Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live

Hamisa Mobeto: Ukiwa na Tabia mbaya hauwezi kushinda Taji Miss Tanzania

0
0
Mwanamitindo Hamisa Mobeto amesema hauwezi kushika nafasi ya kwanza kwenye Shindano la Miss Tanzania kama siyo mrembo, tabia yako ni chafu na huna akili timamu.

Mobeto ameyasema hayo baada ya kuteuliwa kwenye kamati ya kuwa mmoja kati ya majaji katika mashindano ya kumchagua Miss Mwanza mwaka huu yatakayofanyika Leo Usiku katika Ukumbi wa Rock City Mall Jijini hapa.

Pia amesema yeye ni kila mwaka anapata nafasi hiyo ya kuwa jaji. "Nashukuru aliyepewa kuwa msimamizi wa Mamis ni Mwanamke kwahiyo sitegemei kama atapendelea lazima achague mtu sahihi na anayefaa kupewa taji hilo bila upendeleo," alisema mobeto.

Aidha Mobeto amesema kuwa yeye ni mzaliwa wa Mwanza, ana heshimu Jiji hili kwa kutoa Warembo anaamini kati ya Mikoa mitano yenye Warembo wa hali ya juu hapa nchini Mkoa wa Mwanza ni miongoni.


Shabiki wa Argentina Ajiua Baada ya Mess Kuondolewa Kombe la Dunia

0
0
Shabiki wa  Argentina Ajiua Baada ya Mess Kuondolewa Kombe la Dunia
SHABIKI kija­na amepoteza maisha baada ya timu ya taifa ya Argentina kufun­gwa na Ufaransa na kuondolewa katika Kombe la Dunia (World Cup), wikiendi iliyopita.



Shabiki huyo ali­yefahamika kwa jina la Monotosh Halder mkazi wa Habibpur, Wilaya ya Malda nchini India, alipata mfadhaiko mara baa­da ya timu hiyo inayoon­gozwa na Lionel Messi kufungwa mabao 4-3 huku yeye akiwa shabiki mkubwa wa Messi.


Mara baada ya mch­ezo huo, Monotosh, 20, alishindwa kula usiku, akaenda kulala, asubuhi yake wakakuta akiwa amefariki. Polisi hawajaweka wazi sababu za kifo hicho, lakini ndugu zake wote walisema hakuwa akiumwa.



Taarifa za mtaani kwake zinaeleza kuwa aliamua kujiua baada ya kupata mfadhaiko huo wa matokeo hayo.

Baadaye taarifa ya polisi ilisema: “Tunaendelea na uchunguzi na inaonekana ni kama alijiua mwenyewe mara baada ya Ar­gentina kuondolewa kwenye Kombe la Dunia.”

Wawindaji Wawili wa Faru Waliwa na Simba

0
0
Wawindaji Wawili wa Faru Waliwa na Simba
Takribani majangili wawili wa vifaru wame raruliwa na kuliwa na simba katika mbuga ya wanyama huko Afrika ya kusini, maafisa wamesema.

Askari wa doria waligundua mabaki ya watu wawili, na wengine wanahisi ni mabaki ya watu wa tatu, katika mbuga ya wanyama ya Sibuya karibu na Kusini-Mashariki mji mwa mji wa Kenton

Bunduki yenye nguvu kubwa na shoka pia vili kutwa hapo.

Kwa nini huenda ndizi zikatoweka duniani

Mganga aliyedai kuwa na nguvu za kuzuia risasi afariki kwa kupigwa risasi

Katika miaka ya hivi karibuni, Ujangili umeongezeka sana Afrika ya Kusini, ili kutokana na kuongezeka kwa hitaji la pembe za vifaru huko bara la Asia.

Kwa upande wa China, Vietnum na sehemu nyingine nyingi pembe za vifaru zinaaminika kuwa na sifa ya kuongeza hisia za mapenzi.

Mmiliki wa Hifadhi wa Sibuya, Nick Fox katika taarifa yake kwenye ukurasa wa Facebook wa mbuga hiyo amesema watu hao wanao sadikiwa kuwa ni majangiri waliingia katika mbuga hiyo jumapili usiku au mapema siku ya Jumatatu asubuhi.

"Walikosea na kuingia kwenye eneo la kujidai la simba, ni eneo kubwa hivyo hawakuwa na muda mwingi, " Bwana Fox aliliambia Shirika la habari la AFP.

"Hatuna hakika ni watu wangapi walikuwa - kwani kuna mabaki kidogo sana ya miili yao. "

Gigy Money: Prezzo Kafulia Choka Mbaya

0
0
Gigy Money: Prezzo Kafulia Choka Mbaya
Video vixen na Msanii wa Muzikiwa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money ameweka wazi msanii kutoka Kenya Prezzo hivi sasa amefulia vibaya mno.

Gigy Money alifunguka hayo wakati anaongelea uhusiano kati ya Rafiki yake Amber Lulu na mpenzi wake Prezzo

Kwenye mahojiano na Kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Gigy Money ameweka wazi hivi sasa ukimuona Prezzo siyo yule uliyekuwa unamuona kwenye Tv yaani kafulia:

"Yaani Prezzo kakonda kuliko hata unavyomuona Kwenye picha, naona ni stress za kimaisha kwa sababu mimi nimeenda kuperfom juzi juzi Nairobi nimeondoka club nimemuacha Prezzo mpaka asubuhi saa saba za usiku hana direction yoyote.

"Alikuwa ana jina zamani sio sasahivi, hata wanavyomchukulia huko Nairobi sio tunavyomchukulia sisi huku Bongo yaani amefulia choka mbaya hayupo kwenye peak tena hata huku tunamuongelea sababu ya Amber”.

Gigy Money amedai Kenya wasanii wenye majina ni wasanii kama Nyanshinki, Will Paul, Khaligraph na wengine lakini ukimtaja Prezzo watu watakucheka sana.

Shamsa Ford: Peter ni Baba Mzazi wa Marehemu Patrick Casto Namjua Kama Mtangazaji Tu

0
0
Shamsa Ford: Peter ni Baba Mzazi wa Marehemu Patrick Casto Namjua  Kama Mtangazaji Tu
Miongoni mwa mastaa ambao wameendelea kumiminika katia msiba wa mtoto Patrick uliopo Maeneo ya Mwananyamala ni Shamsa Ford, ambaye akiwa msibani hapo amepiga stori na Global Tv na kumzungumzia mtoto huyo pamoja na vuguvugu linaloendelea mitandaoni kuhusiana na baba mzazi wa mtoto Patrick.



Shamsa amesema yeye si mtu wa karibu sana na Muna lakini anajua kwamba aliwahi kuolewa na hapo walipo nyumbani kwa Peter ndiyo kwa baba mzazi wa mtoto, kwa upande wa Casto anamfahamu kama mtangazaji tu wa kituo cha Runinga cha Clouds Tv.

Kangi Lugola Amtimua Kamishna Mkuu wa Magereza Baada ya Kuchelewa Kwenye Kikao kwa Dakika 1

0
0
Kangi Lugola Amtimua Kamishna Mkuu wa Magereza Baada ya Kuchelewa Kwenye Kikao kwa Dakika 1
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, amemfukuza kikaoni Kamishna Mkuu wa Magereza, Juma Malewa kwa kuchelewa.

Lugola amemfukuza Dk Malewa leo Julai 6, saa tano asubuhi ikiwa ni dakika chache baada ya kikao hicho kuanza.

Awali, Lugola alisema ikifika saa 5 kamili, mlango ufungwe na kama alivyoagiza, ulifungwa. Ilipofika saa 5:1 mlango ulifunguliwa ili Dk Malewa aingie.

Baada ya kuingia Dk Malewa, Lugola akahoji kwa nini amefunguliwa mlango?

Licha ya Dk Malewa kuomba msamaha, Lugola alikataa kata kata. Pia Lugola ameagiza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, kumshusha cheo hadi kubaki na nyota tatu, mkuu wa usalama barabarani, Mbeya, Leopold Fungu.

Pia ameagiza Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto mkoa wa Kagera, George Mrutu ashushwe cheo.

Kikao hicho ni cha kimkakati cha viongozi wa vyombo na taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo.

CCM Yamvaa Mbowe Kisa Hiki Hapa

0
0
CCM Yamvaa Mbowe Kisa Hiki Hapa
Chama cha Mapinduzi (CCM), kimefunguka na kumjia juu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe kwamba sio kweli wamezuiliwa kufanya mikutano ya hadhra katika majimbo yao kama wasemavyo bali wao wenyewe ndio hawataki kufanya.

Hayo yamebainishwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa (CCM), Humphrey Polepole kwenye mjadala wa uzinduzi wa ripoti ya pili Twaweza kuhusiana na hali ya siasa nchini uliofanyika Julai 05, 2018 na kusema hakuna chama chochote kilichokatazwa kufanya mikutano ya hiyo.

"Mikutano ya hadhara haijapigwa marufuku ila imewekewa utaratibu mzuri zaidi wa namna ambavyo tunapaswa kufanya siasa katika nchi yetu. Tatizo lililokuwepo katika mikutano ya hadhra haifanyiki na wanaoongoza kutofanya hivyo sio CCM bali ni upinzani, na hawafanyi kwasababu hawaishi katika majimbo yao husika ambayo wamepigiwa kura na wananchi wao", amesema Polepole.

Pamoja na hayo, Polepole ameendelea kwa kusema "kwa mfano Mh. Mbowe tangu alipochaguliwa mwaka 2015 mkutano wake wa kwanza ameufanya Hai mwaka 2017 lakini yeye na chama chake wamekuwa mstari wa mbele kusema wamezuiwa kufanya mikutano ya hadhra".

Kwa upande mwingine, Polepole amewataka Wabunge waende kuishi kwenye majimbo yao ambayo wamepigiwa kura na wananchi wao ili waweze kuwasikiliza na kutatua kero zao ambazo wanakumbana nazo kwa madai hakuna njia nyingine mbadala wa hiyo huku akitolea mfano kwa kuwataja Wabunge wachache ambao hawaishi katika majimbo yao husika kuwa ni Zitto Kabwe, Freeman Mbowe, James Mbatia

Breaking News: Waziri Lugola amshusha Cheo Kamanda na Mkuu wa Kikosi

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema alitaka kuchukua uamuzi wa kumfukuza kazi Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mbeya na Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Kagera lakini Happy Birthday yake ndio imewaokoa.

Hata hivyo, Lugola amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kuwashusha vyeo Makamanda hao.

Akizungumza na waandishi wa habari, Lugola amesema wakati anaapishwa na Rais alimwambia anachukizwa na matukio ya ajali yanatotokea hasa ya Mbeya.

“Ajali nyingi zinatokea Mbeya ambapo ilinibidi niende kwa Kamati ya Usalama, nilibaini kitu kilichofanya nivunje Mabaraza ya Kamati ya Usalama barabarani,”.

Amesema kuwa alichobaini alitaka kujua kuna wajumbe wangapi lakini walishindwa kujua idadi, wala majina, pia wameshindwa kumpa taarifa ya kile wanachokifanya.

“Hivyo lazima nichukue hatua kali ili kunusuru maisha ya watu kwani Rais amechoka kutuma salamu za rambirambi,”.

Kutokana na hatua hiyo amesema anamuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, awashushe vyeo Makamanda hao kutokana na uzembe.

“Leo nilipanga niwafukuze watu kazi ila bahati nzuri kwao mimi nilizaliwa Ijumaa na kwa vile niliimbiwa wimbo wa Happy Birthday To You….nikaona nisiaribu furaha yangu, hivyo nikawaacha,” amesema.

Hii Hapa Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo ya Uume

0
0
Tatizo hili limekuwa likiwaadhiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baada ya kujiona wapo tofauti sana na wengine kwa kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi 6-8 kwanza upungufu wa vichocheo hivi huchochea ukuaji wa uume chongo ambalo hushambulia nerve ambayo uharibu kabisa ukuaji wa uume, ngiri, punyeto, ambayo huathili misuli ya uume, ngiri huleta maumivu, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, korodani moja kuvimba, kutopata choo vizuri, sababu hizi hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na mara nyingi hata nguvu za kiume ( hamu ya tendo la ndoa) hupungua na kwisha kabisa

GEMBE :Ni dawa inayozalisha na kukufanya uume kukua na kuongezeka
NGEMO : Ni dawa bora ya kuongeza nguvu za kiume

Hukutia hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi mara4 nne bila kukinai au kuchoka pia itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk30-45 kwa mtumiaji pia tunatibu kisukari, bp, ngiri, miguu kuwaka moto KAMA HUNAMDA WA KUFIKA OFISINI KWETU UTALETEWA POPOTE TUPO MBAGALA RANGI TATU

 0753471612/ 0715249530
0623 386 305

DR KUZENZA

Kocha Hans Afunguka Sababu za Kumchagua Mwambusi

0
0
Klabu ya Azam FC leo imemtambulisha rasmi kocha wake Mkuu Hans van der Pluijm, ambapo baada ya utambulisho ameweka wazi mipango yake ikiwemo sababu za kumchagua kocha Juma Mwambusi kuwa msaidizi wake.

Hans amesema moja ya mpango wake mkubwa ni kuhakikisha Azam FC inafika mbali zaidi, kuanzia kupata ubingwa wa michuano ya ndani kama Ligi kuu na Kombe la Shirikisho pia kufanya vizuri kwenye michuano ya Kimataifa.

Kocha huyo raia wa Uhalanzi ameelezea sababu za kumchagua Kocha Juma Mwambusi kuwa msaidizi wake, akisema hajaona maana yoyote ya kumtafuta kocha kutoka nje wakati anatambua uwezo wa Mwambusi na anaamini atamsaidi kutimiza mipango yake ndani ya Azam FC.

Naye Meneja wa Azam FC Philip Alando amesema kuwa katika mkataba waliokwisha saini na Hans hawajaweka masharti yoyote kama wafanyavyo vilabu vingine vikimtaka kocha asipofanya jambo kwenye timu wanamfukuza.

Kocha Hans ambaye amewasili nchini siku nne zilizopita akitokea Ghana kwa mapumziko amesema jana alikutana na wachezaji wote na kuwaeleza mambo anayoyahitaji kwaajili ya kufikia malengo ikiwemo nidhamu na kujituma huku pia akiweka wazi kuwa hatoangalia jina la mchezaji bali uwezo na kujituma.

Hiki Hapa Chanzo cha Ajali Zinazotokea Mbeya

0
0
Hiki Hapa Chanzo cha Ajali Zinazotokea Mbeya
Ikiwa ni siku tatu tu, tangu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, kutangaza mabadiliko ndani ya jeshi la polisi nchini ili kuongeza juhudi za kuzuia ajali zilizotokea mara kwa mara katika baadhi ya Mikoa, jijini Mbeya bado hali ni tete kutokana na jiografia ya eneo hilo.

Siku chache tu tangu Jiji hilo lipoteze watu 20 na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mteremko wa Mbalizi Mkoani humo, ambapo ilikuwa pia ni siku chache tangu kutokea kwa ajali iliyosababisha vifo vya Askari wa Jkt, katika mteremko mkali wa eneo la Igodima na kufanya mpaka sasa kuwa na ajali tatu kubwa ndani ya kipindi cha miezi miwili, ukijumlisha na ajali iliyotokea usiku wa jana.

Watu wanne wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika  ajali ya barabarani iliyotokea Usiku wa jana jijini humo, iliyohusisha magari matatu tofauti yaliyogongwa na roli lililokuwa limefeli breki katika mlima wa Igawilo jijini humo.

Kwa mujibu wa Kaimu RPC Mkoa wa Mbeya, Mussa Taibu amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo mkali wa dereva ambaye alikuwa amebeba mzigo mzito kwenye kontena na kupelekea kufeli kwa breki.

“Ajali hiyo imehusisha magari matatu imetokea kwenye mteremko wa mlima Igawilo gari lenye kontena limeliangukia gari aina ya Noah iliyokuwa na abiria na inasadikiwa watu wanne wamepoteza maisha bado zoezi la uokoaji linaendelea kwani jana usiku tulishindwa kuondoa kontena kwakuwa uzito ulikuwa umezidi”, amesema Kaimu Kamanda.

Akizungumzia jiografia ya eneo hilo Kamanda Taibu amewataka madereva na watumiaji wa barabara kuwa makini, na kufanya ukaguzi wa magari yao kabla ya kuanza safari kwani ajali nyingi zinasababishwa na uzembe wa madereva kuendesha magari mabovu.

Mwili wa Mtoto Patriki Wawasili Dar Muna Azimia Airport

0
0
Mwaili wa Mtoto Patriki Wawasili Dar Muna Azimia Airport
Mwili wa Mtoto wa Muigizaji Muna Love anayefahamika kwa jina la Patrick umewasili katika uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere ukitokea Nairobi Nchini Kenya alipokuwa amekwenda kupata matibabu.


Baada ya kutoka Airport mwili huo unatarajia kupelekwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kuhifadhiwa na mapema kesho utatolewa kuelekea katika uwanja wa Leaders Club kwa ajili ya kuagwa na kisha kuzikwa katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Wanajeshi wanne wa Ugana Wafariki Kwenye Mapigano Kati ya Vikosi vya Uganda na DRC Katika Ziwa Edward

0
0
Wanajeshi wanne wa Ugana Wafariki Kwenye Mapigano Kati ya Vikosi vya Uganda na DRC Katika Ziwa Edward
Watu 7 wamefariki wakiwemo wanajeshi 4 wa Uganda katika mapigano kwenye ziwa Edward kati ya vikosi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Uganda, kwa mujibu wa afisa wa Congo aliyenukuliwa na shirika la habari la AFP.

Ziwa Edward lipo katika mpaka kati ya nchi hizo mbili.

Kiongozi kutoka Beni, Donat Kibwana, amenukuliwa na AFP akisema kuwa mashua ya kupiga doria ya Congo ilishambuliwa Alhamisi asubuhi na boti la kupiga 'doria la Uganda'.

Boti la Uganda lilizama na wanajeshi wanne wa taifa hilo na raia watatu walifariki, aliongeza.

Twaweza: Watanzania 'hawako tayari kuandamana'

Onyo la Macron kuhusu vituo vya wahamiaji Afrika

Jaribu Muliwavyo, mbunge kutoka eneo hilo, amekiambia kituo kimoja cha redio Congo kwamba mapigano hayo yanatokana na mzozo wa haki za kuvua.

Huyu Hapa Ndiye Mwanamke Anayeshikiria Rekodi Duniani ya Kufunga Ndoa Nyingi

0
0
Huyu Hapa Ndiye Mwanamke Anayeshikiria Rekodi Duniani ya Kufunga Ndoa Nyingi
Mwanamke Linda Wolfe Raia wa Marekani mwenye miaka 68 ndie anashikilia rekodi za Guiness kwa kuwa Mwanamke aliyewahi kufunga ndoa nyingi zaidi duniani.

Linda anatajwa kufunga ndoa mara 23 na Wanaume tofauti tofauti ambao wote aliachana nao kwa sababu mbalimbali.

Inadaiwa kuwa Linda ana uraibu wa kupenda kufunga ndoa na Wanaume tofauti tofauti kitu kilichopelekea kufikia idadi hiyo ya ndoa 23.

Aidha Linda amebahatika kupata Watoto 7 na Wanaume tofauti tofauti aliooana nao na amebahatika pia kupata Wajukuu wengi.

Kenya Yapiga Marufuku Matumizi ya Dawa ya HIV

0
0
Kenya Yapiga Marufuku Matumizi ya Dawa ya HIV
Wizara ya Afya nchini Kenya imezionya kaunti nchini humo kusitisha kuwapatia wagonjwa dawa za HIV zinazosababisha kasoro miongoni mwa watoto walio tumboni.

Kupitia Mkurugenzi wa huduma za matibabu nchini humo Jackson Kioko, wizara hiyo imewaagiza Wakurugenzi wa afya katika kaunti hizo kuhakikisha kuwa wanawake wajawazito na wale wanaonyonyesha ambao walikuwa wakitumia dawa aina ya kwanza ya Dolutegravir (DTG), waendelee kutumia dawa hiyo hadi watakapomaliza kunyonyesha.

Lakini akina mama wajawazito walio kati ya umri wa miaka 15 hadi 49 ambao wamekuwa wakitumia dawa hiyo wanapaswa kupewa matibabu ya kwanza ya Efavirenz.

Mapigano kati ya vikosi vya Uganda na DRC katika ziwa Edward
Katika taarifa kwa wakurugenzi hao Dkt. Kioko alisema kuwa dawa hiyo iliozinduliwa nchini Kenya mwaka uliopita haifai kutumiwa na wanawake wajawazito na wale wanaonyonyesha kutokana na data chache za usalama wake zilizopo.

Pia ameongezea kwamba kulingana na taarifa ya mwaka 2017, watu wazima wanaotumia dawa ya kwanza ya ARV wataanza kutumia DTG.

Hatahivyo mwenyekiti wa bodi ya madaktari nchini Kenya tawi la magharibi Dkt Anthony Akoto amesema kuwa wizara ya afya inapaswa kutoa sababu za hatua hiyo zikiandamana na ushahidi.

Akizungumza na BBC, Dkt Akoto anasema kuwa kufikia sasa hakuna ushahidi wowote kwamba dawa hiyo ina madhara na akivitaka vitengo muhimu vya serikali katika wizara ya Afya kama vile Kemri, Shirika linalosimamia udhibiti wa ugonjwa wa ukimwi NASCOP, na shirika la ubora wa bidhaa KBS kutoa ushahidi unaothibitisha dawa hiyo haifai kupewa wanawake wajawazito na wale wanaonyonyesha.Kenya Kusitisha

Kangi Aamuru Makamanda Kuja na Ilani ya CCM

0
0
Kangi aamuru Makamanda kuja na ilani ya CCM
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, ameagiza kushushwa vyeo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Mbeya, Leopold Fungu kwa ajali zilizokithiri mkoani humo, na Mkuu wa kikosi cha zimamoto na uokoaji mkoa wa Kagera George Mrutu kwa kushindwa kutimiza majukumu yake.

Kangi ametoa agizo hilo leo, wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam ikiwa ni siku moja tangu kuvunja kwa Baraza la Usalama wa Barabarani Taifa hadi kwenye ngazi ya mikoa na wilaya.

“Katibu Mkuu nakuagiza kumshusha cheo Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Mbeya Leopold Fungu, kutokana na kukithiri kwa ajali za barabarani mkoani humo, na huyu Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto Mkoa wa Kagera, George Mrutu ashushwe cheo kwa matamshi yake ya sababu za yeye kutofika kuzima moto bweni la chuo”, amesema Waziri.

Katika mkutano huo Waziri Lugola, amemfukuza kikaoni Kamishna Mkuu wa Magereza, Juma Malewa kwa kuchelewa kufika kikaoni, na kuwaagiza wakuu wa idara zote za ulinzi na usalama kuja na ilani ya chama cha mapinduzi kabla ya kufanyika kwa kikao kijacho kwani wanatakiwa kufanya kazi kwa kuifuata ilani ya chama chao.

Viwanja vya makazi: Bunju na MapingaViwanja vipo Kimele, ni km 3 kutoka main road.

0
0

Viwanja vya makazi: Bunju na Mapinga
Viwanja vipo Kimele, ni km 3 kutoka main road.
Vipo viwanja size zote kwa bei tofauti: mil 4 for 20/20, mil 6 for 20/30, mil 8 for 20/40, mil 12 for 30/40, mil 16 for 40/40 na mil 24 for 40/60. luksa kulipa kwa awamu.
Hakuna dalali, mpigie mhusika: 0757489709

Pata Tiba ya Tatizo la Nguvu Za Kiume, nasaidia Kukufanya Urudie Mara 5 na kuchelewa kwa Dakika 20

0
0
TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO LINATIBIKA.Baada ya utafiti wa mda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka DR Magise imekuletea tiba ya matatizo hayo kwa kutumia dawa za:

GUMBA POWER:Ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume,dawa hii inamchanganyiko wakutosha wenyekuzalisha vichocheo vingi vya Hemone za Gestrogen vikiwemo vitamin B6&B1,vitamini E,pamoja na madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi,na kuchelewa kufika kileleni zaidi dakka 20-30.

NTINJE:Inarutubisha maumbile ya uume yani kurefusha na kunenepesha nchi 4-7 upana cm3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukiitumia maumbile yako yatabaki kuwa hivyo siku zote,Pia tunatibu Presha,kisukari siku7,ngiri,chango la tumbo tumbo kujaa gesi,kutopata choo vizuri

 TUPO TZ DAR ES SALAAM   MBAGALA RANGI TATU.HUDUMA HII UTALETEWA POPOTE ULIPO .WASILIANA NAMI 0754741788, 0715741788, 0783741788

-DR MAGISE

Wasanii Wasilewe Pesa za Show Muziki Una mwisho Wake- Shilole

0
0
Wasanii Wasilewe Pesa za Show Muziki Una mwisho Wake- Shilole
Msanii wa bongo Fleva Shilole amefunguka kuwa ameamua kuwekeza nguvu zake nyingi kwenye ujasiriamali kwa kuwa anajua kuna leo na kesho mziki unaweza ukabuma kwahiyo biashara zake zitakuwa msaada kwake kwa kuendeleza maisha.

Akizungumza na www.eatv.tv amesema muziki unalipa sana na unalevya kwakua wasanii wengi wanajua muziki utakuwa biashara yake ya milele na kusahau kuna kubuma kwa mziki kwahiyo mwisho wa siku muziki unabuma uku hujawekeza ndo kinakuwa chanzo cha msanii kuishi maisha mabovu.

Shilole amesema mtu anapokuwa marufu lazima aishi maisha ambayo yapo juu kwa gharama kwahiyo kwa siku unakuta mtu anatumia pesa nyingi kuliko anayoingiza kwahiyo kama muziki ukibuma na maisha yapo juu lazima uyumbe.

“Wasanii wasilewe na pesa za 'show' tu inatakiwa kufanya biashara tofauti tofauti ili hata kama muziki utakubumia iwe rahisi kuishi maisha mazuri maana kuna wasanii zamani walikuwa wanafanya vizuri na walikuwa na pesa kwakua tu walijisahau na hawakuogopa kesho yao muziki ulipobadilika tu wakaanza kuishi maisha ya kawaida,”amesema shilole.

Ameongeza kwa kusema vijana wengi wa kileo wanapenda maisha mazuri lakini wanachagua kazi, inatakiwa vijana kama taifa la leo wasichague kazi, kazi ni kazi kikubwa iwe halali ,watu waliofanikiwa wengi walianzia sehemu za kawaida baadaye ndio wanakuja kupata sehemu nzuri kwahiyo vijana waache kuchagua kazi.

Muna Akwamisha Msiba wa Mwanaye Aondoka Huku Mwili wa Patrick Ukizuiwa Airport

0
0
Muna Akwamisha Msiba wa Mwanaye Aondoka Huku Mwili wa Patrick Ukizuiwa Airport
KUFUATIA msanii wa Bongo Movie, Rose Alphonce ‘Muna Love’ kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam bila mwili wa mwanaye Patrick, na mamlaka ya uwanja huo kuzuia mwili kutoka, baba mdogo wa marehemu, Bazo Komu amesema sababu ni Muna kuondoka na nyaraka zitakazosaidia mwili kuchukuliwa uwanjani hapo.



Akizungumza katika uwanjani hapo, Bazo amesema hilo limetokea baada ya mwanamama huyo kupoteza nguvu baada ya kushuka uwanjani hapo na wao kumuingiza kwenye gari pasipo kukumbuka kuchukua nyaraka hizo muhimu.



Aidha, Bazo ameweka wazi kwamba hakuna tatizo lingine ambalo lingesababaisha wao kushindwa kuuchukua mwili wa mtoto kwa kuwa mambo yote yalishapangwa na hakuna tafrani yoyote inayoendelea kuhusiana na mtoto wapi akazikwe.



“Hakuna tatizo lolote, wala hapakuwa na makubaliano ya mtoto azikwe wapi kwa sababu tunajua mama ni nani na baba ni yupi. Kitu kilichotokea ni kwa sababu wote tumemuona Muna hali yake ilivyo. Ameshuka hajiwezi, imebidi ashikiliwe ili aweze kutembea. Tumejisahahu kuzichukua hizo dokumenti baada ya kumuingiza kwenye gari. Na kwa hali ya kawaida huwezi kuingia kwenye pochi ya mwanamke kukagua” amefafanu Bazo.



Ameongeza, “Kwa sasa tunafanya utaratibu wa kujua jinsi gani hizo dokumenti zitafika hapa ili tuweze kuuchukua mwili wa mtoto tuweze kuendelea na taratibu zingine.“
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live




Latest Images