Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Uwezi Amini Kuna Watu Wanakula Nyama ya Paka Kwa Kukosa Chakula cha Kupika

$
0
0
Hii Habari imeripotiwa Kutoka Kenya Mkoa wa Baringo na mtandao unaitwa Nairobi exposed , Inasemekana hali ya chakula huko katika Mkoa huo wa Baringo ni Mbaya Sana Kiasi kwamba wenyeji wa Mkoa huo hutegemea tu chakula cha Misaada na kwa vile chakula hicho hakina huhakika kuna muda huwa kinakosekana kabisa na kufikia wananchi kula nyama ya paka ambao huwafunga..
Tuwaombee Wenzetu Jamani.

Haya Ndio Maneno Aliyoyasema Diamond Kumtakia Siku ya Kuzaliwa Wema Sepetu

$
0
0
Laiti kama Maneno yangelikuwa ni sumu basi amini, Penzi letu lingekuwa lishazikwa na Kuoza...Maana sjui ni kipi hakijazungumzwa.....vya furaha, Chuki, shangwe, fitina, Vita, majungu, Misukosuko na mabalaa ya kila aina....lakini siku zote tumekuwa tukipendana na kuthaminiana kama tumeanzana jana, kwakuwa tulijua si kosa lao, ni hawajui tu niwapi tulipotokea...to the world, you may be one person...But to me, you are the world, My Beautiful World...na kama kukupenda ni uwendaazimu basi ni bora Nikabaki kwenye uchizi wangu kuliko kupata Ufahamu....i may not be physically present to stand by you while you cut your cake, but you’ll be in my thoughts the whole day! Happy birthday Darling....mmeo niko nahangaika, bt i will be coming home soon....Love you mama

Jaji Warioba Azidi Kushambuliwa..Afanaishwa na Maiti Iliyokufa Ikafufuka

$
0
0
Mbunge wa Mbinga Kusini, Kapteni John Komba, kwa mara nyingine amemshambulia aliyekuwa Mweyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, kwa ‘kuwaingilia’ na amemuomba Rais Jakaya Kikwete, amuite na kumkanya.

Katika mchango wake bungeni jana, Komba alianza kwa kusema, “Ninalo moja kubwa la kuchangia hapa, juzi nilizungumza habari hapa, jamani eh..., mtu akishazikwa, akifufuka ni tatizo kubwa katika kijiji kile, kazi haziendi…sasa jana (juzi) mmeona.?”

“Mimi nasema ukweli kabisa, huyu mzee ana nini, ana kitu gani na sisi, mbona anatuingilia sana,” alisema.

Komba alisema anamwomba Rais amwite Jaji Warioba na kumweleza hakumtuma kufanya hivyo isipokuwa kukusanya maoni basi, na inatosha hapo alipofikia.

Alisema, Jaji Warioba alipoteuliwa na Rais kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, kitu cha kwanza alinukuliwa akisema, “mmenichagua mimi na wenzangu sasa naomba mtuache msituingilie, na kweli hakuingiliwa na alifanya kazi na kumaliza vizuri bila kuingiliwa.”

“Lakini anatuingilia sisi, mkuki kwa nguruwe? Yeye amekuwa refarii? 

Anatufuatilia kila tunachofanya, sasa na yeye anasema atapambana na sisi, ataingia mitaani, anapambana na sisi, yeye upande mwingine na sisi upande mwingine, haya, njoo Warioba kwetu, tutaonana,” alisema.

Alisema Jaji Warioba anafanya kinyume na alivyoagizwa, kwani wakati wa kuunda tume yake, Rais alimwambia akusanye maoni basi, na amekusanya mengi.

Alisema Jaji Nyalali alipokuwa anakusanya maoni kuhusu mfumo wa demokrasia ya vyama vingi maoni yalionyesha asilimia 80 ya watu walipenda mfumo wa chama kimoja uendelee na asilimia 20 walipenda mfumo wa vyama vingi, jambo ambalo lilikuja kuheshimwa.

Hata hivyo, alisema anashangaa kuona kila wanachokifanya wajumbe wa BMK, Jaji Warioba kazi yake ni kuzungumzia tunu tu.

“Baba baba huyu kila kitu tunachokifanya yeye tunu tunu tunu tunu tunu tuuu basi,” alisema.

Kuhusu uhalali wa BMK, Komba alisema anashangaa kumwona Warioba ambaye ni Jaji anashindwa kuheshimu uamuzi wa majaji wenzake.

“Majaji wenzake wamesema bunge hili ni halali, sasa Warioba ni jaji gani ambaye hataki kuheshimu hata wenzake, jamani?

Shutuma za Komba dhidi ya Jaji Warioba zinafuatia ushiriki wake katika adhimisho la miaka 19 tangu kuanzishwa kwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) jijini Da es Saam juzi.

Adhimisho hilo pia lilitumika kumkumbuka muasisi wa LHRC, marehemu Dk. Sengondo Mvungi ambaye aliwahi kuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Akizungumzia adhimisho la juzi, Komba alisema wakati Jaji Warioba anazungumza kulikuwa na wazungu wengi, na akaonyesha wasiwasi wake kuwa huenda (Jaji Warioba) amepewa kitu na wazungu hao au ameahidiwa kitu hivyo akataka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kufuatilia.

Alisema jambo la ajabu ni kwamba, “baba huyu kila siku (anatuingilia) anatufuatilia kila tunachofanya.”

Alimtuhumu Jaji Warioba ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu kuwa hana maadili lakini Makamu Mwenyekiti wa BMK, Samia Hassan Suluhu, alimtaka Komba kufuta maneno aliyomtuhumu (Warioba) kuwa hana maadili, naye akasema, “hana maadili ya kujali wenzake kama wanafanya mambo mazuri, isipokuwa anayo maadili ya mambo mengine.”

Kwa upande wake Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo, alizungumza kwa kifupi kuwa anamshauri Jaji Warioba apumzike baada ya kufanya kazi nzuri ya kukusanya maoni ambayo ndiyo yametumika kama msingi wa Katiba.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi, Andrew Chenge alisema kuwa anawaheshimu baadhi ya viongozi wanaoendelea kutoa maoni yao ya kuiponda Rasimu ya Katiba inayopendekezwa hivyo hapendi kabisa kulumbana nao.

Aliwataka Watanzania kuzisoma Rasimu zote mbili (ile ya Jaji Warioba na inayopendekezwa na BMK) ili wapime kuona ni ipi iliyo bora.

Alisisitiza kuwa msingi wa Rasimu ya Katiba inayopendekezwa na BMK ni Rasimu ya Jaji Warioba hivyo madai ya kwamba maoni ya wananchi hayakuzingatiwa hayana ukweli wowote.

Source:Nipashe

Masanja Mkandamizaji Amzidi Utajiri Diamond Platnums

$
0
0
Wadau,
Hii kitu nimeisikia Clouds FM kwenye kipindi cha Gospel Trucks na Harris Kapiga!
Naomba kufahamu zaidi huyu mpendwa uwekezaji wake unakua kiasi gani na anatumia mbinu zipi kukuza kipato chake ili vijana tujifunze kutoka kwa vijana wenzetu. Nilifahamu ana kipato kizuri lakini amekuaje kiasi cha kumzidi Diamond? Mungu amkbarikie zaidi
Asante

Baada ya Wema Kuziponda Simu za Tecno na Huawei Sasa Zimekosa Soko Huko Madukani

$
0
0
Yaani jamani sio siri Wema ndio kila kitu kwa wadada walio wengi Dar es salaam baada ya kuziponda simu haina ya TECNO NA huawei WENGI sasa hawazitaki tena.

Nina ndugu yangu mmoja ana duka kariakoo ya simu ameshangazwa na maneno ya wateja hasa akina dada wakisema tupe simu aina yoyote lakini si alizoponda madam akauliza ndo nani mpaka iwe ivi ! maana angekuwa mmoja ungesema ana lake jambo!

Nimeamini ndo mana makampuni makubwa kama Airtel wanamtumia kwa sababu ana kitu cha ziada.

Ndani ya lisaa biashara inadoda ?

WEMA nitakukumbuka DAIMA no one!!! sijui ana kitu gani jamani nyota yake na kali sana!!

Birthday ya Wema Jana: Diamond Amnunulia Gari Jipya Kama Zawadi ya Birthday

$
0
0
Jumapili ya September 28 ilikuwa ni siku ya kuzaliwa mrembo aliyebeba taji la Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu. katika kusheherekea siku hiyo mpenzi wake Nasib Abdul a.k.a Diamond Platnumz alithibitisha kwa vitendo kuwa mapenzi yao bado yako imara, kwa kumnunulia zawadi ya gari jipya aina ya Nissan.

Picha ya gari hilo la rangi nyeusi iliambaatana na ujumbe mzuri ambao Diamond alimwandikia wema kupitia akaunti yake ya Instagram yenye followers 236,841.

“Nlitama nikupe vingi, wenda ingenisaidia kueleza ni kias gani napenda nikuone ukifurahi kwenye siku yako hii ya kuzaliwa…lakini tu sina uwezo huo mumy… tafadhari pokea kidogo hichi nlichojaaliwa leo….” Huku akionesha gari hilo pichani

Wiz Khalifa Azungumzia Kufumaniwa Na Amber Rose.

$
0
0
Rapper Wiz Khalifa amesema aliachana na mke wake Amber Rose kabla hajaomba talaka yake.
Wiz Khalifa amezungumza haya baada ya Amber kusema kuwa Wiz alikuwa na wanawake wengine, Wiz amesema ni kweli Amber alinikuta na mwanamke ndani ya nyumba saa nane usiku ila tulisha achana kwahiyo sikuwa namsaliti. Wiz aliendelea kusema kuwa amehamia nyumba yake nyingine ila Amber alizidi kumfuatilia. Wiz Khalifa bado anaamini Nick Cannon anamahusiano na Amber Rose.

Mtuhumiwa Auawa kwa Kuchomwa Moto Baada ya Kushindwa Kujieleza

$
0
0
MTU mmoja mwenye umri kati ya miaka 25 na 30 ambaye jina lake halifahamiki, ameuawa baada ya kushindwa kujieleza juu ya pikipiki ambayo yeye na mwenzake walikuwa wanajaribu kuiuza Chalinze.

Watu hao walifika Chalinze wakidai kutokea Gairo wakitaka kuuza pikipiki aina ya Toyo yenye namba za usajili T 336 BZC.

Lakini walipobanwa kuhusu kadi ya pikipiki walibabaika na hivyo kuanza kupigwa ambapo mmoja alitoroka na huyo mwingine kuuawa kwa kuchomwa moto baada ya kipigo.

Tukio hilo limethibitishwa na kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Athuman Mwambalaswa.

Kamanda huyo alisema kwamba tukio hilo lilitokea Septemba 25 mwaka huu, majira ya saa 1 asubuhi eneo la Pera Chalinze wilaya ya Bagamoyo.

Kamanda huyo aliwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na kuwataka kuwapeleka kwenye vyombo vya sheria, ikiwa ni pamoja na polisi ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Picha: Samaki Mwingine Aina ya Nyangumi Aonekana Ufukweni Pemba, Wananchi Wachangamkia Nyama

$
0
0
Wananchi wakikata minufo ya Nyangumi aliyeangukia katika ufukwe wa bahari ya Pemba maeneo ya shamiani, kama wanavyoonekana pichani wakiwa katika harakati hizo.

Wafanyakazi wa Uvuvi pemba wakimpima Nyangumi aliyeonekana Pemba akiwa ameanguka ufukwe wa bahari wa shamiani.

Jinsi ya Kusign Out Kwenye Google Play Kwa Wale Wenye Simu za Android Kama Unataka Kumuuzia Simu Mtu Mwingine

$
0
0
Kumekuwa na Malalamishi Mengi Sana kwenye Hizi Simu za Anroid Pale Unapotaka Kumuuzia ama Kumpa Simu Mtu Mwingine Kwani kutumia hizo simu ni Lazima Uwe Umesign in kwenye Google Play  kwa kutumia e-mail yako ya Gmail ..Sasa kuna kitu kimoja ambacho kinawashinda wengi ni Kusign Out ama kutoka kwenye hiyo Google Play Pale unapokuwa Unataka Kumpa Mtu Mwingine Simu ili asiweze kuona mambo yako, Hii Imepelekea Siri za Watu wengi Kuvuja ikiwemo message za Whats app na E-mail ulizozifanyia Back up kusomwa na watu wengine

Haya Hizi ni Steps Ambazo Unaweza Fanya..Sorry Zipo Kwenye Kidhungu:

Sign Out Using Your Android Settings:

Generally there is no place found in Google Play Store to sign out while using on Android. So, by using this method you can simply sign out from Google Play Store in your Android device. You can simply do it by removing your existing account from Google Play. Read the following steps to know how –

Open Settings in your Android Device and Navigate to Accounts & Sync. Now Tap on the account you want to remove


When you tap on your Google account, you’ll see a screen for Data & Synchronization. Here on the right top corner, you’ll see a drop down button as shown in Picture below. So, tap on it and select Remove account.
That’s all! After removing your account from here, you will be unable to log in to your Google account. Further if you want to log in to your account for any reason like to install any app, then you can again add the same account and then you can simply sing in

Gari Mpya Toyota Porte ya 2005 Inauzwa Kwa Bei Poa, Ndio Imefika Haijatumika Tanzania

$
0
0
Toyota Porte 2005
1290cc
Vvti engine
88000km
Metallic black
Just arrived From Japan
Call/whatsapp +255768570703

Rose Ndauka na Mchumba Wake Malick Waachana Baada ya Kuishi Kama Mume na Mke Kwa Miaka Mitatu

$
0
0
Stori: Imelda Mtema
Ooh…nooo! Wachumba wa muda mrefu, staa wa sinema za Kibongo, Rose Donatus Ndauka na Malick Bandawe ambao maisha yao ya kimapenzi yamekuwa yakitawaliwa na msuguano wa chini kwa chini, hatimaye wameachana, Ijumaa Wikienda linakupa mkanda mzima.

TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini na cha uhakika kimemwaga data kwamba wachumba hao ambao walivalishana pete kwa mbwembwe miaka mitatu iliyopita huku wakipika na kupakua lakini wamekuwa katika mzozo wa muda mrefu wa kifamilia, ambapo mara kadhaa wameripotiwa kuchapana wameachana.
“Unajua hawa jamaa wamekuwa na maisha ya kutoaminiana sana, nadhani wivu ndiyo sababu kubwa, lakini naona safari hii hali imekuwa mbaya zaidi kwa sababu Rose  ameamua kubeba kilicho chake na kuondoka kwa mwenzake,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Hiyo ndiyo habari ya mjini, bidada karudi kwao (Kigogo, Dar) na mwanaye. Ilikuwa ni lazima ndoa isiwepo kwani licha ya kupata mtoto hakukuwa na furaha hata kidogo.”

TATIZO NI NINI?
Ingawa chanzo hicho hakikuweza kuingia kwa undani kuhusu tatizo hasa lililotokea safari hii, lakini kilibainisha kwamba kabla ya tukio la sasa, mzozo mwingine mkubwa uliibuka kati yao.
“Kuna kipindi hali ilikuwa tete sana, Malick akaamua kuchukua mabegi yake na kutokomea kusikojulikana ambako alikaa kwa muda wa kama wiki mbili.

“Haikujulikana alikuwa wapi kwa muda wote huo, lakini baadaye tukamuona jamaa anarudi na maisha yao yakaendelea.

NDOTO YA NDOA YAYEYUKA
“Lakini wakati bado mambo hayajatulia, kumeibuka tatizo lingine kubwa ambalo limesababisha Rose kuamua kuondoka huku ndoto ya ndoa ikiyeyuka,” kilisema chanzo hicho.

VIPI KUHUSU MTOTO?
Katika mtafaruku huo, Malick alikataa katakata mtoto wake kuondoka na mama yake, lakini kutokana na umri wa mwaka mmoja wa kijana wao huyo, Naveen, alilazimika kuondoka na mama yake kwa vile bado ananyonya.

Rose, mmoja kati ya waigizaji warembo wa filamu Bongo, inasemekana kwamba yupo nyumbani kwa wazazi wake, Kigogo kutoka kwa mchumba wake, anayeishi Tandale, Tanesco jijini Dar.

IJUMAA WIKIENDA MZIGONI
Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’ huo, Ijumaa Wikienda lilizama mzigoni ambapo stepu ya kwanza ilikuwa ni nyumbani walikokuwa wakiishi wapenzi ambapo hawakuwepo.

JIRANI ANASEMAJE?
Akizungumza na gazeti hili juu ya kuondoka kwa Rose nyumbani hapo, mmoja wa majirani zake aliyejitambulisha kwa jina moja la Sudi alikuwa na haya ya kusema:
“Rose Ndauka ana muda hatumuoni kama miezi sasa lakini ‘mista’ tunamuonaona labda kama amehama ‘but’ sina uhakika sana.”

ROSE VIPI?
Katika kutafuta ukweli alitafutwa Rose kila kona baada ya simu yake ya kiganjani kutokuwa hewani lakini jitihada ziligonga mwamba hivyo zinaendelea.

Mchumba mtu, Malick alipoulizwa juu ya ukweli wa sakata hilo, alikiri kutokea na kwamba baada ya jitihada zake nyingi za kulinusuru penzi lao kushindikana, amekubali matokeo.
“Nimejitahidi sana kumwelewesha Rose ili apate kunielewa, ajue namna ya maisha yalivyo, lakini imekuwa ni kama kutwanga maji kwenye kinu. Nimekubali yaishe.

“Kinachonisikitisha sana ni kuona kuwa mwanangu anakwenda kulelewa na mwanaume mwingine, inauma sana tena sana,” alisema bila kufafanua maana ya kauli hiyo.
Katika uchumba wao mrefu, Rose na Malick wamejaliwa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Naveen.

Picha za Model Maarufu Bongo Calisa Akiwa na Miss Sinza Wakiwa Kitandani zavuja Mitandaoni

$
0
0
Stori: Gladness Mallya
KABAANG! Miss Sinza 2001 na aliyekuwa pia mshiriki wa Miss Tanzania 2011, Husna Maulid amenaswa akiwa kimalovee laivu kitandani na modo maarufu Bongo aliyejulikana kwa jina moja la Calisa.

Picha hizo ambazo zinamuonesha Husna na Calisa wakiwa wamekumbatiana zimevuja kiitelejensia na kumfikia paparazi wetu kisha akawauliza kulikoni?  Ni wapenzi?

“Siyo kweli sina uhusiano na Calisa, sina boyfriend na sitaki mwanaume kwa sasa, Calisa ni rafiki yangu tu,” alijibu Husna huku Calisa akijibu:

“He hebu ngoja kwanza nitakupigia, hizo picha kaleta nani?”
GPL

Ray C sasa Ataka Kuolewa na Mzee, Ataki Viserengeti Boys

$
0
0
Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
Utu uzima dawa! Staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amefunguka kuwa kwa sasa hana mpenzi wala hajapata mtu wa kumuoa ila anataka kuolewa na mzee atakayeweza kumlea.

Akizugumza na wanahabari wetu kwenye mgahawa wake wa Ray C uliopo Mwananyamala, Dar, mwanadada huyo alisema yeye kama mwanamke anatamani kuolewa na kupata mtoto si na ‘serengeti boy’ bali mzee.

Aliendelea kutiririka kwamba akikosa wa kumuoa atatafuta mwanaume atamlipa kwa ajili ya kuzaa naye tu lakini ni pale atakapokuwa anaweza kulea  mwenyewe.

Ray C aliongeza kuwa, kwa sasa anatafuta wadhamini kwa ajili ya kuendesha taasisi yake ya Ray C Foundation kwani amefanikiwa kuwasaidia watu wengi kupata kazi na kuachana na dawa za kulevya.
GPL

Gari Mpya Aina ya Toyota Passo 2005 Inauzwa Kwa Bei Nafuu, Haijatumika Bongo Ndio Imefika Kutoka Japan

$
0
0



Toyota passo 2005
990cc very economy
Vvti engine
Metallic light blue
Just arrived
Call/whatsapp +255768570703

Skirt Fupi Maofisini Zinapunguza Ufanisi wa Kazi kwa Wanaume

$
0
0
Moja kwa moja nianze kuwaomba dada zangu ambao wanatuvalia vimini ofisini punguzeni au acheni jamani wengine tuna mioyo ya udongo kwa sababu mnapofanya kazi na sisi halafu karibia mapaja yote yapo nje jamani mnatufanya tufanye kazi ambazo hazina ufanisi maana mnatunyima concentration jamani vaeni basi sketi ndefu au kusema sketi fupi inaendana na mambo ya ofisini.
Jamani acheni wengine jamani tuna mioyo ya petroli.

Muuguzi Anusurika Kushambuliwa Chumba cha Operesheni Baada ya Kumzalisha Mwanamke Watoto Wakiwa Wamekufa

$
0
0
Muuguzi wa Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga, Yasinta Thomas, amenusurika kushambuliwa na wananchi wakati akimhudumia binti wa miaka 15 (jina linahifadhiwa), aliyekuwa mjamzito wa miezi sita na kisha kujifungua kabla ya muda watoto mapacha waliokufa.

Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Fredrick Mlekwa, jana alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 12 jioni wakati binti huyo alipofikishwa hospitali hapo akitokea katika Kituo cha Afya cha Kambarage, mjini Shinyanga.

“Tulimfanyia uchunguzi na kugundua alikuwa na mimba ya mapacha lakini wakiwa tayari wamefia tumboni, hivyo muuguzi wa zamu katika wodi ya wazazi alianza kumhudumia ili kuwatoa watoto hao tumboni” alisema.

Alisema wakati muuguzi wa zamu akiendelea na zoezi hilo, mama mzazi wa binti huyo aliingia chumba cha kuzalishia na kumkuta mwanae ametolewa viumbe mfu na kuanza kupiga kelele na kumfokea muuguzi huyo kwa matusi hali iliyosababisha vurugu na wananchi kujaa kutaka kumshambulia muuguzi huyo kwa madai amesababisha vifo vya mapacha hao.

Mlekwa alisema watoto hao walikuwa na uzito wa gramu 200 na 500 na ujauzito huo wa miezi sita uliharibika mapema na kulazimika kuwatoa watoto hao kwa upasuaji mdogo ili kuokoa maisha ya binti huyo.

Mama mzazi wa binti huyo, Mwanahamisi Juma, mkazi wa mtaa wa Mshikamano mjini Shinyanga, alisema mwanaye ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Mwasele, mjini humo, alishindwa kuhudumiwa kutokana na muuguzi huyo kuonekana bize akichati na simu.

“Nilipoingia katika chumba cha kuzalishia nilimkuta mwanangu anajifungua watoto hao huku muuguzi akichati na simu na kutompa msaada wowote unaohitajika, hivyo kuamua kumfokea kwa hasira,” alisema Mwanahamisi.

Hata hivyo, muuguzi huyo, Yasinta, alisema wakati binti huyo anajifungua watoto walikuwa tayari wamekufa hivyo aliamua kuwapigia wenzake simu ili wamsaidie na ghafla alivamiwa na mama huyo na kuanza kuporomoshewa matusi hadi Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo alipoingilia kati na kuokoa.

Tuzo aliyojipa H.Baba ‘Mtumbuizaji Bora’ ni diss kwa Diamond Platnumz?

$
0
0
Pamoja na H.Baba kuwahi kudai kuwa hana tena beef na Diamond Platnumz, kuna kila ishara kuwa mafahari hao wawili bado hawawezi kukaa kwenye zizi moja. Kama umesahau, wacha tukukumbushe; Wasanii hao wawili wamewahi kuingia kwenye beef zito baada ya H.Baba kumtuhumu Diamond amemuibia wimbo wake ‘Sitaki Kulewa’.

So, Jumamosi iliyopita, H.Baba na mke wake, Flora Mvungi waliandaa tuzo zao wenyewe ambazo tofauti na vile wengi wanavyodhani, tuzo hizo zilikuwa serious kabisa kwa kuhusisha watu muhimu kwenye tasnia ya burudani Tanzania, waandishi wa habari na pia kutolewa trophy na fedha taslimu kwa washindi.

H.Baba alijipa tuzo ya ‘Mtumbuizaji Bora’ na tunafahamu kuwa Diamond Platnumz ni mshindi wa kipengele cha ‘Mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki’ kwenye tuzo za KTMA 2013. H.Baba anataka title yake kutoka kwa Diamond?

Haya ni maneno aliyosema wakati akipokea tuzo hiyo:

Tuzo hii hapa ni ya mtumbuizaji bora Tanzania,” alisema muimbaji huyo. “Mimi nina tuzo ya East Africa mtumbuizaji bora, Tanzania sina hata tuzo moja kwa sababu ya nini nimeshatangaza naanzisha hii tuzo kwa akili timamu na wala sivuti bangi. Mimi sivuti sigara wala sinywi pombe, kama kuna msanii anaona hii tuzo sio halali yangu mimi ajitokeze. Promota yoyote ajitokeze huyo msanii alipwe pesa mimi nita- perform bure na awadhihirishie watanzania kwamba yeye ni mkali ya stage Tanzania.

Kama ananizidi mimi, promota amlipe yeye ila mimi kama H.Baba nitaperform bure na nitakuja peke yangu na yeye inatakiwa aje peke yake. Kwa sababu kuna Kiswahili fasaha ambacho kinakosewa kuna neno linaitwa mtumbuizaji bora na kuna watumbuizaji bora. Mimi ni mtumbuizaji bora, wengine ni watumbuizaji bora. Kwanini nasema watumbuizaji bora kwa sababu msanii yeye mwenyewe hajiwezi mpaka awe na watu wakucheza naye, ila mimi binafsi najiweza kwa sababu mimi mwenyewe ninaweza fanya kazi na ikaeleweka.

Ndiyo maana ya hii tuzo niliyopata leo. Ninaowatambua walikuwa watumbuizaji na ninawaheshimu mpaka leo nawataja watu wawili, kuna Mr Nice kuna TID (Top In Dar ) hao ndo watu wanaweza kusimama kwenye show na kuburudisha na watu wakasema asante.

TBS: Wananchi Acheni Kununua Nguo za Mitumba

$
0
0
Shirika la Viwango (TBS) limewataka wananchi kutonunua nguo za ndani za mtumba ili kuua soko la bidhaa hizo zenye athari kiafya.

Kaimu mkurugenzi anayehusika na udhibiti ubora wa TBS, Mary Meela alisema nguo hizo ni hatari kwani zinaweza kueneza magonjwa mbalimbali hasa ya ngozi.

Alisema lengo la ombi hilo ni kukomesha uuzaji wa nguo hizo ambazo zinaweza kusababisha maambukizi kutoka kwa aliyekuwa anavaa nguo hiyo kwenda kwa mtu wa pili.

Meela alisema shirika lake linashindwa kukomesha biashara hiyo kwa sababu halijapewa nguvu za kisheria kukataza watu kufanya biashara hiyo kama ilivyo Zanzibar, hivyo amewataka wananchi kutambua madhara hayo na kuacha kununua.

“Nguo za ndani zina bei ndogo hata mtu wa chini anaweza kumudu. Sioni sababu ya mtu kwenda kununua za mtumba,” alisema.

Tibaigana Aibuka na Kusema 'Wapinzani Wana Haki kuandamana'

$
0
0
Katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake Buganguzi wilayani Muleba, Kamishna Tibaigana alisema suala la maandamano halikumsumbua kwa kuwa alielewa kuwa sheria inayaruhusu, hivyo alichokuwa akifanya ni kuwaita viongozi wa vyama vinavyotaka kuandamana na kufanya nao makubaliano ya namna maandamano hayo yanavyopaswa yafanywe kabla ya kuyaruhusu.

“Pengine hiyo ndiyo sababu sikuwahi kushambuliwa kwa maneno ya kejeli au matusi na wanasiasa kwa kuwa sikuwahi kuzuia maandamano yao bila sababu na hata kama kulikuwa na sababu niliwaita na kuwaeleza na tulikubaliana.

“Kikubwa ni kujenga tabia ya kuwaita viongozi wa waandamanaji na kujadiliana nao, vinginevyo wanaweza pia hata kukufikisha mahakamani wakipinga kuzuiwa maandamano yao,” alisema Tibaigana ambaye alikumbana na sakata la kudai maandamano wakati akiwa Kamanda kwenye mikoa ya Tanga, Arusha na Dar es Salaam.

“Nilikuwa nawaita viongozi nakaa nao tunakubaliana. Hata kama ningeambiwa na kiongozi gani nisitoe kibali, kama hakuna sababu za kweli, nilikataa kwa kuwa kisheria mimi ndiye nawajibika kama vyama vikishtaki. Ili uzuie maandamano unapaswa kuwa na sababu za msingi ambazo ukiwaeleza waandamanaji wanakuelewa.”
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images