Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

ZITTO:SIWATAJI WALIOFICHA MABILION USWISI NG'O

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amevunja ukimya na kusema hayuko tayari kwa sasa kuwataja Watanzania wenye mabilioni huko Uswisi na kuitaka Serikali ifanye uchunguzi.

Zitto ndiye aliyeibua hoja bungeni kuwa kuna Watanzania walioficha Sh315 bilioni katika taasisi za fedha nchini Uswisi.

Katika taarifa yake aliyoitoa jana, Zitto alisema anasita kutaja majina hayo sasa ili kuepusha kile alichosema majina hayo kutumiwa vibaya bila kujali kama Watanzania walizipata fedha hizo kihalali au la na kuzihifadhi nje ya nchi.

Alisema ameshauri mchunguzi wa kimataifa anafaa kufanya kazi hiyo.

Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), amesema wastani wa Sh729.3 bilioni hutoroshwa kila mwaka kwenda nje ya nchi.

Alisema kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema kwamba yeye (Zitto) hakutoa ushirikiano wa kamati inayochunguza sakata hilo si ya kweli.

“Nataka niwahakikishie, nimekutana mara nne na kamati hii. Nimewapa mpaka jina la mchunguzi wa kimataifa atakayeweza kuwasaidia katika uchunguzi huu, leo naambiwa sitoi ushirikiano,” alisema Zitto.

Alisema mchunguzi huyo wa kimataifa ana uzoefu katika uchunguzi wa suala kama hilo na angeweza kuwatambua kwa majina na kiasi cha fedha na pia uhalali na uharamu wa fedha hizo.

Alisema ameshangazwa na hatua ya Serikali kumbeza pale alipopendekeza suala la kutafutwa mchunguzi wa kimataifa lakini siku chache baadaye ikatangaza magazetini nafasi ya kazi hiyo.

Tangazo hilo lilichapwa Desemba 17, mwaka huu siku ambayo Zitto alisema kwamba angesoma maelezo binafsi kujibu kauli ya Jaji Werema. Hata hivyo, alisema alikosa nafasi. Zitto amesema hashurutishwi na azimio la Bunge kutaja majina hayo kwa sababu yeye siyo chombo cha uchunguzi ambacho kinapaswa kuwa na mkono mrefu.

Alisema wakati akikabidhi majina ya Watanzania hao, angependa ushahidi huo uwe umefanyiwa uhakiki na vyanzo vyake vya kimataifa na vyombo vya usalama vya Serikali nchini.

“Siko tayari kutaja kwa sasa. Narudia tena kwa sasa hayo majina maana naweza kusababisha wahukumiwe na umma bila kupitia utaratibu uliowekwa na sheria zetu hapa nchini,” alisema Zitto.

DAYNA NYANGE AKANUSHA KUHUSISHWA NA UCHAFU UFUKWENI

$
0
0
Mwana muziki wa Bongo freva toka mkoani    Morogoro mwana dada Dayna Nyange, amekanusha kuhusishwa na picha 
zilizomuonesha akifanya uchafu ufukweni akiwa na njemba nusu uchi.  Dayna kupitia page yake ya facebook, ameweka wazi kwamba sivyo kama ilivyoandikwa na baadhi ya mitandao kwamba alfumwa badala yake ilikuwa ni sehemu ya location ya video yake ya wimbo mpya wa mimi na wewe


"Jamani izi ni moja ya Picha.... Tulipokuwa location tuna shoot wimbo wangu wa "Mimi Na wewe" Na sivyo kama ilivyo semekana. Na baadhi ya blogs kwamba nimefumwa beach nikijiachia sijui nini Na nani kha! 

MWAMVITA MAKAMBA AMTIA DONGO LA MAANA JACK CLIFF BAADA YA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA

$
0
0
Hayo ndio maneni ya Mwamvita baada ya habari kuwa Jack Amekamatwa china na Madawa ya Kulevya

NAUZA BIKRA YANGU KULIKO NIITOE BURE HALAFU BAADAE NI JUTE

$
0
0
Watu wamekuwa waongo sana , Utasikia ooohh mi ntakuoa ukinipa, siku akishapa tu anachokitaka anakula kona, mi bora tu niuze yangu, Bei poa kabisaa laki tano za kibongo..hayo ni maneno ya Msichana mmoja kutoka Kenya Alivyoandika kwenye Facebook page yake!! LAANA HII..!!

UHAKIKA..NI KWELI ALIYEKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA CHINA NI JACK CLIFF

$
0
0
Rafiki wa karibu wa video vixen maarufu nchini, Jackie Cliff amethibitisha taarifa zinazoendelea kukua kwa sasa kuwa msichana aliyekamatwa na kilo 1.1 ya madawa ya kulevya aina ya Heroin huko Macau, China ni yeye.

Awali tuliandika kuwa pamoja na jina la mrembo huyo kutajwa na vyanzo vingi kuwa ni kweli amekamatwa, tulichelea kulitaja jina lake ili kuepusha kuandika habari isiyo na uhakika. Rafiki huyo wa Jackie, ambaye pia ni rafiki mkubwa Jux mwenye uhusiano wa karibu na Jackie, Chief Rocka (kiongozi wa kundi la Rockaz) ameandika kupitia Instagram:
“I feel so sorry for jackie…God be with u and help u thru this one…we r human we make mistakes…wuldnt want to jump on judgin u like how other people do….this is Bad…2013 plz its enuf.”

Bongo5 imeongea kwa simu na Chief ambaye yupo masomo nchini China kujua undani wa tukio hilo.
“Amekamatwa kweli,” Chief ameiambia Bongo5. “Nlivyosikia story ni kwamba ametoka Bongo akapita Thailand baada ya kutoka Thailand akaenda Macau, Macau ndio akamatwa. Mimi nilijua sababu nilipigia simu watu wa ubalozini baada ya kupata taarifa tu mara ya kwanza nikawapigia watu wa ubalozi nikawaambia ‘bana, ndugu yetu amekamatwa sasa nataka kujua process ikoje kama kuna kumuona au kama kuna chochote. Kuna ubalozi mwingine mdogo upo Hong Kong wao ndio wakaniambia mambo yalivyo kwamba alikuwa yupo yeye na watu wengine wawili Mtanzania na Mnaijeria, yeye ndo kakamatwa, hawa wengine baada ya kuona wanataka kukamatwa wakakimbia,” Chief ameeleza.
eca86bd9dddf141e387d29
Jackie Cliff aliyekamatwa na madawa ya kulevya akiwa amesimama karibu na meza yalipowekwa madawa yaliyotolewa kutoka kwenye mwili wake
Amesema kwakuwa Jackie amekamatwa Macau ambako kuna sheria tofauti na upande wa bara wa China, adhabu yake inaweza kuwa ndogo kuliko ile ya kunyongwa ambayo hutolewa bara.
IMG_7667
Jackie Cliff akiwa chini ya ulinzi baada ya kukamatwa huko Macau
“Inategemea ukimatwa mainland China halafu labda ukamatwa Macau au kwa Macau na Hong Kong ni kama uko kwetu nikama Tanzania na Zanzibar. Kwahiyo yeye alikokamatiwa ni kama yupo Zanzibar ni ndani ya China lakini inajitegemea lakini sheria zake sio kali sana. Lakini sasa mpaka wajaji kutokana na mzigo walioubeba, wengine wanasema miaka mitatu, wengine minne, wengine wanasema wanatoa kama Hong Kong miaka nane so inategemea na akiisaidia polisi akisema watu aliokuwa akiwapelekea mzigo wapi na wakapatikana, I don’t know.”
85a7de969c6911e29c2822000a1fbe4c_7
Jackie ni mrembo aliyeonekana kwenye video za wasanii kibao wa Bongo zikiwemo She Got A Gwan ya Ngwair, Nataka Kulewa ya Diamond Platnumz, Kimugina na zingine
Hata hivyo Chief amesema ameshangaa kuona jinsi Watanzania wanavyomhukumu mtu kabla ya kujua ukweli wa mambo.
“Yaani hii imereveal jinsi ambavyo Watanzania tuko. Sio kwamba nafahamia sana na Jackie, nimefahamiana naye mara ya kwanza na ya mwisho, sikukaa naye hata kwa wiki tatu, I wouldn’t end up judging someone like how people wanavyojudge kwenye Instagram na mitandao mingine kwamba ‘kapatikana, kaumbuka, bado Jux zamu yake, sijui nini.”
eca86bd9dddf141e39412a
Inadaiwa kuwa madawa haya yalipatikana mwilini mwa mrembo huyo. Madawa hayo aina ya Heroin yana thamani ya shilingi milioni 223
Amesema kuonana na Jackie kwa sasa sio rahisi kwakuwa wengine wasema uwezekano huo unaweza kupatikana mwezi wa tatu mwakani.
Chief ameongeza kuwa hakuna sehemu mbaya na hatari kukamatwa na madawa ya kulevya kama China.
“Navyosema kwamba I feel sorry for her ni kwasababu mimi nimekuwa hapa miaka mitano at least naongea kichina yaani hata wakikifunga you can socialise with people lakini sasa kwa yeye ambaye haiongei,… yaani ukiweka ubinadamu, ukiachana na hayo mambo sijui ya madawa ya kulevya yule ni msichana ni kama wasichana wengine wowote , yaani kama dada yako au demu wako akikamatwa awekwe ndani kwenye nchi ya ugeni ni jambo kubwa yaani especially kwa mtu ambaye umeshamfahamu kidogo huwezi kuanza kumjudge kisa amepost picha ya Benz yake, yaani she is a hardworking woman. Suala la madawa sio zuri lakini sio kila mtu anaweza akafanya.”
Rapper huyo amesema picha zilisombaa mtandaoni zikimuonesha msichana mwenye koti la njano akiwa amekamatwa ni za Jackie.
“Ametoka kwenye gazeti la China Daily, ni gazeti kubwa, ni yeye,” amesisitiza.
Mtandao wa China Daily uliandika: Msichana mwenye miaka 28 kutoka Tanzania alikamatwa kwa tuhuma za kumiliki madawa ya kulevya huko -Macao, Dec 19, 2013. Alikuwa ameficha kilo 1.1 za heroin zenye thamani ya $137,720 ( sawa na zaidi ya shilingi milioni 223) ndani ya mwili wake na kuchukua ndege kutoka Thailand hadi Macao. Alisema alikuwa akielekea Guangzhou, mji mkuu wa jimbo la Kusini mwa China Guangdong.
eca86bd9dddf141e3a492b
Waandishi wa habari wakipiga picha madawa ya kulevya aina ya Heroin yaliyokamatwa pamoja na vitu vingine.
Imeandikwa na Bongo5.com

ITS OFFICIAL! D'BANJ AND GENEVIEVE NNAJI ARE BACK TOGETHER AS LOVERS

$
0
0
This is not rumour o...it's fact. The Kokomaster, 33, and Nigerian screen goddess Genevieve Nnaji, 34, are back together two years after they parted ways and this is a LIB exclusive. Genny is currently staying at D'banj's Lekki home, and I hear they are already talking marriage. Yes I said marriage. Don't know if it will happen, but they are currently talking about it, so in case it happens, remember y'all read it here first. *Wink*.

The loved up couple dated on and off from 2009 to 2011 before Genevieve broke off the relationship because of D'banj's commitment issues. Hope it works out for them this time around! 


DINA MARIOS, RUBEN NDEGE, SIYO SIRI TENA

$
0
0
SIYO siri tena! Uhusiano wa kimapenzi kati ya watangazaji nyota Bongo, Dina Marios na Ruben Ndege ‘Ncha Kali’ sasa upo hadharani.
Kwa muda mrefu Dina na Ruben wamekuwa kwenye uhusiano lakini wamekuwa wakijitahidi kuuficha usijulikane na watu, lakini hata hivyo watu wa karibu hasa wanaofanya nao kazi, walifahamu juu ya uhusiano huo.
Akizungumza katika Kipindi cha Leo Tena kinachorushwa na Radio Clouds Fm ya jijini Dar es Salaam, Ijumaa iliyopita kwa mara ya kwanza Dina alifunguka kuhusu kuwa na uhusiano na Ruben huku akiweka wazi kuwa ana mimba yake.

“Ni kweli baba mtarajiwa wa mtoto wangu ni Ruben Ndege ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Skylight Band. Wengi hapa kazini mnajua kuwa tulianza naye mbali. Kulikuwa na kupanda na kushuka, mara kwa mara lakini nashukuru sasa uhusiano wetu umeimarika,” alisema Dina.
Alisema, katika muda aliokuwa katika uhusiano na Ruben, kuna wakati walikuwa wakiachana na kurudiana lakini anamshukuru Mungu kwa kuwasimamia na kuwafikisha katika hatua hiyo.
Siku hiyo Dina alikuwa akiaga wasikizaji wake, kwa vile atakuwa na likizo ya uzazi ya miezi minne wakati huu akisubiri kujifungua na kumlea kichanga chake.

ITAZAME VIDEO MPYA YA NEY WA MITEGO NAKULA UJANA

$
0
0
Ni video ambayo imefanywa nchini Kenya ambapo Ney anasema ametumia zaidi ya dola za kimarekani elfu saba kuifanya. Video ameiachia rasmi December 31 2013 on AyoTV.

KUNA TAARIFA KWAMBA INADAIWA WAZIRI WA FEDHA DK WILLIAM MGIMWA AMEFARIKI DUNIA LEO ASUBUHI

$
0
0
Taarifa tulizozipata muda mfupi uliopita zinasema kuwa Waziri wa Fedha Dk William Mgimwa Amefariki Dunia leo Asubuhi. Tunaendelea kutafuta ukweli wa jambo hili.

Tutazidi kuwapa taarifa Kadri tunavyozipata kutoka vyanzo mbalimbali vya habari ikiwemo serikali ya Tanzania ili tuweze kujua kama Taarifa za Kifo ni za kweli fununu zisizo kweli.

Updates :
-------------

 Waziri wa Fedha William Mgimwa amefariki dunia leo katika hospitali ya Mediclinic Kloff nchini Afrika Kusini alipokuwa akitibiwa.


Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue, ambaye amesema Mgimwa amefariki majira ya saa 5:20 saa za Afrika Kusini ambapo ni sawa na saa 6:20 kwa majira ya Tanzania

MBOWE AMKARIBISHA SUMAYE CHADEMA

$
0
0
MWENYEKITI wa taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amemkaribisha Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye kujiunga na chama chake ili kuendeleza mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa.

Mbowe alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati wa sherehe za ufunguzi wa jengo jipya la ibada zilizofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Usharika wa Lole Mwika na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na kanisa ambapo Sumaye alikuwa mgeni rasmi.

Alisema hoja ya rushwa inayozungumzwa na Sumaye ambayo CHADEMA imekuwa mstari wa mbele kuipiga vita ina msingi, hivyo viongozi wengine wanapaswa kumuunga mkono na kuliomba kanisa lizidi kuwaombea viongozi wa aina hiyo ili wazidi kupaza sauti zao bila hofu.

“Ndugu zangu hoja ya rushwa iliyozungumzwa mahali hapa na Sumaye ni hoja ya msingi sana, haki katika taifa hili ni bidhaa adimu na wale wanaotetea haki katika taifa hili wengine wanailipa kwa gharama ya maisha yao,” alisema.

Alisisitiza kuwa ni vyema viongozi wakawa na mipaka ya vyama vyao vya siasa na kuwa na lengo moja la kusimamia hatma ya taifa kwa kupigania haki bila uwoga ili kuepusha mateso kwa wananchi.

“Viongozi wote kama tukaamua kusimamia hii hoja bila ya kuona  huyu yuko chama gani, yule yuko chama gani, tukafanya hili suala la rushwa ni la taifa, basi tunaweza kupiga hatua, na kama hatutasahau mipaka ya vyama vyetu hakika nchi hii bado wananchi wa kawaida wataendelea kuteseka sana,” alisema.

Mbowe aliomba kanisa lisaidie katika suala hilo ili kuepusha taifa kupasuka kutokana na viongozi kuweka itikadi mbele na kusahau kuwa siasa ni masuala yanayopita.

Alisema hivi sasa vyama vya siasa vimetafsiriwa kama vyombo vya kugombanisha watu, huku baadhi ya viongozi kwa makusudi wakisahau kuwa vyama vya siasa ni vyombo vya uchaguzi vinavyotumika kupata viongozi.

“Tunauana kwa mabomu, tunauana kwa risasi, tunafungana kwa ajili ya siasa, siasa ni kazi ya kupita, kama Mungu amemuandika mtu kuwa na uongozi atapata uongozi bila ya kujali yuko chama gani, kwa hiyo niombe kanisa lifanye suala la uchaguzi kuwa ajenda ya kudumu ya kanisa,” alisema.

Akizungumzia mwaka mpya 2014, Mbowe alisema ni mwaka wa kutisha kwa watu ambao wapo katika siasa adhimu (active politics) wanaoona namna siasa zinavyobadilika na kuwa ni mambo ya kutishia uhai wa watu.

“Huu ni mwaka wa majaribu makubwa na tunaliomba kanisa lisikae mbali, kanisa lina wajibu mkubwa wa kutusaidia wanasiasa maana tunapokuwa ndani ya nyumba za ibada kama hizi kwa kiwango fulani tunaheshimiana,” alisema.

KIBANDA:MAGUFULI ANASIFIWA TANZANIA WAKATI HANA LOLOTE

$
0
0
Absalom Kibanda: Magufuli anasifiwa Tanzania wakati hana lolote
Akiwa katika kipindi cha TV cha Asubuhi Leo ya Channel Ten, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Bw. Absalom Kibanda amesema Magufuli anasifika sana Tanzania kwa kujenga barabara kwa sababu watu hawajatoka nje ya nchi na kuona wenzetu wanavyojenga barabara. Akasema utamsifiaje Magufuli wakati foleni imejaa na inatisha? Akasema ni watu kuwa na fikra finyu na kutokujua kinachoendelea duniani. 
Hii inanikumbusha maneno ya rafiki yangu mmoja anayefanya kazi Ivory Coast ambaye pia aliwahi kuniuliza hivi Tanzania wanamsifia kwa kujenga barabara zipi? Watu hawajaona wenzetu wanavyojenga barabara. Siyo unatumia trilioni kuikarabati Mandela road kwa lanes mbili zilezile na foleni ikabaki pale pale! Kinachomsaidia Magufuli ni ubabe tu but he is empty!

AUNT EZEKIEL AKIRI MUMEWE KUKAMATWA DUBAI

$
0
0
Na Hamida Hassan
STAA wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amekiri mumewe kukamatwa na kupata misukosuko lakini si kufungwa kama baadhi ya watu wanavyoeneza uzushi.

Akipiga stori na mwandishi wetu hivi karibuni, Aunt alisema mumewe, Sunday Demonte alikamatwa kutokana na viza yake kuisha ambapo alishikiliwa kwa muda na alipokamilisha taratibu za ‘kurinyuu’, aliachiwa.
“Nashangaa sana mambo haya yamevuma kuwa mimi nimemuacha mume wangu amefungwa, ukweli ni kwamba mume wangu yuko huru na hata sasa ukitaka ongea naye, ni mwanamke gani atakuwa na furaha hivi wakati mumewe ana matatizo?” alihoji Aunt.

Katika mistari mingine, Aunt alisema watu wengi wanatamani kuona ameachika au kujua mwenendo wa maisha yake na mumewe lakini wanajidanganya kwani yeye ni mwanamke aliyeamua kuolewa na amefundwa hivyo wataambulia patupu.
“Siyo  rahisi mimi kutoa siri ya maisha ninayoishi na mume wangu, ni makubaliano yetu. Kimsingi ndoa yetu iko imara, watasubiri sana na watachoka wenyewe,” alisema Aunt.

LOWASSA ATANGAZA NIA KIMTINDO

$
0
0

Monduli. Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametangaza kuanza rasmi kwa safari aliyoiita ya matumaini ya ndoto zake, ambayo amesema itatimiza ndoto za Watanzania za kupata elimu bure, maji safi na maendeleo ya uhakika.

Akizungumza katika ibada ya shukrani na kuupokea mwaka mpya, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Usharika ya Monduli Mjini, Lowassa bila ya kutaja safari hiyo ni ipi, aliwashukuru watu wote kutoka maeneo mbalimbali nchini, ambao walimsindikiza katika ibada hiyo.

Lowassa alisema anaamini watu hao waliofika, wana uhakika wa ushindi katika safari hiyo kwa kumtegemea Mungu.

“Nimefarijika sana leo kuwaona hapa marafiki zangu wengi. Ninapowatazama hadi machozi yananitoka na kwa uwezo wa Mungu tutashinda kwani nyote mnajua nia na ndoto yangu,’’ alisema Lowassa na kupokelewa na sauti za shangwe kanisani.

Licha ya kutoweka bayana, Lowassa amekuwa akitajwa kuwa ni mmoja wa wanasiasa wanaowania kumrithi Rais Jakaya Kikwete baada ya kumaliza kipindi chake cha uongozi mwakani.

Azungumzia Katiba Mpya.

Akizungumzia Katiba Mpya, ambayo mchakato wake sasa unaelekea katika Bunge Maalumu, licha ya kuipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Warioba alisema ana wasiwasi juu ya muundo wa Serikali Tatu.

“Nina wasiwasi na huu muundo, ni vyema viongozi wa dini, kuliombea taifa tupate Katiba bora kwani maoni ya watu asilimia 40 ambao hawakutaka muundo wa Serikali Tatu lazima yatazamwe,” alisema Lowassa.

Ibada katika Kanisa hilo, ambayo iliendana na harambee ya kuchangia hosteli na zaidi ya Sh89 milioni kupatikana, iliongozwa na Kaimu Askofu wa KKKT, Usharika wa Kaskazini Kati, Solomon Masango.

Katika mahubiri yake, Kaimu Askofu Masango alimtakia kila la heri Lowassa katika safari yake hiyo akisema anamtambua kuwa ni kiongozi bora.

TAARIFA ZA IKULU KUHUSU KIFO CHA WAZIRI WA FEDHA WILLIAM MGIMWA

$
0
0
Rais Jakaya Kikwete amepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha Waziri huyu wa fedha William Mgimwa na kwamba taifa limempoteza katika kipindi ambacho linamuhitaji zaidi kutokana na mchango wake mkubwa.
Katibu mkuu kiongozi balozi Ombeni Sefue ambae ndio ametangaza kifo cha Waziri huyu kwa niaba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, amesema Mgimwa amefariki saa tano na dakika 20 asubuhi hospitalini Afrika Kusini.
Maandalizi ya kuurudisha nyumbani mwili wa Marehemu yanafanywa na Serikali kwa kushirikiana na familia na kwamba taarifa zaidi zitazidi kutolewa kadri zitakavyopatikana.

ZITTO:NIPO TAYARI KUPOKEA MAAMUZI YA KAMATI KUU YA CHADEMA KESHO

$
0
0
Akizungumza katika kipindi cha Baragumu kinachorushwa na televisheni ya Channel 10, Zitto amesema yupo tayari kupokea maamuzi ya kikao cha kamati kuu ambacho kitakaa kesho.japo anaonyesha maamuzi hayo yatakuwa siyo ya haki.

Zitto amekuwa mpole sana na anaonyesha kujua maamuzi ya kikao cha kesho kitu ambacho anasema yeye kama mwanasiasa lazima ajiandae kisaikolojia.

Ila amesema akishindwa kutafuta haki ndani ya chama basi atatumia katiba kupata haki.

Update:
- Zitto anasema watazunguka nchi nzima. Hii imekuja wakati akijibu swali kutoka Karatu swali je watazunguka na nani? Na kupitia chama gani?



WEMA ASEMA MARTINI KADINDA NDIO MWENYE SIRI YA KILA MAFANIKIO ANAYOYAPATA

$
0
0
MSANII nyota wa filamu Bongo Wema Isack Sepetu amefunguka kwa kudai kuwa hawezi kuvunja urafiki na meneja wake Martin Kadinda kwa sababu kama kuna kitu chochote cha mafanikio nyuma yake yupo Kadinda.

Wema Sepetu ameuambia mtandao wa FilamCentral  kuwa hana rafiki anayejua siri zake zaidi ya meneja huyo ambaye amekuwa akimuongoza vema. 

“Kadinda ndo kila kitu kwangu, hata akiondoka na kukaa mbali na mimi kwa muda mrefu ninapokutana naye tu, nitamweleza kila kitu toka siku ya mwisho tuliyoachana, hivyo inakuwa kama sijapoteana naye,yaani ni kama vile nipo naye kila siku iendayo kwa Mungu,”anasema Wema.

Msanii huyu ameendelea kusema kwamba hata kampuni yake ya Endless Fame film aliifungua kwa msaada wa Kadinda baada ya kumshauri  kuwa kwa hadhi yake anastahili kuwa na kampuni na aache kuigiza filamu za watu wengine.

HOT NEWZZ BANK KUU YA TANZANIA YATOA SARAFU YA SH 50,000/-

$
0
0
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa sarafu maalumu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye thamani ya sh 50,000.

Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, alisema jana kuwa sarafu hiyo iliyotengenezwa kwa madini ya fedha kwa asilimia 92.50, imetolewa kwa ajili ya kumbukumbu tu na haitaingizwa katika mzunguko wala kutumika kwa kulipia malipo ya aina yoyote.

Sarafu hii imetolewa maalumu kama maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar, haitatumika kwa manunuzi. 
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki ya BoT ilimnukuu Profesa Ndulu akisema sarafu hiyo imetolewa kwa idadi ya vipande 3,000 kwa ajili ya tukio hilo na kuwahimiza wananchi kuinunua kwa ajili ya kumbukumbu hiyo.


Kwa mujibu wa Gavana, kutolewa kwa sarafu hiyo kunakwenda sambamba na utaratibu wa Benki Kuu kutoa sarafu maalumu za aina hiyo kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya matukio mbalimbali muhimu ya kitaifa na kimataifa.


“Kwa kawaida, baada ya muda, thamani ya sarafu kama hizi huongezeka na kuwa na faida zaidi kwa wanaozimiliki,” alisema Profesa Ndulu.

Gavana Ndulu alieleza sarafu hizo zitapatikana Januari 5 kwa bei ya sh 50,000 katika matawi ya benki za biashara zitakazokuwa zimepata sarafu hizo kutoka Makao Makuu ya Benki Kuu, Dar es Salaam na matawi ya Benki Kuu yaliyoko Zanzibar, Arusha, Mbeya na Mwanza.

“Benki za biashara zinaweza pia zikasambaza sarafu hizi kupitia matawi yake,” alisema gavana na kuongeza taarifa za usambazaji zitatolewa na benki hizo.

Katika sarafu hiyo, upande wa mbele unaonyesha sura ya hayati Sheikh Abeid Aman Karume na maandishi yanayosomeka: ‘Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi’. 

Upande mwingine wa sarafu unaonyesha nembo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, maandishi yanayosomeka: “Miaka Hamsini ya Mapinduzi”, thamani ya sarafu na miaka 1964-2014.

-Tanzania daima

MAPENZI SHIDAAA...BINTI ANALAZIMISHA NDOA ANATAKA KUNISAIDIA KUTOA MAHARI...USHURI JAMANI...

$
0
0
Awali ya yote nina mwanamke mmoja ambaye tulianza naye mapenzi toka tuanze wote kazi kwa sababu tumeajiliwa sehemu moja ila tu tunatofautiana sehemu ya kufanyia kazi yeye anafanyia wilayani na mimi nafanyia mkoani sasa toka tuanze imefika kipindi akabeba ujauzito na saizi ni miezi mitano tangu abebe huo ujauzito sasa anataka nikatoe mahali kwao ili wanitambue wazazi wake rasmi yeye ndio mpanga mahali na anasema ni milioni moja mahali pamoja na masufuria ya shangazi na babu na branket la bibi.Mimi nikamwambia kuwa hicho kiasi sina akasema kuwa yeye atoe laki nne na mimi nimalizie laki sita na leo kanipigia simu kuwa inatakiwa ipelekwe barua ya kishika uchumba pamoja na elfu therathini mimi pia nikasema kuwa saizi sina hela yeye akasema kuwa mimi niandike barua atakuja kuichukua na ataituma nyumbani kwao kwa njia ya posta na ataiweka hiyo elfu therethini na kuituma nyumbani sasa ninachojiuliza ataka tuoane mapema ili amiliki baadhi ya vitu vyangu na pale tutakapotofautiana tugawane kwa sababu ni kabanda kangu kakisasa kabisa na nikikubali atoe siku tumegombana si ndio ataanza kutamba kuwa nilikutolea na mahali au anaharakisha ili aje tukae wote ili kakibanda kangu afanye kiburi ili tukauze jamani hebu tupeane mawazo na kimri ananizidi yeye ana 28 na mimi nina 25.

RAY C AFUNGUKA ASEMA JACKIE CLIFF ANYONGWE KWA KOSA LA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA

$
0
0
Rehema Chalamila amekasirika na kwa jinsi ambavyo anawachukia wauza unga, hana hata chembe ya huruma kwa Jackie Cliff aliyekamatwa na madawa ya kulevya huko Macau, China mwezi December mwaka jana, 2013.Awali Ray C aliweka picha Instagram ya Jackie akiwa amekamatwa na vyombo vya dola nchini humo bila kuandika chochote, lakini mizuka ya kufunguka ilikuja kupanda baada ya baadhi ya followers wake kumtetea Jackie.Wewe tulia mi na hasira maana najua walichonifanya Hawa wauzaji!?!niliingia kwenye madawa na niliwapa kila Kitu hawa wauzaji ili nipate unga maana tayari nilikuwa nimeshaathirika,hawakunionea huruma pamoja na aibu yote walichotaka wao ni pesa ili nipone ndio niheme!!!!!!nilipokuwa na hela walinithamini ila nilipoishiwa walinilaza kwenye box na arosto!!!niliwaomba hata kidogo ili nisiumwe but hawakunielewa ingawa nilishawapa mamilioni ya hela Na nyumba nikauza!!!!!!!sikia tu arosto na omba isiwahi kutokea kwa ndugu yako wala mtoto wako!!!!!!jinsi mama yangu alivyohangaika Na Mimi k**aninA huyu jacky afe tu mbwa mkubwa!!!!na muuaji ndugu za watu wanalala barabarani mmpaka tunaimbwa teja wa mapenzi!!!!yani acha kabisa!!!wafe wanyongwe,mafirauni wenye dhambi kubwa mbele ya mungu!!!ktk jina la yesu!!!!Wanyongwe!!!!!!!Kill them,” aliandika Ray C.

MKE WA MTU AFUMANIWA UGONI NA MUME WA MSANII WA BONGO MOVIE " THEA"

$
0
0
MWAKA ulianza vibaya kwa mke wa mtu ambaye jina lake halikupatikana mara moja kumkimbia mumewe na kumfuata mume wa msanii wa filamu, Ndumbangwe Misayo ‘Thea’ aitwaye Michael Sangu ‘Mike’ jambo lililosababisha ale kichapo cha nguvu na kuuanza mwaka mpya vibaya.

Tukio hilo lililovuta hisia za wengi, lilitokea siku ya mkesha wa mwaka mpya, usiku wa kuamkia Jumatano, katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, Dar ambapo Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ ilikuwa ikikonga nyoyo za mashabiki wake.
KAMERA ZA IJUMAA
Paparazi wetu aliyekuwa ukumbini humo alimuona Mike akiwa upande mwingine na washikaji zake huku wakiendelea kula raha wakati wa shangwe za mwaka mpya wakati mdada huyo ‘kibonge’ akiwa na mumewe na watu wengine wakifanya yao.

Ijumaa lilipata shaka kidogo, baada ya kumuona dada huyo akimwacha mumewe kila wimbo unapokolea na kwenda alipokuwa Mike kisha kucheza naye.
Harufu ya ugomvi ilianza kunukia mapema, baada ya paparazi wetu kumshuhudia mume wa dada huyo akionekana kumkaripia japo kwa sauti ndogo mkewe kila aporudi akitokea kucheza na Mike.
ONYO HALIKUZAA MATUNDA
Pamoja na onyo alilokuwa akitoa mume huyo kwa mkewe mara kwa mara, bado dada huyo alionekana kumfuata Mike na kucheza naye tena kwa ukaribu kama vile wanajuana.
Baadaye jamaa huyo aliamua kuwashirikisha marafiki aliokuwa amekaa nao meza moja kuhusu tabia ya mkewe, wakamsihi asiende tena kucheza lakini bado hakusikia.

“Sisi tulimwambia, mwenzako hataki uende kucheza na yule msanii, anahisi labda kuna kitu kinaendelea lakini hakusikia, sijui ni pombe zilimzidi au vipi,” alisema mmoja wa watu waliokuwa wameketi meza moja na wanandoa hao muda mfupi baada ya tukio la kichapo kutokea.
Akaongeza: “Kuna wakati alikuwa akijifanya ameelewa, lakini sasa alikuwa akiaga na kujifanya anakwenda msalani halafu mumewe akifuatilia anagundua kumbe amemfuata Mike ili wacheze, jamaa akachukia sana.”
KICHAPO
Baada ya mume kuona dharau za waziwazi zikifanywa na mkewe mbele ya watu aliokuwa amekaa nao, aliamua kusimama na kumfuata alipokuwa akicheza na Mike.
Hakuwa na haja ya kuuliza chochote, alimkamata mkewe na kuanza kumshushia kichapo cha nguvu huku wengi wakiendelea kuponda raha kama vile hakuna kilichotokea.

“Ni mke wake? Hizo ni dharau, acha apigwe. Hawa wanawake wa Dar ni wajinga sana. Utamwachaje mumeo uende kushobokea wasanii? Huu ni upuuzi. Ni haki ale kichapo,” alisikika akisema jamaa mmoja aliyekuwa jirani na paparazi wetu.
DAMU CHAPACHAPA
Hasira zilipompanda yule jamaa, hakuchagua mahali pa kupiga, alimvuta nywele na kumpiga makonde kila sehemu ya mwili wake hali iliyosababisha damu imwagike chapachapa (angalia picha ukurasa wa mbele).
Mashuhuda walipoona damu imemwagika ndipo wakaingiwa na huruma na kuamulia ugomvi huo.

UTETEZI WA MKE
Katika kujitetea, mwanamke yule alimlaumu mumewe kwa kumpiga hadi kufikia kutoa damu kwa kosa la kucheza na Mike akisema kwamba, haoni kosa lake.
“Mume wangu unanionea tu bure, huyu sina uhusiano naye wowote ule... nacheza naye tu kama marafiki. Simfahamu na wala sijawahi kumuona zaidi ya kwenye filamu,” alisema mwanamke huyo.

MIKE HUYU HAPA
Kwa upande wa Mike, alipoulizwa na mwandishi wetu kuhusu kisanga hicho alisema, anamshangaa jamaa mwenye mke kwa sababu amemuonea mkewe bila sababu ya msingi.

 
“Kuna kosa gani watu kucheza muziki? Hapa ni ukumbi wa muziki, tena usiku. Hakuna mipaka, yeyote anaweza kucheza na yeyote. Ule mimi naweza kusema ni ulimbukeni wa kutojua mambo.
“Amemuonea... yule dada alikuwa anafurahi tu sherehe za mwaka mpya ambapo staili yake ya kucheza labda imemkera mumewe lakini kama alikuwa hataki mkewe acheze na mtu mwingine, si wangekaa tu chumbani kwao wawashe redio wacheze wawili tu kuliko kuja kuleta kero kwenye kumbi za burudani?” alisema Mike.
Alipoulizwa hajisikii vibaya kucheza na mke wa mtu alijibu kwa kifupi sana: “Kwanza ningejuaje?”

MADAI MENGINE
Ndoa ya Mike na Thea kwa sasa ipo kwenye mgogoro mzito ambapo wawili hao wametengana huku sababu kubwa ikitajwa na vyanzo vyetu kuwa ni Thea kumtuhumu mumewe kuwa hajatulia.
Bado tunafuatilia sakata hili, likikamilika tutawaletea.

-GPL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images