Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Serikali Yapewa Gawio la Bilioni 1.5 na TTCL

$
0
0
Serikali Yapewa Gawio la Bilioni 1.5 na TTCL
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), limetoa gawio la Sh1.5bilioni kwa Serikali, fedha zilizotokana na faida ya Sh28.5 bilioni ya shirika hilo kwa mwaka jana. Shirika hilo lilipata faida ya Sh29.2 bilioni kabla ya kukatwa kodi.



Akizungumza leo Juni 21 mbele ya Rais John Magufuli wakati wa hafla ya kupokea gawio hilo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba amesema faida hiyo inatokana na mabadiliko makubwa yaliyoanza kuonekana kupitia uongozi wa awamu ya tano.



“Tuliahidi kutoa gawio la Sh1 bilioni, lakini baada ya bodi ya shirika kukaa ikaamua kuongeza gawio hilo baada biashara kwenda vizuri,”amesema.



Kindamba amesema katika juhudi za kuimarisha shirika hilo, wameanza kutekeleza maagizo ya Serikali baada ya kupunguza safari za nje kwa waendaji wake na kufuta mikataba mibovu isiyokuwa na manufaa kwa shirika hilo.



Hafla hiyo imehudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TTTCL, Omar Nundu huku Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akishiriki kwa njia ya teknolojia ya mawasiliano ya video moja kwa moja kutoka Dodoma.


Inasikitisha! Ambaka Mama Yake Mzazi Kisha Kumchinja na Panga Hadi Kufa

$
0
0
Inasikitisha! Ambaka Mama Yake Mzazi Kisha Kumchinja na Panga Hadi Kufa
Mkazi wa mtaa wa Wang'waray mjini Babati mkoani Manyara anashikiliwa na polisi akidaiwa kumbaka mama yake mzazi, kisha kumuua kwa kumchinja akitumia panga.



Inadaiwa kuwa mkazi huyo ambaye anaishi nyumba moja na mama yake alifanya tukio hilo akiwa amelewa baada ya kuvuta bangi na kurudi nyumbani ambapo alimkuta mama yake pia amelewa pombe za kienyeji.



Akizungumza  leo Juni 21 na Mwananchi, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Asia Ramadhani alisema mwanamke huyo alifariki dunia Juni  19 saa 4 usiku akiwa nyumbani kwake katika mtaa huo.



Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Agustino Senga amesema mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 51, alifariki dunia kwa kukatwa shingoni na kitu chenye ncha kali baada ya kubakwa.



"Mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa kwenye hospitali ya mji wa Babati (Mrara) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi kabla ya kufanyika kwa mazishi," amesema Kamanda Senga.

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Mafupi na Upungufu wa Nguvu za Kiume? Suluhisho Hili Hapa

$
0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WANA MAUMBILE MAFUPI NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME DR SITTA NDO SULULISHO LAKO tatiza, hili limekuwa likiwaasili watu wengi,sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine, kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo zipo , sababu nyingi zinazosababisha, tatizo hilo baadhi ni (i) upungufu wa vichocheo vya HORMONES ZA CETROGEN ambazo mwanaume, anapobarehe vichocheo hivi, HORMONES hizo, husaidia ukuaji wa uume

SUPER MIZIZI, ni dawa inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi utakayo na kuzibua mlija iliysinyaa,

NSHOLA ni dawa bora, ya kurudisha nguvu, za, kiume bari inatibu ,kabisa kutoa tatizo hilo, na kukupa , hamu ya , kurudia tendo, la ndoa zaidi, ya mala nne 4 ,bila kuchoka atakama unaumli ,wa mika 80,! pia ana ,dawa za ,kutibu, presha ya kupanda ,na kushuka, kisukari kuondoa, mafuta , mwilini ,na maumivu ya, mgogo kiuno, dawa zipo, matazo, ya hedhi, kwa ,wanawake hedhi, zisizokuwa na, mpangilio, na kasonono, pia , vidonda ,vya, tumbo ,(STOMACHI UCLENS) IHUSHI ndoji lako.

NKANYA ni dwa ya mvuto wa kimapenzi ,mchumba mpenzi ariyekuacha, mke mme, atakuludia kwa, mda, wa msaa3 tu , ukishaitumia atarudi ,mwenyewe bila ,ugovi tena, NKOMA ni dawa kuongeza HIPS na mguu wa bia kwa wadada .

HERBON, ni, dawa, ya kuongeza, CD4, NGAKAMA ,ni dawa ya kutibu ,miguu, kufaganzi, na ,kuwaka moto, huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa! DR SITTA, amebobea, kwa tiba asilia

DAR ANAPATIKANA MBAGALA, ZAKHEM, SONGEA BOMBAMBILI SHINYANGA, KAHAMA MJINI, KWA MAELEZO ZAIDI ,

PIGA SIMU 0763172670 au 0715172670

WOTE MNAKALIBISHWA, KAMA, UTAKUWA NA TATIZOUTAHUDUMIWA,

Mahakama Yamruhusu Sethi Kuongea na Mkewe

$
0
0
Mahakama Yamruhusu Sethi  Kuongea na Mkewe
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeruhusu Mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Harbinder Seth  kuongea na mke wake mahakamani baada ya kutokumuona kwa muda wa miezi mitatu.

Ruhusa hiyo imetolewa leo June 21 na Hakimu Mkuu Mkazi, Huruma Shaidi baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha ombi hilo kufuatia kutokuwa na kibali cha kumuona mumewe huyo gerezani.

Kabla ya kutolewa kwa ruhusa hiyo, wakili wa utetezi, John Chuma aliomba mshtakiwa aweze kuonana na mkewe ambaye hajaweza kumuona kwa kipindi cha miezi 3 sababu kipindi chote hicho alikuwa amefiwa na mama mkwe wake( mama wa mkewe).

“Mheshimia tunaomba mshtakiwa namba moja (Sethi) aweze kuongea na mke wake ikiwezekana hata kumkumbatia ili aweze kumpa pole ya kufiwa na mama yake kwa sababu bado hajapata kibali cha kuruhusiwa kwenda kumuona gerezani”

Akijibu ombi hilo Wakili wa serikali kutoka TAKUKURU, Leornad Swai, alidai, ” kwa sababu ni ombi anaomba kusalimiana na mkewe hapa mahakamani sina pingamizi lakini kwa magereza kuna taratibu zake na mkewe alizivuruga yeye mwenyewe”

Kufuatia majibu hayo, Hakimu Shahidi aliruhusu mshtakiwa kuongea na mkewe mahakamani hapo chini ya uangalizi wa askari magereza.

Kesi hiyo ambayo leo ilikuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika, imeahirishwa hadi July 5, mwaka huu.

Mbali na Seth mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni James Rugemalira ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka kumi na mawili ya uhujumu uchumi ,utakatishaji fedha  na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya shilingi bilioni mia tatu.

Umeme Ndio Umekuwa Chaka Lenu Mafisadi- Heche

$
0
0
Umeme Ndio Umekuwa Chaka Lenu Mafisadi- Heche
Mbunge wa Tarime (Chadema), John Heche, amedai chaka la Ufisadi nchini kwa miaka mingi limekuwa ni sekta ya Umeme huku akitaja mifano ya Songes, Richmond, Tegeta Escrow na mingine lakini waliokamatwa mpaka sasa ni Harbinder Singh Seth na James Rugemarila pekee.

Heche ameyasema hayo Bungeni wakati akichangia hoja katika mjadala wa kupitisha Bajeti Kuu ya serikali 2018 / 2019 iliyowasilishwa Bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango.

“Seth na Rugemarila pekee ndiyo wako gerezani peke yao, Je, hao ndiyo waliobika Tsh. Bilioni 306 za nchi hii? Unatengeza ufisadi mwingiune wa kuiba zaidi ya shilingi trilioni 10 za Watanzania kwenye mradi wa Stiegler’s Gorge,” alisema Heche.

Fid Q Afunguka Kuhusu Muziki wa Hip Hop

$
0
0
Fid Q Afunguka Kuhusu Muziki wa Hip Hop
Msanii wa muziki wa hip hop, kutoka mkoani Mwanza, Fid Q amedai kwa vipaji alivyoviona mkoani humo hata akifa leo hawezi kuacha pengo lolote kwenye muziki huo.


Rapa huyo alitoa kauli hiyo mapema wiki hii mkoani Mwanza akiwa katika Tamasha la Sport & Music Festival baada ya kuona kipaji cha kijana mdogo aitwae, Aga Star.

Kijana huyo alipanda jukwaani na kuanza kuchana hali ambayo ilimfanya Fid Q kumpatia nafasi zaidi kutokana na uwezo ambao aliuonyesha.


“Unajua kuna wakati tunafikiria vitu vingi kwenye huu muziki, lakini nilichogundua leo hata nikifa leo huwenda nisiache pengo kama kuna vijana kama hawa ambao wanaonyesha uwezo mkubwa katika uandishi na kuchana,” alisema Fid Q.

Aga Star baada ya kuonyesha uwezo mkubwa alipatiwa ofa ya kurekodi wimbo chini ya producer Mr Ttouch huku DJ Tass akiahidi kumsaidia kwenye promotion.

WCB Kuongeza Msanii Mwingine wa Kike

$
0
0
WCB Kuongeza Msanii Mwingine wa Kike
Label ya WCB ipo katika mchakato wa kuongeza msanii mwingine wa kike.

Hatua hiyo inakuja baada ya kipindi kirefu Queen Darleen kuwa ndiye msanii pekee wa kike katika label hiyo.

Miongoni mwa mameneja wa WCB, Babu Tale katika mkutano na waandishi wa habari alieleza kuwa hilo limekuwa likiuliziwa kwa siku nyingi kwanini WCB hakuna msanii mwingine wa kike, hivyo sasa wameona ni wakati wa kushughulikia hilo.

“Nimetoka kusemwa juzi, tukaambiwa tuongeze msichana mpya nikawaambia hapana, muda ukifika tutaongeza,” amesema.

“So tutaongeza haya ni maoni yenu ambayo mmekuwa mkitusapoti, tutakuja kuongeza msanii wa kike ambaye tunajua mtamfurahi wote,”

Kwa kipindi alichokuwa WCB, Queen Darleen ameweza kuachia ngoma kama Kijuso, Ntakufilisi, Touch na kushiriki kwenye wimbo ‘Zilipendwa’ ambao uliwakutanisha wasanii wote wa label hiyo.

Mess Amponza Mama Yake Kisa Hiki Hapa

$
0
0
Mess Amponza Mama Yake Kisa Hiki Hapa
Wakati timu ya taifa ya Argentina ikitarajiwa kutua dimbani leo katika mchezo wake dhidi ya Croatia, mama wa Nyota wa timu hiyo Lionel Messi amesema kuwa anasikitishwa na kitendo cha mwanae kushambuliwa kwa maneno na mashabiki kwa tukio la kukosa penati.

Celia Cucittini ambaye ni mama mzazi wa Messi amesema kuwa kinachoendelea kwa sasa kuhusu mwane na kueleza kusikitishwa na hali hiyo huku akisema Messi anaumia sana kwa hali hii ya sasa na wamuache kwa kuwa analipambania taifa.

“tangu Messi akose penati kumekuwa na maneno mengi mabaya juu yake na mashabiki wa timu ya taifa ya Argentina pia wamekuwa wakimshambulia sana kwa maneno, kama kuna mtu anataka kurudi na kombe nyumbani basi Messi namba moja”, amesema mzazi huyo.

Kubwa tangu michuano ya kombe la dunia ianze ni tukio la nyota wa Argentina Lionel Messi kukosa tuta katika mchezo wao wa ufunguzi dhidi ya timu ya taifa ya Iceland.

Hadi sasa Argentina wana alama moja tu katika kundi lao D na hii leo watakipiga dhidi ya Croatia huku Gabriel Mercado akionya kwamba Messi ana njaa kali ya kumwadhibu yeyote.

Timu hizi zimeshawahi kukutana mara nne huku Argentina wakiipiga Croatia mara mbili, Croatia wakipata ushindi mara moja na mara moja huku ya mwisho wakitoka bila suluhu.

Rais wa Zimbabwe Apanga Foleni Kununua Kuku wa Kukaanga

$
0
0
Rais wa Zimbabwe Apanga Foleni Kununua Kuku wa Kukaanga
Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amewashangaza watu baada ya kuonekana kwa mama ntilie akiwa amepanga foleni kwa ajili ya kununua kuku wa kukaanga.



Tukio hilo la aina yake lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo Rais huyo alipigwa picha akiwa amepanga foleni akiwa na wananchi wa kawaida huku akiwa anasubiri kupatiwa huduma ya kuku wa kukaangwa.



Kitendo hicho kimetajwa kwamba ni mwonekano tofauti na utawala uliopita kwani Rais huyo anapenda kujichanganya na wananchi wa kawaida kuliko mtangulizi wake, Robert Mugabe.



Rais  Mnangagwa alionekana akiwa amepanga foleni hiyo kwenye kibanda cha mama ntilie mmoja kilichopo katika mji mdogo wa Chegutu uliopo kilomita 100  kutoka mji mkuu wa Harare.



“Baada ya foleni yake kufikiwa aliagiza vipande viwili pamoja na Juisi vyenye gharama ya Dola 3.75 kisha akatoa Dola 20 na kuniambia nisimrudishie chenji inayobaki, alisema Isabel Mtongerwa aliyekuwa akimhudumia Rais Mnangagwa.



Mwanasiasa huyo anakuwa karibu zaidi na watu  kutokana na kutumia sana mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter ukilinganisha na mtangulizi wake.

Urusi Yakabiliwa na Upungufu wa Bia, Mashabiki Walalamika

$
0
0
Urusi Yakabiliwa na Upungufu wa Bia, Mashabiki Walalamika
Nchini Urusi ambapo inadaiwa kuwa jiji la Moscow linakabiliwa na upungufu wa bia unaodaiwa kusababishwa na tabia ya baadhi ya Mashabiki waliyoenda kutazama Kombe la Dunia nchini humo kupenda kufakamia bia kwa wingi.

Kwa mujibu wa mashabiki waliopo katika jiji la Moscow wamenakiriwa wakilalamika kuwa wamekuwa wakisubiria kwa muda mrefu katika migahawa wanapoagiza bia kutokana na uhitaji wake kuwa mkubwa huku zikiwa chache.

Aidha nchi ya Urusi inatajwa kukamata nafasi ya 14 kwa unywaji wa bia duniani huku ikidaiwa kuwa uwepo wa mashabiki katika nchi hiyo walioenda kutazama kombe la Dunia umesaidia kunyanyua sekta ya bia nchini humo iliyokuwa inashuka.

Aidha mashabiki walioenda kushuhudia michuano hiyo wamevitaka viwanda vinavyotengeneza bia nchini humo kuongeza uzalishaji wa bia ili wasipate shida kuzipata

Je ni Kweli Watoto Wengi 'Hupatikana' Msimu wa Baridi ?

$
0
0
Je ni kweli watoto wengi 'hupatikana' msimu wa baridi ?
Mtaalam wa maswala ya ngono nchini Kenya Maurice Matheka amepinga dhana kwamba misimu ya baridi huchochea kuzaliwa kwa watoto wengi.

Katika mahojiano na BBCswahili, mtaalam huyo anasema kwamba fikra hiyo imetumiwa na wanaume kama chambo cha kuwavutia wanawake katika mazungumzo wakati wa msimu wa baradi.

Matheka anasema kuwa Waafrika wamelelewa katika tamaduni ambazo zinawafanya kuhisi kana kwamba mkutano wowote wa mume na mke katika eneo la faragha huchochea kufanyika kwa mapenzi.

''Ni kweli kwamba misimu ya baridi huwachochea wanaume na wanawake kukumbatiana ,lakini swala kwamba hatua hiyo inaweza kuchochea ngono sio la kweli. Wenzetu wazungu kwa mfano wana misimu ya baridi lakini hilo halitokei'', alisema mtaalamu huyo.

''Msimu wa baridi humuathiri mwanamume na hivyobasi yeye hutaka joto mwilini lakini sio kwamba watu wanapokumbatiana husababisha kufanyika kwa tendo la ngono''.

Kulingana na mwanasayansi huyo, matokeo yalibaini kwamba wanafunzi waliotekeleza ngono chini ya mara moja kwa wiki walikuwa na kiwango cha juu cha kinga ikilinganishwa na wale ambao hawakushiriki kabisa.

Wadau Wadai Dogo Aslay Anajichanganya kwa Demu Mpya...Lazima Apate Tabu

$
0
0

Aslay anajichanganya tu wadau wanadai huko anapoenda lazima apate tabu , Wanamwesabia Siku lazima arudi kwa Tessy Mama mtoto wake aliyembwaga...Pichani ni Ex wake kushoto na kulia ni kifaa kipya anachojitambia Instagram...Nani zaidi hapo??

Rais Magufuli Aionya Wizara ya Kazi kwa Kuajiri Wafanyakazi Vilaza

$
0
0
Rais Magufuzi Aionya Wizara ya Kazi kwa Kuajiri Wafanyakazi Vilaza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameinyooshea kidole wizara ya kazi na ajira kuwa kuna watu wameajiriwa lakini wanafanya kazi chini ya kiwango jambo ambalo hapendezwi nalo.

Rais ametoa kauli hiyo mapema leo wakati akipokea gawio la Serikali kutoka Shirika la Simu Tanzania (TTCL) , ambapo amesema kuwa suala hilo ameliona na amewaachia wabunge walitazame kwa mapana.

“Wizara ya Kazi kuna matatizo matatizo huko, nimeshayaona, nimeanza kuyafuatilia, kuna wengine vilaza kabisa lakini wanaletwa huko kuja kufanya kazi, hili nitalishughulikia, nalichomekea tu ili wabunge walitazame”, amesema Rais Magufuli.

Wizara hiyo ambayo iko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) inaongozwa na Waziri Jenista Mhagama, pamoja na Naibu wake Anthony Mavunde.

Je Bangi Inaweza Kuwa Tiba Katika Penzi Lililozorota?

$
0
0
Je Bangi Inaweza Kuwa Tiba Katika Penzi Lililozorota?
Adam na Dounia kutoka mji wa Luton, Uingereza wamekuwa wakitumia bangi kabla ya kushiriki tendo la ndoa kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Mara nyingine hutumia bangi ili kuondoa hali ya wasiwasi katika chumba chao cha kulala, alielezea Dounia.

Anasema kwamba yeye hutumia marashi yaliochanganywa na bangi katika sehemu zake za siri ili kujipatia joto, kitu ambacho hawezi kuishi bila kufanya .

Huku Canada ikihalallisha utumizi wa bangi -likiwa taifa la pili la pekee kutengeza bidhaa kutokana na mmea huo baada ya Uruguay- nayo serikali ya Uingereza ikitaka kufanyia marekebisho sheria kuhusu utumizi wa bangi kama tiba, watu wanaangazia masuala mengine muhimu ambayo mmea huo unaweza kutoa.

Adam na Dounia ni miongoni mwa idadi ya watu, inayozidi kuongezeka, wanaotumia bidhaa za bangi wakati wa kujamiiana kwa lengo la kuongeza 'mahanjam'.

''Sijiamini, sina mwili mzuri unaovutia'', alisema Dounia. "Lakini bangi inanisaidia kusahau fikira kama hizo na kufanya mwili wangu na akili yangu kutulia, kupitia kuchoma mishumaa iliotengezwa na bangi katika chumba changu".

Kwa mfano Wahindi wanaamini kwamba kinywaji cha bangi kinapandisha mihemko ya kutaka kufanya ngono, huku Wamisri wa zama za kale wakidaiwa kutumia bangi iliochanganywa na asali katika sehemu zao za siri ili kupunguza joto lililopo katika kizazi chao.

Na sasa huku sheria kuhusu utumizi wa bangi zikiendelea kulegezwa, idadi ya watu wanaotumia bidhaa za mafuta ya masaji, marashi mishumaa na maua yanayotengezwa kutokana na bangi inazidi kuongezeka.

Neno 'Cannasexual' lilianzishwa na mshauri wa masuala ya ngono Ashley Manta kutoka California 2013 ambaye alianzisha mafunzo ya ngono kutokana na mmea huo wa bangi.

Anaelezea: "Ninawashauri watu kuimarisha maisha yao ya ngono kwa kutumia mmea wa bangi. Kwa kawaida, hii inamaanisha kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na mwathiriwa katika warsha na makundi, mara nyingine kwa kutumia vifaa kuelezea."

Warsha hizo huangazia masuala kadhaa ikiwemo ujuzi ama uhodari wako, kuajiamini, mazungumzo machafu na zaidi.

Utumizi wa bangi huangaziwa wakati wote kuhusu ni wapi unaweza kusaidia hususan muda, kiwango na mbinu ya utumizi wake.

"Kimsingi, ni uchanganyaji wa bangi na akili iliyoshawishika kingono wakati wa kuchagua bidhaa unazotaka kutumia mwilini ili kuongeza raha na vitendo vya kimapenzi, na kuongeza faraja na ujasiri," anasema.


Ongezeko la watu wanaotumia bangi katika mapenzi linamaanisha kwamba wafanyibiashara wa bangi nchini Marekani wanadai kwamba wanajaribu kukidhi mahitaji ya bidhaa zinazosababisha mihemko kama vile mafuta yanayopakwa katika sehemu za siri za wanawake.

Wakati Adam na Dounia walipoanza kutumia bidhaa hiyo 2015, Adam tayari alikuwa mtumiaji wa mara kwa mara wa bangi, sana sana alipendelea kutumia kabla ya kufanya mapenzi.

Papa Francis Amteua Mrithi wa Kadinali Pengo

$
0
0
Papa Francis Amteua Mrithi wa Kadinali Pengo
Papa  Mtakatifu  Francis amemteua Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi kuwa Askofu Mkuu Mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo kuu la Dar es Salaam, Tanzania.

Katika barua iliyotolewa na na Katibu Mkuu TEC, Raymond  Saba imesema kwamba Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi alikuwa ni Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Mwanza, Tanzania.

Kwa uteuzi huo wa Papa Francis, Askofu Ruwaichi atachukua nafasi ya Polycarp Pengo

Askofu Mkuu Ruwaichi alizaliwa tarehe  Januari  30, 1954, huko Mulo, Kilema, Jimbo Katoliki la Moshi na baada ya masomo na mafunzo yake ya kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre Novemba 25,  1981 na Februari 9  1999, akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Mbulu na kuwekwa wakfu tarehe 16 Mei 1999.

Tarehe 15 Januari 2005, Mtakatifu Yohane Paulo II alimteuwa Askofu Ruwaichi kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Dodoma na kusimikwa rasmi tarehe 19 Februari 2005

Hata hivyo 2011 Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Mwanza na kusimikwa rasmi tarehe 9 Januari .

Waziri Mkuu wa New Zealand Ajifungua Mtoto wa Kike

$
0
0
Waziri Mkuu wa New Zealand Ajifungua Mtoto wa Kike
Waziri mkuu wa New Zealnd Jacinda Ardern amejifungua mtoto wake wa kwanza wa kiki wa uzani wa kilo 3.31.

Hii inamfanya awe kiongozi wa pili katika historia aliye madarakani kujifungua mtoto.

Bi Ardern alilazwa kwenye hospitali moja mjini Auckland siku ya alhamisi.

Mbali na kuwa Kiongozi wa pili katika historia kujifungua akiwa uongozoni, ni waziri mkuu mwenye umri mdogo zaidi kuliongoza New Zealand tangu 1856.

Bi Ardern mwenye umri wa miaka 37 atachukua mapumziko kwa muda wa wiki sita huku Naibu wake, Winston Peters akichukua usukani.

Hata hivyo ushauri wake utahitajika kwa baadhi ya masuala muhimu ikiwemo kusoma kumbukumbu ya mkutano wa mawaziri licha ya kuwa likizoni.

"Niko na hakika tunapitia hisia nyingi zinazopitiwa na wazazi wengine pia, na vile vile tunatoa shukrani kwa ukarimu na taarifa za pongezi kutoka watu wengi. Asanteni." Aliongeza kwneye taarifa aliyotoa.

Bi Ardern, ambaye alichaguliwa mwezi Oktoba mwaka uliopita, alitangaza Januari mwaka huu kuwa yeye na mpenzi wake Clarke Gayford walitarajia mtoto.

"Mimi sio mwanamke wa kwanza kuwa na majukumu mengi. Mimi sio mwanamke wa kwanza kufanya kazi nikiwa na mtoto. Kuna wanawake wengi walionitangulia katika hili, "

Mwingine kujifungua uongozini ni waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhutto, aliyejifungua mtoto wa kike mnamo mwaka 1990.

Alikuwa kiongozi wa kwanza kujifungua akiwa ofisini.

Ongeza Nguvu za Kiume na Hamu ya Tendo Hata Kwa Wenye Kisukari na BP

$
0
0

Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume au ukosefu wa hamu ya tendo la ndoa limezidi kuongezeka kwa kasi duniani kote na limekuwa chanzo kikubwa cha ndoa nyingi na mahusiano kukosa uaminifu kutokana na wengi kutoka nje ya ndoa ili kupata mtu atakayemtosheleza na kumfikisha kileleni. Pia udogo wa maumbile ni tatizo kubwa na limekuwa likiwakosesha wanaume wengi uwezo wa kujiamini katika tendo na kusababisha tendo hilo kutokufanyika kwa usahihi. Hili pia huchangia kwa kiasi kikubwa wanawake wengi kwenda nje ya ndoa ( MAHUSIANO) kutafuta mbadala wake.
BAADHI YA DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI KAMA:-
☆Kukosa hamu ya tendo la ndoa
☆Uume kusimama kwa ulegevu
☆Kuwahi kufika kileleni
☆Uume kusinyaa katikati ya tendo
☆Kushindwa kurudia tendo kwa wakati
☆Kuchoka sana baada ya round ya kwanza na hata kukinai kabisa.

Kwa kutumia mimea tiba na matunda bila kemikali sasa
@markson_beauty_pr Tunakuletea suluhisho la matatizo hayo hata kwa wenye "KISUKARI NA PRESSURE" kwa:-
1.HANDSOME UP ORIGINAL:- kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @250,000/=
2.SHARK POWER ni gely ya kupaka inayoongeza uume kwa wastani wa inch 5.5 hadi 6 @150,000/=
3.VigRX CREAM:- ni gely iliyoboreshwa mahususi kwa ajili ya kuongeza maumbile kwa wastani wa inch 6.5 hadi 8 na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @200,000/=
4.Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @150,000/=
5.Spray ya kuchelewesha kufika kileleni na kuweza kurudia tendo ×3. @150,000/=
BIDHAA HIZI HAZINA MADHARA KIAFYA NA ZIMETHIBITISHWA
NA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO).
KWA BIDHAA HIZI NA NYINGINE NYINGI TEMBELEA UKURASA WETU WA INSTAGRAM :-
@markson_beauty_pr
@markson_beauty_pr
@markson_beauty_pr
WEB:www.markbeauty.org
Wasiliana nasi Popote
ulipo duniani kwa (+255)
0767447444 na
0714335378
UTAPATA HUDUMA
NB:Matokeo ni uhakika na garantii na hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.
#OngezaUume
#NguvuZaKiume
#HandsomeUpOg
#BidhaaTz

Denmark yalazimishwa sare ya bao 1 – 1 na Australia kombe la dunia nchni Urusi

$
0
0

Michuano ya Kombe la Dunia 2018 imeendelea tena leo kwa timu ya taifa ya Denmark kucheza mchezo wake wa pili wa hatua ya makundi dhidi ya timu ya taifa ya Australia.


Mchezo wa Denmark ulikuwa na mvuto zaidi kwa upande wa Tanzania, hii inatokana na uwepo wa staa wa Denmark mwenye asili ya Tanzania Yussuf  Yurary Poulsen ambaye mchezo uliopita aliipatia ushindi Denmark dhidi ya Peru wa goli 1-0.

 

Denmark leo wakicheza mchezo wao wa pili wameambulia sare ya kufungana goli 1-1, goli la Denmark lilipatikana dakika ya 7 kupitia kwa staa wao Christian Eriksen lakini Australia walisawazisha goli hilo dakika ya 38 kwa mkwaju wa penati baada ya Yussuf Poulsen kushika mpira katika eneo la hatari.


Poulsen baada ya kushika katika eneo la hatari na kusababisha penati alioneshwa kadi ya njano ikiwa hiyo ni kadi yake ya pili katika World Cup 2018 na amesababisha penati kwa mara ya pili, Yussuf anakuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya World Cup kusababisha penati nyingi (2) katika msimu mmoja toka 1966.


Sare hiyo sasa inawaweka pazuri Denmark kwa kufikisha point nne na wanahitaji point moja tu mchezo ujao dhidi ya Ufaransa ili wafuzu hatua ya 16 bora au kama ikitokea bahati mbaya wakapoteza, basi watahitaji kuomba Peru amfunge Australia mechi ya mwisho huku Ufaransa leo afanikiwe kumfunge Peru.

Rais Magufuli: “Kuna vilaza wanaajiriwa nawaona tu”

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameinyooshea kidole wizara ya kazi na ajira kuwa kuna watu wameajiriwa lakini wanafanya kazi chini ya kiwango jambo ambalo hapendezwi nalo.


Rais ametoa kauli hiyo mapema leo wakati akipokea gawio la Serikali kutoka Shirika la Simu Tanzania (TTCL) , ambapo amesema kuwa suala hilo ameliona na amewaachia wabunge walitazame kwa mapana.


“Wizara ya Kazi kuna matatizo matatizo huko, nimeshayaona, nimeanza kuyafuatilia, kuna wengine vilaza kabisa lakini wanaletwa huko kuja kufanya kazi, hili nitalishughulikia, nalichomekea tu ili wabunge walitazame”, amesema Rais Magufuli.


Wizara hiyo ambayo iko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) inaongozwa na Waziri Jenista Mhagama, pamoja na Naibu wake Anthony Mavunde.

Mitihani ya kidato cha sita yasababisha Intaneti kuzimwa

$
0
0

Serikali nchini Algeria imelazimika kuzima huduma ya Internet nchi nzima kuepuka udanganyifu katika mitihani ya kidato cha sita inayoendelea nchini humo. 

Imeelezwa kuwa pia vifaa vyote ambavyo hutumika kupatia huduma ya Internet vimekatazwa kufikishwa katika maeneo ya karibu ambapo mitihani hiyo inafanyika huku mitambo maalumu ikifungwa kubaini uwepo wa vifaa hivyo. 

Kwa mujibu wa Serikali huduma hiyo ya Internet itaendelea kukosekana kutokea June 21 mpaka June 25 siku ambayo mitihani itakuwa inamalizika. 

Aidha duru za kuaminika zinasema kuwa Serikali hiyo imeamua kuchukua uamuzi huo baada ya mitihani ya mwaka 2016 kuvuja sana kwenye mitandao ya kijamii hivyo wameamua kuzima Internet ili kubana upenyo wa mitihani hiyo kuvuja mitandaoni mwaka huu.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>