Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Ndugu wa marehemu Sam wa Ukweli wamlaani aliyesema kafariki kwa UKIMWI, wenyewe waeleza kilichomuua

$
0
0

Ndugu wa marehemu Sam wa Ukweli wamemjia juu producer wa muziki ambaye alikuwa wa kwanza usiku wa jana kutoa taarifa za kifo cha ndugu yao kinyume na taratibu huku akitangaza kuwa marehemu alikuwa anaugua ugonjwa wa UKIMWI wa kurogwa.


Mdogo na mjomba wa marehemu Sam wa Ukweli wamesema kuwa marehemu amekufa kwa malaria na UTI na magonjwa hayo yameanza kumsumbua tangu ijumaa ya wiki iliyopita baada ya kuwasili kutoka Singida alikoenda kwenye show.

Msikilize hapa mdogo mtu na Mjomba wa marehemu wakielezea sakata hilo pamoja na mipango ya mazishi ya ambapo kesho mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda Bagamoyo kwa ajili ya mazishi.

VIDEO:


Zari Afikisha Followers Mil 4 Instagram, Aomba Kila Mtu Amchangie Dola Moja

$
0
0

Zari Afikisha Followers Mil 4 Instagram, Aomba Kila Mtu Amchangie Dola Moja
-

From @zarithebosslady - Wapendwa wangu Sina cha Kuwalipa Zaidi ya kusema ASANTENI sana kwa 4M followers.
Ninyi Ni Ma Ndugu kwangu, Mmekua Nami Bega Kwa Bega Kwenye Shida na Raha. Sasa Mnichiangieni $1 kila mtu tujenge clinic ya wanawake sehemu yoyote dar, Najua tukiipata Baba Magufuli atatupa kiwanja....😁😁 #JustSaying
PENDA SANA NYINYI.❤
THANK YOU SO MUCH FOR 4M.
LOVE YOU ALL🌹

Breaking News: Wananchi 35 watiwa mbaroni kwa kuchoma moto gari la abiria

$
0
0
Na James Timber, Mwanza
Wananchi 35 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa kosa la kuchoma gari la abiria aina ya Isuzu yenye namba usajili  T 257 BJX baada ya kugonga wanafunzi wawili na kusababisha kifo cha mmoja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amesema kuwa tukio hilo limetokea Kata ya Bugogwa wilayani Ilemela Majira ya saa 1:40 asubuhi barabara ya Igombe amesema ajali hiyo ni dereva kutokuwa mwangalifu.

"Chanzo cha ajali hiyo ni wanafunzi walikuwa wanaenda shule wakavuka barabara ndipo walipogogwa na kusababisha kifo cha Naomi Opiyo mwenye umri wa miaka 12, wa darasa la nne na majeruhi kwa mwenzake Burton Opiyo wote wanafunzi wa Shule ya Msingi Kisundi," alisema Msangi.

Kamanda alisema kuwa baada ya ajali hiyo dereva alikimbia na wananchi wakawasha moto gari hilo ambapo ni kinyume na taratibu kwani walianza kufanya shambulio kwa mwananchi aliyewakataka wasijichukulie sharia mkononi na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili.

Aidha Kamanda ametoa onyo kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwani atakayebainika anafanya vitendo hivyo atatiwa nguvuni.

Ukikutana na Simba Uso kwa Uso Fanya Hivi ili Asikutafune Mzima Mzima

$
0
0

Wataalamu wa masuala ya wanyama wanasema ukikutana na simba usimkimbie bali mtazame usoni, kwani kutokana na hilo Simba ana kawaida ya kuona aibu na kukuaacha uende zako.

Je, wewe ukikutana naye utatoka nduki au utafuata ushauri wa wataalamu?

Muone Ustadhi Ashrafu Atimize ndoto yako..Anatumia Nyota na Nguvu za Asili Kutibu

$
0
0

Muone Ustadhi Ashrafu Atimize ndoto yako. yawezekana ulizaliwa nanyota yakitajiri ila watu wabaya wameikalia mpaka sasa ikawa hufahamu chochote. Mtafute ust Ashrafu Airudishe nyota yako yakitajiri kwakupitia pete inayoendana na nyota yako. Ust Ashrafu Ananguvu zamajini katika utendaji wake.

Anauwezo wakutoa Mali kwakupitia pete nakwakupitia majini wake. Na anauwezo wakuzirudisha Mali zilizopotea kwanjia zakichawi kwakupitia Pete yakifalme Ambayo inayong'aa muda wowote nakubadilikabadilika rangi. Ust Ashrafu Ametembea baadhi ya nchi kwakuwapatia watu huduma mbalimbali. Kama vile maradhi yakisukari, presha, ukimwi, bawasiri, tezidume, mwiliwote kupooza nakutetemeka, NK. Navilevile Amewapatia wengi huduma yamvuto wa kibiashara, nayamvuto wakimapenzi.

Nawengi wametoa shukrani zao kwa ust Ashrafu namna Alivyozirudisha Ndoa zao zilizo sambaratika kwamuda mrefu. Mtafute ust Ashrafu ili akusaidie juu yamambo yako. Nahuyu ust anasaidia matatizo yauzazi, nguvu zakiume, kuwashwa mwilini, kutokwa namapere usoni nasehemu za siri, NK. Na anadawa yakumtuliza mume asiesikia nakutulia inayoitwa limbwata. Na anadawa yakumrudisha mpenzi ktk mahusiano kwamda mchache.

Na amezipatanisha familia nyingi zilizogombana. Na anauwezo wakufarakanisha maadui waliokua pamoja.

Mtafute Ustadhi Ashrafu kwa no. 0768486717-0627423037 Au Mtafute kwa whasapp 0659438578

Hizi ndio namba zake mpigie muda wowote usiogope yupo kwaajili yako. Mpigie hupate muongozo wa bure naushri. Ustadhi Ashrafu huduma zake hupatikana mahala popote utakapo muhitaji, ila sehemu kuu anapatikana Bagamoyo.

Waraka KKKT Waibua Mapya Bungeni..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya June 8

$
0
0


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya June 8

Waziri Mwijage Aipongeza Kampuni Ya Total Kwa Kuzindua Mafuta Ya Magari Rafiki Kwa Mazingira

$
0
0
Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage ameipongeza kampuni ya mafuta ya TOTAL kwa kuwa mstari wa mbele kwenye kuhakikisha kuwa watanzania wanapata mafuta bora ya vyombo vya moto.

Mwijage alizungumza jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa mafuta ya vyombo vya moto aina ya TOTAL Excellium kutoka kampuni ya mafuta ya TOTAL. Mafuta hayo yaliyotengenezwa kwa teknolojia ya ubora wa juu ya kimataifa ya TOTAL EXCELLIUM, kwa bidhaa zinazotumia mafuta ya Petroli na Diesel katika soko la Tanzania.

“Uzinduzi wa mafuta haya umekuja wakati muafaka kwani sasa tuko kwenye wiki ya mazingira na mafuta haya yanapunguza uchafuzi wa hali ya hewa utokanao na vyombo vya moto, nawapongeza kampuni ya TOTAL kwa kuwaletea watanzania bidhaa bora, na mimi na utaalamu wangu wa mafuta nafahamu hii ni hatua kubwa sana kwenye teknolojia ya kuboresha mafuta,” alisema Mwijage.

Mafuta haya mapya yana uwezo wa kusafisha injini na kuwezesha injini kufanya kazi kwa kipindi kirefu, kuwezesha matumizi kidogo ya mafuta na kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa utokanao na moshi wa vyombo vya moto.

Mafuta ya TOTAL EXCELLIUM yanapatikana katika vituo vyote vya kuuza mafuta vya kampuni ya TOTAL kwa gharama ya bei ya kawaida ya mafuta kwenye soko.

Tarik Moufaddal, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya TOTAL nchini anasisitiza, “Kuzinduliwa kwa TOTAL EXCELLIUM, katika soko la Tanzania ni hatua mpya na muhimu kwetu nchini hususani katika kufanikisha dhamira yetu ya kuingiza bidhaa bora za nishati. Tunayo dhamira ya kuwapatia wateja wetu bidhaa zenye ubora wa hali ya juu, sambamba na huduma bora kupitia mtandao wetu ambao umeenea nchini kote, uzinduzi wa TOTAL EXCELLIUM, unadhihirisha kuwa tumejipanga kuleta mapinduzi yenye kuleta manufaa katika sekta ya mafuta nchini.”

“TOTAL EXCELLIUM imetengenezwa kwa teknolojia ya juu ya kisasa ambayo inawezesha kusafisha injini, kuwezesha injini kufanya kazi kwa kipindi kirefu bila kuchoka, matumizi kidogo ya mafuta kuendesha injini, kupunguza uchafuzi wa mazingira utokanao na moshi na ni mazuri kwa matumzi ya aina zote za magari kuanzia madogo mpaka makubwa,” aliongeza Tarik.

“Uzinduzi huu ni moja ya ubunifu mkubwa wa kampuni uliolenga kuhakikisha wateja wetu wanapata bidhaa bora na kuwawezesha matumizi kidogo ya mafuta yaliyotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa ya Excellium.

"TOTAL EXCELLIUM imetengenezwa kwa ubunifu wa teknolojia za kisasa zenye kuleta ubora. Timu yetu ya wataalamu wa utafiti wamefanikisha kutengeneza mafuta haya kukidhi mahitaji ya wateja wetu wanaotumia magari ya kisasa ambayo yanahitaji umakini mkubwa katika matunzo ya injini kwa matumizi yao ya kila siku”  Mkurugenzi wa Mtandao wa TOTAL wa Nikesh Mehta.

“Zaidi ya watafiti makini na wataalamu wenye uzoefu mbalimbali wanafanyia kazi suala la kuleta bidhaa za mafuta na vilainishi vya injini na mitambo zenye ubora mkubwa zaidi katika kituo chetu cha utafiti cha Solaize,nchini Ufaransa.Wataalamu hao wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka miwili kuboresha mafuta ya TOTAL EXCELLIUM.

"Zaidi ya kanuni za kisayansi 2,300 zimefanyiwa majaribio katika maabara kwa zaidi ya masaa 6,000 na mafuta haya yamefanyiwa majaribio ya awali barabarani kwa zaidi ya masaa 8,500 sawa na kilometa 300,000.

"Haya yote yanathibitisha uhakika na ubora wa mafuta ya TOTAL EXCELLIUM na yanasafisha injini za magari na kupunguza uharibifu wa mazingira,” anasema Marsha Msuya, Mkurugenzi wa Masuala ya Ndani ya kampuni ya TOTAL.

Credit: Fullshangwe

CUF yawang'ang'ania Lipumba, Seif

$
0
0

NA FATUMA MUNA
Chama cha Wananchi CUF, kimeitaka Serikali kuunga mkono hoja ya Mbunge wa Jimbo la Chonga  Mohamed Juma Khatib, kufanya ukaguzi lazimishi wa fedha za Umma ikiwa ni pamoja na Msajili wa vyama vya siasa Jaji Mutungi, Maalim Seif, Ibrahimu  Lipumba wahojiwe walikopeleka Bilioni 2 za Chama.


Hayo yamesemwa na Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma Mbarala Maharagande wakati akiwapongeza Wabunge wa chama hicho wakiongozwa na Mhe. Khatib, kwa kutekeleza wajibu wao vizuri na kuibua ufisadi wa fedha za umma unaofanywa watu aliowaita matapeli wa kisiasa, na wasaliti ndani ya CUF kwa njia ya Ruzuku ya serikali kwa vyama vya siasa nchini.

Katika kikao cha bunge Juni 5, 2018, wakati akichangia bajeti ya wizara ya Fedha kwa mwaka wa 2018/2019, Mhe. Khatib aliomba bunge lijadili na kupitisha azimio la Katibu Mkuu wa CUF-Chama cha Wananchi Mhe. Seif Sharif Hamad ahojiwe na vyombo husika ili aeleze ni kwa nini hakufunga na kuwasilisha taarifa ya mahesabu ya Chama kwa mwaka wa fedha wa serikali ulioishia Tarehe 30/6/2016 na kueleza ni wapi zilopo takriban Tshs. bilioni 2 zinazodaiwa kulipwa kwa CUF kutoka ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa Nchini, Jaji Francis Katabazi Mutungi.

Mbarala amesema kwamba mbunge anapohoji juu ya matumizi mabaya ya fedha za serikali na kukubali mtu yeyote ambaye anaonekana kuhusika na ubadhilifu wa fedha za umma ahojiwe na kuchukuliwa hatua, Mbunge huyo anastahili kupongezwa na huo ndio utekelezaji wa jukumu la msingi la kuisimamia na kuishauri serikali.

Pamoja na hayo Mbarala amekanuasha taarifa za Seif kutowepo ofisini kwake kwa kusema kuwa "Katibu Mkuu yupo Ofisini kwake MaKao Makuu ya Chama cha CUF Mtendeni, Unguja Zanzibar akiendelea na Majukumu yake ya kila siku kama Kawaida. Kwa mujibu wa katiba ya CUF ibara ya 90 NA 93 Maalim Seif Sharif Hamad ndiye CHIEF ACCOUNTING OFFICER na wala si vinginevyo".

Hata hivyo Mbarala amesema  Lipumba, Sakaya na Kambaya wanatakiwa kuwaomba radhi Watanzania kwa wizi wa Fedha za umma walioufanya hali ya kuwa si Viongozi halali wa CUF na kwamba Baraza Kuu la Uongozi la Taifa lililoketi Tarehe 28/8/2016 liliwasimamisha uanachama na baadae Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Tarehe 27/9/2016 kuwafukuza uanachana aidha, Mkutano Mkuu Maalum wa Tarehe 21/8/2016 uliridhia Maamuzi ya Lipumba kujiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa CUF toka mwaka 2015 Agosti 5.

AliKiba Amuonya Mbwana Samatta

$
0
0

Nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, ‘Alikiba’ amemuonya  mshambuliaji wa KRC Genk, Mbwana Samatta kwa kumwambia kuwa atahakikisha timu yake inafanya vizuri watakapokutana Jumamosi katika mchezo maalum wa kuchangia elimu utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Alikiba amesema kuwa atahakikisha mpinzani wake anaondoka akiwa analia kutokana na kuchagua kikosi bora kwa ajili ya mchezo huo utakaowajumuisha wachezaji wengi wa kimataifa.

“Nitahakikisha Samatta anaondoka analia kwani kikosi changu kipo vizuri nikiwa na wachezaji wanaocheza ndani na nje ya Tanzania, tunaye Uhuru Selemani ambaye naamini kwa ushirikiano wake na wengine tutapata matokeo mazuri”, amesema Kiba.

Jumamosi, timu ya Alikiba na timu ya Samatta, zitapambana katika uwanja wa taifa ukiwa ni mchezo maalum wa kuchangia elimu.

Tanzania yaporomoka viwango FIFA

$
0
0

Tanzania imeshuka nafasi tatu katika viwango vya soka vinavyotolewa kila mwezi na Shirikisho la soka duniani (FIFA), huku timu ya Taifa ya Ujerumani ikiendelea kuwa kinara katika msimamo huo na nchi ya Tonga imeshika nafasi ya mwisho kwa dunia.


Katika orodha iliyotolewa leo Juni 7, 2018 na FIFA, imeonesha Tanzania imeshuka kutoka nafasi ya 137 mpaka 140, na kwa upande wa bara la Afrika, Tanzania ipo nafasi ya 39 huku Tunisia ikiwa kinara Afrika.

Kwa upande wa Afrika Mashariki, Uganda wameonekana kuongoza licha ya kushuka kwa nafasi nane duniani kwa kushika nafasi ya 82, huku wakifutiwa na Kenya(112), Rwanda(136), Tanzania(140), Burundi (148) na Sudan Kusini (156)

Pamoja na kushika nafasi ya 21 duniani lakini Tunisia ni namba moja kwa Bara la Afrika wakifuatiwa na Senegal ambapo kidunia wapo nafasi ya 27, Jamhuri ya kidemokrasia Kongo (38), Morocco (41), Misri (45) Ghana (47), Nigeria (48), Cameroon (49) Burkina Faso (52) na Mali (64) zipo 10 bora na Somalia ikishika nafasi ya mwisho.

Bara la Ulaya, limeendelea kuongoza ambapo nchi saba zimefanikiwa kutinga 10 bora ya mataifa bora duniani wakiongozwa na Ujerumani aliyeshika na nafasi ya kwanza na nafasi ya pili imekwenda kwa Brazil wakifuatiwa na Ubelgiji, Ureno, Argentina, Uswisi, Ufaransa, Poland, Chile na Hispania walioshika nafasi ya 10.

Auwa Mwanae Akimchapa na Fimbo

$
0
0

Jeshi la Polisi katika Wilaya ya Pader, nchini Uganda, linamshikiliwa Bwana Omony Odokonyero (30) kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mwanae mwenye umri wa miaka saba kilichotokana na kuchapwa  fimbo.


Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor limeripoti leo Juni 7 2018, katika kijiji cha Omakigira, ambapo mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Richard Odokonyero, mwanafunzi wa shule ya msingi Pader Ogom alipigwa na fimbo baada ya kukataa kwenda shule akitaka kupelekwa kwa bibi yake.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho Charles Lalobo, amethibitisha tukio hilo na kudai kuwa mzazi huyo amekuwa na tabia ya kumpiga mtoto wake mara kwa mara na siku ya tukio alikuwa akimpiga na fimbo kichwani  hivyo kupelekea kuzimia kabla ya kufariki

“Hili ni tukio ambalo halikupaswa kutokea, kuna njia nyingi za kutumia kama mzazi ili kufundisha watoto wao lakini sio kutoa athabu kali, Polisi wanapaswa kuchukua hatua kali na kuhakikisha mtuhumiwa anaadhibiwa” amesema Bwana Lalobo

Msemaji wa Jeshi la Polisi katika mkoa wa Aswa River, Jimmy Okema, amesema kuwa Jeshi hilo linamshikili mtuhumiwa katika Makao Makuu ya Polisi Pader na kuongeza kuwa endapo uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani kwa kosa la mauji.

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Mafupi na Upungufu wa Nguvu za Kiume? Suluhisho Hili Hapa

$
0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WANA MAUMBILE MAFUPI NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME DR SITTA NDO SULULISHO LAKO tatiza, hili limekuwa likiwaasili watu wengi,sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine, kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo zipo , sababu nyingi zinazosababisha, tatizo hilo baadhi ni (i) upungufu wa vichocheo vya HORMONES ZA CETROGEN ambazo mwanaume, anapobarehe vichocheo hivi, HORMONES hizo, husaidia ukuaji wa uume

SUPER MIZIZI, ni dawa inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi utakayo na kuzibua mlija iliysinyaa,

NSHOLA ni dawa bora, ya kurudisha nguvu, za, kiume bari inatibu ,kabisa kutoa tatizo hilo, na kukupa , hamu ya , kurudia tendo, la ndoa zaidi, ya mala nne 4 ,bila kuchoka atakama unaumli ,wa mika 80,! pia ana ,dawa za ,kutibu, presha ya kupanda ,na kushuka, kisukari kuondoa, mafuta , mwilini ,na maumivu ya, mgogo kiuno, dawa zipo, matazo, ya hedhi, kwa ,wanawake hedhi, zisizokuwa na, mpangilio, na kasonono, pia , vidonda ,vya, tumbo ,(STOMACHI UCLENS) IHUSHI ndoji lako.

NKANYA ni dwa ya mvuto wa kimapenzi ,mchumba mpenzi ariyekuacha, mke mme, atakuludia kwa, mda, wa msaa3 tu , ukishaitumia atarudi ,mwenyewe bila ,ugovi tena, NKOMA ni dawa kuongeza HIPS na mguu wa bia kwa wadada .

HERBON, ni, dawa, ya kuongeza, CD4, NGAKAMA ,ni dawa ya kutibu ,miguu, kufaganzi, na ,kuwaka moto, huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa! DR SITTA, amebobea, kwa tiba asilia

DAR ANAPATIKANA MBAGALA, ZAKHEM, SONGEA BOMBAMBILI SHINYANGA, KAHAMA MJINI, KWA MAELEZO ZAIDI , PIGA SIMU 0763172670 au 0715172670

WOTE MNAKALIBISHWA, KAMA, UTAKUWA NA TATIZOUTAHUDUMIWA,

Kauli ya Hali Kiba Yazua Gumzo Mitandaoni " Dini Yangu Hairuhusu Kumposti Marehemu"

$
0
0
Kauli ya Hali Kiba Yazua Gumzo Mitandaoni " Dini Yangu Hairuhusu Kumposti Marehemu"KAULI ya Msanii wa Bongo Fleva, Alikiba aliyofunguka kwa mara ya kwanza kuhusu kutowaposti wasanii au watu maarufu kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii wanapofariki akisema dini yake haimruhusu kumposti marehemu imepokelewa kwa mitazamo tofauti na mashabiki na wadau mbalimbali wa sanaa na mitandao ya kijamii nchini.



Kufuatia kauli hiyo inayotrendi mitandaoni, baadhi ya wadau wamehoji iwapo dini anayoisema inamruhusu kuzaa watoto wanne nje ya ndoa na kila mmoja akawa na mama yake, au ina mruhusu kufanya sanaa ya muziki, kutembea na wanawake na kuwaacha na mambo mengine mengi ambayo yameendelea kuibuliwa mitandaoni kufuatia kauli yake hiyo.



Akizungumzia jambo hilo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyik jana Juni 7, 2018 jijini Dar es salaam, Alikiba alisema kuwa sababu kubwa ya kutoposti picha kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii ambapo amedai kuwa kufanya hivyo ni kinyume na dini yake ya kiislamu.

Aslay Afunguka Penzi Lake na Nandy

$
0
0
Aslay Afunguka Penzi Lake na Nandy
NI kijana wa Temeke, alianza kufahamika mwaka 2011 baada ya kutoa ngoma iitwayo Nakusema, alitamba pia akiwa chini ya Band ya Yamoto Band iliyoanzishwa mwaka 2013 lakini baada ya bendi hiyo kufa mwaka 2017, alianza kufanya muziki akiwa solo.

Ana umri wa miaka 23, ana mashabiki kibao ndani na nje ya Bongo, mwezi Januari mtandao namba moja Afrika wa kusambaza nyimbo ‘online’ uitwao Not Just Ok, kutoka Nigeria ulimtaja kuwa mwanamuziki wa Bongo Fleva anayefanya vizuri zaidi nchini humo!

Nakupa zaidi; Ndani ya mwezi mmoja huachia ngoma mbili mpaka tatu, ngoma yake inayotamba kwa sasa inaitwa Nibebe, video zake nyingi hupendelea kufanyia uswazi au vijijini na anatengeneza ‘chemistry’ nzuri akikaa kwenye wimbo na mwanamuziki Nandy!

Hapo vipi? Bila shaka umenusa chochote kwa kijana huyu ambaye msikilizaji wa Muziki wa Bongo Fleva huwezi kuepuka kumsikia kutokana na fujo alizonazo za kuachia ngoma. Jina lake la kuzaliwa anaitwa Aslay Isihaka Nassoro a.k.a Dogo Aslay na kazi zake za muziki zinasimamiwa na meneja wake wa muda mrefu aitwaye Chambuso.

Dogo Aslay, hivi karibuni ameingia kwenye ‘headlines’ baada ya kuposti kwenye mitandao ya kijamii mjengo wa maana ambao wengi walijiongeza kwamba ni mjengo wake. Lakini pia mkali huyu wa ngoma ya Subalkheri Mpenzi, mara kwa mara amekuwa akiingia kwenye headlines kwa mambo mengi ikiwemo ‘life style’ yake. Kufahamu mengi kuhusu yeye huyu hapa akifanya mahojiano na Showbiz Xtra;

Showbiz Xtra: Kwanza nini siri ya video zako nyingi kufanyia uswazi na vijijini?

Aslay: Unajua mimi nimezaliwa uswazi na nimekulia uswazi. Kwa hiyo mara nyingi nimekuwa nikihitaji kuwakilisha asili yangu. Lakini ukweli ni kwamba nyuma ya hilo baada ya kutoka Yamoto, kwangu kidogo maisha yaliyumba, nikawa sina uwezo wa kufanya video nje ya nchi kama Sauz, ila niliamini sauti yangu inaweza kunibeba, na nilipotoa kazi zilipokelewa vizuri. Kwa hiyo uswazi ni mahali sahihi zaidi kwangu.

Showbiz Xtra: Kwa hiyo huna mpango kabisa wa kutoka zaidi ya hapo kufanya video?

Aslay: Mipango ipo, mwaka huu ni mwaka wa maajabu, watu wategemee makubwa kwa maana mbali na uswazi tutakwenda huko ambako mashabiki wetu wanapenda kuona pia tunafanya kazi.

Showbiz Xtra: Mtandao wa Not Just Ok, ulikutaja kuwa unasikilizwa zaidi Afrika Magharibi na ukaahidi kufanya kazi na wewe, mipango ipo vipi?

Aslay: Mipango ipo chini ya menejimenti yangu wao ndiyo wanaweza kuizungumzia zaidi.

Showbiz Xtra: Hapo awali umezun-gumzia baada ya kutoka Yamoto Band maisha yaliyumba, tofauti zaidi ni ipi kipindi upo na Yamoto na sasa ukiwa solo?

Aslay: Hakuna tofauti zaidi, labda kipato kule nilikuwa ninapata kipato kidogo sasa napata zaidi lakini maisha ni yaleyale.

Showbiz Xtra: Kuhusu kipato unatajwa kuwa miongoni mwa wanamuziki wenye mkwanja mrefu kwa sasa, ikiwa ni pamoja na kuishi ‘luxury life’, tuweke wazi una mkwanja kiasi gani benki na mali gani hasa unamiliki?

Aslay: Mungu anajaalia kwa kiasi chake, lakini siwezi kuweka wazi juu ya pesa ninazomiliki wala mali, lakini maisha ninayamudu kwa kupitia kipaji changu.

Showbiz Xtra: Mjengo uliyoposti hivi karibuni ni wako na upo maeneo gani?

Aslay: Kuna mipango mingi sana mwaka huu nitaiweka wazi kwenye kikao na waandishi wa habari wote, hata hili tutalizungumzia hapo.

Showbiz Xtra: Lakini mashabiki zako wangependa kufahamu kwa sasa, weka wazi hata kidogo?

Aslay: Wawe wavumilivu kila kitu kitakuwa wazi.

Showbiz Xtra: Vipi kuhusu nyumba uliyopewa kipindi kile na uongozi wa Yamoto Band, bado unaimiliki au nini kinaendelea kwenye nyumba hiyo?

Aslay: Tuzungumzie zaidi kazi yangu ya muziki.

Showbiz Xtra: Unahusishwa kutoka na wanawake wanaokuzidi umri, umewahi kuhusishwa kuwa na uhusiano na Vick Kamata, hili lina ukweli kiasi gani?

Aslay: Halina ukweli wowote.

Showbiz Xtra: Lakini pia unahusishwa kutoka kimapenzi na Nandy, hili je unalizungumziaje?

Aslay: Nandy ninafanya naye kazi tu sina uhusiano naye.

Showbiz Xtra: Malizia kwa lolote.

Aslay: Yaah! Mashabiki wangu wategemee mambo makubwa, kuna picha nimeposti mtandaoni za mwanamke anayeonekana mjamzito ni projekti yangu mpya, vitu vingi vinakuja mwaka huu.

Zari Kuwasaidia Wanawake wa Dar ....... Ajipanga Kujenga Kliniki ya Wanawake

$
0
0
Zari Kuwasaidia Wanawake wa Dar ....... Ajipanga Kujenga Kliniki ya Wanawake
Mwanadada Zari the boss lady ameingia tena kwenye headlines leo June 7,2018 baada ya kuwashangaza mashabiki kwa kuomba mchango wa dolla 1 ambayo ni shillingi 20,00 ya Kitanzania kwaajili ya kujenga kliniki ya wanawake DSM baada ya kufikisha mashabiki Milioni 4 katika mtandao wa instagram.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Zari ameandika “Wapendwa wangu Sina cha kuwalipa zaidi ya kusema ASANTENI sana kwa 4M followers. ninyi ni ndugu kwangu, mmekua nami bega kwa bega kwenye shida na raha”

“Sasa Mnichiangieni $1 kila mtu tujenge clinic ya wanawake sehemu yoyote dar, Najua tukiipata Baba Magufuli atatupa kiwanja….😁😁 #JustSayingPENDA SANA NYINYI.❤THANK YOU SO MUCH FOR 4M.
LOVE YOU ALL🌹”



Zari ametoa mawazo hayo na kusema kuwa endapo mashabiki hao millioni 4 watafanikiwa kufikisha kiwango flani cha fedha basi Rais JPM hatoshindwa kutoa kiwanja kwaajili ya kujenga kliniki hiyo itakayowasaidia wanawake lakini hajaweka wazi itakuwa inahusika na kutibu magonjwa gani zaidi.

Ghana Yavunja Chama cha soka Kutokana na Tuhuma za Rushwa

$
0
0
Ghana Yavunja Chama cha soka Kutokana na Tuhuma za Rushwa
Ghana imevunjilia mbali chama cha soka baada ya rais wake kunaswa katika video akionekana akipokea 'zawadi ya pesa'.

Kwesi Nyantakyi alipigwa picha akipokea $65,000 kutoka kwa mwandishi habari mpekuzi aliyejifanya kuwa mfanyibiashara aliye na hamu kubwa kuwekeza katika soka Ghana.

Mpaka sasa hajasema chochote kuhusu tuhuma hizo.

Waziri wa michezo Isaac Asiama amesema chama hicho 'kimevunjiliwa mbali mara moja' mtandao wa GhanaWeb umeripoti.

Waandishi wanasema uchunguzi huo uliofanywa na mwandishi habari anayekumbwa na mzozo Anas Aremayaw Anas umezusha maswali kuhusu soka barani Afrika.

Katika makala hiyo ndefu, iliopewa jina 'wakati ulafi na rushwa zinapokuwa kawaida', ilikabidhiwa kwa maafisa wa serikali mwezi uliopita na kuonyeshwa wazi mbele ya umma kwa mara ya kwanza siku ya Jumatano.

Amesema hatua za muda za kuongoza soka Ghana zitatangazwa hivi karibuni, kukisubiriwa kuundwa chama kipya.

Nyantakyi ni makamu wa rais wa shirikisho la kandanda Afrika na pia mwanachama katika baraza la Fifa - taasisi inayosimamia soka duniani.

Tangu achukuwe uongozi wa chama cha GFA, ametuma ujumbe mkuu dhidi ya kupambana na rushwa.

Hatahivyo katika makala hiyo ya upekuzi inamuonyesha akiweka pesa hizo $65,000 "za kununua vitu" katika mfuko mweusi wa plastiki.

Trump Atoa Maneno Makali Kuelekea Mkutano wa Mataifa Tajiri G7

$
0
0
Trump Atoa Maneno Makali Kuelekea Mkutano wa Mataifa Tajiri G7
Kumekuwa na maneno makali kutoka kwa Rais Donald Trump kuelekea mkutano wa mataifa tajiri G7 unaotarajiwa kufanyika nchini Canada na, kwamba inatoza ushuru mkubwa kwa bidhaa zitokazo Marekani na kusabisha mazingira magumu yasiyoenda na sera za kifedha.

Kitendo cha Trump kuongeza ushuru katika bidhaa za chuma kumemuweka katika mazingira ya kutofautiana na mataifa wanachama wa G7.

Akizungumza awali na waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau mjini Ottawa, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliwaambia waandishi wa habari kwamba watatumia mkutano ujao wa G7 kumshawishi rais Trump dhidi ya msimamo wake kibiashara.

Nitarudia kumwambia rais Trump kwamba hatua alizochukua hazina manufaa hata kwa uchumi wa taifa lake. Kwa mimi hili ni jambo lililowazi, huwezi kuanzisha vita vya kibiashara na washirika wako.

Sisi sote tunashirikiana katika mzozo wa Syria na Iraq na maeneo mengine duniani.

Ni washirika na tunabadilishana taarifa, majeshi yetu yanashirikiana kulinda uhuru wetu.

Katika mazingira ya kimataifa tunayokabiliana kwa siku za leo hatuwezi kuanzisha vita vya kibiashara miongoni mwetu.

Nitajaribu kumshawishi kurejea katika hali ya kawaida kibiashara na kuondoa hali hii ya hofu kibiashara."Anasema Macron.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ni rais wa pili Afrika kulakiwa na Donald Trump Marekani
Hata hivyo Macron amesisitiza kuwa bado muungano wao unaweza kusonga mbele hata bila Marekani kama italazimika kuwa hivyo.

" Labda Rais Trump hajali kuhusiana na kujitenga kwake, lakini hatujali tupo tayari hata kuwa mataifa sita, kama itabidi kwa sababu mataifa hayo sita yanawakilisha umoja wetu na hadhi yetu yenye manufaa kwa mujibu wa historia ya muungano huu na dunia ya sasa."ameongeza Macron

Hatua ya hivi karibuni ya Rais Trump ya kuongeza ushuru kwa bidhaa za washirika wake imezua mzozo mpya wa kibiashara.

Yanga Yampelekea Barua Manji Kisa Hiki Hapa

$
0
0
Yanga Yampelekea Barua Manji Kisa Hiki Hapa
MAANDALIZI ya Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Yanga yamekamilika kwa asilimia kubwa huku ikipanga kutoa mwaliko maalum kwa aliyekuwa mwenyekiti na mfadhili wao Yusuf Manji.



Yanga imepanga kufanya mkutano huo Jumapili hii kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi, Masaki jijini Dar es Salaam.



Akizungumza na Championi Ijumaa, Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa alisema tofauti na Manji wamepanga kuwaandikia barua ya mwaliko viongozi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.



“Baadhi ya ajenda zitakazowasilishwa kwenye mkutano huo ni pamoja na ushiriki wa Yanga katika michuano ya kimataifa ikiwemo hatua tuliyofikia kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho, Mapato na Matumizi, bila ya kusahau mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji.



“Pia, suala la uchaguzi wa kujaza nafasi zilizokuwa wazi huenda likawasilishwa kupitia mengineyo ingawa kuna uwezekano mkubwa kwa ajenda hiyo kuondolewa ili kuwapa nafasi wanachama kujadili masuala muhimu,” alisema Mkwasa ambaye amewahi kuwa kocha wa Yanga.



Manji ni kati ya wanachama wenye nguvu kubwa kwenye timu hiyo ya Jangwani na baadhi wanaamini kuwa anaweza kuwasaidia kutoka kwenye taabu walizonazo sasa za kiuchumi kama atakubali kurejea.

Hivi Ndivyo Kocha wa Simba Alivyoonyesha Jeuri

$
0
0
Hivi Ndivyo Kocha wa Simba Alivyoonyesha Jeuri
Kocha Mfaransa Pierre Lechantre hakuwahi kudumu na timu zaidi ya mwaka mmoja, wakati huo Klabu ya Simba nayo imekuwa na kawaida ya kutokudumu na kocha kwa kipindi cha mwaka mmoja au zaidi katika miaka ya hivi karibuni.


Kocha Joseph Omog peke yake ndiye aliyedumu kwa mwaka mmoja na zaidi, Mcameroon huyo aliiweza Simba kurejea kwenye michuano ya kimataifa baada ya kukosa kwa miaka minne, Simba ilianza timua timua ya makocha tangu msimu wa 2011/12.

Uongozi wa Simba ulitangaza kumuajiri Mfaransa Lechantre kuwa kocha wa klabu hiyo akichukua mikoba ya Mcameroon Joseph Omog aliyetimuliwa katikati ya msimu uliopita wa 2017/18, lakini taarifa ni kuwa huenda Mfaransa huyo akafungashiwa vilago  Simba baada ya kutokuwa na maelewano mazuri na uongozi.

Kwa mujibu wa Mtandao wa www.transfermark.hezrog.kr.com  unaojihusisha na kutoa takwimu za masuala mbalimbali ya michezo umeonyesha kocha Lechantre ana wastani wa kufundisha timu si chini ya mwaka kabla ya kuondoka ama kutimuliwa.

Mfaransa huyo aliwashangaza watu pale alipoamua kuvunja mkataba wake wa kuifundisha timu ya taifa ya Senegar wiki mbili baada ya kukubali kuchukua jukumu hilo mwaka 2012.

Pierre Lechantre alianza kufundisha soka barani Afrika na timu ya taifa ya Cameroon, (Indonitable Lions) kuanzia Januari 1, 1999 hadi Juni 30, 2001 ni sawa na siku (911).

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo

$
0
0
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images