Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live

Marekani yawashtaki raia 12 wa Russia kwa kuhujumu uchaguzi 2016

$
0
0

Katika mashtaka mapya dhidi ya raia wa Russia yaliyofunguliwa Ijumaa na mwendesha mashtaka maalum, raia 12 wa Russia ambao ni maafisa usalama wa jeshi wameshutumiwa kuingilia kati uchaguzi wa urais 2016.

Mwendesha mashtaka maalum wa Marekani Robert Mueller na Naibu Mwanasheria Mkuu Rod Rosenstein wametangaza mashtaka hayo yamefanywa na washauri wa mahakama jijini Washington.

Watuhumiwa 11 kati yao walifunguliwa mashtaka kwa kushiriki katika hujuma ya kudukua kompyuta, kuiba nyaraka na kuzitoa kwa umma ili kuyumbisha uchaguzi.

Mtuhumiwa wa 12 amefunguliwa mashtaka ya kushiriki katika hujuma kompyuta ya taasisi iliyokuwa na jukumu la kusimamia uchaguzi, ikiwemo bodi za majimbo ya uchaguzi, mawaziri wa majimbo na kompyuta zinazogawanya software na teknolojia zinazotumiwa kusimamia uchaguzi,” Rosenstein amesema.

Raia hao wa Russia walikuwa wanafanya kazi katika vitengo viwili vya ujasusi vilivyo ndani ya jeshi la Russia, idara ya ujasusi ya nchi hiyo, kwa mujibu wa mashtaka hayo.

Mashtaka hayo yametolewa kabla ya mkutano wa Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Russia Vladimir Putin utakaofanyika Helsinki Julai 16. Rosenstein amesema alimpa rais muhtasari wa tuhuma hizo dhidi ya majasusi wa Russia mapema wiki hii.

“Rais anafahamu kwa ukamilifu hatua iliyochukuliwa na Idara hii,” Rosenstein ameuambia mkutano wa waandishi wa habari.

Mwezi Februari, mwendesha mashtaka maalum alitangaza mashtaka dhidi ya mtandao mmoja wa Russia wa kampuni ya Troll, wafanyakazi 12 na mfadhili wao.

Chelsea imemtangaza Kocha Wake Mpya Baada ya Kumtimua Antonio Conte

$
0
0

ENGLAND: Klabu ya soka ya Chelsea imemtangaza aliyekuwa kocha wa Napoli ya Italia, Maurizio Sarri(59) kuwa kocha wake mpya

Sarri anayechukua nafasi ya kocha Antonio Conte aliyesitishiwa mkataba wake amesaini mkataba wa miaka mitatu

Aidha, Sarri anakuwa kocha Muitaliano wa 12 kuwahi kuzinoa timu zinazoshiriki ligi kuu nchini humo huku akiwa kocha Muitaliano wa 6 kuwahi kuinoa timu ya Chelsea pekee

Je, unadhani Chelsea watapata mafanikio makubwa na kocha huyu mpya katika msimu ujao?

Mchezaji Kombe la Dunia Atimkia Tanzania Baada ya Kutolewa

$
0
0

Kiungo wa timu ya taifa ya Spain 🇪🇸 na klabu ya Atletico Madrid Koke yupo mapumzikoni katika mbuga ya NgoroNgoro Tanzania - Koke alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Spain walioshiriki katika michuano ya Kombe la Dunia na kutolewa katika hatua ya 16 bora.

Hii ni Habari Njema Kwa Wale Wote Waliohangaika na Matatizo ya Magonjwa Sugu Yaliyokosa Tiba

$
0
0



"HII NI HABARI NJEMA KWA WALE WOTE WALIOHANGAIKA NA MATATIZO YA MAGONJWA SUGU NA YALIYOKOSA TIBA" sasa usikate tamaa tiba imepatikanika kwa DK. ABDALA MUSSA anatibu matatizo kama yafuatayo:

Nguvu za kiume, uzazi, kisukari, tezi dume, vidoda vya tumbo, mgongo kuuma, miguu kuwaka moto na mataizo uliyonayo

1/ITAGULA- ni dawa ya mkosi kuosha nyota, kumvuta mpenzi, mke, mume, kuua kesi na kupata kazi haraka kama umeomba maombi serikalini au kampuni binafisi unaitwa ndani ya siku mbili 2/

NINJIWE- ni dawa inayomaliza matatizo ya wanaume heshima ndani ya ndoa, kuwa na nguvu za kiume milele na kukomaza mbegu na kuwa na uwezo kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara 5 bila kuchoka kama umezaraulika na kufanya tendo na kusinyaa uume dawa ipo dozi yake siku sita vidoge 12 pia kuna na unga inayokomaza uume ndani ya siku 7 unapona kabisa.

3/MPALALA- ni dawa ya kutibu busha miguu kuwaka moto, kiuno, kisukari.

4/NGEKEWA- ni dawa ya kuvuta wateja kwenye biashara yoyote kuwa na wateja wengi katika biashara na kuzuia chuma ulete. 4/LINGWATA- ni dawa ya punguza unene, mafuta tumbo, matiti, miguu, hipsi na kutengeneza shepu dawa hii ni ya unga ukitumia utaona mabadiliko baada ya siku 3.

5/DUBISHO- ni dawa zindiko la mwili, majumba, gari, biashara, mteja wangu huduma utaipata mahali popote ulipo kuna wanasaplai mahali ulipo kama huna muda wa kufika osifini mkoa wa dar-es-salaam, iringa, kanda ya ziwa wilaya ya bunda. angalizo kwa wateja usitume sms wala kubipu huduma yangu ni kuanzia saa 12 asubui hadi saa 12 jioni kwa wateja wa dar-es-salaam ofisi ipo buguruni na mbagala zakhem na kwa wale walio nje ya mkoa dawa hizi mtazipata kwa njia za mabasi. punguzo la bei kwa wateja 5 wa kisukari na nguvu za kiume

KWA MAWASILIANAO ZAIDI WASILIANA NA DK. ABDALA MUSSA KWA SIM NAMBA 0767-171773/ 0716-608959 WOTE MNAKARIBISHWA:

Zari Katika Mahaba Mazito na Mzungu...Diamond Tupa Kule

$
0
0

Mwanamke mjasiriamali @zarithebosslady Aingia katika Headline na kuzua sinto fahamu mtandaoni baada ya kupost Picha hii akiwa katika mahaba mazito na mwanaume wa kizungu.... Tukio hili limewaacha mashabiki katika maswali mengi kuwa ndiye Mrithi wa @diamondplatnumz Au sio...Mpaka sasa haijafahamika Kama kidume huyo ana mahusiano ya kimapenzi na zari au ndio mambo ya kizungu.

Ray Vanny aachana na Ushindani wa Mavazi na Mastaa wenzake

$
0
0

Msanii wa muziki kutoka lebo ya muziki ya WCB Wasafi, Rayvanny ameiambia Dizzim Online kuwa anaamini ushindani upande wa mavazi anabaki kuwa yeye ni mwenye ujuzi na yuko katika viwango vya kuvaa vitu vya gharama zaidi hivyo hahitaji tena kushindana.

Akizungumzia hatua ya kutotaka tena kujihusisha na ushindani wa mavazi, Rayvanny aliongeza kuwa kwa sasa ana mambo mengi ya maana ya kufanya ikiwemo kujikuza zaidi kimuziki na kuandaa maisha mazuri ya mwanae JayDan kwa sasa na siku za Usoni.

Kwa sasa Rayvanny anafanya vizuri na wimbo wake mpya kwa jina 'Chombo', ambapo pia amegusia kuwa kutokana na mapokezi mazuri ya audio ya wimbo huo, mashabiki watengemee kupokea video ya wimbo huo muda wowote kuanzia sasa

Donge la barafu lawaondoa Wanakijiji zaidi 160

$
0
0

Donge kubwa la barafu lililopo katika maji limekaribia kijiji kimoja magharibi mwa Greenland na kusababisha uokoaji iwapo lingevunjika na mawimbi yake kusababisha mafuriko katika nyumba za kijiji hicho. 

Barafu hiyo imepita nyumba hizo kwa urefu katika kijiji hicho na haikusongea siku moja ,kulingana na vyombo vya habari vya eneo hilko. 

Maafisa wa eneo hilo wanasema hawajawahi kuona donge kubwa la barafu kiasi hicho. 

Msimu wa jua uliopita , watu wanne walifariki baada ya mawimbi kusababisha mafuriko katika nyumba kadhaa kaskazini magharibi mwa eneo la Greenland kufuatia tetemeko la ardhi. 

Wanakijiji 169 wanaoishi karibu na donge hilo la barafu wameokolewa kulingana na chombo cha habari cha Denmark Ritzau. 

''Kuna nyufa na mashimo yanayotufanya kuwa na hofu kwamba huenda donge hilo likavunjika , mwanachama wa baraza la kijiji hicho Susanne Eliassen aliambia gazeti la eneo hilo la Sermitsiaq. 

''Kampuni ya umeme na matangi ya mafuta ya kijiji hicho yapo karibu na ufukwe wa kijiji hicho'', alisema. 

Baadhi ya wataalam wameonya kuhusu kutokea kwa madonge mengi ya barafu kutokana na mabadiliko ya hali ya anga, hatua inayozidisha hatari ya kutokea kwa vimbunga vya Tsunami. 

Mnamo mwezi Juni wanasayansi wa chuo kikuu cha New York walitoa kanda ya video ya donge kubwa la barafu lililokuwa likivunjika mashariki mwa Greenland. 

Magaidi Watano Wajisalimisha

$
0
0

Magaidi watano wajisalimisha na wengine wapatao 76 waangamizwa na jeshi la Uturuki katika operesheni ilioendeshwa Şırnak na Mardi kwa muda wa wiki moja.


Kulingana na taarifa zizlitolewa na makao makuu ya jeshi la Uturuki ni kwamba magaidi wanne wa kundi la PKK wametoroka katika ngome zoa Kaskazini mwa Irak  wameonekana wakisalimisha katika jeshi la Uturuki Silapi Şırnak . 

Vilipuzi vilivyokuwa katika maficho ya wanamagmbo wa PKK vimelamatwa katika eneo la  Guçlukonak. 

Katika eneo  moja Şırnak watuhumiwa 16 wakiwemo  wanawake watatu  kutoka Ufaransa wamewekwa baada ya operesheni dhidi ya wanamgmbo wa PKK/PYD. 

Pata Tiba ya Tatizo la Nguvu Za Kiume, nasaidia Kukufanya Urudie Mara 5 na kuchelewa kwa Dakika 20

$
0
0
TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO LINATIBIKA.Baada ya utafiti wa mda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka DR Magise imekuletea tiba ya matatizo hayo kwa kutumia dawa za:

GUMBA POWER:Ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume,dawa hii inamchanganyiko wakutosha wenyekuzalisha vichocheo vingi vya Hemone za Gestrogen vikiwemo vitamin B6&B1,vitamini E,pamoja na madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi,na kuchelewa kufika kileleni zaidi dakka 20-30.

NTINJE:Inarutubisha maumbile ya uume yani kurefusha na kunenepesha nchi 4-7 upana cm3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukiitumia maumbile yako yatabaki kuwa hivyo siku zote,Pia tunatibu Presha,kisukari siku7,ngiri,chango la tumbo tumbo kujaa gesi,kutopata choo vizuri

 TUPO TZ DAR ES SALAAM   MBAGALA RANGI TATU.HUDUMA HII UTALETEWA POPOTE ULIPO .WASILIANA NAMI 0754741788, 0715741788, 0783741788

-DR MAGISE

Watiwa mbaroni kwa tuhuma za kuua na kuchoma moto

$
0
0

WATU wawili wakazi wa kata ya Ruiwa wilayani Mbarali wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mkulima Shukrani Ismail (29) na kisha kuuchoma moto mwili wake. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amewataja watuhumiwa wanaowashikilia kuwa ni Shabani Ramadhani (19) na Salum Ramadhani (39) wote wakazi wa Ruiwa wilayani Mbarali. 

Akizungumzia tukio hilo, Matei alisema Julai 9, mwaka huu, Ismail aliondoka nyumbani kwake ambapo hakuonekana tena hadi maiti yake ilipopatikana Julai 12, ikiwa imechomwa moto katika mashamba ya mpunga. 

Amesema kabla ya kukumbwa na mauti kulikuwa na mgogoro wa mashamba baina ya Ismail na watuhumiwa na kwamba polisi wanaendelea na upelelezi. 

Wakati huo huo, waganga watatu wanaodaiwa kuwa wa jadi wapiga ramli, wakiwemo wawili kutoka mkoani Tabora wanashikiliwa kwa tuhuma za kukutwa na nyara ya serikali. 

Kamanda Matei amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Peter Daudi (34), mkazi wa mlima Njiwa wilayani Chunya, wengine ni Seif Juma na Salum Moses wote wakazi wa Tabora. 

Amesema watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na pembe ya tandala kinyume cha sheria na kwamba uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.

Rais Magufuli alitaka baraza la wadhamini la CCM kufanya tathmini ya mali za CCM

$
0
0

Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli amelitaka Baraza jipya la wadhamini la chama hicho kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kufanya tathmini ya mara kwa mara ya mali za chama na jumuiya zake


Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Gerson Msigwa imesema Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Julai 13, 2018 alipokutana na wajumbe wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais Magufuli amesema baraza hilo linapaswa kutekeleza majukumu yake ipasavyo, ambayo ni kusimamia mali zote za chama na jumuiya zake, kufanya tathmini ya mara kwa mara ya mali za CCM na jumuiya zake, kutoa ushauri juu ya mabadiliko yoyote yanayohitajika katika umiliki wa mali.


Mwenyekiti huyo amesema pamoja na kutekeleza majukumu mengine ambayo yatakabidhiwa kwake na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa.


Rais Magufuli amesisitiza hatarajii kuona dosari za usimamizi wa mali za chama zikiendelea na amewataka wajumbe hao kuhakikisha CCM inanufaika na mali zake na kuachana na utegemezi ambao umekuwa ukisababisha kuomba misaada kutoka kwa watu.


Naye Mwenyekiti wa baraza hilo Anna Abdallah amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwaamini na kuwateua kuunda baraza hilo na ameahidi watahakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa umakini na kwa maslahi ya CCM.


“Mambo hayatakuwa kama walivyozoea huko nyuma kwamba kila mtu anamiliki kipande chake cha mali za chama, hapana, mali zote za chama ni mali ya Baraza la Wadhamini wa Chama Cha Mapinduzi” amesema Anna


Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema baraza hilo la kwanza kuundwa baada ya kufanyika marekebisho ya katiba ya chama, litasimamia mali za CCM pamoja na kusimamia utekelezaji wa mapendekezo ya tume ya kufuatilia mali za chama ambayo yeye alikuwa mwenyekiti wake.


Wajumbe wa baraza hilo ni; John Chiligati, Jaji mstaafu Mark Bomani, Balozi mstaafu Daniel Ole Njoolay, Pandu Ameir Kificho, Christopher Gachuma, Dk Haruni Kondo na Hassan Omar Mzee.

Dawa Bora za Nguvu za Kiume na Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa

$
0
0

DAWA BORA ZA NGUVU ZA KIUME NA KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA 
Baada ya utafiti wa muda mrefu juu ya matatinzo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurundia tendo kwa haraka Sasa inakuletea suluhisho juu ya matatizo haya kwa kutumia dawa za FULL POWER 

Full Power dawa asili yenye vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume dawa hii inamchanganyiko wa kutosha kuzalisha vichocheo vingi vya hernone za gestro gen zikiwemo vitamin b6 na b1 vitamin e pamoja na madini aina ya zinc 

Itakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wakufanya tendo la ndoa zaidi hatua nne au zaidi na kuchelewa kufika kileleni zaidi ya dakika 20/30 ZAT 50 

Inarundisha maumbile ya uume yaani kurefusha na kunenepesha nchi 3/7 na upana cm 3/4 standard.kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukitumia maumbile yatabaki kuwa hivyo siku zote pia anatibu matatizo mengine kama presha kisukari ngiri chango la tumbo kujaa gesi kutopata choo vizuri minguu kuwaka moto matatizo ya uzazi bawasili na magonjwa ya zinaa kama kisonono na kaswende 

Tunapatikana Dar es Salaam  na mikoan wasiliana na DR Oshinda no 0755505099 au 0714126118  Karibuni kwa hunduma bora 

Uwezi Amini Hizi Hapa Faida za Kunywa Maziwa Mtindil

$
0
0

Mtindi unaorodheshwa kuwa miongoni mwa vyakula bora kutokana na kuwa na virutubisho vingi vya aina mbalimbali ambavyo vina faida nyingi katika mwili wa binadamu.
Vikitajwa kwa uchache virutubisho hivyo, imethibitika kuwa mtindi ni chanzo kizuri cha ‘Calcium’, ‘Phosphorus’, ‘Riboflavin (vitamin B2), ‘Iodine’, ‘vitamin B12’, ‘Pantothenic acid (vitamin B5) ‘Zinc’, ‘Potassium’ na ‘Molybdenum’. Mbali ya virutubisho hivyo, ndani ya mtindi kuna ‘bakteria hai’ ambao ni muhimu kiafya katika mwili.

HUREFUSHA MAISHA
Utafiti unaonesha kuwa unywaji wa mtindi mara kwa mara, hasa katika kundi la wazee, uwezo wa mwili wa kupambana na magonjwa mbalimbali umeonesha kuongezeka na kufanya mfumo wa kinga ya mwili kuwa imara zaidi.

Katika utafiti mmoja, walichaguliwa wazee 162 ambao walipewa utaratibu wa kunywa mtindi na maziwa zaidi ya mara 3 kwa wiki na kufuatiliwa maendeleo yao kwa muda wa miaka mitano. Baadaye utafiti huo ulionesha kuwa idadi ya vifo vya wazee hao ilipungua kwa asilimia 38 ukilinganisha na kundi la wazee wasiotumia au waliotumia mtindi kiasi kidogo sana.

KINGA KWA KINA MAMA
Aidha, mtindi umeonesha kuwa na uwezo mkubwa wa kutoa kinga dhidi ya maradhi ya kuambukiza ukeni (vaginal infections). Katika utafiti mmoja uliohusisha wanawake wenye magonjwa ya kuambukiza sehemu za siri, baada ya kutumia mtindi kiasi cha paketi moja kila siku kwa muda wa miezi sita, maambukizi waliyokuwanayo wanawake hao kabla yalitoweka.

KINGA YA MWILI
Utafiti uliofanywa kwa wanyama, wakiwemo panya na kuchapishwa kwenye jarida moja la masuala ya virutubisho nchini Marekani (Journal Of Nutrition), umeonesha kuwa unywaji wa mtindi kila siku, huamsha na kuupa nguvu mfumo wa kinga ya mwili kupambana na magonjwa kadhaa ya maambukizi, ikiwemo saratani ya utumbo.

HUONDOA LEHEMU MBAYA MWILINI
Katika hatua nyingine, mtindi umeonekana kuwa na uwezo wa kupunguza kiwango cha lehemu mbaya mwilini (LDL (bad) cholesterol) na wakati huo huo kupandisha kiwango cha lehemu nzuri mwilini (HDL (good) cholesterol). Kwa maana nyingine, ikiwa mtindi unaondoa lehemu mbaya, mtumiaji anajiepusha pia na hatari ya kupatwa na tatizo la shinikizo la damu.

KUPUNGUZA UZITO
Mbali ya faida hizo, mtindi pia umeonekana kupunguza mafuta (fat) mwilini na kwa maana hiyo una uwezo wa kupunguza unene unaotokana na mafuta mengi mwilini.

MUHIMU KUZINGATIA
Jambo muhimu la kuzingatia ni unywaji wa mtindi halisi uliotengenezwa kutokana na maziwa halisi ya ng’ombe, siyo mtindi uliotengenezwa kutokana na maziwa ya unga. Siri kubwa iliyomo kwenye mtindi ni ule uchachu unaotokana na ‘bakteria hai’ wanaopatikana baada ya maziwa kuganda na kuchachuka.

Hizi Hapa Sababu za Mtoto Kuzaliwa kabla ya Wakati "Njiti"

$
0
0

Kila mwaka watoto takribani milioni 15 huzaliwa kabla ya miezi tisa yaani njiti na idadi hii imekuwa ikiongezeka siku hadi siku. Ni moja kati ya sababu inayochangia kwa wingi vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano duniani.

Shirika la Afya Duniani (WHO) lilikadiria takribani watoto milioni moja walipoteza maisha kutokana na tatizo hili mwaka 2015, hata hivyo, inaelezwa robo tatu ya vifo hivyo vingeweza kuzuilika. Kwa kila watoto kumi wanaozaliwa, mmoja kati yao ni njiti. Na pia, takribani watoto milioni moja hupoteza maisha kila mwaka kutokana na tatizo hilo kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na WHO.

Je nini chanzo cha watoto kuzaliwa Njiti?

Wanawake wenye historia ya kupatwa na uchungu mapema, wapo katika hatari ya kuzaa njiti ukilinganisha na wasio na historia hiyo.

Pia, kuwa na mimba yenye zaidi mtoto mmoja huchangia kuzaa njiti. Utafiti mbali mbali uliofanyika, unaonyesha nusu ya watoto wanaozaliwa mapacha ni njiiti ukilinganisha na anayezalizaliwa peke yake.

Chanzo kingine ni kwa wanawake wenye matatizo katika maumbile ya mfumo wa uzazi, nao wapo katika hatari zaidi. Sababu nyingine ni maradhi katika njia ya mkojo, UTI, maradhi yanayosababishwa na ngono zembe ukiwamo Ukimwi, kisonono, kaswende na trikomonasi.

Tatizo la shinikizo la damu, kutokwa na damu katika sehemu za uzazi, mama kuwa na uzito mdogo au mkubwa kupitiliza kiasi wakati wa ujauzito, kujifungua mara kwa mara katika kipindi kifupi, kuchanika kwa mfuko wa uzazi na kondo la nyuma kabla ya wakati na kisukari cha mimba huchangia katika tatizo hili.

Mambo megine yanayochochea ni umri wa mjamzito. Inaelezwa wanawake wanaojifungua wakiwa chini ya umri wa miaka 18 wapo katika hatari ya kuzaa njiti kwani katika kipindi hicho mfumo wa uzazi unakuwa bado haujakomaa.

Wanawake walio na umri unaozidi miaka 35 wapo katika hatari pia kwasababu katika umri huu mkubwa, wengi wao huwa na maradhi chochezi kama kisukari na shinikizo la damu.

Matatizo ya kifamilia, msongo wa mawazo na ya kisaikolojia kama kupigwa na kuteswa wakati wa ujauzito, kufanya kazi za kusimama kwa muda mrefu ni moja ya mambo yanayochochea.

Dalili zinazoambatana na tatizo hili

Maumivu chini ya mgongo, yanayoweza kuwa ya kudumu au kuja na kuondoka na hayaondolewi kwa kubadilisha pozi.

Kutokwa na maji maji na damu sehemu ya siri yanayoashilia kupasuka kwa chupa. Kupatwa na uchungu zaidi ya mara nne ndani ya saa moja.

Mtoto njiti anaweza kukumbwa na matatizo gani

Matatizo ambayo huwakumba watoto wanaozaliwa njiti ni pamoja nay a kupumua, kwani wakati huu mfumo wa hewa huleta shida kwa sababu mapafu yanakuwa hayajakomaa.

Shida nyingine ni upande wa ulaji au unynyaji kutokana na mfumo changa wa chakula. Mara nyingine watoto hawa hupatwa na matatizo katika kusikia na kuona ambayo huchochewa na kuchelewa kwa ukuaji wa mfumo wa fahamu, hali hii huathiri ukuaji wa mtoto kwa ujumla.

Mambo muhimu ya kuzingatia

Hakikisha kipindi cha ujauzito hautumii vilezi, sigara na dawa za kulevya, hudhuria kliniki kwa ajili ya afya ya uzazi pamoja na kupima maradhi ya zinaa, pata muda wa kutosha wakupumzika kwa kujiepusha na kazi nzito na zinazohusisha kusimama kwa muda mrefu, pata lishe ya kutosha yenye virutubisho muhimu kwa ajili ya ukuaji wa mtoto na afya ya uzazi. Kujiepusha na mimba katika umri mdogo hasa chini ya miaka 18 na kuzingatia maagizo ya uzazi wa mpango kwa kuepuka kubeba mimba kila baada ya muda mfupi, hasa ulio chini ya miaka 2. Si jukumu la mama tuu, bali pia baba, katika kuutunza ujauzito ili kuepusha matatizo katika kipindi cha ujauzito.

Wamama Ambao Huwa Wanawapiga Sana Watoto Wao wa Kiume Huwa Hawana Mapenzi na Waume zao

$
0
0

Wakuu, nimefuatilia muda mrefu hawa wamama ambao wakipata mwanya wa kuwaadhibu watoto wao, hutembeza kipigo cha haja/ cha mbwa koko na nimegundua kuwa huwa na chuki kama sio kuwapenda waume zao ambao ndio baba watoto!

Suala la kuwapiga watoto si kosa ila wapo ambao hutembeza kipigo cha adabu kiasi kwamba unahisi huyo mtoto anaweza kufa.

Hivyo niwashauri tu wamama,kuwa chuki zenu wewe na mumeo msizihamishie kwa watoto mtakuja kuwaua bure.

Muswanu!

TFF yapitisha mfumo mpya wa ligi daraja la kwanza

$
0
0

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imekubaliana kupitisha mfumo wa Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambapo kuanzia msimu ujao FDL itachezwa katika makundi mawili yenye timu 12. 

Timu 1 kutoka kila kundi itapanda kwenda Ligi Kuu wakati timu ya 2 na ya 3 katika kila kundi zitacheza mtoano kwa mechi za nyumbani na ugenini na washindi katika mechi hizo watacheza na timu iliyoshika nafasi ya 17 na 18 katika Ligi Kuu kupata timu mbili zitakazocheza Ligi Kuu huku timu mbili za nafasi ya 19 na 20 zikishuka daraja. 

Timu hizo mbili za Ligi Kuu zilizoshika nafasi ya 17 na 18 kama zitapoteza michezo yao zitashuka Daraja kuungana na zilizoshika nafasi ya 19 na 20. 

Nia ya dhati ni kuongeza ushindani wa Ligi Kuu,FDL na SDL. 

Vilevile Kamati ya Utendaji imekubaliana kuchezwa kwa mashindano ya Taifa Cup kati ya Mwezi Juni na Julai 2019 huku pia ikipitisha kuchezwa kwa mashindano ya Vijana U15 katika mtindo uliokuwa unatumika kwenye Copa Coca Cola wakati yale ya U17 yenyewe yatahusisha klabu za Ligi Kuu, Daraja la Kwanza na Daraja la Pili kwa pamoja. 

Nayo mashindano ya Kombe la Shirikisho yataanzia katika ngazi ya mkoa ambapo kila mkoa utakuwa na bingwa wake.

Tumia Super Mkuyati Kurudisha Heshima ya Ndoa

$
0
0
SUPER MKUYATI ILIYO IMARA KURUDISHA HESHIMA YANDOA

Super mkuyati nidawa ya mitishamba iliyo sheheni miti mbalimbali na kugundulika ina pambana na magonywa sugu ya uzazi na ukosefu wa nguvu

SUPER MKUYATI inanguvu (3) nainafanya kazi kwapamoja (1) itakufanya uchelewe kufika kileleni ndani ya dk 15-20 bila kuchoka (2) ina zalisha homon kwa wingi na kukufanya uwe na mbengu nyingi zenye vimeleo vya uzazi vyilivyokomaa (3) inaongeza ume mdogo uliosinyaa,kunenepesha uume na kurefusha adi nchi 5-8 na upanda sm 2-3 dawa hii haina mazara kwa mtumiaji ata kwa wazee walionaumri 60-80

SUPER MKUYATI ponyo la maradhi yako tumia Leo uone mjabu yake

 FIKA OFISI YETU ZINAPATIKANA DR MTONI KIJICHI KAMA UNA NAFASI UTALETEWA POPOTE ULIPO KWA WAMIKOANI UTATUMIWA

DR GATUNDU

0717777402/0768408794

Sababu kuu 7 za kwanini kila mwanaume anahitaji mwanamke sahihi

$
0
0

Kwangu kipindi ambacho kilinivutia sana ni kipindi cha kampeni za uchaguzi nchini Marekani. 

Ni pale Obama akiwa katika kampeni kwenye moja ya majimbo kugombea duru ya pili ya uraisi aliposimamisha hotuba yake na kutambua uwepo wa mkewe Michelle. 

Obama alisema, "Mke wangu amekuwa bega kwa bega na mimi tokea niko chuo, kuna kipindi nilishindwa kulipa ada ila yeye ndiye aliyenilipia" 

Obama akaenda mbali zaidi na kukiri mbele ya jamii ya kimataifa kwamba asingekuwepo hapo alipo kama sio mke wake Michelle. 

Hivyo basi, nashauri kwamba mwanamke ambae mwanaume atakua nae huenda akawa chachu ya mafanikio na baraka kwake au anaweza akamrudisha nyuma kabisa katika mipango yake. 

Sababu kuu 7 za kwanini iwe isiwe mwanaume lazima upate mwanamke alie sahihi. 

1. Kila mwanamke anao uwezo wa kukuridhisha kimapenzi ila mwanamke sahihi na bora pekee ndiue anaeweza kuku-challenge kiakili na kuwa 'intellectually inspired'. 

2. Mwanamke yeyote anaweza kukuteka kihisia, ila yule sahihi pekee ndiye mwenye uwezo wa kukuteka kiroho na ukamtumikia Mungu wako. 

3. Mwanamke yeyote anaweza akakushawishi muandike mpango wa harusi (wedding plan), ila mwanamke sahihi peke yake ndie mwenye uwezo wa kukuandikia na kukushauri mpango wa biashara (business plan) 

4. Kila mwanamke anaweza akakubusu tena 'French kiss' ila mwanamke bora pekee ndio mwenye uwezo wa kukutamkia maneno yaliyojaa busara na hekima. 

5. Kila mwanamke anaweza akakupenda sana tu tena kama una pesa, ila mwanamke aliye bora pekee ndiye anaeweza kusimama na wewe hata kukuinua pale utakapokuwa huna kitu. 

6. Mwanamke yeyote anao uwezo wa kukushibisha kwa kukupikia chakula kitamu, ila mwanamke bora pekee ndio mwenye uwezo wa kukulisha chakula cha ubongo. 

7. Kila mwanamke anao uwezo wa kukushawishi chumbani ila mwanamke bora pekee ndio mwenye uwezo wa kukushawishi umrudie Mungu wako. 

Mwisho ngoja nihitimishe kwa kusema hivi ukisoma vitabu vya kihistoria kuhusu Winstom Churchhill mpaka Abraham Lincoln, na kutoka kwa Nelson Mandela mpaka kwa Martin Luther King Jr lao moja kwamba “No matter how strong a Man is, he is only as strong as the Woman he marries” Kwa tafsiri yangu ya kuunga unga isiyo sahihi sana Wanamaanisha "haijalishi ni kwa kiasi gani mwanaume una nguvu, nguvu zako zina athiriwa kwa kiasi kikubwa na mwanamke utakaemuoa"

Giza latanda Chadema, Mgombea Atoweka

$
0
0

Giza la sintofahamu ladaiwa kutanda Mkoa wa Iringa, ikiwa ni baada ya mgombea wa udiwani kwa tiketi ya CHADEMA kutojulikana alipo baada ya kuchukuliwa na na watu wasiojulikana mapema ya leo.

Akizungumza na www.eatv.tv, kuhusu sintofahamu hiyo kwa njia ya simu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amesema kwamba sintofahamu hiyo ilianza kujitokeza siku ya juzi baada ya aliyekuwa mgombea wa Kata ya Kwakilosa kunyang'anywa fomu na mtu aliyemuonyesha bastola hali iliyomuingiza woga mgombea Godfrey Luchagile na kumfanya ajitoe katika kinyang'anyiro hicho.

Akizidi kufafanua Msigwa amesema kwamba mgombea mwingine wa Kata ya Galilonga, Pallaiga Andrew yeye amekamatwa na jeshi la polisi kwa kosa la kugushi fomu ya uchaguzi akiwa eneo la kurudisha fomu yake.

"Hii ilianza juzi baada ya Mgombea Godfrey Luchagile, kudai kutishwa na bastola kisha kunyang'anywa fomu ya uchaguzi, baadaye mgombea aliyepatikana kuziba nafasi yake ndg. Hamid Mfalingungi naye kapotea mapema ya leo, huyu wa Galilonga yeye alinyang'anywa fomu lakini bahati nzuri alikuwa ameshaitoa 'photocopy' wakati anairudisha anaambiwa kagushi hivyo wamempeleka polisi ili kupoteza muda wa kupokea fopmu. Hatujui nia yao kwani katika Kata tatu tumemaliza zoezi hili salama ila hizi mbili ndiyo mambo haya yanaibuka,"

Akizungumzia kwa undani kuhusu tukio hilo, Katibu wa CHADEMA mkoani Iringa Jackson Mnyamwani amesema kuwa wakati sinema hiyo inaendelea Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, kata ya Kwakilosa, Ndg. Fuad Mwakitosa amegoma kupokea fomu ya mgombea ambaye ilirudishwa na wadhamini wake kitu ambacho ni kinyume na utaratibu.

Pamoja na hayo, Mch Peter Msigwa amesema kwamba tayari siku ya jana walikwisha wasiliana na Mkurugenzi wa Uchaguzi Taifa Athuman Kihamia kwa ajili ya sintofahamu hiyo lakini mpaka sasa hakuna kitu kinachoonekana kuendelea.

Hata hivyo www.eatv.tv, ilipomtafuta Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, Juma Bwire kuzungumizia matukio hayo simu yake haikupokelewa, na juhudi za kumpata Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Ndg. Fuad Mwakitosa bado zinaendelea.

Uchaguzi wa marudio unatarajiwa kufanyika Agosti 12, 2018, katika jimbo la Buyungu, Kigoma na kata 77 baada ya madiwani wengi kuhama vyama vya upinzani na kuhamia CCM wakidai wanaunga mkono juhudi za Rais John Magufuli.

UPDATE

Mgombea wa Udiwani Hamid Mfalingungi amepatikana akiwa kituo cha polisi, hajaruhiswa kuzungumza na mtu yoyote.

Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Iringa, Jackson Mnyamwani amethibitisha kuonekana kwa mgombea huyo ambapo amesema mgombea wao ameonekana muda mfupi baada ya muda wa kurejesha fomu za uchaguzi kuisha.

Amebainisha kwamba kwa sasa wanawasiliana na makao makuu ya chama ili waweze kupata msaada wa kisheria wa kujua jambo gani la kufanya kuweza kupata haki yao.

Timu ya Gor Mahia Yafungiwa Miaka Miwili Kisa Kiburi

$
0
0

Baraza la vyama vya michezo Afrika Mashariki na kati CECAFA limeifungia klabu ya Gor Mahia kushiriki michuano ya Kagame Cup kwa muda wa miaka miwili.

Adhabu hiyo imetangazwa na Katibu mkuu wa CECAFA, Nicolas Musonye kwenye mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam hii leo.

Baada ya kuifunga klabu ya JKU katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano hiyo ya Kagame, Gor Mahia iligoma kwenda kuchukua medali zake na kuamua kuondoka.

Waandaaji wa mashindano hayo walilazimika kuiita klabu ya Simba jukwaani  baada ya kuisubiri Gor Mahia kwa takribani dakika tano bila mafanikio. 

“Tuliandaa kila kitu kwaajili ya utoaji wa zawadi lakini Gor Mahia hawakutokea katika tukio, mbali na hilo pia walipofika hapa walikataa hoteli, waligomea vyumba vya kubadilishia nguo na jana hawakutokea mbele ya wageni wetu “. 

“Pia tumemuonya kocha wa Gor Mahia (Dylan Kerr) kwa kuwatolea lugha chafu makamisaa wa mchezo na tumeshalitaarifu shirikisho la soka Kenya (FKF) , lakini kwa sisi hawatoshiriki mashindano ya Kagame Cup kwa miaka miwili ijayo “. Amesema Musonye.

Mashindano hayo yamemalizika kwa Azam Fc kuibuka washindi baada ya kuifunga Simba 2-1 na kufanikiwa kuutetea ubingwa huo ambao katika mashindano yaliyofanyika kwa mara ya mwisho mwaka 2015.
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live




Latest Images