Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live

Ofisa Tarafa Atiwa Mbareoni Kwa Kuomba Rushwa ya Laki 3

$
0
0

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani hapa imemfikisha mahakamani ofisa tarafa ya Siloka katika halmashauri ya wilaya ya Bukombe kwa makosa ya kuomba na kupokea rushwa.


Mshatakiwa huyo Tumbo Madaraka alifikishwa mahakamani mbele ya hakimu wa mahakama ya wilaya ya Bukombe, Veronica Seleman.


Mwendesha mashtaka wa Takukuru, Husna Kiboko aliieleza mahakama kuwa Aprili 28, 2018 katika halmashauri ya wilaya ya Bukombe mshtakiwa  alimkamata mtu aliyebeba magogo bila kibali halali na kumuomba hongo ya Sh350,000 ili asimchukulie hatua za kisheria.


Amedai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa kinyume na kifungu cha 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.


Mshtakiwa alikana kutenda kosa na yuko nje kwa dhamana baada ya kukidhi vigezo vya kuwa na wadhamini wawili wenye mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh5 milioni.


Kesi hiyo itatajwa tena Julai 17,2018 kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Mrema awataka watanzania kumuunga mkono JPM

$
0
0

Watanzania wametakiwa kumuunga mkono rais John Magufuli kwa juhudi anazofanya kuimarisha uchumi na kuwahudumia wanyonge wenye shida bila kujali itikadi za vyama vyao vya siasa. 

Mwenyekiti wa taifa wa bodi ya Parole, Agustine Mrema amesema hayo wakati wa ibada ya kumshukuru Mungu kwa kupona  maradhi ya saratani kwenye parokia  la Uomboi ya kanisa katoliki  jimbo kuu  Moshi. 

Mrema amesema kuwa tangu aingie madarakani rais Magufuli  amefanya kazi kubwa ya kuwasaidia watu wenye matatizo ikiwemo yeye kwa kumpeleka India kupata matibabu na katika hali hiyo alianzisha mchango kanisani wa ujenzi wa nyumba za mapadre wa parokia ya Uomboi kama sadaka ya kumshukuru mungu. 

Akizungumza baada ya ibada hiyo paroko wa parokia ya Uomboi Padre Juvenal Kimario amemshukuru Dkt.Mrema kwa kuanzisha mchango huo ambao zitahitajika shs.28mil/= kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo. 

Baadhi ya waumini waliohudhuria ibada hiyo iliyokwenda sanjari na uzinduzi wa uzinduzi wa serikali ya kijiji  cha Kiraracha wamewataka viongozi wengine kuiga mfano wa kumshukuru mungu hadharani baada ya kupata shida mbali mbali.

Jambazi Sugu latoroka gerezani kwa Helkopta

$
0
0

Jambazi sugu ametoroka jela kwa kutumia ndege aina ya helikopta katika jela moja mjini Paris , mamlaka ya Paris imesema. 

Redoine Faid alisaidiwa na watu kadhaa waliojihami ambao walitengeneza mwanya katika lango la jela hiyo huku helikopta hiyo ikitua katika uwanja karibu na jela hiyo. 

Ndege hiyo ilipaa hadi eneo la Gonessa lililopo karibu na jela hiyo ambapo ilipatikana na maafisa wa polisi. 

Faid 46, amekuwa akihudumia kifungo cha miaka 25 kwa jaribio la wizi wa mabavu lililotibuka ambapo afisa mmoja wa polisi aliuawa. 

Hii ni mara yake ya pili kutoroka jela: Mwaka 2013 alitoroka jela baada ya kuwatumia walinzi wanne kama ngao huku akilipua milango kadhaa kwa kutumia kilipuzi. 

Alifanikiwa kutoroka chini ya nusu saa baada ya kuwasili katika jela hiyo iliopo kaskazini mwa Ufaransa. 

Mwaka 2009 Faid aliandika kitabu kuhusu uzoefu wake katika mitaa ya Paris iliojaa uhalifu na kuwa mtu aliyekukuwa akivunja sheria mara kwa mara. 

Sheria inasemaje unapoua wakati ukijaribu kujilinda?

$
0
0

Wakati  mwingine  kujilinda  waweza  kukuita  kujitetea, kujiokoa au kujikinga.  Ni hali ambayo  mtu hufanya jitihada za kujinasua katika  tendo ovu linalotekelezwa na  mtu  mwingine  dhidi  yake.   Mfano  wake  ni  kama  kuvamiwa  na  majambazi, kutekwa, kufanyiwa  fujo  ya  aina  yoyote, kupigwa au  kujaribu  kupigwa n.k. Matukio ya  namna  hii  au  yanayofanana  na  haya ni  sehemu  yetu  ya  maisha.  Yumkini yanapotutokea huwa tunachukua hatua. Na moja ya hatua    za awali kabisa  tunazochukua huwa ni kujaribu kujitetea au kujikinga  nayo.

Umevamiwa  nyumbani   na  majambazi,  umefanyiwa  fujo  njiani  kwa sabasbu  yoyote ile  na  wewe  unaamua  kujitetea  ili  usidhurike,  na  katika  kujitetea  huko unasababisha  kifo  cha  mtu – awe  yule aliyetaka kufanya  fujo au mwingine mpita  njia, sheria inasemaje kuhusu mkasa  wa  aina  hii?  Makala itaeleza  japo  mambo  ya  msingi  kuhusu  hali hii. 

 

1. HAKI YA KUJILINDA

Haki  ya  kujilinda  ni  haki  ya  kisheria. Ni  haki  ambayo  ipo  kwa  kila  mtu.  Mbali  na  kuwa  haki hii  ni ya  kisheria  pia  haki hii ni  ya  kuzaliwa. Kuna  tofauti  kati  ya  haki  kuwa  kisheria  na  kuwa  ya  kuzaliwa. 

 Haki  za  kisheria  ni  zile  haki  zote  ambazo  zimeelezwa  ndani  ya  sheria.  Zimekuwapo  baada  ya sheria  kutungwa na  hivyo  kabla  ya  sheria  kutungwa  hazikuwapo. Haki  ya  kuzaliwa  ni  haki  ambayo  imekuwapo  tangu  mwanadamu  wa  kwanza  alipoumbwa. Ni haki ambayo  mtu  anazaliwa  nayo. 

Haki  hii  haihitaji  kuwa  ndani  ya  sheria ili  mtu  awe  nayo  isipokuwa  tu  anapozaliwa  huzaliwa nayo, hukua nayo  na  hufa  nayo. Kujilinda  au  kujitetea  pale  mtu  anapotaka  kukudhuru hakuhitaji kuwa ndani  ya  sheria ili ndiyo umzuie asikudhuru, isipokuwa ni  jambo ambalo  hutokea  lenyewe (automatic). Lipo tu hata sheria isiliseme.    Kwa hiyo, pamoja na kuwa haki  ya  kujilinda usidhurike ni  haki ya  kisheria, lakini  kubwa  zaidi  ni kuwa haki  hii  ni  haki  ya  kuzaliwa.  

Haki nyingine  za  kuzaliwa  ni  kama  haki  ya  kuishi. Ukishazaliwa haki ya  kuishi  inakuwapo siyo  mpaka  iwe  kwenye  sheria, haki  ya  kuzungumza, ikiwa  umezaliwa  unazungumza  basi  hiyo  ni  haki  ambayo  husubiri  sheria  iitoe, haki  ya  kutembea n.k. Haki  ambazo  si  za  kuzaliwa  ni  kama  hizo  za kuchagua au  kuchaguliwa,  kupiga kura, haki  elimu n.k.

 

2.   UNAPOSABABISHA KIFO UKIJARIBU KUJILINDA/KUJITETEA

Kifungu  cha  18 cha  Kanuni za Adhabu, sura  ya  16 kinasema  kuwa mtu  hawezi  kuwajibika  kijinai  kwa  kitendo alichokifanya wakati wa kutimiza  haki  yake  ya  kujitetea, kumtetea  mtu  mwingine,  au  kutetea  mali. 

Kifungu  hiki  kinasomwa  na  kifungu  cha  18c kinachosema  kuwa  haki  ya  kujilinda, kumlinda  mtu  mwingine au  mali itatumika  kwa  mtu  yeyote  ambaye  katika  kutumia  haki hiyo  atasababisha kifo  au  dhara  kubwa  kwa  mtu  mwingine. 

Maana  ya  vifungu  hivi  ni  kuwa  haki  ya kujilinda  itatumika  kama  kinga  kukuondolea hatia  ya  jinai  iwapo umesababisha  kifo. Lakini  ili ikubalike  kama  kinga  na  usitiwe  hatiani  kwa  kosa  la  kuua,  vifungu  hivi  vimetoa  masharti  yafuatayo:

( a ) Kwanza  wewe  uliyesababisha  kifo  uwe  umesababisha  kifo  hicho  kwa  nia  njema  kwa  maana  ya  kuwa  ulikuwa  kweli  kabisa  ukijilinda  usidhurike. Isije  kuwa  unatumia  nafasi  ya  kujilinda  kumuua  au  kumdhuru  mtu  mwingine   kwa  makusudi  ukijifanya  ulikuwa  ukijilinda. Swali la ‘ulifanya makusudi au  kwa  nia  njema ya  kujilinda’ litathibitishwa  kitaalamu  na  mazingira ya tukio husika.

( b ) Kitendo ulichofanyiwa  kiwe  ni  kitendo  ambacho  kiukweli  ulitakiwa  kutumia  nguvu  kiasi  cha  kusababisha  kifo. Isiwe mnatupiana maneno mawili matatu halafu unasababisha kifo kwa  kisingizio  kuwa ulikuwa ukijilinda usidhurike. Kuwe  na  mazingira  ambayo hata  ukiyatizama  yafanane  na  hatua  ya  kujikinga  hadi  kusababisha  kifo.

( c )  Pia  ikiwa  kitendo  kinahusu  kubaka  au kufanya  kinyume  na  maumbile,  kinga  ya  kujikinga  hadi  kusababisha  kifo inaswihi.

( d ) Pia  kujikinga/kujitetea hadi kusababisha  kifo kunakubalika  ikiwa tendo linahusisha  kuteka  nyara  au  kutorosha.

( e ) Pia  matendo  kama  kuvunja  na  kuingia, unyang’anyi, kuchoma moto, nayo yanakubalika   katika  kujikinga  hadi  kusababisha  kifo. 

Kwa kumalizia,  zingatieni  kuwa  ikiwa  upo  katika  mazingira unayoweza kujikinga/kujitetea  bila  kusababisha  kifo  au  madhara  makubwa,  basi  ni  vema  kufanya  hivyo. Kujikinga hadi  kuua liwe chaguo  la mwisho  pale  unapokuwa huna  namna  nyingine  yoyote  isipokuwa  kufanya  hivyo. 

 

Meneja Ashikwa na Kigugumizi Afya ya Wema Sepetu

$
0
0

DAR ES SALAAM: SIKU chache baada ya video inayomuonesha ‘sweetheart wa Tanzania’ Wema Sepetu akiwa hospitali kusambaa mitandaoni na kuzua gumzo kubwa, meneja wake, Neema Ndepanya amepata kigugumizi kuongelea video hiyo.

Katika video hiyo inayoonekana kuchukuliwa hivi karibuni, inamuonesha Wema akiwa katika hali ya kuumwa huku pembeni mama yake, Miriam Sepetu akimsindikiza kuingia katika chumba cha hospitali ambapo nesi mmoja anaonekana kuwapokea.

Baada ya kuvuja kwa video hiyo,Risasi Jumamosi lilimsaka Wema ili kupata ukweli juu ya afya yake lakini kama kawaida yake simu iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi ‘SMS’ kwa njia ya WhatsApp haukujibiwa.


Hata hivyo baada ya hatua hiyo, mapaparazi wetu walitinga nyumbani kwa mama yake, Sinza, Meeda kwa ajili ya kufuatilia ukweli wa msanii huyo lakini napo hawakufanikiwa kwani waligonga geti na hakuna aliyetoka kuwaeleza kinachoendelea nyumbani hapo.

Baada ya kutoka nyumbani kwa mama Wema, alisakwa meneja wa Wema, Neema Ndepanya ambapo alipopokea simu na kuhojiwa kuhusiana na video hiyo, alipata kigugumizi na kudai kuwa hawezi kuongelea.

“Jamani nipo mbele ya watu hapa siwezi kuongelea suala hilo nitakutafuta baadaye tuongee,” alisema meneja huyo.

Licha ya kusema hivyo, meneja huyo hakupiga simu hadi tunakwenda mtamboni. Alipopigiwa tena hakupokea.

Hivi karibuni Wema aliwahi kuripotiwa kwenda nchini India kwa matibabu baada ya mama yake kuiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mwanaye amekwenda kutibiwa.

Meneja huyo huyo aliwahi kunukuliwa na moja ya gazeti ndugu na hili na kudai kuwa Wema alikwenda nchini humo kwa matibabu ya tumbo.

Muone Ustadhi Ashrafu Atimize ndoto yako..Anatumia Nyota na Nguvu za Asili Kutibu

$
0
0

Muone Ustadhi Ashrafu Atimize ndoto yako. yawezekana ulizaliwa nanyota yakitajiri ila watu wabaya wameikalia mpaka sasa ikawa hufahamu chochote. Mtafute ust Ashrafu Airudishe nyota yako yakitajiri kwakupitia pete inayoendana na nyota yako. Ust Ashrafu Ananguvu zamajini katika utendaji wake. 

Anauwezo wakutoa Mali kwakupitia pete nakwakupitia majini wake. Na anauwezo wakuzirudisha Mali zilizopotea kwanjia zakichawi kwakupitia Pete yakifalme Ambayo inayong'aa muda wowote nakubadilikabadilika rangi. Ust Ashrafu Ametembea baadhi ya nchi kwakuwapatia watu huduma mbalimbali. Kama vile maradhi yakisukari, presha, ukimwi, bawasiri, tezidume, mwiliwote kupooza nakutetemeka, NK. Navilevile Amewapatia wengi huduma yamvuto wa kibiashara, nayamvuto wakimapenzi. 

Nawengi wametoa shukrani zao kwa ust Ashrafu namna Alivyozirudisha Ndoa zao zilizo sambaratika kwamuda mrefu. Mtafute ust Ashrafu ili akusaidie juu yamambo yako. Nahuyu ust anasaidia matatizo yauzazi, nguvu zakiume, kuwashwa mwilini, kutokwa namapere usoni nasehemu za siri, NK. Na anadawa yakumtuliza mume asiesikia nakutulia inayoitwa limbwata. Na anadawa yakumrudisha mpenzi ktk mahusiano kwamda mchache. 

Na amezipatanisha familia nyingi zilizogombana. Na anauwezo wakufarakanisha maadui waliokua pamoja. 

Mtafute Ustadhi Ashrafu kwa no. 0768486717-0627423037 Au Mtafute kwa whasapp 0659438578 

Hizi ndio namba zake mpigie muda wowote usiogope yupo kwaajili yako. Mpigie hupate muongozo wa bure naushri. Ustadhi Ashrafu huduma zake hupatikana mahala popote utakapo muhitaji, ila sehemu kuu anapatikana Bagamoyo.

Croatia Yaing'oa Denmark Kombe La Dunia Kwa Penalti 3-2, Mtanzania Yussuf Poulsen Kuungana Na Ronaldo, Messi Kurejea Nyumbani

$
0
0

Croatia imetinga robo fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuifunga Denmark anayochezea Yussuf Poulsen kwa penalti 3-2.


Hii ni baada ya mechi kwisha kwa dakika 120 kukiwa na sare ya bao 1-1, yote mawili yakiwa yamefungwa ndani ya dakika 4 za mwanzo.


Mikwaju ilikuwa na burudani kubwa huku makipa wa kila upande wakionyesha ujuzi wa kupangua penalti.


Ivan Raktic ndiye aliyemalizia mkwaju wa mwisho na kuimaliza Denmark ambayo ilionekana kama ina nafasi ya kusonga baada ya kipa wake, Kasper Schmeichel kuonyesha ujuzi akipangua penalti mfululizo.

Hii Hapa Mpya Kuhusu Viongozi Walioteuliwa na Rais Magufuli Jana

$
0
0

Hii Hapa Mpya Kuhusu Viongozi Walioteuliwa na Rais Magufuli Jana

Zitto Kabwe Amtupia Dongo Mwigulu Baada ya Kutumbuliwa...Pole Pole Amvaa Zitto na Kumjibu

$
0
0

BADA ya Rais Magufuli kutangaza mabadiliko madogo katika Wizara kadhaa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba kuachwa, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe wameanza kuvutana mitandaoni kuhusu kuachwa kwa Mwigulu.

Kupitia mtandao wa wa Twitter Zitto Kabwe amemkaribisha, Dkt. Nchemba kwa kumwambia sasa ni wakati wake wa kuwatumikia wananchi na kwamba msimamo wake ndiyo uliomponza.

Kufuatia kauli hiyo, Humphrey Polepole katika ukurasa wake, ameamua kumvaa Kiongozi huyo wa ACT kwa kumuita mzee wa kurukia treni kwa mbele 

Rais amefanya mabadiliko kutokana na dhamana aliyopewa na Katiba na si vinginevyo na kumtaka asipotoshe watu.

Nape Nhauye Naye Atia Neno Kutumbuliwa Kwa Mwigulu Nchemba

$
0
0

Upande wa Mbunge wa Mtama ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Nape Nnauye amemkaribisha kiongozi huyo na kumtaka waungane kuwatumikia wananchi.

Breaking News: Lebron James Aikacha Cleveland, Asajiliwa Lakers Kwa Bilion 351,320,200,000

$
0
0
BREAKING NEWS!!!
Inaripotiwa kuwa Siku Mbili tu baada ya LeBron James kumaliza Mkataba wake na timu ya CLEVELAND Amepata Deal na amekubali Kusaini na Timu ya Kikapu ya LAKERS Kwa Dola za Kimarekani Milioni 154, sawa na Pesa za kitanzania Shilingi Bilioni 351,320,200,000 kwa Mkataba wa Miaka Minne.

Historia inasema alikuwepo Kareem Abdul-Jabbar bila kusahau Magic Johnson na kisha akafuata Kobe Bryant “Black Mamba”. Alfajiri ya Leo mchezaji Lebron James amehama kutoka Cleveland Cavaliers ambako alikataa kuendelea na Mkataba na ametua Los Angeles Lakers. Swali pekee ni kuwa, je atafikia mafanikio ama kuwafunika hao waliomtangulia kwenye mioyo washabiki wa Lakers?

Hii Hapa Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo ya Uume

$
0
0
Tatizo hili limekuwa likiwaadhiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baada ya kujiona wapo tofauti sana na wengine kwa kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi 6-8 kwanza upungufu wa vichocheo hivi huchochea ukuaji wa uume chongo ambalo hushambulia nerve ambayo uharibu kabisa ukuaji wa uume, ngiri, punyeto, ambayo huathili misuli ya uume, ngiri huleta maumivu, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, korodani moja kuvimba, kutopata choo vizuri, sababu hizi hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na mara nyingi hata nguvu za kiume ( hamu ya tendo la ndoa) hupungua na kwisha kabisa 

GEMBE :Ni dawa inayozalisha na kukufanya uume kukua na kuongezeka 
NGEMO : Ni dawa bora ya kuongeza nguvu za kiume 

Hukutia hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi mara4 nne bila kukinai au kuchoka pia itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk30-45 kwa mtumiaji pia tunatibu kisukari, bp, ngiri, miguu kuwaka moto KAMA HUNAMDA WA KUFIKA OFISINI KWETU UTALETEWA POPOTE TUPO MBAGALA RANGI TATU 

 0753471612/ 0715249530 
0623 386 305 

DR KUZENZA

Croatia Yatinga Hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Dunia

$
0
0
Croatia Yatinga Hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Dunia
Timu ya taifa ya Croatia imefanikiwa kutinga hatua ya robo Fainali ya Kombe la Dunia baada ya kushinda kwa penati 3-2 dhidi ya Denmark baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya 1-1.



Ushindi huo wa Croatia umeifanya nchi hiyo kuvunja mwiko ambao umedumu kwa miaka 20 wa kufuzu hatua ya robo fainali ambapo mara ya mwisho ilifika hatua hiyo ilikuwa ni kwenye Fainali zilizofanyika mwaka 1998 nchini Ufaransa.

Croatia ilitokea nyuma na kusawazisha dakika ya 4 bao lililofungwa sekunde ya 57 tu na Mathias Jørgensen wa Denmark. Mshambuliaji Mario Mandzukic  ndio alisawazisha ambapo mchezo ulidumu kwa 1-1 hadi dakika 120 na baadae penati.

Katika mikwaju ya penati Denmark walikosa tatu na kupata 2 huku Croatia wakikosa mbili na kupata 3. Waliokosa kwa upande wa Denmark ni nahodha Christian Eriksen, Lasse Schøne na Nicolai Jørgensen. Kwa Croatia wamekosa Milan Badelj na Josip Pivaric.

Waliopata kwa upande wa Denmark ni Simon Kjær na Michael Krohn-Dehli. Croatia waliopata ni Andrej Kramaric, Luka Modric na Ivan Rakitic. Timu hiyo sasa itakutana na wenyeji wa Fainali hizo timu ya Urusi kweney mchezo wa robo fainali.

Chin Bees Awapa Makavu Wasanii Wanaofanya Kiki Kutambulisha Kazi Zao

$
0
0
Chin Bees Awapa Makavu Wasanii Wanaofanya Kiki Kutambulisha Kazi Zao
MSANII wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Musa Ramadhani ‘Chin Bees’ amechukizwa na baadhi ya wasanii wanaopenda kufanya kiki ili waweze kutambulisha kazi zao na kusema kuwa kufanya hivyo kunawapunguzia mashabiki.


Akizungumza na Over Ze Weekend, Chin alisema anashangaa kuona wasanii wenzake wakifanya kiki mitandaoni wakati muziki ni biashara ambayo inahitaji ubunifu tu ili uweze kufanya vizuri na mashabiki wafurahie muziki wako.



“Mimi nachukizwa kwa kweli, wasanii wapo kwenye biashara kwa hiyo ni bora ukafanya kazi kwa ubunifu kuliko kufikiri kiki ndio itakayokufanya ukauza nyimbo zako, unaweza ukatengeneza kiki na bado usifanye biashara ukawa umejishushia heshima tu,”alisema Chin.

Gari Ndogo Yateketea kwa Moto Daraja la Kigambo

$
0
0
Gari Ndogo Yateketea kwa Moto Daraja la  Kigambo
AJALI mbaya imetokea leo Jumatatu, Juni 2, 2018 asubuhi baada ya gari dogo aina ya IST kuteketea kwa moto katika Daraja la Nyerere (Kigamboni), jijini Dar es Salaam.


Inadaiwa kuwa, ajali hiyo imetokea wakati dereva wa gari hilo akilipia fedha ili avuke ng’ambo.


Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika, huku kukiwa hakuna taarifa ya majeruhi wala vifo vilivyoripotiwa kutokana na ajali hiyo.


Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia mitandao yetu.

Rais Magufuli Leo Atawaapisha Viongozi Aliowateua Jana

$
0
0
Rais Magufuli Leo Atawaapisha Mawazili Aliowateua

Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwaapisha wateule wotw aliowateua ambapo sherehe hiyo itafanyika katika ukumbi uliopo Ikulu Jijini Dar leo.

Uongozi wa Yanga Kuweka Wazi Mbadala wa Nsajigwa

$
0
0
Uongozi wa Yanga Kusaka Mbadala wa Nsajigwa
Uongozi wa klabu ya Yanga umesema upo kwenye harakati za kumsaka mbadala wa Shadrack Nsajigwa ambaye alikuwa Kocha Msaidizi wa timu hiyo.

Nsajigwa maarufu kama Fuso aliachana na Yanga kwa madai ya kuwa alikuwa anahitaji kupumzika hivyo ilifikia uamuzi wa kuamua kujiuzu nafasi hiyo kuwapa nafasi wengine.

Nsajigwa alikuwa sehemu ya benchi la ufundi Yanga tangu aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mzambia George Lwandamina ambaye aliondoka klabuni hapo kimyakimya bila kuaga.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kumapata mbadala wa Nsajigwa na pale atakapopatikana watakuwa tayari kumtangaza siku za usoni.

Wakati kikosi cha Yanga kipo kambi hivi sasa kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC utakaopigwa Julai 18 2018 jijini Nairobi.

Maneno ya Nape Nnauye Baada ya Mwigulu Nchemba Kutumbuliwa

$
0
0
Maneno ya Nape Nnauye Baada ya Mwigulu Nchemba Kutumbuliwa
Mbunge wa Mtama, Mhe. Nape Nnauye ametoa kauli yake ya kwanza baada ya Rais Magufuli kutangaza kumtumbua aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba.

Nape amesema anamkaribisha Nchemba kwenye maisha ya kawaida ya ubunge ili kuanza majukumu yake ya kawaida ya kuwatumikia wananchi wake waliompa kura.

“Cde Karibu Sana! Tuliolelewa humu ni kama Mwanzi, upepo ukivuma Mwanzi unalala, upepo ukiisha Mwanzi unasimama ukiwa imara zaidi! Tuwatumikie waliotupa kura!“ameandika Nape Nnaute kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Mhe. Nape ni moja ya wabunge wa CCM waliowahi kuteuliwa na kutumbuliwa na Rais Magufuli katika kipindi kifupi cha mwaka 2015 hadi 2017.

Shamsa Ford Asimamia Maneno Yake Kuhusu Vazi la Irene Uwoya

$
0
0
Shamsa Ford Asimamia Maneno Yake Kuhusu Vazi la Irene Uwoya
MREMBO wa Bongo Muvi, Shamsa Ford amemkingia kifua muigizaji mwenzake Irene Uwoya baada ya watu kumtolea maneno machafu kwenye mtandao wa kijamii kuhusiana na vazi alilovaa la ufukweni.

Akizungumza na Over Ze Weekend, Shamsa alisema kuwa watu wa kwenye mitandao ya kijamii siku zote hawana jema unaweza kufanya kitu kizuri lakini mwisho ya yote likaonekana sio jambo jema hivyo vazi alilovaa Uwoya kwake haoni kama lina shida yoyote.


“Watu wanamtukana Uwoya, kwa vile tu nafikiri hawaelewi sidhani kama Uwoya kuna kosa alilofanya kuvaa nguo ile labda angepita nalo barabarani ingekuwa ni tatizo lakini yopo ufukweni kuna shida gani?” alihoji Shamsa.

Uwoya alizua gumzo kwenye mitandao ya kijamii wiki iliyopita baada ya kutupia picha mbalimbali zilizomuonesha akiwa kwenye vazi linaonesha maungo yake ya ndani kwa urahisi.

Mama Wema Aporomosha Matusi Mazito Kisa Mwanaye

$
0
0
Mama Wema Aporomosha Matusi Mazito Kisa Mwanaye
MIRIAM Sepetu ambaye ni mama mzazi wa staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu juzikati amejivunjia heshima ya kuitwa mama baada ya kumporomoshea ‘mitusi mizito’ mwandishi wetu kisa kuulizwa tu juu ya kilichomsibu mwanaye baada ya video kusambaa ikimuonesha Wema akiingia kwenye hospitali moja iliyopo jijini Dar.



Awali baada ya video hiyo kusambaa yaliibuka maneno yaliyozua gumzo kwa wiki nzima iliyopita ikidaiwa kuwa, hali ya Wema siyo nzuri kufuatia kufanyiwa oparesheni na kukatwa utumbo.

Kufuatia tetesi hizo, mwandishi wetu alifanya jitihada za kufika kwenye hospitali ambayo ilidaiwa staa huyo alikuwa amelazwa lakini madaktari na manesi hawakuwa tayari kutoa ushirikiano.



Hata hivyo, kwa nyakati tofauti meneja wa Wema, Neema Ndepanya ameulizwa kuhusu kinachomsumbua msanii wake lakini hakuwa tayari kutoa maelezo ya kunyooka licha ya kuwahi kukiri kuwa, staa huyo ana matatizo ya tumbo.


Kutokana na usiri uliotawala kuhusu afya ya Wema, gazeti hili juzi Jumamosi lililazimika kumtafuta mama Wema kupitia simu yake ya mkononi na alipopatikana baada ya kujua kuwa alikuwa akiongea na mwandishi, alianza kuporomosha ‘mitusi mizito’ isiyoandikika gazetini.



“Wewe mwandishi……(tusi zito)…. tena nakuambia……. (tusi tena),” alisema mama Wema ambapo baada ya mwandishi kuona anaambulia matusi asiyostahili, ilibidi akae kimya.

Aidha, wakati mama huyo ambaye kwa umri wake na kile alichokuwa akikitoa mdomoni vilikuwa haviendani, akiwa hewani bila kujua kuwa mwandishi hajakata simu, alianza kuwaeleza watu aliokuwa nao kuwa amemkomesha mwandishi.



Swali ni je, kulikuwa na ulazima gani wa mama Wema kutukana matusi hayo wakati alichotakiwa kufanya ni kufafanua tu juu ya kile kinacho zungumzwa mitaani kuhusu afya ya mwanaye? Je, kwa matusi hayo atakuwa amepata faida gani kama siyo kuambulia aibu tu? Majibu anayo yeye!
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live




Latest Images