Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

A-Z Kuhusu Ajali Iliyoua Wanafunzi wa UDSM

$
0
0
A-Z Kuhusu Ajali Iliyoua Wanafunzi wa UDSM
Katibu Mteule wa Serikali ya Wanafunzi kitivo cha Sayansi ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Hussein Amri Aman, amekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusu mwanafunzi Maria Godian Soko aliyefariki dunia kwa ajali kuwa alikuwa mjamzito na kwamba zinapaswa kupuuzwa.


Amri ameyasema hayo wakati akizungumza na www.eatv.tv, ambapo ameeleza kwamba marehemu Soko alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya pumu na ndiyo sababu kuu iliyomfanya awe anakimbizwa hospitali kwa ambulance.

Amesema, kutokana na ukaribu wake yeye na marehemu aliweza kumfahamu kuwa alikuwa akisumbuliwa na pumu kwa muda mrefu na mara nyngi humsababishia kupoteza fahamu.

"Marehemu Maria alikuwa na matatizo ya pumu ambayo yalimsababishia kifua kubana hadi kuzimia hivyo majira ya saa mbili kasoro tulifanya utaratibu wa kuita ambulance ya chuo na kumchukua hapa mabibo hostel kumpeleka hospitali ya chuo kwa matibabu zaidi"

Ameongeza "Wakati taratibu za kumpeleka hospitali ya chuo zinaendelea ndipo ajali mbaya ikatokea pale riverside, taarifa zinazoendelea kusambaa kwamba marehemu alikuwa mjamzito anaenda kujifungua sio za kweli".

Katika ajali hiyohadi sasa walioripotiwa kufariki ni wanafunzi wawili ambao ni Maria Godian Soko (Mwaka wa kwanza COSS) na Steven E Sango  (CPE CoET mwaka wa pili) pamoja na dereva James

Mwanafunzi mwingine aliyekuwepo katika msafara huo ni Abishai Nkiko (Bsc Industrial Engineering mwaka wa 3 CoET) hali yake ni mbaya na anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya taifa ya muhimbili.

Maria Godian Soko ( B.A in psychology mwaka wa kwanza) amefariki jana usiku baada ya ambulance ya chuo kugongana na lori majira ya saa mbili  maeneo ya riverside -Ubungo  wakati alipokuwa akikimbizwa hospitali  baada ya kubanwa na pumu hali iliyomfanya kupoteza fahamu.
Chanzo: EATV

Kubenea Awapigania Wanaume Wenye Wake Zaidi ya Mmoja

$
0
0
Kubenea Awapigania Wanaume Wenye Wake Zaidi ya Mmoja
Serikali  inaangalia namna ya kuhakikisha wanaume wenye wake zaidi ya mmoja wanaingiza wenzi wao hao kwenye huduma ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Ahadi hiyo ilitolewa jana bungeni jijini hapa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Joseph Kakunda.

Kakunda alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema).

Katika swali hilo, Kubenea alihoji kwa kuwa NHIF inatambua mke mmoja, serikali ina mpango gani kuruhusu wake wawili kuingizwa kwenye mfuko huo tofauti na ilivyo sasa.

Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika, naibu waziri huyo alisema serikali inatambua kuwa wananchi wake wana dini ambapo moja -kiislam - inaruhusu kuoa mke zaidi ya moja.

Alisema kutokana na ukweli huo, itaangalia namna ya kulifanyia kazi suala hilo.

“Serikali tunatambua kuwa wananchi wana dini na inaruhusu kuoa mke zaidi ya mmoja, acha tulichukue ili kulifanyia kazi,” alisema Kakunda.

Mbali na kuingizwa mke wa pili, naibu waziri huyo aliahidi pia kuangalia uwezekano wa bima hiyo kuwakinga pia wazazi wa mwanachama.

Huduma za NHIF kwa wanachama zinahusu pia wenza na watoto wasiozidi wanne na walio chini ya umri wa miaka 18, vinginevyo wawe wanasoma.

Kwa watoto wanaosoma, ukomo wa huduma hiyo ni pale watakapotimiza umri wa miaka 21.

Madaktari Wagundua Donald Ngoma Amechanika Mtulinga wa Mguu

$
0
0
Madaktari Wagundua Donald Ngoma Amechanika Mtulinga wa Mguu
Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imethibitisha rasmi kuingia kandarasi ya mwaka mmoja na mshambuliaji Donald Ngoma hapo jana siku ya Jumatatu atakaoanza kuutumikia kuanzia msimu ujao baada ya vipimo vyake kukamilika na kugundulika kuwa amechanika mtulinga.


Zoezi hilo la vipimo lilienda vema kwenye Hospitali ya Vincent Pallotti nchini humo, ambapo imegundulika amechanika mtulinga wa mbele wa goti la mguu wa kulia (Anterior Crusiate Ligament), majeraha yatakayomweka nje hadi Agosti 11 mwaka huu atakaporuhusiwa kucheza mechi za ushindani.

Awali pande hizo mbili ziliingia makubaliano ya mkataba huo (memorandum of understanding) kwa sharti la kumfanyia vipimo vya afya jijini Cape Town, Afrika Kusini kujua undani wa majeraha ya goti aliyokuwa nayo.

Meneja wa timu hiyo, Phillip Alando ameiyambia tovuti ya klabu hiyo kuwa tayari wameingia mkataba na mshambuliaji huyo hatari kutoka nchini Zimbabwe baada ya kuridhishwa na ripoti za vipimo kutoka kwa wataalamu nchini Afrika Kusini.

“Nathibitisha kuwa leo (jana) tumeingia mkataba rasmi na Ngoma (Donald), mashabiki watambue ya kuwa mchezaji huyo atakuwa ni miongoni mwa wachezaji wapya watakaovaa jezi ya Azam FC msimu ujao, hakuna asiyemfahamu Ngoma, anaijua vema ligi yetu na changamoto ya mechi za kimataifa hivyo tunatarajia mambo mazuri kutoka kwake,” amesema Alando.

Tayari Ngoma ameshakabidhiwa jezi namba 11 aliyokuwa akitumia kwenye timu yake ya awali ya Yanga, ambapo usajili wake ni sehemu ya mapendekezo ya benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu mpya, Hans Van Der Pluijm aliyewahi kufanya naye kazi pamoja akiwa kwa Wanajangwani hao.

Ngoma, 28, anaungana na Mzimbabwe mwenzake Tafadzwa Kutinyu, ambaye naye ameshasaini kuitumikia Azam FC msimu ujao akitokea Singida United, raia mwingine wa taifa hilo aliyeko kwenye kikosi hicho ni beki wa kushoto, Bruce Kangwa, atakayekuwa akiitumikia timu hiyo kw
Chanzo:Global Publishers

Sakata la Kuvuja kwa Video ya Faragha Haikuniachanisha na Nandy- Bill Nass

$
0
0
Sakata la Kuvuja kwa Video ya Faragha Haikuniachanisha na Nandy- Bill Nass
Msanii Bill Nass amesema stakata la kuvuja kwa video ya faragha kati yake Nandy haukumuachanisha na mpenzi wake.

Rapper huyo amesema kwa kipindi hicho mpenzi wake ndio alikuwa mtu wake wa karibu zaidi.

“Hapana sijaaachana na mpenzi wangu nipo naye hadi sasa na ndio mtu pekee nilikuwa nawasiliana naye kila saa. She is very clever anajielewa, alitazama kwanza, alijua, akaangalia ni kwa namna gani anaweza kujenga kuliko kuharibu zaidi,” Bill Nass ameiambia Bongo5.

Hivi karibuni Nandy akiwa katika media tour nchini Kenya alisema kuwa Boyfriend wake amemkataza kuzungumzia suala hilo ila bado penzi lao lipo pale pale.

Utakumbuka April 12, 2018 ndipo ilivuja video mtandaoni ya utupu ambayo iliwaonyesha Bill Nass na Nandy wakiwa faragha.
Chanzo: Bongo5

Sakata la TCRA Kusitisha Oniline Media Latua Bungeni...... Saed Kubenea Awasha Moto

$
0
0
Sakata la TCRA Kusitisha Oniline Media Latua Bungeni...... Saed Kubenea Awasha Moto
Sakata la Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) kutekeleza kanuni za maudhui, limewasilishwa bungeni na mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea akitaka maelezo ya kina ya Serikali kwani inaminya uhuru wa habari.

Kubenea akitumia Kanuni ya 47 (1) (2) (3) leo bungeni Juni 12, 2018 akitaka kuahirishwa kwa shughuli za Bunge ili kujadili suala hilo.

“Kuanzia jana TCRA imesitisha usambazaji wa taarifa za social media, kwa tangazo hilo YouTube zote haziruhusiwi toka jana, Blog zote haziruhusiwi toka jana, website na redio zote ambazo ziko online haziruhusiwi toka jana,” amesema Kubenea na kuongeza:

“Kwa hiyo Mamlaka ya Mawasiliano wanasema mpaka Juni 15 mwaka huu, wale ambao watakuwa hawajalipia ada zao hawataruhusiwa. Mahakama Kuu kanda ya Mtwara ilisitisha hivyo nao wakazingatia agizo hilo la Mahakama.”

Kubenea amesema, “jana asubuhi, tangazo linatoka na watu hawajajiandaa, Bunge liahirishe shughuli zake za muda ili mjadala huu lijadiliwe na Serikali iweze kujibu suala hili, dunia imesimama hakuna taarifa zinatoka Tanzania kwenda kwingine na hata webstite zingine za serikali hazitoki nje.”


Akitoa maelezo ya kiti, Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga amesema, “hili la Kubenea sisi bungeni hatuwezi kuahirisha, waliofunga wana sababu zao na watakapokuwa tayari watafungua kama kawaida.”
Chanzo: Mwananchi

Rais Magufuli Achangia Milioni 10 Ujenzi wa Msikiti Dar

$
0
0
Rais Magufuli Achangia Milioni 10 Ujenzi wa Msikiti Dar
RAIS John Magufuli ametoa pesa taslim kiasi cha Tsh. Milioni 10 kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa mifuko 600 ya sementi itakayosaidi kwenye ujenzi wa Msikiti Mkuu wa BAKWATA unaoendelea kujengwa Kinondoni Jijini Dar es Salaam.



Rais ametoa mchango huo leo Juni 12, 2018 wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Msikiti huo unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme wa Morocco.



Msikiti huo ambao utakuwa mkubwa kuliko misikiti yote nchini Tanzania utabeba zaidi ya watu 8,000 na unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili au mei mwakani.

Nilaumuni kwa ‘Bao la Mkono’ Sio kwa Hili la Jamii Forums – Nape Nnauye

$
0
0
Nilaumuni kwa ‘Bao la Mkono’ Sio kwa Hili la Jamii Forums – Nape Nnauye
Mbunge Mtama, Nape Nnauye amejikutaka akijibu hoja mbali mbali mtandaoni kufuatia mtandao wa Jamii Forums kusitisha kutoa huduma.

Utakumbuka Jamii Forums wamefikia hatua hiyo kutokana na kanuni za maudhui ya kimtandao za mwaka 2018.

Sasa Nape Nnaye alianza kueleza hisia zake kuhusu hilo kwa kuandika kwenye mtandao wa twitter; Hili la JF linafikirisha! Ukizuia watu kusema wayawazayo unaweza Kutana nao….. kimya kimya!.

Baada ya tweet hiyo idadi kubwa ya wachangia walionekana kuomnyooshea kutokana kipindi akiwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo alipitisha sheria ya huduma za vyombo vya habari kwa mwaka 2016

Hata hivyo Nape aliwataka wachangia kutofautisha vitu hivyo kwani ni sheria mbili tofauti.

“Nimeuliza hili swali toka mwanzo kina uhusiano gani wa hizi sheria mbili? Au tunakaririshwa au hatujui tunachotaka kusema,” alijibu Nape na mjadala kuendelea.

Utakumbuka katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa October 2015 wakati Nape Nnaye akiwa Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ndipo alipoeleza kuwa chama hicho kingeshinda uchaguzi huo hata kwa bao la mkono kauli ambayo iliiubua mjadala mpana.

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Mafupi na Upungufu wa Nguvu za Kiume? Suluhisho Hili Hapa

$
0
0

KWANINI BAADHI YA WANAUME WANA MAUMBILE MAFUPI NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME DR SITTA NDO SULULISHO LAKO tatiza, hili limekuwa likiwaasili watu wengi,sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine, kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo zipo , sababu nyingi zinazosababisha, tatizo hilo baadhi ni (i) upungufu wa vichocheo vya HORMONES ZA CETROGEN ambazo mwanaume, anapobarehe vichocheo hivi, HORMONES hizo, husaidia ukuaji wa uume 

SUPER MIZIZI, ni dawa inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi utakayo na kuzibua mlija iliysinyaa, 

NSHOLA ni dawa bora, ya kurudisha nguvu, za, kiume bari inatibu ,kabisa kutoa tatizo hilo, na kukupa , hamu ya , kurudia tendo, la ndoa zaidi, ya mala nne 4 ,bila kuchoka atakama unaumli ,wa mika 80,! pia ana ,dawa za ,kutibu, presha ya kupanda ,na kushuka, kisukari kuondoa, mafuta , mwilini ,na maumivu ya, mgogo kiuno, dawa zipo, matazo, ya hedhi, kwa ,wanawake hedhi, zisizokuwa na, mpangilio, na kasonono, pia , vidonda ,vya, tumbo ,(STOMACHI UCLENS) IHUSHI ndoji lako. 

NKANYA ni dwa ya mvuto wa kimapenzi ,mchumba mpenzi ariyekuacha, mke mme, atakuludia kwa, mda, wa msaa3 tu , ukishaitumia atarudi ,mwenyewe bila ,ugovi tena, NKOMA ni dawa kuongeza HIPS na mguu wa bia kwa wadada . 

HERBON, ni, dawa, ya kuongeza, CD4, NGAKAMA ,ni dawa ya kutibu ,miguu, kufaganzi, na ,kuwaka moto, huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa! DR SITTA, amebobea, kwa tiba asilia 

DAR ANAPATIKANA MBAGALA, ZAKHEM, SONGEA BOMBAMBILI SHINYANGA, KAHAMA MJINI, KWA MAELEZO ZAIDI ,

PIGA SIMU 0763172670 au 0715172670 

WOTE MNAKALIBISHWA, KAMA, UTAKUWA NA TATIZOUTAHUDUMIWA, 

Updates: Trump aridhika na mazungumzo pamoja na Kim, Wasaini Makubaliano Maalumu

$
0
0

Rais Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wamemaliza mazungumzo ya kwanza ya kihistoria kwa kutia saini taarifa juu ya ahadi za kuangamiza silaha za nuklia za Korea Kaskaizni.


Trump akizungumza baada ya kutia saini hati hiyo amesema ameridhika kabisa na mazungumzo na wameanzisha uhusiano mzuri kati yao.


"Ninadhani uhusiano kamili kati yetu na Korea Kaskazini utabadilika na kua tofauti na namna ilivyo kua awali na tumeweza kukuza uhusiano mzuri kuliko vile tulivyotarajia."


Akiulizwa ikiwa atamualika Kim Washington alijibu, Bila shaka.


Kim kwa upande wake amesema wamekubaliana kuacha nyuma yaliyopita na kufungua ukurasa mpya wa uhusiano.


Kabla ya kutia saini Trump na Kim walikutana kwa mara ya kwanza na kupeana mkono asubuhi katika hoteli ya Capella kwenye kisiwa cha mapumziko cha Sentosa, huko Singapore.


Baadae  tena wakakutana ana kwa ana kwa karibu dakika 40, kabla ya kutoka na kukutana pamoja na wajumbe wao wa vyeo vya juu. Katika mkutano huo kulikuwepo mawaziri wa mambo ya nchi za nje na wakuu wa usalama wa taifa wa kila upande.


Walipomaliza mazungumzo hayo viongozi hao walikula chakula cha mchana wakiendelea na mazungumzo bila yakufahamika kile walichokua wanazungumza.


Miongoni mwa masuali muhimu ni namna ya kuangamiza kabisa silaha za nuklia za Korea kaskazini, kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani huko Korea Kusini, suala la wajapan walotekwa nyara, kuheshimiwa haki za binadam, Korea Kaskazini, kuondolewa vikwazo na ushirikiano wa baadae kati ya nchi hizi mbili. 

Wanawake Mungu Anawaona...Ona Huyu Mwanamke Alichomfanyia Mmewe Mpaka Kapatwa na Kizunguzungu Cha Ghafla

$
0
0

Jamaa kaamka asubuhi, kavaa track suit na kumuamsha mkewe!

MUME: Amka twende jogging mke wangu?

MKE: Alaaa kwa hiyo una maana mi tipwatipwa?

MUME: Hapana si hivyo jogging ni nzuri kwa afya.

MKE: Kwa hiyo una maana mi mgonjwa?

MUME: Basi yaishe endelea kulala🤗
MKE: Kwa hiyo unaniona mi mvivu sana sio?

MUME: Hujanielewa mpenzi wangu sikuwa na maana hiyo baby

MKE: Kwa hiyo mie mjinga mpaka nashindwa kukuelewa?

MUME: Jamani mi sijasema hilo

MKE: Kwa hiyo mie muongo?

MUME: Chonde tusiendeleze haya asubuhi namna hii

MKE: Kwa hiyo mie ndio naendeleza ugomvi?

MUME: Sikia we lala mie naenda jogging.
MKE: Ndio zako hizo mambo yote unafanya peke yako hunishirikishi"🤐

MUME: Unajua nimeanza kusikia kizunguzungu
MKE: Unaona nikiongea kidogo unakimbilia kuumwa, mbinafsi sana wewe...

MUME: Basi ngoja tu nilale siendi jogging
Mke: Kwahiyo ulikua unanijaribu?


Wanawake Mungu anawaona

*NDIO MAANA WANAUME TUNAKUFA MAPEMA NA KUWAACHA WENGI MKIWA WAJANE*

Rosa Ree Afichua Tetesi Zilizokuwepo Kuhusu Kujiunga WCB

$
0
0

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Rosa Ree amejibu iwapo alishafanya mazungumzo na WCB kwa lengo la kujiunga na label hiyo.

Rosa Ree ambaye awali kabisa alikuwa katika label ya The Industry ameiambia Bongo5 kuwa hawajawahi kuzungumza hilo ila ni watu ambao wamekuwa bega kwa bega na yeye katika muziki wake.

“Hapana ilikuwa hamna, ndiyo timu mzima ya WCB wamekuwa wakinisapoti katika muziki wangu. Nafurahia hilo ila hatukuwahi kufikia hatua hiyo,”

Utakumbuka October 2017 wakati Rosa Ree anaweka wazi kumalizika kwa mkataba wake The Industry katika mahojiano na Bongo5 alijibu kuhusu hilo pia.

“Am open to anything as long as ina manufaa kwangu but hatujaongea” alisema.

Rosa Ree kwa sasa yupo katika label ya Dimo Production kutoka nchini Afrika kusini ambayo ndio imefanikisha kolabo yake ‘ Way Up’ na rapper Emtee kutoka nchini Afrika Kusini.

Kutana na Mtaalam Sharif Hamad Kalala Mchambuzi wa Nyota za Binadamu na Tiba Asili

$
0
0
KUTANA NA SHARIF HAMAD KALALA NI
SHARIFU MCHAMBUZI WA
NYOTA ZA BINAADAMU NA NI MWENYE UPEO MKUBWA KUTAFITI MATATIZO YAKO KABLA YA KUTOA USHAURI WAKE WA TIBA AlJALISHI MBALI ULIKO TIBA YAKE UMFIKIA YEYOTE MWENYE UITAJI POPOTE
DUNIANI.

 SHARIF HAMAD KALALA NI TABIBU MWENYE KUBRI TOKA KWA ALAH ANATIBU KWA NJIA YA VITABU VYA QUR-AN, DAWA ZA ASILI ZA MITI SHAMBA PAMOJA NA DAWA ZA KIARABU.
ANATIBU KWA NJIA YA SIMU KWA KUTOA
MAELEKEZO NAMNA YA MATUMIZI YA DAWA UKIWA NCHI YOYOTE MKOA WOWOTE KWA MATATIZO YAFUATAYO:-

 KUFANIKISHA NDOA KWA UNAYE MPENDA KWA HARAKA. KUMRUDISHA MPEZI NDANI YA MASAA 12 TU.
 ULIJALI (NGUVU ZA KIUME) NDANI YA /IKI MMOJA TU
MIGUU KUWAKA MOTO KUTAFSIRI NDOTO MFARAKANO WA WANANDOA MFARAKANO KAZINIKUPANDISHWA CHEO NDANI YA SIKU SABA 7 TU.
KUTOA PETE YA BAHATI KUTOA MAJINI MACHAFU IKIWA NI KWENYE MWILI WA BINADAMU MAJUMBANI NA KWENYE BIASHARA.

KUPATA MAFANIKIO YA MALI BILA YA MASHARTI. KUPANDIKIZANYOTA YA KUBASHIRI KUFUNGUA UZAZI KWA WALIYO FUNGWA KWA NJIA YA USHIRIKINA KUTOA VIFUNGO VYOTE VILIVYO FUNGWA KWENYE BIASHARA. ANA UWEZO MKUBWA WA KUPANDIKIZA NYOTA YA KUMPATA YEYOTE UMPENDAYE KWA KUMUOA AU KUWA NAYE.

ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIYE MBALI PIA ALIYE CHUKULIWA
KWA NJIA YAMSUKULE
NAO UWEZO WA KUUA KESI SUGU NA MPYA NDANI SIKU 7 TU.

MENGINEYO MENGI ZAID YALIYO KUWA SUGU PIGA KWA WALE WALIYO ANGAIKA SEHEMU MBALI MBALI SHARIF HAMAD KALALA NI SULUISHO. ENDAPO UTAMSIKILIZA KWA YALE ATAKAYO KUSHAURI NA KUKUPA
ELEKEZI.
 TIBA NI KWA DINI ZOTE POPOTE ULIPO NJE NA NDANI YA NCHI.
MOBILE +255 -673 025 376
WhatsApp +255-757 069 066

Trump Aridhika na Mazungumzo Pamoja na Kim, Wasaini Makubaliano Maalumu

$
0
0
Trump Aridhika na Mazungumzo Pamoja na Kim, Wasaini Makubaliano Maalumu
Rais Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wamemaliza mazungumzo ya kwanza ya kihistoria kwa kutia saini taarifa juu ya ahadi za kuangamiza silaha za nuklia za Korea Kaskaizni.

Trump akizungumza baada ya kutia saini hati hiyo amesema ameridhika kabisa na mazungumzo na wameanzisha uhusiano mzuri kati yao.

"Ninadhani uhusiano kamili kati yetu na Korea Kaskazini utabadilika na kua tofauti na namna ilivyo kua awali na tumeweza kukuza uhusiano mzuri kuliko vile tulivyotarajia."

Akiulizwa ikiwa atamualika Kim Washington alijibu, Bila shaka.

Kim kwa upande wake amesema wamekubaliana kuacha nyuma yaliyopita na kufungua ukurasa mpya wa uhusiano.

Kabla ya kutia saini Trump na Kim walikutana kwa mara ya kwanza na kupeana mkono asubuhi katika hoteli ya Capella kwenye kisiwa cha mapumziko cha Sentosa, huko Singapore.

Baadae  tena wakakutana ana kwa ana kwa karibu dakika 40, kabla ya kutoka na kukutana pamoja na wajumbe wao wa vyeo vya juu. Katika mkutano huo kulikuwepo mawaziri wa mambo ya nchi za nje na wakuu wa usalama wa taifa wa kila upande.

Walipomaliza mazungumzo hayo viongozi hao walikula chakula cha mchana wakiendelea na mazungumzo bila yakufahamika kile walichokua wanazungumza.

Miongoni mwa masuali muhimu ni namna ya kuangamiza kabisa silaha za nuklia za Korea kaskazini, kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani huko Korea Kusini, suala la wajapan walotekwa nyara, kuheshimiwa haki za binadam, Korea Kaskazini, kuondolewa vikwazo na ushirikiano wa baadae kati ya nchi hizi mbili.

Mwanamke Amuua Mwanaye wa Miaka 3 kwa Kumpiga Mawe

$
0
0
Mwanamke Amuua Mwanaye wa Miaka 3 kwa Kumpiga Mawe
Jeshi la Polisi katika eneo la Murang’a nchini Kenya, linamshikilia mwanamke mmoja kwa tuhuma za kumpiga na mawe mtoto wake wa miaka mitatu na kusababisha kifo chake.

Gazeti la Daily Nation limesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia June 11 2018 katika Kijiji cha Tuthu, mwanamke huyo pia alimshambulia mama yake kwa mawe ambapo alijeruhiwa na kusadikika kuwa mwanamke huyo huenda ana matatizo ya akili.

Mashahidi katika eneo hilo wamedai kuwa mwanamke huyo alianza kurusha mawe kwa watu waliopo katika eneo hilo na kisha badae waliona mwili wa mtoto ukiwa umelala chini ndipo waliamua kuita viongozi wa eneo hilo.

Akithibitisha tukio hilo kamanda wa Polisi katika eneo hilo Ben Kipkoech amesema mtuhumiwa huyo atakabiliwa na kosa la mauji ingawa Polisi wamepata taarifa za kuwa mwanamke huyo ana matatizo ya akili lakini watahitaji ripoti ya daktari kuthibitisha

Kauli Aliyoitoa Leo Rais Magufuli kwa Viongozi wa Dini Kuhusu Matamko Yao

$
0
0
Kauli Aliyoitoa Leo Rais Magufuli kwa Viongozi wa Dini
Rais Dkt. John Magufuli amewataka viongozi wa dini nchini Tanzania kuacha tabia ya kuwatafuta wasemaji wa dini zao bali wanapaswa wazungumze wao wenyewe kitu wanachotaka kukifikisha kwa waumini wao ili kuweza kunusuru chumvi za watu watakaotumwa kuwazungumzia.


Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo leo Juni 12, 2018 wakati alipokuwa anafanya ukaguzi wa Msikiti Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa Kinondoni Jijini Dar es Salaam kwa kupitia mfadhili Mfalme Mohammed wa sita kutoka Morocco.

"Mkishakuwa na wasemaji wengi katika masuala ya dini hata yale mnayoyasema yanakosa maana na mara nyingi huwa yanakosa muelekeo na wasikilizaji hawataelewa kuwa hayo yanayosemwa yanatoka kwa viongozi wa dini au na wengine waliotumwa na wanaotumwa mara nyingi wanapenda kuweka chumvi kwa manufaa yao binafsi", amesema Rais Magufuli.

Pamoja na hayo, Magufuli ameendelea kwa kusema "panapozungumzwa neno lolote linalohusu masuala ya dini au ushauri wowote unaohusika na dini, unapaswa uzungumzwe na watu wa dini wenyewe kama ni masheikh azungumze Mufti, kama Mchungaji azungumze Mchungaji msitafute wasemaji kwa niaba yenu, mtakuwa mnatupoteza pabaya".

Mbali na hilo, Rais Magufuli amewahakikisha viongozi wa dini zote nchini kuendelea kushirikiana nao kwa hali na mali kwa kuwa serikali haina dini.

"Napenda kuwaahidi viongozi wa dini zote kwamba serikali yangu itaendelea kushirikiana na dini zote na niendelee kuwaomba viongozi wa dini msiwe na wasemaji ambao sio viongozi wa dini. Mnapokuwa viongozi wa dini halafu mkawatumia wasemaji ambao sio viongozi wa dini labda ni wanasiasa, mtakuwa mnachanganya dini na siasa ambacho ni kitu kibaya sana", amesisitiza Magufuli.

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amepewa ahadi na wakandarasi wa ujenzi wa msikiti huo ambao utakuwa unabeba zaidi ya watu elfu nane (8,000) kuwa unatarajiwa kukamilika mwaka 2019 kati ya mwezi Aprili au Mei
Chanzo: EATV

Mahakama Yaweka Zuio kwa Benki Zote Nchini Kutoa Pesa za Ruzuku CUF

$
0
0
Mahakama Yaweka Zuio kwa Benki Zote Nchini Kutoa Pesa za Ruzuku CUF
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeweka zuio la muda kwa benki zote nchini kutotoa pesa zozote za ruzuku ya Serikali kwa Chama cha Wananchi (CUF), hadi kesi zinazohusu mgogoro wa uongozi unaofukuta ndani ya chama hicho zitakapoamuriwa

Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Wilfred Dyansobera, Ijumaa iliyopita kufuatia maombi yaliyowasilishwa na Bodi ya Wadhamini wa chama hicho, kambi ya Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.

Bodi hiyo kupitia kwa mawakili wake Juma Nassoro na Daimu Halfani waliwasilisha mahakamani hapo maombi hayo, baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuruhusu ruzuku ya zaidi ya Sh.600 milioni.

Msajili wa Vyama alitoa kiasi hicho cha ruzuku kwa chama hicho, kambi ya Mwenyekiti wake wa Taifa anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba, licha ya kuwepo kwa amri ya kumzuia kutoa ruzuku kwa chama hicho kambi yoyote.

Kufuatia maombi hayo, Jaji Dyansobera katika uamuzi wake wa Ijumaa ametoa amri ya kuzizuia benki zote nchini kutoa ruzuku ya Serikali kwa chama hicho kambi yoyote kulingana na uamuzi wake wa awali dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Kwa uamuzi huu chama hicho hakitaweza kutoa pesa yoyote katika akaunti zake zinazohusiana na ruzuku ya Serikali, hadi kesi zilizoko mahakamani zinazotokana na mgogoro huo wa uongozi zitakapoamuriwa.
Chanzo: Mwananchi

Mhasitu Atumia Kanga Kujinyonga Katika Choo cha Baa

$
0
0
Mhasitu Atumia Kanga Kujinyongea Katika Choo cha Baa
Watu wanne wamefariki dunia Mkoani Kilimanjaro, katika matukio tofauti, likiwamo la Mhasibu wa Taasisi ya fedha ya utoaji wa mikopo kwa wakulima na wafugaji (Brac), Victoria Kimario, kujinyonga kwa kutumia kanga katika choo cha Baa moja iliyoko Mkuu Wilaya ya Rombo.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari leo Juni 12, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah, alisema vifo hivyo vilitokea kwa nyakati na maeneo tofauti, Juni 9, mwaka huu.

Akizungumzia tukio la mhasibu wa Brac kujinyonga, Kamanda Issah amesema, tukio hilo lilitokea majira ya saa 4:45 usiku katika choo cha baa inayojulikana kwa jina la Mgombani iliyoko eneo la Mkuu.

“Choo cha baa ambacho alikutw amarehemu ni jirani na alikokuwa akiishi na uchunguzi bado unaendelea, ili kubaini chanzo cha kujinyonga kwake,”amesema Kamanda Issah.

Katika tukio jingine, kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Hassan Bakari(27)mkazi wa kijiji cha Rau River, kata ya Mabogini, amefariki baada ya kujinyonga kwa kutumia shuka la kimasai juu ya mti.

Kamanda alisema kijana huyo ambaye alikuwa dereva wa mitambo ya ujenzi wa barabara, alikutwa amejinyonga kwenye mti jirani na nyumbani kwao Juni 9 mwaka huu.

Wakati huo huo, Fidelis Kimaro,mpakia mizigo (kuli) kwenye magari ya mizigo, mkazi wa Vunjo Mashariki, amefariki dunia baada ya kuruka kwenye gari.

“Mwili wa marehemu ulikutwa pembeni ya barabara kuu ya Arusha-Dar es Salaam, eneo la njia Panda ya Himo, saa 6 mchana na uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa aliruka kwenye gari alipofika maeneo ya nyumbani kwake na gari alilokuwepo lilikimbia na tunaendelea kulitafuta”a,esema

Katika tukio lingine, mwili wa Bakari Anasey (43)mkazi wa Siha  ulikutwa katika mashamba ya Mountain Side ukiwa na majeraha yanayoonyesha kuchomwa na kitu vyenye ncha kali.

Dudu Baya Afunguka Mazito Kuhusu Mwanaye Willy

$
0
0
Dudu Baya Afunguka Mazito Kuhusu Mwanaye Willy
Msanii wa Bongo Flava, Dudu Baya ameonesha kutopendezwa na kitendo cha mwanae, Willy kutoa wimbo bila hata kumsikilizisha.

Dudu Baya amesema Willy angetakiwa kufanya hivyo kwani na yeye ni msanii pia.

“Mimi ni mwanamuziki, yeye ni mwanamuziki na mimi ni baba yake hajawahi kunisikilizisha ngoma ina maana kawasilizisha baba zake wengine,” amesema.

“Kwa hiyo mama yake yeye ndio anajua baba zake wengine ndio maana kawasikilizisha wale, hajaja kuniimbia mimi hata freestyle,” Dudu Baya ameiambia Clouds TV.

Dudu Baya ameongeza kuwa toka ameanza muziki amewasaidia wasanii wengi kupitia project zake mbali mbali kama Dudu Baya Foundation na Dar Scandal na hadi sasa anafanya hivyo.

Wanajeshi wa Uganda Wawakamata Polisi wa Kenya na Kuwasweka Rumande

$
0
0
Wanajeshi wa Uganda Wawakamata Polisi wa Kenya na Kuwasweka Rumande
Wanajeshi wa Uganda wanawashikilia maofisa usalama watatu wa Kenya katika kile kinachoonekana ni utata unaozingira haki ya uvuvi kwenye Ziwa Victoria.

Maofisa hao walikamatwa na kupokonywa silaha na wanajeshi wa UPDF Jumatatu karibu na Mageta na Kisiwa cha Hama ndani ya Ziwa Victoria na walipelekwa katika nchi kavu jirani kwa kutumia boti.

Mashuhuda waliliambia gazeti la Nation kwamba maofisa hao walipokonywa bunduki na simu zao kabla ya kupeleka gereza la Bugiri nchini Uganda majira ya saa 12:00 jioni.

Kamanda wa polisi wa Kaunti ya Siaya Patrick Lumumba alisema mkasa huo uliotokea saa 9:00 alasiri uliwahusisha wanajeshi wanane waliokuwa kwenye gari la doria.

Maofisa, alisema walizingirwa na wakawekwa pamoja na wavuvi wa Kenya waliokutwa wakivua samaki kwenye eneo la Uganda.

Lumumba alisema washambuliaji, walikuwa wamejihami kwa silaha nzito, kwanza waliteka boti tano na wakachukua injini zao.

"Maofisa wetu walizidiwa na washambuliaji waliokuwa wamejihami kwa silaha walioweka mtego wa kuvizia wakidhani ni raia na wavuvi,” alisema Lumumba.

Kamishna wa Mkoa wa Nyanza Moffat Kangi alipanga kwenda kujaribu kupata ufumbuzi wake.

Tuweke Kiki Pembeni Tufanye Muziki- Wakazi Afunguka

$
0
0
 Tuweke Kiki Pembeni Tufanye Muziki- Wakzi
Wakazi ni mmoja ya rappers ambao hawataki kuamini kwenye mambo ya kiki katika kuboost ngoma za wasanii bali anaamini muziki mzuri unaweza kufanya vizuri hata bila ya kiki.

Wakazi amesema kuwa kwa sasa wasanii wa muziki wa Bongo Fleva wanafanya vioja kiasi kwamba hata mashabiki wanajua ni kiki kuna wimbo unatoka.

“Tuweke kiki pembeni tufanye muziki, nadhani muziki ndiko unakoelekea hata raia wanaosikiliza muziki na kuufuatilia wameanza kuchoka sasa. Kwa sababu unakuta mtu kafanya vioja hadi unajua kuwa hii sasa single inakuja,”ameeleza Wakazi kwenye mahojiano yake na Times FM kwenye kipindi cha Playlist.

“Halafu angalia sometimes mambo ya kiki yanavyokuwaga mabaya, inawezekana ikaleta shop value ile unayohitaji ili watu wasikilize bidhaa yako halafu baadae unakuta watu wanaizungumzia kiki yako kuliko hata wimbo wako, wakati wewe unataka wimbo uzungumziwe ili upate show,”amesema Wakazi.
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images