Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Jibu la Ruby Kuhusu Kujihusisha na Mambo ya Ushirikina

$
0
0

Msanii wa Bongo Flava, Ruby amefunguka kuhusu kuhusisha muziki wake na masuala ya kushirikina.

Muimbaji huyo anatayetamba na ngoma ‘Niwaze’ katika mahojiano na Papaso, TBC FM amesema kwa upande wake ni kitu ambacho hakifahamu kabisa.

“Siko hivyo na wala sijawahi, mimi nina bibi yangu, nina babu yangu wapo Tanga na ndio nyumbani kwetu hayo mengine siyajui,” amesema Ruby.

Ameendelea kwa kusema kuwa siri ya mafanikio ni Mungu, kufanya muziki mzuri, kuwapenda mashabiki wake na aina ya watu ambao ameamua kufanya nao kazi.

 Tazama Rosa Ree na Emtee Walivyokinukisha Kwenye Chupa Hili..Bonyeza Play

Tawi la Yanga Mwanza lamjia juu Mzee Akilimali

$
0
0

Tawi moja la Yanga mkoani Mwanza limeibuka na kupiga kauli ya Mjumbe wa Baraza la Wazee Yanga baada ya kuibuka na kueleza kuwa anataka kugombea nafasi ya Uenyekiti ndani ya klabu hiyo.

Mzee huyo ameibuka hivi karibuni na kutangaza kuwa atagombea nafasi hiyo ili kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti, Yusuph Manji ambaye alijiuzulu ili kupumzika.

Kwa mujibu wa Radio One kupitia kipindi cha Spoti Leo, Kiongozi wa tawi hilo, Mhando Madega, amesema kuwa mzee huyo amekuwa mnafiki na mchochezi kwani amekuwa akiibuka pale Yanga inapokuwa haina wakati mzuri.

Aidha, Madega ameongeza kwa kueleza kuwa Akilimali hajawa na msaada wowote ndani ya Yanga zaidi ya kutupia lawama uongozi ambao umekuwa ukiipigania klabu katika nyakati zote ambazo inapitia.

Madega ameuomba uongozi wa Yanga uangalie namna ya kumsimamisha Akilimali ikiwezekana kumfuta kabisa uanachama ndani ya klabu kwani amekuwa akileta sintofahamu nyingi zisizokuwa na maana.

Tukio la Ubakaji St Florence Lazua Hofu kwa Usalama wa Wanafunzi

$
0
0

Dar es Salaam. Tukio la wanafunzi wa kike wa Shule ya Msingi ya St Florence kudaiwa kunajisiwa na mwalimu, limeongeza hofu ya usalama wa watoto shuleni baada ya matukio mengine kutikisa nchi katika miaka ya karibuni.

Tukio hilo limetokea takriban miaka 13 baada ya familia ya mwanamuziki Nguza Viking kukamatwa kwa kosa la kunajisi watoto wa kike maeneo ya Sinza.

Pia imetokea takriban miaka miwili baada ya walimu wa Shule ya Sekondari ya Mbogamo mkoani Njombe kumpiga mwanafunzi hadi kupoteza fahamu baada ya kumkuta na simu ya mkononi.

Pia limetokea takriban mwaka mmoja baada ya walimu wa Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Mbeya kumshambulia mwanafunzi wa kidato cha tatu kwa kosa la ukaidi.

Ni mwaka jana tu wakati wanafunzi 32 wa Shule ya Sekondari ya St Lucky Vincent walipofariki ajalini wakati wakienda shule jirani kwa shughuli za masomo.

Pamoja na tukio la wanafunzi wa Lucky Vincent kuwa la ajali, hofu ya usalama wa wanafunzi wanapokuwa shuleni au ziara za kimasomo sasa limeibuka upya baada ya tukio la St Florence.


Baada ya wazazi wa watoto wanaosoma shuleni hapo kupata taarifa, baadhi waliripoti kituo cha polisi na wengine kwenda shuleni kujaribu kuhamisha watoto wao kwenda shule nyingine.

Lakini bado hawana uhakika na huko waendako.

“Mwalimu ni mtu wa kuaminiwa. Mzazi anapompeleka mtoto shule anajua mwanae yupo mikono salama,” alisema mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi alipoulizwa maoni yake kuhusu usalama wa wanafunzi shuleni.

“Sasa huyu mtu akianza kuwa mbakaji na mlawiti, hii ni hatari mno, tunapaswa kumsaidia mtoto ajisimamie.”

Alisema njia ya kuwasaidia watoto wa kike ni kuwafundisha ukweli kuhusu ukatili wa kingono, viungo, vyao vya mwili na uwezo wa kusema pale wanapoona dalili za kufanyiwa ukatili huo.

Alisema ni lazima shule za msingi na sekondari ziwe na mikakati ya kuwafundisha watoto namna ya kujinasua kwenye mitego ya wabakaji na walawiti ambao huja kwa sura ya kuwapenda huku wakiwapa zawadi wakati mioyoni mwao wanapanga kufanya ukatili.

“Mtoto akishafikishwa shuleni aambiwe ukweli kabisa kwamba asikubali kuitwa ofisini kwa mwalimu wa kiume kisha mlango wa ofisi hiyo ukafungwa wakiwa wawili tu, wala asikubali zawadi, kukumbatiwa au kuchezewa mwili wake wakiwa faragha,” alisema.

Medesta Kimonga, ambaye ni mtaalamu wa saikolojia wa Chuo cha Ualimu Tanga, anaona matatizo hayo ya ukatili kwa watoto yanatokana na ukosefu wa maadili ya kitaaluma.

“Unakuta mtu huyo alipata kazi kwa sababu hana kazi na hana wito wa ualimu, hivyo haoni mzigo wa malezi isipokuwa kuwajeruhi watoto,” alisema.

Kimonga Alisema athari za watoto kufanyiwa ukatili wa kingono ni nyingi na kubwa ni zile za kisaikolojia.

Kimonga alisema mtoto aliyefanyiwa hivyo na kukosa msaada wa kisaikolojia hukumbwa na ugonjwa wa kuzubaa.

“Ukimpa kazi anaweza kuifanya kwa muda mrefu sana, lakini anaweza pia kupoteza kabisa kumbukumbu,” alisema.

Alishauri jamii nzima kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.

Naye Venus Kimei, diwani wa Kata ya Mikocheni ambako shule hiyo iko, alisema lazima watoto waambiwe ukweli kwamba wasimwamini mtu yeyote kuwashika miili yao hasa sehemu za siri.

“Wawekewe msingi mzuri wa kukataa wenyewe, lakini baadaye waweze kujieleza kwa wazazi na walezi wanaowaamini,” alisema.

Alisema Serikali inapaswa kuandaa walimu wa saikolojia watakaoweza kuwasaidia watoto shuleni bila kuogopwa.

“Mtoto anapokutana na jambo gumu hasa la kutongozwa na mwalimu, asikae kimya. Ajengewe msingi wa kutoogopa na kutoa taarifa kwa mtu mwingine anayemwamini na atakayemsaidia,” alisema.

Lakini mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa), Eda Sanga aliwatwisha mzigo wazazi.

“Wazazi wana nafasi kubwa ya kuwajibika kuwasaidia watoto wao kujitambua na kutokuwa waoga,” alisema Sanga.

Alisema katika tafiti mbalimbali walizowahi kufanya waligundua kuwa wengi hufanyiwa ukatili wa kingono na watu wa karibu wakiwamo walimu.

“Wazazi na walezi wasiwe mbali na watoto, wawajengee kujiamini na kupambana na mambo haya wao wenyewe, wapewe uwezo wa kusema wanapokutwa na majanga ya aina hii,” alisema.

Alisema ushirikiano baina ya jamii, walimu, wazazi au walezi na Serikali ndiyo utakaosaidia kutokomeza tatizo hilo.

“Tunahitaji mjadala wa kijamii kujua chimbuko la haya matatizo ni nini? Kuna haja ya kuwatafuta wana saikolojia ili wawasaidie waliofanyiwa ukatili,” alisema.

Utafiti Waonyesha Kuwa sauti ya Muziki Huathiri Aina ya Chakula Inayoagizwa Migahawani

$
0
0

Utafiti umeonyesha kuwa sauti ya muziki huathiri aina ya chakula ambacho huagizwa katika migahawa.

Katika utafiti uliofanywa na wanafunzi wa chuo kikuu cha Florida, imeonekana kuwa wateja hupendelea kuagiza vyakula kama kachumbari na vile viisvyokuwa na mafuta pale muziki wenye sauti ndogo unapopigwa.

Na pale muziki wenye sauti kubwa unapopigwa basi vyakula kama burger na chips huagizwa kwa wingi.

Utafiti huo umefanywa katika moja ya mgahawa nchini Sweden.

Sura Yake Yamsababishia Majanga, Akamatwa na Polisi

$
0
0

Tosin Olakunle raia wa Nigeria anayejishughulisha na kupamba nyuso za watu na mitindo ya nywele amejikuta akikamatwa na jeshi la polisi kwa kile walichodai kuwa eti ni ‘mwembamba sana halafu ana sura ya kike wakati yeye ni mwanaume’.

Olakunle alijikuta akitoa N2,000 ambayo ni sawa na zaidi ya shilingi 12,647 za kitanzania ili kupatiwa dhamana katika kituo cha polisi cha Iwaya  alipokuwa ameshikiliwa na jeshi hilo.

Akielezea mkasa huo Olakunle amesema kuwa ilikuwa jumatatu ya May 28 alipokuwa anaenda kwa mteja wake mmoja kumhudumia na ndipo alipokuwa katika stendi ya Lamata katika mji wa Ojota alipozuiliwa kupanda basi na mtu aliyemtaka ajitambulishe.

“Nilimuuliza kwanini nijitambulishe kwako? Jamaa akanijibu kuwa yeye ni polisi na akanitaka nimpe vitambulisho vyangu kitu ambacho nilitelekeza. Lakini akaniuliza tena kwa nini naonekana kama mwanamke kwenye kitambulisho changu? Nikamjibu kuwa nimekuwa na kitambulisho hicho kwa muda mrefu sasa baadae akaniambia niingie kwenye gari nakuniambia kuwa mimi ni shoga” alisimulia Olakunle.

“Nilimpa simu pamoja na iPad yangu ili akague kuona kama atakuta kitu chochote ambacho kitathibitisha mimi nahusika na vitendo hivyo na nikamwambia kuwa mimi pia ni mwanamitindo wa nywele wala sijapaka vipodozi na wala sina michoro (tattoo) kwenye mwili wangu lakini bado hakunielewa na kuendelea kunishikilia” aliongeza Onlakunle.

Aidha baadae Onlakunle alipelekwa katika kituo cha polisi cha Iwaya na alipouliza kwa nini anashikiliwa na polisi?, askari huyo akamwambia kuwa “wewe ni mwembamba sana na unaonekana kama wewe ni shoga”

Olankunle alimalizia kwa kusema kuwa ilibidi awe mpole ili ajiepushe na kipigo na ikambidi atoe fedha N2,000  na kujidhamini ili aweze kuachiwa huru huku akimkosa mteja wake waliyokuwa wamepanga kukutana.

Wasiliana na Dr Mabula Anatibu Upungufu wa Nguvu za Kiume, Busha na Matatizo ya Maumbile Madogo kwa Mwanaume

$
0
0

TUNATIBU NA KUPONESHA KABISA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME UUME MDOGO BUSHA BILA KUPASUA PRESHA VIDONDA VYA TUMBO
Asilimia kubwa ya wanadamu wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali na wapo waliongahika sehemu mbalimbali bira MAFANIKIO MABULA CLINIC ni kituo cha tiba asilia kilichopo mbagara zakhemu njia kuu ya JESHINI JE HUNAUPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME AU UUME WAKO MDOGO NA MWEMBAMBA?

MAPRO PAWER NO 2 ndio Tiba kwa sasa utibu matatizo matatu kwa pamoja 1hitakufanya uchelewe kufika kilekeni dikika 15-20 kwa tendo la kwanza 2 uhimalisha misuli iliyoregea na kusinyaa hasa kwa wale walio hasirika na upigaji punyeto 3 itakufanya upate amu ya kurudia tendo zaidi ya Mara tatu

KWA NINI UJIONE MPWEKE PALE UKUTANAPO NA MPENZI AU MKE WAKO kisa unawai kukojoa au unakomea bao moja tu na huku dawa zipo MAKAKANUA mix ni dawa iliyochanganywa na miti Shamba 9 na Kuwa na uwezo wa kuongeza uume saizi upendayo inchi 5-8 Kwa Urefu na unene sentimita 1-5 dawa hizi hazina madhara yoyote kwa mtumiaji ata wazee wenye umri mkubwa wanapona? zipo dawa za mvuto wa mpenzi mme au mke Kwa masaa matatu tu na kukupigia simu yeye mwenyewe mvuto wa biashara kutengeneza mwonekano mzuri wa mwili kwa wanawake yani shepu tunatibu ngiri miguu mgongo na kiuno kuumwa kupunguza kitambi minyama uzembe matiti na mwili mkubwa

TIBA NA USHAULI MUONE DR MABULA AU PIGA SIMU NO 0752348593 UDUMA ZANGU UTAZIPATA POPOTE ULIPO KAMA UWEZI KUFIKA OFISINI

Kwa Mwanamke Naangalia Sura Kwanza, Tabia Tutaelekezana – Diamond Platnumz

$
0
0
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesema kuwa yeye kigezo kikubwa anachotumia kumpata mwanamke mwema wa kuoa ni kuangalia sura na sio tabia kama wengi wanavyosema.

Diamond akitetea msimamo wake kwenye kipindi cha Kaa Hapa kinachorushwa TBC 1, amesema kuwa mwanamke huwezi kumbadilisha sura kwa namna yoyote ile lakini tabia ni rahisi kumbadilisha.

Akielezea kuhusu kigezo hicho, Diamond amesema kama angetoa asilimia kwa vigezo vya sura na tabia basi asilimia 70 angetoa kwa upande wa sura na asilimia 30 zilizobaki ndio angeangalia tabia.

“Kiukweli tabia tunapenda lakini wakati mwingine sura nazo zina uzito wake, Kiukweli tabia mnaweza kuelekezana ila sura kuelekezwa mtaelekezana vipi?. Tabia tunajifunza kama alijifunza kuchukia atajifunza kupenda, sura atajifunza vipi?, Kwa mwanamke mimi naangalia sura kwanza , tabia tutaelekezana.“amesema Diamond Platnumz.

Hata hivyo, kupitia kipindi hicho Diamond Platnumz amefunguka kuhusu zile picha za faragha zilizovuja akiwa na Hamissa Mobetto kwa kusema kuwa walikuwa location wakirekodi kipindi cha TV.

Rais Magufuli Amewapandisha Vyeo Maafisa 9 wa Magereza

$
0
0


Leo June 2, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa 4 wa Jeshi la Magereza kutoka Naibu Kamishna wa Magereza (Deputy Commissioner of Prisons – DCP) hadi kuwa Kamishna wa Magereza (Commissioner of Prisons – CP).

Pia amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Magereza wengine 5 kutoka Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (Senior Assistant Commissioner of Prisons – SACP) hadi kuwa Naibu Kamishna wa Magereza (Deputy Commissioner of Prisons – DCP).

Maafisa waliopandishwa vyeo kutoka DCP na kuwa CP ni wafuatao

Hamis Ngarama
Tusekile Mwaisabila
Augustine Sangalali Mboje
Gideon Marco Nkana
Maafisa waliopandishwa vyeo kutoka SACP na kuwa DCP ni,

Julius Mayenga Sang’udi
Afwilile Mwakijungu
John William Masunga
Phaustine Marint Kasike
Joram Yoram Katungi

Utafiti: Chai Huongeza Uwezo wa Mwanamke Kushika Mimba

$
0
0

UTAFITI: Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Boston nchini Marekani imebanishwa kuwa unywaji wa chai vikombe 2 kwa siku humuongezea mwanamke uwezo wa kushika ujauzito

Utafiti huo uliwahusisha Wanawake 3,600 na kuonesha kuwa wale wanaokunywa vikombe 2 vya chai kwa siku, wana 27% ya kupata ujauzito ikilinganishwa na ambao hawanywi chai

Aidha, Wanawake wanaotumia vinywaji baridi vya aina mbili kwa siku, hupunguza uwezekano wao wa kushika ujauzito kwa 20%

Hata hivyo, Mtafiti mmoja ameeleza kuwa utafiti zaidi unahitajika ili kujua kama chai ya kijani ndiyo husaidia wanawake kupata ujauzito au ni ya aina gani

Dawa Bora za Nguvu za Kiume na Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa

$
0
0

DAWA BORA ZA NGUVU ZAKIUME NA KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA. baada ya utafiti wa muda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka sasa MWASELE HERBAL CLINIC. inakuletea suluhu juu ya matatizo haya kwa kutumia dawa za FULL POWER .ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu zakiume. dawa hii ina mchanganyiko wa kutosha kuzalisha vichocheo vingi vya hormone za gestrogen ziwemo vitamin B6&B1, vitamini E pamoja madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na muzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi na kuchelewa kufika kileleni zaidi ya dakika 20-30. ZAT 50 inarudisha maumbile ya uume yaani kurefusha na kunenepesha ulefu nchi 3-7, upana cm, 3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukitumia maumbile yatabaki kuwa hivyo siku zote . pia tunatibu matatizo mengine kama presha, kisukari , ngiri ,chango la tumbo,tumbo kujaa gesi, kutokupata choo vizuri,miguu kuwaka moto,matatizo ya uzazi, bawasili namagonjwa yazinaa kama kisonono nakaswende.

Tunapatikana DAR ES SALAAM. SHINYANGA NA ZANZIBAR. kwa wakazi wa dar es salaam utaletewa huduma hii popote ulipo . wa mikoani tunawatumia kwanjia ya mabasi .

Wasiliana nasi kwa simu no 0717702227 au 0754568767.DR . SAGUDA nyote mnakaribishwa

Utafiti: Kukaa Sana Kwenye Gari na Ofisini Kuna Sababisha Afya Mbaya Kwa Binadamu

$
0
0

AFYA: Imethibitika kwamba kukaa muda mrefu kwenye magari, ofisini au kwenye viti kunasababisha matokeo hasi kwa afya ya binadamu

Kukaa muda mrefu pia kunahusishwa na kusababisha uzito uliopitiliza, magonjwa ya moyo, kisukari na magonjwa mengine yasiyoambukiza

Kupitia utafiti mpya uliotolewa hivi karibuni, hamasa inatolewa kwamba baadhi ya shughuli za mwili ikiwemo njia rahisi za kuimarisha misuli zinaweza kumsaidia mtu kukabiliana na athari za kiafya za kukaa muda mrefu

Katika utafiti huo wataalamu walichambua data za watu 400,000 wenye umri wa kati nchini Uingereza

Watafiti hao walifanya ulinganifu wa ripoti za watu waliofanya shughuli za mwili kama mazoezi na muda waliotumia kuangalia runinga au kompyuta

Kutokama na uchambuzi huo wa data Wamebaini kuwa watu ambao wana misuli dhaifu wana uwezekano wa asilimia 31 ya kufa mapema kama watatumia saa mbili mbele ya runinga, ukilinganisha na watu wenye misuli imara ambao wanatumia muda kama huo

Pia watu hao wana hatari kwa asilimia 21 kupata magonjwa ya moyo na 14% kupata kansa ukilinganisha na wale wenye misuli imara.

Tundu Lissu Ampinga Spika Ndugai Sakata la Ripoti ya Uvuvi na Gesi Asilia

$
0
0

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amefunguka na kuwataka Wabunge wenzake bila ya kujali itikadi ya vyama vyao kutoshiriki kwenye hafla ya kupokea na kukabidhi taarifa za kamati maalum za kuchunguza na kushauri sekta ya Uvuvi wa bahari kuu na Gesi asilia iliyopangwa kufanyika kesho.


Lissu ametoa kauli hiyo jana mchana kupitia ukurasa wake wa kijamii mara baada ya Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuutarifu umma kuwa Juni 2, 2018 Spika wa Bunge Job Ndugai atapokea ripoti hizo ambazo zimepangwa kufanyikia katika viwanja vya Bunge mbele ya lango kuu la kuingilia.


Kutokana na hilo, Lissu amedai kitendo hicho ni kinyume na zinaharibu taratibu za kisheria kwa kuwa taarifa za uchunguzi za Bunge huwa zinawasilishwa bungeni tena mbele ya wabunge wote na kujadiliwa endapo itahitajika kabla ya kukabidhiwa serikalini.


"Nawaomba Wabunge wasikubali kushiriki katika maziko haya ya mamlaka ya kikatiba na kikanuni ya Bunge. Wadai taarifa hizi ziwasilishwe kwanza bungeni na kujadiliwa na wabunge, kama Spika Ndugai na watu wake wasipokubali kufanya hivyo, basi nawashauri wabunge wote wasusie hafla hiyo", amesema Lissu.


Pamoja na hayo, Lissu ameendelea kwa kusema "wabunge watakaoshiriki hafla wajue, au waambiwe, kwamba wanashiriki kwa ushiriki au uwepo wao katika mazishi ya mamlaka ya kikatiba ya Bunge ya kuisimamia na kuishauri serikali kwa kupitia majadiliano bungeni. 


"Kwa utaratibu huu, Bunge halitajadili, na watanzania hawataona wala kusikia tena taarifa za kamati za uchunguzi za Bunge kama zile za Richmond wa Bunge la Spika Sitta na Operesheni Tokomeza na Tegeta Escrow wakati wa Bunge la Spika Anna Makinda". ​


Kwa upande mwingine, Lissu amesema hakuna kanuni ya Bunge inayoruhusu Kamati yoyote ya Bunge kupeleka taarifa yake serikalini moja kwa moja, bila kupitia bungeni na kujadiliwa na wabunge.

Jay Moe: Muziki wa hip hop umekuwa biashara

$
0
0

Msanii mkongwe wa muziki wa hip hop, Jay Moe amedai kwa sasa kuna vitu vingi ambayo vimebadilika kutoka wa wasanii wa muziki wa hip hop kutoka na muziki kubadilika na kuwa biashara tofauti na zamani.

Rapa huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Bata’, amedai kwa sasa kila pesa ambayo inawekezwa kwenye muziki inatakiwa kurudi.

“Sasa hivi tunawekeza sana kwenye muziki tofauti na miaka ya zamani tunatoa wimbo tu hakuna uwekezaji wowote ambao tulikuwa tunaweka,” Jay Moe alikiambia kipindi cha Ladha 3600 cha Efm. “Lakini sasa hivi au miaka ya sasa hivi muziki umekuwa biashara, kwahiyo lazima pia unavyowekeza uhakikishe uwe na target nzuri ya kuweza kujua pesa yangu itarudi vipi,”

Moe ni mmoja kati ya wasanii wakongwe ambao wameweza kurudi kwenye game baada ya kukaa kando kwa muda mrefu.

Hii Hapa Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo ya Uume

$
0
0
Tatizo hili limekuwa likiwaadhiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baada ya kujiona wapo tofauti sana na wengine kwa kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi 6-8 kwanza upungufu wa vichocheo hivi huchochea ukuaji wa uume chongo ambalo hushambulia nerve ambayo uharibu kabisa ukuaji wa uume, ngiri, punyeto, ambayo huathili misuli ya uume, ngiri huleta maumivu, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, korodani moja kuvimba, kutopata choo vizuri, sababu hizi hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na mara nyingi hata nguvu za kiume ( hamu ya tendo la ndoa) hupungua na kwisha kabisa

GEMBE :Ni dawa inayozalisha na kukufanya uume kukua na kuongezeka
NGEMO : Ni dawa bora ya kuongeza nguvu za kiume

Hukutia hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi mara4 nne bila kukinai au kuchoka pia itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk30-45 kwa mtumiaji pia tunatibu kisukari, bp, ngiri, miguu kuwaka moto KAMA HUNAMDA WA KUFIKA OFISINI KWETU UTALETEWA POPOTE TUPO MBAGALA RANGI TATU

 0753471612/ 0715249530
0623 386 305

DR KUZENZA

Nataka Niache Muziki Lakini Najikuta Nashindwa..na Mziki Nao Umenikataa

$
0
0

Msanii mkongwe wa Bongo Flava, Ferooz amesema kuwa kuna wakati anatamani kuacha muziki lakini anashindwa.

Muimbaji huyo ameeleza sababu ya kutaka kufikia uamuzi huo ni kuonekana si kitu wakati ameutoa mbali muziki huo.

“Kikubwa kinachoniumiza nikiangalia game nilipolitoa mpaka lilipofika halafu bado naonekana mimi ndio nimekosea, mkosefu namba moja,” amesema.

“Game linanisahau kwa kifupi, mkapa nafikia fikra za kusema ni quit kufanya muziki, ni quit kufanya game, nitangaze nimeacha muziki. Nataka niache muziki lakini najikuta kwamba nashindwa kwa sababu imeshakuwa kwenye damu,” Ferooz ameiambia Wasafi TV.

Ameongeza kuwa licha ya kufanya muziki kwa takribani miaka 20 sasa amekuwa pia akifanya mambo mengine lakini mwisho wa siku anajikuta amesharudi kwenye muziki. Wimbo wa mwisho kutoa Ferooz unakwenda kwa jina la Najaribu.

Kamati Maalumu Ya Bunge Yaibua Madudu, Maya ziti Watajwa

$
0
0

Kamati iliyoundwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kuchunguza mwenendo wa biashara ya sekta ya gesi asilia nchini imebaini madudu katika sekta hiyo ikiwamo mikataba ya serikali na wawekezaji ilivyoliingiza hasara taifa kupitia sekta hiyo huku mfanyakazi mmoja akilipwa mamilioni.


Mwenyekiti wa Kamati hiyo iliyoundwa Novemba mwaka jana, Dunstan Kitandula amesema hayo bungeni jijini Dodoma leo wakati akiwasilisha ripoti ya kamati hiyo kwa Bunge.


Katika ripoti hiyo, Kitandula amewataja mawaziri zamani wa iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini, Daniel Yona, Nazir Karamagi, William Ngeleja na marehemu Abdallah Kigoda kuingia mikataba hiyo, ambayo alisema imekuwa ikiliingizia hasara taifa.


“Mawaziri hao walikuwa wakisaini mikataba hiyo na makampuni ya kigeni kupitia aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Yona Kilaghani.


“Aidha, katika uchunguzi wetu, kamati ilibaini mfanyakazi mmoja wa kigeni wa Kampuni ya Payet, analipwa mshahara wa Sh milioni 96 kwa mwezi tofauti na wazawa ambao wanalipwa mshahara kidogo.


“Kutokana na hali hiyo, kamati inapendekeza vyombo vya dola vichunguze mikataba yote katika sekta ya gesi iliyoingiwa na viongozi hao ili kuona kama walikuwa na nia njema au waliiisaini kwa kujali maslahi yao,” amesema Kitandula.

Dawa Bora za Nguvu za Kiume na Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa

$
0
0

Baada ya utafiti wa muda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka sasa

MWASELE HERBAL CLINIC. inakuletea suluhu juu ya matatizo haya kwa kutumia dawa za

FULL POWER .ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu zakiume. dawa hii ina mchanganyiko wa kutosha kuzalisha vichocheo vingi vya hormone za gestrogen ziwemo vitamin B6&B1, vitamini E pamoja madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na muzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi na kuchelewa kufika kileleni zaidi ya dakika 20-30. ZAT 50 inarudisha maumbile ya uume yaani kurefusha na kunenepesha ulefu nchi 3-7, upana cm, 3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukitumia maumbile yatabaki kuwa hivyo siku zote . pia tunatibu matatizo mengine kama presha, kisukari , ngiri ,chango la tumbo,tumbo kujaa gesi, kutokupata choo vizuri,miguu kuwaka moto,matatizo ya uzazi, bawasili namagonjwa yazinaa kama kisonono nakaswende.

Tunapatikana DAR ES SALAAM. SHINYANGA NA ZANZIBAR. kwa wakazi wa dar es salaam utaletewa huduma hii popote ulipo . wa mikoani tunawatumia kwanjia ya mabasi .

Wasiliana nasi kwa sim no 0717702227 au 0754568767.DR . SAGUDA nyote mnakaribishwa

Mfahamu Mwanamke Anayeweza Kukutabiria Siku ya Kifo kwa Kunusa

$
0
0

Ari Kala raia wa Australia mwenye miaka 24 amegeuka gumzo duniani baada ya kudai kuwa ana talanta ya kugundua watu wanaokaribia kufa kwa kunusa tu harufu zao lakini cha kushangaza ni kwamba talanta yake hiyo haimuwezeshi Ari kumsaidia mtu anayekaribia kufa aepukane na kifo.

Mwanadada huyo ambaye kwa sasa anasomea taaluma ya saikolojia anasema kuwa aligundua talanta yake hiyo alipokuwa na miaka 12 alipokuwa ameenda kumtembelea mjomba wake aliyekuwa amekaribia kufa na ndipo aliponusa harufu mbaya ya mtu anayekaribia kufa ambayo hakuna mtu mwingine aliyeweza kunusa harufu hiyo.

“Nilidhani ni harufu ya mabaki ya mwili wa mjomba kwa sababu ilikuwa harufu mbaya sana ambayo sijawahi kuinusa. Lakini hakuna mtu mwingine aliyeweza kuinusa harufu hiyo” alisema Ari.

Ari aliongeza kuwa baadae alikuja kugundua kuwa mara kwa mara ameweza kunusa kifo na kuna wakati mwingine anaona ni mzigo kuwa na talanta hiyo na huwa anatamani kuwaambia watu wanaotaka kufa kwamba wanakaribia kufa lakini baadae huacha kwa sababu hilo sio jukumu lake.

Kwa sasa Ari Kala anawafundisha wanawake wenye umri kati ya 25-45 wanaotoka kwenye jamii zinazoamini uchawi kutumia vizuri talanta na vipaji vyao katika kuisaidia jamii.

Makumbusho ya Iddi Amin Kujengwa Uganda

$
0
0

Uganda wanafikiria kuvutia Watalii wengi duniani kwenda nchini humo kwa kujenga Makumbusho ya Vita ya Uganda itakayokuwa na historia na taarifa zote za nchi hiyo katika kipindi kibaya cha historia ya Uganda.

Katika Makumbusho hayo Mauaji na maovu yote yaliyotendeka wakati wa miaka 8 ya utawala wa Rais wa zamani wa nchi hio Nguli Idi Amin pamoja na jeshi la waasi Lord’s Resisitance Army (LRA) yataoneshwa.

“Tunataka kuweka kumbukumbu na historia ya taifa hili wazi” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa wa Bodi ya Utalii ya Uganda Stephen Asiimwe.

Katika Makumbusho hayo ya Vita ya Uganda kutakuwa pia na historia ya taifa hilo kabla ya ukoloni na wakati wa ya ukoloni.

“Historia inakuwa utajiri kadri siku zinavyokwenda na kuwa ya kuvutia kama mvinyo” aliongeza Asiimwe huku akiweka sawa kuwa Makumbusho hayo hayana nia ya kuamsha hisia mbaya na kupotosha watu juu ya historia ya nchi hio.

Hata hivyo baadhi ya taarifa zinazomuhusu Idi Amin ambazo zitakuwepo kwenye makumbusho hayo ni pamoa;

Alijiunga na jeshi la King’s African Rifles akiwa kwenye miaka ya 20
Alichukua madaraka mwaka 1971
Watu takribani 400,000 wanadaiwa kuuawa katika utawala wake
Mwaka 1972 aliwafukuza watu wote wa jamii kutoka bara la Asia akiwatuhumu kwa kushusha uchumi wa nchi hiyo
Alibadili dini na kuwa Muislamu na kuoa wake watano na kufanikiwa kupata watoto wengi huku akisisitiza kuitwa ‘Bigg Daddy’
Alijitangaza kama Mfalme wa Uskochi na kuzuia uvaaji wa nguo fupi
Mwaka 1979 aliondoshwa na majeshi ya Tanzania na kukimbia nchi
Na mwaka 2003 alifariki nchini Saud Arabia
Aidha John Sempebwa ambaye ni makamu Mkurugenzi Mtendaji wa Muongozaji wa Bodi ya Utalii ya nchi hiyo amesema kuwa anawakatalia wale wote wanaosema kuwa nchi hio inataka kuwarejeshea maumivu wananchi wake yanayotokana na matukio ya huko nyuma kwa kujenga kwa Makumbusho hayo.

Mafisadi Kubanwa kwa Kutumia Kifaa cha Kubaini Waongo

$
0
0

Leo June 2, 2018 Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa maafisa wa ngazi za juu ya serikali yake wanaohusishwa na ufisadi watapimwa kwa kutumia kifaa maalumu cha kubaini watu waongo ili kukabiliana na ufisadi uliokithiri nchini humo.

“Kifaa hicho ambacho kitafichua maadili ya wafanyakazi ni miongoni mwa mikakati ya kukabiliana na tatizo hilo” Rais Kenyatta.

Rais Kenyatta alinena hayo baada ya kufichuliwa kwamba shilingi bilioni 8 za Kenya zilitumbuliwa katika idara moja ya serikali.

Kashfa hiyo ambayo imetokea katika shirika la vijana la huduma kwa jamii NYS ambapo vyeti bandia na malipo ya ziada yalifanyika wakati wahusika ambao ni wauzaji wa bidhaa waliokuwa wanatakiwa kulipwa hawakulipwa kama vyeti na hati za malipo hizo feki za zinavyoonyesha.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais Kenyatta alipokuwa akihutubia wananchi kwenye sherehe za miaka 55 tangu Kenya ipate uhuru ni kwamba, wakuu wote wa idara za kutoa zabuni na zile za serikali watafanyiwa ukaguzi mpya ikiwemo kupimwa na kifaa maalumu  cha kuwabaini watu waongo ili kujua maadili yao.

“ Maafisa watakao feli watasimamishwa kazi” alisema rais Kenyatta.
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images