Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live

Mayweather Aonyesha Jeuri ya Pesa Anunua Saa ya Almasi ya Bilioni 40.2 Sawa na Mshahara wa Pogba na 50 Cent kwa Mwaka Mzima

0
0
Mayweather Aonyesha Jeuri ya Pesa Anunua Saa ya Almasi ya  Bilioni 40.2
Mwanamasumbwi Floyd Mayweather ameendelea kujiwekea rekodi zake za kununua bidhaa za gharama zaidi duniani kwani ukiachana na magari ya kifahari anayomiliki, sasa amenunua saa yenye gharama kubwa zaidi duniani.

Mayweather kupitia ukurasa wake wa Instagram ameionesha saa hiyo aina ya  “The Billionaire Watch” na kutaja gharama yake kuwa ni Dola milioni $18 sawa na tsh bilioni 40.2 .

Saa hiyo iliyotengenezwa mwaka 2015 na kampuni ya Jacob & Co inatajwa kuwa ndio saa yenye gharama zaidi duniani kwa sasa na imetengenezwa kwa almasi.

Mayweather amenunua saa hiyo kutoka kwa sonara maarufu zaidi duniani, Mjapani Tadashi Fukushima na kueleza kuwa hawaamini kabisa masonara wengine kwa kile alichoeleza kuwa matapeli.

Kwa gharama ya dola milioni $18 ni pesa anayolipwa kiungo wa Klabu ya Manchester United, Paul Pogba kwa mwaka ambapo yeye analipwa Euro milioni 15.4 hii ni kwa mujibu wa gazeti la Marca .

Kwa upande mwingine, Rapa 50 Cent amemtukana Mayweather kwa kumuita mpumbavu kwa kununua saa hiyo yenye gharama kama hiyo.

“Man they done found the 1 fool in the 🌎 world, dumb enough to buy that watch. LOL🤨get the strap,”ameandika 50 Cent kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Floyd Mayweather buys watch worth $18 million and 50 Cent drags him for it

Daimond Awatolea Uvivu Timu Zari na Mobetto "Msiniletee U-team kwa Watoto Wangu"

0
0
Daimond Awatolea Uvivu Timu Zari na Mobetto "Msiniletee U-team kwa Watoto Wangu"
Msanii wa Bongo Fleva Nassib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz kupitia akaunti yake ya Instagram amesema habagui watoto wake na wala hapendi mambo ya utimu. Kupitia akauntihiyo ameweka picha akiwa na mwanaye Daylan na kuandika:

“His is my Kid and he will forever be my Kid, tena My Beloved Kid, na si vinginevyo. Halafu cha kuongeza, msiniletee U-team wenu kwa watoto wangu! they are all my Kids, Nawapenda na siwezi mtenga wala kumbagua yeyote,”

Diamond Platnumz ni baba wa watoto watatu, watoto wawili ‘Tiffah na Nillan’ akiwa amezaa na Zari The Boss Lady na mtoto wa mwisho, Daylan akiwa amezaa na Hamisa Mobeto.

Kitendo cha Mobeto kuzaa na Diamond wakati mwimbaji huyo bado alikuwa na mahusiano na Zari,  kilipelekea warembo hao kuanza kurushiana maneno mitandaoni,  kitu kilichozaa kile kinachoitwa Team Hamisa na Team Zari.

Rais Magufuli Amteua Balozi Mstaafu Daniel Njolay Kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mkurabita

0
0
Rais Magufuli Amteua Balozi Mstaafu Daniel Njolay Kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mkurabita
Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ni kuwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemteua Balozi (mstaafu) Daniel Ole Njolay kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya MKURABITA na uteuzi wake ulianza tarehe 17 April, 2018.

Kufuatia uteuzi huo, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo Kisheria, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Kapt (Mstaafu) George H. Mkuchika (Mbunge) amefanya uteuzi wa wajumbe wa Bodi hiyo.

Ajali yaua Watano na Kujeruhi Watu Watatu Mkoani Mtwara

0
0
Ajali yaua Watano na Kujeruhi Watu Watatu Mkoani Mtwara
Ajali mbaya imetokea mkoani Mtwara na kusababisha vifo vya watu watano na watatu kujeruiwa baada ya gari aina ya Toyota Noah walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka, kisha kuwaka moto.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Lucas Mkondya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa ajali hiyo ilitokea jana saa 10 jioni katika kijiji cha Chingweje wilaya ya Nanyumbu mkoani hapa.

 Kati ya waliofariki dunia ambao wametambulika ni dereva wa gari hilo Babuu Maroro
huku maiti nyingine wameshindwa kutambulika baada miili yao kuungua na moto.

Amesema  majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa katika Hospitali ya Mkomaindo Masasi ni Daria Bushiri (30) mkazi wa Masuguru, Afkam Ling'ande (4) na Khalid Salum  ambaye ni kondakta wa gari hilo.

“Lilivyoanza kuwaka moto, watu watatu walitoka salama ila watano walioshindwa kutoka waliungua, kati yao wawili wameungua vibaya na hawatambuliki. Watatu kidogo wanaweza kutambulika. Tunaomba ndugu jamaa kujitokeza kutambua miili ya marehemu ambayo imehifadhiwa katika hospitali ya Mkomaindo.”



Moto Mkubwa Wateketeza Soko Kenya 15 Wafariki Dunia

0
0
Moto Mkubwa Wateketeza Soko Kenya 15 Wafariki Dunia
Takriban watu 15 wamefariki katika moto mkubwa uliokumba soko moja katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.

Zaidi ya watu 50 walijeruhiwa katika moto huo uliotokea katikati ya usiku na kusababisha uhuribifu wa mali nyingi.

Soko hilo la Gikomba ndio soko kubwa zaidi katika mji huo na moto hutokea mara kwa mara swala linalosababisha uvumi kwamba huenda kuna watu wanaochoma soko hilo, kulingana na gazeti la The Standard nchini Kenya

Huduma ya ambalensi ya St John inasema kuwa moto huo ulianza saa nane za usiku Alhamisi afajiri kabla ya kuenea katika nyumba zilizopo karibu na vibanda vya soko hilo kabla ya kudhibitiwa baada ya dakika 90.

Baadhi ya waathiriwa walichomwa huku wengine wakivuta moshi wenye sumu walipojaribu kuokoa mali yao.

Maafisa wa hospitalini wanasema kulikuwa na watoto watano miongoni mwa waliofariki.

Ukimwi na Mimba Vilinisumbua Sana- Gigy Money

0
0
Ukimwi na Mimba Vilinisumbua Sana- Gigy Money
Msanii na 'video vixen’ maarufu nchini, Gift Stanford 'Gigy Money’ amesema kuwa katika vitu vilivyowahi kumtesa akilini kwake wakati wa ukuaji wake ni pamoja na nasaha za mama yake kuhusu kujikinga na maambukizi ya UKIMWI pamoja na mimba za utotoni.

Gigy amefunguka hayo kupitia KIKAANGONI ya East Africa Television, inayorushwa mubashara kwenye ukurasa wake wa Facebook, ambapo amesema alipopevuka mama yake alimwambia kuwa kuna mimba na UKIMWI anatakiwa kujiepusha na vishawishi.

''Nilipopevuka tu mama yangu akaniambia kuna Mimba na UKIMWI hivyo vitu vilinisumbua sana lakini vilinisaidia'', amesema Gigy Money.

Gigy amesema kuwa vitisho hivyo vilimsaidia, ambapo kwa sasa ametimiza umri wa miaka 21, akiwa mzima wa afya na amefanikiwa kujifungua mtoto wake kawaida.

Dawa Bora za Nguvu za Kiume na Kukosa hamu ya tendo la Ndoa

0
0

DAWA BORA ZA NGUVU ZAKIUME NA KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA. baada ya utafiti wa muda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka sasa

MWASELE HERBAL CLINIC. inakuletea suluhu juu ya matatizo haya kwa kutumia dawa za FULL POWER ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu zakiume. dawa hii ina mchanganyiko wa kutosha kuzalisha vichocheo vingi vya hormone za gestrogen ziwemo vitamin B6&B1, vitamini E pamoja madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na muzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi na kuchelewa kufika kileleni zaidi ya dakika 20-30.

ZAT 50 inarudisha maumbile ya uume yaani kurefusha na kunenepesha ulefu nchi 3-7, upana cm, 3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukitumia maumbile yatabaki kuwa hivyo siku zote . pia tunatibu matatizo mengine kama presha, kisukari , ngiri ,chango la tumbo,tumbo kujaa gesi, kutokupata choo vizuri,miguu kuwaka moto,matatizo ya uzazi, bawasili namagonjwa yazinaa kama kisonono nakaswende.

tunapatikana DAR ES SALAAM. SHINYANGA NA ZANZIBAR. kwa wakazi wa dar es salaam utaletewa huduma hii popote ulipo . wa mikoani tunawatumia kwanjia ya mabasi .

Wasiliana nasi kwa sim no 0717702227 au 0754568767.DR . SAGUDA nyote mnakaribishwa

Mambo Haya Usimfanyie Mkeo, Okoa Nyumba yako

0
0


Mpende mke wako mzuri
Usimkaripie mke wako ukiwa unaongea nae. Inamuumiza sana.
Mithali 15:1

Usimuongelee ubaya kwa mtu yeyote. Mke wako atakua kile ambacho unamuita
Mwanzo 2:19

Usimpe mwanamke mwingine upendo anaostahili mke wako. Huo ni uasherati.
Matayo 5:28

Usimlinganishe mke wako na mwanamke mwingine. Kama huyo mwanamke alikua anakufaa basi Mungu angekupa umuoe
2wakorinto 10:2

Uwe mpole, mvumilivu na msikivu. Amevumilia mengi na amejitolea na ameacha vingi ili awe pamoja nawe. Inamuumiza sana unapokua mkali na kumkera
Waefeso 4:2

Usimfiche chochote. Mmekua kitu kimoja na hivyo ni msaidizi wako, usiweke siri yoyotr kati yenu
Mwanzo 2:25

Usiseme kitu kibaya kuukosoa mwili wake. Amejitolea uzuri wake na mwili wake kukuzalia ww watoto. Ni binadam pia mwenye moyo, sio mwili tu.
Mithali 18:22

Usiulinganishe mwili wake na thamani yake. Mthamini hata pale mtakapofikia uzee
Waefeso 5:29

Usimkaripie kwenye umati wa watu. Suluhisheni matatizo yenu chumbani mkiwa wenyewe.
Matayo 1:19

Mshukuru kwa kuwalea watoto wenu vizuri, nyumba yako pamoja na wewe. Kwani amejitolea kufanya hayo yote.
1wathesalonike 5:18

Mapishi ya wanawake hayafanani. Furahia mapishi ya mke wako. Sio rahisi kumpikia mtu milo mitatu kwa siku kwa siku 365 kwa mwaka kwa miaka mingi mlioishi wote
Mithali 31:14

Usiwaweke ndugu zako kabla yake. Yeye ni mke wako. Ndiye anaekaa na ww. Lazma umpe kipaombele kabla ya ndugu zako.
Mwanzo 2:24

Wekeza katika ukuaji wake kiroho. Mnunulie vitabu, na chochote ambacho kitamsaidia kukua kiroho atembee na Mungu siku zake zote. Hicho ndicho kitu cha pekee unachoweza kumfanyia mke wako.
Waefeso 5:26

Tumia mda wako ukiwa nae kujifunza bibilia na kusali
James 5:16

Tenga mda wa kukaa nae, kucheza nae na kufurahia uwepo wake. Kumbuka, utakapofariki, yeye ndiye ataaesimama pembeni ya kaburi lako. Huenda marafiki zako wakawa na kazi nyingi na kushindwa kuhudhuria.
Mhubiri 9:9

Usitumie pesa zako kumrubuni au kumpelekesha. Pesa zako ni za kwake pia. Mmekua kitu kimoja na ni mrithi wa kila ulicho nacho ulieunganishwa nae na Mungu.
1peter 3:7

Usifichue madhaifu yake. Utakua unajifichua na ww. Mlinde.
Ephesians 5:30

Waheshimu wazazi wake na kuwa na moyo wa upole kwa ndugu zake.
Wimbo ulio bora 8:2

Usiache kumuambia ni jinsi gani unampenda kila siku ya maisha yake. Mwanamke hachoki kusikia hilo.
Ephesians 5:25

Kua katika njia ya Mungu, ndicho kitu kitakacho kufanya uwe mume bora na mwenye hofu ya Mungu.
Warumi 8:29.

OKOA NYUMBA LEO


Askofu Mwenye Wake 24 na Watoto 149 Amehukumiwa Kifungo

0
0
Askofu Mwenye Wake 24 na Watoto 149 Amehukumiwa Kifungo
Viongozi wawili wa dini, mmoja akiwa askofu nchini Canada wamehukumiwa kifungo cha ndani (house arrest) pamoja na kipindi cha uangalizi, kwa kosa la kuoa wanawake wengi na kuzaa watoto wengi.

Shirika la habari la AP, limeripoti kuwa Askofu Winston Blackmore na mwenzake James Oler walikutwa na hatia mahakamani tangu July mwaka jana lakini wiki hii wamehukumiwa.

Blackmore ana wanawake 24 pamoja na watoto 149 huku Oler akiwa na wanawake watano.

Mahakama imemhukumu Blackmore mwenye miaka 61, kifungo cha ndani ya nyumba kwa miezi sita pamoja na mwaka mmoja wa kipindi cha uangalizi (probation).

Wakati huohuo, Oler mwenye umri wa miaka 53 amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu cha ndani ya nyumba pamoja na mwaka mmoja wa uangalizi.

Mbali na hukumu hiyo, Mahakama hiyo imempa adhabu Blackmore ya kufanya kazi za kijamii kwa saa 150 pamoja na Oler saa 75.

Awali, wawili hao walikuwa wanakabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela.

Gazeti la nchini humo la Globla News, limeripoti kuwa Blackmore alianza kuwaoa wake zake tangu miaka zaidi ya ishirini iliyopita.

Imeelezwa kuwa alipokuwa anawaoa wanawake hao, wanawake 10 aliwaoa wakiwa na umri wa miaka 17, watatu walikuwa na umri wa miaka 16 na mmoja alikuwa na umri wa miaka 15.

Katika utetezi wao, wamedai kuwa wameonewa kwani walikuwa wanafanya jambo ambalo linakubalika kwenye imani yao.

Walikuwa wakifanya kazi kama maaskofu wa kanisa linalofahamika kama ‘Fundamentalist Church of Jesus Christ of Latter-Day Saints’

Tumia Super Mkuyati Kurudisha Heshima ya Ndoa

0
0
SUPER MKUYATI ILIYO IMALA HESHIMA YANDOA super mkuyati nidawa ya mitishamba iliyo sheheni miti mbalimbali na kugundulika ina pambana na magonywa sugu

SUPER MKUYATI inanguvu (3) nainafanya kazi kwapamoja (1) itakufanya uchelewe kufika kileleni ndani ya dk 15-20 bila kuchoka (2) ina zalisha homon kwa wingi na kukufanya uwe na mbengu nyingi zenye vimeleo vya uzazi vyilivyokomaa (3) inaongeza ume mdogo uliosinyaa,kunenepesha uume na kurefusha adi nchi 5-8 na upanda sm 2-3 dawa hii haina mazala kwa mtumiaji ata kwa wazee walionaumri 60-80

SUPER MKUYATI ponyo la maradhi yako tumia Leo uone mjabu yake

OFISI YETU ZINAPATIKANA DR MTONI KIJICHI KAMAUNA NAFASI UTALETEWA POPOTE ULIPO KWALE WAMIKOANI UTATUMIWA DR GATUNDU Sm 0717777402/0768408794

Chid Benz Asakwa Usiku na Mchana

0
0
Chid Benz Asakwa Usiku na Mchana
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wamiliki wa Sober House Tanzania, Pilli Missanah ametangaza rasmi kumtafuta msanii maarufu Chid Benz kwa lengo la kutaka kumsaidia kutoka katika janga la utumiaji wa dawa za kulevya ili aweze kurudi katika maisha yake ya kawaida kama alivyokuwa awali.

Pilli ametangaza hilo kupitia kipindi cha eNewz inayorushwa na EATV baada ya Chid kurudi kwa mara nyingine tena kujihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya mpaka kufikia hatu ya kupoteza muelekeo wa maisha yake huku marafiki, ndugu na baadhi ya jamaa kuonekana kama wamemtenga kwasababu ya mambo yake.

"Mimi ndio mtu wa kwanza kumshauri Chid Benz aje Sober house, nimeshamfuatilia sana na hata sasa hivi bado naendelea kumfuatilia ili niweze kumsaidia kwasababu ni kijana bado tuna muhitaji. Kuna uwezekano mkubwa wa Chid kuacha vitu anavyo vitumia na kuwa mtu wa kawaida. Ila tatizo ni moja tu anapaswa akubali tatizo na wala asifiche fiche mambo", amesema Pilli.

Pamoja na hayo, Pili ameendelea kwa kusema "Chid anahitaji huruma yetu sisi wala tusimnyanyapae, tusimseme vibaya wala kumnyoshea vidole. Kusaidiwa kwake ni kumchukua na kumpeleka kwenye tiba ndio msaada mkubwa anaohitaji kwa sasa. Mimi mpaka sasa hivi nimeshamuwekea 'deffender' mtaani yani akionekana tu akamatwe hata kwa nguvu ili wamlete kwangu".

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa Awasili Dar Kukuza Uhusiano

0
0
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa Awasili Dar Kukuza Uhusiano
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amewasili Dares salaam katika ziara ya kwanza nchini humo tangu aingie madarakani.

Ni ziara ya siku mbili ambayo imetajwa kulenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje.

Amewasili asubuhi hii na kupokewa na mwenyeji wake Ras John Pombe Magufuli katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Akiwa Tanzania kiongozi huyo anatarajiwa kutembelea chuo cha kilimo alikosomea miongoni mwa wapiganjiaji uhuru waliotoka nchi za kusini mwa Afrika.

Itakumbukwa kwamba Rais Magufuli alikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika waliompongeza rais Mnangagwa kwa kuchukua uongozi wa nchi pasi kushuhudia ghasia za aina yoyote.

Huenda ziara hii inafuata mualiko rasmi kwa Mnangagwa kutoka rais Magufuli uliowasilishwa na ujumbe wa chama tawala CCM ulioongozwa na aliyekuwa katibu mkuu Abdulrahman Kinana waliokwenda Zimbabwe mwezi uliopita.


Kinana alifanya ziara hii mwishoni mwa mwezi may kabla ya kuachia ngazi kama katibu mkuu wa CCM.

Mnangagwa, aliingia madarakani mnamo Novemba kufuatia mapinduzi ya jeshi dhidi ya kiongozi mkongwe Robert Mugabe.

Mzazi Mwenzie na Chege Awatolea Povu Wanawake Wanaomtaka Mumewe

0
0
Mzazi Mwenzie na Chege Awatolea Povu Wanawake Wanaomtaka Mumewe
Mzazi mwenzake na staa Chege Chigunda ambaye amewatolea povu wanawake ambao wamekuwa wakimjia juu na kumsema vibaya kuhusiana na  Chege na hivyo amewataka wanawake hao wabadilike kwa kupendana na kuonyeshana ushirikiano.

Hii ni kutokana na tetesi kudai kuwa ujumbe huo  kupitia ukurasa wa instagram wa Zahra umemlenga Chege ambaye anadaiwa kuwa amezaa na mwanamke mwingine ambaye aliwahi kumtumia message Zahra na kumtaarifu kuhusiana na ishu hiyo.

Zahra aliandika “Ifikie stage wanawake tubadilike, kwanini wanawake hatupendani lakini? Kipindi Chege yuko bachelor hakuna hata mtu alishawahi kwenda kwenye media or social network yoyote na kumzungumzi vibaya, leo amekuwa star kiasi gani hadi mtake kumuharibia CV yake jamani , kipindi hakai na mwanamke mlikuwa mnamuona muhuni sio handsome na maneno ya kashfa kwa kaka wa watu”

“Hakuna hata aliokubali kuacha mambo yake na kuamua kumzalia kila mtu alikuwa anamdharau kwa style yake, leo mimi nimeamua kuishi naye na kumzalia mnaanza vitu vya ajabu ili baadae muanze kusema wasanii sio wanaume mbona kaachana na mzazi mwenzie? Kwanini uwe mvivu na wakati unapenda kula? Jaribu kwenda shambani anza kulima, palilia mazao yako uje uvune mwenyewe sio ukute kimepikwa tu uanze kula”

“Nipumzishe na DM zenu mtoto wa watu , wewe mwanamke uanemfanyia ubaya leo mwanamke mwenzako kumbuka na wewe kesho utafanyiwa hivyo hivyo, tujaribu kupendana na kusapotiana jamani, hakuna alokamilika hapa duniani , unamsema leo sijui anawanawake wengi, je wewe kwa mtu wako upo peke yako? Nabaki pale pale wanawake tupendane , ndio kwanza mtoto ana miezi mitatu mmeanza hivi haya nikizaa wa pili si mtanirushia mabomu? JITATHMINI ,UTHAMINIKE”

Marufuku Mtumishi Kulala na Gari ya Serikali Nyumbani kwake- Waziri Majaliwa

0
0
Marufuku Mtumishi Kulala na Gari ya Serikali Nyumbani kwake- Waziri Majaliwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma wanaoishi nje ya eneo lao la kazi wawe wamehamia ifikapo July 30, mwaka huu.

“Tunataka watumishi wa umma wawajibike na waishi katika vituo vyao vya kazi. Nawataka watumishi wote wa wilaya hii wanaoishi Dodoma wawe wamehamia hapa ifikapo July 30 mwaka huu na wasiohamia nipewe majina yao,” amesisitiza Majaliwa

Pia ameagiza magari yote ya Serikali baada ya kuisha muda ya kazi yawe yameegeshwa kwenye ofisi za halmashauri na ni marufuku kwa magari hayo kulala nyumbani kwa mtu.

Kagame Cup Kuzinduliwa Rasmi Kesho

0
0
Kagame Cup Kuzinduliwa Rasmi Kesho
Michuano ya Kombe la Kagame inatarajia kuzinduliwa rasmi kesho Ijumaa kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Michuano hiyo ambayo inashirikisha klabu kutoka nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambazo ni  12.

Tanzania imewakilishwa na timu nne ambazo ni Simba, Singida United na Azam FC za Tanzania Bara pamoja na JKU ya Zanzibar.

Katika uzinduzi huo Uwanja wa Azam, timu za JKU na Vipers SC zitafungua dimba katika mechi itakayochezwa saa 8.00 mchana na saa 10.00, Azam itaikaribisha Kator FC ya Sudan Kusini.

Pia, saa 11.00 jioni, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, utapigwa mchezo kati ya Singida United na APR Rwanda.

Ntazaa Mtoto Mwingine Mapema Iwezekanavyo- Aika

0
0
Ntazaa Mtoto Mwingine Mapema Iwezekanavyo- Aika
Msanii wa Bongo Fleva ambaye pia ni mmoja wa memba wa kundi la Navy Kenzo, Aika Mareale amesema kwa kuwa mtoto wake wa kwanza Gold, aliyezaa na memba mwenzake Emmanuel Mkono ‘Nahreel’ ndio amemfungulia njia na sasa atamleta mtoto mwingine mapema iwezekanavyo.


Akizungumza na eatv.tv Aika amesema kuwa, amezaa mtoto mmoja na ameona raha kuwa mama hivyo basi hana muda wa kujishauri tena bali ni kumleta mdogo wa Gold mapema wala sio muda wa kupoteza hivi sasa na kukaa miaka mitatu au minne ndio kuzaa mtoto mwingine.

“Najisikia furaha sana kuwa mama hata wa watoto watano hivi nimeona raha ya kuzaa na hivi sasa niko njiani kuleta mtoto mwingine mambo ya kupishana muda mrefu sio sawa kabisa,” amesema Aika.

Pia ameongeza kuwa kusema alikuwa kwenye mahusiano muda mrefu na nahreel bila kuzaa ,alichelewa hivyo kwakua walikuwa wanasubiria muda mwafaka ufike na muda huo umefika.

Spika Ndugai Amtimua Bungeni Mbunge wa CUF

0
0
Mbunge CUF atimuliwa bungeni
Mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali ametolewa nje ya ukumbi wa Bunge  leo Alhamisi Juni 28, 2018 na Spika Job Ndugai.

Ndugai amechukua uamuzi huo baada ya kuibuka mvutano kati yake na mbunge huyo.

Mvutano huo ulianza baada ya Bobali kusimama na kumpa taarifa mbunge wa Siha (CCM), Dk Godwin Mollel aliyekuwa akichangia kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2018, kuunga mkono kufutwa lwa  kifungu cha 17A cha Sheria ya Sekta ya Korosho ili kuruhusu ushuru unaotokana na mauzo ya korosho ghafi  nje ya nchi kuingizwa katika Mfuko Mkuu wa Serikali.

Wakati Bibali akiendelea kutoa taarifa yake kwa Dk Mollel, Ndugai alimtaka akae chini kwa maelezo kuwa anachokizungumza hakina uhusiano na anachokieleza mbunge huyo wa Siha.

Bobali kabla hajamaliza kumpa taarifa Dk Mollel, Spika Ndugai amemtaka Bobali kukaa chini kwa kile alichomweleza kwamba anachokizungumza hakina uhusiano na anachochangia Dk Mollel

Mara baada ya Bobali kuketi,  Spika Ndugai alimtaka aheshimu kikao cha Bunge.

Baada ya kumtaka Dk Mollel kuendelea na mchango wake, Ndugai amesema, “mheshimiwa Bobali toka nje tukutane mkutano ujao wa Bunge.”

Simba Yawatambulisha Rasmi Dida, Wawa na Kagere

0
0
Simba Yawatambulisha Rasmi Dida, Wawa na Kagere
Klabu ya Simba imewatambulisha rasmi wachezaji wake wapya iliowasajili wiki hii mbele ya waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu hiyo yaliyoko Msimbazi, Kariakoo, Dar es Salaam.

Wachezaji hao ni pamoja na beki Pascal Wawa aliyewahi kuichezea Azam FC, Mlinda Mlango Deogratius Munish 'Dida' ambaye pia aliwahi kuichezea Yanga pamoja na Meddie Kagere kutoka Gor Mahia FC.



Kagere amekabidhiwa jezi namba jezi namba 14, Dida akipewa jezi namba 32 na Wawa akikabidhiwa namba 27.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, ameshindwa kuweka wazi juu ya mikataba waliyoingia na klabu lakini ikielezwa kuwa wamesaini miaka miwili kwa kila mmoja.

Baada ya utambulisho huo, Manara amefunguka na kueleza klabu imedhamiria kufanya usajili wa wachezaji hao ili kukipa nguvu kikosi cha Simba kwa ajili ya mashindano mengi ambao inakabiliwa nayo siku za usoni.

Kauli hiyo ya Manara imekuja kufuatia baadhi ya mashabiki na wadau wa soka kuhoji kwanini Simba inasajili wachezaji wengi na walioenda umri, lakini Manara amewakingia kifua kwa kueleza wana maana pana kufanya hivyo.

Manara ameeleza Simba itakuwa inakabiliwa na mashindano mengi hivyo inawapasa kuwa na kikosi kipana zaidi ukizingatia na ligi ijayo itakuwa na mechi nyingi kutokana na timu kuwa ishirini tofauti na mwanzo.

Pata Tiba ya Tatizo la Nguvu Za Kiume........Inasaidia Kukufanya Urudie Mara 5 na kuchelewa kwa Dakika 20

0
0


TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO LINATIBIKA.Baada ya utafiti wa mda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka DR Magise imekuletea tiba ya matatizo hayo kwa kutumia dawa za:

GUMBA POWER:Ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume,dawa hii inamchanganyiko wakutosha wenyekuzalisha vichocheo vingi vya Hemone za Gestrogen vikiwemo vitamin B6&B1,vitamini E,pamoja na madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi,na kuchelewa kufika kileleni zaidi dakka 20-30.

NTINJE:Inarutubisha maumbile ya uume yani kurefusha na kunenepesha nchi 4-7 upana cm3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukiitumia maumbile yako yatabaki kuwa hivyo siku zote,Pia tunatibu Presha,kisukari siku7,ngiri,chango la tumbo tumbo kujaa gesi,kutopata choo vizuri

 TUPO TZ DAR ES SALAAM   MBAGALA RANGI TATU.HUDUMA HII UTALETEWA POPOTE ULIPO .WASILIANA NAMI 0754741788, 0715741788, 0783741788

-DR MAGISE

Zitto Kabwe Ataka Mwanasheria Mkuu wa Serikali Achukuliwe Hatua Kwa Kulipotosha Bunge

0
0

Wabunge Zitto Kabwe na Cecil Mwambe leo Alhamisi Juni 28, 2018 wamemuomba Spika Job Ndugai kuitaka Kamati ya  Maadili, Kinga na Madaraka ya Bunge kumhoji na kumchukulia hatua Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG),  Dk Adelardus Kilangi kwa madai kuwa amekipotosha chombo hicho cha Dola.


Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) na Mwambe (Ndanda-Chadema) wametoa kauli hiyo leo bungeni mjini Dodoma wakati wa mjadala wa Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2018.


Wakati Mwambe akizungumza katika mjadala huo, Zitto alisimama na kumpa taarifa kutokana na kile alichokuwa akizungumza.


“Juzi wakati mawaziri wakijibu hoja mbalimbali za wabunge, AG alipewa nafasi ya kuchangia. Sina hakika kama ni makusudi au kuna mtu alimwagiza kuamua kulidanganya Bunge,” amesema Mwambe.


Alinukuu kidogo kile alichokisema AG Kilangi kwamba, “pamoja na marekebisho yatakayoletwa na Serikali, kwamba hukumu iliyotolewa na mahakama Desemba mwaka 2000, fedha zilizokuwa zinakatwa za Export levy zilikuwa ni mali ya umma.”


Mwambe alipingana na maelezo yaliyotolewa na AG siku mbili zilizopita kuwa fedha za ushuru wa mauzo ya korosho nje ni za umma na Serikali ndio yenye mamlaka ya kupanga matumizi yake, akisema kuwa fedha hizo ni za wakulima.


Katika maelezo yake siku hiyo, Dk Kilangi alisema fedha za ushuru wa mauzo ya korosho nje ni za umma zinazokusanywa na bodi ya zao hilo kwa niaba ya Serikali, kwamba msimamo huo umetokana na uamuzi katika kesi zilizofunguliwa na Mfuko wa Korosho katika Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa na haujawahi kupingwa.


Wakati Mwambe akieleza hayo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William OleNasha alisimama na kupingana na maelezo yake na kubainisha kuwa kilichozungumzwa na AG ni sahihi.


Maelezo hayo yalimnyanyua Zitto na kubainisha kuwa kilichoelezwa na AG kuhusu kesi hiyo si sahihi


“Mwanasheria Mkuu wa Serikali alilipotosha Bunge kwa kusoma kesi ambayo haikuwapo bungeni na ninatoa hoja mheshimiwa Spika  iagize kamati ya maadili imhoji AG kwa kulipotosha Bunge, aadhibiwe katika hili.”


Mara baada Zitto kueleza hayo, Mwambe alimuunga mkono akitaka mwanasheria mkuu huyo wa Serikali achukuliwe hatua.
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live




Latest Images