Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live

Tabia za Wasichana wa Tanzania Kulingana na Makabila Yao

$
0
0
1.WASUKUMA:
Hawa ni madem tuseme tu blackbeauty yaani mademu wana ngozi smooth ya kupendeza sana lakini niweusi kama mkaa but mimi huwapendea one thing. Demu msukuma akikupenda amekupenda for real ("Eti" walivyo mabwegge washaanza kusmile aaaiii..!) Hawa ni mademu hawapendi usafi, sufuria ya kupika chakula ndio wanaoshea nguo ndio wanaogea .na pia kufulia chupi zao. Figure ni nzuri sana sauti poa kama ya rihana lakini tabia ni mbovu.

2.WARANGI
Hawa ni mademu wengine wasupuu sana yaani hawa ndio mungu alicopy paste the real image yake akawapa yaani mademu wameiva poa, rangi ya mtume figure nzuri lakini ni wafupi, shida moja tu, wao ni washamba sana wamelogewa kazi za bar.

3.WABENA
Mademu wana sura middle body, figure nzuri lakini ngozi ngumu kama ya ngamia shida ingine ni kuiga iga kama wachina ushamba nao ni asili yao asipofanya kazi ya ndani kwake maisha ni bado.

4.WACHAGA
Hawa ni madem wanajua maisha ni nini yaani madem wako na bidii sana lakini shida ni wezi!!! sura wako poa sana,body figure aina shape yaani yao wengi ni flat screen na pia ziko shapeless.

5.WANYAKYUSA
Hawa ni mademu wana tabia nzuri yaani mademu watulivu but shida ni sura aipo sura haiko, body na figure iko D ni watu wako hardworking sana ushamba pia upo kwa wingi hupenda Kujivunia kuwa washamba.

6.WAZARAMO
Tunajua nyinyi mnajua kupika poa sana, watoto wazuri wameiva lakini matusi yanashinda akili zenu na uvivu yaani demu ameiva lakini akikutusi unafeel tu kumlima makofi kazi yao kubwa kupaka rangi kucha.

7.WAZIGUA
Mademu wasupuu kama mtoto wa Kagame figure poa lakini shida ni kimbelembele na makelele sjui ni nani aliwafunza kulia kisanii kwenye misiba pia mna hasira za kishenzi na utoto mwingi na kujiona eti mnajuuuwa, kumbe hewa tu.

Asante na matusi nishazoea ila ukweli tutawaeleza tu.

Kenya Yapaa Kiuchumi na Kuwa Katika Nchi za Uchumi wa Kati

$
0
0
Kenya imezidi kuimarika ki uchumi na kujikuta inahama kutoka nchi maskini na kuwekwa kundi la nchi zenye uchumi wa kati duniani na hivo kujikuta inakuwa miongoni mwa nchi 4 zeneye uchumi imara kusini mwa jangwa la sahara.
Saurce BBC.

Ugonjwa wa Ebola Watua Marekani, Mgonjwa wa Kwanza Agundulika

$
0
0
Mgonjwa wa kwanza wa ugonjwa hatari wa virusi vya Ebola amegundulika nchini Marekani, imethibitishwa katika mji wa Dallas, Texas.
Maafisa katika kituo cha afya cha Texas katika hospitali ya Presbyterian wamesema mgonjwa ambaye hakutajwa ametengwa katika hospitali hiyo.
Mgonjwa huyo anasemekana kuwa ni mtu anayeaminika kuambukizwa ugonjwa huo nchini Liberia kabla ya kuonyesha dalili za ugonjwa huo.
Zaidi ya watu 3,000 tayari wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ebola huko Afrika Magharibi na idadi ndogo ya wafanyakazi wa Marekani wa mashirika ya misaada wamepata nafuu baada ya kupelekwa kutibiwa Marekani.
Jumatatu, maafisa wa kituo cha afya cha Texas katika hospitali ya Presbyterian ya Dallas wamesema mgonjwa ambaye hakutajwa jina alikuwa akichunguzwa virusi vya Ebola na ametengwa katika hospitali hiyo.
Shirika la Afya Duniani, WHO limesema mpaka sasa zaidi ya watu 3,000 wamekufa kutokana na virusi vya Ebola, wengi wa waliokufa ni kutoka Liberia.
Nchini Nigeria, nchi yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika kuna wagonjwa 19 waliothibitika kuugua ugonjwa wa Ebola na watu wanane wamekufa tangu mgonjwa wa kwanza kuthibitishwa nchini humo mwezi Julai..
Kuna mgonjwa mmoja aliyethibitika nchini Senegal, lakini hakuna taarifa za kifo mpaka sasa.
Ebola ni ugonjwa hatari wa virusi kuwahi kuzuka duniani.

Jussa Anena - 2/3 Bunge la Katiba Imekwama Angalia Mahesabu Hapa

$
0
0
The game is over!
Kwa mujibu wa Samuel Sitta alivyotangaza jana, jumla ya Wabunge wote wa Bunge la Katiba = 629
Tanganyika = 419
Zanzibar = 210
2/3 ya 210 = 140
1/3 ya 210 = 70
Kwa hesabu ndogo tu hapo ni kwamba kuinyima Rasimu ya Vijisenti theluthi mbili (2/3) ya Zanzibar zilitakiwa zaidi ya kura 70 (kwa maana zikipatikana 71 itakuwa hapana 2/3 ya Zanzibar).
Sasa naomba tuhesabu pamoja. Miongoni mwa wajumbe 210 wa Bunge la Katiba wanaotoka upande wa Zanzibar:
Wawakilishi wa CUF = 33 
Wabunge wa CUF ZNZ = 25
Wabunge wa Chadema ZNZ = 4
Wana UKAWA walotoka ZNZ miongoni mwa 67 = 5
Walopiga wazi HAPANA jana = 7
Wajumbe wawili (Mwanasheria Mkuu wa SMZ Othman Masoud na mjumbe Abdalla Abbas) hawakupiga kura = 2
Jumla = 76
Kuinyima two thirds ya Zanzibar ilitakiwa anything above 70 out of 210. 
Hapa pana 76
Kwa lugha rahisi kufahamika ni kwamba Katiba inayopendekezwa haitopita maana haikupata theluthi mbili ya Zanzibar.
Hapa hatujui matokeo ya kura zilizopigwa SIRI. Pia wapo wale waliotajwa kwamba wameorodheshwa watapiga kura wakiwa nje ya Bunge Maalum. Lakini hata ukichukulia zote zitakuwa NDIO basi haziwezi kubadilisha uhalisi na ukweli wa kitakwimu uliopo hapo juu.
Kwa kifupi ni kwamba theluthi mbili ya kura za Wajumbe wote wa Bunge la Katiba wanaotoka Zanzibar HAIPO.
Sijui wale waliolazimisha kuendelea na Bunge Maalum la Katiba bila ya kupata maridhiano ya pamoja na wakapelekea kutumika mabilioni ya fedha za walipa kodi masikini wa Tanzania huku wakijua kwamba hawatopata theluthi mbili ya kura za Wabunge wote wa Zanzibar sasa watasemaje?

Nani Alimuelewa Mh.sitta Aliposema Wanataka Kujadiliana na Walio Piga Kura ya Hapana Bunge la Katiba

$
0
0
Wakati wa kipindi cha bunge Jana, kama ambayo wengi wenu humu mlimsikia, mwenyekiti wa Bunge la Katiba Mh. Samwel Sitta alisema ameunda kamati ya maridhiano kwa lengo la kukutana na kujadiliana na wajumbe waliopiga kura ya hapana kwa ibara zote za katiba siku ya jana na aliongezea kuwa sio kitu cha kawaida kwa mtu kukaa muda huo waote bungeni alafu apige kura ya hapana. Ambacho sijakielewa ni,lengo la kujadiliana na waliopiga kura ya hapana ni nini?Baadaya ya mjadala,ina maana wanaweza kupewa fursa ya kupiga kura tena kama watabadili misimamo yao?Ana maana kuwa pia UKAWA walikuwa sahihi kutohudhuria vikao kwani wangeshiriki alafu siku ya mwisho wakapiga kura ya hapana wangeonekana wa ajabu na wangeundiwa kamati ya maridhiano?nilijiuliza maswali mengi bila majibu,walau nianze na haya kwa mwenye ufahamu wa kile kinachoendelea ukizingatia kuwa kuna waliopiga kura ya hapana kwa siri,nao wanatakiwa wahudhurie kikao cha maridhiano au ni vipi?

Gari Aina la BMW Alilopewa Kama Zawadi na Maneja Wake Martin Kadinda Lazua Maneno

$
0
0
Achana na lile gari aina ya Nissan Murano alilozawadiwa na mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, gari lingine aina ya BMW 545i aliloletewa Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ kwenye pati ya ‘bethidei’ yake ni utata mtupu na maswali kibao

NYUMBANI KWA MADAM
Pati hiyo ambayo iliandika historia katika ulimwengu maridhawa wa mastaa iliangushwa nyumbani kwa mwanadada huyo, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar, wikiendi iliyopita ambapo alitimiza umri wa miaka 26.
Katika shughuli hiyo, waalikwa ambao sehemu kubwa walikuwa watu wenye majina, walikula na kunywa kuanzia mchana hadi usiku mnene.

NISSAN MURANO
Akiwa Marekani, Diamond alimuagiza mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ apeleke gari aina ya Nissan Morano lenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 36 za madafu ikiwa ni zawadi ya jamaa huyo kwa mkewe huyo mtarajiwa.

Alipoliona gari hilo, Wema alipigwa na butwaa huku akimshukuru Diamond ambaye kwa sasa amempachika jina la Chibu baada ya lile la Dangote ‘kueksipaya’.

MANENO KUNTU
Huku akiambatanisha na picha ya gari hilo, kupitia ukurasa wake wa Instagram alimwandikia Wema: “Nilitazama nikupe vingi huenda ingesaidia kukueleza ni kiasi gani napenda nikuone ukiwa umefurahi kwenye siku yako hii ya kuzaliwa...lakini tu sina uwezo huo Mumy...tafadhali pokea hicho kidogo hiki nilichojaliwa leo.”

BMW UTATA MTUPU!
Gari aina ya BMW alilokabidhiwa na meneja wake, Martin Kadinda ndilo habari ya mjini huku nyuma yake kukiwa na maswali kibao.
MAMA WEMA AHOJI
Wa kwanza kuhoji alikuwa ni mama mzazi wa Wema, Mariam Sepetu ambaye alikataa kwamba Kadinda hawezi kutoa zawadi ya gari kama hilo hivyo minong’ono ikawa ni mingi.
Baada ya kuona hivyo, Kadinda alitoa kadi ya gari hilo lenye namba spesho za usajili ambapo jina la mmiliki lilisomeka Wema Sepetu.

MKONGO ATAJWA
Hata hivyo, pamoja na utetezi wake, maneno yaliendelea kusambaa kama moto wa kifuu kwamba nyuma ya gari kuna stori kubwa inakuja.

Minong’ono mingine ilikwenda mbele zaidi huku jamaa mmoja mfanyabiashara kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Mkongomani) akitajwa kulinunua na kumpa Kadinda akakabidhi.
Baada ya kuona gari hilo lenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 56 za madafu zinaleta utata, kama kawaida yake, Kadinda alikimbilia kwenye ukurasa wake wa Instagram akaandika:

“....Gari hili linatokana na kazi ndogo tuzifanyazo na sapoti kubwa ya watu wanaotutakia mema. Peke yangu nisingeweza bila sapoti yao....”

MSISITIZO
Akizungumza na gazeti hili juu ya sakata hilo, Kadinda alisema kwa msisitizo: “Ni mimi ndiye nimemnunulia Wema hilo gari.”

MASWALI
Huku Kadinda akisisitiza hivyo, waalikwa walibaki na maswali vichwani likiwemo lile linaloulizwa zaidi kwamba iweje yeye (Kadinda) aendeleshe gari la thamani ndogo aina ya Toyota Corola halafu ampe Wema BMW?
“Hapa pana kitu na kitakapobumburuka itakuwa soo, ni bora Kadinda angefunguka ukweli kuliko kuja kunyooshewa vidole baadaye, ngoja tusubiri,” alisikika mmoja wa mastaa walioalikwa (jina kapuni).
GPL

Bifu la Waigizaji Kati ya Flora Mvungi na Nisha Lafika Pabaya

$
0
0
Stori: Gladness Mallya
WASANII wawili waliowahi kuwa marafiki wa kupika na kupakua, Flora Mvungi na Salma Jabu ‘Nisha’ bifu lao sasa limefika pabaya baada ya hivi karibuni kuwaacha watu midomo wazi kwa kitendo chao cha kupitana kama hawafahamiani.

Ishu hiyo ilitokea wikiendi iliyopita kwenye sherehe ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya staa wa filamu, Wastara Juma iliyofanyika katika ukumbi wa Dar West uliopo Tabata jijini Dar es Salaam. Wawili hao walikutana mlangoni wakati wa kuingia, lakini Flora alimpita Nisha kama hamfahamu na kama hiyo haitoshi, walipoingia ndani, kila mmoja alikaa meza yake.

Wakati sherehe zikiendelea, ukafika wakati wa kufungua shampeni na baada ya tukio hilo, Nisha alipewa jukumu la kuwagawia wageni waalikwa kwa kuwamiminia kwenye grasi zao, lakini alipofika kwenye meza aliyokaa mwenzake, Flora alikataa glasi yake kuwekwa kinywaji hicho.

Baada ya tukio hilo, paparazi wetu aliwafuata mastaa hao na kuwauliza kulikoni, na Flora alisema: “Sikumuona Nisha mimi, na shampeni nimekataa kwa sababu huwa siipendi.”

Kwa upande wake, Nisha alisema: “Mimi sikumuona Flora, kuhusu Shampeni mbona nilimimina kwenye glasi zote jamani!”

Shehe: Aunt Ezekeil Hana Ndoa Tena Kwa Mujibu wa Dini ya Kiislam

$
0
0
Stori: Gladness Mallya na Chande Abdallah
SHEIKH Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa ameweka wazi kuwa msanii nyota wa filamu, Aunt Ezekiel ambaye aliolewa na Sunday Demonte hana ndoa kutokana na kukaa mbali na mumewe kwa zaidi ya miezi sita.

“Hakuna ndoa kati ya mtu yeyote ambaye amezidi miezi 6 bila kukutana na mumewe kwa mujibu wa dini ya kiislamu.

“Kwa kawaida mwanamke ambaye hajakutana na mumewe kwa miezi 6 au zaidi baada ya ndoa yao, hupaswa kwenda mara moja Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) kulalamika na hatimaye kudai talaka, ikiwa mwanamke ameridhika na hali hiyo, naye akaamua kukaa kimya huku akifanya mambo yake na kuanzisha uhusiano na wanaume wengine maana yake amejitoa mwenyewe kwenye mamlaka ya mumewe, hivyo hapo kunakuwa hakuna ndoa tena,”alisema Shehe.
GPL

Aliyemchapa Raila Odinga Bakora za Matako Ashitakiwa

$
0
0
MWANAMUME aliyemshambulia kiongozi wa Cord, Raila Odinga na Gavana wa Jimbo la Kwale, Salim Mvurya ameshtakiwa juzi katika mahakama ya Kwale nchini Kenya.Bwana Lengo Karisa Mudzomba (40), alishtakiwa mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi wa Kwale, Christine Njagi kwa kuwashambulia viongozi hao wawili na kuvuruga mkutano wao katika soko la Kinango Jumatatu ya Septemba 29, mwaka huu. Baadaye mtuhumiwa aliachiliwa kwa dhamana.

Bw Mdzomba alikiri mashtaka hayo na kuomba mahakama impe muda wa kuomba msamaha kutoka kwa wanasiasa hao. “Nimekubali mashtaka dhidi yangu ila naomba mahakama hii inipe muda wa kuomba msamaha kwani kosa si kosa ila kurudia kosa ndiyo kosa,” alisema Lengo.

Mtuhumiwa huyo alidai atahitaji muda wa wiki mbili kufanya hivyo akisema familia yake iko mbali.

Kiongozi wa mashtaka George Mungai alikubali ombi hilo akisema litatoa fursa kwa waathiriwa kujitokeza.

Mahakama iliamua kutaja kesi hiyo Oktoba 14, 2014 na Bw Mudzomba hakupinga.

Mwajiri wa mshtakiwa, Bi Nassim Issa, alisema alishangazwa na tukio hilo kwani hakulitarajia.

Bi Issa alimtaja Bw Mdzomba kuwa mtu mpole, mnyenyekevu na mwenye akili timamu.

“Nimekuwa nikiishi naye kama mfanyakazi wa nyumbani kwa muda wa miezi mitatu na hakuonyesha dalili zozote za upungufu wa kiakili,” alisema Bi Issa.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 60 alifichua kuwa siku ya tukio hilo alimkuta Bw Mdzambo ameketi nje ya nyumba yake akionekana mwenye hasira nyingi.

Shikamoo Wasanii wa Bongo, Naomba Mnijibu Maswali Yangu

$
0
0
1.Mimi nashindwa kuwaelewa kabisa, Hivi ni kweli nyie ni mambo safi? Yaani hela mnazo za kutosha au wanawazushia?
2.Hivi ni kweli zile picha za uchi ninazo ziona kwenye mitandao ya kijamii na magazeti ni kweli au wanawasingizia?
3.Hizo nyumba ninazosikia mnajenga, wengine nasikia wanasema wananyumba nne, je ni kweli ni zenu au ni za kuzugia kibongobongo ili maisha yaende? Kama ni zenu kwanini bado mnakaa nyumba za kupanga?


4.Samahani kwa maswali yangu, nia yangu ni kutaka kutoamini watu wanayo yasema.
Kuna watu nliona na kuhakikisha wanayo yafanya ni kweli Mfano, Mhogo mchungu na Kingwendu wana nyumba kule Mbagala, Ney wa Mitego ana nyumba, Masanja joti na Mpoki, vengu, wakuvwanga wananyumba japo bado baadhi yao hawajamalizia, Madee anagari na kashanipa lifti.


Lady jay dee ana nyumba ana range ana kampuni, Juma nature ana nyumba na benz, Matonya alijengewa nabarabuu japo yeye kamalizia so ni nyumba yake ipo Tanga, Prof.Jay ana nyumba kimara na gari Mbili. Marehemu Kanumba alikua na gari, Ray wa bongo movie ana gari na Mke(chuchu hans) wanaishi pamoja sijajua kama kaoa kihalali sababu huyu mwanamke alikua mke wa mtu.


Dully sykes aka Mr Misifa anamiliki nyumba Tabata ana gari aina Honda anamiriki studio pia(Dhahabu records). Afande Sele kajenga Morogoro.

Ndugu zangu Wasanii, Kuna baadhi yenu sijui wanachokifanya.

1.Diamond nasikia ana hela yaani utajiri unao karibia billion, Kanunua Mtaa Kijitonyama Makumbusho, ana nyumba nne. Hivi haya maneno ni kweli?
Mfano juzi kati alipiga picha kwamba Kanunua V8 kumbe gari ni ya Papa Chifu Kiumbe.

Diamond ana nyumba nne lakini Mbona Mama yake Hamhamishi Pale Tandale Kila siku ya Mafuriko maji yanaingi Ndani?. Kaka Diamond anasema anahela na wasanii wengine lakini Mbona bado amepanga? Kwanini Hajakamilisha nyumba japo moja tu ahamie?

Diamond anasema ana hela, Mbona wacheza show wake Wanaishi Maisha ya dhiki kiasi kwamba kwenda makwao wanaenda kwa kujificha. Wacheza show wapo nane, kwenye hiyo billion ameshindwa kutoa hata mil 50 japo awanunulie magari used?. Anazidiwa na Nyandu tozi anayesomesha Ndugu zake sekondari karibia watoto sita.

Kaka diamond anasema Kanunua Mtaa Makumbusho, Mbona mbona akienda kwa Wema gari anapaki nje?

2.Wema Sepetu sidhani kama kweli Mambo safi, ananitia Mashaka kwa sababu Mara ya kwanza alisema amejenga nyumba Kijitonyama kumbe nyumba ni ya Mama Ngoma Mwisho wa siku akahama na sasa yupo Makumbusho. Siku za nyuma alidanganya Kanunu Gari aina ya AUDI na akawa nanipita eti hi figganigga lakini Mwisho wa siku Akaja kunyang'anywa pale Maeneo ya Namanga na Kampuni ya Majemba sababu gari ilikua ya Kaka CK(Clement huyu anayetembea na Kajala) na alikua hajamaliza kuilipia alipoinunua. Yani ile Gari Clement akua hajamaliza deni kwa mtu aliyemuuzia. Baada ya Kunyan'ganywa Diamond akasema atamnunulia V8. Hadi leo sijaona V8.

Kama Wema na Diamond wangekua na Hela wangeshindwa kulipia kipindi chao cha IN MY SHOES cha channel 5 hadi kimefungwa na Wanadaiwa bado. Kweli wana hela?

Nimetaja hawa baadhi sababu ndio Habari ya Mjini. Naomba Mniondoe ushamba wangu jamani, Hizi hela zenu wasanii Mnaosema Mnahela, Mmeziweka wapi? Au ni kipi cha maana Ambacho mumefanya. Sioni chochote zaidi ya kununua vinywaji, nguo, kuazima Magari, Majungu na Umbea. Naomba mnifafanulie hela zilipo.

Ingependeza Mtu aishi maisha yake kama Anavyo fanya B12. B12 Angarau anajitahidi ana duka pale Mwenge japo wateja sasa wamepungua sababu ya kuhamisha kituo cha basi lakini Maisha kapiga bao. Hana nyodo anatoa hai kwa washikaji. Nia yangu ujirudi kwa sababu umri unaenda na dogo kashaanza shule.

Nyie Bongo Movie Hela zenu zipo wapi? Watu wanashindwa hata kuwasaidia sababu wanajua Mnahela kumbe weupe.
Nawapenda Sana ndugu zangu. Mia

Written By figganigga Via JF

Pozi za Picha za Director Mkubwa wa Video Bongo Zaleta Utata Huko Instagram..

$
0
0
Haya mambo ya instagram sasa sijui ndo coming out the closet au ndo tunaenda sambamba na kina lulu kwa mwendo wa WCW wtva! Jack Wolper upo hapo? Ma selfie hayooo. innanilah......koh!

Soma Comments za Jamii Forums Hapa: Jamii Forums

Alikiba Yuko Wapi..Team Kiba Mko Wapi Mbona Kimya ?

$
0
0
Jamani wale Team Alikiba vipi tena mbona Kimya, Hatumsikii Kabisa Kiba Tena si mlisema Amerudi Upya Kukufuta Kiti chake Mavumbi na Kukikalia
Habari ya mwana imeishia wapi?
Tupeni Update yupo wapi? Show Wapi? Anapanga kufly kwenda kufanya show nchi ipi na ipi?

Eti jamani vitu kama hivyo, hata kama ni Udaku wa uongo nyie tuleteeni tuu Tumpe Kick, acheni kumdrop down mtu wenu Jamani.


Clouds FM Wamshindwa Kumtumia Diamond Kwenye Show zao za Fiesta

$
0
0
Wakati wasanii wakibongo kwa ujumla wao wakihangaika na shoo za Fiesta msimu huu, Diamond ameendelea kujidhihilisha kwamba ni msaanii mkubwa sana kiasi cha jamaa wa Clouds Entertainments kushidwa kumtumia vilivyo mwaka huu kwenye show zao!

Ieleweke kwamba kipindi hiki huwa ni cha neema kwa wasanii nyumbani ambao wengine hufikia kuomba angalau tu wapate fursa japo tu ya kupanda jukwaani kuonana na mashabiki.

Diamond kwa kipindi kirefu sasa amekuwa ni msanii wa Tanzania mwenye show nyingi sana nje ya nchi kiasi kwamba imeshindikana kumbakisha hapa nyumbani kushiriki show za hapa. 

Pamoja na upizani mkubwa mno naoupata kijana ameendelea kukomaa na kujenga heshima hata kwa wale ambao bado walikuwa wabishi kumkubali Diamond.

Tunachoweza kusema kwa sasa ni kumtakia mafanikio mema na aendelee kufanya haya mapinduzi makubwa kabisa kimuziki wa Tanzania. Keep it up Diamond.

Chenge: Asilimia 75 ya mapendekezo ya Katiba Mpya ni ya Tume

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge la Katiba, Andrew Chenge amesema Katiba inayopendekezwa imebeba asilimia 75 ya maudhui ya Rasimu ya iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Chenge alitoa kauli hiyo jana mjini Dodoma alipokuwa akihitimisha michango ya hoja za wajumbe wa Bunge hilo na kamati waliyoitoa wakati wa kuhakiki Rasimu ya Katiba hiyo.

“Bunge hili limeboresha Rasimu ya Katiba vizuri sana. Rasimu hii imebeba asilimia 75 ya maudhui ya Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba (Joseph) na nyie wajumbe mmeboresha kwa asilimia 25 tu,” alisema Chenge.

Chenge, ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), aliwataka wajumbe na wananchi wasidanganywe na tafsiri zinazotolewa pembeni baada ya Mahakama kutoa hukumu yake.

Katika hukumu iliyotokana na kesi iliyofunguliwa na mwandishi wa habari, Saed Kubenea, Mahakama ilitamka kuwa Bunge la Katiba lina mamlaka ya kuboresha na kurekebisha rasimu ya Tume.

“Maoni ya wananchi yamezingatiwa kwa kiwango cha juu sana na matumaini ya Watanzania juu ya Katiba hii ni makubwa. Mambo yao yanayowagusa yamezingatiwa,” alisema.

Picha Instagram: Hamisa Mabeto Atupia Picha Zilizoleta Gumzo na Kuwaacha Watu na Maswali

$
0
0
Wengi sana wamekoment kuhusiana na staa huyu kutupia picha na hili vazi…..Hebu toa maoni yako wewe unasemaje – vazi hili lipo vipi kwa maadili yetu?  Na wakati huo huo  juzi tu amemtambulisha Mpenzi wake.



Kimenuka! Kajala Amshitaki Mama Wema, Kisa Kamili Kiko Hapa

$
0
0
KIMENUKA! Habari ya mjini kwa sasa ni bethidei ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kutimiza miaka 26 tangu kuzaliwa, lakini ndani ya tukio hilo, mengine yameibuka!

Miongoni mwa yaliyoibuka kwenye sherehe hiyo iliyofanyika Jumapili iliyopita nyumbani kwa Wema, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar es Salaam ni madai ya mama Wema, Mariam Sepetu kudaiwa kupewa nafasi ya kutoa ‘neno la hekima’ lakini akaitumia kumvurumishia mitusi aliyekuwa shosti wa Wema, Kajala Masanja.
KUNASWA KWA SAUTI NA PICHA
Baada ya sherehe hiyo, Jumatatu na Jumanne, mitandao mingi ya kijamii ilitumbukiza video yenye sauti ikimuonesha mama Wema akimrushia matusi Kajala kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokana na kukorofishana kwa mwanaye na Kajala aliyewahi kumfadhili mahakamani kwa kumlipia faini ya shilingi milioni 13 asiende jela kwa kesi ya kuuza nyumba iliyokuwa na zuio la kisheria.


KAJALA AAMUA ZITO
Katika kufuatilia sakata hilo, Amani lilinyetishiwa kwamba Kajala baada ya kushindwa kuvumilia, ameamua kumshitaki mahakamani mama Wema.
Chanzo chetu kinadai kuwa Kajala alifikia uamuzi huo baada ya kushauriwa na familia sanjari na wafuasi wake (Timu Kajala) ambapo sasa, timu hiyo na Timu Wema wameingia vitani tena.
“Kajala ameshawasiliana na wanasheria wawili na kutoa maelezo yake, wao wanaandaa faili ili mashitaka yafike mahakamani, amekasirika sana.“Amesema mama Wema ametumia nafasi ya kukutana na watu kumdhalilisha bila kumpa nafasi ya kujitetea, ameona si sawa hata kidogo,” kilisema chanzo hicho ambacho ni jirani na Kajala.

MATUSI YENYEWE
Katika sauti, mama Wema anasikika akitamka matusi (hayaandikiki gazetini)  huku Wema naye anasikika akimsihi mama yake asimtaje jina Kajala kwa kuwa kufanya hivyo ni kumpaisha. Hapa inamaanisha kwamba, Wema alitaka mama yake afunguke lakini bila kutamka jina la mtu.
AGUNDUA TIMU KAJALA IMO NDANI YA BETHIDEI
Katika hatua nyingine, mama Wema alisema kauli iliyoashiria kwamba Timu Kajala ilikuwemo ndani ya bethidei ya mwanaye. “Nasema haya huku najua humu ndani kuna Timu Kajala, lakini nasema….(matusi mazito)”
KAJALA SASA
Baada ya madai hayo yote, juzi, Amani lilimsaka Kajala kwa njia ya simu ili kumuuliza ukweli wa madai hayo. Licha ya kutopokea simu ya paparazi wetu, alitumiwa ujumbe mfupi wa maneno ‘SMS’ na kuulizwa kila kitu.
Hata hivyo, badala ya kujibu alikaa kimya, baada ya dakika kama kumi na tano  alimrushia kwa simu mwandishi wetu video hiyo ambayo anadai kutukanwa na mama Wema bila kusema chochote hali iliyotafsiriwa kuwa kama alisema; ‘hebu oneni wenyewe jamani, nimemkosea nini mama Wema?

ALICHOKIFANYA MARTIN KADINDA
Katika hatua nyingine siku hiyo, meneja wa Wema, Martin Kadinda alikuwa na kazi ya ziada kuhakikisha, mama Wema na mama Diamond, Sanura Kasim ‘Sandra’ hawakai jirani au meza moja licha ya kwamba watoto wao wamependana.
“Kadinda ana kazi ngumu sana, unajua anatakiwa kuhakikisha kwamba mama Wema na mama Diamond hawakai meza moja. Sijui anaogopa nini, kwani hawa si watu ambao watoto wao wana mpango wa kuoana?” alihoji mwalikwa mmoja.
KUMBUKUMBU MUHIMU
Katika bethidei hiyo, Wema alizawadiwa magari mawili, Nissan Murano lenye thamani ya shilingi milioni 36 alilopewa na Diamond na BMW 545i lenye thamani ya shilingi milioni 56, inadaiwa alizawadiwa na Kadinda!

Amber Rose Kaitaja Sababu Nyingine ya kuachana na Wiz Khalifa, Picha ya Ushahidi iko Hapa Pia

$
0
0
Kuvunjika kwa ndoa ya mastaa Amber Rose na Wiz Khalifa kumeendelea kuchukua nafasi kwenye headlines za dunia na hii ni baada ya Amber kutaja chanzo mojawapo cha kuvunjika kwa uhusiano huo.
Kwenye interview ya Radio Amber amesema kingine kilichomkasirisha ni kuona Wiz anawaendekeza warembo flani wawili mapacha ambao inaaminika amekua akijihusisha nao kimapenzi.
Amber amesema alipenda kuiokoa ndoa yake ili waendelee kuwa pamoja lakini anaeonekana kukataa kuendelea kuwa kwenye ndoa ni Wiz mwenyewe, Amber anasema hata taarifa za mwanzoni kwamba walitengana siku nyingi kabla ya kutaka talaka zilikua za uongo…. hakufanya maamuzi yao sababu alitaka kuiokoa ndoa yake

Amber amemshutumu Wiz kwa kutoka kimapenzi na hawa mapacha kwenye hii picha hapa chini…

Sitta Akalia Moto, Apambana na Viongozi wa Kikristo

$
0
0
MWENYEKITI  wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta, amejiweka katika wakati mgumu kwa kuzua mgogoro mpya dhidi ya viongozi wa dini ya Kikristo, baada ya kuita waraka wao kuwa ni wa kipuuzi na wa hovyo hovyo.


Huku yeye akisema kuwa waraka wao una lugha ya UKAWA, wao wamesisitiza kwamba ni waraka wa kinabii, kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi.

Wakati yeye akikemea waraka wao, maaskofu wamesema ile ilikuwa sauti kutoka mbinguni, na kwamba anapambana na Mungu.

Wakati yeye akisema waraka wao haukuwa na utukufu wowote, wao wamemfananisha yeye na Goliati wa kwenye Biblia aliyeshindwa na Daudi kwa sababu ya jeuri na matusi kwa Mungu. Wamesisitiza kwamba kwa sababu ya jeuri yake, wataanzia pale atakapoishia baada ya Bunge Maalumu la Katiba.

Juzi na jana asubuhi, Sitta alitoa maneno ya kejeli dhidi ya viongozi wa Kikristo, hasa Jukwaa la Wakristo,  ambao walitoa waraka kuonyesha kutoridhishwa kwao na mwenendo wa Bunge Maalumu la Katiba.

Sitta alitoa kauli hiyo bungeni alipokuwa akielezea mwenendo wa upigaji kura za kupitisha ibara na sura za rasimu ya katiba inayopendekezwa, akisema amekuwa akituhumiwa kwenye mitandao kwamba anadharau maaskofu.

Mwanasheria Mkuu Z’bar akataa rasimu ya Sitta, Wenzake wamwita UKAWA, Wataka Kumpa Kipigo

$
0
0
MWANASHERIA Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, jana alinusurika kupigwa na wajumbe wenzake wa Bunge Maalumu la Katiba baada ya mwanasheria huyo kupiga kura ya wazi ya “hapana,” kukataa rasimu ya Katiba inayopendekezwa na Bunge hilo.

Awali, Othman alikuwa amesusia Bunge hilo na kujiuzulu katika kamati ya uandishi iliyoandaa rasimu hiyo, akidai kwamba hoja 17 za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zimepuuzwa katika katiba mpya.

Jana asubuhi, mwanasheria huyo aliingia ghafla ukumbini, muda mfupi baada ya Bunge kuanza huku baadhi wajumbe ambao hawakuwepo wakati wa kupiga kura, wakiwa wamemaliza kufanya hivyo, lakini wakati Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta, akimalizia matangazo ili kuahirisha Bunge. Ndipo alipotaarifiwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar alikuwa amefika, apewe nafasi ya kupiga kura.

Othman alisimama taratibu, kwa kusitasita mithili ya mtu aliyelazimishwa, akasema, “napiga kura ya wazi, na vifungu ambavyo sivikubali ni ibara ya 2, 9, 70, 71,72,73,74, 75, 128,129,158,159,160,161,243 hadi
251 na nyongeza ya kwanza, vingine vilivyosalia navikubali.”

Vifungu alivyokataa vinahusu mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2), ukuu wa katiba (9), muundo wa muungano (70), utekelezaji wa shughuli za mamlaka ya nchi (71), mamlaka ya serikali ya jamhuri ya muungano (72) na mamlaka ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar yasiyo ya
muungano (73).

Uhusiano kati ya serikali ya jamhuri ya muungano na serikali ya Mapinduzi Zanzibar (74), wajibu wa viongozi wakuu kulinda muungano (75), madaraka ya kutunga sheria (128), utaratibu wa kubadilisha katiba (129), SMZ na mamlaka yake (158), Rais wa Zanzibar na mamlaka yake (159), Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na kazi zake.

Baraza la Wawakilishi la Zanzibar (161) na kuanzia ibara ya 243 hadi 25, inahusu Mfuko Mkuu wa Hazina na Fedha za Jamhuri ya Muungano wakati nyongeza ya kwanza ni kuhusu mambo 16 ya muungano.

Baada ya Othman kupiga kura hiyo, Bunge lilionekana kutaharuki hususani wajumbe kutoka Zanzibar, na muda mfupi baadaye alisimama Yahaya Kasimu Issa na kuomba aruhusiwe aseme kidogo.

“AG amepiga kura wakati kwenye mjadala hakuwepo… na si kwamba alikuwa anaumwa bali kwa kejeli yake ya kuonesha kwamba amesoma.

“Tulitegemea awepo hapa tangu mwanzo lakini yeye akatoroka…hivi mwanasheria kama huyu ana maslahi gani kwa Wazanzibari? Yaani Rais amemteua awe msaidizi wake wa kazi lakini yeye ametoroka…hivi unaweza kutuambia tuna maslahi gani na mtu kama huyu?” Alihoji huku akishangiliwa.

Wajumbe wenzake wa Zanzibar walianza kupiga makofi na kumzomea mwanasheria huyo wakimwita “kamanda aliyekimbia vita, msaliti, UKAWA, hafai aondoke,” na kejeli nyingine, lakini yeye alikuwa mtulivu tu kwenye kiti chake.

Baada ya kuona vurugu hizo, Sitta aliinuka na kutangaza kufunga mjadala huo huku akiwataka wajumbe waache kumwandama mwanasheria huyo kwa kuwa kikatiba na kisheria, anao uhuru wa kuamua anavyoona inafaa kwani mle ndani hajaingia kwa wadhifa wake bali amepiga kura kama mjumbe.

Kauli hiyo ya Sitta, haikufua dafu kwani baada ya Bunge kuahirishwa,Wazanzibari wengi waliendelea kumzomea huku wakiinuka kwenye viti na kuanza kumfuata wakitaka kumpiga.

Baadhi ya viongozi wakuu wa Zanzibar, wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Idd waliingilia kati na kisha askari wa Bunge walizingira eneo hilo na kumwondoa wakimpitisha mlango wa viongozi wakuu.

Matokeo ya Katiba Mpya Haya Hapa, Ukawa Kubalini Matokeo Tujenge Nchi

$
0
0
Matokeo ya Katiba Mpya ndio haya, imepita!, japo Watanzania tulitaka "Katiba Bora", lakini BMK Imetupatia "Bora Katiba!", if you can't get what you want, just take what you get!, hivyo natoa wito kwa Wana UKAWA, na wale waumini wote wa rasimu ya Warioba, tukubali matokeo!, tuweke silaha chini na ku surrender rasmi. CHADEMA sitisheni maandamano na ku concentrate on what is next, ndio most important kuliko hata hii katiba.

Hata akidi kama isingetimia, ingetimilizwa na kura za Ndio hata kama hazikutosha, zimetosheshwa na zisinge tosheleza kupata "Bora Katiba!".

Zingetoshelezwa!, mchezo mzima umemalizwa kwenye kura za siri na kura za nje ya BMK, na maadam kura za siri, hairuhusiwi kusema nani amepiga nini, deal ni kutangaza kura ya siri moja tuu, ila kila aliyepiga ajue hiyo ndie ile kura yake, kiwisha game, The end justify the means.

Huu ni ushindi mkubwa sana kwa Samweli Sitta, huyu awe ndie rais wetu 2015 ili kukamilisha process ya implementation ya Katiba Mpya.

Pasco.
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live




Latest Images