Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live

Juan Cuadrado Akabidhi Jezi kwa Mwenye Namba Yake

$
0
0
Juan Cuadrado Akabidhi Jezi kwa Mwenye Namba Yake
Baada ya kukamilika kwa uhamisho wa Cristiano Ronaldo kutua klabu ya Juventus, mashabiki wa Turin wanahitaji mchezaji huyo kukabidhiwa jezi ya namba yake halisi.

Katika zoezi hilo la jezi anaepoteza zaidi ni kiungo wa Colombia, Juan Cuadrado ambaye anavaa namba saba kabla ya ujio wa Ronaldo.

Mcolombia, Juan Cuadrado kiroho safi amekubali kumuachia jezi hiyo mchezaji mpya wa Juventus, Cristiano Ronaldo baada ya kuandika kwenye mtandao wake wa Twitter kuwa ni heri kumkabidhi. ”Ni vema zaidi kutoa kuliko kupokea,” amesema Cuadrado.
Cristiano Ronaldo mwenye umri wa miaka 33 amejiunga na Juventus ya nchini Italia juzi kwa dau la pauni milioni 105 akitokea Real Madrid.

Ronaldo ambaye ni mshindi mara tano wa Ballon d’Or ametumia misimu tisa Madrid baada ya uhamisho wake wa pauni milioni 80 akitokea Manchester United huku akiondoka na kuwacha rekodi ndani ya klabu hiyo kwa kufunga jumla ya mabao 451.

Nahodha huyo wa Ureno ameondoka Real baada ya kushinda mataji mawili ya La Liga titles, mawili Copa del Rey na mataji manne ya klabu bingwa barani Ulaya.

Gigy Money: Mastaa Tuliobaki ni Mimi na Zari Tu....Wengine Hamna Kitu

$
0
0
Gigy Money: Mastaa Tuliobaki ni Mimi na Zari Tu....Wengine Hamna Kitu
Video vixen na Msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money ameibuka na kudai staa pekee ambaye yupo kwenye level zake ni Baby mama wa Diamond Platnumz, Zari.

Gigy Money amefunguka hayo alipokuwa anaongelea trend yake ya kubadilisha Mawigi na mawiving siku za hivi karibuni.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Gigy amedai yeye na Zari ndio mastaa pekee ambao wanabadilisha nywele kichwani na wengine wote wanakuwa na tabia ya kurudia rudia nywele kichwani.

"Yaani hao wanaojiita mastaa wengi Hawako katika level zangu maana sitaki kufanana nao ndio maana natumia pesa nyingi.

"Hata wewe ukifatilia utajua mademu wanaobadilisha nywele kuna Zari na Gigy na labda nimuweke Irene Uwoya lakini kwa kuwa na yeye ni mtu wa siku nyingi namtoa lakini kwa sasa hivi ni mimi na Zari tu na tunavaa human hair hatuvai plastiki kabisa”.

Lakini pia Gigy Money amedai yeye ni kivutio cha taifa hasa mwili wake umekuwa kivutio kwa wengi ndio maaana anapenda kuchezesha mwili wake na ku twerk Kwenye shoo zake.

Peter Amuwakia Muna Kwa Kusambaza Picha Zake Chafu Mtandaoni

$
0
0
Peter Amtuhumu Muna Kwa Kusambaza Picha Zake Chafu Mtandaoni
Mzazi mwenza wa Muna anayejulikana kama Peter Zachariah amemjia juu mzazi mwenzake na kudai yeye ndiye mtu  aliyehusika kwa usambazaji wa picha zake Chafu Kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Peter alidai kuwa anajua wazi anayezisambaza picha hizo mitandaoni ni Muna kwa nia ya kumchafua kwa sababu Aprili, mwaka huu alirudi nyumbani kwake Mwananyamala-Kisiwani na kujifanya kuwa anapanga vitu vyake ndani ya nyumba hiyo kumbe nia ni kunasa picha hizo.

"Unajua chochote kinachoendelea hivi sasa najua wazi ni mpango wa Muna, anajitahidi kuufanya ili mimi nionekane wa ajabu baada ya kuona watu walivyonichukulia tofauti kwenye kipindi chote cha msiba wa mtoto wetu hivyo anataka kunichafua lakini mimi kwa hilo sitetereki“.

Peter amekiri alikuwa Kwenye Mahusiano na mwanamke huyo baada ya kuachana na Muna na kumtaja kwa jina la Rehema na kudai kuwa Muna anamfahamu mwanamke huyo.

"Kinachonishangaza mimi Muna anataka kujifanya huyo mwanamke ni mpya kwake lakini sio kabisa, anajua kila kitu na jinsi alivyokuwa akitangatanga kwa wanaume tofautitofauti, mimi ningeishi vipi kama mwanaume? Nafikiri anajua fika kwa kufanya hivyo atanichafua mimi kumbe anajichafua yeye”.

Mgogoro wa Muna na mumewe ulijulikana hadharani hivi karibuni mara baada ya mtoto wao kipenzi Patrick kufariki nchini Kenya alipokuwa amekwenda kutibiwa.

Mara baada ya Patrick kufariki, mjadala mzito uliibuka mitandaoni ambapo kuna baadhi walisema baba yake ni Mtangazaji wa Clouds TV, Casto Dickson aliyewahi kuwa mpenzi wa Muna lakini wengine wakasema ni wa Peter.

Muna alipotafutwa atoe neno kuhusu tuhuma hizo hakupatikana haraka. Siku chache zilizopita Muna alitangaza atafanya mkutano na waandishi wa habari na kujibu tuhuma zote.

Machangudoa Watiwa Mbaroni Kwa Kuwauzia Ngono Wanafunzi

$
0
0
Machangudoa Watiwa Mbaroni Kwa Kuwauzia Ngono Wanafunzi
Jeshi  la Polisi mkoani Katavi limewakamata wanawake 14 wanaodaiwa kufanya biashara ya kuuza miili yao maarufu ‘madadapoa’ au  'Machangudoa', ambao inadaiwa wateja wao wakubwa wakiwa wanafunzi wa kiume wa sekondari.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda, alisema watuhumiwa hao walikamatwa juzi usiku kufuatia msako uliofanyika katika Mtaa wa Majengo maarufu ‘Mtaa wa Fisi’ katika Mji wa Mpanda Manispaa ya Mpanda, huku akisisitiza msako huo ni endelevu.

Alibainisha kuwa msako huo ulifanyika katika madanguro matano na nyumba ya kulala wageni jirani na kituo cha mafuta cha Allyen katika Mji wa Mpanda.

Kamanda Nyanda alieleza kuwa madada hao kabla ya kupelekwa mahakamani, watachukuliwa alama za vidole vyao na kupigwa picha.

Alisema msako huo umefanywa kufuatia malalamiko ya wazazi kuwa wanafunzi wa kiume wa sekondari ni miongoni mwa wateja wa uhakika wa ‘madadapoa’ hao, huku wakionyesha wasiwasi wao wa uwezekano wa kupata maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Taarifa za uhakika zinaeleza wengi wa ‘madadapoa’ hao wanatoka mikoa ya Tabora, Kigoma, Mbeya, Rukwa, Singida, Manyara, Arusha, Dodoma na mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Inadaiwa kuwa ‘dadapoa’ hao awali walikuwa wakifanya biashara hiyo ya kuuza miili yao katika machimbo ya madini ya dhahabu ya Isumamilolo mkoani Katavi, lakini baada ya dhahabu kupungua na biashara yao kudorora, waliamua kuvamia Mtaa wa Fisi na kuendelea na biashara ya kuuza miili yao.

Baadhi yao ambao wamenusurika kukamatwa wakati wa msako huo, walikiri kuwa wamepanga nyumba yote ambapo wanamlipa mmiliki nyumba Shilingi 6,000 kila siku kwa kila chumba, hivyo kwa mwezi kila chumba kinalipiwa Shilingi 180,000.

“Biashara ni nzuri inalipa sana kwani katika siku nzuri napata na kuwahudumia kingono wateja kati ya kumi hadi kumi na watano … wateja wetu wa kubwa ni wanafunzi wa sekondari na vijana wa kiume ambao wanachangamsha sana biashara,” alibainisha mmoja wao.

Mwarabu Akanusha tetesi za Kutimuliwa WCB

$
0
0
Mwarabu Akanusha tetesi  za Kutimuliwa WCB
Baunsa anayemlinda Msanii wa Bongo Fleva, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ anayefahamika zaidi kwa jina la Mwarabu Fighter amefungukia tetesi zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa amefukuzwa kazi na nafasi yake imeshikiliwa na mtu ambaye tunamuona hivi sasa akiwa anamlinda Mbongo fleva huyo.

Mwarabu amekanusha tetesi hizo na kusema kuwa bado yupo WCB na anaendelea kufanya kazi na Diamond kama kawaida, kutokumuona naye ni kwa sababu ya taratibu za kiofisi ambazo hawezi kuziweka wazi ila siku yoyote tutamuona naye.

 Mwarabu amefunguka hayo alipokuwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokwenda kutoa nyuzi alizowekewa siku chache zilizopita baada ya kupata ajali.

COSTECH Waikubali Barua Walioiandikia TWAWEZA

$
0
0
COSTECH Waikubali Barua Walioiandikia TWAWEZA
MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),  Amos Nungu,  amekiri kuwa barua iliyosambaa mitandaoni kwenda taasisi ya utafiti ya Twaweza  ni yao.

Nungu aliyasema hayo leo ofisini kwake wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu barua iliyotumwa na tume yake kwenda Twaweza ikiwataka kujieleza kwa kuendesha utafiti bila ya kibali cha tume yake.

Kiasi cha wiki mbili zilizopita, Twaweza ilifanya utafiti kuhusu hali ya siasa na wanasiasa nchini na kutoa matokeo yake.


Simba Kushitakiwa FIFA Kisa Kakule

$
0
0
Simba Kushitakiwa FIFA Kisa  Kakule
Simbva Kushitakiwa FIFA Kisa  KakuleImeripotiwa kuwa uongozi wa klabu ya Kiyovu kutoka Rwanda umetishia kwenda FIFA kwa madai ya mchezaji wake, Fabrice Kakule, kuonekana na timu ya Simba akifanya mazoezi jijini Dar es Salaam.

Taarifa kutoka Rwanda zinaeleza kwa mujibu wa Rais wa Kiyovu, Jean Pierre, amesema atafanya mipango ya kupeleka mashtaka FIFA akieleza kuwa Kakule bado ana mkataba na Kiyovu ambao unamaliza mwaka kesho.

Pierre amefunguka akiwataka Simba ni vema wakakutana kufanya makubaliano juu ya mchezaji wake badala ya kumsajili kinyemela, jambo ambalo linaenda kinyume na tataribu za usajili wake.

Inaelezwa kuwa Kakule atakuwa anamaliza mkataba wake mwishoni mwa mwezi Julai mwaka kesho hivyo Pierre amewataka Simba kumuachia mchezaji wake mara moja au wakae mezani ili waweze kumalizana.

Kakule tangu awasili nchini amekuwa akifanya mazoezi na mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18 ambacho kipo katika mashindano ya KAGAME yanayoendelea hivi sasa jijini Dar es Salaam.

Dawa Bora za Nguvu za Kiume na Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa

$
0
0

DAWA BORA ZA NGUVU ZA KIUME NA KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA
Baada ya utafiti wa muda mrefu juu ya matatinzo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurundia tendo kwa haraka Sasa inakuletea suluhisho juu ya matatizo haya kwa kutumia dawa za FULL POWER

Full Power dawa asili yenye vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume dawa hii inamchanganyiko wa kutosha kuzalisha vichocheo vingi vya hernone za gestro gen zikiwemo vitamin b6 na b1 vitamin e pamoja na madini aina ya zinc

Itakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wakufanya tendo la ndoa zaidi hatua nne au zaidi na kuchelewa kufika kileleni zaidi ya dakika 20/30 ZAT 50

Inarundisha maumbile ya uume yaani kurefusha na kunenepesha nchi 3/7 na upana cm 3/4 standard.kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukitumia maumbile yatabaki kuwa hivyo siku zote pia anatibu matatizo mengine kama presha kisukari ngiri chango la tumbo kujaa gesi kutopata choo vizuri minguu kuwaka moto matatizo ya uzazi bawasili na magonjwa ya zinaa kama kisonono na kaswende

Tunapatikana Dar es Salaam  na mikoan wasiliana na DR Oshinda no 0755505099 au 0714126118  Karibuni kwa hunduma bora 

Raia wa India ambaye hajakata kucha kwa miaka 66 amefanya maamuzi mapya

$
0
0

Leo July 11,2018 nakufikishia stori hii kutoka huko nchini India ambapo Raia wa nchi hiyo aitwae Shridhar Chillal hatimaye ameamua kuzikata kucha zake za mkono ambazo alikuwa hajazikata kwa miaka 66.

Chillal alianza kuzifuga kucha hizo toka mwaka 1952 na anashikilia rekodi ya Guiness kwa kuwa Mtu mwenye kucha ndefu zaidi duniani huku kucha zake zikitajwa kuwa na urefu wa sentimita 909.

Aidha kwa sasa Chillal ana miaka 82 na ameona ni muda sahihi wa kuzikata kucha zake hizo ambapo imedaiwa kuwa atafanya tukio hilo kwenye jengo moja la makumbusho nchini humo.

Huu Hapa Ugonjwa wa Zinaa Uliogeuka Sugu, Hausikii Dawa

$
0
0

Ugonjwa usiojulikana sana wa zinaa unaibuka kuwa usiosikia dawa ikiwa watu hawatakuwa waangalifu, wataalamu wameonya.

Ugonjwa huo unaojulikana kamaMycoplasma genitalium (MG) hauna dalili lakini unaweza kuwa na madhara ikiwemo kusababisha utasa kwa wanawake.

MG unaweza kukoswa kutambuliwa na kama hautatibiwa vizuri unaweza kuwa sugu kwa madawa.

Shirika la Uingereza linalohusika na afya ya ngono na HIV limeznzisha shuguhli ya kutoa ushauri.

Nakala yake inalaeza jinsi ya kutambua na kutibu ugonjwa wa MG.

MG ni ugonjwa gani?

Mycoplasma genitalium ni bakteria ambayo inaweza inaweza kuambukiza wanaume na kuathiri uume kusababisha vigumu kupitisha mkojo.

Kwa wanawake inaweza kuathiri sehemu za uzazi na kusababisha uchungu na hata kuvuja damu.

Ugonjwa huo unaojulikana kama Mycoplasma genitalium (MG) hauna dalili lakini unaweza kuwa na madhara ikiwemo kusababisha utasa kwa wanawake.

Ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kwa njia ngono isiyo na kinga kutoka kwa mtu ambaye tayari ana ugonjwa huo, Mpira wa kondomu unaweza kuzuia maambukizi.

Mara ya kwanza ugonjwa huu ulitambuliwa nchini Uingereza mwaka 1980 na unaaminika kuwaathiri asilimia moja au mbili ya watu wote.

MG mara nyingi hauna dalili na hautaji wakati wote matibabu lakini unaweza kukosa kutambuliwa au kuchukuliwa kuwa ugonjwa tofauti.

"Matumizi wa kondomu"

Kuangamziwa ugonjwa wa MG kwa kutumia aina moja ya dawa inayofahamika kama macrolides, kumeshuka kote dunaini. Usugu wa ugonjwa huu unakadiriwa kufikia asilimia 40 nchini Uingereza.

Hata hivyo dawa moja inayojulikana kama azithromycin bado inautibu mara nyingi.

Dr Peter Greenhouse, mshauri wa masuala ya ngono huko Bristol anawashauri watu kuchukua tahadhari.

"Ni wakatai ambapo watu wanafahamu kuhusu Mycoplasma genitalium," alisema.

"Kuna sababu nzuri ya kubeba kondomu wakati wa likizo za msimu wa joto na kuzitumia.

Uwezi Amini Barack Obama na Mkewe Wapo Tanzania, Na Hii Ndio Hotel Waliofikia

$
0
0

HOTELI za Singita Grumeti iliyo kwenye hifadhi ya Taifa ya Serengeti, ambayo imempokea Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama, ni moja ya hoteli zenye hadhi kubwa duniani ambayo imekuwa ikipokea ugeni wa watu mashahuru duniani.

Kabla ya ujio wa Obama na familia yake, Marais wengine wastaafu wa Marekani Bill Clinton aliyewahi kuwa Rais wa 42 wa Marekani na George W Bush nao waliwahi kufikia katika hoteli hiyo.

Taarifa zinaeleza kuwa mmiliki wa kampuni za Microsoft duniani bilionea Bill Gates naye ni miongoni mwa mabilionea waliowahi kufikia katika hoteli hiyo.

Pia bilionea wa Kirusi anayemiliki Klabu ya Chelsea ya Uingereza, Roman Abramovich, alipotembelea nchini Septemba 2009 alilala katika hoteli hiyo.

Mwingine ni bilionea wa kihindi, Mukesh Ambani ambaye kwa sasa anaingia katika orodha ya matajiri 20 duniani aliwahi kufika nchini na kufikia kwenye hoteli hiyo.

Uongozi wa hoteli hiyo haukuweza kupatikana haraka kwa ajili ya kutoa mwelekeo wa gharama zake kwa sasa, lakini baadhi ya vyanzo vyetu ambavyo vimewahi kufika hotelini hapo, vinadai kwa usiku mmoja gharama hapo ni mamilioni ya shilingi mbali na huduma atakazotaka mteja.

Katika eneo hilo kuna malazi ya kwenye mahema na nyumba za kisasa zilizojengwa katika hali ya kuendelea kulinda uoto wa asili.

Katika malazi hayo, mteja anaweza kuendelea kuangalia wanyama akiwa ndani ya chumba chake na mandhari ya kuvutia iliyozunguka eneo hilo.

Kutokana na mazingira ya asili kuendelea kutunzwa kwenye eneo hilo, wanyama hufika mpaka karibu kabisa na zilipo nyumba ama mahema jambo linaloongeza umaarufu na ubora wa hoteli hiyo.

Katika eneo la hema namba 10 lililoko ukanda wa kaskazini wa hifadhi hiyo, jirani kabisa na eneo la wazi la Kijiji cha Makundusi, Pori la Akiba la Grumeti na Hifadhi ya Wanyamapori ya Ikona, limejengwa vyema kwenye kilima cha Sasakwa eneo ambalo linatoa fursa ya kujionea hifadhi hiyo kwa ukubwa wake.

Kampuni ya Singita inayomiliki hoteli hiyo imekuwa ikijihusisha na uhifadhi wa wanyama katika maeneo kadhaa duniani kwa karibu miaka 25 iliyopita ikimiliki hoteli 12 za kifahari ambazo zimekuwa zikiongoza kwa tuzo za ubora katika maeneo matano ya Afrika.

Taarifa za mitandaoni zinaeleza kuwa wasafiri wengi wenye uwezo kifedha, wamekuwa wakipendelea  kutumia hoteli hizo kutokana na namna zilivyo na maeneo mapana ya kutosha na uzuri wa maeneo yanayozizunguka, ukomo wa idadi ya wageni na magari yanayoingia na upekee wa kuwaona wanyama uwapo kwenye mahema ama ndani ya nyumba.

Inaelezwa kuwa huduma ambazo zimekua zikitolewa zimewafanya wateja wengi kuona mabadiliko katika vipindi vyote vya maisha yao mara wanapoondoka katika maeneo hayo, hivyo kuzifanya kuwa sehemu za kukumbukwa.

Kutokana na ubora wake, Hoteli ya Singita Grumeti Reserves inatajwa kuwa kithibitisho cha utajiri wa vivutio vilivyopo Tanzania, ikitajwa kuwa ni hoteli namba moja duniani, baada ya kuchukua tuzo mara mbili mfululizo.

Tuzo hizo hutolewa kila mwaka na taasisi maarufu ya Marekani ijulikanayo kama US Travel and  Leisure ambayo hujishughulisha na viwango vya biashara ya utalii duniani.

Mmiliki wa hoteli hiyo ni Mmarekani Paul Tudor ambaye ameshawahi kuwekwa kwenye orodha ya mabilionea katika jarida la Forbes ambaye anashirikiana na Luke Bailes wa Afrika Kusini.

Sasakwa Lodge

Hii ni moja ya sehemu ya hoteli iliyopo kwenye kilima kinachoitwa Sasakwa Hill, ambayo imejengwa kwa mawe na matofali, huku paa lake likijengwa kwa bati kisha kuwekewa mawe ya nakshi wanayoyaita ‘slates’ ambayo hupatikana maeneo hayo.

Inaelezwa kuwa ndiyo lodge kubwa kuliko zote hotelini hapo ina vyumba vilivyojengwa kwa mtindo wa “cottages” vipatavyo 15.

Sabora Plains Tented Camp ipo katika eneo tambarare ambalo wageni wengi wanaofika mbugani hapo hupenda kupumzika na kuota jua.

Nyingine ni Singita Explore, Singita Mara River Tented Camp, Faru Lodge, Serengeti House  ambazo zote zimekuwa zikihudumia wateja wake kwa gharama tofauti kutokana na chaguo lao wawapo kwenye hifadhi hizo za Serengeti.

Huyu Rais Mpya wa Mexico Kauzu Kweli, Akataa Ulinzi wa Aina yoyote, No Bodyguards na Usalama wa Taifa

$
0
0

Mexico City, Mexico. Rais mteule wa Mexico, Andres Manuel Lopez Obrador ambaye ameahidi kukaribisha mageuzi nchini mwake amesema raia wa kawaida wa nchi hiyo ndiyo watakaomlinda na wala hapendelei kuona kikosi au kitengo chochote maalumu kikiandaliwa kwa ajili ya kuhakikisha ulinzi wake.

Rais huyo alipata ushindi wa kishindo katika uchaguzi uliofanyika Julai 1, amekuwa akitembea mitaani na kukutana na watu huku akiwa hana walinzi wowote. Katika safari zake hizo amekuwa akizunguka na gari yake aina ya Volkswagen Jetta na hakuna kizuizi chochote kinachoweza kukwamisha kukaribiwa na watu.

Katika tukio la karibuni, mmoja wa wafuasi wake alifanikiwa kuwapita walinzi waliokuwa katika jengo la Ikulu na kumkaribia na kisha kumkumbatia. Alikuwa amekwenda Ikulu kukutana na Rais anayemaliza muda wake, Enrique Pena Nieto.

Akizungumzia tukio hilo, Lopez Obrador alisema “Ngoja sauala hili liwe wazi. Sihitaji walinzi. Inamaanisha kuwa wananchi ndiyo watakaonilinda mimi,” alisema mwanasiasa huyo ambaye ataapishwa Disemba 1. Aliongeza akisema “Matumaini yangu hawatanidhuru,”. Kitendo chake hicho cha kukataa walinzi kimekosolewa vikali na baadhi ya wataalamu wa masuala ya usalama wa taifa na ulinzi wa viongozi.

OFA!OFA!OFA Je Umepungukiwa Nguvu za Kiume na Umetumia Dawa Bila Mafanikio?

$
0
0

OFA!OFA!OFA je umepungukiwa nguvu za kiume na umetumia dawa bila mafanikio? sasa utapona kwa sh 15000 tu ofa ni kwa watu kumi wakwanza kila siku ofa hii itadumu ndani ya wiki 2 baada ya hapo bei itakuwa nyingine na kama hujapona tunakurudishia hera yako ! 

Dawa hii ni dawa ya maajabu huwezi kuamini Ila wengi wameiamini, inatibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na utapewa garantee ya mwezi mmoja dawa hii inapatikana hapo hapo ulipo nyumbani kwako na tutakupatia maelezo ya namna ya kuiandaa wewe mwenyewe na baada ya kuiandaa utakunywa Mara moja tu,na hautatumia dawa yoyote ya nguvu za kiume dawa hii inawafaaa watu kuanzia miaka 18 mpaka miaka 70 zaidi ya miaka hyo haitakusaidia ni dawa ya asilia haina madhara yoyote. 

Watafiti na waganga wameikubali pia hii dawa inawafaa hata wanawake wasiopata hisia za mapenzi pia tunaweza kukutumia dawa popote ulipo lakini c kwa bei ya ofa ukiitumia dawa hii unakuwa na uwezo wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara 3 bila hamu kuisha na itakufanya uwe na uwezo wa kufanya tendo la ndoa muda wowote imesaidia watu zaidi yawatu 148 ndani ya mwakammoja tangu igunduliwe Dr kiboko mganga wa tiba za jadi toka kisiwani mafia pia tunatibu magonjwa mbalimbali kurudisha mpenzi aliye kuacha,biashara iliyoyumba, kuondoa mikosi, nyota na nk maelezo zaidi Wasiliana na Dr kiboko 0679923297

Ushauri wa Nikki Mbishi Baada ya Basata Kutaka Mapato "Wasanii Tutafute cha Kufanya Sanaa Ishakufa"

$
0
0
Ushauri wa Nikki Mbishi  Baada ya Basata Kutaka Mapato  "Wasanii Tutafute cha Kufanya Sanaa Ishakufa"
Kufuatia mabadiliko mbalimbali yaliyotangazwa na BASATA kwa wasanii wa muziki na waigizaji wa filamu nchini Tanzania, Rapper Nikki Mbishi ameibuka na ushauri kwa wasanii wa muziki.


Rapper Nikki Mbishi kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa kwa sasa wasanii wa muziki watafute kazi nyingine ya kufanya kwani ya sanaa ya muziki nchini imeshakufa na hakuna namna.

“Kwanza kampuni zenyewe hazitoi deals kwa wasanii directly mpaka middleman ahusike na analipwa cha udalali bado BASATA nao wanataka hapo hapo duh, wasanii tutafute cha kufanya sanaa ishakufa, chemchemi za mapato zinazidi kukauka..Ukisoma ajira hakuna,ukijiajiri vikwazo juu ya vikwazo mpaka ujasiriamali unakushinda,mbona awamu tutarudi vijijini kuchoma mkaa na Best Nasso japo Wizara ya mali asili na utalii nayo itakuja kubana tena.“amesema Nikki Mbishi na kuifungukia serikali.

“Laiti Serikali ingetazama uwiano wa waajiriwa na waliojiajiri isingeweka terms kandamizi kiasi cha watu kujipiga mpaka risasi wenyewe maana tunakoelekea Mungu sitiri..Nchi yako mwenyewe ila unaweza hata kukufuru ukajiuliza “Hivi mimi nafanya nini hapa Duniani?”. Kuna siku biashara ya muziki wetu itakuwa kama ile ya kuuza madawa ya kulevya tu,maana utaambiwa santuri zako zote HARAM.“ameandika Nikki Mbishi.

Kwa upande mwingine Nikki wa Mbishi ameenda mbali zaidi na kudai kuwa kama kungelikuwa na uwezekano basi Mungu angepeleka miaka 20 mbele ili kuwe na uwezekano wa kuivunja BASATA kwani haipo kwa ajili ya kulea wasanii.

“Mungu angepeleka mbele miaka hata 20 leo iwe 2038 labda tungeanua matanga ya mawazo mfu tupate mawazo mapya yenye manufaa kwa kizazi kilichopo..Vunja BASATA jenga hata BAR watu walewe maana haitulei bali inatutesa tu,“ameandika Nikki Mbishi.

COSTECH Yaijia Juu Twaweza Baada ya Kusambaza Barua Mitandaoni.

$
0
0
COSTECH Yaijia Juu Twaweza Baada ya Kusambaza Barua Mitandaoni
Wakati taasisi ya TWAWEZA ikipewa siku saba kujieleza ni kwanini isichukuliwe hatua za kisheria kwa kutoa matokeo ya utafiti bila ruhusa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), imesema kuwa imesikitishwa na kusambaa kwa barua hiyo mtandaoni.

Mara baada ya kusambaa kwa barua ya TWAWEZA iliyoandikwa kutokea COSTECH, Kaimu Mkurugenzi wa tume hiyo Dkt. Amos Nungu amesema kuwa baada ya kufuatilia barua hiyo waligundua kuwa ni yao.

“Baadaya kufanya uchunguzi tuligundua kuwa barua inayosambaa mitandaoni ni yetu tulioiandika kwenda TWAWEZA, tunasikitika kuona mawasiliano halali ya kiofisi yanapelekwa mitandaoni hata kabla ya kujibiwa”, amesema Dkt. Nungu.

Dkt. Nungu amesema kuwa COSTECH pekee ndio chombo cha kutoa ushauri katika masuala yote yanayohusu sayansi, teknolojia na uvumbuzi na moja ya majukumu yake ni kusajili na kutoa vibali vya tafiti zote za muda mfupi na mrefu zinazofanywa nchini.

Mwishoni mwa wiki iliyopita TWAWEZA ilitoa ripoti ya utafiti wa sauti za wananchi ukieleza hali ya siasa nchini, ambapo utafiti ulionesha kuporomoka kwa ukaribu wa wananchi na viongozi wa vyama vya siasa.


Nicki Minaj Amtumia Cardi B zawadi ya Dola 5,000 Baada ya Kujifungua

$
0
0
Nicki Minaj amtumia Cardi B zawadi  ya Dola 5,000
Baada ya taarifia kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na ujio wa mtoto wa kike katika familia ya Cardi B pamoja na Offset ambao walibahatika kupata mtoto July 10,2018 Nicki Minaj afurahishwa na taarifa hizo na kutuma zawadi.

Zawadi alizotuma Nicki Minaj zinatajwa kufikia thamani ya Dola 5,000 ambazo ni sawa na zaidi ya Shilingi Milioni 11 za kitanzania ingawa hapo awali wawili hao waliwahi kuhusishwa katika bifu na kukanusha bifu hilo na kuonekana pamoja katika maonyesho ya mavazi ya Met Gala mwaka huu 2018.

Inadaiwa kuwa kwa sasa Cardi B pamoja na Nicki Minaj wamekuwa na ukaribu ingawa wengi wamekuwa wakiwahusisha kuwa wawili hao wanaugomvi.

Nyota wa Filamu za Ngono Aliyemtishia Trump Akamatwa

$
0
0
Nyota wa filamu za ngono aliyemtishia Trump akamatwa
Nyota wa filamu za ngono nchini Marekani Stormy Daniels amekamatwa kwenye klabu moja ya burudani huko Ohio, kwa mujibu wa wakili wake.

Bi Daniels alikamatwa kwa madai kuwa alimruhusu mteja kumgusa jukwaani, "kwa njia ambayo haikuwa ya kingono," wakili Michael Avenati aliandika katika twitter.

Bi Daniels alijikuta kwenye mfarakano na Rais Donald Trrump baada ya kusema kuwa alifanya mapenzi naye mwaka 2006 madai ambayo Trump anayakataa.

Bw Avenatt aliandika katika twitter kuwa Bi Daniels ambaye jina lake kamili ni Stephanie Clifford, alikuwa akicheza mtindo ambao amekuwa akiucheza kote nchini kwenye karibu vilabu 100.

Mwanamitindo Ang'atwa na Papa Akipiga Picha Baharini

$
0
0
Mwanamitindo Ang'atwa na Papa Akipiga Picha Baharini
Kisiwa cha Exuma nchini Bahamas kina umaarufu wa michanga meupe iliopo ufuoni mwa bahari , maji masafi na maneo mengi ya kuvutia.

Hivyobasi mwanamitindo Katarina Zarutskie alipozuru ufuo huo pamoja na mpenzi wake, mwezi uliopita alikuwa na ari ya kutumia maeneo mazuri ya fukwe hiyo ya bahari.

Baada ya chakula cha mchana na familia katika eneo linalojulikana kama Staniel Cay, Katarina aliwaona watu waliokuwa wakiogelea karibu na papa mchanga katika eneo moja.

Licha ya familia ya mpenzi wake kuwa na wasiwasi, alikuwa yuko tayari kuingia katika maji hayo ili kupiga picha nao.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 19 anatarajiwa kuanza mafunzi ya shahada mbili za uuguzi na biashara mjini Miami na sio mgeni wa maswala ya bahari baada ya kukuwa akifanya michezo ya baharini nyumbani kwao huko mjini California.

''Kutokana na ufahamu wangu wa kuteleza majini na kuogelea chini ya maji najua kwamba papa wachanga huwa salama'', aliambia BBC .

Nimeona watu wengi wakipiga picha nao katika mtandao wa Instagram

Samaki huyo amekuwa kivutio cha watalii, akizurura katika gati mbali mbali na kuonekana katika maelfu ya picha zilizosambazwa katika mitandao.

Anasema kwamba baada ya dakika chache za kuchukua mkao , raia mmoja wa eneo hilo alimshawishi kuolea majini huku mwili wake ukiangalia juu.

''Wakati huo watu walikuwa wameanza kupiga picha , nilipokuwa nikilala kuangalia juu nilihisi kitu kimenivuta chini'', alisema.

Babake mpenzi wake alikuwa akimpiga picha Katarina wakati huo, na kwa bahati nzuri akapata kisa chote katika kamera yake.

Kiungo wa JKU Asaini Miaka Mitatu Singida United

$
0
0
Kiungo wa JKU Asaini Miaka Mitatu Singida United
Klabu ya Singida United imefanikiwa kuinasa saini ya  mchezaji Feisal Salum Abdalah “FEI TOTO” kwa kandarasi ya miaka mitatu.

Katika kikao cha pamoja cha Uongozi wa JKU na Singida United, wameshakubaliana gharama za kufidia mkataba (transfer fee) wa miaka miwili ambayo mchezaji huyo alibakiza kuitumikia JKU.

index
Toto ambaye alikuwa akihusishwa kutua Yanga amefikia makubaliano na uongozi wa Singida kwa kusaini kandarasi hiyo na sasa atakuwa sehemu ya kikosi cha walima alizeti hao katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Hii ni mwendelezo wa kukisuka kikosi cha Singida United kilichopo chini ya kocha Hemedi Selemani Morocco ambaye amechukua mikoba kutoka kwa Mholanzi Hans Van Der Pluijm aliyetimkia Azam FC

Kesi ya Tido Mhando Yapigwa Kalenda Hadi Julai 18

$
0
0
Kesi ya Tido Mhando Yapigwa Kalenda Hadi Julai 18
Kesi inayomkabili Mkurugenzi mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando imepigwa tena kalenda na itasikilizwa Julai 18 mwaka huu.

Kesi hiyo ilipaswa kusikilizwa leo Julai 12, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, lakini Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) Leonard Swai alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa shahidi waliyemtarajia atoe ushahidi leo ana udhuru hivyo akaomba kesi hiyo ipangiwe tarehe nyingine.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Shaidi aliipanga kesi hiyo hadi Julai 18,2018 ambapo mashahidi wa upande wa mashtaka wataendelea kutoa ushahidi katika kesi hiyo.

Katika kesi hiyo tayari mashahidi watatu wa upande wa mashtaka wamekwishatoa ushahidi  katika kesi hiyo,  ambao ni Ofisa uchunguzi wa Takukuru, Victor Lesuya, Mwanasheria wa TBC, Gwakisa Mlawa na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TBC, Clement Mshana.

Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh887.1 milioni.

Katika kesi hiyo inadaiwa kuwa Juni 16, 2008,   akiwa Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Tido ambaye alikuwa mkurugenzi wa TBC, kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, jambo  ambalo ni kinyume na Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BVl.

Tido  anatetewa na Wakili Ramadhani Maleta na yupo nje kwa dhamana.
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live




Latest Images