Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Nahreel na Aika Waweka Wazi Mipango ya Kufunga Ndoa

0
0
Nahreel na Aika Waweka Wazi Mipango ya Kufunga Ndoa
Wasanii Nahreel na Aika wanaounda kundi la Navy Kenzo ambao pia ni wapenzi wamefunguka kuhusu mipango ya kufunga ndoa.

Nahreel ambaye ni producer pia katika mahojiano na FNL ya EATV alieleza kuwa muunganiko wao kama wapenzi ni muhimu zaidi kwa sasa kabla ya ndoa.

“Mimi na Aika nadhani the bond ni special, wedding ni important kufanyika katika maisha lakini Bond yangu na Aika is very special,” alisema Nahreel.

Kwa upande wake Aika alieleza kuwa; ‘Na tusiwafundishe watu wengine kuwa walazimishe kuingia kwenye ndoa kabla mtu hajawa tayari kuwa na ile bond, ni muhimu sana’.

Navy Kenzo ambao wanatamba na ngoma yao mpya inayokwenda kwa jina la Fella, katika mahusiano yao ambayo yamedumu kwa takribani miaka 10 sasa wamejaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume.

Mbowe Alazwa Muhimbili Baada ya Kudondoka Ghafla Alfajiri ya Leo

0
0
Mbowe Alazwa Muhimbili Baada ya Kudondoka Ghafla Alfajiri ya Leo
Mahakama imeambiwa kuwa mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kudondoka ghafla alfajiri.

Jeremiah Mtobesya ambaye ni wakili wa Mbowe, aliiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, kuwa mteja wake alianguka leo Juni 18 akiwa nyumbani kwake.

Kadhalika, Mahakama imeelezwa kuwa Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai, amefiwa na kaka yake, Henry Mbowe.

Akiwasilisha taarifa hiyo, Wakili Mtobesya alieleza kuwa Mbowe ambaye ni mshtakiwa namba moja katika kesi namba 112 ya 2018 amefiwa na kaka yake usiku wa kuamkia leo.

Awali Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi aliiambia mahakama kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya washtakiwa Mbowe na wenzake wanane kusomewa maelezo ya awali PH na kwamba wamejiandaa na wapo tayari.

Hata hivyo aliiambia mahakama kuwa Juni 12 na 14 , 2018 walipokea mapingamizi ya kisheria na kwamba wapo tayari kuendelea na mapingamizi hayo.
Chanzo: Mwananchi

“Unaweza Usiipende Sura ya Magufuli”- RC Mongella

0
0
“Unaweza Usiipende Sura ya Magufuli”- RC Mongella
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, amesema kuwa hakuna sababu ya msingi kwa mtu yeyote nchini ambaye ana hoja za kutilia shaka utendajikazi wa Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli labda kuwe na sababu nyingine ambazo ni nje ya utendajikazi.


Mongella ameongea hayo Juni 17, 2018 wakati wa uzinduzi wa kivuko kipya cha MV Mwanza ambacho kitafanyakazi katika eneo la Kigongo-Busisi, na kuongeza kuwa Serikali ya awamu ya tano imefanikiwa kufanya mambo makubwa katika kipindi cha muda mfupi tangu kuingia madarakani chini ya Rais Magufuli.

“Unaweza kumsema Magufuli labda hupendi sura yake, lakini huna namna ya kusema huyu mtu hafanyikazi, Serikali inapiga kazi leo tunaona meli MV Mwanza itaenda pale Kigongo feri kwenda Busisi ina uwezo mkubwa, ni jambo kubwa hii meli ni ya kisasa zaidi ni nyepesi, ina kwenda kasi na inabeba mzigo mkubwa” amesema Mongella

Mongella ameongeza kuwa kivuko hicho cha kisasa kitasaidia ufanisi katika sekta ya usafiri wa majini katika ziwa victoria kwasababu itasafirisha mizigo mikubwa kwa wakati mmoja na kwa gharama nafuu na kuwataka wananchi kuunga mkono jitihada za maendeleo zinazofanywa na Rais Magufuli.

Kivuko cha MV Mwanza kina uwezo wa kubeba uzito wa tani 250, kitafanya kazi katika eneo la Kigongo–Busisi Mkoani Mwanza na utengenezaji wake umegharimu jumla ya shilingi bilioni 8 na kitaweza kubeba abiria 1000 na magari 36 kwa wakati mmoja.

Kiboko Azua Taharuki Baada ya Kuonekana Kihonda, Morogoro

0
0
Kiboko Azua Taharuki Baada ya Kuonekana Kihonda, Morogoro
Kiboko ameonekana leo asubuhi eneo la kata ya Kihonda, manispaa ya Morogoro barabara kuu ya Dodoma-Morogoro.

MCL Digital ilifika eneo la tukio na kushuhudia kiboko huyo akiwa kajificha chini ya kalavati lenye maji.

Awali, wanafunzi wa darasa la saba waliokuwa wakielekea shule ndiyo walikuwa wa kwanza kumuona kiboko huyo akiwa kwenye barabara ya lami eneo hilo.

Baadaye alitoka barabarani na kuingia kwenye kalavati la maji.

Ilionekana kama umati wa watu uliokuwa katika eneo hilo ulimtia hasira kiboko huyo ambaye alikuwa akitoka na kuingia kwenye maji.
Chanzo: Mwananchi

Hili Ndilo Kanisa la Walevi la Afrika Kusini Linalotukuza Unywaji Pombe

0
0
Hili Ndilo Kanisa la Walevi la Afrika Kusini Linalotukuza Unywaji Pombe
Wakati wa kumuomboleza mwanaharakati aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi Afrika Kusini Winnie Mandela, siku moja, kundi la waumini walioonekana kulewa walizua kionja.

Walikuwa wakilia na kuimba "Mama, Mama". Walijitetea kwamba nao pia walikuwa na haki ya kumuomboleza mtu waliyemuenzi sana.

Hakuwa mwingine ila Papa Makiti kiongozi wa kanisa jipya nchini Afrika Kusini ambalo limekuwa likiwashangaza wengi.

Kanisa hilo linalofahamika kwa jina Gobola (yaani nipe Ulevi ninywe kidogo kwa Lugha ya Kitswana, moja ya lugha rasmi nchini humo) lina mwaka mmoja hivi tangu lianzishwe.

Mwasisi wa kanisa hilo ni Father Tsietsi D Makiti, 53, ambaye kwa sasa anajiita Papa Makiti. Hujieleza kama papa wa kwanza mweusi kutoka bara la Afrika.

Alilianzisha kanisa hilo katika baa moja, na kanisa hilo hufanya ibada zake katika baa na vilabu.

Mhubiri awaomba waumini wamnunulie ndege Marekani
Aliambia mwandishi wetu wa Afrika Kusini Omar Mutasa kwamba kanisa la Gobola na ulevi, vyote ni vya Mungu na ni wajibu wake kuwapa nasaha bora walevi wote waliofukuzwa kwenye makanisa mengine.

Kanisa kuu la Gobola limo ndani ya baa inaitwa Freddie's Tarvern na mwenye baa hiyo Askofu Freddie Mathebula ndiye naibu wa Papa Makiti, husaidia kuongoza mahubiri na ibada wakati mwingine.

Tangu kuanzishwa kwake, kanisa hilo limekuwa likipata umaarufu na inakadiriwa kwamba kwa sasa lina waumini kati ya 500 na 2,000, ingawa idadi yenyewe ni vigumu kuithibitisha.

'Huu ni ukumbi kwa watu kuja pamoja kwa jina la Mungu bila kuaibishwa kwa kuwa walevi," anasema.

Jay Z na Mkewe Beyonce Waachia Albamu ya Pamoja Wamtaja Trump

0
0
Jay Z na Mkewe Beyonce Waachia Albamu ya Pamoja Wamtaja Trump
Kumekuwepo na tetesi kwa muda mrefu lakini hatimaye nyota wa muziki - Beyonce na mumewe Jay-Z - wametoa albamu yao ya pamoja.

Albamu hiyo imepewa jina Everything is Love (Kila Kitu ni Mapenzi).

Albam hiyo inapatikana katika huduma ya kusikiliza na kununua nyimbo mtandaoni inayomilikiwa na Jay-Z kwa jina Tidal.

Beyonce alitoa tangazo la kutolewa kwa albamu hiyo akiwa kwenye jukwaa London na wawili hao waliwashukuru mashabiki wao kwa kujitokeza kuwatazama wakati wa tamasha yao ya kuizuru dunia.

Alisema: "Kwa sababu twawapenda sana, tuna kitu cha kipekee sana kwa ajili yenu."

Beyonce na Jay-Z katika video yao mpya ya muziki, nyuma yao ni picha ya Mona Lisa
Video ilichezwa kwenye skrini na mwishowe kukatokea ujumbe kwamba 'ALBAMU IMETOKA SASA'.

Video ya muziki ya dakika sita ilitolewa punde baadaye, ambayo iliandaliwa katika makumbusho maarufu duniani ya Louvre mjini Paris.

Hamornize Kiboko Amwita Mpenzi Wake Sarah Stejini Hiki Ndicho Alichomfanyia Mbele ya Mashabiki

0
0
Hamornize Kiboko Amwita Mpenzi Wake Sarah Stejini Hiki Ndicho Alichomfanyia Mbele ya Mashabiki
MWANAMUZIKI Harmonize amemfanyia saparaizi ya pekee mpenzi wake aitwaye Sarah, raia wa Italia, baada ya kumuita stejini na kumweleza anavyompenda mbele ya mashabiki, akimpa ushauri wa kuacha kufuatia stori za mitandao ambazo zinasababisha migogoro isiyo na maana kwa wapendanao.

Alimalizia kwa kucheza naye stejini huku mashabiki wakimshangilia kwa kumpata “Mtasha” huyo.

Chid Benz Akamatwa na Mzigo wa Gramu Tano Bangi Dodoma

0
0
Chid Benz Akamatwa na Mzigo wa Gramu Tano Bangi Dodoma
STAA wa Bongo Fleva, Rashidi Makwiro maarufu kama ‘Chid Benz’ amekamtwa na Jeshi la Polisi jijini Dodoma kwa tuhuma za kukutwa na mzigo wa bangi kiasi cha gramu tano.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema hayo leo Jumatatu, Juni 18, 2018 wakati akizungumza na wanahabari jijini humo baada ya kumtia mbaroni msanii huyo.

Hii ni mara ya pili kwa Chidi kukamatwa na madawa ya kulevya huku akidai kuwa alishaacha kutumia madawa hayo na anaendelea na matibabu Sober House.

Hii ni sehemu ya taarifa ya polisi kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa mbaliombali akiwemo Chidi.


Hakuna Mwanamke Wa Kunipindua Kwa Dogo Janja- Uwoya

0
0

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Irene Uwoya amefunguka na kuweka wazi kuwa bado hajaona mwanamke ambaye anaweza kimpindua kwa mume wake staa wa Bongo fleva Abdul Chende ‘Dogo Janja’.

Uwoya ameweka wazi kuwa yeye ni mwanamke anayejiamini sana na anaamini kuwa mume wake anampenda na anajua kuwa hakuna mwanamke anayeweza kuingilia penzi lao.

Irene Uwoya amefunguka hayo Kwenye mahojiano na Global Publishers ambapo amesema alipoamua kuingia kwenye ndoa na mwanamuz­iki huyo alijua wazi ‘nyakun­yaku’ wapo, la­kini kikubwa anajiamini.

Mimi sio mwan­amke wa kufuatana na mume nyuma kwa sababu najiamiani kuliko na ninajua wazi hakuna ambaye anaweza kunin­yakulia mume wan­gu. Najiamini kila idara mimi sina wasiwasi wowote”.

Uwoya amesisitiza kuwa hata mume wake aende wapi na aone mwanamke gani hawezi kumuacha yeye maaana anajiamini na anaamini kuwa amekamilika idara zote.

Miujiza ya Maalim Khatibu Kutoka Bagamoyo Pwani

0
0

MAALIM KHATIBU anawashukuru wale wote wanaopiga simu za shukrani, na wale ambao bado wanamatatizo musikate tamaa kwa kuchelewa kupokelewa simu zenu,

(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu) 

MAALIM KHATIBU Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN dawa za asili ya afrika na njiwa,

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu MAALIM KHATIBU sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata maelekezo yake,

 ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO   HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, NA KUPONYA MAGONJWA SUGU, ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI, 

JE UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU, 

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE) 

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No: 

Mobile +255 710-332103
WhatsApp +255 766-705404
Instagram: Follow@maalim_khatibu

USHAURI: Ni vyema kupiga simu kuliko kutuma sms ili upate msaada kwa wakati.

Waziri wa Maji Kavunja Bodi ya Wakurugenzi ya DAWASA

0
0

Waziri wa Maji na Umwagiliaji (Eng) Isack Kamwele amemsimamisha kazi Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi, Romanus Mwang'ingo kwa tuhuma za ubadhirifu na udanganyifu katika utekelezaji wa mradi wa kuchimba visima maeneno ya Kimbiji na Mpera huko Kigamboni, Jijini Dar es salam.


Maamuzi hayo ya Waziri Kamwele yamekuja leo Jumatatu, Juni 18 baada ya serikali kupokea taarifa za kuwepo kwa udanganyifu katika mradi huo ambapo mbali na ubadhirifu uliogundulika pia upo udanganyifu wa idadi ya visima  vilivyokamilika kama ambavyo taarifa zilizowasilishwa wizarani  na DAWASA na uhalisia katika eneo la utekelezaji miradi.


Aidha Taarifa ya Waziri Kamwele imesema kuwa kutokana na kuwa Mhandisi Mwang'ingo ndiye aliyekuwa Msimamizi Mkuu wa mradi huo kwa niaba ya DAWASA na seerikali basi anatengua nafasi yae hiyo ili kupisha uchunguzi wa TAKUKURU.


Aidha Waziri amemteua Dkt. Sufian Masasa kukaimu nafasi hiyo mpaka utaratibu mwingine utakapokamilika.


Pamoja na hayo Waziri Kamwele amevunja Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA kwa kushindwa kuchukua hatua mapema katika kunusuru mradi huo.

Mwigulu ajibu wanaoibeza na Kusema Bajeti ya Mwaka Huu ni 'Bajeti Hewa'

0
0

Serikali ya awamu ya tano kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema wanaobeza Bajeti ya mwaka 2018/2019 ni hewa hawaelewi maana halisi ya Bajeti yenyewe.


Mh. Mwigulu ametoa kauli hiyo wakati wa mahafali ya kwanza ya vijana wa Chama cha Mapinduzi wa vyuo vikuu vya Mkoa wa Kilimanjaro na kusema kuna watu wameibuka wakidai Bajeti ya serikali ya mwaka 2018/2019, ya Shilingi trilioni 32.47 iliyowasilishwa Juni 14 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango ni hewa jambo ambalo si sahihi.


"Haijawahi kutokea Bajeti ya Maendeleo kuwa hewa, hivyo wanaozungumza na kujadili kwenye mitandao ya kijamii kuwa ni hewa hawaelewi maana halisi ya Bajeti", amesema Mwigulu.


Kwa upande mwingine, Mwigulu amesema kuwa ni lazima kufunga mkanda na kujenga misingi itakayoiwezesha nchi kusimama na kujitegemea

Tunatibu na Kuponesha Kabisa Tatizo la Upungufu wa Nguvu za Kiume, Busha Bila Kupasua na Vidonda vya Tumbo

0
0
TUNATIBU NA KUPONESHA KABISA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME BUSHA BILA BILA KUPASUA NA VIDONDA VYA TUMBO: kwa nini uhendelee kuteseka NA kujiona mpweke pale ukutanapo NA mke au mpenzi wako kwa sababu tu hunaupunguvu wa nguvu za kiume na uume mdogo

MAPRO POWER NO 2 ndio tiba sahii ya kukurudishia heshima ya ndoa yako 1 itakufanya uchelewe kufika kileleni mda wa dakika 15-20 kwa tendo LA kwanza 2 itaufanya uume wako uhonekane mkubwa hasa kwa wale wanaume ambao wamefanyiwa tohara wakiwa wadogo sana au wakiwa watu wazima kwani ipo dawa ya kuimalisha misuli ya uume 3 itakupa uwezo wa kurudia tendo LA ndoa zaidi ya Mara tatu 4 uhuimalisha misuli iliyolegea na kusinyaa ?

WAI SASA UPATE TIBA YA UKWELI NA UHAKIKA NA NI TOFAUTI NA ULIZOWAI KUTUMIA ata wazee wa miaka 80 wanatumia na kupona kabisa ? Tunatoa dawa za uzazi maumivu ya mgongo na kiuno ,kupunguza kitambi ,matiti makubwa,dawa za kisukari,presha,dawa za mvuto wa mpenzi ambaye akutaki au hakuhudumii ipasavyo kutengeneza shepu kwa kina Dada, fika ofisini kwetu MBAGALA ZAKHEMU BARABARA YA JESHINI HIENDA KIBONDEMAJI utaona ifisi himeandikwa MABULA CLINIC

AU PIGA SIMU NO 0743362017 DR AGU

KWA AMBAO HAWANA NAFASI YA KUFIKA OFISINI UDUMA HII UTALETEWA

Miili ya Wanajeshi Waliokufa kwa Ajali Mbeya Kuagwa Kesho

0
0
Miili ya Wanajeshi Waliokufa kwa Ajali Mbeya Kuagwa Kesho
Mwili wa Mwanajeshi mmoja, vijana 10 wa JKT na Wafanyakazi wawili wa basi la Igunga Express waliofariki June 14 mwaka huu katika eneo la maili tano mtaa wa Igodima Mbeya itaagwa kesho katika kambi ya JKT Itende

Akizungumza na waandishi wa Habari leo June 18, 2018 katika ukumbi wa JKT Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Jeshi la Wananchi (JWTZ ) Kanali Ramadhan Dogoli amesema taratibu zote zimekamilika.

Amesema taratibu zote zitafanyika kambini hapo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Jeshi na kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Mbeya.

Aidha Kanali Dogoli amesema chanzo cha ajali hiyo kinachunguzwa na mamlaka husika ambapo taarifa itatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.

Hata hivyo amewaomba Wananchi jijini Mbeya kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia tukio la kuagwa miili hiyo ambapo baada ya kuagwa miili itasafirishwa kwenda maeneo mbalimbali nchini.

Majeruhi wameendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa Mbeya, JKT Itende na Hospitali ya Jeshi Mbalizi.

Waziri wa Maji Amsimamisha Kazi Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA..... Bodi ya Wakurugenzi Yavunjwa

0
0
Waziri wa Maji Amsimamisha Kazi Afisa Mtendaji Mkuu na Kavunja Bodi ya Wakurugenzi ya DWASA
Waziri wa Maji na Umwagiliaji (Eng) Isack Kamwele amemsimamisha kazi Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi, Romanus Mwang'ingo kwa tuhuma za ubadhirifu na udanganyifu katika utekelezaji wa mradi wa kuchimba visima maeneno ya Kimbiji na Mpera huko Kigamboni, Jijini Dar es salam.

Maamuzi hayo ya Waziri Kamwele yamekuja leo Jumatatu, Juni 18 baada ya serikali kupokea taarifa za kuwepo kwa udanganyifu katika mradi huo ambapo mbali na ubadhirifu uliogundulika pia upo udanganyifu wa idadi ya visima  vilivyokamilika kama ambavyo taarifa zilizowasilishwa wizarani  na DAWASA na uhalisia katika eneo la utekelezaji miradi.

Aidha Taarifa ya Waziri Kamwele imesema kuwa kutokana na kuwa Mhandisi Mwang'ingo ndiye aliyekuwa Msimamizi Mkuu wa mradi huo kwa niaba ya DAWASA na seerikali basi anatengua nafasi yae hiyo ili kupisha uchunguzi wa TAKUKURU.

Aidha Waziri amemteua Dkt. Sufian Masasa kukaimu nafasi hiyo mpaka utaratibu mwingine utakapokamilika.

Pamoja na hayo Waziri Kamwele amevunja Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA kwa kushindwa kuchukua hatua mapema katika kunusuru mradi huo.


Nina Kazi Nyingi za Kuniingizia Fedha Kuliko Muziki- Shilole

0
0
Nina Kazi Nyingi za Kuniingizia Fedha Kuliko Muziki- Shilole
Msanii wa Bongo Flava, Shilole amema si kweli kuolewa kwake kunamfanya kushuka kimuziki.

Muimbaji huyo akizungumza katika show ya Davido mwishoni mwa wekeend iliyopita amesema kuwa amekuwa kimya kutokana ana kazi nyingi nje ya muziki ila sio ndoa.

“Sio kweli, mimi ningekuwa nimepungua kwenye game usingenifanyia interview sasa hivi. Sio kweli nina kazi nyingi za kuniingizia fedha kuliko muziki,” alisema Shilole.

Tangu Shilole aipoolewa December 06, 2017 hajatoa wimbo wowote, wimbo wake wa mwisho kutoa unaitwa Kigori ambao ulitoka August 07, 2017.

Licha ya Shilole kuwa msanii kwa upande mwingine ni mjasiriamali ambapo kwa sasa anamiliki biashara kadhaa kama mgahawa wa chakula ‘Shishi Food’, na bidhaa za Shishichili.

Madaktari Wamficha Mbowe ..... Waliopanga Kwenda Hospitali Kumuona Watakiwa Wasitishe Kwenda

0
0
Madaktari Wamficha Mbowe ..... Waliopanga Kwenda Hospitali Kumuona Watakiwa Wasitishe Kwenda
Jopo la Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam ambapo amelazwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamewapiga marufuku watu kuenda kumtazama Mbowe kwa kile wanachodai kuwa yupo kwenye vipimo.


Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Itifaki, Uenezi, Mawasiliano na Mambo ya Nje CHADEMA, John Mrema leo Juni 18, 2018 kupitia mtandao wao maalum wa chama baada ya kupita masaa machache tokea ilipo ripotiwa taarifa ya kiongozi huyo ndani ya Mahakama kuwa ameshindwa kuhudhuria kesi yake kutokana na kuanguka ghafla na kukimbizwa Hospitalini.

"Nimefika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikolazwa Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. Freeman Mbowe, kwa sasa madaktari wameshauri kuwa mgonjwa hataweza kuonwa kwa kuwa yuko kwenye vipimo. Hivyo kwa wale wote ambao walikuwa wamepanga kwenda hospitali kumuona mnaombwa msitishe hadi mtakapopewa taarifa nyingine", amesema Mrema.

Kwa upande mwingine, Mkurugenzi wa Itifaki, Uenezi, Mawasiliano na Mambo ya Nje CHADEMA, John Mrema amesema hali ya Mbowe kwa sasa inaendelea vizuri tofauti na alipopelekwa hapo awali.

Kiboko Aliyeleta Taharuki Moro Auliwa.... Wananchi Wagaiwa Nyama Yake

0
0
KUFUATIA mnyama aina ya Kiboko aliyeibuka na kuzua taharuki kwa saa kadhaa jirani na makazi ya watu maeneo ya Kihonda Mbuyuni karibu na Kanisa la Mangwea nje kidogo ya mji wa Morogoro, ameuawa kwa kupigwa risasi kisha kukatwa kichwa na Maofisa Maliasili, huku nyama yake ikigawiwa kwa wananchi waliokuwa eneo la tukio.
KUFUATIA mnyama aina ya Kiboko aliyeibuka na kuzua taharuki kwa saa kadhaa jirani na makazi ya watu maeneo ya Kihonda Mbuyuni karibu na Kanisa la Mangwea nje kidogo ya mji wa Morogoro, ameuawa kwa kupigwa risasi kisha kukatwa kichwa na Maofisa Maliasili, huku nyama yake ikigawiwa kwa wananchi waliokuwa eneo la tukio.

Kabla ya kuuwawa kwa kiboko huyo anadaiwa hakuleta madhara yoyote kwa watu na wananchi wamejitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo ambalo limewaacha na mshangao mkubwa.

Askofu Akamatwa kwa Utapeli Dodoma

0
0
Askofu Akamatwa kwa Utapeli Dodoma
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia Askofu Martin Gwila wa Kanisa la Agape Sanctuary International kwa tuhuma za utapeli wa kiasi cha zaidi ya Sh 63 milioni.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema kiasi hicho cha fedha alikipata baada ya kuwadanganya watu mbalimbali kuwa atawapa ajira kupitia kanisa lake.

Pia anadaiwa kuwalaghai waumini akiwataka watoe fedha ili wasajiliwe na alitoza viwango tofauti vya fedha.

“Askofu huyo alikamatwa mwishoni  mwa  wiki jijini Dodoma na alipokea fedha hizo pasipo kutoa ajira yoyote huku akitoa vitisho kwa waliotoa fedha hizo,” alisema

Kamanda Muroto  amesema kuwa kanisa hilo ambalo makao yake makuu yapo Arusha halijasajiliwa kwa mujibu wa sheria kama kanisa bali aliisajili Agape Sanctuary kama kampuni binafsi.

Mtuhumiwa atafikishwa mahakani muda wowote kuanzia sasa.

Polisi Watuhumiwa Kuomba Rushwa ya Kreti za Bia

0
0
Polisi Watuhumiwa Kuomba Rushwa ya Kreti za Bia
Polisi nchini Uganda wanatuhumiwa kuwalazimisha wananchi wawanunulie kreti za bia kama namna ya kutoa rushwa ili waweze kuwaachia huru ndugu zao ambao wapo jela kwa kuvunja sheria za nchi.

Baadhi ya wakazi wamesema wamekuwa wakilazimishwa kufanya mambo nje ya sheria kutokana na kuwa na hamu ya kuwatoa ndugu zao waliofungwa jela.

“Hapa , kama polisi wakimkamata mtu, kitu cha kwanza wanachoomba ni kreti za bia kuanzia kreti 5 hadi 6 kabla ya kufikiria kumuachia ndugu yako” amesema Ms Lilian Andama Lawrence ambaye ni mkazi wa Offaka.

Wakazi hao wameyasema hayo mbele ya wafanyakazi wa Taasisi za Haki ya binadamu (FHRI), Freedom House na ”Judicial Service Commission” (JSC), ambao walitembelea eneo hilo.

Ms Sydey Etima-Ojara, ambaye ni msaidizi na mshauri wa chama cha JSC na Ms Maria Kaddu Busuulwa ambaye Mwenyekiti wa Taasisi ya Haki na sheria wa FHRI wamesema kuwa wanahitaji kuwaelimisha wakazi juu ya kukataa kutoa rushwa inayoombwa na polisi hao.

Ameongezea kuwa kufuatia tukio hili kuna uhitaji mkubwa wa kuwasimamia vyema polisi ili kudhibiti vitendo hivyo.
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images