Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live

Trump: ICE Inafanya Kazi Nzuri kwa Uhamiaji

$
0
0
Trump: ICE Inafanya Kazi Nzuri kwa Uhamiaji
Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumapili ali-itetea idara iliyohusika kudhibiti wahamiaji nchini Marekani-ICE dhidi ya wito kutoka kwa baadhi ya wapinzani wa Democrat kwamba ifutwe

Rais Trump aliandika kwenye Twitter kwamba wa-Liberali wa mrengo wa kushoto pia wanajulikana kama wa-Democrat wanataka kufutwa kwa ICE ambayo inafanya kazi nzuri na wanataka mipaka kuachwa wazi. Uhalifu utakuwa mwingi na hautaweza kudhibitiwa.

Katika mahojiano yake na kituo cha televisheni cha FOX NEWS cha Marekani, Rais Trump alisema kutoka mtazamo wake wa kisiasa kwamba analipenda suala hilo linalohusu uhamiaji. Aliendelea kusema kwamba kama wa-Democrat wanaendelea na wito wao wa kufuta idara hiyo kwa matamshi yake “ninafikiri hawataweza kushinda uchaguzi mwingine”.

Maelfu ya waandamanaji waliandamana Jumamosi nchi nzima ya Marekani dhidi ya sera ya utawala wa Trump ya kutostahmili wahamiaji hususan suala la hivi karibuni la watoto kutenganishwa na familia zao kwenye mpaka wa Marekani na Mexico

Mohamed Salah Kuendelea Kuitumikia Liverpool..... Asaini Miaka 5

$
0
0
Mohamed Salah Kuendelea Kuitumikia Liverpool..... Asaini Miaka 5
KLABU ya Liverpool imemsainisha mkataba wa miaka mitano, mshambuliaji Mohamed Salah kuendelea kuitumikia timu hiyo hadi mwaka 2023 huku akiongezewa mshahara mara mbili zaidi kutoka £100,000 hadi £200,000 (Tsh. Milioni 530.9) kwa wiki.

Salah ambaye ameifungia Liverpool mabao 44 katika mechi rasmi 52, alizocheza tangu ajiunge, anakuwa mchezaji wa kwanza kwa Liverpool kulipwa mkwanja mkubwa zaidi kwenye historia ya timu hiyo.

Rais Magufuli Awaonya Viongozi wa Dini

$
0
0
Rais Magufuli Awaonya Viongozi wa Dini
Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema ili kuepuka chuki, vurugu na mafarakano katika taifa, viongozi wa dini wanatakiwa kujiepusha na kukejeli dini ama dhebu lingine wakati wote wanapotekeleza majukumu yao wasiruhusu siasa kuingilia majukumu ya dini.

Dkt. Magufuli amesema hayo katika hotuba yake iliyosomwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Muhagama, wakati wa ibada ya kuwekwa wakfu askofu mteule Ezekiel Yona wa kanisa la Monravian jimbo la Magharibu Mkoani Tabora.

Waziri Mhagama amesema kuwa serikali itaendelea kusimamia katiba ya nchi ili kila dhehebu na waumini wa madhahebu mbalimbali waweze kuabudu bila shida yoyote.

Kwa habari kamili msikilize hapa chini Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Muhagama akielezea zaidi.

Mfalme Mswati Kuwalipisha Kodi Raia wa Kigeni Watakaowaoa Wanawake wa Swaziland

$
0
0
Mfalme Mswati Kuwalipisha Kodi Raia wa Kigeni Watakaowaoa Wanawake wa Swaziland
Mfalme Mswati wa swaziland ametuma mswaada bungeni kuhusu kutungwa kwa sheria mpya kwa raia kutoka nje ya nchi hiyo kulipa kodi watakapofunga ndoa na wanawake nchini Swaziland kwa kutozwa kiasi cha 30,000 lilangeni ( dola 2,200) .

Mfalme Mswati ametuma mswaada huo bungeni huku akidai kuwa sheria hiyo ni kwa ajili ya kuwalinda wanawake nchini humo.

“ Lengo la sheria hii ni kuwalinda wanawake na matendo ya unyanyasaji kutoka kwa wapenzi wao wa kigeni wanaotumia njia ya kuoa wanawake wetu kwa ajili ya kupata uraia” amesema Msemaji wa Serikali Percy Simelane.

Aidha mswada huo umepingwa vikali na mmoja wa wanaharakati wa kutetea haki za wanawake Dumsane Dlamini akidai kuwa sheria hiyo itawanyima haki wanawawake nchini Swaziland maana wanawake hao huwapenda wanaume wa kigeni kwa utanashati na wanajua thamani ya mapenzi.

Lakini 2016, Wizara ya mambo ya Kigeni ilianzisha mpango wa kutoa uraia kwa wageni nusu milioni hasa kutoka Asia ambao watakuwa sehemu ya idadi ya raia 1.3 milioni ya wananchi wote wa Swaziland .

Rais wa Urusi Aipongeza Timu ya Taifa Lake kwa Kupata Ushindi Dhidi ya Hispania

$
0
0
Rais wa Urusi Aipongeza Timu ya Taifa Lake kwa Kupata Ushindi Dhidi ya Hispania
Rais wa Urusi, Vladimir Putin ameipongeza timu ya taifa hilo kwa kupata ushindi dhidi ya Hispania na kujihakikishia kusonga mbele mchezo wa michuano ya kombe la dunia inayoendelea kwenye nchi hiyo mwaka huu 2018.

Urusi ambayo ni mwenyeji wa michuano hiyo imeingia huku ikionekana kuwa timu dhaifu lakini imeweza kufanya maajabu makubwa mpaka sasa baada ya kutinga hatua ya robo fainali baada ya kuwafunga Saudi Arabia na Misri mpaka inatinga hatua ya robo fainali.



Timu hiyo ambayo imepata mafanikio makubwa mpaka sasa ya Urusi imehudhuriwa mara moja wakati wa ufunguzi na rais wa nchi hiyo wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo ya FIFA.

Putin ameshindwa kuhudhuria kwenye mechi dhidi ya Hispania iliyopigwa kwenye dimba la Luzhniki jijini Moscow kwa sababu ya majukumu ya kiserikali yanayo mkabili.

Kwa mujibu wa msemaji wake, amesema kuwa Putin alimuita meneja wa kikosi cha Urusi, Stanislav Cherchesov kabla ya mechi na kumtakia kilalakheri na hata baada ya mchezo huo alimpa pongezi.

Kutumbuliwa kwa Mwigulu Hakumsafishi Anatakiwa Kushtakiwa kwa Kugharimu Maisha ya Watu- Nassari

$
0
0
“Kutumbuliwa kwa Mwigulu Hakumsafishi Anatakiwa Kushtakiwa kwa Kugharimu Maisha ya Watu- Nassari
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amedai aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba anapaswa kushtakiwa kwa kuwa ameshindwa kusimamia mambo mengi wakati akiwa waziri.

Nassari ametoa kauli hiyo leo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, ikiwa zimepita saa kadhaa tangu kutangazwa kwa mabadiliko ya baraza la mawaziri, huku Mwigulu akiachwa.

“Kutumbuliwa kwa Mwigulu hakumsafishi kwa wananchi. Mengi ameshindwa kusimamia kwa maslahi yetu. Alikuwa wa kwanza kusema kuwa Abdul (Nondo-mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam) alijiteka,” amesema.

“Watu wamepotezwa wameokotwa kwenye viroba na (Mwigulu) kusema ni jambo la kawaida. Alitakiwa kushtakiwa kwa kugharimu maisha ya watu.”

Hata hivyo baadhi ya watu walichangia alichokieleza Nassari walimuunga mkono na wengine kupingana naye.

Mmoja wa watu hao, Miriam Shelutete‏ amesema, “sioni kama kuna ovu lolote alilofanya linalongojea kupata msamaha wa wananchi, alisimamia alichokiamini na kutufikisha hapa tulipofika leo.”

“Uwaziri wake haikuwa dhamana ya milele, kwa wakati ule alionekana ni mtu sahihi ila kwa wakati huu amepatikana mwingine wa kuendeleza safari.”

Watumiaji wa Facebook, WhatsApp na Twitter Waanza Kulipa Kodi Uganda

$
0
0
Watumiaji wa Facebook, WhatsApp na Twitter Waanza Kulipa Kodi Uganda
Raia wa Uganda wanaotumia mitandao ya kijamii ya Facebook, WhatsApp na Twitter kuanzia leo watalazimika kulipa kodi ili kutumia mitandao hiyo.

Serikali ya Uganda inatarajia kukusanya kodi ya mamilioni ya dola kwa mwaka kupitia kodi hiyo mpya.

Wakosoaji wanaiangalia kodi ya kutumia mitandao ya kijamii kuwa ni njama ya Rais Yoweri Museveni ya kufanya maisha ya wapinzani wake kuwa magumu.

Museveni ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1986, anaishutumu mitandao ya kijamii kwa kusambaza taarifa za uongo na uvumi.

Kila mtumiaji wa mitandao hiyo nchini humo, atalipa shilingi 200 kwa siku na kampuni ya simu zimetwikwa jukumu la kukusanya kodi hiyo.

Inakadiriwa watu milioni 17 kati ya Waganda milioni 40 wanaotumia Intaneti kupitia simu zao za mikononi.

Mengi Azindua Kitabu Chake Asimulia Maisha Magumu Aliyopitia " Nililala Chini Wageni Wangu Walikuwa Mende na Panya"

$
0
0
Mengi Azindua Kitabu Chake Asimulia Maisha Magumu Aliyopitia " Nililala Chini Wageni Wangu Walikuwa Mende na Panya"
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi leo Jumatatu Julai 2, 2018 amezindua kitabu chake kiitwacho ‘I can, I must, I will’ chenye kurasa 311, katika hafla iliyofanyika jijini hapa na kuhudhuriwa na Rais John Magufuli.

Kitabu hicho kina ujumbe mbalimbali kuhusu masuala ya kitaifa, kiroho, mafanikio na mafunzo mbalimbali kwa vijana hasa katika ujasiriamali na kujitegemea.

Akizungumzia kitabu hicho, Dk Mengi amesema kimeelezea maisha yake kabla ya mafanikio na mambo aliyoyafanya baada ya kupata mafanikio.

“Maisha yangu awali nililala chini wageni wangu walikuwa mende na panya lakini niliamua kuwa ninaweza kuondoka kwenye umaskini na niliamua kuondoka katika hali hiyo na niliweza kweli,” amesema Mengi.

Amesema wazazi wake walikuwa masikini lakini wenye uwezo wa kujituma katika kazi.

“Mama yangu aliitwa mama wa kibiashara, baba yangu alikuwa ananunua kondoo waliokonda sana anawalisha na baada ya kuuza anauza kwa bei kubwa,” amesema.

Amesema baadhi ya watu humhoji kwamba anasaidia watu na anaweza kufilisika, “nina wajibu hata nikiishi miaka mia sitafilisika, siogopi, Mungu alinifundisha kutoa, mama yangu chakula aliwapa watoto wasioweza, wale ndio sisi tulikula kwa hiyo nimejifunza mbali hili.”

Pata Tiba ya Tatizo la Nguvu Za Kiume........Inasaidia Kukufanya Urudie Mara 5 na kuchelewa kwa Dakika 20

$
0
0
TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO LINATIBIKA.Baada ya utafiti wa mda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka DR Magise imekuletea tiba ya matatizo hayo kwa kutumia dawa za:

GUMBA POWER:Ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume,dawa hii inamchanganyiko wakutosha wenyekuzalisha vichocheo vingi vya Hemone za Gestrogen vikiwemo vitamin B6&B1,vitamini E,pamoja na madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi,na kuchelewa kufika kileleni zaidi dakka 20-30.

NTINJE:Inarutubisha maumbile ya uume yani kurefusha na kunenepesha nchi 4-7 upana cm3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukiitumia maumbile yako yatabaki kuwa hivyo siku zote,Pia tunatibu Presha,kisukari siku7,ngiri,chango la tumbo tumbo kujaa gesi,kutopata choo vizuri

 TUPO TZ DAR ES SALAAM   MBAGALA RANGI TATU.HUDUMA HII UTALETEWA POPOTE ULIPO .WASILIANA NAMI 0754741788, 0715741788, 0783741788

-DR MAGISE

Mmoja Afariki dunia kwa kukosa hewa safi ndani ya mgodi

$
0
0
Mtu mmoja amefariki dunia na mwingine yuko mahututi katika Hospitali ya Wilaya ya Longido baada ya kuvuta hewa nzito ya baruti ndani ya mgodi wa madini ya rubi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng’anzi alisema kwamba tukio hilo lilitokea usiku wa Juni 30.

Alimtaja marehemu kuwa ni Baraka Lenguti (28) mkazi wa KIA wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro ambaye maiti yake ilichukuliwa na askari polisi wa Longido kwa ajili ya uchunguzi.

Alisema kwamba majeruhi aliyelazwa katika Hospitali ya Longido hajafahamika na bado yuko mahututi.

Kamanda Ng’anzi alisema mkasa huo umetokea baada ya wachimbaji hao kuingia ndani ya mgodi kabla ya muda wa saa 48 baada ya ulipuaji wa baruti kufanyika.

Alisema kwamba kwa mujibu wa kanuni za madini zilizowekwa na Serikali wachimbaji wakishalipua baruti katika miamba husubiri kwa muda wa saa 48 ndipo wanaruhusiwa kuendelea na shughuli.

Gigy Money alilimiss Buku la Mo J “Tunataka Kuzaa Mtoto wa Kiume”

$
0
0
Msanii Gigy Money amezungumza baada ya kuoneka wakiwa pamoja na mzazi mwenzake Mo J ambaye ni mtangazaji wa Choice Fm, Gigy amesema kwamba wamerudiana kutokana na wote wawili kuwa wanapendana hata hivyo yale yote aliyozungumza kuhusu Mo J yalikuwa ni hasira ila mtoto ni wa Mo J.
Gigy pia ameongelea suala la wawili hao kupanga kuzaa mtoto mwingine wakiume na ishu ya Mama yake kama kamsamehe Mo J na vipi n inani aliyeanza kumuomba msamaha mwenzie..? Bonyeza PLAY hapa chini kutazama

Tunatibu na Kuponesha Kabisa Tatizo la Upungufu wa Nguvu za Kiume, Busha Bila Kupasua na Vidonda vya Tumbo

$
0
0
TUNATIBU NA KUPONESHA KABISA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME BUSHA BILA BILA KUPASUA NA VIDONDA VYA TUMBO: kwa nini uhendelee kuteseka NA kujiona mpweke pale ukutanapo NA mke au mpenzi wako kwa sababu tu hunaupunguvu wa nguvu za kiume na uume mdogo

MAPRO POWER NO 2 ndio tiba sahii ya kukurudishia heshima ya ndoa yako 1 itakufanya uchelewe kufika kileleni mda wa dakika 15-20 kwa tendo LA kwanza 2 itaufanya uume wako uhonekane mkubwa hasa kwa wale wanaume ambao wamefanyiwa tohara wakiwa wadogo sana au wakiwa watu wazima kwani ipo dawa ya kuimalisha misuli ya uume 3 itakupa uwezo wa kurudia tendo LA ndoa zaidi ya Mara tatu 4 uhuimalisha misuli iliyolegea na kusinyaa ?

WAI SASA UPATE TIBA YA UKWELI NA UHAKIKA NA NI TOFAUTI NA ULIZOWAI KUTUMIA ata wazee wa miaka 80 wanatumia na kupona kabisa ? Tunatoa dawa za uzazi maumivu ya mgongo na kiuno ,kupunguza kitambi ,matiti makubwa,dawa za kisukari,presha,dawa za mvuto wa mpenzi ambaye akutaki au hakuhudumii ipasavyo kutengeneza shepu kwa kina Dada, fika ofisini kwetu MBAGALA ZAKHEMU BARABARA YA JESHINI HIENDA KIBONDEMAJI utaona ifisi himeandikwa MABULA CLINIC

AU PIGA SIMU NO 0743362017 DR AGU

Rais JPM Ampa Milioni 10 Wakonta Kapunda

$
0
0
Rais JPM Ampa Milioni 10 Wakonta Kapunda
Rais Dkt. John Magufuli amempatia msaada wa Tsh. Milioni 10, binti Wakonta Kapunda mwenye ulemavu wa miguu na mikono anayeandika kwa kutumia ulimi, ili zimsaidie kutimiza ndoto yake ya kuwa mwongozaji wa filamu (film director).



Magufuli ametoa pesa hizo leo Jumatatu, Julai 2, 2018 katika Ukumbi wa Serena Hotel jijini dar es Salaam wakati akizindua kitabu cha mfanyabiashara Dkt. Reginald Mengi kinahoitwa ‘I Can, I Must, I Will- The Spirit of Success’ chenye maudhui ya kumfundisha Mtanzania kujikwamua kutoka kwenye umaskini.



Mbali na Magufuli, Mzee Mengi pia amempatia binti huyo kiasi cha dola 20,000 (sawa na Tsh. Milioni 45.45) kutokana na kuandika andiko bora la biashara ambapo Mzee Mengi huwasaidia vijana wa Kitanzania wanaoweza kuandika na kutekeleza andiko zuri la kibiashara ili waweze kuondokana na umaskini.



Wakonta alipata ajali na wanafunzi wenzake wa Kidato cha sita katika, Shule ya Sekondari Wasichana Korogwe, mkoani Tanga mwaka 2012 na kumsababishia ulemavu huo, lakini hakukata tamaa amekuwa akipambana ili aweze kutimiza ndoto zake, na leo njia imeanza kuonekana baada ya kupokea msaada huo ambao ni jumla ya ya Tsh. Milioni 55.45.

NEC Yatangaza Uchaguzi Mdogo Jimbo la Buyungu

$
0
0
NEC Yatangaza Uchaguzi Mdogo Jimbo la Buyungu
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) itafanya uchaguzi mdogo kwenye Jimbo la Buyungu, Mkoani Kigoma na kwenye Kata 79 za Tanzania Bara.



Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage amesema uchaguzi huo utafanyika tarehe 12 mwenzi ujao (Agosti) na fomu za uteuzi wa wagombea zitatolewa kuanzia tarehe 8 hadi 14 mwenzi huu (Julai).

“Uteuzi wa Wagombea utafanyi katarehe 14 Julai, mwaka huu. Kampeni za Uchaguzi zitafanyika kati ya tarehe 15 Julai, hadi tarehe 11 Agosti, mwaka huu na siku yauchaguzi itakuwa ni tarehe 12 Agosti mwaka huu,” alisema.

Jaji Kaijage amebainisha kwamba Tume imetangaza uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge kwenye Jimbo hilo la Buyungu baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Ndugu Job Ndugai.

“Tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, aliitarifu Tume uwepo wa nafasi wazi ya Mbunge wa Jimbo la Buyungu katika Halmashauri ya Kakonko Mkoani Kigoma kufuatia kufariki kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Mheshimiwa Kasuku Samson Bilago,” alisema Kaijage.

Watu 11 wa Familia Moja Wanyongwa

$
0
0
Watu 11 wa Familia Moja Wanyongwa
Watu 11 wa familia moja wamepatikana wakiwa wamekufa kwenye nyumba iliyo katika mji mkuu wa India Delhi, huku 10 kati yao wakiwa wananing'inia katika dari la nyumba hiyo, kwa mujibu wa polisi.

Mwanamke mmoja aliye na takribani miaka 70 alipatikana kwenye sakafu ya nyumba. Wengi wa wale waliokuwa wamekufa walikuwa wamefungwa macho na mikono nayo ilikuwa imefungwa kwa kamba mgongoni.

Familia hiyo imeishi wilaya ya Burari mjini Delhi kwa zaidi ya miaka 20 licha ya kwamba wametokea katika maeneo ya Rajathan uku familia hiyo ikiwa inamiliki maduka mawili katika ghorofa ya chini kwenye jengo la ghorofa tatu.

“Nilipokuwa naenda dukani niliona mlango ukiwa umefunguliwa na nilipoingia ndani niliona miili ya watu hao ikiwa imening’inia katika dari uku imefungwa mikono kwa nyuma” amesema Gurchan Sigh alipokuwa akiojiwa na moja ya chombo cha habari mjini Delhi.

Uku taarifa ya awali kutoka polisi inazungumzia karatasi zenye maandishi walizozipata kwenye nyumba hiyo ambazo zinaashiria kufanyika kwa matambiko yanayoonekana kuwa na uhusiano na vifo hivyo.

“bado tunasubiri matokeo ya upasuaji, na kuwahoji majirani na kuchunguza video za CCTV eneo hilo” amesema afisa mmoja wa polisi alipokuwa akizungumza na chombo cha habari uko mjini Dehli..

Sababu za mauaji hayo pamoja na wahusika bado hazijawekwa wazi na polisi mjini Delhi imesema kutoa taarifa baada ya uchunguzi kufanyika.

Mwenyekiti UVCCM Apandishwa Kizimbani Kwa Kusambaza Taarifa za Uongo

$
0
0
Mwenyekiti UVCCM Apandishwa Kizimbani Kwa Kusambaza Taarifa za Uongo
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) Wilaya ya Tarime, Godfrey Francis leo Jumatatu Julai 2, 2018 amepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Tarime, kushtakiwa kwa kosa la kusambaza taarifa za uwongo kwa njia ya mtandao wa kijamii.

Taarifa hizo ni kuhusu kukamatwa kwa mmiliki wa kampuni ya mabasi ya Zakaria, Peter Zakaria.

Kiongozi huyo ambaye jana alihojiwa na polisi kwa saa kadhaa amesomewa mashtaka na mwendesha mashtaka wa polisi, Kazeni Mrita.

Mbele ya hakimu mkazi Veronica Mugendi, Mrita amedai mshtakiwa amesambaza taarifa hizo mchana wa Julai Mosi, 2018 kwa kuandika kuwa Zakaria alitaka kutekwa na watu wasiojulikana ambao hata hivyo aliwazidi nguvu kwa kuwajeruhi wawili kati yao.

Francis anayetetewa na wakili Onyango Otieno ameachiwa kwa dhamana hadi Jalai 30, 2018 shauri hilo litakapotajwa.

Ametimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja amesaini hati ya dhamana ya Sh2 milioni.

“Watanzania Tuache Kukatishana Tamaa”-Rais JPM

$
0
0
“Watanzania tuache kukatishana tamaa”-JPM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amesema kuwa watanzania wengi wana tabia ya kukatishana tamaa, pindi wanapoona mtu akifanya jitihada za kujikwamua kimaendeleo.

Rais Magufuli ametoa wito huo leo, wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Dkt. Reginald Mengi kinachoelezea historia ya maisha yake kinachoitwa ‘I can, I must, I will’ ambacho amekiandika mwenyewe.

Rais Magufuli amesema kuwa imejengeka tabia ya watanzania kukatishana tamaa katika jitihada za kujikwamua kiuchumi, na kusababisha wasio jiamini kuishia njiani katika mapambano dhidi ya umaskini.

“Watanzania tuache tabia ya kukatishana tamaa, na nina fahamu katika kukatisha tamaa wapo wengi walioambiwa hawawezi kufanya kazi ya madini lakini yote hayo ni kwasababu ya watu kutaka kukatisha tama”, amesema Rais Magufuli.

Kitabu cha Dkt. Reginald Abraham Mengi kimezinduliwa rasmi leo na Rais Dkt. Magufuli akipatiwa nakala ya kitabu cha 'I Can, I Must, I Will- The Spirit of Success' pamoja na viongozi wengine wakuu waliohudhuria.

Dunia Imeisha! Mchungaji Akamatwa Baada ya Kukutwa Akiuza Tiketi za Kwenda Mbinguni

$
0
0
Dunia Imeisha! Mchungaji Akamatwa Baada ya Kukutwa Akiuza Tiketi za Kwenda Mbinguni
Mchungaji mmoja aliyefahamika kwa jina la Tito Wats, anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuwauzia watu tiketi alizodai ni za kuingilia Mbinguni

Anasema alitokewa na Yesu, akampa tiketi ili awagawie watu wenye dhambi ili siku ikifika waingilie kwenye mageti ya mbinguni.

Bei ya tiketi moja ni USD 500 zaidi ya Milioni moja ya Kitanzania.

Alipokamatwa amesema hajali, maana anajua anateswa kwa sababu ya kufanya kazi ya Mungu.

Watu wengi wanaandamana kupinga kukamatwa kwa mchungaji wao, kwa sababu hizo pesa wanazotoa ni zao, na kwa hiyari yao kwa ajili ya uzima wao.

Maelfu ya Wanawake na Watoto Waandamana Kumpinga Trump

$
0
0
Maelfu ya Wanawake na Watoto Waandamana Kumpinga Trump
Maelfu ya watu wameandamana miji mbalimbali nchini Marekani kupinga msimamo wa Rais Donald Trump wa kukabili wahamiaji nchini humo.

Msimamo wa Trump ulisababisha watoto kutenganishwa na wazazi wao na kuwekwa katika mahema na vizuizi mbalimbali.

Trump alituma ujumbe kupitia mtandao wa kijamii akisema kuwa sheria za uhamiaji za nchi hii, (Marekani) ni za kijinga kuliko zote duniani” na kwamba wahamiaji warejeshwe katika nchi zao bila ya kupewa fursa ya kupitia mchakato wa kisheria kabla ya kuondolewa nchini.

Muungano wa wanaharakati, yakiwemo makundi ambayo yaliandaa maandamano makubwa ya wanawake miaka miwili iliyopita, wamesaidia kuratibu maandamano zaidi ya 600 katika miji mikubwa na midogo nchini humo.

Miji ambayo watu walijitokeza kuandamana ni pamoja na  Hawaii na Puerto Rico, kadhalika katika daraja la kimataifa kati ya El Paso, Texas na Juarez, Mexico na  Antler, North Dakota.

Mjini Washington, mtoto wa kike wa miaka 12 aitwaye Leah, ambaye wazazi wake ni wahamiaji wasio na kibali cha kuishi Marekani, alitoa ujumbe wenye hisia kali kwa watoto wote wahamiaji.

“Nataka niwaambie watoto walioko mpakani na nchi nzima wasikate tamaa na wapiganie kuungana na familia zao. Sisi sote ni binadamu na tunastahili kupendwa na kusimamiwa! Sisi ni watoto!” aliuambia umati mkubwa uliokuwa ukimshangilia.

Mchungaji wa ngazi ya juu wa kanisa la The King United Church of Christ, Missouri, Traci Blackmon, aliuambia umati wa waandamanaji mjini Washington, “Tulikuwa katika njia hii siku za nyuma. Lazima tusisahau hili. Lazima tukumbuke siku zote hili si tu suala la sera salama ya uhamiaji bali ni itikadi ya ubinafsi.”

Kadhalika mjini Washington, Lin-Manuel Miranda, aliyebuni muziki wa “Hamilton” aliimba wimbo uliokuwa mahsusi kuwaliwaza wazazi ambao hawana uwezo wa kuwaimbia watoto wao ambao wamechukuliwa kwa nguvu kutoka mikononi mwao.

Waandamanaji huko New York, ambako ni nyumbani kwa Trump, walikuwa wakiimba “Hakuna chuki, hakuna vitisho, wahamiaji wanakaribishwa hapa Marekani!” huku kukiwa na jua kali walivuka daraja la Brooklyn kwenda katika moja ya uwanja wa kitongoji cha Brooklyn.

Wakati wakiandamana kuvuka daraja, wengi wao waliimba “Ni aibu.” Madereva wa magari walipiga honi kuunga mkono maandamano hayo.

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo

$
0
0
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live




Latest Images