Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli Awalilia Watu 14,waliokufa Kwa Ajali Ya Hiance Iliyogongana Na Lori La Mchanga Mkuranga

$
0
0

Rais Dkt. John Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko taarifa ya vifo vya watu 14 waliopoteza maisha baada ya basi dogo walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori la kubebea mchanga katika eneo la Dundani Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.


Dkt. Magufuli amesema hayo katika salamu zake za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo baada ya kupita masaa kadhaa tokea ajali hiyo kutokea leo Juni 25, 2018 wakati basi dogo lililowabeba wanafamilia, ndugu na jamaa waliokuwa wakielekea Msata kuhudhuria sherehe za kumaliza mafunzo ya kijeshi  kwa mtoto wao, kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa linatoka Dar es Salaam kwenda Dundani kuchukua mchanga.


"Naomba unifikishie pole nyingi kwa wanafamilia wote waliopatwa na msiba, waambie naungana nao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kuondokewa na wapendwa wao, na sote tuwaombee marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi", amesema Rais Magufuli.


Kwa upande mwingine Rais Magufuli pia amewaombea majeruhi wanne wa ajali hiyo wapone haraka ili waweze kuungana na familia zao na kuendelea na majukumu yao ya kila siku.

Maskini: Msanii D'Banj afiwa na Mtoto wake

$
0
0

Habari zilizopatikana ni kwamba mtoto wa kiume wa mwanamuziki maarufu wa Nigeria,  D’Banj, amefariki dunia. 

Mtoto huyo ambaye alimzaa na mkewe Didi Lineo mnamo  Mei 2017 na aliyepewa jina la D’Banj mwenyewe la Daniel Oyebanjo III, inasemekana kwamba amekufa kwa kuzama majini. 

D’Banj ameshea picha ya rangi nyeusi kwenye akaunti yake ya Instagram na kuandika: 

Trying Times 💔🖤. But my God is Always and Forever Faithful 🙏. 

Adakwa Akiuza Sambusa za nyama ya Paka

$
0
0

Maafisa wa Polisi nchini Kenya wanamshikilia mwanaume mmoja anayejulikana kama James Mukangi, kwa kuwauzia watu sambusa zinazotengenezwa kwa nyama ya paka. 

Mukangi amekamatwa Jumapili ambapo inadaiwa amekutwa akimchuna ngozi paka, huku akidaiwa kuwauzia wauzaji wa sambusa nyama hiyo, na pia wenye migahawa, Gazeti la Star limesema mwenyewe amekiri kupika sambusa kwa kutumia nyama hiyo. 

Taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari nchini humo, zinasema Mukangi amekiri kuuza nyama ya paka zaidi ya elfu moja mjini humo tangu mwaka 2012. 

Mukangi amewaambia wanahabari kwamba ameanza biashara hiyo baada ya kuona upungufu wa nyama sokoni, "Huwa nawaambia wateja wangu kwamba huwa naipata nyama hii kutoka Gioto (jaa la kutupa taka), lakini huwa hawajui kwamba ni nyama ya paka," amenukuliwa na gazeti la Nation. 

Aidha Mukagi ameongeza kuwa huwa anauza pia ngozi za paka na kwamba kwa kila paka hujipatia takriban Shilingi 500 sawa na (Dola 5 za Marekani).

CCM Itafutika Kusini, Huku Nikutudharau - Nape Nnauye

$
0
0
CCM itafutika Kusini, huku nikutudharau - Nape Nnauye
Mbunge wa Jimbo la Mtama (CCM) Nape Nnauye, akichangia hoja katika mjadala wa kupitisha Bajeti Kuu ya serikali 2018 / 2019 iliyowasilishwa Bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango amesema,


"Nilipoleta hoja hapa ilikuwa ni hoja ya kusimamia utekelezaji wa sheria, sheria haisimamiwi, tunakumbusha isimamiwe hela ziletwe, Badala ya kutuletea hela zetu Dk. Mpango unaleta sheria ya kuzifuta kabisa asilimia mia zije kwenu, kwa kweli huku nikutudharau kwa hali ya juu, hii si sawa, zungumzeni namna ya kuleta hela mlizochukua hii habari ya sheria mnayotaka kubadilisha toeni kwanza." Nnauye Amesema


Vile vile ameongelea swala la kusemekana kuwa na matumizi mabaya ya fedha kwenye mfuko wa zao la korosho, na kuuliza swali kuwa dawa ya kutibu tatizo hilo je nikuufuta mfuko huo, au kuchukua hela? ambapo alishindwa kujizuia kwa uchungu na kuongelea kuwapo kwa hati chafu za Hazina, na kumtaka Waziri wa fedha Dk. Mpango kuwa na huruma ambapo kama hawatakuwa makini CCM itakufa Kusini mwa nchi, Hivyo amemtaka Dk. Mpango kurejesha pesa zao na kubadilisha uamuzi ambao wameuchukua.

Nilichomewa Nyumba Yangu Moto, Nilimpoteza Baba Lakini kwa Hili Sitakubali – Hawa Ghasia

$
0
0
Nilichomewa Nyumba Yangu Moto, Nilimpoteza Baba Lakini kwa Hili Sitakubali – Hawa Ghasia
Mbunge wa Mtwara Vijijini (CCM), Hawa Ghasia amesema kuwa wakati wa sakata la gesi alikaa upande wa serikali kuitetea kupeleka gesi kokote Tanzania aliamini inatenda haki lakini badala yake nyumba yake ilichomwa na alimpoteza baba yake.



Ghasia ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma, wakati akichangia hoja ya bajeti ya serikali ambapo amesema kwa hili la korosho hawezi kubaliani na mapendekezo ya serikali kufuta asilimia 65 ya fedha zinazotokana na mauzo ya korosho.

“Kwanza nianze kwa masikitiko makubwa sana ambayo yanasambazwa kwa makusudi dhidi ya Wabunge wanaotetea kupelekewa pembejeo Kwenye maeneo yao.Tuna taarifa jana watu wamekaa vikao waje humu kutudhalilisha Wabunge tunaowatetea wananchi wetu wapate pembejeo,” amesema Hawa.

“Wabunge wote humu ndani tuna haki sawa za kutetea wananchi wetu. Anayetoka Kwenye pamba ataitetea pamba, anayetoka Kwenye madini atatetea madini yake, anayetoka Kwenye korosho ana haki ya kuitetea korosho yake.Mimi napenda niwahakikishie wananchi wanaolima korosho; Wabunge wao tupo imara, tutapambana kuhakikisha haki hii inapatikana. Hata kama haitapatikana, wajibu wetu tutautimiza kama wawakilishi kuja kuwatetea wananchi,” ameongeza

“Mimi nilikaa upande wa serikali wakati wa gesi. Niliitetea Serikali kupeleka gesi kokote Tanzania kwa sababu nilijua serikali inafanya haki. Nilichomewa nyumba yangu moto. Mabomba ya kupeleka maji Kijijini kwetu yaling’olewa. Mikorosho ya Baba yangu ilikatwa. Minazi ya Baba yangu ilikatwa. Katika process hiyo nilipoteza Baba yangu. Bado nilimshukuru Mwenyezi Mungu nilisema Alhamdulilah Alhamdullilah Alhamdulillah! Kwa sababu niliona serikali inachokifanya iko sahihi,” alisisitiza Ghasia.

“Ninachosema kama kuna mtu amefanya ubadhilifu, hata kama ni Hawa Ghasia Kwenye mfuko wa korosho, nipelekeni Mahakamani.Hao wananchi tunaowambia wabunge wa Kusini wabinafsi wanataka kuigawa nchi wana akili na wanajiongeza.”

Kauli ya Chris Brown Baada ya Kukosa Tuzo za BET “Sihitaji Tuzo Ili Niwe Mfalme”

$
0
0
Kauli ya Chris Brown Baada ya Kukosa Tuzo za BET  “Sihitaji Tuzo Ili Niwe Mfalme”
Hii ni nyingine ya kuifahamu kutoka Marekani kuhusiana na staa maarufu Chris Brown ambaye amezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na caption yake ambayo  imehusishwa na tuzo za BET zilizofanyika June 25,2018.

Chris Brown amepitisha miaka mitatu mfululizo bila kushinda tuzo za BET ikiwa 2016,2017 hakushinda na mwaka huu 2018 alitajwa kwenye vipengele viwili Best Male RnB/Pop Artist na Video Director of the year na hajaibuka mshindi.

Kupitia instagram account Chris Brown ameandika “Sihitaji tuzo ili niwe mfalme” ambapo caption hiyo inahusishwa kuwa imemchukiza staa huyo kutokana na kufanya kazi kwa bidii lakini haibuki mshindi.

Mohamed Salah Kustaafu Kuichezea Misri

$
0
0
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Misri anayecheza club ya Liverpool ya England Mohamed Salah jina lake limezidi kuchukua headlines kiasi cha kudaiwa kutaka kutangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Misri.



Mohamed Salah anadaiwa kutaka kufanya hivyo baada ya picha yake  kiongozi wa kisisa wa Chechen Mr Ramzan Kadyrov kusambaa mitandaoni na kuanza kumkosoa staa huyo kwa kudai anatumika kisiasa, Ramzan ni kiongozi wa jimbo la Chechen nchini Urusi na amekuwa akidaiwa kuwa na sifa ambazo sio nzuri.

Hivyo kuonekana kwa MO Salah katika picha ya pamoja na kiongozi huyo kumezua maneno kiasi cha staa huyo kukasirishwa na kudaiwa kutaka kustaafu timu ya taifa kwani kuonekana katika picha ya pamoja na kiongozi huyo ni kama kumuunga mkono na matendo yake, MO Salah pia imeripotiwa kuwa amepewa uraia wa jimbo la Chechen.

Mashabiki wa soka nchini Misri baada ya kusikia taarifa za MO Salah kutaka kuachana na timu ya taifa kwa kuandamwa na maneno baada ya picha yake na Ramzan kusambaa, wameanza kupost ujumbe wenye #IamWithSalah kama njia ya kuonesha wapo pamoja nae na wasingependa astaafu, kama ufahamu timu ya taifa ya Misri imekuwa Chechen nchni Urusi kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia.

Mpinzani Mkuu wa Rais Erdoğan Akubali Matokeo ya Uchaguzi

$
0
0
Mpinzani Mkuu wa Rais Erdoğan Akubali Matokeo ya Uchaguzi
Mpinzani mkuu wa rais Erdoğan,Muharrem İnce ameyapokea na kuyakubali  matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Uturuki.

Muharrem alikuwa akiwania kiti cha urais kupitia chama cha CHP.

Akihutubia katika mji mkuu wa Ankara,Muharram amesema kuwa amekubaliana na matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa Jumapili usiku.

Rais Erdoğan amechaguliwa kwa mara nyingine kuliongoza taifa la Uturuki.

Ameshinda kwa asilimia 52.2 huku Muharram akiwa na asilimia 30.6.

Vilevile Muharrem amekanusha madai ya kupokea vitisho vya aina yoyote.

Walitucheka Tumesajili Wazee Lakini Ndio Wametuwezesha Kufika Hapa Tulipo- Haji Manara

$
0
0
Uongozi wa Klabu ya Mabingwa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC umefunguka na kudai katika kuelekea usajili wa ligi Kuu msimu ujao watahakikisha wanaongeza wanaume zaidi kuliko waliokuwa nao katika kipindi hiki ambao wamewapa mafanikio makubwa.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Haji Manara leo Juni 25, 2018 na kusema walichekwa na kudhalilishwa sana kwenye msimu ulioisha kwa kusajili wachezaji wazee kama watu wasemavyo lakini ndio waliowawezesha kupata ubingwa.

"Nakumbuka vema tulipowasajili hawa Wanaume (John Bocco, Emmanuel Okwi na Erasto Nyoni) jinsi tulivyodhihakiwa, waliitwa wahenga tukaambiwa tumesajili 'ICU' na maneno mengi. Tena hata baadhi ya wanasimba walitulaumu viongozi",ameandika Manara.

Pamoja na hayo, Manara ameendelea kwa kusisitiza kuwa "tulijua 'what we did' na imelipa, hao ndio wachezaji bora katika msimu huu. Hakuna ubishi na sijasikia lalamiko lolote, sasa 'for next season' pamoja na usajili tulioufanya tutaongeza wanaume. Tunayakumbuka vema maelekezo ya Mh Rais wa nchi".

Majigambo hayo ya Haji Manara yamekuja baada ya kupita siku moja tokea zilipotolewa Tuzo za Ligi Kuu Tanzania Bara na timu yake kuweza kuchukua Tuzo nyingi zaidi ya washiriki wengine waliokuwepo katika kinyang'anyiro hicho licha ya maneno mengi yaliyokuwa yanaiandama timu yake kuwa ilisajili wachezaji wazee ambao wasingeweza kuitumikia klabu ipasavyo lakini ikawa ndivyo sivyo.

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0

Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo. 

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa. 

MIHAYO: 
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako. 

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521 

Tupo Mbagala 

Msambwanda wa Snura Watia Shaka...Mwenyewe Adai Hajawahi Tumia Dawa

$
0
0

"Sijawahi kutumia dawa za kichina za kuongeza makalio kama watu wanavyofikilia. Mimi nina utofauti kidogo jinsi nilivyoumbwa kiukweli ukiachaSn hiyo shepu yangu watu wanayoiongelea, ukiniangalia tu unajua tu ni ‘Original".


**Ameyasema hayo Snura kuhusu Shepu yake

Makombe feki ya Kombe la Dunia yakamatwa Argentina, ndani yalikuwa yamejazwa Cocaine na bangi

$
0
0
Makombe feki ya Kombe la Dunia yakamatwa Argentina, ndani yalikuwa yamejazwa Cocaine na bangi (+video) By Godfrey Mgallah | June 25, 2018 - 5:35 pm
Maafisa wa usalama nchini Argentina, wamekamata makombe 8 bandia yenye muonekano sawa na ule wa Kombe la Dunia yakiwa yamejazwa misokoto ya bangi na Cocaine.



Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, Makombe hayo 8 yamekamatwa Ijumaa ya wiki iliyopita mjini Isidro Casanova katika jimbo la Greater Buenos Aires.

Makombe hayo kiujumla yalikuwa yamebeba kilo 20 za bangi na kilo 10 za Cocaine na mafurushi kadhaa ya mafataki.

Jeshi la Polisi mjini Isidro Casanova limethibitisha taarifa hizo na tayari watu nane wanashikiliwa kwa tukio hilo na imekadiriwa kuwa kila kombe lilikuwa na mzigo wa Cocaine wenye thamani ya dola $14,819 sawa na tsh milioni 33.

Tazama makombe hayo yakipasuliwa na jeshi la polisi.


Bongo5

RC Makonda Noma...Apigania Hati ya Nyumba ya Bi Zainab Mpaka Imepatikana..Tazama Video

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amekabidhi hati ya nyumba ya Bi Zainab na mumewe ambayo ilikuwa mikononi mwa Benki ya FNB kutokana na mgogoro wa eneo lao kuwa na deni katika benki hiyo.

 Bi Zainab alipata umaarufu mkubwa kufuatia sakata lake la kununua eneo ambalo hakuwa na taarifa nalo na kujenga nyumba bila kufahamu kuwa aliyemuuzia eneo hilo alikuwa amekopa benki kwa kuweka rehani eneo hilo.

 Siku chache baada ya kujenga watu wa Benki walifika na kuanza taratibu za kuuza nyumba yake, lakini sakata hili lilitua mikononi mwa RC Makonda ambaye alichukua hatua za awali kwa kustopisha zoezi la kuuza nyumba hiyo.

 RC Makonda amekabidhi hati hiyo kwa Shabani Amiri ambaye alifika kwa ajili ya kumuwakilisha Bi Zainab ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani akimuuguza Mumewe anayesumbuliwa na tatizo la moyo lililotokana na mshtuko baada ya Benki hiyo kutaka kuuza nyumba yao.

VIDEO:

Source:GPL

Download Hapa Application ya Udaku Special Kwenye Simu Yako Kushuhudia Vimbwanga Mtaani na Stori za Mapenzi

Joshua Nassari Naye Ajilipua Sakata la Korosho "Huo ni Wizi Hakuna Lugha Nyingine"

$
0
0

Mbunge wa Arumeru Mashariki ( Chadema),  Joshua Nassari amekifananisha na wizi kitendo cha Serikali kushindwa kutoa Sh 210 bilioni kama asilimia 65 ya fedha za ushuru wa mauzo ya korosho nje ya nchi kwa kuwa jambo hilo lipo kisheria. 


Akizungumza katika mjadala wa bajeti ya Serikali mwaka 2018/19 leo Juni 25, 2018 bungeni mjini Dodoma, Nassari amesema asilimia kubwa ya wabunge bungeni wanawawakilisha wakulima, wafugaji na wavuvi.


Amesema hata dhana ya Tanzania ya viwanda inategemea malighafi za kutosha zinazotokana na zao hilo lakini bajeti imekuwa ikipungua mwaka hadi mwaka.


"Leo hii tunaongelea Serikali ya viwanda, sheria ya export levies ilikuwa na lengo la kuongeza uzalishaji wa korosho zetu ndani ya nchi, sasa badala yake Serikali inaiba hela za wananchi, huu ni wizi hakuna lugha nyingine”  -Nassari


Amesema shughuli za kilimo cha korosho sasa zimepanuka na wakulima katika mikoa 17 sasa wanalima zao hilo la biashara lakini Serikali haitaki kutoa fedha hizo ambazo wakulima wamekuwa wakizitegemea.


Amesema kama Serikali ilitunga sheria ya korosho iweje sasa itake kuibadilisha ili fedha hizo ziende katika Mfuko wa Hazina.

Serikali yaondoa vibali wanaosafirisha samaki wa kitoweo

$
0
0

Serikali imeondoa sharti la wananchi wanaosafirisha samaki kwa ajili ya kitoweo kuwa na vibali.


Uamuzi huo uliotangazwa jana Juni 24, 2018 mjini Sengerema na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina utahusisha wananchi wanaosafirisha samaki wa kitoweo hadi kilo 20 kutoka sehemu moja kwenye nyingine.


Akizungumza wakati wa uteketezaji wa zana haramu za uvuvi zenye thamani ya zaidi ya Sh2.3bilioni, kati yake zikiwemo zana zenye thamani ya Sh1.5 bilioni za mfanyabiashara Josefu Kando (Njiwa Pori), Waziri Mpina amesema uamuzi huo wa Serikali unalenga kutoa fursa kwa wananchi kufaidi na kutumia rasimali za Ziwa Victoria.


Pamoja na kufuta vibali vya kusafirisha kitoweo, Waziri Mpina amesisitiza kuendelea kwa operesheni dhidi ya uvuvi haramu huku akiwaagiza wanaoendelea kumiliki zana haramu za uvuvi kuzisalimisha kabla hawajafikiwa ya mikono mirefu ya dola.


Mkuu wa opereshemi dhidi ya uvuvi haramu wilayani Sengerema, Wenceslaus Luhasile ameahidi kuendeleza vita dhidi ya uvuvi haramu na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano wanapobaini vitendo hivyo katika maeneo yao na kuahidi kutunza siri za wanaotoa taarifa.


Kauli hiyo iliungwa mkono na mkuu wa wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole aliyeongeza kuwa jukumu la kulinda rasilimali za nchi ni la kila Mtanzania kwa ajili ya faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Wabunge CCM wazomeana kisa korosho

$
0
0
Sakata  la malipo ya mauzo ya korosho limeendelea kuteka mjadala wa Bunge, safari hii likisababisha watunga sheria kutoka chama tawala CCM kuzomeana huku Mbunge wa Kilwa Kusini, Seleman Bungara 'Bwege' (CUF) akitolewa ukumbini kwa kuchochea vurugu ndani humo.

Akichangia mjadala huo, Mbunge wa Bukoba Vijijini, na Katibu wa Wabunge wa CCM, Jason Rwekiza, alisema kuwa analazimika kufafanua kauli iliyotolewa na Hawa Ghasia, Mbunge wa Mtwara Vijijini kuwa kipo kikundi cha wabunge wanaotaka kuwachafua.

Alisema yeye akiwa ni Katibu wa Wabunge wa CCM ndiye anayepanga wachangiaji wa chama hicho bungeni.

"Nalisema hili kwa sababu Mheshimiwa Hawa Ghasia amesema kuna watu wamepangwa na serikali kuwachafua, hii siyo sahihi," Rweikiza alisema. "Orodha ya wachangiaji nimepanga mimi, naomba mnisikilize tulia… tulia... nisikilizeni," alisisitiza mbunge huyo baada ya kuibuka zomeazomea dhidi yake bungeni.

Katika mjadala huo, Ghasia alisema anasikitishwa na maneno yanayosambazwa kwa makusudi dhidi ya wabunge wanaotetea kupelekwa pembejeo kwenye maeneo yao.

"Kuna taarifa kuwa jana (juzi) watu walikaa vikao, wameandaliwa kuja bungeni kuwadhalilisha wabunge hao wanaotetea wananchi, ili wapate pembejeo na kutetea wakulima wapate fedha zao," Ghasia alisema na kueleza zaidi:

"Wabunge wote humu ndani tuna haki sawa za kutetea wananchi wetu. Anayetoka kwenye pamba ataitetea, anayetokea kwenye madini atatetea madini yake na korosho ana haki ya kuitetea korosho yake.

"Na mimi napenda niwahakikishie wananchi kwa ujumla kuwa wabunge wake tupo imara. Tutapambana kuhakikisha haki hii inapatikana na hata isipopatikana, wajibu wetu tutautimiza kama wawakilishi wa wananchi ambao tulichaguliwa kuja kuwatetea bungeni.

"Leo tunaambiwa kuwa eti ni wabinafsi, na ni mbinafsi? Kuna watu wanakuja kusimama wanasema wao ndiyo wanaijua korosho kushinda mtu mwingine humu ndani."

Alisema hata ukifika Chuo Kikuu cha Mzumbe, utakuta ripoti za utafiti wake kuhusu korosho na hata utafiti wake wa shahada yake ya uzamili ulikuwa unahusu namna ya kuifufua korosho na kuitafutia soko.

Kama ilivyokuwa wiki iliyopita wabunge wa pande zote mbili waliendelea kuibana serikali kulipa kiasi hicho cha fedha walipokuwa wanaendelea na mjadala wa mapendekezo ya bajeti kuu ya serikali kwa mwaka ujao wa fedha na Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017.

Hoja hiyo imeteka mjadala huo kutokana na serikali kuonekana kushindwa kutekeleza matakwa ya Sheria ya Tasnia ya Korosho, inayotaka asilimia 65 ya mauzo ya korosho inatakiwa irudishwe Bodi ya Korosho na asilimia 35 inatakiwa kupelekwa Mfuko Mkuu wa Serikali.

Kabla ya mjadala huo kuanza Jumatatu iliyopita, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bajeti, Hawa Ghasia, aliwasilisha taarifa ya kamati yake bungeni siku hiyo na kueleza kuwa serikali imeshindwa kupeleka kwenye Bodi ya Korosho Sh. bilioni 201.281.

Kati yake, Sh. bilioni 91.15 ni za mwaka 2015/16 na Sh. bilioni 110.131 ni za mwaka 2016/17.

Ghasia alibainisha kuwa serikali imepeleka Sh. bilioni 10 kwenye mfuko hivyo, bado unaidai Sh. bilioni 81.15 za msimu uliotangulia, hivyo kuathiri zao hilo kwa kiasi kikubwa katika upatikanaji wa pembejeo.

Wakati kamati hiyo ikieleza hayo, jana Mbunge wa Mtama, Nape Nauye (CCM), alisema kuna uwezekano wa kuizika CCM mikoa ya kusini kama serikali haitatoa fedha hizo.

Alisema kuwa aliwahi kutoa hoja bungeni kuhusu suala hilo akitaka kusimamia utekelezaji wa sheria, lakini cha kushangaza anaona serikali inaacha kutekeleza sheria iliyopo huku ikiwasilisha mapendekezo bungeni kufuta ulipaji wa fedha hizo kwa wakulima na badala yake ziende serikali kuu.

Alisema kitendo hicho ni hatua ya serikali kuonyesha dharau kwa wakulima na Bunge, jambo alisisitiza si sawa na haikubaliki.

“Mimi nadhani maoni yangu hebu tuzungumzie namna ya kuleta fedha mlizochukua, hii habari ya kubadilisha sheria iacheni kwanza," Nape alisema.

"Maisha haya ni yetu, tusifike mahali tukafika huku maana ni pabaya sana. Leo mnataka kutupeleka kwenye korosho na hela mliyotarajia kuipata hamtaipata tena maana zao hilo linakufa.

“Mapendekezo yangu tuzungumzie namna ya kupata hela yetu, kueni na huruma kwetu na mapendekezo haya yanaenda kutuweka mahali pagumu sana.

“Nataka kuwaanbia, msipopeleka fedha za korosho kwa wakulima mtakuwa mmeizika CCM kabisa katika mikoa ya kusini maana kutakuwa hakuna namna nyingine ya kuweza kujinasua."

Wakati Nape akichangia, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Stella Manyanya, alisimama kutoa taarifa, akimtaka mbunge huyo kutowatia hofu wakulima wa korosho nchini.

Kutokana na hali ya zomea zomea na vurugu, Mwenyekiti wa Bunge, Azzan Zungu aliyekuwa anaongoza kikao cha jana, alisimama na kuwataka wabunge watulie, akieleza kuwa kila mtu ana uhuru wa kuchangia.

Rwekiza aliendelea kuchangia, akieleza kuwa orodha ya wachangiaji huwa anaipanga yeye na kwamba Ghasia hakupangwa licha ya kuwa kupata nafasi hiyo jana.

Wakati mjadala huo ukiendelea, Zungu alitoa angalizo la mwisho kwa wabunge waliokuwa wanapiga kelele kwa kuzomea na baadaye akaagiza Bwege atoke ndani ya Ukumbi wa Bunge kutokana na kusababisha vurugu.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya June 26

$
0
0

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya June 26

Muone Ustadhi Ashrafu Atimize ndoto yako..Anatumia Nyota na Nguvu za Asili Kutibu

$
0
0
Muone Ustadhi Ashrafu Atimize ndoto yako. yawezekana ulizaliwa nanyota yakitajiri ila watu wabaya wameikalia mpaka sasa ikawa hufahamu chochote. Mtafute ust Ashrafu Airudishe nyota yako yakitajiri kwakupitia pete inayoendana na nyota yako. Ust Ashrafu Ananguvu zamajini katika utendaji wake.

Anauwezo wakutoa Mali kwakupitia pete nakwakupitia majini wake. Na anauwezo wakuzirudisha Mali zilizopotea kwanjia zakichawi kwakupitia Pete yakifalme Ambayo inayong'aa muda wowote nakubadilikabadilika rangi. Ust Ashrafu Ametembea baadhi ya nchi kwakuwapatia watu huduma mbalimbali. Kama vile maradhi yakisukari, presha, ukimwi, bawasiri, tezidume, mwiliwote kupooza nakutetemeka, NK. Navilevile Amewapatia wengi huduma yamvuto wa kibiashara, nayamvuto wakimapenzi.

Nawengi wametoa shukrani zao kwa ust Ashrafu namna Alivyozirudisha Ndoa zao zilizo sambaratika kwamuda mrefu. Mtafute ust Ashrafu ili akusaidie juu yamambo yako. Nahuyu ust anasaidia matatizo yauzazi, nguvu zakiume, kuwashwa mwilini, kutokwa namapere usoni nasehemu za siri, NK. Na anadawa yakumtuliza mume asiesikia nakutulia inayoitwa limbwata. Na anadawa yakumrudisha mpenzi ktk mahusiano kwamda mchache.

Na amezipatanisha familia nyingi zilizogombana. Na anauwezo wakufarakanisha maadui waliokua pamoja.

Mtafute Ustadhi Ashrafu kwa no. 0768486717-0627423037 Au Mtafute kwa whasapp 0659438578

Hizi ndio namba zake mpigie muda wowote usiogope yupo kwaajili yako. Mpigie hupate muongozo wa bure naushri. Ustadhi Ashrafu huduma zake hupatikana mahala popote utakapo muhitaji, ila sehemu kuu anapatikana Bagamoyo.

CHADEMA, CUF Waja na Mkakati Mpya

$
0
0

Viongozi wa Baraza la Vijana wa CHADEMA Taifa wakiongozwa na M/kiti wa BAVICHA Taifa Patrick Sosopi, leo amekutana Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui ma kuweka mikakati ya kuwapigania  vijana wanaokosa haki zao za msingi hasa za kupiga kura visiwani Zanzibar.


M/Kiti BAVICHA Taifa, Patick Ole Sosopi aliyevalia nguo nyeusi za chama, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Mhe.Nassor Ahmed Mazrui leo mapema alipozuru na ujumbe wake Ofisi kuu ya CUF Zanzibar.

Akiwa katika ziara huko Zanzibar, Sosopi ambaye ameongozana na wa Makamu M/kiti  BAVICHA Zanzibar Zeudi Mvano na Katibu Mwenezi wa BAVICHA Taifa, Edward Simbeye, wamesema kwamba  vijana wengi wanakosa haki zao kwakuwa tu ni wapinzani hivyo Masheha huwanyima barua za utambulisho ili kupata cheti cha kuzaliwa na hatimaye kitambulisho cha kupiga kura.

Pamoja na hayo viongozi hao wameweka mikakati mbalimbali  ya kuimarisha UKAWA kwa upande wa visiwani ambapo kikao hicho kimeweka baadhi ya misimamo ya utekelezaji wa ushirikiano katika utendaji wa shuguli za Taasisi mbili za Vijana kwa maana ya JUVICUF na BAVICHA.

Mbali na hayo viongozi hao wamepanga namna ya kuwasaidia viongozi wakuu wa vyama vyao (CHADEMA, CUF) ili kuwapunguzia majukumu katika kazi za siasa na kuamsha ari mpya ya kusaka mabadiliko kuondokana na mkwamo wa kisiasa.

EATV
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images