wa kiwanda hicho, Bw. Edwin Nkwanga aandae orodha ya watumishi wote yenye kuonyesha kila mtumishi analipwa nini na aifikishe kwake haraka.

“Hapa kuna watu wanalipwa sh. milioni saba hadi 10 na wengine wanalipwa sh. 120,000. Niletee orodha yenye kuonyesha jina, cheo na kiwango cha mshahara, lakini pia uonyeshe anapata stahili zipi, kama ni posho ya nyumba, maji au umeme,” amesema.

Amesema nia ya Serikali ni kutaka kupanga upya mishahara yao ili waweze kupatikana watumishi wa kutosha.

Wakati akikagua kiwanda hicho, Waziri Mkuu alielezwa kwamba kuna mashine 88 ambazo ziling’olewa kwenye kiwanda hicho na hazijulikani zimepelekwa wapi.

Mapema, akitoa taarifa fupi ya kiwanda hicho, Naibu Meneja Mkuu wa kiwanda hicho, Bw. Shadrack Nkelebe alisema kiwanda hicho kimesimamisha uzalishaji tangu Desemba 2017 ili kufanya ukarabati na kimeshindwa kuendelea nao kwa sababu ya madeni.

“Kiwanda kilikuwa na watumishi 3,000 lakini sasa hivi wamebakia 726 baada ya wengine kupunguzwa na kulazimishwa kwenda likizo licha ya teknolojia kubakia ni ileile. Kiwanda kinakabiliwa na changamoto nyingi lakini kwa sehemu kubwa ni za kutengeneza. Tumepigana vita katika kujenga uchumi wa Taifa kupitia kiwanda hiki, lakini tumekwama. Tunahitaji nguvu ya ziada ili tutoke hapa,” alisema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

Matibabu ya Wema Sepetu India, Mimba Yatajwa

$
0
0
DAR ES SALAAM: Siku chache baada ya mrembo Wema Sepetu kudaiwa kuelekea nchini India kwa ajili ya matibabu, habari nyuma ya pazia zimeleza kuwa, sehemu kubwa ya tatizo linalomsumbua mrembo huyo ni kusaka ujauzito.

 Mei 29, mwaka huu, Wema alishindwa kutokea katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar katika kesi ya madawa ya kulevya inayomkali ambapo mama yake aliwasilisha nyaraka zilizoonesha kuwa bintiye amekwenda nchini India kwa ajili ya matibabu.

 Chanzo kilicho karibu na mrembo huyo kimeeleza kuwa, kwa muda mrefu Wema amekuwa akihangaika kupata mtoto hivyo ameona aende India ili kuweza kusaka suluhu.

“Wema anatamani kuwa mama jamani, hajachoka na ha hakati tamaa. Ameamua kwenda India na nasikia matibabu ya safari hii nasikia yatahusisha pia upasuaji,” alisema mtoa habari huyo.

 Baada ya kunasa ubuyu huo, Ijumaa lilijaribu kuwasiliana na mama yake mzazi Wema, Miriam Sepetu bila mafanikio lakini hata hivyo, baadaye alipatikana meneja wake, Neema Ndepanya, akafunguka:

“Mimi ninachofahamu ni kwamba amekwenda India kwa ajili ya matibabu ya tumbo na si vinginevyo,” alisema Neema.
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live




Latest Images