Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Bodi na Menejimenti ya Benki Kuu Kuhojiwa na Kamati ya Bunge Leo

$
0
0
Bodi na Menejimenti ya Benki Kuu Kuhojiwa na Kamati ya Bunge Leo
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) leo Alhamisi Juni 7, 2018 inakutana na bodi na menejimenti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuihoji juu ya tuhuma zinazowakabili.

Benki hiyo inatuhumiwa kutumia bima binafsi badala ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Akizungumza na MCL Digital leo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma, mwenyekiti wa PAC Naghenjwa Kaboyoka amesema watakutana na BoT leo.

“Leo tumewaita na tutakutana nao. Baada ya kukutana nao taarifa tutaiwasilisha kwa Spika kama alivyotuagiza," amesema Kaboyoka ambaye pia ni mbunge wa Same Mashariki (Chadema)

Tuhuma kuhusu BoT ziliibuliwa na mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga Juni 4, 2018 bungeni  katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango mwaka 2018/19.

Amlinga amesema BoT inatumia Sh12bilioni kwa mwaka badala ya Sh1bilioni kugharamia matibabu ya watumishi wake.

Mawigi Awatolea Povu Wanawake Wanaomtaka Kimapenzi Diamond

$
0
0
Mawigi Awatolea Povu Wanawake Wanaomtaka Kimapenzi Diamond
MSANII wa filamu za Kibongo, Mary Mawigi ameibuka na kuwatolea povu wanawake wanaomshobokea kimapenzi mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na kuwataka waache kwani anawadhalilisha na kuwafanya chombo cha starehe.

Akizungumza na Amani, Mawigi alisema kuwa, wanawake ambao wako kwenye uhusiano na Diamond au wanaotamani kuwa naye wanatakiwa kujifunza kuwa mwanaume huyo amekuwa akiwachukulia kama chombo cha starehe na akichoka anachukua mwingine hivyo wasiendelee kumkubali.

“Kwani Diamond ana nini cha dhahabu ambacho wanaume wengine hawana hadi wanawake wamgombee kiasi hicho?

“Ninawashauri wanawake wenzangu waache kugombea au kulumbana mambo ambayo hayana faida maishani mwao, wasimame, wafanye kazi wao kama wao, maisha yataenda vizuri tu,” alisema Mawigi.

Ningekuwa Mimi ndo Daimond Ningewapiga Chini Hamisa Mobetto, Wema na Zari- Yusuph Mlela

$
0
0
Ningekuwa Mimi ndo Daimond Ningewapiga Chini Hamisa Mobetto, Wema na Zari- Yusuph Mlela
MSANII wa bongo Movies, Yusuph Mlela amefunguka na kusema angekuwa yeye ndo’ Diamond Platinumz, basi asingekuwa na uhusiano na Zari, Hamisa Mobeto wala Wema Sepetu lakini kwa sababu Diamond ndiyo maisha aliyoyachagua basi hana budi kuendelea nayo.

“Kiukweli mimi siwezi kumshauri kitu, Diamond ana maisha yake na maamuzi yake pia, kwa hiyo yeye afurahie tu maisha yake its ok, mimi siwezi kumpangia. Ningekuwa mimi nisingekuwa nao wote (Zari, Mobeto wala Wema), siyo kwamba siwapendi, kwanza sitembei na watu maarufu ninatoka na watu wa kawaida tu,” alisema Mlela.

Mahakama Kuu Yaiamuru Halotel Kumlipa Zaidi ya Milioni 68 Mwanamke Waliyemuita ‘Kahaba’

$
0
0
Mahakama Kuu Yaiamuru Halotel Kumlipa Zaidi ya Milioni 68 Mwanamke Waliyemuita ‘Kahaba’
Mahakama Kuu imeamuru mwanamke aliyetimuliwa katika hoteli moja ya kifahari kwa kudaiwa kuwa kahaba alipwe fidia ya dola 30,000 za Marekani ambazo ni zaidi Milioni 68 za Kitanzania katika Mahakama kuu ya Kenya iliyopo Nairobi.

Jaji Msagha aliitaka hoteli ya Intercontinental kulipa fidia ya milioni 2 na mwanasheria mkuu wa serikali milioni 1 kwa Winfred Clarke kwa kumdunisha na kumharibia jina.

Tukio hilo lilitokea miongo miwili iliyopita mwanamke huyo alipofika hotelini kwa nia ya kufurahia kinywaji akiwa na rafiki yake kabla ya kusimamishwa na mlinzi wa hoteli kwa sababu hakuwa ameandamana na mwanaume.

Clarke hata hivyo, alienda hadi eneo la kuuzia vileo ambapo aliagiza bia mbili kabla ya kulazimishwa kulipa “ada ya kujisitiri” ambayo hakuelewa ni kwa nini alitakiwa kulipa.

Baadaye, alitolewa kwa nguvu kutoka hotelini humo na kuzuiwa kukaa eneo ambalo wageni wanakaa wanapongojea teksi, kabla ya polisi kuitwa na kumkamata ambapo alizuiliwa kwa siku mbili.

Nitamsaidia Wema Lakini Siyo Zari- Kajala

$
0
0
Nitamsaidia Wema Lakini Siyo Zari- Kajala
STAA wa Bongo Movies, Kajala Masaja ‘Kay’ amesema anaweza kumsaidia jambo rafiki yake wa kitambo Wema Sepetu lakini siyo mzazi mwenzake na Diamond, Zari kwani hamjui wala hajawahi kumsaidia kwa lolote.



Kajala amesema hayo wakati akipiga Stori na Global TV Online usiku wa kuamkia leo kwenye Bethidei ya Gabo Zigamba, baada ya kuhojiwa iwapo ikitokea Wema na Zari wote wana matatizo na yeye Kajala akawa na nafasi ya kumsaidia mmoja wao anemsaidia yupi.



“Sijui niongee je, lakini nitamsaidia Wema, siwezi kumsaidia Zari kwa sababu sijawahi kumjua wala hajawahi kunisaidia kwa lolote,” alisema Kajala.



Siku za hivi karibuni, ukiachilia mbali Hamisa Mobeto, Wema alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kuolewa na Diamond baada ya kuachana na Zari, lakini stori za chini ya kapeti zinadati tayari Diamond amesharudiana na Zari na sasa hivi wote wapo Afrika Kusini wanajiachia na familia yao ya watoto wawili.

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Mafupi na Upungufu wa Nguvu za Kiume? Suluhisho Hili Hapa

$
0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WANA MAUMBILE MAFUPI NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME DR SITTA NDO SULULISHO LAKO tatiza, hili limekuwa likiwaasili watu wengi,sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine, kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo zipo , sababu nyingi zinazosababisha, tatizo hilo baadhi ni (i) upungufu wa vichocheo vya HORMONES ZA CETROGEN ambazo mwanaume, anapobarehe vichocheo hivi, HORMONES hizo, husaidia ukuaji wa uume

SUPER MIZIZI, ni dawa inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi utakayo na kuzibua mlija iliysinyaa,

NSHOLA ni dawa bora, ya kurudisha nguvu, za, kiume bari inatibu ,kabisa kutoa tatizo hilo, na kukupa , hamu ya , kurudia tendo, la ndoa zaidi, ya mala nne 4 ,bila kuchoka atakama unaumli ,wa mika 80,! pia ana ,dawa za ,kutibu, presha ya kupanda ,na kushuka, kisukari kuondoa, mafuta , mwilini ,na maumivu ya, mgogo kiuno, dawa zipo, matazo, ya hedhi, kwa ,wanawake hedhi, zisizokuwa na, mpangilio, na kasonono, pia , vidonda ,vya, tumbo ,(STOMACHI UCLENS) IHUSHI ndoji lako.

NKANYA ni dwa ya mvuto wa kimapenzi ,mchumba mpenzi ariyekuacha, mke mme, atakuludia kwa, mda, wa msaa3 tu , ukishaitumia atarudi ,mwenyewe bila ,ugovi tena, NKOMA ni dawa kuongeza HIPS na mguu wa bia kwa wadada .

HERBON, ni, dawa, ya kuongeza, CD4, NGAKAMA ,ni dawa ya kutibu ,miguu, kufaganzi, na ,kuwaka moto, huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa! DR SITTA, amebobea, kwa tiba asilia

DAR ANAPATIKANA MBAGALA, ZAKHEM, SONGEA BOMBAMBILI SHINYANGA, KAHAMA MJINI, KWA MAELEZO ZAIDI , PIGA SIMU 0763172670 au 0715172670

WOTE MNAKALIBISHWA, KAMA, UTAKUWA NA TATIZOUTAHUDUMIWA,

Kambi ya Upinzani yaitaka KKKT, Kanisa Katoliki kutoijibu serikali

$
0
0

Kambi ya Upinzani Bungeni, imewataka viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Kanisa Katoliki, kutoijibu serikali kuhusu barua waliyopewa na Msajili wa Vyama ya kukanusha waraka wao.

Leo June 06, 2018 Jijini Dodoma Mbunge wa Vunjo, James Mbatia akizugumza na waandishi wa habari kwa niaba ya kambi hiyo amesema mamlaka za nyaraka za makanisa hayo ni mamlaka ya kibiblia.

Amesema makanisa hayo makubwa nchini yamekuwa yakitoa huduma kubwa katika jamii hivyo kwa jambo lililofanywa na msajili wa vyama kisaikolojia wamedharauliwa.

“Sisi tunawashauri viongozi hawa wa dini kutowajibu serikali halafu tuone wanachukua hatua gani,” amesema.

Kwa upande wake Mbunge wa Kibamba, John Mnyika amesema serikali inapaswa kukanusha barua hiyo na kwamba jambo hilo halitakwisha watatumia kanuni za bunge ndani siku 10 kuomba miongozo hadi pale serikali itakapotoa majibu.

Hapo awali Bungue Mbatia alihoji suala hilo wakati wa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Hata hivyo Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson alimkia kifua Waziri Mkuu akisema kwamba itakumbukwa kuwa Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea alihoji kuhusu masuala ya dini lakini Spika Job Ndugai akamwambia waziri mkuu hawezi kujibu masuala ya imani.

Wasanii 6 Kutoka BSS Wanaofanya Vizuri, Kwa Mujibu wa Madam Rita

$
0
0

Chief Judge wa Shindano la Bongo Star Search (BSS), Madam Rita Paulsen ametaja wasanii sita kutoka kwenye shindano hilo ambao kwa sasa wanafanya vizuri.



Madam Rita amesema si kweli wasanii kutoka BSS hawafanyi vizuri ila wanafanya kwa namna nyingine kutokana na siasa zilizopo kwenye muziki wa Bongo Flava kwa sasa.

Wasanii aliowataja kufanya vizuri ni pamoja na Walter Chilambo, Peter Msechu, Kala Jeremiah, Haji Ramadhani, Frida Amani na Angel Kato.

“Wapo wengi wanafanya vizuri, wapo kama Walter Chilambo yupo kwenye gospel kama wewe si mtu wa gospel utajuaje kama ni big star. Kuna wengine wapo kwenye mabendi, Haji Ramadhani ni mtu muhimu kwenye Twanga Pepeta, kuna Peter Msechu, Kala Jeremiah,” amesema.

“Kuna ma-presenter wa radio, Frida Amani wimbo wake kwa sasa unafanya vizuri kila mahali, Angel Mary wanafanya vizuri,” Madam Rita ameiambia Wasafi TV.

Madam Rita Paulsen amesisitiza kuwa wote hao wanafanya vizuri ila inategemea anayewatazama anataka awasikie wapi wakifanya vizuri ila anachojali si wao kusikika tu bali ni kuona na maisha yao yamebadilika kitu ambacho wamefanikiwa.

Nandy adai amekatazwa na Boyfriend wake kumzungumzia Bill Nass, kisa?

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo, Nandy amedai kuwa amekatazwa na Boyfriend wake kuzungumzia kile kilichotokea kati yake na Bill Nass.

Muimbaji huyo ameiambia U-Head, Clouds FM kuwa hata alipokuwa katika media tour nchini Kenya ni kitu ambacho alikuwa anaulizwa mara kwa mara na kukiri kuwa kilikuwa kinamsumbua.

“Kawaida nimefanya interview hayo maswali yalikuwepo, hakikuwa kitu kidogo kilienda mbali sana na kilinisumbua kiukweli lakini yameshapita,” amesema.

“Unavyoniuliza maswali sijui ya Bill Nass nimeshakatazwa na Boyfrind wangu kuyaongelea mambo hayo,” amesisitiza Nandy.

Utakumbuka April 12, 2018 Nandy na Bill Nass walikamata headlines za kiburudani Bongo hasa katika upande wa udaku kufuatia kuvuja kwa video yao ikiwaonesha wakiwa faragha. Suala hilo lilifika hadi bungeni na polisi waliweza kuwahoji wahusika.

Peter Msigwa, DC Kasela Warushiana Maneno 'Machafu' Mitandaoni Kisa Msiba wa Mapacha

$
0
0
Siku moja baaada ya pacha walioungana, Maria na Consolata kuzikwa, kumetokea mzozo baina ya Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela katika akaunti ya mtandao wa kijamii wa Twitter.

Mzozo ulianza jana Juni 6, 2018 baada ya Msigwa kuandika twiti akisema: “DC Kasesela anafanya siasa kwenye msiba wa Maria na Consolata. Bila aibu hajaacha kutaja jina langu akidhani kwa kufanya hivyo itamsaidia kisiasa. Kasesela usitumie huo msiba kwa faida ya kisiasa. Shame on you! Umeshindwa hata kumtambua Meya wa mji.”

Asubuhi ya leo Juni 7, 2018 Msigwa ameandika tena twiti akisema: “DC Kasesela kila wakati is looking for attention! niliwahi kusimuliwa watu wa aina hii! Kukiwa na harusi anatamani awe bwana harusi! Kukiwa na ubatizo anatamani awe mbatizwaji! Kukiwa na msiba anatamani awe jeneza. Boys are always looking for attention, men always have attention.”

Akijibu hilo, Kasesela akaandika: “Mheshimiwa Mbunge is this Real you?! Nimesema neno gani baya?”

Msigwa akaandika: “Umesema mbele ya hadhara kuwa mimi sijatuma rambirambi ulijuaje? Kwani mimi nilipaswa kukupa wewe ? Hao wabunge wa CCM hawajakuambia kama nilichangia! Kwani unadhani watu wa Iringa hawamjui mbunge wao?”

Kasesela: “Omba re play you should not stress yourself nimegundua hukunisikia umeambiwa.”

Msigwa: “Nimekusikia watu walikushangaa sana unaposema eti Rita ni mbunge wa Iringa! Na walikupinga! Umeshindwa kumheshimu Meya wa Mji! Hata wewe hustahili heshima.”

Kasesela: “Sasa Rita Kabati ni mbunge wa wapi.”

Msigwa: “Acha ushamba”

Kasesela: “Mimi nimekubali ushamba toka jana Kaka”

Msigwa; “Kwa Kweli washamba wanaviherehere!”

Dawa Bora za Nguvu za Kiume na Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa

$
0
0
Baada ya utafiti wa muda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka sasa

MWASELE HERBAL CLINIC. inakuletea suluhu juu ya matatizo haya kwa kutumia dawa za

FULL POWER .ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu zakiume. dawa hii ina mchanganyiko wa kutosha kuzalisha vichocheo vingi vya hormone za gestrogen ziwemo vitamin B6&B1, vitamini E pamoja madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na muzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi na kuchelewa kufika kileleni zaidi ya dakika 20-30. ZAT 50 inarudisha maumbile ya uume yaani kurefusha na kunenepesha ulefu nchi 3-7, upana cm, 3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukitumia maumbile yatabaki kuwa hivyo siku zote . pia tunatibu matatizo mengine kama presha, kisukari , ngiri ,chango la tumbo,tumbo kujaa gesi, kutokupata choo vizuri,miguu kuwaka moto,matatizo ya uzazi, bawasili namagonjwa yazinaa kama kisonono nakaswende.

Tunapatikana DAR ES SALAAM. SHINYANGA NA ZANZIBAR. kwa wakazi wa dar es salaam utaletewa huduma hii popote ulipo . wa mikoani tunawatumia kwanjia ya mabasi .

Wasiliana nasi kwa sim no 0717702227 au 0754568767.DR . SAGUDA nyote mnakaribishwa

Menejimenti ya rapa Falz yawajibu waislamu wanaotaka afute video ya wimbo wake wa ‘This is Nigeria’

$
0
0

Baada ya kikundi cha waislamu cha The Muslim Rights Concern (MURICO) cha nchini Nigeria kumtaka rapa Falz kufuta video ya wimbo wake mpya wa ‘This is Nigeria’, hatimaye uongozi wa rapa huyo umekijibu kikundi hicho.

Uongozi huo umesema kuwa hakuna sehemu yoyote katika sheria za Nigeria inayokataza mtu kucheza akiwa amevaa Hijab hivyo kikundi hicho labda kina lengo lingine juu ya msanii wao.

“Hakuna chochote ambacho tunaweza kusema kwa sasa, zaidi ya kuwaeleza kuwa hatuwezi kufuta video hiyo kwa kile tunachoona kuwa hakuna tatizo.  Na kama kutakuwa na tatizo basi waende mahakamani nadhani huko tutaongea vizuri zaidi,“amesema Femi Soro moja ya viongozi wa Menejimenti ya FALZ.

Juzi waislamu nchini Nigeria walimpa siku 7 rapa Falz kufuta video ya wimbo huo kwenye mtandao wa YouTube wakidai kuwa ameidhalilisha dini ya Kiislamu kwa kuwavalisha wanawake hijab na kuwachezesha kwenye video hiyo.

Hana Hamu ya Kufanya Mapenzi na Mimi..Naomba Ushauri

$
0
0
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 30, nina mpenzi wangu wa muda mrefu toka 2014 japo mapenzi yetu yamekuwa hayana muendelezo muzuri kutokana na tabia za huyu mwenzangu. Tulianza mahusiano yetu vizuri sana baadae mwenzangu alibadilika ghafla, nikaja kugundua alikuwa na mahusiano na wanaume wengine (zaidi ya mmoja) tukawa tumepotezana kwa mda kidogo coz alikuwa hapokei simu wala kujib text zangu alafu akawa ni mtu wa kusafiri sana kumbe alikuwa anasafiri na hao mabwana zake, siku nimekutana nae nilimuona na dalili za mimba roho iliniuma sana, mwanzoni alidanganya baadae akakubali akawa ametoa hiyo mimba akaomaba nimsamehe kwa sababu nampenda sana tena sana nikawa nmemsamehe.

Tukawa pamoja kwa mda mfupi baadae alianza tabia yake ya kuruka ruka na starehe kwa sana, niliamua kumuacha japo roho ilikuwa inaniuma alafu yeye hata hajali kila kitu kwake poa tu. Baadae alirudi akaanza kunitafuta akaomba msamaha kama kawaida yake, kupenda ni hatari sana jamani nilimsamehe tukaanza kuwa pamoja, alikaa kwangu kwa muda wa week, nikaanza michakato kwenda kutoa posa na mahari kwao.

Sasa alivyorudi nyumbani kwao akaanza tena unaweza mpgia simu anakuambia sipo nyumbani nipo kwa dada angu fulani, au kwa bibi nitarudi kesho, au nipo hospitali bibi anaumwa baadae simu inapotea hewani hata siku mbili akipatika anakuambia huku kijijini simu ilizima charge. Sasa kilichonichosha zaidi sasahivi hana hata hamu ya mapenzi kabisa tofauti na navyomjua mimi, huyu mpenzi wangu hapo awali alikuwa akiniona tu hutumii nguvu nyingi kumuandaa, lakini sasa hivi hata ukifanyeje hawezi kuwa tiyari hadi umpake mafuta kidogo. na unaweza kumuomba hata mwezi nzima anakuambia sijisikii, sina hamu.

Naomba ushauri wadau, nifanje ili aweze thamini hisia zangu, au hata kama nikimuacha nifanyeje coz nampenda sana huyu dada natamani awe mke wangu wa ndoa, kuna vitu huwa vinanifanya nimpende sana ni rafiki, mnataniana na kucheka, mpole ila sasa ndo hayo mambo yake, nilishajaribu kumuacha nashindwa nafuta namba kila kitu ila akinipigia tu au nikumuona tu nabadilisha mawazo.

By Von G

Kwanini Sisi Wanawake/Wasichana Wanene na Wenye Makalio Hatupati Waume wa Kutuoa?

$
0
0

Nimefanya uchunguzi yakinifu na nikajiridhisha kwa 95% kuwa sie wanawake wanene na wenye makalio makubwa huwa ni ngumu sana kuolewa, kwa nini?

1. Tunaongoza kwa kuwa vimada kwa waliooa, lakini sisi hatuolewi:
(a) Miili yetu imepitwa na wakati?
(b) Labda wanadhani tutashindwa mechi?
(c) Au Wanaogopa Kuchapiwa maana tunatamaniwa na wengi?

2. Tufanyaje ili nasi tupate wanaume wa kutuoa?
(a) Tuifanyie miili yetu diet/tujikondeshe ili tuwe wembamba,
(b)Tuanze kuwatongoza wanaume.

NALILETA MEZANI TULIJADILI.

Wabunge wa Upinzani Waingilia Kati Waraka wa Pasaka wa KKKT...... Waitaka Kanisa Kutoijibu Barua ya Serikali

$
0
0
Wabunge wa Upinzani Waingilia Kati Waraka wa Pasaka wa KKKT......  Waitaka Kanisa Kutoijibu Barua ya Serikali
WABUNGE wa upinzani wamewataka viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Kanisa Katoliki kutoijibu serikali kuhusu barua waliyopewa na Msajili wa Vyama akiwataka kukanusha waraka wao wa Kwaresma na Pasaka.



Mbunge wa Vunjo, James Mbatia, akizugumza na wanahabari kwa niaba ya kambi hiyo leo jijini Dodoma, amesema mamlaka za nyaraka za makanisa hayo ni mamlaka ya Kibiblia na kwamba makanisa hayo makubwa nchini yamekuwa yakitoa huduma kubwa ya kiroho kwenye jamii, hivyo kwa jambo lililofanywa na Msajili wa Vyama wamedharauliwa.



“Naomba niseme kwamba, tunawashauri viongozi wa dini kutowajibu serikali, halafu tuone wanachukua hatua zipi,” amesema.



Mbunge wa Kibamba (Chadema) na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Bara, John Mnyika, ameitaka serikali kukanusha barua hiyo na kwamba watatumia anuni za bunge kwa siku kumi kuomba miongozo hadi serikali itakapotoa majibu ya jambo hilo.



“Hapa Naibu Spika ametumia madaraka vibaya akimkingia kifua Waziri Mkuu Kassim Majaliwa asijibu jambo hili bungeni.  Ndani ya siku kumi sisi tutauliza maswali, tutaomba miongozo hadi serikali iwajibike, tutafanya kwa umoja wetu hadi haki ya viongozi hawa wa dini ipatikane,” amesema Mnyika.



Jana barua ilisambaa kwenye vyombo vya habari ikieleza kuwa Msajili wa Vyama nchini ameyataka makanisa ya KKKT na Katoliki kufuta waraka wao wa Pasaka na Kwaresma kwa serikali huku akimtaka Askofu Mkuu wa KKKT kufika ofisini hapo kuchukua malimbikizo ya madeni wanayodaiwa na wayalipe ndani ya siku saba.



Leo Juni 7, 2018 Mbatia alimuuliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, bungeni  akitaka kusikia kauli ya serikali kuhusu kuwataka viongozi hao wa dini kufuta waraka huo. Hata hivyo spika alikataa na kusema swali hilo haliwezi kujibiwa bungeni na Waziri Mkuu.

Taharuki Yatanda Simba Kocha Wake Atoweka Kambini Ghafla Ajulikani Alipo

$
0
0
Kocha wa Simba Atoweka Kambini Ghafla Ajulikani Alipo
Katika hali isiyotarajiwa, kocha mkuu wa Simba, Pierre Lechantre ametoweka klabuni hapo huku ikiwa haijaeleweka mara moja kama amerejea jijini Dar es Salaam ama kwao Ufaransa.

Inasemekana kwamba Lechantre amekasirishwa na kitendo cha mabosi wa timu hiyo kumchunia kumpa mkataba mpya huku kukiwa na ukosoaji mkubwa wa namna timu ya Simba inavyocheza kwa sasa hivyo kuamua kuondoka.

Habari za kutoka ndani ya Simba zimebainisha kuwa kocha msaidizi, Masoudi Djuma ndiye anakaimu nafasi hiyo kwa sasa na ndiye atakuwepo kwenye benchi wakati Simba ikicheza na Kakamega Homeboys katika nusu fainali ya SportPesa, leo Alhamisi.

Viongozi wa Simba wameshindwa kuwa na majibu wa uhakika juu ya Lechantre huku wakidai kuwa watatoa taarifa kamili mara baada ya mechi hiyo ya nusu fainali.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Said Tulily ambaye yuko na timu hiyo mjini hapa alisema watatoa taarifa kamili baada ya mchezo huo wa nusu fainali.

Lechantre alijiunga na Simba mapema mwaka huu na kufanikiwa kuipa taji la Ligi Kuu Bara walilokuwa wamelikosa kwa misimu mitano mfululizo.

Rais Museveni Apiga Marufuku Matumizi ya Mifuko ya Plastiki

$
0
0
Rais Museveni Apiga Marufuku Mifuko ya Plastiki
Rais Yoweri Museveni ameamrisha maafisa wa usalama nchini kuhakikisha kuwa marufuku ya kutumia mifuko ya plastiki nchini inatekelezwa.

Ametaka kampuni 45 nchini za kutengeneza plastiki kusitisha utengenezaji wa mifuko ya plastiki katika hatua ya kufufua marufuku ya serikali ambayo imekuwepo lakini isiyotekelezwa.

"Marufuku ya utengenezaji, usambazaji na uuzaji na matumizi haijafutiliwa mbali na inapswa kutekelezwa, alisema Museveni.

Sheria ya mwaka 2009 ya fedha inapiga marufuku "uingizaji, utengenezaji, uuzaji na utumiaji wa mifuko na magunia ya plastiki kuanzia Machi 31, mwaka 2010.

Hatahivyo kama ilivyo kwa baadhi ya mataifa yalioendelea, utekelezaji wa sheria hiyo ndio tatizo, ni nchini Uganda ni kama ambaye ziligonga mwamba kufuatia tofuati zilizoibuka miongoni mwa mawaziri nchini huku kukiwepo shinikizo kutoka kwa watengenezaji wa plastiki.

Museveni ameamrisha maafisa wa usalama nchini kuhakikisha kuwa marufuku ya kutumia mifuko ya plastiki nchini inatekelezwa

Museveni ameamrisha maafisa wa usalama nchini kuhakikisha kuwa marufuku ya kutumia mifuko ya plastiki nchini inatekelezwa
Makampuni ya kutenegenza mifuko hiyo yamelalamika kuwa kuidhinishwa kwa marufuku bila ya kuwepo kwa matumizi mbadala kunawaweka katika hali mbaa wauzaji wa bidhaa madukani kwa kutokuwana mahali pa kuwawekea wateja vbidhaa hizo.

Na pia kwamba itafunga nafasi za ajirawakati viwanda vinapunguza utengenezaji wa mifuko hiyo.

Uganda ni miongoni mwa nchi za Afrika zilizoidhinisha marufuku ya kutumia , kuuza au kutengeneza mifuko ya plastiki.

Kenya imepiga marufuku mifuko hiyo mnamo 2017 na imeorodheshwa miongoni mwa mataifa 50 yaliochukuwa hatua hiyo katika ripoti kubwa ya Umoja wa mataifa kuwahi kutolewa inayopendekeza kuwa serikali duniani zinahitaji kufikiria kupiga marufuku au kuidhinisha kodi kubwa kwa watengenezaji mifuko hiyo ya plastiki.

matumizi ya plastiki na athri zake duniani
Katika baadhi ya mataifa , kuna sheria dhidi ya matumizi ya plastiki lakini tatizo linakuwa katika utekelezaji wa sheria hizo.

Mabaki ya Ndege Iliotoweka na Abiria 10 Nchini Kenya Yapatikana

$
0
0
Mabaki ya ndege iliotoweka na abiria 10 nchini Kenya yapatikana
Mabaki ya ndege ya kampuni ya FlySax yaliopatikana katika eneo la Aberdares yameharibika vibaya kulingana na katibu wa idara ya uchukuzi Paul Maringa.

Kulingana na afisa huyo mabaki hayo ya ndege ya 208 Cesna yenye nambari ya usajili wa 5Y-CAC yalipatikana mwendo wa saa kumi na mbili alfajiri kufuatia operesheni kali ya usakaji wa ardhini uliotekelezwa na wataalam wa jeshi .


Kreni mbili za angani kutoka katika ndege za jeshi na polisi zitaongoza juhudi za uokoaji baada ya hali ya anga kuimarika.

Baadhi ya maafisa wa usalama wanaoshiriki katika operesheni ya uokoaji wa ndege aina ya Flysax katika msitu wa Aberdare
Ndege hiyo inayodaoiwa kufanyiwa ukaguzi wa mitambo mara kwa mara ilikuwa imesafiri kuelekea Homabay na Maasai Mara mapema siku ya Jumanne kabla ya safari hiyo ya kuelekea Nairobi.

Marubani wake wawili waliripotiwa kuwa na uzoefu na inahofiwa kwamba ilipaa na kuingia katika eneo lenye hali mbaya ya anga juu ya mlima wa Aberdare katika eneo la Kinangop huko Nyandarua ambapo mawimbi yake ya simu yalipatikana mwendo wa saa kumi na moja jioni siku ya Jumatano.

Mara ya mwisho ya mawasiliano kati ya marubani wa ndege hiyo na mnara wa kudhibiti ndege uliopo katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi ni wakati ndege hiyo ilipokuwa umbali wa kilomita 60 kutoka Nairobi.

Ilitarajiwa kutua katika uwanja huo wa JKIA mwendo wa saa kumi na moja jioni kufuatia safari hiyo ya saa moja kutoka Kitale.

Peter Msigwa, DC Kasela Warushiana Maneno 'Machafu' Mitandaoni Kisa Msiba wa Mapacha

$
0
0
Peter Msigwa, DC Kasela Warushiana Maneno 'Machafu' Mitandaoni Kisa Msiba wa Mapacha
Siku moja baaada ya pacha walioungana, Maria na Consolata kuzikwa, kumetokea mzozo baina ya Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela katika akaunti ya mtandao wa kijamii wa Twitter.

Mzozo ulianza jana Juni 6, 2018 baada ya Msigwa kuandika twiti akisema: “DC Kasesela anafanya siasa kwenye msiba wa Maria na Consolata. Bila aibu hajaacha kutaja jina langu akidhani kwa kufanya hivyo itamsaidia kisiasa. Kasesela usitumie huo msiba kwa faida ya kisiasa. Shame on you! Umeshindwa hata kumtambua Meya wa mji.”

Asubuhi ya leo Juni 7, 2018 Msigwa ameandika tena twiti akisema: “DC Kasesela kila wakati is looking for attention! niliwahi kusimuliwa watu wa aina hii! Kukiwa na harusi anatamani awe bwana harusi! Kukiwa na ubatizo anatamani awe mbatizwaji! Kukiwa na msiba anatamani awe jeneza. Boys are always looking for attention, men always have attention.”

Akijibu hilo, Kasesela akaandika: “Mheshimiwa Mbunge is this Real you?! Nimesema neno gani baya?”

Msigwa akaandika: “Umesema mbele ya hadhara kuwa mimi sijatuma rambirambi ulijuaje? Kwani mimi nilipaswa kukupa wewe ? Hao wabunge wa CCM hawajakuambia kama nilichangia! Kwani unadhani watu wa Iringa hawamjui mbunge wao?”

Kasesela: “Omba re play you should not stress yourself nimegundua hukunisikia umeambiwa.”

Msigwa: “Nimekusikia watu walikushangaa sana unaposema eti Rita ni mbunge wa Iringa! Na walikupinga! Umeshindwa kumheshimu Meya wa Mji! Hata wewe hustahili heshima.”

Kasesela: “Sasa Rita Kabati ni mbunge wa wapi.”

Msigwa: “Acha ushamba”

Kasesela: “Mimi nimekubali ushamba toka jana Kaka”

Msigwa; “Kwa Kweli washamba wanaviherehere!”

Kwa Mara ya Kwanza Toka Aingie Ikulu Trump Afuturu na Waislam White House

$
0
0
Kwa Mara ya Kwanza Toka Aingie Ikulu Trump Afuturu na Waislam White House
Rais Donald Trump wa Marekani kwa mara ya kwanza tangu kuingia ofisini alifuturu pamoja na waumini wa dini ya Kiislamu katika ikulu ya White House.

Ingawa White House haijatoa orodha kamili ya wageni walioalikwa kwenye hafla hiyo, waandishi wa habari waliohudhuria wamedokeza kwamba wengi wa waliokuwepo walikuwa maafisa wa serikali na mabalozi wa nchi za Kiislamu.

Ni mara ya kwanza kwa Trump kufuturu na waislamu White House baada ya kuepuka zoezi hilo mwaka jana. Kwa miongo kadhaa imekuwa kama desturi kwa marais wa Marekani kufuturu na waislamu katika ikulu wakati wa Ramadhan.

Licha ya hatua ya Trump ya kualika waumini wa dini ya Kiislamu kufuturu kwenye ikulu, mamia ya watu walikusanyika nje ya White House kupinga rais huyo kwa sera na matamshi mabaya dhidi ya dini ya Kiislamu wakati wa kampeni na hata wakati wake kama rais.

Rais huyo pia amekemewa kwa kupitisha marufuku ya usafiri dhidi ya wasafiri wanaotoka nchi za Kiislamu.
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live


Latest Images