Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104664 articles
Browse latest View live

Bilionea Ampangishia Lulu Michael Jumba la Kifahari, Ampa Jeuri ya Pesa Kuwazidi Wema na Kajala

$
0
0
Stori: Hamida Hassan, Gladness Mallya na Musa Mateja.
Madai mazito ya kushtua mtaani yanasema kwamba staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, mambo yake kwa sasa yapo juu ya mstari baada ya bilionea kutoka jijini Arusha (jina tunalihifadhi kwa sasa) kudaiwa kujitosa kumlea akianza kwa kumpangishia jumba kubwa la kifahari.

TWENDENI USHUANI
Habari hizo za mitaani zilidai kwamba bilionea huyo amempangishia Lulu mjengo huo wa maana uliopo ushuani maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Kimuonekano, nyumba hiyo iliyoshuhudiwa na wanahabari wetu mwanzoni mwa wiki hii haina tofauti na ile mijengo iliyozoeleka ya mastaa wakubwa wa Marekani kwa maana ya kujitosheleza kwa kila kitu ndani yake.

Kwanza ni nyumba yenye fensi kubwa na kuingia getini lazima ujieleze ‘vizuri’ na ukiingia huufikii mlango wa nyumba kwani kuna ‘kamwendo’.

Nje ya nyumba hiyo kuna ‘parking’ ya magari madogo zaidi ya kumi huku chini kukiwa na tarazo na pembeni kuna bustani nzuri iliyopandwa maua ya kuvutia.“Amehamia hivi karibuni, anaonekana muda wa kutoka na kuingia tu.
“Lulu ni binti mrembo mwenye mvuto wake, ukizingatia ana nyota pia ya kupendwa, kwa hiyo siyo mtu wa kukaa uswazi,” alidai mtoa habari wetu na kuongeza:

“Bidada kaula maana nasikia jamaa ameahidi kumpa matunzo ya nguvu.
“Alianza kwa kumnunulia lile gari la kifahari la Toyota Rav4 New Model analotembelea Lulu, sasa naona kamuweka pazuri na kweli nyumba inaendana na hadhi yake.

ADAIWA KUMPA JEURI YA KUWAFUNIKA KAJALA, WEMA
“Nasikia jamaa amempa jeuri ya kuwafunika kabisa Kajala (Masanja) na Wema (Sepetu) ambao inasemekana wana mkwanja wa kumwagamwaga ovyo.”

LULU LAIVU!
Kupitia Kipindi cha Nirvana kinachorushwa na EATV, Lulu alionekana ndani ya mjengo huo uliojaa mazagazaga ya thamani.Mjengo huo una makabati makubwa ya nguo na viatu kiasi kwamba mtu unaweza ukahisi umeingia kwenye duka la nguo (boutique) na viatu kibao.

Akizungumza kwa kujiamini Lulu alisema kuwa anapenda vitu vizuri hasa linapokuja suala la kupiga pamba ndiyo maana amejaza pamba kali kwenye makabati.“Kimsingi sipendi shida, napenda kuvaa vizuri, kula vizuri, kulala pazuri na mambo yote mazurimazuri,” alisema Lulu.

BILIONEA GANI?
Ili kupata undani wa mwanaume huyo, gazeti hili lilichimba ambapo kwa mujibu watu wa karibu na Lulu, jamaa huyo ni mfanyabishara mkubwa wa madini jijini Arusha.

“Kama mtakumbuka, huyo jamaa aliwahi kuwagombanisha Lulu na Husna (Maulid) kwani mwanzoni alikuwa mwanaume wa Husna.“Hivi unajua kabla ya ishu hiyo, Lulu na Husna walikuwa mashosti lakini baadaye wakawa kama paka na panya kisa tu ni huyo bilionea,” kilidai chanzo hicho.

LULU ASAKWA
Baada ya kunyetishiwa habari hiyo ya mtaani, gazeti hili lilimsaka Lulu hadi nyumbani kwake na lilipomkosa lilimtafuta kwa njia ya simu na alipopatikana alifunguka:

“Kiukweli kabisa nyumba ninayoishi sasa mimi na familia yangu siyo kwamba nimepangishiwa wala kununuliwa na sijui bilionea au kigogo yeyote, hayo ni maneno ya watu tu. Unajua watu wanaongea sana, wanadhani mimi siwezi kujimudu,” alisema Lulu kwa kujiamini.
GPL


Amanda Azua Balaa Mtaani Baada ya Kuvaa Nguo Fupi , Masela Wamfuata Nyuma na Kumpigia Miluzi

$
0
0
Stori: Chande Abdallah

Msanii wa filamu, Tamrina Posh ‘Amanda’ hivi karibuni alizua balaa la aina yake baada ya kukatiza mtaani akiwa amevaa kigauni kilichokaribia kuacha wazi makalio yake.

Tukio hilo lililowashangaza wengi lilijiri eneo la Mwenge Bamaga jijini Dar wakati msanii huyo alipokuwa akitembea kuelekea kwenye mgahawa uliopo eneo hilo.

Huku akitembea kwa staili ya ‘hamsini…mia…hamsini…mia…’, Amanda alionekana kufanya makusudi kwani kadiri wanaume walivyokuwa wakijikusanya kumshangaa, ndivyo alivyoongeza mikogo na kuwaacha miudenda ikiwatoka.

Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wanaume ambao wengi wao ni madereva wa Bajaj na mafundi gereji walionekana kumzodoa huku wakieleza kuwa, ni msanii asiyejiheshimu.

“Yule kutuvalia sisi vile ndiyo nini? Mavazi yale yanavaliwa klabu usiku tena wanaovaa vile ni wale wasioithamini miili yao, tukisema anatutangazia biashara tutakuwa tunakosea?” alihoji fundi mmoja aliyefahamika kwa jina la Juma.

Katika kujua sababu ya kuvaa kigauni hicho, mwandishi wetu alimfuata Amanda lakini kabla ya kuulizwa chochote aliingia kwenye gari na kuondoka zake baada ya kuwachimba mkwara waliokuwa wakimpigia miluzi. Baadaye alipopigiwa, simu iliita bila kupokelewa.
GPL

Shoga la Kiume Lafunguka Jinsi Linavyompagawisha Mwanaume Wake..'End of the World'

$
0
0
Mwanaume mmoja ajulikanaye kwa jina la Saidi amenaswa na Kamera akielezea jinsi anavyompagawisha mpenzi wake wa kiume, alikuwa akipiga stori na Mashosti zake wa Kike..
Angalia Video Hapa chini:

Aibu!Hii Ndio Video ya Mchungaji Aliyenaswa Akila Uroda na Muumini Wake

$
0
0
Wakaazi wa eneo la Rosters jijini Nairobi walishuhudia kioja si haba wakati mchungaji wa kanisa moja liliko mtaani pumwani alipofumaniwa na mke wa wenyewe kwenye tendo la ndoa.

Hata hivyo, mchungaji huyo alijitetea kuwa alikuwa kwenye pilkapilka za kutoa huduma. Mwanahabari Lofty Matambo anamshike mshike huo.

VIDEO HAPO CHINI

Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba Watishiwa Maisha

$
0
0
Siku tatu kabla ya Bunge la Katiba kuanza kupigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, watu wasiojulikana wameanza kusambaza vitisho vya kuwatia hofu wajumbe wa Bunge hilo.

Watu hao wamesambaza vipeperushi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma usiku wa kuamkia jana, wakiwataka wajumbe kutoingia bungeni vinginevyo yatakayowapata watajuta, huku wajumbe kutoka Zanzibar wakitishiwa kwa ujumbe wa simu kupitia mtandao wa WhatsApp.

Kunani Jamani Tanzania Tunaelekea Wapi?

Diamond 'Kusema Ukweli Sina Mahusiano na Meninah. Kila Mtu Anajua Mie Wangu ni Wema'

$
0
0
Hatimaye Diamond Platnumz amefunguka kuhusu tetesi zinazoendelea kuwa ameachana na Wema Sepetu na kwamba ana mpango wa kufunga ndoa na Meninah,  Diamond alisema kuwa tetesi hizo zimekuwa zikimhuzunisha kwa kiasi kikubwa.

“Unajua hizi habari kiukweli zimekuwa zikinihuzunisha sana,” amesema superstar huyo wa muziki wa Bongofleva Tanzania.

 “Unajua mie ni mtu mmoja ambaye sipendi kuzunguzia mambo ya rumors, siju magazeti huwa sipendi kuzungumzia kabisa, kwa kuwa najua kabisa siwezi kubishana na media kwakuwa media ni kubwa, maana najua utaongea na huyu na yule siku ya siku utagombana na watu. Ndio maana huwa nakaa kimya,” ameongeza Diamond anayetusua shows katika nchi mbalimbali ndani na nje ya Africa kwa sasa.

“Kusema ukweli hili suala limekuwa likiniumiza ‘eti sijui kuna vikao vya harusi mie nataka kumuoa Meninah’. Kusema ukweli sina mahusiano na Meninah. Kila mtu anajua mie nina mahusiano na Wema.

“Wema ndo mpenzi wangu, ila wakati mwingine nakuwa naelewa ile inakuwa ni trick ya kibiashara. Mtu anajua hata nikimuandika vipi ‘Diamond sijui kafanya nini watu hawawezi kumchukia!

Kwahiyo wanaamua kunitengenezea chuki na maadui kwa watu kuwa nipo na mwanamke wangu halafu namsaliti” alisema Diamond  na  kuongeza

Baby Madaha atamani penzi la Wema na Diamond, Natamani Ingekuwa Mimi

$
0
0
MWANAMUZIKI mwenye vituko kila kukicha Bongo,  Baby Joseph Madaha, ametoa dukuduku lake la moyoni na kusema kuwa kila kukicha anayatamani mapenzi ya Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond’ kama angekuwa yeye.

Akizungumza na paparazi wetu, Baby alisema kuwa kila akiwaona Wema na Diamond anatamani sana na yeye awe kwenye uhusiano wenye kupendwa na kuhamasisha kama ulivyokuwa wa mastaa hao kiasi ambacho amefikia hatua ya kuwaonea wivu.

Kiukweli nikiwaona hawa watu nasikia mpaka wivu na kuna wakati natamani niwe mimi jamani maana sifikiri kama kuna ‘kapo’ kali hapa Bongo kama hii jamani, naitamani hadi basi,” alisema Baby.

UKAWA Yaitaka Polisi Kuzuia Mikutano ya Kinana Nchini, Kama Ilivyozuia Maandamano ya Ukawa

$
0
0
UMOJA wa Katiba ya Wananchi “Ukawa” wamemtaka Mkuu wa Jeshi la  Polisi nchini,  kuzuia mikutano ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahaman Kinana,  kama alivyozuia mikutano na maandamano ya vyama vya siasa  vinavyoundwa  na Ukawa.
Hayo yamezungumzwa na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  Lissu wakati akizungunmza na waandishi wa habari leo, makao makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam .

Aidha umoja huo umetoa tamko juu ya amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu mamlaka ya Bunge Maalum la Katiba kwa kumuunga mkono Saed Kubenea  aliyekuwa amefungua kesi ya kuitaka

Mahakama Kuu itoe ufafanuzi wa mamlaka ya bunge hilo  kwa mujibu wa kifungu cha 25 cha sheria ya mabadiliko ya katiba, sura ya 83 ya sheria za nchi yetu.

Dkt. Slaa: Sitta ni Kielelezo cha Mfumo Uliooza, Mlinda Mafisadi na Ufisadi

$
0
0
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemshukia Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, kikisema kiongozi huyo si mwadilifu, si mwaminifu na mnafiki, akiwa ni mwakilishi na kielelezo cha mfumo uliooza katika serikali ya CCM uliolifikisha taifa hapa lilipo.

Kimesema kuwa tabia za Sitta hasa katika kuua mijadala ya kifisadi ndani ya bunge, kwa ajili ya kulinda maslahi yake binafsi ya kusaka vyeo, inamfanya asiwe tofauti na watuhumiwa wengine wa ufisadi ndani ya chama chake na serikalini, kikishutumu kuwa mlinda ufisadi na mafisadi ama ni naye ni fisadi kama wenzake au ni fisadi mkubwa kuliko mafisadi wenyewe.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Iringa jana Ijumaa, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibroad Slaa alisema kuwa Sitta hana uwezo wowote wa kukisema chama hicho wala viongozi wake, akimtaka amalize kwanza matatizo waliyonayo yeye na wenzake ndani ya CCM, likiwemo la kujivua gamba, ambalo linaonekana kuwashinda.

Katika mkutano huo chama hicho kilisema pia kuwa hatua ya polisi kuzuia mikutano ya Operesheni Sangara-M4C kwa siku tano, kupisha shughuli ya sensa, kumekisaidia chama hicho kugundua mbinu na mikakati mizuri ya kuwafikia wananchi kwa mikutano ya ndani, ikiwa ni maandalizi ya mikutano ya hadhara, hivyo kupata mafanikio zaidi mkoani Iringa kuliko ilivyokuwa mkoani Morogoro.

Sitta ni kielelezo

Katibu Mkuu huyo wa CHADEMA ambaye aliwaambia waandishi wa habari kuwa amelazimika kumzungumzia mtu lakini kwa nia ya kuonesha alivyo kielelezo cha ubovu wa mfumo na uongozi wa serikali na CCM, alidai kuwa kwa sababu ya tabia ya unafiki aliyonayo Sitta, kiongozi huyo ni sawa na viongozi wengi wa serikali ya CCM akiwafafanisha na mbwa mwitu waliovaa ngozi ya kondoo.

“Nchi hii imefika hapa ilipo kwa sababu ya viongozi aina ya Sitta ambao hawasiti kusema uongo hadharani, wanafiki, hawana uadilifu, waongo, walio tayari kusaliti maslahi ya umma kulinda maslahi ya tumbo, Sitta yeye ana uzoefu gani, huu wa kulinda mafisadi bungeni kwa kupindisha hoja za ufisadi ili apate ubunge na uspika.

“Hivi Sitta atuambie anaposema CHADEMA haina watu wenye uwezo lini tuliwahi kusema tukiingia serikalini tutakuja na watu wetu wote au ndiyo yale mawazo ya kijinga kwamba CHADEMA wakishika nchi watapata wapi ikulu…atuambie kuna chuo kikuu chochote kinafundisha uwaziri au kuna chuo kikuu kinafundisha ukatibu mkuu wa wizara, asitupangie sisi namna ya kupata viongozi wetu.

“Hivi hajui kuwa Mwalimu alipopata nchi aliandaa watendaji. Hoja za kipuuzi, mtu akitoa hoja za kipuuzi, naye atakuwa mpuuzi tu wa kupuuzwa, tumefika hapa, nchi imegubikwa na uozo wa ufisadi kwa sababu ya mawaziri wa aina ya Sitta ambaye haogopi kuropoka hadharani, tena akiwatukana wapiga kura, ambao pia wengi wao ni vijana.

Hoja ya kuchezesha disko

“Anaposema Mbowe ni mchezesha disko anataka kupeleka ujumbe gani, anataka kusema nini…kwamba ni kosa, kwa hiyo anamaanisha wacheza disko ni criminals (watenda jinai), kwa hiyo wacheza disko ambao pia ni wapiga kura na wengi ni vijana ni criminals, je hajui kuwa kuna mawaziri wenzake wanaokesha pale Billicanas Club,” alisema Dkt. Slaa.

Aliongeza kusema kuwa hoja hiyo ya kumshambulia Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kwa sababu ya kumiliki ukumbi wa mziki, kuwa nayo ni hoja mbele ya watu makini, Dkt. Slaa alisema waziri huyo amedhihirisha alivyo mbumbumbu wa sheria na hajui lolote, tofauti na ambavyo siku zote ametaka kuonekana mbele ya jamii.

“Ni dhahiri hana uzoefu wowote na hajui, ndiyo maana ameishia kwenda kuwatukana wapiga kura yeye akifikiri anaimaliza CHADEMA, maana wacheza disko ndiyo wapiga kura hao hao, lakini yeye kama msomi kweli, tena anasema ni mwanasheria, alipaswa aelewe kuwa duniani kuna nyumba za disko za staha, zimesajiliwa na zinafanya kazi kwa mujibu wa sheria na zimepewa leseni na serikali.

“Huyu Sitta kila siku anajiita yeye mwanasheria kumbe mbumbumbu kupindukia tu hana tofauti na wana CCM wenzake ambao jamii inawashangaa kwa matendo na kauli zao, ku-run club ni sawa na ku-run biashara nyingine yoyote, almuradi iendeshwe kisheria na kihalali, sasa kama anaona ni kosa aiambie serikali yake ifute leseni ya biashara hizo.

“Tulitegemea mtu ambaye anataka kuonekana ni mstaarabu, anahoji uzoefu wa wenzake nay eye anasema ana uzoefu angekuja na mawazo ya kupeleka nchi mbele kumbe yuko sawasawa tu na wenzake ndani ya CCM,” alisema Dkt. Slaa.

Ameingia kichwakichwa, kwenye tope

“Leo nalazimika kumzungumzia mtu, Watanzania wanajua mara chache sana CHADEMA huwa tunalazimika kuzungumzia watu badala ya masuala…lakini nitazungumza kwa namna ambayo huyo mtu atakuwa anawakilisha mfumo huu wa serikali ya CCM na chama chao jinsi ulivyooza na kutufikisha Watanzania hapa tulipo.

“Samuel Sitta ameingia kichwa kichwa kwenye matope ambayo hawezi kutoka wala kujinasua, muda mrefu tumemhifadhi lakini leo tutampiga ngumi za uso lakini kwa namna ambayo atakuwa anawakilisha mfumo huu uliooza…

“Ghafla tu ameamua kuibuka na kuzingumzia CHADEMA, badala ya kujenga chama chake, bila kujua amedhihirisha kuwa CHADEMA sasa ni tishio kwao, maana huwezi kuzungumzia kitu ambacho hakikuathiri, amedhihirisha namna ambavyo yeye wenzake sasa wanatapatapa kweli kwa sababu ya CHADEMA.”

Makombora zaidi; mlinda ufisadi na mafisadi

Dkt. Slaa alisema kuwa wakati chama hicho kilipoanza kuasisi hoja ya ufisadi nchini kikiwa mstari wa mbele kupiga vita kila aina ya ufisadi, Sitta wakati huo akiwa Spika wa Bunge, ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuweka vikwanzo na vizingiti akilinda maslahi yake nay ale ya chama chake, badala ya maslahi ya wananchi.

“Yeye ndiye aliyepindisha hoja ya Zitto katika kashfa ya Buzwagi ambapo waziri alikuwa amesaini mkataba uliokuwa kinyume kabisa na maslahi ya nchi, tena akasaini nje ya nchi hotelini. Zitto aliposimama bungeni, Sitta badala ya kuangalia hoja hiyo kwa maslahi ya nchi, yeye na wenzake akaipindua kuwa Zitto amesema uongo bungeni.

“Huyu bwana hastahili hata kuwa waziri, anajidai yeye mpiganaji na mpambanaji, wapi? Katika hoja ile nani alikuwa mpiganaji Zitto au Sitta, akapindisha makusudi hoja ya ufisadi mkubwa wa Buzwagi kulinda maslahi anayoyajua mwenyewe. Wakamfukuza Zitto bungeni kwa miezi minne, baadae kelele zilivyozidi huku nje, wakaamua kumrejesha bungeni kimya kimya baada ya mwezi mmoja tu hivi.

“Lakini pia ni Sitta huyu huyu alizima hoja ya ufisadi wa BoT, mambo yote yale ya EPA, Kagoda, Deep Green sijui nini kila kitu kilichokuwa kikihusu BoT. Mtakumbuka aliwatangazia Watanzania kuwa nyaraka za Dokta Slaa ni fake za kuokoteza kwenye internet na nitampeleka polisi, mpaka leo hakunipeleka. Lakini Sitta alikuwa anajua tangu mwanzo, kadri nilivyokuwa nikikusanya documents alikuwa anajua na nampatia copy, mpaka ikafikia ile document kubwa ya mwisho.

“Lakini kwa unafiki wake ameahirisha bunge Ijumaa, Jumamosi akachukua ile document na kwenda nazo TBC akisema ni fake na atanipeleka polisi, lakini leo yako wapi…sasa mtu wa namna hii hafai hata kuwa naibu waziri, mtu yeyote anayelinda mafisadi na ufisadi ni fisadi kuliko mafisadi wenyewe, nawaambia haya kwa sababu tumefika hapa kwa sababu ya kuwa na viongozi, wakiwemo mawaziri wanafiki na waongo kama hawa.

“Lakini ili mjue Sitta ni mtu wa aina gani na kwamba hastahili kuaminika na Watanzania, haikuishia hapo, ufisadi wa Richmond mnajua alivyomaliza mjadala ule kihuni bungeni. Hadi leo hoja ile haina majibu, wakati tunahoji bungeni akafunga hoja ile kidikteta, sasa tunauliza huo ndiyo uzoefu alionao yeye au walionao wenzake, uzoefu wa kulinda mafisadi na ufisadi wa CCM na serikali yao, lakini sisi tunajua kwa nini alipindisha hoja ya Richmond, wakati huo alikuwa anabembeleza ili ateuliwe kuwania ubunge na baadae uspika, mnaona huyu ni mtu wa kuaminika kweli?”

“Hivi kwa matendo ya aina hii Sitta anaweza kutoka nje na kusema yeye ni jasiri na mzalendo, katika majasiri na wazalendo wa kweli Sitta hana sifa hizo, ndiyo maana wameshindwa hata kuyavua magamba kama walivyosema, sasa aende kwanza kwenye chama chake na serikalini, asaidie kuyaondoa magamba kabla hajaanza kutafuta aibu ya kuanikwa zaidi,” alisema Dkt. Slaa.

Siri zaidi; Sitta haaminiki

Dkt. Slaa aliongeza kusema kwa kutoboa siri zaidi namna ambavyo, yeye na Mwenyekiti wa CHADEMA Mbowe, walikuwa wakiendesha mazungumzo na Sitta wakati mwingine kwenye Ofisi ya Spika juu ya Sitta kuhamia CHADEMA na kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, akisema kuwa ulikuwa ni wakati ambapo waziri huyo pamoja na wenzake walipokuwa wameunda Chama Cha Jamii (CCJ) wakiwa bado wako CCM.

Alisema kuwa hata wakati huo bado Sitta alikuwa akionekana kutojiamini na maamuzi yake, ambapo wakati wa majadiliano ya kugombea urais, Sitta alisema kuwa kuna kundi la wabunge takriban 55 watiifu kwake ambao walikuwa tayari kuhama naye kumfuata CHADEMA. 

“Leo natoa siri ambayo sijawahi kuitoa, Sitta ni mhanini. Tumekutana naye mara 100 na zaidi, tumeandikiana vimemo bungeni vya kukutana, wakati mwingine tumekutana hata Speaker’s lounge, tumekutana na Sitta na Mwenyekiti Mbowe, ambaye leo anamwita ni mchezesha disko mara nyingi tu. Lakini hata wakati huo pia hakuonekana kuwa jasiri, maana alikuwa ana wasiwasi nani wanamfuatilia au nani wanamuona, si mtu jasiri hivyo. 

“Zikiwa zimebaki kama siku tano kabla ya kumaliza bunge la mwezi wa saba, kila nikimwandikia kimemo, hataki hata kunitazama, Sitta akayeyuka bila hata kutuaga, baadae CHADEMA tukaamua kutumia utaratibu mwingine na tukaweza kusonga mbele mpaka kufika pale tulipofika. Lakini baada ya uchaguzi akaja mwenyewe kunifuata akinishukuru sana na kunipongeza kuwa nilikuja na hoja tofauti kwenye uchaguzi akisema hata yeye asingeweza kufika tulipofika.

“Lakini hapo sasa tulishamshtukia na kugundua kuwa anataka kugombea uspika kupitia CHADEMA, nataka kuonesha namna huyu mtu alivyo mnafiki, mpotoshaji, nampatia challenge kama kweli yeye ni muumini mzuri akanushe haya, maana ametulazimisha kusema, kwa hoja zake za kupotosha watu na akumbuke, maana huwa anakwenda makanisani na anachanga mapesa, akumbuke maandiko yanasema, yeyote atakayepotosha wadogo hawa, anastahili kutoswa baharini, Makamu Mwenyekiti hapa ametumia Quran kufafanua vizuri,” alisema Dkt. Slaa.

“Maana kwa hakika anataka kupotosha watu ili waone kuwa kuchezesha disko ni suala lisilokuwa sahihi, huo ni upotoshaji, kama anataka kuonesha si sahihi mbona serikali yake hiyo hiyo inaendelea kukusanya kodi. Sasa ilipofikia kwenye suala la kugombea uspika, siku ile jina lake limekatwa kwa sababu walitaka mgombea mwanamke, alinipigia simu usiku wa saa tisa, bahati mbaya nilikuwa nimeweka simu silence, hakunipata.

“Saa 12 nikapokea simu ya mke wake, Margreth Sitta, anasema baba anakutafuta tangu usiku, anataka kuzungumza nawe, nikasema sawa, akaniambia Dokta Slaa wamenifanyia kitu kibaya sana, mimi nimeamua sasa nitagombea uspika kwa tiketi ya CHADEMA, najua umeshateua tayari mtu wa kugombea tayari, lakini naomba nikuhakikishie nafanya press conference saa 4 asubuhi leo, natangaza rasmi kugombea uspika kupitia CHADEMA. Nikamjibu CHADEMA maamuzi hayafanywi na mtu mmoja, nikamwambia asubiri niwasiliane na Mwenyekiti wangu wa chama.

“Baadae tukakubaliana tukutane nyumbani kwake, lakini akawa anasema tusubiri kwanza anamalizia kupanga mikakati na wabunge 55 wa CCM, lakini akisisitiza kuwa uamuzi wake uko pale pale, nikamuuliza vipi kuhusu press conference mbona muda unakaribia, akasema hakuna shida yeye atatuma tu watu wake wataitisha haraka, akasema lakini wanataka kumpatia unaibu waziri, hivyo bado anasumbuana nao, kengele ikalia kichwani sasa huyu mtu akipewa uwaziri itakuwaje.

“Baadae ananiambia, Dokta Slaa nimepigiwa simu na bwana mkubwa naenda kuonana naye, tangu wakati huo Sitta akapotea mpaka saa 8 ndiyo anapatikana, akaanza kuniambia ni lazima aende kwanza Urambo kuwaaga wazee, maana hawezi kuhama bila baraka zao, nikamuuliza vipi kuhusu press conference akasema tutaifanya Jumatatu ijayo Dar es Salaam, akaniambia; tena saa 9 uje uone statement ambayo nimeshaiandika ili na wewe uongeze inputs, Sitta huyu akaniambia kuwa Anne Makinda hatakaa zaidi ya miezi sita kwenye kiti cha uspika.”

Dkt. Slaa alisisitiza akisema kuwa nchi imefika hapa ilipo ikiwa imegubikwa na uozo wa ufisadi kila kona, ukiongeza idadi ya maadui wa taifa, kutoka watatu hadi wanne (umaskini, ujinga, maradhi na ufisadi/CCM) kuanzia ngazi ya chini hadi juu, kwa sababu ya ukosefu wa uadilifu, uaminifu kama Waziri Sitta.

Atalipuliwa zaidi

Dkt. Slaa alisema kuwa ameamua kuzungumza hayo machache kwa sasa, lakini ataongeza ‘kumlipua’ zaidi Sitta endapo atajitokeza kujibu haya ya sasa.

“Yeye ana uzoefu gani Sitta, hana uadilifu, si mwaminifu, nchi hii imeoza kwa sababu ya viongozi ya aina ya Sitta, nataka ajibu kwanza hayo kisha nitamlipua zaidi. Ana uadilifu gani katika nchi hii, ametumia mabilioni ya hela ya walipa kodi wa Tanzania kujijengea Ofisi ya Spika Urambo, tunauliza kuna spika wa Urambo au alijua yeye atakuwa spika wa milele au basi Makinda awe anakwenda Urambo wakati wa mapumziko ya bunge.

“Tulichoamua bungeni ni kwamba kila mbunge ajengewe ofisi yenye thamani isiyozidi milioni 40, lakini yeye akaenda kujijengea ofisi ya milioni 350 tena kwa kasma tofauti na inavyotakiwa lakini kibaya zaidi tendering process ya vifaa vya ofisi haikufutwa na vililetwa na kampuni ambayo majuzi imehusishwa na Blandina Nyoni, hakuna mahali tendering imefanyika, amefanyia ufisadi mali ya taifa,” alisema Dkt. Slaa.

Mahakama ya A. Mashariki Yatengua Ubunge wa wabunge wa EAC kutoka Tanzania

$
0
0
Ni muda mfupi uliopita jopo la majaji wa mahakama ya Afrika mashariki huko Arusha imetoa uamuzi wa Shauri ambalo ilifunguliwa na CHADEMA ( Antony Komu ) aliyekuwa mgombea wa Chadema katika Bunge la Afrika mashariki , ambaye alifungua kesi ya msingi kuhusu kukiukwa kwa hati ya makubaliano ya Afrika ya mashariki , kutokana na Chadema kutokupata nafasi wakati hati iko wazi na imeelezea kinagaubaga jinsi ya kupata wawakilishi kutokana na uwiano wa vyama katika mabunge ya nchi washirika .

mahakama ya Afrika mashariki , imesema kuwa Bunge na serikali walikiuka hati hiyo ibara ya 50 , na pia kitendo cha kumpa fursa kugombea John Lifa Chipaka wakati chama chake hakina mbunge ni muendelezo wa kukiukwa kwa hati hiyo ya Afrika mashariki .

Jopo la Mawakili wa Chadema lilikuwa likiongozwa na Edson Mbogoro , Aidha mahakama imeitaka serikali kulipa Antony Komu gharama zote za kesi .

Huu ni muendelezo wa CCM kujidhalilisha kwa kutumia mabavu kwani mliofuatilia mtakumbuka kuwa kulikuwa na ubishani mkubwa sana wa kikanuni ndani ya Bunge siku ya uchaguzi huo, hukumu hii itasaidia sasa ile kesi ya pili ambayo iko mahakama kuu Dodoma ya kuitaka mahakama hiyo itengenezwe uchaguzi ule na irudi we upya kuendelea kwa kasi .

Kupata Wanawake Siku Hizi Husumbuki Kuwapata, Nawashangaa Wanaobaka Wanawake

$
0
0
Digitari imerahisisha sana maisha, hata mapenzi wakuu yapo ya kidigitari. Zile habari za analogia mwanamke unamtongoza leo kula issue mwakani hazipo tena.

Leo ukijisikia una hamu ya kungonoko weka msimbazi wako kwenye walleti taratibu unajiondokea nyumbani humalizi hata kilomita mbili wa kukuchuna anakuwa ameshapatikana. Sana sana kama unawaogopea macho wanawake warembo unaokutana nao njiani unaweza kutembea kilometa nyingi kidogo, lakini ukweli ni kwamba wanawake wengi warembo rahisi sana kuwapata kwa sababu hawajiamini lakini mbili wanaume wengi wamejengeka na kasumba kwamba kuoa mwanamke mrembo utapata stress ,bp, sheli nk.

Mwanamke unampata unasex naye na zaidi ya zaidi huna hata sababu ya kujua jina lake ,kwa sababu mkiachana na biashara imeisha , sana sana kama pombe yake imekuridhisha utachukua namba yake ya simu. Kama pombe yenyewe imezidi maji kimea kidogo mkiachana ndo imetoka hiyo.

Kwa mazingira yalivyo sasa huwa najiuliza kwa nini watu wanabaka,kila nikifikiria huwa sipati jibu kwa kweli.

Faida Ama Uzuri wa Kuoa Single Mothers na Wadada Over 35 years

$
0
0
Ndoa nyingi zina changamoto lakini nimegundua ukioa single mother au dada ambae ni 35+ hawa watu mara nyingi huwa ni wife materials ukilinganisha na hawa wenye age ya 20-35.

*Hawa watu wana commitment sana katika ndoa zao.
*Wanakuwa washapitia changamoto nyingi zinazohusisha mahusiano so huwa hawasumbui.
*Wengi wamekomaa kiakili na wanajua jinsi ya kuhandle mume na familia kwa ujumla
wana mazuri mengi.

Kama hujaoa ukipata watu wa namna hii usipoteze fursa.

Mambo ya Kishamba Ambayo Mwanaume wa Sasa Hutakiwi Kuyafanya

$
0
0
1. Kufuata mkumbo, kutokuwa na maamuzi yako mwenyewe.

2. Kuongea lugha chafu, huwezi kumaliza sentensi bila matusi.

3. Kuvaa mlegezo.

4. Kunyoa panki, kiduku au kuacha afro.

5. Kuvaa viatu vya four angles au vyenye soli kubwa.

6. Kukimbia mimba au kutelekeza familia.

7. Kunywa pombe bila kipimo, kushinda bar bila sababu maalumu utadhani wewe kreti.

8. Kuvaa suruali za model au bwanga au kuvaa mayeno.

9. Kumpiga mwanamke awe mkeo, mpenzi wako au hata rafiki tu.

10. Kuwa na hulka ya kupigana, yani huwezi ku-solve tatizo kwa njia nyingine zaidi ya kuwaza kupigana.

11. Kuwa wa kwanza kulala na wa mwisho kuamka.

12. Kuvaa tshirts zenye maneno makubwa na mbaya zaidi yasiyo na maana.

13. Kulakula hovyo, hyo tabia tuwaachie wanawake

14. Kuvaa vitu oversize ili udumu nayo muda mrefu.

15. Kuvaa mikanda oversize, unakuta mkanda mkubwa had uajikunja ukiwa kwenye luks au una buckle kubwa.

16. Kuvaa tshirts zilizokatwa mikono.

17. Kuvaa boshori.

18. Kukaa vijiweni bila kuwa na shughuli ya maana kufanya.

19. Kuwaza starehe muda wote, weekend ikifika utasikia 'mwana bata wapi?'

20. Kuhonga vimada huku wanao hawana viatu au uniform za shule zimechakaa kupitiliza!! Na mbaya zaidi unawalaza hadi njaa we unakula raha na vimada tu by Ligogoma

21. Kuendekeza michepuko ilhali umeoa tena mke mrembo kweli kweli by Ligogoma

22. Kutojiwekea malengo ya kiuchumi, unaishi tu kama ndege.

23. Kuacha mindevu hovyohovyo bila maana.

Mchinjaji wa Mateka wa Wanamgambo wa Kiislam IS Atambuliwa

$
0
0
Mkurugenzi mkuu wa FBI James Comey amesema kitengo chake kimemtambua mtu ambaye huficha sura yake ambaye ni muuaji,ambaye pia huoneshwa wakati akiwachinja mateka watatu kwenye video inayo nadi wanamgambo wa dola ya kiislam IS.
Pamoja na hayo Bwana Comey amegoma kuutaja uraia wa mtu huyo ama hata kutaja jina lake,ingawa imeshajulikana lafudhi ya mtu huyo kuwa ni mwenye asili ya mji wa London, na Comey amesema kwamba utambuzi wa mtu huyo umefanikishwa kwa msaada mkubwa wa marafiki wa kimataifa.
Muuaji huyo wa waandishi James Foley na Steven Sotloff pamoja na mfanyakazi wa kujitolea David Haines walipigwa picha ya video na kuwekwa kwenye mitandao na wanamgambo hao wa dola ya kiislam na kusaidia kufanya maamuzi juu ya mipango ya wapiganaji wa jihad.

Hali si Swari Kwa Vera Sidika, Uso Waanza Poromoko Kwasababu ya Kujichubua

$
0
0

Habari zimeendea Kenya kuwa yule dada aliyezungumziwa sana kwa kujichubua ngozi na kuwa mweupe hali si swari kwani ngozi ya uso kwa sasa imeanza kuporomoka kama ilivyokuwa ya michael J, Inasemekana ili kutoka nje ni lazima ajipake foundation nyingi ili kuweka sawa , Angali hizo picha utafikiri amejipaka Unga usoni

Mwanamke Apigwa Mawe Hadi Kufa Huko Somalia Baada ya Kufanya Mapenzi Nje ya Ndoa

$
0
0
Mwanamke mmoja ameuawa kwa kupigwa mawe nchini Somalia na kundi la wanamgambo wa Al Shabaab.
Ripoti zinasema kuwa takriban watu 200 akiwemo gavana wa eneo hilo walishuhudia watu wakimpiga mawe mwanamke huyo kwenye mji wa Barowe.
Mwanamke huyo wa umri wa miaka 30 alikuwa ameshutumiwa kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa.
Wadadisi wanasema kuwa mauaji hayo ini ishara ya ushawishi wa kundi la Al shabaab hata baada ya kushambuliwa na serikali ya Somalia pamoja na vikosi vya muungano wa Afrika.
Mji wa Barowe ambao uko umbali wa kiomita 200 kutoka mji mkuu Mogadishu umekuwa ngome ya Al Shabaab.

Amber Rose avunja ukimya tuhuma za kuchepuka na mme wa Mariah Carey, aeleza chanzo cha kumuacha Wiz Khalifa

$
0
0
Amber Rose aliwashtua mashabiki wake na Wiz Khalifa baada ya kuripotiwa kutengana na mumewe huyo huku akifanya taratibu za kupata talaka yake kisheria.

Baada ya taarifa hizo kusambaa kwenye vyombo vya habari siku mbili zilizopita, iliripotiwa kuwa chanzo cha yote ni Amber Rose kuchepuka na  mme wa Mariah Carey, Nick Cannon ambaye pia ndoa yake iko katika sintofahamu.

Hata hivyo, Amber Rose amethibitisha kuwa Wiz Khalifa alikuwa akimsaliti na wanawake wengine huku akikanusha vikali tuhuma za kuchepuka na mwanaume yeyote kwa kipindi chote cha ndoa yao.

Ameendelea kusisitiza kuwa hivi sasa anakijikita katika malezi ya mtoto wao wa kiume, Sebastian.

Amber ameandika tweet kadhaa kupitia twitter kuhusu sakata hilo.

Please stop with the fake stories. I would never ever ever cheat on my husband in a million years I think u guys know this..... Unfortunately my now ex husband can't say the same…. I'm devastated and crushed but my main focus is Sebastian. Thank u for all the support in this difficult time.

Kajala: Watu Wanaamini Sana Magazeti, Sina Utajiri Huo Wanaousema na Siwezi Kumwajiri Wema Sepetu

$
0
0
Kajala Masanja amedai kuwa maisha yake hayajabadilika sana kama ambavyo magazeti ya udaku yamekuwa yakiandika.

Muigizaji huyo wa filamu alisema kuwa tetesi kuwa ana fedha nyingi kiasi cha kuwa na mpango wa kumwajiri Wema Sepetu ni uzushi mtupu. “Mbona maisha yangu ni ya kawaida sana,” Kajala aliiambia Bongo5.

“Mimi naona nipo vilevile hakuna kubwa sana lililongezeka. Nafanya shughuli zangu tu. Tatizo watu wanaamini sana magazeti. Mimi i sina utajiri huo wanaouzungumzia, Kajala ni yule yule,” alisisitiza.

Hivi karibuni Kajala alizindua filamu yake fupi iitwayo ‘Mbwa Mwitu’.

‘I Should Have Known’ – Wema Sepetu Apost Ujumbe Uliowafumba Wengi Instagram

$
0
0
Kuna tetesi kuwa Wema Sepetu na Diamond Platnumz hawapo tena pamoja. Magazeti ya udaku yameandika kuwa Diamond anataka kuoa.. lakini mwanamke anayetaka kumuoa si Wema, ni Meninah! Hatujaweza kuthibitisha ukweli wa tetesi hizo lakini kuna dalili nyingi kuwa hakuna amani tena paradiso.

Tetesi za kuvunjika kwa power couple hiyo ya Bongo, zimechochewa zaidi na post ya mafumbo ya Wema Sepetu kwenye Instagram. Katika post hiyo, Wema ameweka picha yenye rangi nyekundu pekee yake na kuandika ‘I shouldve known’.

Picha hiyo imezua maswali mengi kwa followers wake zaidi ya 211,133 kwenye mtandao huo unaopendwa Tanzania.



Haya ni baadhi ya maoni:

modestae68

@wemasepetu haya mbwa mwitu huyoooo katoka hakuna cha princess sasha,superstar wala ile filam uliyosema unacheza kama mgonjwa wa kansa ukanyoa kipara yaani naumia kuona hivyo wema vp? Acha mambo ya kugawa pesa majukwaani sio wote wanaokushangilia unapopanda ktk majukwaa wengine wanakuzomea hukui? Acha kulewa sifa za team za kukusifia kila ufanyalo yaani sijui niseme nn nikiona wenzio wanavyosonga mbele naumia alafu wewe unaonyesha ufahari majukwaani mmmh kweli hakuna kizuri kinachokosa kasoro haya watakaonitukana poa tu lkn mm wema ni kama mdogo wangu nampenda sana ndio maana namwambia sasa wale waliozoea kutukana tukaneni mpaka mchoke lkn nyie nyie mlikuwa mnasema ktk kampen ya bring our wema hivyo sitoshangaa.mm nitaongea mpaka siku nikiona mabadiliko nafikiri ndio siku nitakayoridhika japo ni kwa faida yake na siyo yangu ila sio mbaya kumwambia mtu kitu chenye faida kwake hata kama huna faida nacho.am still love u wema.

mwelumwikya

I saw this coming @wemasepetu you are a beautiful girl with brains you should not worry at all he is only 25

patrarobert

sitaki kuamini kuwa uko kwenye majuto…na hasa kama majuto yenyewe yanahusiana na mahusiano yako ya kimapenzi….bt kama ndivyo;kwanza pole…kila kitu knatokea kwasababu…angalia ulipojkwaa,nyanyuka futa vumbi…anza upya…Kama n jambo lingine…do the same:ILA U BETTER START LIVING…START ACTING LIKE A LADY…kila mtu ana kasoro zake…n kweli ila zako znaonekana zaidi kwa sababu u r on spotlight…na kwasababu u r an attention seeker…achana na hayo mambo wema…sitaki kuamini kuwa wewe n sikio la kufa…tuko wengi yametukuta mengi sababu ya kutosikiliza wazazi…kusema tu “nampenda mama angu,she z my everything”bila kumtii na kufuata maagizo yake n bure…na AMINI kuwa u wont rest mpaka ukianza kumtii mzazi wako…kama ni huyo diamond atakusumbua mpaka uchanganyikiwe kwasababu huo uhusiano hauna baraka za mama ako…unaweza ona kama kakuruhusu…inabidi akuache ufanye utakalo ili dunia ikufundishe…HUJACHELEWA… @wemasepetu @wemasepetu

callyrissanen

Sijui unachokiongelea kama ni majuto au surprise nzuri. Cha muhimu nakwambia kama dada mkubwa lol, acha starehe za kugawa pesa kwenye kadamnasi. Wekeza hizo pesa uende vacation hata hapo PARIS TUU wewe na umpendaye, sio lazima awe baby yako chibu. Weka pesa na ujijengee tabia ya kutoka outings za kwenda kwenye hotel nzuri kula chakula kizuri wewe na familia yako au mtu umpendaye, sio lazima awe baby yako Chibu. Weka pesa nenda gym kujikeep busy angalau mara 3 kwa wiki, sio lazima na baby yako chibu kwani utapata personal trainer. Weka pesa na acha kuwanufaisha hao wacheza show kwani ukifulia watapata maneno ya kutungia wimbo. Take care and remember that;this too shall pass!!

magz_16

You all need to leave these two have fun and enjoy each other as it lasts.Diamond is still a young boy…!!!How old is he again!!!Hes got a looong way to go as a man.@wemasepetu ….if i were you..i would just focus more on making money and building my future!!Build a house…be a business woman…date real men that will not be intimidated to help me rise up there….I would make money more than even Diamond himself…I would rise like i have never before..and why?coz i carry a powerful name…iam beautiful..and Educated too.I wouldnt go clubbing splashing money on artists..i will go out there make money than all my exes…and my current boyfriend.I would make sure…east Africa knows who # Wema..as a Brand..and not just as diamond girlfriend.I wish you all the best sweetie….stay Focus

Unahisi anajuta kurudiana na Diamond na huenda wakawa wameachana kweli? Tupia maoni yako.

Kali:Mchungaji Awasugua Matiti Wadada Kuwaombea Waweze Kuwa na Uwezo wa Kupata Watoto

$
0
0
Kila Siku zinavyoenda Vioja vinavyofanywa na Wachungaji wa Dini Vinaibuka , Baada ya hivi Karibuni mchungaji mmoja kuwalisha Nyasi Wafuasi wake Mwingine Ameibuka Nchini Kenya Akidai kuwaponya Wanawake ambao hawapati watoto Kwa Kuwasugua Matiti yao Huko Akiwaombea Katika ofisi yake....End of The World...!!
Viewing all 104664 articles
Browse latest View live




Latest Images