Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Abdul Nondo Afunguka Wanafunzi Bungando Kufukuzwa Chuo

$
0
0
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), wameuomba uongozi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya Bugando, kuwarudisha chuoni wanafunzi 10 waliofukuzwa na kusimamishwa chuo kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo kutaka wanafunzi walipe ada elekezi ya Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU).

Aidha, umedai kuwa kwa kushirikiana na taasisi nyingine kama Kituo cha sheria na Haki za Binadamu (LHRC), wataangalia hatua muhimu zaidi, kati ya kukata rufaa chuoni kama ilivyoelekezwa katika sheria za wanafunzi, kupinga uamuzi uliofanyika au kwenda mahakamani.

Wanafunzi hao waliofukuzwa wamo viongozi wa Serikali ya Wanafunzi akiwamo aliyekuwa Rais wa Wanafunzi, Timoth Stephen, aliyekuwa Spika wa Bunge la Wanafunzi 2016/17, Godfrey Lameck na wengine nane waliosimamishwa kwa muda wa miezi tisa.

Wanafunzi hao wanadaiwa kupinga baadhi ya mambo chuoni hapo ikiwamo kuondolewa kwa fedha za faini kwa wanafunzi waliochelewa kulipa ada na kupandisha ada bila kupitishwa na TCU na kukubaliwa na wanafunzi wenyewe.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana  Jumapili Juni 10, Mwenyekiti wa TSNP, Abdul Nondo, amesema  kutokana na hali hiyo wanatarajia kuandika barua kwa kushirikiana na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), kwenda Wizara ya Elimu na TCU kupinga hatua zilizochukuliwa dhidi ya wanafunzi hao.

“Pia tunaomba Wizara ya Elimu na TCU, kuratibu na kutofumbia macho vyuo vya aina hii ambavyo hujiamulia kwa matakwa yao wenyewe, hivyo vyuo vinapaswa kufuata taratibu na sheria zilizowekwa.
“Tunawaomba wadau wote wa elimu, viongozi wakiwamo wabunge, taasisi binafsi na Watanzania kwa ujumla kupinga kwa nguvu zote suala hili na kuomba kwa pamoja ili wanafunzi hao warudishwe chuoni kwani nchi bado inahitaji wasomi wakiwamo madaktari ambao nchi inawasomesha hivyo haiwezekani iwapoteze kwa mtindo wa aina hiyo.

Unamkumbuka Ronaldo De Lima? Apewa Shavu Nono Kombe la Dunia Mwaka Huu

$
0
0
NGULI wa soka wa zamani Ronaldo De Lima wa Brazil, amepewa majukumu ya kuzindua rasmi fainali za Kombe la Dunia 2018 kwenye mechi ya ufunguzi kati ya wenyeji Urusi dhidi ya Saudi Arabia Alhamisi ya Juni 14.

Kwa mujibu wa FIFA Ronaldo atakuwa na jukumu la kupeleka uwanjani Kombe la Ubingwa wa Dunia ambalo mataifa 32 yaliyofuzu yatakuwa yanaliwania. Ronaldo atatambulisha Kombe hilo tayari kwa kufungua mashindano hayo ambayo yatamalizika Julai 15.

 Mbali na Ronaldo shughuli nzima ya burudani kwenye ufunguzi huo itasimamiwa na mwimbaji wa Pop kutoka nchini Uingereza Robbie Williams ambaye ataungana na msanii wa Urusi Aida Garifullina.

 Seherehe za ufunguzi wa fainali hizo zitaanza majira ya saa 6:00 mchana kwenye uwanja wa  Luzhniki jijini Moscow. Urusi na Tanzania zinaendana kwa saa isipokuwa katika mij kadhaa.

 Ronaldo De Lima amechukua Kombe la Dunia mara 2 akiwa na timu yake ya  taifa Brazil mwaka 1994 na 2002. Pia nguli huyo allibuka mfungaji bora wa fainali za mwaka 2002 kwa kufunga jumla ya mabao 8.

TAMBUA Faida Kuu 4 Utakazozipata Kama Ukiacha Kulala na Simu Yako Kuanzia Leo..!!!

$
0
0
Wengi wetu naamini tumekuwa na kajitabia kakulala na karibu na simu usiku kwenye vitanda vyetu pasipo kufahamua madhara ya kijitabia hicho.

Sasa leo ninayo mambo kadhaa yakukwambia msomaji wangu wa www.dkmandai.com kuhusu hii tabia ya kulala na simu usiku.

Zifuatazo ni faida utakazozipata endapo utaacha kulala na simu usiku kitandani kwako.

1.Utalala usinginzi mzuri na wa kutosha.

Inaaminika kuwa mtu ambaye hulala karibu na simu  usiku hulala usingizi wa mang'amng'amu kwa kuwa muda mwingi huwa akihisi huenda kunasimu itaingia. Hivyo endapo kuanzia leo ukiacha kulala na simu usiku itakusaidia kulala usingizi mzuri na wa kutosha usiku.

2. Hautakuwa mtumwa wa msongo wa mawazo tena

Kwa kawaida unapolala na simu unakuwa unamawazo mengi pengine bila wewe mwenyewe kujijua huenda unawaza kwanini fulani haja kupigia usiku huo au atakupigia saa ngapi kukwambia usiku mwema hivyo unajikuta unajipatia msongo wa mawao usio na sababu na hivyo kuathiri afya yako bure. Ili kuondokana na hilo ni vyema kuweka mbali simu yako wakati wa kulala au kuweka silent kabisa.

3. Utafanya kazi / biashara zako vizuri

Kwasababu sasa unapoacha kulala na simu inamaana utapata mda mzuri na wakutosha wa kulala vizuri hivyo hata kazi zako au biashara utazifanya kwa ufanisi zaidi.

4. Utajisikia mwenye afya zaidi

Kwa sababu utakuwa unalala vya kutosha na watu wenye kulala vizuri huwa ni wenye afya.

Huyu Hapa Muuza Madawa ya Kulevya Aliyependwa na Wananchi Mpaka Kupewa Jina la Yesu na Mlinzi wa Amani

$
0
0
TAJIRI WA UNGA AKAWA MWEMA MPAKA AKAITWA YESU

Christopher Coke a.k.a Dudus, ni tajiri wa dawa za kulevya, akiongoza genge la Shower Posse.

Genge hilo na mtandao mzima wa unga, Dudus au President alirithi kutoka kwa baba yake, Lester Coke a.k.a Jim Brown au Ba-Bye aliyeuawa gerezani mwaka 1992.

Shower Posse makao makuu yake yapo Tivoli Gardens, Kingston, Jamaica.

Dudu alikuwa mtu mwema. Alisaidia fedha familia maskini, alilipia ada wanafunzi ambao wazazi wao hawakuwa na uwezo, zaidi alitengeneza ajira nyingi kwa vijana.

Hayo yalisababisha apendwe sana. Dudus aliitwa Rais wa Tivoli Gardens, alilindwa na kila mwananchi. Serikali ya Jamaica pia ilimlinda, maana alikuwa mfadhili wa viongozi.

Marekani ilitaka Dudus akamatwe lakini Serikali ya Jamaica haikutekeleza.

Dudus alipokamatwa na Marekani mwaka 2010, kwananchi wa Jamaica, hususan wakazi wa Tivoli Gardens, waliingia mitaani na kuandamana, wakitaka Dudus aachiwe huru.

Wananchi walikuwa na mabango yaliyoandikwa kuwa Dudus ni mlinzi wa amani ndani ya Tivoli Gardens, hivyo aachiwe. Wapo waliokwenda mbali zaidi na kuandika kwamba kumkamata Dudus ni sawa na alivyokamatwa Yesu kwa sababu ni mtu safi.

Wananchi wa Jamaica, hasa wa wakazi wa Tivoli Gardens, walikuwa hawaambiwi kitu kuhusu Dudus. Tuhuma zote za kuhusika na dawa za kulevya, waliona ni uzushi.

Ijumaa ya Juni 15, 2012, Mahakama ya Kuu ya New York, ilimhukumu Dudus kifungo cha miaka 23 jela. Miaka 20 ikiwa kwa kosa la kupanga njama na kufanya biashara haramu na miaka mitatu kwa kosa la kuuza bunduki Marekani bila utaratibu.

Sheria ya Marekani ni kufilisi mali zote za wauza dawa za kulevya pindi wanapokutwa na hatia, lakini imekuwa vigumu kumfilisi Dudus, maana uwekezaji wake wote ameufanya Jamaica ambako Serikali inamlinda.

Hata sasa, genge la Shower Posse linaendelea na kazi ya usafirishaji wa bangi, cocaine na silaha kwenda Marekani, japokuwa bosi wao yupo jela.

Ipo hofu kuwa hata baada ya Dudus kumaliza kifungo jela, huenda Serikali ya Marekani isimwachie huru kwa sababu ya hofu kwamba atarudi kazini kwake na kuzidi kuwaangamiza Wamarekani kwa kuwauzia dawa za kulevya na silaha haramu.

Huyo ndiye Dudus wa Tivoli
By @luqmanmaloto

Wasiliana na Dr Mabula Anatibu Upungufu wa Nguvu za Kiume, Busha na Matatizo ya Maumbile Madogo kwa Mwanaume

$
0
0
TUNATIBU NA KUPONESHA KABISA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME UUME MDOGO BUSHA BILA KUPASUA PRESHA VIDONDA VYA TUMBO
Asilimia kubwa ya wanadamu wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali na wapo waliongahika sehemu mbalimbali bira MAFANIKIO MABULA CLINIC ni kituo cha tiba asilia kilichopo mbagara zakhemu njia kuu ya JESHINI JE HUNAUPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME AU UUME WAKO MDOGO NA MWEMBAMBA?

MAPRO PAWER NO 2 ndio Tiba kwa sasa utibu matatizo matatu kwa pamoja 1hitakufanya uchelewe kufika kilekeni dikika 15-20 kwa tendo la kwanza 2 uhimalisha misuli iliyoregea na kusinyaa hasa kwa wale walio hasirika na upigaji punyeto 3 itakufanya upate amu ya kurudia tendo zaidi ya Mara tatu

KWA NINI UJIONE MPWEKE PALE UKUTANAPO NA MPENZI AU MKE WAKO kisa unawai kukojoa au unakomea bao moja tu na huku dawa zipo MAKAKANUA mix ni dawa iliyochanganywa na miti Shamba 9 na Kuwa na uwezo wa kuongeza uume saizi upendayo inchi 5-8 Kwa Urefu na unene sentimita 1-5 dawa hizi hazina madhara yoyote kwa mtumiaji ata wazee wenye umri mkubwa wanapona? zipo dawa za mvuto wa mpenzi mme au mke Kwa masaa matatu tu na kukupigia simu yeye mwenyewe mvuto wa biashara kutengeneza mwonekano mzuri wa mwili kwa wanawake yani shepu tunatibu ngiri miguu mgongo na kiuno kuumwa kupunguza kitambi minyama uzembe matiti na mwili mkubwa

TIBA NA USHAULI MUONE DR MABULA AU PIGA SIMU NO 0752348593 UDUMA ZANGU UTAZIPATA POPOTE ULIPO KAMA UWEZI KUFIKA OFISINI

Mwakyembe Aipa Yanga Miezi Miwili Kukamilisha Uchaguzi

$
0
0
Mwakyembe Aipa Yanga Miezi Miwili Kukamilisha Uchaguzi
Baada ya klabu ya Yanga kufanya mkutano wake mkuu wa mwaka hapo jana na kufanikiwa kuteua kamati ya kuivusha timu kwenye kipindi cha mpito, timu hiyo imepewa miezi miwili na Waziri Mwakyembe ili ikamilishe uchaguzi wake.


Waziri Mwakyembe ambaye ndiye mwenye dhamana ya Michezo nchini, amewataka viongozi wa Yanga kuziba nafasi zilizowazi ndani ya timu hiyo ili kuhakikisha Katiba ya timu inaendekea kulingwa na kufuatwa vizuri.

''Najua uchaguzi mkuu wa klabu yenu ni 2020 lakini kuna nafasi ambazo zinatakiwa kujazwa hivyo mapengo hayo yazibwe ndani ya miezi miwili sitaki kuona inachukua miezi 9 au mwaka'', aliwaambi viongozi wa Yanga.

Yanga inatakiwa kuziba naasi mbalimbali ambazo zipo wazi ikiwemo ya Mwenyekiti wa klabu endapo aliyekuwa mwenyekiti wao Yusuf Manji hatarejea kwenye nafasi yake. Nafasi zingine ambazo zipo wazi ni wajumbe wa kamati ya utendaji.

Hata hivyo katika mkutano huo wa jana, wanachama kwa pamoja walikubaliana kufanya mabadiliko kisha kuteua Bodi mpya ya wadhamini pamoja na kamati maalum ya kuhakikisha timu inavuka kwenye kipindi hiki cha mpito.
chanzo: EATV

Pingamizi la Mbowe na Viongozi Chadema Latupiliwa Mbali Mahakamani

$
0
0
Pingamizi la Mbowe na Viongozi Chadema Latupiliwa Mbali Mahakamani
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetupilia mbali pingamizi la viongozi wa CHADEMA akiwemo Freeman Mbowe la kutaka kesi ya kufanya maandamano ifutwe badala yake imeagiza hati ya mashtaka ibadilishwe.

Hata hivyo, upande wa utetezi kupitia wakili wa Peter Kibatala, umetangaza nia ya kukata rufaa kupinga uamuzi huo.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambapo amesema anakubaliana na hoja 2 za upande wa mashtaka kati ya hoja zao 8 za pingamizi.

Katika kesi hiyo pingamizi kuu la upande wa utetezi wameiomba mahakama hiyo ifute kesi hiyo kwa sababu baadhi ya mashtaka ni batili.

Katika uamuzi wake Hakimu Mashauri amesema hakuna haja ya kesi hiyo kufutwa badala yake anaagiza upande wa mashtaka uifanyie marekebisho hati ya mashtaka.

Hata hivyo, wakili Kibatala amedai kuwa wanatangaza nia ya kukata rufaa kwa sababu kama mahakama imeona mashtaka hayo ni batili kwanini isingeyafuta badala yake imeagiza yabadilishwe.

Upande wa mashtaka kupitia Wakili wa serikali Mkuu, Paul Kadushi umedai kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Mahakama za Mahakimu hakuna uwezekano wa kukata rufaa katika uamuzi mdogo ambao hauwezi kuathiri kesi.

“Naomba mahakama ipuuzie hoja hizo na nia hiyo ni batili,”ameeleza Kadushi.

Kutokana na mvutano huo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi June 12,2018 ili kutoa uamuzi kama upande wa mashtaka ukate rufaa ama lah.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika.

Mbunge wa Tarime mjini Esterher Matiko, Katibu wa chama hicho Dk Vicenti Mashinji, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, mbunge wa Tarime vijijini, John Heche na mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na jumla ya mashtaka 12 katika kesi ya jinai namba 112 ya mwaka 2018 ikiwamo kula njama, kufanya mkusanyiko usio halali kinyume cha sheria na kuendelea kufanya mkusanyiko usio halali ama maandamano yaliyosababisha kifo cha Akwilina.

Nikki Mbishi Awatolea Povu Watangazaji Wanaouliza Kuhusu Alikiba na Daimond

$
0
0
Nikki Mbishi Awatolea Povu Watangazaji Wanaouliza Kuhusu Alikiba na Daimond
Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Nikki Mbishi ameonyesha kukerwa aina fulani ya uulizaji maswali katika interview.

Nikki Mbishi amesema katika interview maswali kuhusu Diamond na Alikiba ndio hushamiri ila anachojivunia ni kwamba na yeye uhoji pia. Kupitia ukurasa wake wa twitter ameandika;

Kila interview wanauliza “Una mpango wowote wa kufanya ngoma na Ali Kiba au Diamond?” Hapo basi mtangazaji ndio anajiona kamaliza mwenyewe…#UFALA

Wakiitwa wengine interviews wanahojiwa ila nikiitwa mimi nawahoji wao ndio maana wanakuwa mabubu nikitimba….I’m proud of it. Great monday to all pointless and dumb presenters out there,peace!

September 15, 2017 katika kipindi cha XXL, Clouds FM, msanii Alikiba alikiri kuwa baadhi ya watangazaji wanashindwa kuwa na mtindo mzuri katika kuuliza maswali katika interview.

“Kwanza kabisa unapokuwa unanifanyia interview, mimi nafanya kama mazungumzo ya kawaida na kwa stori ya kawaida mimi nina haki ya kukuuliza chochote ninachojisikia, sio wewe uniulize tu,” alisema Alikiba.


Zaidi ya Viongozi 900 Mali Zao Kuchunguzwa na Serikali Kisa Hiki Hapa

$
0
0
Zaidi ya Viongozi 900 Mali Zao Kuchunguzwa na Serikali Kisa Hiki Hapa
Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela amesema kuwa wamefanya uchambuzi ambapo kwasasa zaidi ya viongozi 900 wanahakikiwa mali zao.

Akizungumza na Wanahabari leo, Juni 11, 2018, Nsekela amesema kuwa sababu ya kwanza iliyofanya kuhakiki mali hizo ni kudhibitisha tamko walilopeleka na uhalisia wa mali hizo.

“Sasa tumefikia mahali ambapo tuende kuhakiki kwa baadhi ya viongozi nasema kwa baadhi ya viongozi kwasababu kuna sababu nyingi, sababu kubwa tunasema ni rasilimali fedha tunasema kwamba kama fedha hatuna za kutosha hatuwezi kuwahakiki viongozi wengi kwa hivi sasa tumefanya uchambuzi wa viongozi 900 ambao sasa tunakwenda kuwahakiki mnaweza mkasema mnahakiki kwa sababu gani, sababu ya kwanza ni kudhibitisha uhalisia wa mali hizo kulinganisha na tamko walilotuletea, tunatafuta thamani ya hizo mali walizonazo hao viongozi na uhalali wa hizo mali kwa maana ya kwamba hizo mali walizipataje” amesema Nsekela.

Nsekela ameongeza “Kama mnavyojua sisi tunazungumzia suala zima la Maadili kwamba kiongozi awe na Maadili na mimi kama kiongozi na mmoja wapo wa viongozi nikitoa tamko langu na nikitaka kuhakiki tunataka tujue zile mali nilizo nazo na uwezo wangu kuna uwiano gani hapo, hizo mali nimepata kihalali au sijapata kihalali, kwahiyo unaweza ukauliza maswali mengi hapo,kwahiyo sababu kubwa la kwenda kuhakiki hizo mali ni hiyo hapo, kuangalia uhalali wa mali za sisi viongozi jinsi zilivyopatikana, maana yake ni kwamba sisi viongozi tunatakiwa tuwe na mali zilizopatikana kihalali na sio vinginevyo kwahiyo ndiyo zoezi kubwa tunaloenda kulifanya kuanzia tarehe 18 mwezi huu ndio tutaanza zoezi hilo la kuhakiki hao viongozi tuliowachagua na litatuchukua wiki nne au mwezi mmoja nadhani mpaka tarehe 18 mwezi July na kwasababu ni zoezi nyeti, tumeona ni vizuri viongozi kwanza tuwaambie kwamba kuna zoezi hilo linakuja.”

Ikumbukwe Disemba 27, 2017 Nsekela aliwahimiza Viongozi wa Umma kukamilisha taratibu za ujazaji wa fomu za tamko la rasilimali na madeni kabla ya Disemba 31 mwaka huo.
Chanzo: Bongo5

Shamsa Ford Ayatoa Muhanga Maisha Yake "Hata Uwe Mwema Kiasi Gani Binadamu Atakutia Ubaya''

$
0
0
Shamsa Ford Ayatoa Muhanga Maisha Yake "Hata Uwe Mwema Kiasi Gani Binadamu Atakutia Ubaya''
Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford amefunguka na kujitoa muhanga wa maisha yake kwa kile alichokieleza kuwa haogopi kuonekana mbaya kwa binadamu wa aina yoyote katika hii dunia kadri siku zinavyozidi kusonga mbele.


Kauli hiyo ya Shamsa Ford imekuja baada ya kuwepo wimbi kubwa la vijana wengi wa kizazi cha sasa kuhofia kufanya mambo yao ya kimaendeleo kwa kuhofia au kuogopa walimwengu kwa maneno yao yasiyokuwa na baraka hata wawafanyia jambo gani kubwa lakini mwisho wa siku wao wanaambulia kudharauliwa na mengineyo.

"Siku zinavyozidi kwenda nimejikuta siogopi kuonekana mbaya kwa binadamu yoyote. Nimegundua binadamu hata uwe mwema kiasi gani lazima atakutafutia kasoro ya kukutia ubaya", amesema Shamsa.

Pamoja na hayo, Shamsa Ford ameendelea kwa kusema "binadamu hata uwe mpole, mnyenyekevu na mwenye upendo lazima wakusengenye kwa ubaya ni ngumu sana kuishi na binadamu na huwezi kumlizisha kila binadamu ni bora uishi maisha unayoona wewe ni sahihi kwako".

Kwa upande mwingine, Shamsa Ford amesisitiza kuwa kuishi na binadamu kuna hitaji umakini wa hali ya juu pamoja na hekima ili mradi uende nae sawa bila ya kukwazana kwa namna yoyote ile.

Kubenea Amwomba Rais Magufuli Kumuwajibisha Jaiji Mutungi "Huyu Mutungi ni Hatari Apaswi Kuachwa Amepoteza Sifa"

$
0
0
Kubenea Amwomba Rais Magufuli Kumuwajibisha Jaiji Mutungi "Huyu Mutungi ni Hatari Apaswi Kuachwa Amepoteza Sifa"
Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea amemuomba Rais John Magufuli kumuwajibisha Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi kwa madai kuwa ameshindwa kutimiza wajibu wake.

Kubenea ametoa kauli hiyo leo Juni 11, 2018 katika mkutano wa wabunge wa Ukawa waliozungumzia hatima ya ruzuku za CUF, kufuatia ofisi ya msajili kuendelea kutoa ruzuku ya chama hicho upande wa Profesa Ibrahim Lipumba, bila kujali zuio la mahakama.

CUF kimekumbwa na mgogoro tangu mwaka 2016 baada ya Profesa Lipumba ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, kurejea katika uongozi ikiwa ni mwaka mmoja tangu alipoandika barua ya kujiuzulu. Mgogoro huo umesababisha kufunguliwa kesi mahakamani.

Amesema kitendo kinachofanywa kwa sasa na Jaji Mutungi ni sawa na kuibaka demokrasia, hakikubariki kwa maelezo kuwa kinachafua uso wa Tanzania kimataifa.

“Haiwezekani jambo hili likawa linatokea na Rais anaangalia bila ya kulifanyia kazi. Huyu Mutungi ni hatari hapaswi kuachwa aendelee kwani amepoteza sifa na anaonekana kuwa na maslahi furani,” amesema Kubenea.

Mbunge wa Malindi Ali Saleh (CUF) amesema msajili wa vyama ndio chanzo cha mgogoro ndani ya chama hicho kwa kuwa anafanya mambo kinyume hata na maagizo ya mahakama.

Saleh amesema Msajili alitumia ujanja kukataa kupokea zuio la mahakama kuhusu ruzuku katika kesi namba 80 ya mwaka 2018 lililotolewa Mei 29, 2018 ili atoe kwanza fedha hizo, huku akipongeza uamuzi wa mahakama kutoa zuio wakati fedha zikiwa hatua ya mwisho kutolewa katika moja ya tawi la benki moja jijini Dar es Salaam.

Amesema kitendo cha kukataa hukumu ya mahakama ni kosa kisheria na kuhoji ujasiri anaoupata msajili huyo.

Naye mbunge Mchinga (CUF) Hamidu Bobali amesema msajili amesharuhusu Sh600 milioni kuingizwa katika akaunti ya wilaya ya chama hicho,  lakini uongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho walibaini jambo hilo na kuzizuia.

Amedai fedha hizo zilikuwa maalum kwa ajili ya kuendesha mkutano wa chama hicho uliopangwa kufanyika mkoani Singida.
Chanzo: Mwananchi

Alichosema Mkubwa Fella Baada ya Aslay Kuachana na Mzazi Mwenzie "Nasubiri Nipigiwe Simu na Wahusika Niweze Kusuruhisa"

$
0
0
Mkubwa Fella Ashtushwa Ishu ya Aslay Kuachana na Mzazi Mwenzie "Nasubiri Nipigiwe Simu na Wahusika Ili Niweze Kusuruhisa"
Mkurugenzi wa kundi la Yamoto Band na Meneja wa Diamond Platnumz, Mkubwa Fella ameshtushwa na taarifa za msanii wa muziki, Aslay kuachana na mzazi mwenzie.

Mkubwa Fella amedai kuwa hakupata taarifa hizo moja kwa moja bali aliziona mtandaoni na kama ni kweli basi anasubiri apigiwe simu na wahusika ili aweze kusuruhisha.

Aslay wiki iliyopita kwenye mahojiano yake na Bongo5 alisema kuwa kwa sasa hayupo tena kwenye mahusiano na mzazi mwenzie akieleza kuwa wameshindwana. Tazama video ya Aslay hapa chini

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH mzee khamisi Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

$
0
0

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH mzee khamisi Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Mzee khamisi Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU.

Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Mzee khamisi Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..

Na mengi zaidi whatsapp +255 623448511 au 0783636592 au +255 622588038
NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Watangazaji kupenda kuuliza kuhusu Diamond na Alikiba, Nikki Mbishi awatolea uvivu

$
0
0
Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Nikki Mbishi ameonyesha kukerwa aina fulani ya uulizaji maswali katika interview.

Nikki Mbishi amesema katika interview maswali kuhusu Diamond na Alikiba ndio hushamiri ila anachojivunia ni kwamba na yeye uhoji pia. Kupitia ukurasa wake wa twitter ameandika;

Kila interview wanauliza “Una mpango wowote wa kufanya ngoma na Ali Kiba au Diamond?” Hapo basi mtangazaji ndio anajiona kamaliza mwenyewe…#UFALA

Wakiitwa wengine interviews wanahojiwa ila nikiitwa mimi nawahoji wao ndio maana wanakuwa mabubu nikitimba….I’m proud of it. Great monday to all pointless and dumb presenters out there,peace!

September 15, 2017 katika kipindi cha XXL, Clouds FM, msanii Alikiba alikiri kuwa baadhi ya watangazaji wanashindwa kuwa na mtindo mzuri katika kuuliza maswali katika interview.

“Kwanza kabisa unapokuwa unanifanyia interview, mimi nafanya kama mazungumzo ya kawaida na kwa stori ya kawaida mimi nina haki ya kukuuliza chochote ninachojisikia, sio wewe uniulize tu,” alisema Alikiba

Irene Uwoya Afunguka Kutokewa na ‘Mzimu’ wa Masogange

$
0
0
Muigizaji wa filamu Bongo, Irene Uwoya na mumewe, Dogo Janja wamefunguka sababu ya wao kuhama nyumba waliokuwa wakiishi hapo awali.

Dogo Janja amesema wamelazimika kuhama nyumba hiyo na kwenda kupanga nyumba nyingine ambayo hulipa US Dollar 800 kwa mwezi kutokana na umbali, pili mkewe, Irene alikuwa akisumbuliwa na kumbumbuka za mara kwa mara kuhusu marehemu Agnes Gerald ‘Masogange’.

“Nahisi kama nilikuwa namuona hivi, kwa hiyo nikashindwa, eeeh!! mara nyingi pia nahisi kama anapita hivi,” amesema Irene Uwoya.
“Of cause inaweza kuwa sababu kila akijitahidi inashindikana kwa sababu alikuwa ni mtu tumemzoea sana,” Dogo Janja ameiambia Clouds FM.
Marehemu Agnes Gerald ‘Masogange’ alifariki April 20, 2018 katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, Dar es Salaam, alikuwa rafiki wa karibu sana na Irene Uwoya.

JamiiForum Wafunga Mtandao kwa Muda, Ni Baada ya TCRA Kupiga Marufuku Wasio na Leseni Kuendelea Kuhabarisha Umma

$
0
0
Mamlaka ya Kudhibiti Mawasiliano nchini, TCRA imepiga marufuku kwa vyombo vya habari kupitia maudhui ya mtandaoni ambavyo havina leseni ya kuendesha shughuli hiyo kuweka jambo au taarifa yeyote katika mitandao yao.

TCRA imetoa siku 5 kuanzia leo Juni 11, hadi Juni 15, 2018 kuhakikisha vyombo hivyo vya habari vinakamilisha usajili na kuwa na leseni ya urushaji wa matangazo kupitia mtandao, imesisitiza kuwa kuanzia Juni 15, mwaka huu hatua kali zitachukuliwa kwa watakaokiuka agizo hilo.

Kufuatia agizo hilo Uongozi wa Mtandao wa Jamii Forums uliojikita katika kuhabarisha umma mtandaoni umeomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza mara baada ya kuamua kutii agizo hilo la kusitisha huduma ya utoaji habari mpaka pale utakapokamilisha usajili huo.

Katika ukurasa wa mtandao huo, JamiiForums wameandika;
”Kutokana na notisi iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Juni 10, 2018 inayotoa muda mfupi wa kututaka kusitisha utoaji huduma mara moja kabla ya Juni 11, 2018, tunalazimika kutii mamlaka na hivyo huduma hii haitapatikana kwa muda wakati tukifanya jitihada za kuhakikisha huduma inarejea.

"Tunasikitika kuwa tunalazimika kufikia hatua hii ghafla lakini ni matumaini yetu kuwa wateja wetu mtaendelea kuwa wavumilivu katika kipindi hiki”

Shabiki Mwanamke Apagawa Jukwaani Awatoka Mabaunsa na Kumkumbatia Wizkid Kisha Kuzimia

$
0
0
Staa mwenye ushawishi mkubwa katika game ya muziki kutokea Nigeria Wizkid maarufu kama ‘Starboy’ alitumbuiza Weekend ya June 9,2018 Ghana kwenye Tamasha la “Ghana Meets Naija 2018” katika viwanja vya Fantasy Dome.

Show hio ilikuwa kubwa kutokana na wingi wa mashabiki kuhudhuria tamasha hilo katika utumbuizaji wa Wizkid ulimfanya mmoja wa mashabiki kupanda juu ya stage na kumkumbatia Wizkid  kitu kilichowalazimu walinzi kumtoa kitendo hicho kilimfanya shabiki huo kuzimia baada ya kukumbatiwa na Wizkid.

Tukio hili liliwashangaza watu wengi ikiwemo Wizkid mwenyewe na huenda tukio hili likawa miongoni mwa matukio ya kushangaza ambayo Wizkid hatoweza kuyasahau katika maisha yake.

VIDEO:

Masunzu Power Mix Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo

$
0
0
MASUNZU POWER MIX DAWA BORA YA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO

🌸MASUNZU POWER MIX ni dawa ya asilia yenye mchanganyiko wa mitishamba 7 yenye maajabu yafuatayo (1) inatibu upungufu wa nguvu za kiume Mara dufu na kuimalisha uume uliolegea wakati wa tendo la ndoa (2) kurefusha uume uliorudi ndani nchi 5-8 (3) kunenepesha uume sm4 ya upana itakufanya uchelewe kufika kileleni dk (15-20) kwa tendo la kwanza na utakuwa nauwezo wa kurudia tendo la ndoa Mara (2-4) bila hamu kuisha nainatibu kabisa. Dawa hii haina madhara yoyote kwa mtumiaji huanza kufanya kazi baada ya dk 50 tu 🌾🌾🌾🌾🌾🌾🌾🌾

MATATIZO HAYA HUSABABISHWA NA ngiri. au umejichua kwa muda mrefu. Punyeto kisukari. Presha. Tumbo kujaa gesi na kuunguruma chini ya Kitovu. Kutopata choo vizuri. Msongo wa mawazo. Kaswende. Gono. Haya yote husababisha kuwa na maubile madogo na kukosa nguvu za kiume

🌸SOSOMA DX. ni dawa ya kumvuta mme au mke au mpenzi wako arudi haraka na kuanza mapenzi mapya kama mlivyo anza mwanzo baada ya masaa 2 atarudi na kutulia ndani ya nyumba na kutimiza ahadi yako

🌸GINDU EXTRA ni dawa ya kutibu kisukari siku 14 unapona kabisa hata kama imepanda itashuka haraka Sana. Tunatibu busha bila upasuaji nk. Dar es salaam tunapatikana buguruni chama au unaweza kuletewa popote ulipo

Wasiliana na tabibu ATHUMAN SIMU +255673552294 / +255784552299

Hivi Ndivyo Walinzi 12 wa Rais Kim Jong Un Wavyoulinda Msafara Wake Singapore

$
0
0
Hivi Ndivyo Walinzi 12 wa Rais Kim Jong Un  Wavyoulinda Msafara Wake Singapore
Ulimwengu kwa mara nyengine ulipata fursa ya kuwatazama walinzi 12 wa rais wa Korea kaskazini Kim Jong Un wakikimbia wakati walipokuwa wakiulinda msafara wake nchini Singapore.

Lakini wana majukumu mengi kwa sababu linapojiri swala la usalama wa kiongozi huyo, taifa la Korea liko tayari kufanya chochote .

Mchanganuzi Michael Madden anaelezea zaidi kuhusu kundi hili la wanaume. Wakati anapokuwa Korea Kaskazini , mlinzi wa karibu wa Kim ana laini tatu tofauti zinazomzunguka.

Walinzi wanaokimbia kandokando ya gari lake aina ya Limousine na wale wanaotembea kwa mguu ni miongoni mwa maafisa wa afisi kwa jina Central Party Office #6, inayojulikana rasmi kuwa afisi ya wapiganaji.

Wao ndio wanaomlinda rais huyo na huchaguliwa kutoka katika jeshi la Korea. Huchaguliwa kutokana na vigezo vya , urefu-wanatakiwa kuwa na urefu sawa na kiongozi wao na wawe wanaweza kuona vizuri.

Wanatakiwa kuwa na uwezo kama vile kupiga risasi na kupigana judo, karate na masumbwi.



Hivi Ndivyo Irene Uwoya na Dogo Janja Walivyoukimbia Mzimu wa Masogange

$
0
0
Hivi Ndivyo Irene Uwoya na Dogo Janja Walivyoukimbia Mzimu wa Masogange
Muigizaji wa filamu Bongo, Irene Uwoya na mumewe, Dogo Janja wamefunguka sababu ya wao kuhama nyumba waliokuwa wakiishi hapo awali.

Dogo Janja amesema wamelazimika kuhama nyumba hiyo na kwenda kupanga nyumba nyingine ambayo hulipa US Dollar 800 kwa mwezi kutokana na umbali, pili mkewe, Irene alikuwa akisumbuliwa na kumbumbuka za mara kwa mara kuhusu marehemu Agnes Gerald ‘Masogange’.

“Nahisi kama nilikuwa namuona hivi, kwa hiyo nikashindwa, eeeh!! mara nyingi pia nahisi kama anapita hivi,” amesema Irene Uwoya.

“Of cause inaweza kuwa sababu kila akijitahidi inashindikana kwa sababu alikuwa ni mtu tumemzoea sana,” Dogo Janja ameiambia Clouds FM.

Marehemu Agnes Gerald ‘Masogange’ alifariki April 20, 2018 katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, Dar es Salaam, alikuwa rafiki wa karibu sana na Irene Uwoya.

Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images