Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Je hiki Kipigo cha Katiba ni Uthibitisho UKAWA Sii Lolote Sii Chochote, 2015 Ni CCM Tena?

0
0
Kufutia hiki kipigo cha Katiba Mpya kwa kundi la Wana UKAWA, Tume ya Warioba na Watanzania wote wapenda demokrasia ya kweli!, jee kinaweza kuwa ndio kiashiria cha awali kuwa hawa Wa UKAWA sii lolo, sii chochote, hata kama wataunganisha nguvu, na kumsimamisha mgombea mmoja!, na hata mgombea huyo akiwa ndie Joseph Sinde Warioba mwenyewe, bado watapigwa mwereka?!.

Huu unaweza kuwa pia ndio uthibitisho hata CUF, kule Zanzibar sii lolote sii chochote!, 2015 ni CCM Tena?!.

Ni swali tuu!.

Pasco

Steve Nyerere: “Bongo movie watanikumbuka

0
0
MSANII wa filamu Bongo aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amesema kuwa ana mengi ya kujivunia katika klabu hiyo ambayo anaamini yatawafanya wasanii wakumbuke kipindi cha uongozi wake.

Akipiga stori na paparazi wetu, Steve alisema kuna vitu vingi ambavyo ameifanyia Klabu ya Bongo Movie ikiwemo kurudisha heshima katika jamii kwa ujumla kuwa klabu hiyo haihusiani na vitendo vya kifuska bali ni wasanii wanaojiheshimu na kuthamini kazi zao kwa kukemea maovu.

“Naamini wasanii wa Bongo Movie watanikumbuka kwa mengi niliyowafanyia, hata kama wanatazama mabaya yangu lakini yapo na mazuri ambayo ni wazi hayapingiki, niliondoa matabaka pamoja na kufanya mambo mbalimbali ya kimaendeleo ni wazi jinsi ilivyo sasa ni tofauti na nilivyoingia madarakani, nimewakutanisha na fursa mbalimbali na kusimamia nidhamu,” alisema Steve.

Tanzania Yashuka Kiwango cha Uongozi Bora Katika Nchi za Afrika

0
0
Tanzania tumbles in governance index
Dar es Salaam. Tanzania performance in the 2014 Mo Ibrahim Index of African Governance has tumbled—with the country dropping five places—from 10th position in 2012 to 15th in the latest index—that ranked 52 countries in Africa.

But, in the East African region, Tanzania ranks second behind Rwanda, followed by Kenya, Uganda and Burundi.

Ni rahisi sana Sana Kwa Mwanandoa Aliyeajiriwa Hapa Mjini Kuchepuka, Hivi Ndivyo Wanavyofanya

0
0

Nina uzoefu kidogo na mambo ya kazi za ajira maofisini, nimefanya hivi kwa muda mrefu. Wakati flani nilifanya kazi katika ofisi zilizo katikati ya jiji, kule mitaa ya Posta jijini Dar es Salaam.
Ofisi nyingi za serikali na watu binafsi zinapatikana mitaa ile. Kutokana na sababu hiyo, kuna idadi kubwa pia ya migahawa, hoteli, mama ntilie, pub na kadhalika.
Kuna mambo mawili makubwa yenye ushawishi mkubwa wa usaliti. Ofa za chakula au vinywaji na usafiri. Kwa kawaida, wafanyakazi wa ofisi moja hupenda kutoka pamoja wakati wa chakula cha mchana, wenyewe tunapendelea zaidi kusema lunch!
Kila mmoja ana sehemu yake anayokula kulingana na kipato chake, wapo wanaokwenda Southern Sun kupata chakula cha mchana, na wapo wanaowafuata mama ntilie wanaojibanza kwenye vichochoro vingi vilivyopo mjini.
Huko ndiko tunakokutana na akina dada waliovalia vizuri na kupendeza, wakitokea katika maofisi mbalimbali, huwezi kujua yupi ni mhudumu wa chai, yupi ni bosi, wote wanang’ara. Na hapa ndipo ofa za misosi zinapoanza kushawishi ngono.
Kijana mmoja mwenye kipato kikubwa ofisini kwake, atavutiwa na msichana mrembo mwenye mshahara wa wastani. Ili kumsogeza karibu, atalipia chakula cha siku hiyo na kumualika kwa kesho yake. Kulipiwa chakula ni jambo dogo, lakini lenye thamani kubwa sana. Si rahisi mtu aliyekulipia chakula kwa nia njema, ukaacha kumshukuru na hata kumwelekeza unapofanya kazi.
“Mimi nipo pale Oj Traders,” msichana anaweza kujita mbulisha jina na kusema anapofanyia kazi huku mkaka akimweleza kuwa yeye ni mhasibu katika ofisi flani. Watakapo
kutana mara ya pili, wataachiana namba za simu.
Baada ya hapo, mkaka atafanya mbwembwe za kuhamahama maeneo ya lunch ili mradi tu mdada wa watu aingie kwenye laini. 
Ukimaliza suala la lunch, kuna hii kitu foleni, hasa kwa wakazi wa Dar es Salaam. Raha ya kufanya kazi katikati ya jiji inaingia shubiri kadiri jioni inavyozidi kusogea. Kuanzia saa kumi, ni vurugu katika vituo vya daladala na hasa wakati kama huu ambao bodaboda zimezuiliwa kuingia mjini.
Wenye magari binafsi ndiyo wakati wao wa kujidai, ingawa foleni inawakumba wote. Lakini ni afadhali ukiwa kwenye foleni ndani ya gari dogo, mko wawili kuliko foleni, umeshika bomba kwenye daladala.
Siyo rahisi kwa mdada kukataa lifti ya kijana mwenye gari. Na katika foleni ndefu, ni wazi kwamba hadi mwisho wa safari, watakuwa wameshabadilishana namba. Kwa msichana, kuwa na uhakika wa usafiri kila siku ni ukombozi.
Tusidanganyane, hakuna msichana ambaye hatajua kuwa lunch au usafiri anaopewa unahitaji malipo maalum, ambayo ni penzi. Hali hii haiko Dar tu, bali nchi nzima na pengine duniani kote.
Mwanamke aliyeajiriwa anakuwa katika mitihani mikubwa zaidi ya kusaliti ndoa au uhusiano wake, kwa sababu hata kama haitakuwa kwenye chakula au usafiri, bado watu anaokutana nao katika utendaji wake, wanaweza kumghasi. Fikiria anakutana na mabosi, marafiki wa mabosi wake, wafanya biashara, atapona kweli?
Hata hivyo, simaanishi kama tabia hii inawakumba waajiriwa wote, isipokuwa nadhani ni sehemu kubwa wanahusika!
By Mike Tee

Taarifa ya Balozi wa Tanzania China Kuwatishia Wafungu wa Madawa ya Kulevya Waliokamatwa China

0
0
Gazeti la South China Morning Post linadai kuwa Balozi wa Tanzania nchini China Luteni Generali mstaafu Abdulrahman Shimbo amewatishia wafungwa wa Kitanzania walioko magerezani Hong Kong kwa kupatikana na hatia ya kusafirisha madawa ya kulevya nchi humo. Balozi Shimbo anadaiwa kuwaonya wafungwa hao kuwa familia zao nchini Tanzania zitakuwa hatarini kama wafungwa hao wataendelea na kampeni yao ya kuwaonya Watanzania wengine kutojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya. 

Mwezi uliopita Balozi Shimbo alifanya zaira katika gereza la Stanley nchini Hong Kong. "Ziara ya balozi wetu ilikuwa kama janga kwetu" alisema Gervas, ambaye ni moja ya wafungwa katika gereza la Stanely." Gervas aliongeza "Ametukatisha tamaa katika kampeni yetu dhidi ya madawa ya kulevya, ikiwa ni pamoja na kututahadharisha kuwa tuwe makini au tutahatarisha maisha ya familia zetu Tanzania. Pia Balozi Shimbo alienda mabli zaidi na kukosoa kampeni zetu akisema kuwa hazijaleta mabadiliko makubwa".

Hata hivyo, Edmund Kitokezi, ambaye ni afisa katika Ubalozi wa Tanzania uliopo jijini Beijing, amekanusha kuwa Balozi Shimbo amewatishia wafungwa hao na kuongeza kuwa badala yake Balozi aliwapa moyo wa kufunguka zaidi. "Tunaunga mkono kampeni yao - hii ndiyo position ya serikali. Siyo kazi ya ubalozi kumwambia kila mtu aachane na hiyo kampeni" alisema Kotokezi.

Watanzania waliofungwa Hong Kong walianza kampeni yao dhidi ya biashara ya madawa ya kulevya kwa kuandika barua ambazo zimekuwa zikichapishwa na Padri Fr John Wotherspoon katika tovuti yake  Padri Wotherspoon anatoa huduma za kiimani katika magereza huko Hong Kong. 


Kuvunjika Kwa Uchumba wa Rose Ndauka Wanawake Wawili Watajwa

0
0
STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka ameanika ukweli kuhusu uhusiano wake na aliyekuwa mchumba wake Malick Bandawe baada ya kuwagundua wanawake wawili aliozaa nao mbali na yeye.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Rose aliamua kufungasha virago vyake na kurudi kwa mama yake mzazi maeneo ya Kigogo baada ya kugundua kwamba mchumba’ake huyo alizaa na wanawake wawili tofauti na yeye ambaye ni wa tatu.

“Alichokizungumza Malick kwamba alishamuweka chini Rose na kuzungumza naye si kweli, ila yeye Rose aliamua kurudi kwao baada ya kugundua jamaa ana wanawake wawili aliozaa nao kabla yake,” kilisema chanzo hicho.

Akaongeza: “Kile kilichosemwa na  Malick kuwa anasikitika kuona mtoto wake anakwenda kulelewa na mwanaume mwingine ni kujitetea tu lakini ukweli ni kwamba mwanaye analelewa na yeye mwenyewe kwa sababu yuko nyumbani kwa mama yeke.”

Juzi, paparazi wetu alimtafuta Rose kwa njia ya simu yake ya mkononi, alipopatikana na kusomewa madai hayo alikata simu huku akisikika akisema hayuko tayari kufunguka lolote kwa sasa.
GPL

Ukawa Sasa Waja na Tuhuma Nzito Kuhusu kura za Bunge la Katiba

0
0
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umeibua shutuma dhidi ya uongozi wa Bunge Maalumu la Katiba kwamba unawarubuni kwa fedha baadhi ya wajumbe wa umoja huo ili kuipigia kura Katiba inayopendekezwa.

Kamati ya Ufundi ya Ukawa, ilisema jana kuwa wajumbe wanaorubuniwa wapige kura ya ‘ndiyo’ kwa ahadi ya kupewa zaidi ya Sh500 milioni ni wa CUF na wengine wanne wa Chadema wanaotoka Zanzibar.

Hata hivyo, Katibu wa Bunge la Katiba, Yahya Khamis Hamad alikanusha madai hayo, akisema hajasikia kitu kama hicho na ndiyo kwanza alikuwa anasikia hilo kutoka kwa mwandishi wa habari hizi... “Hakuna kitu kama hicho, hilo jambo ndiyo nalisikia kutoka kwako.”

Kutokana na madai hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ukawa, John Mnyika alisema kamati hiyo ilianza kikao cha siku mbili kuanzia jana kujadili hali hiyo na kutoa mapendekezo kwa uongozi wa juu wa umoja huo.

Licha ya Mnyika kukataa kutaja majina ya wajumbe waliorubuniwa, wajumbe wa Chadema wanaotokea Zanzibar ni Zeudi Abdallah ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), Maryam Msabaha, Mwanamrisho Abama na Raya Ibrahim. “Tumewataka wajumbe wetu wote kukusanya ushahidi na kuuwasilisha kwa viongozi wa Ukawa,” alisema Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara.

Aliongeza, “Chadema ina wajumbe wanne, watatu ni wabunge wa kawaida na mmoja wa kuteuliwa na Rais (Kundi la 201). Tumepata taarifa kutoka kwa wajumbe hao kwamba wanapigiwa simu na uongozi wa Bunge ukiwataka wasaini karatasi za kupigia kura ili uongozi wa Bunge uchakachue kura.

“Tumeanza kikao kujadili suala hili ila tumeamua kwanza tuueleze umma kupitia vyombo vya habari juu ya ‘uharamia’ unaofanywa na Bunge la Katiba linaloongozwa na Sitta (Samuel) na Makamu wake Samia (Suluhu Hassan).”

Dada wa Diamond Esma Atoa Mipasho Kupitia Instagram Week Mbili tu Baada ya Kuolewa

0
0
Dada wa Mwanamuziki Diamond Anayejiita Esma Plainum Ambae Ameolewa Hivi Karibuni na Petit Man Amepost Video Kwenye Instagram Page yake Huku Akitoa Mipasho ya Taarabu yenye Kuwananga Wanao Ona Wivu Juu Yake Kuolewa...Baadhi ya Maneno yanasikika Akiimba
'Mwaona Donge la Nini Kama Mnaweza Pandani Juu mkazibe'

Je Kunani Tena ? 

Jionee Mwenyewe Hapa:



Lemutuz Aanzisha Mission ya Kuwashughulikia Wanao Tukana Wengine Kupitia Mitandao ya Kijamii

0
0
Kwa Kile Kinachoonekana ni Kukerwa na Watu wanao tumia Mitandao ya Kijamii Kama facebook na Instagram Kutukana Wengine Mzee Mzima Lemutuz Ameanzisha Misheni ya Kuwakomesha Wale wote Wenye Tabia Hizo Kwa kushirikiana na Polisi..

Hii Hapa Chini ni Message aliyopost Kupitia Ukurasa Wake wa Instagram Leo:

"Good Morning Instagram leo ninarudi tena Polisi Makao Makuu kuendelea na this thing wanyonge wanatukanwa sana kwenye mitandao WHY? Ina maana Serikali ya Tanzania haipo mitandaoni? Wananchi wanaoishi kwa hofu ya kutukwanwa kwenye Mitandao yao wenyewe katika nchi yao wenyewe wataenda kupiga kura kweli? Je wataiamini Serikali yao? Mbona wakitukanwa viongozi Serikali inaonekana mitndaoni ni maswali yanayohitaji majibu ya haraka sana toka kwa Serikali yetu! Kama una tatizo na my mission ichukie my MESSAGE sio mimi cause nawasaidia tu WANYONGE! Na it is ok na my God "- Le Mutuz

Laana! Kijana Adata na Penzi la Nguruwe Huko Sumbawanga….Aamua Kuacha Shule Baada ya Kunogewa

0
0
UNAWEZA kudhani ni Hekaya za Kusadikika! Lakini ni kisa cha kweli kwamba mama mzazi amemshitaki polisi mwanawe wa kiume, ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili mwenye umri wa miaka 16, kwa kile anachodai amechoshwa na tabia ya mwanawe ya kufanya mapenzi na nguruwe wao jike mara kwa mara na hata kujikuta akiacha shule.

Amelalamika akidai kuwa kijana huyo amenogewa `penzi’ la mnyama huyo maarufu hapa kama “kitimoto au noah”, kiasi cha kumfanya aache masomo na kuwa mtoro sugu shuleni.

Nguruwe huyo jike, inadaiwa anafugwa na familia ya mwanafunzi huyo anayesoma katika shule moja ya umma ya sekondari katika Manispaa ya Sumbawanga.

Hayo yalithibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Polisi Jamii mkoani Rukwa, Sixmund Kibassa aliyemweleza mwandishi wa habari hizi jana kuwa mama mzazi wa mtoto, ameripoti tukio hilo katika jeshi polisi.

Kibassa alisifu uamuzi huo, akisema ni mafanikio makubwa yanayotokana na Mpango Shirikishi wa Kitengo hicho wa kuwarejesha shuleni watoto, ambao ni watoro sugu.

Alisema mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa) ni miongoni mwa watoro sugu 70 kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari katika Manispaa ya Sumbawanga, waliorejeshwa hivi karibuni kupitia mpango huo shirikishi wa kuwarejesha watoro shuleni, unaotekelezwa na Kitengo cha Polisi Jamii mkoani humo.

Kibassa alisema wazazi na walezi wenyewe wanafika katika kitengo hicho cha polisi jamii na kuripoti kuhusu watoto wao ambao wamekatiza masomo.

Alisema wazazi na walezi hao, wanafichua kwamba watoto wao hao licha ya kutokwenda shuleni, pia nyumbani hawaonekani na kwamba baadhi yao wamebainika kutumia muda wao mwingi kunywa pombe vilabuni badala ya kusoma.

“Ni juzi tu mama mmoja alinifuata na kuripoti kisa cha mwanawe wa kiume anayesoma Kidato cha Pili katika shule moja ya sekondari, kwamba licha ya kuwa mtoro sugu shuleni, lakini pia amekuwa na tabia chafu ya kufanya mapenzi na nguruwe wao jike mara kwa mara…Nilipomhoji kijana huyo alikiri kufanya hivyo …basi tulimnasihi,“alieleza.

Kwa mujibu wa Kibassa, baada ya kumsihi mwanafunzi huyo, alikubali kuendelea na masomo, ambapo alirejeshwa shuleni kwake na kupokewa na walimu na wanafunzi wenzake kwa furaha.

Akizungumzia tukio hilo, Daktari wa Tiba ya Binadamu, Dk Paulo Maiga alisema mwanadamu kufanya mapenzi na mnyama, kuna madhara makubwa, ikiwemo kuambukizwa virusi ambavyo vikiingia katika mwiliwa binadamu, kuna uwezekano mkubwa visiweze kutibiwa.

“Hili ni tatizo kubwa, madhara yake ni makubwa, huyu nguruwe anaweza kuwa ameshambuliwa na virusi vya ugonjwa ambao ukiingia na kumshambulia mwanafunzi huyo, upo uwezekanao mkubwa kusiwepo na tiba,“ alisisitiza Dk Maiga.

Kweli Mwisho wa Dunia Umekaribia..Embu Ona Huyu Mchungaji Anavyomwombea Huyu Mama

0
0
Wanawake MUNGU awasaidie sana Mjue kujenga Mahusiano binafsi ya karibu na MUNGU mwenyewe kuliko kutegemea sana kuombewa hovyo hovyo,Kisa tu Umeambiwa na Rafiki yako kwamba yuko Apostle flani ana Upako sana.
Ndio ni kweli mna Matatizo mengi yamewasonga yakiwemo Ndoa zenu Watoto wenu,Biashara zenu,na Kadharika,Na mara nyingi nia yenu ni kufunguliwa kwenye hivyo vifungo vinavyowasumbua.Na shetani yuko karibu sana nanyi kwasababu anajua Nguvu iliyomo ndani yenu, ila wengi wenu hamjielewi.Ndio maana Mnafanyiwa vitu vingi sana kwa jina la kukombolewa na baadhi ya Watumishi kwa imani kwamba Mtapona.Na ndio maana kila huduma maombezi Mmejaa nyie na Ndio maana inakuwa rahisi sana kwenu kudhurumiwa mambo mengi kwa kujenga imani kubwa sana kwa watu kuliko BABA yenu.
Hebu tazama picha kama hii,Mumeo akikukuta unafanyiwa Maombi ya Staili hii "Atakuelewa kweli!?
Jifunzeni kumlilia MUNGU vyumbani mwenu na Mkumbusheni ahadi zake juu ya Maisha yenu na vizazi vyenu

Hii Ndio Zawadi Aliyopewa Diamond Jana Kwenye Birthday Yake, Kwa Taarifa yako Haikutoka Kwa Wema

0
0
Jana Ilikuwa Ni Siku ya Kuzaliwa ya Mwanamuziki Anaye Make Headlines Bongo na Nje ya Nchi Diamond Platnumz, Hakika wengi Walisubiri Kuona Mpenzi wake Wema Sepetu Atamzawadia Zawadi gani Kwa Vile Yeye Alizawadiwa gari na Diamond..So Wengi Tulisubiri kuona Atafanya nini ....Lakini Jana Zawadi kubwa iliyotolewa ilikuwa ni Gari Aina la BMW ambalo Diamond Alipewa Zawadi na Management Team yake ..Ikimaanisha kina Babu Tale....Mie Sikuwepo kwenye Party Hiyo kwa anayejua Wema Alitoa zawadi Gani Atujuze Basi Hapo Kwenye Comment.

Kiingereza cha Diamond,The Sporah Show na Kile Cha Shigongo, Straight Talk Africa

0
0
Well,inatia moyo kuona waswahili sasa tunaanza kuwa majasiri wa kufanya interview za kiingereza(JAPO BROKEN) na hasa ujasiri huo unapofikia hatua ya kufanya interview katika vipindi vya TV vinavoangaliwa na watu wengi duniani kote.So,jana tar.30/9 nilimsikiliza Diamond akiamua kuwa jasiri na kupima uwezo wake wa kukimudu kimombo pale alipofanya interview ya kimombo na Mrembo Sporah Njau wa The Sporah Show kinachorushwa Clouds TV kutokea London.

Na wakati huu namsikiliza Eric Shigongo akifanya interview na presenter mahiri wa kipindi cha Straight Talk Africa,Prof Chaka Ssali wa The Voice of Africa.Nawapongeza kabisaaaaaa but man,we can still pick a hole or two in the interviews: (1).The guys are trying too hard to impress and to sound relevant,nafikiri wakati mwingine wasipanie au wasiwe na fikra kuwa ndugu zao tunaowaangalia huku tuwakome,i mean wafanye interview wakiwa totally focused on the issues raised in the interviews na wasitake tunaowasikiliza "tuwakome" (2).Sporah alizungumza Queen's English wakati Diamond alitaka watazamaji tuamini kuwa yeye ni Kanye West au 50 Cent.

Hivyo hivyo Eric Shigongo wants us to believe kuwa yeye ni wa mitaa ya Brooklyn New York wakati yeye ni Msukuma through and through....ninachosema,they need not fake their accent,mbona Chaka Ssali ni profesa na anazeekea Marekani lakini hathubutu kusema accent ya kimarekani?

Yeye bado anapiga kiingereza chake cha Kabale Uganda and he's doing good!Nasema hivi,wanastahili pongezi lakini wazungumze kiingereza cha kawaida tu wasitake kutafuna maneno kama kina Obama,kufanya hivyo kunawaboa viewers because for one,they are not fluent,sasa kama hauko fluent utatakaje kujiongelesha accent ya kimarekani,people!Wanigeria na Wakenya mbona wanaongea tu kivyao vyao and we have come to like Nigerian English'oooo,haven't we?

Hongera Diamond,hongera Shigongo,mna afadhali kuliko Mh.Membe,siku moja nilimsikiliza kwenye kipindi kilekile cha Straight Talk Africa niliboreka sana,sikuona tofauti yake na Mulugo

Kura mbili zapitisha Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, Wabunge Waserebuka Ndani ya Bunge

0
0
 Licha ya upinzani kutoka makundi kadhaa ya wananchi, Bunge la Katiba jana lilihitimisha kazi yake kwa kupitisha Katiba inayopendekezwa baada ya kupata theluthi mbili za wajumbe wa kila upande wa Muungano.

Matokeo hayo yaliyohitimisha mchakato huo, yalifanikishwa kwa tofauti ya kura mbili za wajumbe katika baadhi ya ibara na nyingine kwa kura moja tu, ikimaanisha kuwa iwapo kura hizo mbili zingekosekana hadithi ingekuwa tofauti.

 Kutangazwa kwa matokeo hayo kuliwafanya wajumbe walioshiriki mchakato hadi hatua ya mwisho baada ya wenzao wa kundi la Ukawa kususia, kulipuka kwa furaha, nyimbo, tambo, vijembe na vigelegele huku wakijimwaga ukumbini kusakata dansi.

Akitangaza matokeo hayo, Naibu Katibu wa Bunge hilo, Dk Thomas Kashililah alisema hali ya upigaji kura ilikuwa ni nzuri na kila kura za kila upande zilitosheleza na kutoa uhalali wa Katiba inayopendekezwa kupelekwa kwa wananchi.

Katibu huyo alianza kutoa matokeo ya upande wa Zanzibar ambako wajumbe wengi walikuwa na wasiwasi kuwa huenda usipate akidi ya kura 146 iliyotakiwa.

Kwa jumla, kura za ‘ndiyo’ za Zanzibar zilikuwa ama 147 au 148 na ‘hapana’ ama saba au nane; wakati kwa matokeo ya Tanzania, wajumbe waliopiga kura walikuwa 335 na kura moja tu ndiyo ilikataa ibara zote na kura mbili zilichomoza kukataa baadhi ya ibara.

Matokeo hayo yalithibitishwa na mawakala Amina Makilagi na Waziri Rajabu Salum ambao walisimama na kueleza namna ambavyo kura hizo zilihesabiwa kwa uhuru mpana.

Kuserebuka bungeni

Baada ya matokeo hayo, Ukumbi wa Bunge ulihanikizwa kwa nyimbo za mipasho na mafumbo zikiambatana na kuwashwa vipaza sauti bila ya utaratibu na wajumbe kurukaruka na kukumbatiana kwa furaha.

Hali hiyo, iliwalazimu walinzi wa viongozi kuingia ndani ya ukumbi kwa kuweka hali ya amani kwani wajumbe walianza kuvamia viti vyao kwa nia ya kuwapongeza.

Hali ilipozidi, walinzi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda walimwondoa haraka na kumweka katika chumba maalumu hadi hali ilipotulia huku idadi kubwa ya walinzi ikisogea kwa Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta.

Tazama picha zote za birthday ya Diamond ilivyokuwa jana. Apewa zawadi ya gari aina ya BMW X6

0
0
 Tazama picha zote za birthday ya Diamond ilivyokuwa jana. Apewa zawadi ya gari aina ya BMW X6 na Team ya Uongozi Wake










Kweli Mapozi Kikohozi, Wazidiwa Nakuanza Kufanya Yao Ndani ya Dala Dala

0
0

Kale Ka Usemi kuwa Mapenzi ni Kikohozi Kamedhiirika Juzi Huko Kenya Baada ya Wapenzi Wawili Kuanza Kunyonyana Ndimi Ndani ya Matatu ama Dala Dala Bila Kuona Aibu Kuwa kuna Watu wanawaangalia , Abiria Walibaki na Mshangao tu na kubaki wakishuuhudia sinema ya bure huku wengine wakipiga picha na kuzituma kwenye mitandao ya kijamiii....

Mke Akosea na Kumtumia Mume Wake Picha ya Uchi Aliyokuwa Anamtumia Mchepuko Wake

0
0
Dada mmoja Mitaa ya Migomeni Dar es Salaam Amezua Kioja Baada ya Kumtumia Mume wake Picha ya uchi Kupitia Whats app, Inasemekana Mume alikuwa Kazini Akashangaa Message imeingia kwenye simu yake kucheki ni mke wake kamtumia picha ya uchi , Jamaa anadai toka amuoe huyo dada miezi sita iliyopita hakuwa kumtumia picha kama hizo kitu kilichosababisha jamaa arudi nyumbani na kumshushia kipigo cha Haja Mke Wake Huku Majirani wakishuhudia Mpaka Mke alipokiri kuwa alikuwa anamtumia mtu mwingine ambaye ni mchepuko wake...Baada ya kukiri jamaa alimtupia mizigo yake nje aende kwao...Haya Jamaa Tuweni Makini ...

Kivazi cha Min Sketi Chazua Balaa Huko Arusha, Demu Atamani Ardhi Ipasuke

0
0
Kivazi cha Min Sketi Kidogo Kimtokee Puani Dada mmoja Huko Arusha Mitaa ya Soko kuu Katika ya Mji Baada ya Vijana Kuanza Kumzomea na Kumfuata nyuma Wakitaka Kumshika Makalio , lilikuwa ni tukio la aina yake lililovuta Hisia za watu wengi, Watu walivyozidi ilibidi Dada huyu kukimbilia kwenye Duka moja kujisitiri ndio ikawa salama yake ...Jamani wadada tunapotoka out tujiangalie tumevaa nini ...Vijana huko mtaani wananjaaaaa msije Adhirika..

Belle 9: Sioni Chemistry kati yangu na Diamond Platnumz

0
0
Mwimbaji wa Bongo Flava kutoka Morogoro, Belle 9 hafikirii kufanya collabo na Diamond Platinumz hivi karibuni kwa kuwa bado haoni chemistry (muendano sawa) kati yao.

Akiongea katika Exclusive Friday ya kipindi cha Sunrise cha 100.5 Times Fm, Belle 9 amesema haoni kama kuna chemistry kati yake na mwimbaji huyo ingawa haweki mipaka ya collabo kati yao, ikitokea wamepata kitu wanaweza kufanya.

“Kama ikitokea nina wimbo ambao yeye anaweza kuplay part yake vizuri tunaweza tukafanya. Ikitokea mimi nimeandika wimbo ambao nahisi kabisa yeye akikaa atafit tunaweza tukafanya. Lakini sio chemistry hapo kwanza.” Belle 9 ameiambia Sunrise ya 100.5 Times Fm.

Mwimbaji huyo amesema hivi sasa anafikiria kufanya kazi na mzee Zahir Zorro au Banza Stone kwa ajili ya kupata kitu cha kipekee.

“Hawa vijana wanaimba vizuri. Kiwango kipo, sijasema sioni… lakini the same. Mimi ninahitaji kitu unique kwa sababu nahisi kwa kumshirikisha Zahir au Banza Stone hivi…yaani watu ambao mimi naweza kuchukua kitu pale. Kuna watu wengi ambao naweza kujifunza vitu vingi.” Belle 9 amefafanua.

Hata hivyo, amesema wasanii wapya wa kizazi kipya wanafanya vizuri sana pia na akawataja wengi aliowashirikisha kwenye nyimbo zao kuonesha jinsi anavyowakubali.

Baada ya P Diddy kusema J Lo Anamfunika Kim Kardashian kwa 'Makalio', J Lo Nae Amzungumzia P Diddy

0
0
Rapper mkongwe mwenye mafanikio makubwa, P Diddy juzi alimwagia sifa aliyekuwa mpenzi wake enzi hizo Jennifer Lopez akieleza kuwa alikuwa mwenye bahati sana kuwa nae.

 Aliongeza kuwa hata hivi sasa ni mkali na na kwamba ana makalio aka asset bomba zaidi hata ya Kim Kardashian.

J Lo pia amefunguka yake kuhusu P Diddy wakati anaongea na Access Hollywood  na kueleza kuwa alijifunza mengi sana wakati wa uhusiano wao na kwamba amechangia sana katika maendeleo yake kimuziki.

Hivi ndivyo J Lo alivyoeleza:

"We spent three years of our lives together, you know almost every single day,As much as he roots for me and as proud as he is of me and of the time we had together, I, I am just as proud to see what he's done.Seeing him involved in Revolt and all the things that he's done as a business man and still being so true to his music and his art trying to uplift his community in his own way, and it's the same thing that I try to do and I feel like I learned a lot from him coming up, watching him. He gave me so many cues and taught me so many things,' I'll always be grateful to him for that and I love that he can be so supportive of me so many years later and that there's still so much mutual respect, admiration and love there.
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images