Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live

IGP Sirro Kafanya mabadiliko kwa makamanda wa polisi kwa baadhi ya mikoa, RPC Wa Mbeya Kaondolewa

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amefanya mabadiliko ya makamanda wa polisi kwa baadhi ya mikoa.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Julai 3, 2018  iliyosainiwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa, inasema mabadiliko hayo yanalenga kuongeza juhudi za kuzuia ajali zilizotokea mara kwa mara katika baadhi ya mikoa.

Katika mabadiliko hayo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Deusdedit Nsimeki aliyekuwa makao makuu ya upelelezi Dar es Salaam anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi (RPC) Mkoa wa Simiyu.

Aliyekuwa RPC Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ulrich Matei anakwenda kuwa RPC Mkoa wa Mbeya.

Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kaimu RPC Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi, Mussa Taibu amehamishiwa makao makuu ya polisi Dar es Salaam.

Aliyekuwa RPC Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Wilbroad Mutafungwa anakwenda kuwa RPC Mkoa wa Morogoro, nafasi yake ikichukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi, Emmanuel Nley kutoka makao makuu ya polisi Dar es Salaam.

Wengine waliohusika na mabadiliko hayo ni aliyekuwa Ofisa Mnadhimu Mkoa wa Geita Kamishna Msaidizi wa Polisi, Stanley Kulyamo anayekwenda kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Tazara.

IGP Sirro amewataka makamanda wa polisi wa mikoa nchini, kuendelea kuwajibika ipasavyo katika kuhakikisha ajali hazitokei katika maeneo yao na kuwachukulia hatua kali madereva watakaosababisha ajali kwa uzembe.


Kutana na Dr Mabula Kukutibu Matatizo ya Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo

$
0
0

TUNATIBU NA KUPONESHA KABISA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME UUME MDOGO BUSHA BILA KUPASUA PRESHA VIDONDA VYA TUMBO :

Asilimia kubwa ya wanadamu wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali na wapo waliongahika sehemu mbalimbali bira MAFANIKIO MABULA CLINIC ni kituo cha tiba asilia kilichopo mbagara zakhemu njia kuu ya JESHINI JE HUNAUPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME AU UUME WAKO MDOGO NA MWEMBAMBA?


MAPRO PAWER NO 2 ndio Tiba kwa sasa utibu matatizo matatu kwa pamoja itakufanya uchelewe kufika kilekeni dikika 15-20 kwa tendo la kwanza 2 uimalisha misuli iliyoregea na kusinyaa hasa kwa wale walio asirika na upigaji punyeto 3 itakufanya upate hamu ya kurudia tendo zaidi ya Mara tatu.

KWA NINI UJIONE MPWEKE PALE UKUTANAPO NA MPENZI AU MKE WAKO kisa unawai kukojoa au unakomea bao moja tu na huku dawa zipo

MAKAKANUA mix ni dawa iliyochanganywa na miti Shamba 9 na Kuwa na uwezo wa kuongeza uume saizi upendayo inchi 5-8 Kwa Urefu na unene sentimita 1-5 dawa hizi hazina madhara yoyote kwa mtumiaji ata wazee wenye umri mkubwa wanapona.

Zipo dawa za mvuto wa mpenzi mme au mke Kwa masaa matatu tu na kukupigia simu yeye mwenyewe mvuto wa biashara kutengeneza mwonekano mzuri wa mwili kwa wanawake yani shepu tunatibu ngiri miguu mgongo na kiuno kuumwa kupunguza kitambi minyama uzembe matiti na mwili mkubwa

TIBA NA USHAULI MUONE DR MABULA AU PIGA SIMU NO 0752348593 UDUMA ZANGU UTAZIPATA POPOTE ULIPO KAMA UWEZI KUFIKA OFISINI

TFF yadaiwa Milioni 50

$
0
0
Kampuni ya Ulinzi inayojulikana kwa jina la 'Kiwango Security' imewaondoa wafanyakazi wake wote katika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa madai ya kuwa haijalipwa fedha zake.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Uendeshaji wa Kampuni hiyo, Sunday Marwa, amefunguka na kusema wanaidai TFF kiasi cha fedha zaidi ya milioni 50 za kitanzania ambazo zinapaswa kulipwa ili huduma ya walinzi kufanya kazi iendelee.

Marwa amesema wameamua kufanya hivyo kwa maana deni lingekuwa kubwa na hivyo imewabidi wafanye hivyo ili lisizidi kuongezeka.
“Kampuni imefikia hatua ya kufanya maamuzi hayo kutokana na walinzi wetu kuzidi kufanya kazi katika ofisi ambazo haziwalipi chochote, jambo ambalo sisi kama ofisi tumeona ni kuwatesa bure wafanyakazi wetu”, amesema Marwa.

Mbali na ofisi hizo, Marwa amesema Kiwango Security iliingia mikataba miwili na TFF ambapo walinzi walikuwa wanazilinda ofisi za TFF pamoja na kwenye makazi ya Rais wa Shirikisho hilo Wallace Karia.

Www.eatv.tv imeutafuta uongozi wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF), ili kujibu tuhuma hizo lakini hawakuonesha ushirikiano.

Video: Matokeo Ya Vipimo Vya Ukimwi Vya Rayvanny

$
0
0
Baada ya Rayvanny msanii kutoka wasafi classic inayomilikiwa na Diamond Platinumz a.k.a Simba kupima HIV maambukizi ya virusi vya ukimwi na kuweka hadharani matokeo huku akiwasii wasanii wenzake wa Wasafi sanasana akionyesha msisitizo kwa Harmonize na Richmavoko. Rayvanny aachia video online instagram kuonyesha wafuasi wake kuwa mambo ni safi kabisa.

VIDEO:

Apandishwa kizimbani kwa kumkashifu Rais Magufuli. Alisema 'Rais kitu gani bwana!'

$
0
0
Misungwi. Mkazi wa Wilaya ya Ngara, Kagera Justin Emmanuel (31) amefikishwa Mahakama ya Wilaya Misungwi mkoani Mwanza, kwa tuhuma ya kutoa lugha chafu dhidi ya Rais John Magufuli.

Mwendesha mashtaka wa polisi Ramsoney Sarehe alisoma hati ya mashtaka mbele ya ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Erick Marley leo Julai 3.

Sarehe amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha sheria namba 89 (1) ya mwaka 2002.

Amesema mshtakiwa alitoa lugha ya kumdhihaki Rais Juni 25 katika Kivuko cha Kigongo saa 10:00 jioni kwa kutamka maneno ya “Rais kitu gani bwana”.

Hata hivyo mshtakiwa alikana kosa hilo na hakimu aliahirisha shauri hilo hadi Julai 26 itakapotajwa tena mahakamani.

Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kuwa na mdhamini mmoja aliyewasilisha bondi ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh500, 000.

Chanzo: Mwananchi

Rais wa Ufaransa Anatarajiwa Kutembelea Casino

$
0
0
Rais wa Ufaransa Anatarajiwa Kutembelea Casino
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa kutembelea ukumbi wa starehe mjini Lagos Nigeria unaomilikiwa na nguli wa muziki ( Afro beat)   kutoka Nigeria, Fela Kuti na kuwa Rais wa kwanza kuingia katika ukumbi huo maarufu kwa watumiaji wa marijuana, wacheza uchi na kamari.

Rais Macron baada ya mkutano wa Umoja wa Afrika uliofanyika jumapili katika mji mkuu wa Mauritania (Nouakchott ) anatarajiwa  kuelekea     Abuja Nigeria ambapo atakutana na  mwenyeji wake Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari na kuzungumzia suala la usalama na mpango wa kupambana na ugaidi.

Aidha Rais Emmanuel Macron baada ya mazungumzo na mwenyeji  wake Rais Buhari atahudhuria mkutano wa wanamitindo kutoka maeneo tofauti  Afrika na waigizaji wa Nollywood utakaofanyika katika ukumbi huo wa starehe (Casino).

Mwakilishi wa taasisi ya utamaduni mjini Lagos Ibrahim Tcha-Tchere amesema kuwa  lengo kuu la Rais Macron ni mpango wa kuanzisha mahusiano mapya kati ya Ufaransa na Nigeria kuhusu utamaduni.

Mahakama Yatengua na Kufuta Amri ya Kumkamata na Kumfunga Babu Tale

$
0
0
Mahakama Yatengua na Kufuta Amri ya Kumkamata na Kumfunga Babu Tale
Mahakama Kuu imetengua na kufuta amri ya kuwakamata na kuwafunga gerezani wakurugenzi wa Tip Top Connection Company Limited, Hamis Shaban Taletale maarufu Babu Tale na ndugu yake Idd.

Uamuzi wa kufuta amri hiyo ulitolewa juzi na Jaji Edson Mkasimongwa baada ya kujiridhisha kuwa haikuwa halali kutokana na mamlaka iliyoitoa kutokuwa na uwezo wa kufanya hivyo.

Februari 16 naibu msajili wa mahakama hiyo, Wilbard Mashauri aliamuru Babu Tale na nduguye Idd wakamatwe na kupelekwa kifungoni katika Gereza la Ukonga kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya mahakama na Aprili 4 alitoa na kusaini hati ya kuwakamata.

Katika hukumu iliyotolewa na Jaji Agustine Shangwa Februari 18, 2016 ndugu hao waliamriwa kumlipa fidia ya Sh250 milioni, mhadhiri wa dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kutokana na makosa ya kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake.

TRA Yaweka Wazi Kuhusu Kulipia Kodi Mtandao wa Whatsapp

$
0
0
TRA Yaweka Wazi Kuhusu Kulipia Kodi Mtandao wa Whatsapp
Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), imekanusha taarifa zinasombazwa kupitia mitandao ya kijamii zilizodai kuwa mtandao wa ‘whatsapp’ utaanza kulipiwa kuanzia Julai 10, mwaka huu.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Mamlaka ya Mapato (TRA), Richard Kayombo imesema kuwa taarifa hizo zinazodai kuwa mtandao huo utaanza kulipiwa kiasi cha shilingi elfu 15 kuanzia Julai 10 hazina ukweli wowote.

“Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), inapenda kuufahamisha Umma kuwa, taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zikidai kwamba Mtanzania yeyote anayetumia whatsapp atatakiwa kulipia shilingi 15,000/= kuanzia tarehe 10 mwezi huu ni za uongo”, imesema taarifa.

Mamlaka hiyo imetoa wito kwa watumiaji wa mtandao ya kijamii kuwa makini na kupuuza taarifa hizo kwakuwa hazina ukweli wowote.

Kigwangalla Atoa Siku 90 Kufanyika kwa Sensa ya Mamba

$
0
0
Kigwangalla Atoa Siku 90 Kufanyika kwa Sensa ya Mamba
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk.  Hamisi Kigwangalla, ametoa miezi mitatu kwa Taasisi ya utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kufanya utafiti na sensa ya mamba katika ziwa Rukwa ili kubaini idadi yake.

Alisema baada ya utafiti huo ataishauri serikali namna ya kudhibiti madhara yanayosababishwa na mamba hao kwa wananchi hususan wa jimbo la Songwe, ikiwamo kuwavuna kama idadi yao itabainika kuwa kubwa.

Dk. Kigwangalla alitoa agizo hilo jana katika kijiji cha Maleza Kata ya Mbangala Wilaya ya Songwe mkoani Songwe alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo kutatua mgogoro uliopo baina ya wananchi na mamba wa Ziwa Rukwa.

“Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori ambayo ipo chini ya wizara yangu, nawaagiza wafike hapa mara moja na ndani ya miezi mitatu wanipe majibu nini kifanyike kupunguza madhara yanayotokana na mamba kwenye Ziwa Rukwa, wafanye sensa watuambie kuna mamba wangapi, lakini pia watushauri nini tufanye ili kudhibiti mamba hao wasiendelee kusababisha athari kubwa kwenye maisha ya watu wanaoishi jirani, lakini pia wanaoutumia ziwa.

“Kwa sababu madhara yanaweza yakawa mengi, inawezekana mamba wameshakuwa wengi na samaki wamebaki wachache, hivyo hata mamba nao mwishowe wataanza kufa ama wataanza kutafuta chanzo kingine cha chakula pengine ndio maana wameanza kutafuta binadamu anayekwenda ziwani kwa sababu sasa wanakuwa na njaa, inabidi wasogee ufukweni wawinde chochote kinachosogea karibu na maji,” alifafanua Dk. Kigwangalla.

Dk. Kigwangalla alitoa agizo hilo kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa kwake na Mbunge wa Songwe, Philipo Mulugo, ambaye alisema kumekuwapo na matukio mengi ya mamba kushambulia na kuua wananchi wa vijiji jirani wanaofuata huduma mwambao wa Ziwa Rukwa.

Katika hatua nyingine, Dk. Kigwangalla ametoa miezi mitatu kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuandaa mpango wa kitaifa kwa kila wilaya na vijiji nchini utakaoweka utaratibu maalum wa namna na sehemu wananchi watakayopata huduma ya kuni na mkaa.

“Utaratibu uwekwe na muuweke nchi nzima, kila wilaya, kila kata, kila kijiji uwekwe utaratibu wananchi watapata wapi mkaa, watapata wapi kuni, kibali cha kuvuna kitapatikana wapi, utaratibu uwe wazi, sio kusubiri kwenye mageti unakamata, hapana weka utaratibu kwanza, ukishaweka utaratibu atakayevunja sheria hata ukimkamata ukimpeleka polisi utakuwa umemrahisishia OCD kazi,” alisema.

Jike Shupa'Waliotembea na Mimi Wapime Ukimwi'

$
0
0

VUTA picha ‘umetembea’ na mwanamke halafu ghafla anakwamba ukapime Ukimwi, utakuwa kwenye hali gani? Ndivyo alivyoibua mshtuko msanii wa filamu za Kibongo, Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ baada ya kuibuka na kusema; “wanaume niliotembea nao kimapenzi zamani na sasa, wakapime Ukimwi ili kujua afya zao.”

NI WIKI ILIYOPITA

Kauli hiyo aliitoa msanii huyo mara baada ya kuachia picha yake ya nusu utupu katika mtandao wa Instagram inayoonyesha vipele na makovu maeneo ya mapaja, mwishoni mwa wiki iliyopita.



YAIBUA GUMZO

Dakika chache baada ya kuweka picha hiyo, gumzo la aina yake liliibuliwa na wafuasi wa mtandao huo huku kila mtu akieleza lake.

Kuna ambao walimchamba kwa kumwambia anajidhalilisha kwa kuweka picha za nusu utupu wakati anajua kabisa sheria zinakataza.

“Huyu naye vipi? Hata kama ndio kutafuta umaarufu sio kwa staili hii, anajitafutia tu matatizo maana siku hizi sheria zinawabana sana wasanii wanaoendekeza kujiachia utupu,” alichangia mdau mmoja mtandaoni.


WENGINE WACHOMEKEA YA UKIMWI

Kwenye wengi huwa hakukosi jambo, mbali na waliomtukana Jike Shupa na kusema amejidhalilisha, wapo wengine waliojiongeza kwa kutazama picha hiyo kwa jicho la tatu na kumhusisha msanii huyo na ugonjwa wa Ukimwi.

“Hebu angalia hivi vipele vilivyomtoka huyu atakuwa na ngoma tu si bure,” alichangia mdau mwingine mtandaoni huku akiungwa mkono na wafuasi wengine kibao.

Kuanzia hapo, upepo ukageuka kutoka kwenye ishu ya picha za utupu na moto wa Ukimwi ukawaka kama vile wa petroli.



VIGOGO, MASTAA MATUMBO JOTO

Kutokana na mjadala huo kuwa mkubwa mtandaoni, waliibuka wachangiaji mbalimbali walioeleza jinsi mastaa na vigogo mbalimbali ambao wanaaminika wamewahi kubanjuka na mrembo huyo jinsi walivyopata presha.

“Jamani nyinyi mnachangia lakini kuna mastaa na vigogo kibao ambao wamewahi kutembea naye humu sasa hivi matumbo joto, kama yule (anamtaja jina) na yule (anataja jina la msanii mkubwa) hali ni mbaya sasa hivi nyie mnashabikia tu humu,” alichangia mchangiaji mmoja mtandaoni.



HUYU HAPA JIKE SHUPA

Mjadala huo umelifanya gazeti hili limtafute msanii huyo ili kujua siri ya kuweka picha hiyo iliyozua mjadala mtandaoni na alipopatikana live, akafunguka kama ifuatavyo:

Ijumaa Wikienda: Habari za siku Jike Shupa, kuna hii picha yako iko mtandaoni, unaonekana uko nusu utupu mapaja yalionekana yana vipele vingi na makovu. Picha hiyo imezua mjadala sana. Kwa nini uliamua kuiweka hadharani?


Jike Shupa: Habari yangu ni nzuri. Kuhusu picha niliamua kuiweka mwenyewe na wala haina tatizo.

Ijumaa Wikienda: Unasema haina shida, lakini mjadala unaoendelea mtandaoni ni kwamba wewe ni mgonjwa sijui wa…

Jike Shupa: Sasa watu wameona tu hilo, kuna jambo kubwa zaidi ya picha hiyo. Hiyo picha ni trela. Ujumbe wangu ni kwamba wote waliotembea na mimi wakapime maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Ijumaa Wikienda: Kwa kauli hiyo unamaanisha nini?



Jike Shupa Namaanisha kwamba si hawa watu wanaishangaa hiyo picha yenye vipele na makovu? Nataka wote waliokuwa na waliotembea na mimi wakapime Ukimwi.

Ijumaa Wikienda: Lakini umeyachukualiaje maoni ya watu ya mtandaoni, hasa kuhusu suala la kujidhalilisha?

Jike Shupa: Sioni tatizo.

Wakati mwandishi wa habari hii anazungumza naye, Jike Shupa hakuonekana kuwa mgonjwa, ila mwili wake uliojaa vipele na makovu ulionekana dhahiri maeneo ya mikononi na miguuni.


KUMBUKUMBU

Mbali na picha hiyo ya wiki iliyopita, Jike Shupa amewahi pia kutupia picha nyingine ya akiwa ameanika ‘ikulu’ yake hadharani lakini kama hiyo haitoshi, amekuwa akinaswa kwenye matukio maovu likiwemo lile la kudaiwa kuwauza mastaa wenzake.

STORI: Imelda Mtema, DAR

Madereva wawili wa mabasi ya Mbunge Msukuma watiwa mbaroni

$
0
0


Jeshi la polisi mkoani Geita linawashikilia madereva wawili wa kampuni ya mabasi ya King Msukuma kwa makosa ya kuendesha magari yakiwa mabovu na kuhatarisha usalama wa abiria waliokuwa wakisafiri kutoka Mwanza kwenda Kagera na jingine likitokea Kagera kwenda Mwanza.

Ubovu wa magari hayo ulisababisha abiria 120 kulazimika kulala kwenye kituo kikuu cha polisi Geita hadi walipoletewa usafiri mwingine jana asubuhi na kuendelea na safari zao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 3, Kamanda wa polisi mkoani hapa Mponjoli Mwabulambo amesema magari hayo yalikamatwa jana saa 11 jioni katika operesheni ya ukaguzi wa magari inayoendelea mkoani hapa.

Mponjoli amesema katika operesheni waliyoifanya walikagua magari 59 na 47 yalikutwa na makosa madogomadogo na kutozwa faini, mawili yalikuwa na matatizo makubwa na kuzuiwa kuondoka huku mengine yakiruhusiwa kuendelea na safari baada ya kuonekana hayana tatizo.

Amesema madereva wa mabasi ya kampuni ya King Msukuma wanaoshikiliwa ni Kini Daud (50) na Omary Oloyce.

Ed Sheeran kacopy wimbo, adaiwa Bilioni 225

$
0
0
STAA wa R&B, Ed Sheeran yamemkuta! Unaweza sema hivyo kwa maana nyingine baada ya familia ya aliyekuwa mkali wa muziki huo, marehemu Marvin Gaye kutaka ilipwe dola milioni 100 (zaidi ya bilioni 225 za Kibongo) kwa kosa la kuibiwa wimbo.

Kwa mujibu wa Kampuni ya Structured Asset Sales, inamdai Ed kiasi hicho cha pesa kutokana na kuiba Wimbo wa Let’s Get It On na kuubadili baadhi ya vitu kisha kuuita Thinking Out Loud. Ed anadaiwa kukopi midundo, melodi, sauti pamoja na kiitikio cha mbali kutoka katika wimbo huo uliowahi kuimbwa mwaka 1973.

Mtoto wa Marvin Gaye, Ed Townsend Jr kwa kushirikiana na Structured wameshafikia pazuri ambapo wamewalalamikia makampuni ya Sony/ATV Music, Atlantic Records na mwandishi ambaye ni Ed.Hata hivyo, bado Ed hajatoa ufafanuzi wowote juu ya madai hayo ya kuiba wimbo.

Wimbo wa Thinking Out Loud wa Ed uliachiwa Novemba, 2014 na kuwa namba moja katika chati kubwa duniani za Billboard.

Babu Tale "Nimegundua Bongo kuna Mpausha na Kumkondesha Diamond "

$
0
0

Babu Tale "Nimegundua Bongo kuna Mpausha na Kumkondesha Diamond "
_

Regrann from #babutale - Nimegundua bongo kunampausha msanii wangu. Videmu,madeni ya wasanii,kusimamia tv kama alishawahi kua nayo utotoni,kusakamwa,kukesha kila siku studio utazani msanii aliyetoka juzi sasa anaogopa kufeli,kujitia udairecta kwenye kila kazi za wasanii wa wasafi na kazi zake utazani alisomea utotoni. Nilichoamua ni kuongea na Universal kijana abaki uku mpaka msimu wa Wasafi festival. Mjue uwa mnaniumiza mkiwa mnamsakama msanii wangu kakonda mpaka mnafikia atua ya kumfananisha na Mareham Bi kidude😂😂😂😂 Sasa nimeamua arudi na naamini Universal watanisaidia maana mwenyewe siwezi #ABoyFromTandaleUSATour

Tanzia: Mtoto wa Casto Dickson na Muna Love Afariki Dunia...

$
0
0

Inauma sana Mtoto wa Casto Dickson na Muna Love Afariki Dunia...Mtoto huyo ajulikanae kama Patrick alikuwa akiuguzwa huko Nairobi alipokuwa amelazwa Hospitalini...

Zamaradi Mketema Aliyekuwa ana ongoza juhudi za kumchangia matibabu huko inatagram ameconfirm kifo chake

Regrann from #zamaradimketema - Tumejitahidi ila MUNGU ana mitihani yake, mikono inatetemeka ila ndio ukweli, PATY AMEFARIKI!! Pumzika kwa amani Baba.. - #regrann

Mfanyakazi (Msaidizi wa Nyumbani) Ana Busara Kuliko Mke Wangu

$
0
0
Wandugu, mimi ni mfanyakazi wa Benki mmojawapo hapa Dar es Salaam,
1. Nimeoa mwaka wa 7 sasa, nina watoto watatu, wawili kati yao wanasoma Shule ya Msingi.

2. Dada wa kazi hapa nyumbani (Housegirl) tupo nae mwaka wa 5 sasa. Kiukweli (bila unafiki) Dada huyu ni mtu mwenye busara na mvumilivu pia mchapakazi haswaa na anawajali watoto katika kuwaandaa kwenda shule, usafi wa nyumbani, vyakula (pia kubana matumiz yasiyo ya lazima).

3. Mke wangu naye ni mfanyakazi (Mwalimu wa Shule ya Msingi, tatizo lipo kwenye namna tunavyoishi humu ndani, mke amegeuka kuwa mtu wa KUGOMBEZA, akiingia home anagombezwa kila mtu kuanzia House girl, mimi mumewe na changanya watoto.

4. Pamoja na kugombezwa kote huko binti wa kazi huwa hajibu zaidi ya kuwa mkimya kisha huendelea na kazi zake, na wakati mwingine huomba radhi hata kama kosa si lake.

5. In short, mama mwenye nyumba akiwepo ni wote tunakuwa wapole, ni mwendo wa kugombezwa tu mpaka inapofika mida ya kulala, takribani saa 5 usiku.

NB: Najuta kumuoa huyu mwanamke wa Kichaga toka Lambo, Machame.

Baba Diamond 'Mondi Atapata Tabu Sana'

$
0
0
LICHA ya hivi karibuni staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kumposti baba yake, Abdul Jumaa kwa mara ya kwanza kwenye ukurasa wake wa Instagram, mzee huyo ameibuka na kusema akifa mwanaye huyo atapata tabu sana.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, baba Diamond alisema aliiona picha hiyo ambayo mwanaye huyo aliiweka ambayo waliipiga wakiwa pamoja yaani yeye, mama Diamond na Diamond mwenyewe kipindi hicho akiwa mtoto.

 Aliendelea kusema kwamba, kutokana na Diamond kushindwa kumsaidia inavyostahili na kutomjali kipindi hiki akiwa hai, siku akifariki dunia atapata tabu sana kwani atatamani angekuwepo lakini haitawezekana tena.

“Niliiona hiyo picha na nilijisikia kawaida na niliiona ni nzuri, haina tatizo lolote pia Diamond mimi ni baba yake hata iweje na ninajua ananichukia sasa hivi kwa kuwa bado ananiona niko hai lakini atakuja kupata taabu sana pindi nitakapokufa,’’ alisema baba Diamond.

 IKO HIVI

Wiki iliyopita Diamond aliweka picha ya zamani akiwa mdogo inayomuonyesha akiwa na mama yake Sanura Kassim ‘Sandra’ na baba yake, Abdul wakiwa wametokelezea ile mbaya ambapo wafuasi wake wengi walionekana kumpongeza huku wengine wakimshushua kuwa inakuwaje sasa anamposti wakati alishasema kwamba baba huyo alimtelekeza.


“Huyu baba walimsingizia kuwa kamtelekeza Diamond mbona hapo wapo wote na anaonekana alikuwa mkubwa tu, huyu Bi Sandra kuna chuki aliipandikiza kati ya mtoto na baba, si mnaona anavyotaka kuipandikiza pia kwa deeylan (mtoto wa Mobeto) na baba ake,’’ aliandika mmoja wa mashabiki kwenye posti hiyo.

 Mara kadhaa baba Diamond amenukuliwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari akimlalamikia mwanaye kwamba hamsaidii inavyostahili huku akitolea mfano kipindi hiki ambacho anasumbuliwa na tatizo la miguu achilia mbali kutokuwa na uhakika wa kula msosi wa maana.

STORI: Memorise Richard, DAR 

Muone Ustadhi Ashrafu Atimize ndoto yako..Anatumia Nyota na Nguvu za Asili Kutibu

$
0
0
Muone Ustadhi Ashrafu Atimize ndoto yako. yawezekana ulizaliwa nanyota yakitajiri ila watu wabaya wameikalia mpaka sasa ikawa hufahamu chochote. Mtafute ust Ashrafu Airudishe nyota yako yakitajiri kwakupitia pete inayoendana na nyota yako. Ust Ashrafu Ananguvu zamajini katika utendaji wake.

Anauwezo wakutoa Mali kwakupitia pete nakwakupitia majini wake. Na anauwezo wakuzirudisha Mali zilizopotea kwanjia zakichawi kwakupitia Pete yakifalme Ambayo inayong'aa muda wowote nakubadilikabadilika rangi. Ust Ashrafu Ametembea baadhi ya nchi kwakuwapatia watu huduma mbalimbali. Kama vile maradhi yakisukari, presha, ukimwi, bawasiri, tezidume, mwiliwote kupooza nakutetemeka, NK. Navilevile Amewapatia wengi huduma yamvuto wa kibiashara, nayamvuto wakimapenzi.

Nawengi wametoa shukrani zao kwa ust Ashrafu namna Alivyozirudisha Ndoa zao zilizo sambaratika kwamuda mrefu. Mtafute ust Ashrafu ili akusaidie juu yamambo yako. Nahuyu ust anasaidia matatizo yauzazi, nguvu zakiume, kuwashwa mwilini, kutokwa namapere usoni nasehemu za siri, NK. Na anadawa yakumtuliza mume asiesikia nakutulia inayoitwa limbwata. Na anadawa yakumrudisha mpenzi ktk mahusiano kwamda mchache.

Na amezipatanisha familia nyingi zilizogombana. Na anauwezo wakufarakanisha maadui waliokua pamoja.

Mtafute Ustadhi Ashrafu kwa no. 0768486717-0627423037 Au Mtafute kwa whasapp 0659438578

Hizi ndio namba zake mpigie muda wowote usiogope yupo kwaajili yako. Mpigie hupate muongozo wa bure naushri. Ustadhi Ashrafu huduma zake hupatikana mahala popote utakapo muhitaji, ila sehemu kuu anapatikana Bagamoyo.

Aliyesimamishwa na Mwigulu Kwa Waraka wa KKKT Arejea Kazini, Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Jumatano ya July 4

$
0
0

Aliyesimamishwa na Mwigulu Kwa Waraka wa KKKT Arejea Kazini, Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Jumatano ya July 4

Maneno ya Huzuni ya Rais Magufuli akimlilia Profesa Majimarefu

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Yustino Ndugai kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mkoani Tanga Steven Hillary Ngonyani maarufu “Profesa Majimarefu”.

Profesa Majimarefu amefariki dunia usiku July 2, 2018 katika katika hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akipatiwa matibabu.

Katika salamu hizo Rais Magufuli ameelezea kusikitishwa na kifo cha Profesa Majimarefu ambaye alikuwa Mbunge hodari na aliyewapenda na kuwapigania wananchi wa Jimbo lake la Korogwe.

“Spika Ndugai nimehuzunishwa sana na kifo cha Profesa Majimarefu, tumempoteza mtu aliyejitoa kuwahudumia wananchi kwa juhudi zake zote, aliyependa maendeleo na aliyekuwa rafiki wa watu, nakupa pole sana wewe Spika, Wabunge wote, familia ya Marehemu, ndugu, jamaa na wote walioguswa na kifo hiki” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufulli amemuombea Profesa Majimarefu apumzishwe mahali pema peponi.

TRA Yakanusha Watanzania Kulipia WhatsApp

$
0
0
TRA Yakanusha Watanzania Kulipia WhatsApp

Soma Taarifa Rasmi hapa chini:


Viewing all 104756 articles
Browse latest View live




Latest Images