Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live

Baba Mzazi Patriki Aongea Mazito Wakati wa Kumuaga Mwanaye " Mimi Ndiye Mume wa Ndoa wa Muna na Baba Halali wa Patriki''

0
0
Baba Mzazi Patriki Aongea Mazito Wakati wa Kumuaga Mwanaye " Mimi Ndiye Mume wa Ndoa wa Muna na Baba Halali wa Patriki''
IKIWA ni dakika chache kabla ya kuanza kwa zoezi la kuaga mwili wa mwanaye Patrick, katika Viwanja vya Leaders jijini baba wa marehemu, Peter Zacharia amenyanyuka kwenye kiti chake na kutoa kauli kwa wale waliokuwa wakipindisha ukweli kuhusu uhalali wa yaye kuwa baba wa mtoto huyo.



Akizungumza kwa jaziba leo viwanjani hapo, Peter amesema yeye ni baba halali wa Patrick na ni mume halali wa Rose Alphonce Nungu ‘Muna‘ kwani alitoa mahali na wakafunga ndoa, waliishi pamoja na kufanikiwa kupata mtoto kabla ya kuhitilafiana, hivyo watu wanaopindisha ukweli na kusema isivyo kwenye mitandao ya kijamii na kumrubuni Muna waache.




“Nataka niwambie Watanzania mjue, nililipa mahali, nikafanya vikao, tukafunga ndoa na mama mkwe akanikabidhi mwanaye, nafahamu Patrick ametokea wapi, makundi ya kumchanganya huyu hayakunifurahisha hasa wanaomdanganya Rose.



“Nimehangaika kuhakikisha namuaga mwanangu pale Mwanyamala, mimi ni maarufu sana lakini sipendi kuonekana kwenye vyombo vya habari, mtoto aliyelala pale (Peter) alinipenda na mimi nilimpenda sana, aliniita Baba Peter, alikuwa akiniombea. Haya yaliyotokea tuyaache. nawashukuru nyote mliokuja kunifarihji, Mungu awabariki sana,” alisema Paba Peter.

JPM Kuwaongoza Watanzania Kwenye Mapokezi ya Ndege Boeing 787-8 Dreamliner

0
0
JPM Kuwaongoza Watanzania Kwenye Mapokezi ya Ndege Boeing 787-8 Dreamliner
RAIS Dkt. John Magufuli kesho Jumapili Julai 08, 2018 atawaongoza watanzania katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyonunuliwa na serikali ya Tanzania.



Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa alasiri ya leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu ya Rais, Gerson Msigwa na kusema ndege hiyo inatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam majira ya saa 8:00 mchana ikiwa inatokeaa Seattle nchini Marekani.


Hii ni ndege ya nne kuwasili nchini kati ya ndege 7 zilizonunuliwa na serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuliwezesha Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kuimarisha huduma zake.

Rais Magufuli Awatunuku Kamisheni Maafisa Wa Jeshi

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi  Mkuu Dkt. John  Pombe Magufuli  amewatunuku Kamisheni  Maafisa  wapya 123 wa Jeshi la Ulinzi na Wananchi wa Tanzania  (JWTZ) katika cheo ha Luteni UsO.

Rais Magufuli amewatunuku Kamisheni Maafisa hao wapya wa Jeshi la Ulinzi na Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu  ambao walikuwa wanafunzi katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi, kilichopo Monduli Arusha leo  [Jumamosi Julai 7, 2018] katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo hicho, Luteni Generali Paul Massao  Maafisa waliohitimu kozi ya 63 mwaka 2017 jumla yao ni 123 kati yao 118 ni watanzania,  na wahitimu 5 kutoka nchi za Uganda,  eSwatini, na Rwanda.

“Kati ya Maafisa  watanzania 118  wanawake ni 3 na wanaume 115, ambapo Maafisa 121 walipata mafunzo yao katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Mondulu  na Maafisa wa 2 walipata mafunzo yao nchini India” alifafanua Luteni Generali Massao.

Sambamba na kuwatunuku Kamisheni Maafisa hao kwa cheo cha Luteni Usu, Rais Magufuli ametoa zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri ambao ni Emmanuel Kakuba Afisa aliyefanya vizuri zaidi darasani, Danie Meshack aliyefanya vizuri zaidi kwenye mafunzo, na katika medani ni Ramadhan Kakombe.

Wengine, ni Amstrong Mwamwesige kutoka Uganda aliyefanya vizuri kutoka nchi rafiki pamoja na Beatrice Kipinge ambaye ni mwanamke aliyefanya vizuri zaidi.

Aidha, wahitimu 87 waliachishwa mafunzo kwa sababu mbalimbali ikiwemo magonjwa, utovu wa nidhamu ama mtu kuomba kwa hiari yake.

Hafla hiyo ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wa ilipambwa na burudani kutoka vikundi mbalimbali ikiwemo kikundi cha ngoma za asili pamoja na kikundi cha mziki wa dansi cha Jeshi cha Mondulu jijini Arusha.

Aidha, tangu kuingia kwake madarakani mwaka 2015  hii ni mara ya 6 ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwatunuku Kamisheni Maafisa wa Jeshi la Ulinzi na Wananchi Tanzania (JWTZ).

Azam Yafunguka Siku ya Shabaan Idd Kutua Hispania

0
0
Azam Yafunguka Siku ya Shabaan Idd Kutua Hispania
Klabu ya soka ya Azam FC kupitia kwa meneja wake Phillip Alando, imesema mshambuliaji wao Shaaban Idd ambaye amesajiliwa na timu ya Tenerife ya Hispania, ataondoka nchini mara baada ya michuano ya Kombe la Kagame.


Mchezaji Shaaban Idd mwenye jezi nyeupe kwenye moja ya mechi za timu yake.

Akiongea leo na eat.tv meneja huyo amesema kila kitu kimeshawekwa sawa kati ya Azam FC na Tenerife FC, hivyo mchezaji huyo ataondoka hivi karibuni baada ya michuano ya Kombe la Kagame ambayo inaendelea hapa nchini huku Azam FC akiwa ndio bingwa mtetezi.

''Shaaban tayari ana mkataba wake na Tenerife na taratibu zote ameshakamilisha, kilichobaki ni kumaliza kuitumikia klabu yetu kwenye michuano ya Kagame kisha asafiri kwenda Hispania kwaajili ya kuanza maisha mapya ya soka la kimataifa'', amesema Alando.

Shaaban Idd anaungana na nyota mwingine wa Tanzania anayechezea timu hiyo, Farid Mussa. Alando ameongeza kuwa wao kama timu wataendelea kuendeleza vipaji hata kama timu hazitawanunua moja kwa moja lakini kwa vipaji vya nyota hao wataendelea kuwaruhusu wakacheze kwa mkop

Mshambuliaji huyo amesaini mkataba miaka 2 kucheza kwa mkopo ndani ya Tenerife. Msimu uliopita klabu ya Tenerife ilimaliza katika nafasi ya 11 kwenye ligi daraja la pili ya Hispania maarufu kama  'Segunda B' ambayo washindi watatu huwa wanapanda ligi kuu.

Hakuna Amjuae Mume Kama Mke Wake...Embu Soma Kisa Hichi

0
0

Discussion by a couple over mobile late at night.

Wife : _Where are you? Speaking so tensed. What happend?_

Husband : _I'm in the car dear. But the steering wheel, clutch pedal, brake pedal, accelarator pedal are all stolen from our car.. What to do??_

Wife : *You drunk again??*

Husband : _..A little... but how does that matter? Think about the car first..._

Wife : *Expected.. You idiot.. Change from left seat to the right seat. You'll find everything.....*

🍺🍻🍷🥃🍾
Nobody knows you better than your WIFE..💐 🙏😂

Timu ya taifa ya England Yaua Mtu na Kuingia Nusu Fainali

0
0

Timu ya taifa ya England imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Dunia Urusi kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sweden. 

Mabao ya England yamefungwa na Harry Maguire (30') pamoja na Dele Alli aliyefunga katika dakika ya 58 ya kipindi cha pili. 

Ushindi huo unawafanya England kuingia hatua hiyo ya nusu ikiwa ni baada ya miaka 24 ambapo mara ya mwisho ilikuwa 1990. 

Baadaye majira ya saa 3 kamili usiku, Croatia watakuwa kibaruani kukipiga dhidi ya wenyeji Urusi. 

Kumbuka tu kuwa mechi zote hizi zinaonekana mbashara kupitia king'amuzi cha Star Times.

Mo akwamisha mchakato wa kocha mpya Simba

0
0

Bilionea wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ amedaiwa kuchelewesha mkataba wa kocha anayetajwa kuanza kuinoa timu hiyo kwa kuchukua mikoba ya Mfaransa, Pierre Lechantre. 

Jumapili iliyopita, uongozi wa Simba unadaiwa kumshusha nchini, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji kwa ajili ya kuwa kocha mkuu wa timu hiyo baada ya hivi karibuni Lechantre kufungashiwa virago vyake klabuni hapo. 

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba ambazo Championi Jumamosi limezipata zimedai kuwa Aussems angekuwa tayari ameishapewa mkataba wa kuinoa timu hiyo lakini zoezi hilo limekwama kutokana na kile kilichodaiwa Mo kuwa safarini. 

Kutokana na hali hiyo, kocha huyo imemlazimu asubiri mpaka bilionea huyo atakaporejea nchini. 

“Mpaka sasa Aussems hajapewa mkataba wowote kutokana na Mo kuwa safarini kwa hiyo hakuna ambacho kimefanyika mpaka sasa. 

“Labda muda wowote kuanzia leo kama Mo atakuwa amesharudi nchini basi ndipo anaweza kupatiwa mkataba wa kuinoa timu yetu,’ kilisema chanzo hicho cha habari. 

Walipotafutwa viongozi wa Simba ili waweze kulizungumzia hilo hakuna aliyekuwa tayari kusema chochote zaidi ya kudai kuwa hawana taarifa juu ya kocha huyo. 

Hata hivyo, Kocha huyo ambaye tayari amefanikiwa kukiona uwanjani mara mbili kikosi cha Simba katika michuano ya Kombe la Kagame kikicheza dhidi ya APR pamoja na Singida United lakini hakutaka kuweka wazi mpango wake huo wa kutaka kujiunga na Simba.

Njia 4 Rahisi za Kumtokea au Kumtongoza Msichana Uliyevutiwa Naye

0
0

Kujifundisha jinsi ya kumuapproach mwanamke kwa mara ya kwanza si jambo gumu la kufanya kama utafuata kanuni na masharti na kuyahifadhi baadhi ya michongo kwa moyo. Michongo ni maneno ya kwanza ambayo mtu hutumia kuanzisha maongezi na mwanamke. 

Maneno haya ndio mara nyingi hutumiwa na wanaume mara yao ya kwanza wanapomshobokea mwanamke. Ukiitumia vizuri michongo itakupa wewe nafasi ya kumvutia mwanamke kwa uharaka zaidi. 

Ingawa wanaume wengi hutegemea zaidi bahati ama kukosa, hauwezi kamwe kufaulu kumridhisha mwanamke iwapo hujui kuipanga michongo yako vizuri pindi unapokutana na mwanamke unayemzimia kwa mara ya kwanza. 

Ok. Kukusaidia kujipanga vyema,  tumeweza kuiorodhesha baadhi ya michongo iliyowazi na iliyofunge na jinsi ya kuitumia. 

Aina ya michongo -wazi na funge 
Unaweza kumuapproach mwanamke bila wasiwasi kwa kutumia michongo aina mbili -wazi na funge. Michongo ile mizuri zaidi inakuwezesha wewe kuonekana kujiamiani, mcheshi na kuonekana mtu anayevutia zaidi kuwaliko wengine walioko karibu nawe. 

Ijapokuwa michongo iliyowazi inahitaji mtu mwenye kujiamini kwa kiasi cha juu, michongo funge inaweza kutumika na yeyote yule bora tu ufuate masharti ya kuitumia. 

Michongo iliyofunge 
Aina hii ya michongo ni rahisi kuitumia kwa mwanamke na si rahisi kwake kuelewa kama unatumia maneno kama hayo ukiwa na ajenda fulani. Michongo hii ni kuanzia matukio, kumsifu ama kuangazia mazingira. Kila aina ya michongo hii ina manufaa yake na pia upungufu wake kiasi fulani kulingana na mazingira ambapo yanatumika. [soma: Hatua za kufanya kama mwanamke anakataa kujibu texts zako] 

1. Matukio 
Aina hii ya michongo ni rahisi kuikumbuka na ukiitumia kwa mwanamke atakupa atenshen yake automatic. Michongo hii hutumika ili kutaka atenshen ya mwanamke kwa kujaribu kumuuliza maswali ambayo yanalingana na mazingira aliyeko. 
Baadhi ya aina ya michongo iliyofunge ni kama: 
"Unaweza kujua wakati gani gari lingine la abiria linaweza kufika hapa?" 

"Je unajua sehemu nzuri ambayo mtu anaweza kujiinjoy katika huu mji?" 

"Nlikuwa nataka kuvuta sigara lakini kibiriti changu sikioni, naweza kuomba chako?" 

"Nilikuwa sijamaliza kuandika maswali ya mwalimu kwa ubao, unaweza kunisaidia kitabu chako?" 

2. Kumsifu 
Aina hii ya michongo inakaribiana na ile ya wazi lakini kwa mpango flani inazuia kumfanya mwanamke kuelewa ajenda yako kwa uharaka. Michongo hii inafaa zaidi wakati ambapo inatumika katika vilabu, sehemu za kujivinjari ama sehemu yeyote ile ambayo unaona inaweza kutumika. 
Kabla hujamsifu, ni lazima uhakikishe ni kwanini unamsifu manake mara nyingi unapomsifu mwanamke kuhusu jambo fulani atataka kujua kwa nini unammiminia sifa kama hizo. 
Baadhi ya michongo ya kumsifu ni kama vile; 

"Dress uliyoivaa imekupendeza, yaani imekufanya kuonekana mfano wa malaika" 

"Una pozi lengine ajab, lazima wewe ni dansa flani" 

"Nimependezwa na mtindo wako wa nguo na umbo lako, umetoklezea" 

Ujanja wa kutumia aina hii ya michongo ni kuhakikisha unacheza na tabia na umbo lake, hakikisha kuwa unajaribu kumchunguza ili kupata mambo ambayo anayapenda kumhusu yeye. Usisahau ya kuwa utafiti umebainisha kuwa wanawake hupenda sana kusikia wakisifiwa. 

3.  Kuangazia mazingira 
Kulingana na mazingira, unahitaji kuifahamu sanaa ya kuingia katika akili ya mwanamke na kufahamu kile ambacho anafikiria. Ukifahamu kile ambacho anafikiria, itakuwa ni jambo jema zaidi. 
Kwa mfano,  kama mwanamke anajaribu kusoma lakini kila dakika anasumbuliwa na jambo fulani, unaweza kumuuliza: "Si inaonekana ni vigumu zaidi kusoma wakati ambapo jua ni kali zaidi huko nje?" 

Kama umekutana na kundi la wanawake na ungetaka kuanza kuongea nao, unaweza kuwaapproach halafu useme "Nyinyi wanawake mnaonekana mnaenjoy sana na wenye nishati, kwani kitu gani kinachoendelea ambacho nakikosa?" 

Pia kama kuna mwanamke unayemzimia na hujawahi kuongea na yeye unaweza kumwambia "happy birthday" 

Michongo iliyowazi 
Kama wewe una confidence na unajiamini kuwa unaweza, basi njia yako ya kutumia ni michongo iliyowazi. Kumbuka kuwa kama wakati wowote utaonyesha unyonge katika sauti yako juwa ya kwamba michongo yako itaanguka hapo hapo na utajiaibisha mwenyewe. [soma: Jinsi ya kumfanya mwanamke akutamani] 

Kutumia michongo iliyowazi itakuwezesha wewe kukupatia matokeo ya haraka kwa sababu ni kuwa wanawake hupenda wanaume ambao wanajiamini kwa mambo wanayoongea na kufanya. Kama mwanamke ataonyesha dalili zozote za kutaka kuongea nawe kwa njia ya miondoko ya mwili, basi unafaa kutumia michongo iliyowazi. 

Baadhi ya michongo iliyowazi ni kama vile: 
"Unaoneka mrembo, unaweza kuniruhusu nitake kukujua zaidi?" 

"Nilikuwa nimekuona kutoka upande ule mwingine wa nyumba na nikaamua kuja kukusalimia, bila hivyo ningeishi kujutia kukosa kumjua mwanamke mrembo zaidi maishani mwangu" 

Mwisho ni kuwa hakikisha kuwa baada ya kutumia hii michongo kupata atenshen ya mwanamke, hakikisha unaendeleza maongezi yenu. Jaribu kupata kulijua jina lake halafu ujibidiishe kulitumia kila wakati, lazima atapenda. 

Usisahau kutumia sanaa za kutongoza kwa kujua vitu ambavyo mnagawa interest pamoja, jinsi ya kumfurahisha na kadhalika. Hii utamfanya apendezwe na wewe na mudan usiomrefunatakuzoea.

Sumaye Afunguka Alichosema Ikulu..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya July 8

0
0

Sumaye Afunguka Alichosema Ikulu..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya July 8

Muone Ustadhi Ashrafu Atimize ndoto yako..Anatumia Nyota na Nguvu za Asili Kutibu

0
0
Muone Ustadhi Ashrafu Atimize ndoto yako. yawezekana ulizaliwa nanyota yakitajiri ila watu wabaya wameikalia mpaka sasa ikawa hufahamu chochote. Mtafute ust Ashrafu Airudishe nyota yako yakitajiri kwakupitia pete inayoendana na nyota yako. Ust Ashrafu Ananguvu zamajini katika utendaji wake.

Anauwezo wakutoa Mali kwakupitia pete nakwakupitia majini wake. Na anauwezo wakuzirudisha Mali zilizopotea kwanjia zakichawi kwakupitia Pete yakifalme Ambayo inayong'aa muda wowote nakubadilikabadilika rangi. Ust Ashrafu Ametembea baadhi ya nchi kwakuwapatia watu huduma mbalimbali. Kama vile maradhi yakisukari, presha, ukimwi, bawasiri, tezidume, mwiliwote kupooza nakutetemeka, NK. Navilevile Amewapatia wengi huduma yamvuto wa kibiashara, nayamvuto wakimapenzi.

Nawengi wametoa shukrani zao kwa ust Ashrafu namna Alivyozirudisha Ndoa zao zilizo sambaratika kwamuda mrefu. Mtafute ust Ashrafu ili akusaidie juu yamambo yako. Nahuyu ust anasaidia matatizo yauzazi, nguvu zakiume, kuwashwa mwilini, kutokwa namapere usoni nasehemu za siri, NK. Na anadawa yakumtuliza mume asiesikia nakutulia inayoitwa limbwata. Na anadawa yakumrudisha mpenzi ktk mahusiano kwamda mchache.

Na amezipatanisha familia nyingi zilizogombana. Na anauwezo wakufarakanisha maadui waliokua pamoja.

Mtafute Ustadhi Ashrafu kwa no. 0768486717-0627423037 Au Mtafute kwa whasapp 0659438578

Hizi ndio namba zake mpigie muda wowote usiogope yupo kwaajili yako. Mpigie hupate muongozo wa bure naushri. Ustadhi Ashrafu huduma zake hupatikana mahala popote utakapo muhitaji, ila sehemu kuu anapatikana Bagamoyo.

Wenyeji Kombe la Dunia Urusi Wala Kichapo Kitakatifu na Kutolewa ..Hivi Ndo Ilivyokuwa

0
0
Wenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia Urusi wameyaaga rasmi mashindano hayo kwa kichapo cha mabao 4-3 kwa njia ya matuta dhidi ya Croatia.

Mchezo huo ulifikia hatua hiyo baada ya dakika 120 kwenda sare ya mabao 2-2 na changamoto ya mikwaju ya penati ikaamuliwa kupigwa.

Mabao ya yaliyopatikana ndani ya dakika 90 kwa upande wa Urusi yaliwekwa kimiani na Denis pamoja na Fernandez.

Wakati huo Croatia walijipatia mabao yao kupitia kwa Andrej na Vida.

Baada ya michezo hatua ya robo fainali kukamilika jana, Croatia walioingia nusu fainali watacheza dhidi ya England huku Ufaransa wakikipiga na Ubelgiji.

Mwigulu Nchemba Kasema Hawezi Kujiuzulu Ubunge....Adai Uongozi ni kupokezana kijiti

0
0

Mbunge wa Iramba Magharibi, Dk Mwigulu Nchemba amewataka wakazi wa jimbo hilo kutosikiliza maneno ya watu wanaosema kuwa anaweza jiuzulu nafasi ya ubunge baada ya kuondolewa katika baraza la mawaziri.

Dk Mwigulu alitoa kauli jana wakati akiwa kwenye mkutano na wakazi Kata ya Ulemo kijiji cha Misigiri wilayani Iramba mkoani Singida.

Alisema uongozi ni kupokezana kijiti na kwamba si kweli kwamba analengo la kuacha nafasi hiyo na kwamba ataendelea kuwatumikia wananchi wa jimbo lake kwa mda wote tofauti na mwanzo alivyokuwa kwenye majukumu ya kitaifa.

Alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais John Magufuli kwa kumwamini na kumpa na nafasi katika serikali yake hadi alipombadilisha na hana kinyongo chochote, ataendelea kufanya kazi chini ya mwenyekiti wa CCM na serikali pale itakapoitajika huduma yake.

Alifafanua kuwa uliona wapi mchezaji akasajiliwa kwenye klabu yake, kisha akaitwa timu ya taifa na siku akiondoka timu ya taifa anasema klabu yenu siichezei.

“Hao wanaosema nataka kujiuzulu ubunge, wanataka kutengeneza jambo la ugomvi. lakini kwangu sioni kama ni ugomvi wala tatizo nimerudi kuwatumikia wananchi wa jimbo kwa kazi mlionituma"

CUF Ya Lipumba Yasema Itashiriki Uchaguzi Mdogo Uliotangazwa

0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya ambaye ytuko upande wa Profesa Lipumba  amesema chama hicho kitashiriki uchaguzi wa ubunge katika majimbo ya Buyungu, Jangombe na kwenye Kata 79.

Akizungumza jana Sakaya alisema chama hicho kimepokea barua kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kikielezwa kuwa majimbo na kata hizo, yapo wazi.

Alisema kutokana na mabadiliko yaliyofanyika NEC na katika vyombo vya Dola ni wazi kuwa wataibuka na ushindi katika chaguzi hizo

“Naomba ifahamike kuwa CUF ipo moja na uamuzi wa chama ni kushiriki uchaguzi,  wanachama wasisikilize maneno ya watu ambao hawahusiki na chama," alisema Sakaya.

Alisema wapo wanaojitambulisha kuwa viongozi wa CUF wanasema hawatoshiriki, si kweli wamachama  na wenye nia ya kutaka kugombea ubunge na udiwani wajitokeze.

"Uchaguzi wa ubunge jimbo la Kinondoni tulilalamikia utaratibu ulivyokuwa na namna NEC walivyokiuka. Ila kw amabadiliko yaliyofanyika sasa, naamini hali itakuwa nzuri,” alisema Sakaya.

Pia nae Profesa Ibrahim Lipumba amewataka wanachama kuzipuuza habari kuwa wamesusia kushiriki chaguzi hizo.

Waziri Majaliwa Afunguka juu ya Wanaojiteka

0
0
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya vyama vya ushirika duniani yaliyofanyika jijini Mwanza Majaliwa amesema, viongozi ambao wanasafilisha fedha za vyama vya ushirika kinyume na utaratibu na baadae kusema kuwa wamevamiwa na kuporwa fedha hizo watawajibishwa kisheria.

"Wizi na ubadhirifu ulioshamiri unadhoofisha maendeleo ya ushirika mjitathimini na kusababisha hasara kubwa na kuwa mzigo wa serikali ili kulipa fedha hizo", amesema Waziri Mkuu Majaliwa

Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa ameongeza kuwa serikali itaangalia upya mpangilio wa mnada wa kahawa mkoani Kilimanjaro na badala yake ufanyike katika mikoa husika inayozalisha kahawa ili mkulima afike ,mwenyewe kwenye mnada na kushuhudia bei halisi.

Hii Hapa Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo ya Uume

0
0
Tatizo hili limekuwa likiwaadhiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baada ya kujiona wapo tofauti sana na wengine kwa kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi 6-8 kwanza upungufu wa vichocheo hivi huchochea ukuaji wa uume chongo ambalo hushambulia nerve ambayo uharibu kabisa ukuaji wa uume, ngiri, punyeto, ambayo huathili misuli ya uume, ngiri huleta maumivu, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, korodani moja kuvimba, kutopata choo vizuri, sababu hizi hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na mara nyingi hata nguvu za kiume ( hamu ya tendo la ndoa) hupungua na kwisha kabisa

GEMBE :Ni dawa inayozalisha na kukufanya uume kukua na kuongezeka
NGEMO : Ni dawa bora ya kuongeza nguvu za kiume

Hukutia hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi mara4 nne bila kukinai au kuchoka pia itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk30-45 kwa mtumiaji pia tunatibu kisukari, bp, ngiri, miguu kuwaka moto KAMA HUNAMDA WA KUFIKA OFISINI KWETU UTALETEWA POPOTE TUPO MBAGALA RANGI TATU

 0753471612/ 0715249530
0623 386 305

DR KUZENZA

Waziri wa Kilimo Akabidhiwa Tuzo Ya Heshima Kwa Kuimarisha Sekta Ya Ushirika Nchini

0
0
Na Mathias Canal-WK, Mwanza
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim M. Majaliwa (Mb) amemkabidhi tuzo ya heshima Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba kwa kazi kubwa aliyoifanya na anayoendelea kuifanya katika kuimarisha sekta ya ushirika nchini katika kipindi cha muda mfupi tangu alipoteuliwa kuhudumu katika nafasi hiyo.

Tuzo hiyo imetolewa jana 7 Julai 2018 wakati wa kilele cha siku ya ushirika Duniani na Mhe. Waziri Mkuu kwa niaba ya wanaushirika ambao ndio wameandaa Tuzo hizo ikiwa ni heshima na Utumishi mkubwa kwa Waziri Tizeba katika kipindi kifupi kwa kurudisha imani ya ushirika kwa wananchi waliokuwa wamepoteza matumaini kutokana na baadhi ya viongozi wabadhilifu kujinufaisha na Ushirika kinyume na utaratibu.

Tuzo hiyo kwa Dkt Tizeba inatolewa wakati ambapo ni siku moja pekee imepita tangu Waziri huyo wa kilimo kutangaza Kiama kwa viongozi na baadhi ya watendaji wa vyama vya ushirika wanaofanya ubadhilifu wa Mali za wanaushirika kwa manufaa yao pekee pasina kuwanufaisha wanachama wote.

Kwa msisitizo mkubwa hapo  Julai 6, 2018 Mhe. Dkt Tizeba alieleza kwa ukali kuhusu ubadhilifu wa rasilimali za ushirika unaofanywa na baadhi ya viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika kwenye hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la wanaushirika Tanzania linalofanyika kwa siku mbili katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.

Kongamano hilo liliambatana na maonesho ya bidhaa na shughuli zinazofanywa na vyama hivyo vya ushirika kote nchini ambapo wanachama wamepata fursa ya kubadilishana uzoefu, na kujadili mafanikio na changamoto wanazokabiliana nazo katika uendeshaji wa sekta ya ushirika nchini na kutoa maoni yao kwa serikali.

Dkt Tizeba amesisitiza kuwa serikali inafanya juhudi mahususi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanahamasishwa na hatimae kujiunga kwenye vyama vya ushirika kulingana na shughuli zao za kiuchumi ili kuondoa dhana kuwa vyama vya ushirika ni kwa ajili ya Kilimo cha Mazao ya biashara ya nchi za nje.

Pia, alisema kuwa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kupitia serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Dkt John Pombe Magufuli- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua na kuthamini mchango wa ushirika wa Taifa katika kuyafikia malengo ya milenia na malengo mbalimbali ya nchi kama uimarishwaji wa sekta ya viwanda, Kilimo, Mifugo, uvuvi na biashara na kuchangia katika ongezeko la kipato kwa wananchi na hatimaye kuchangia katika ukuaji wa pato la Taifa.

Tuzo hiyo ya kuimarisha sekta ya ushirika nchini pia imetolewa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli sambamba na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim M. Majaliwa (Mb).

VIDEO:Taji la Miss Mwanza 2018 limemuangukia Sharon Hedlam

0
0
Mashindano ya kumpata mrembo wa Jiji la Mwanza 2018 yamefanyika usiku wa July 06, Rock City Mall, ambapo mrembo Sharon Headlam amekuwa mshindi wa kwanza na ndio atayeiwakilisha Mwanza kwenye mashindano ya Miss Tanzania 2018.

VIDEO:

Hii Ndio Jinsi ya Mwanamke Kuepuka Kuwa Mchepuko

0
0
Mara nyingi asilimia kubwa ya wanawake hupenda kuwa na wanaume wanaojiweza kiuchumi. Lakini baadae wanapotambua kwamba mwanaume huyo ameshaoa hushangaa sana, huumia na kusema waliwaamini kuwa wako single na kwamba wanaume wote ni mbwa tu.

Wanaume sio mbwa au paka shume, ni nyie wenyewe ndio mnashindwa kuwaelewa na hamtaki kufanya uchunguzi. Mlishaambiwa kwamba nyuma ya mwanaume mwenye MALI na MAFANIKIO kuna mwanamke. Na wewe unataka mwanaume aliyefanikiwa. Unategemea nini?

Kama utakutana na mwanaume ambae ni handsome, ana mali, anaendesha gari nzuri, yuko vizuri kiuchumi, basi huyo sio mumeo mtarajiwa, huyo ni mume wa mtu fulani kwa muda huo. Ni agharabu sana kukutana na mwanaume anayejiweza halafu akawa single, either uwe shareholder au unyang'anye share zote za mwanamke mwenzako kitu ambacho sio busara hata kidogo.

Mume wako mtarajiwa yupo anahangaika kutoka na maisha, anapigania ndoto zake. Huenda yupo shambani, Konda wa Dala dala, yupo anauza duka mahali, anapiga kitabu chuo, au yupo anabeti. Kimsingi yupo anapigania kuchomoka kimaisha. Anakusubiri tu wewe umpe support na back up ya kutosha ili atoke katika umaskini

Nimevumilia Nimeshindwa, Mpenzi Wangu Amerudi Amelewa na Hana Nguo ya Ndani 'Boxer'

0
0
Jamani nasumbuliwa na shemeji yenu ndoa hii ina tabu sana nimevumilia mpaka basi , Jana Mume Wangu karudi nyumbani saa nne usiku amelewa chakari , akajilaza tu kitandani na suti yake , nikaamua nimvue ili alale vizuri , cha kushangaza wadau nikakuta hana Nguo ya Ndani Bukta ama Boxer ambayo alivaa asubuhi baada ya kumpigia pasi....

Sasa nimebaki najiuliza maswali mengi ilikuwaje akaivua na alienda tu kazini na jioni aliniambia anapata moja mbili na marafiki zake?


Bado sijamuuliza nini kilitokea ila naombeni ushauri nifanyaje?

Hatimaye Boeing 787-8 Dreamliner Kutua Leo Tanzania

0
0
RAIS Dkt. John Magufuli leo Jumapili Julai 08, 2018 atawaongoza watanzania katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyonunuliwa na serikali ya Tanzania.

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa alasiri ya jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu ya Rais, Gerson Msigwa na kusema ndege hiyo inatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam majira ya saa 8:00 mchana leo ikiwa inatokeaa Seattle nchini Marekani.

Hii ni ndege ya nne kuwasili nchini kati ya ndege 7 zilizonunuliwa na serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuliwezesha Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kuimarisha huduma zake.
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live




Latest Images