Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Kesi ya Mbowe na Vigogo Wengine CHADEMA Yakwama Tena

$
0
0
Kesi ya Mbowe na Vigogo Wengine CHADEMA Yakwama Tena
Kesi ya kufanya mikusanyiko na maandamano yasiyo halali, inayowakabili viongozi tisa wa Chadema, akiwamo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, imeshindwa kuendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Kesi hiyo imeshindwa kuendelea leo Julai 18, kwa sababu upande wa mashtaka wanasubiri uamuzi wa maombi yaliyowasilishwa Mahakama Kuu, na washtakiwa hao.

Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa ili kusubiri maamuzi ya maombi yaliyopelekwa Mahakama Kuu.

Nchimbi akisaidiana na Wakili Zainabu Mango na Saimon Wankyo, alidai kuwa maombi ya awali yaliyowasilishwa Mahakama Kuu, yalisikilizwa wiki iliyopita na kupangiwa Julai 20, kwa ajili ya kutolewa maamuzi hivyo wanaomba ipangwe tarehe ya karibu kwa ajili ya kusubiri maamuzi yatakayotolewa.

Hata hivyo, wakati kesi hiyo inatajwa jana, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, hakuwepo mahakamani hapo kutokana na kuuguliwa na mke wake ambaye amelazwa katika Hospitali ya Bugando.

"Kesi imekuja kwa ajili ya kutajwa tunasubiri uamuzi wa maombi yaliyowasilishwa Mahakama Kuu, na washtakiwa hawa," alidai Nchimbi.

Nchimbi baada ya kueleza hayo, Wakili wa utetezi Peter Kibatala akisaidia na Jeremiah Mtobesya, alidai kuwa mapingamizi ya awali yameshatolewa, hivyo wanaomba mahakama iendelee kuitaja kesi hiyo.

"Ni kweli John Heche hayupo mahakamani hapa na nimepata taarifa kutoka kwa mdhamini wake, kuwa   anauguliwa na mke  wake, lakini mdhamini wake anazo fomu za matibabu,  ataziwasilisha hapa mahakamani," alisema Kibatala.

Kibatala alifafanua kuwa kama mapingamizi hayo yatafanikiwa basi kesi itapangwa kwa ajili ya kusikiliza na kama hayatafanikiwa itaendelea kupangwa kwa ajili ya kutajwa.

Baada ya mdhamini huyo kuwasilisha fomu hizo mahakamani hapo, upande wa mashtaka walidai kuwa hawana pingamizi juu ya uthibitisho huo wa matibabu.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 25, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Viogozi hao wa Chadema, wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe walifungua maombi ya mapitio Mahakama Kuu dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), wakipinga uamuzi na amri mbalimbali zilizotolewa na Mahakama ya Kisutu katika kesi hiyo.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu, Dk Vincent Mashinji; naibu makatibu wakuu John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar).

Wengine ni mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa; mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko; mbunge wa Kawe, Halima Mdee; mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 112 ya mwaka 2018, washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo Februari 16, 2018 katika barabara ya Kawawa, Mkwajuni Kinondoni ambalo wanadaiwa kusababisha vurugu zilizosababisha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline

NEC Yawapiga Barua CHADEMA

$
0
0

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeiandikia barua Chadema ikitaka utambulisho wa mawakala watakaosimamia uchaguzi wa marudio wa jimbo la Buyungu na Kata 77 Agosti 12, 2018.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 18, 2018 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila amesema barua hiyo inawaelekeza wakala atatambulishwa kwa msimamizi wa uchaguzi kwa barua ya chama, picha mbili za pasapoti na kitambulisho chochote chenye picha.


Hata hivyo, Kigaila amekosoa uamuzi huo wa Tume kwa madai hawajapewa mwongozo wowote wa mawakala siku ya kupiga kura, jambo linaloweza kusababisha sintofahamu kama ilivyokuwa kwenye uchaguzi wa jimbo la Kinondoni.


"Kwenye uchaguzi uliopita wa Kinondoni mawakala wetu waliambiwa hawana utambulisho wowote kutoka Tume, jana wametuandikia barua wanatoa masharti lakini hawasemi siku ya uchaguzi itakuwaje, mawakala watatambuliwa vipi," amesema Kigaila.


Kigaila amesema Tume hiyo haijayafanyia kazi malalamiko ya Chadema licha ya kuandikiwa barua na Katibu Mkuu wake, Dk Vincent Mashinji kukutana na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk Athumani Kihamia.


Amesisitiza wataendelea kupigania haki ya wagombea wa chama hicho na wanakwenda kushinda kwenye uchaguzi huo.


"Mkurugenzi ametuambia ili kuepusha makosa yaliyofanyika kwenye uchaguzi wa Kinondoni mawakala waje na vitambulisho. Kumbe wanatambua Uchaguzi wa Kinondoni ulikuwa na kasoro lakini hawajamchukulia hatua zozote msimamizi wa uchaguzi wa Kinondoni kwa kuharibu uchaguzi," amesema.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi wa Chadema, Reginald Munisi amewataka polisi kufanya kazi zao badala ya kuingilia uchaguzi kwa kuwakamata wagombea wa Chadema.


"Kuna kata 18 ambazo wagombea wa Chadema wameenguliwa. Mpaka sasa kuna maeneo watu wetu wamekataliwa rufaa zao, kwa mfano Rombo. Tumeandika malalamiko yetu kwa Tume," amesema Munisi.

Madereva kutokuona ndio chanzo cha ajali Singida

$
0
0

Jeshi  la  Polisi  mkoa  wa  Singida  kwa   kushirikiana  na  shirika  la  Sightsaver  wameendesha  zoezi  la  kuwapim a  macho  Madereva  na  kubaini  kuwa  kati  ya  madereva  miamoja  madereva  kumi  wanauoni  hafifu ,jambo  ambalo  linaweza  kuwa  ni  moja  ya  chanzo  cha  kusababisha  ajali. 

Hatua   hiyo  imefikiwa  kwenye  zoezi  la  siku  kumi  la mafunzo  kazini  kwa  madereva  na   kuwapima  macho  na  kubaini  kati  ya  madereva  elfumoja  miatano  na  tatu  walio  kwishapimwa  madereva  miamoja na sitini  na  tano  wamebainika  wanauoni  hafifu  huku   wakiendesha  vyombo  vya  moto. 

Awali   kamanda  wa   Polisi  mkoa  wa  Singida  ACP  Debora  Magiligimba  amesema  baadhi  ya  ajali  zimekuwa  zikisababishwa  na   uoni  hafifu  kwa  madereva,  ndio  maana  jeshi  la  polisi  likaamua    kuwapima  macho  dereva  wote  wa mkoa  wa  Singida. 

Kwaupande  wake  mratibu  shirika    lisilo  la  kiserikali  la  Sightsaver   Bwana  Edwin   Maleko  amesema  toka  waanze  kutoa  huduma   za  matibabu  ya  macho mwaka 2016,kwa  zoezi  la  kupima  madereva  ni  mara  ya  kwanza   na  wamekuta  wagonjwa   ni  wengi,huku  madereva  waliopimwa  wakipongeza  zoezi  hilo. 

Ndalichako aitaka TCU kuongeza ubora wa vyuo vikuu

$
0
0

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako ameiagiza Tume ya vyuo vikuu nchini TCU kuongeza kasi ya kuhakiki ubora wa vyuo vya elimu ya juu na vitakavyobainika kukosa vigezo hata kiwe cha serikali kifungiwe kwani suala la ubora wa elimu  ni jambo la lazima kwani  hakuna haja ya kuwa na msururu  wa vyuo visivyokuwa na tija. 

Prof Ndalichako ameyasema hayo alipokuwa akifungua maonyesho ya vyuo vikuu ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi. 

Wakati akizindua maonyesho hayo Prof Ndalichako amevitaka Vyuo vikuu kutafuta suluhu changamoto zinazoikumba jamii  na  kuonyesha fursa  mbalimbali zilizopo katika sekta ya kilimo,viwanda ambapo baadhia ya vyuo vimemweza kuhusu tafiti walizofanya katika maeneo hayo. 

Katika maonyesho hayo baadhi wanafunzi wamejitokeza kupata taarifa za namna ya kujiunga na vyuo vya ndani na nje ya nchi na kupatiwa maelezo ya kina.

Shilole Anaendelea Kumsuta MunaLove.."Adai Alikuwa Anapata Kiki Kupitia Marehemu Patrick"

$
0
0

Shilole azidi kumshambulia Munalove Mtaondaoni aandika ujumbe huo Mzito ...Usipitwe kabisaa...soma KISHA Drop comment Mdau..( Hii ni Hatari)
Jisomee hapa chini

Baada ya Ben Pol Kumla Ebitoke na Kusepa, Ebitoke Atambulisha Mchumba wake Mpya

$
0
0

Mchekeshaji Maarufu mtandaoni @ebitoke ambaye kipindi cha miezi kadhaa iliyopita alikuwa katika mahusiano na Msanii Benpol mpaka kufikia hatua ya kutoana Bikra sasa apata mwaume mpyaa baada ya Kuachana na muimbaji huyo.... Kwa Taarifa zilizopo ni kwamba Mchumba huyo ni Muarabu anayefanya kazi zake Dubai Na Tanzania... Chanzo makini kabisaa chakuamini kimeendelea kumwaga ubuyu kuwa Ebitoke haambiwi wala hasikii kwa mwanaume huyo na wameanza vikao vya harusi kwaajili ya Ndoa baina ya wawili hao... sambamba na Hilo Ebitoke ameonekana kumzimia Mwarabu huyo anayefahamika mtandaoni kwa jina la @manlikeaiman Kwani amekuwa akimpost Mara kwa Mara katika Insta Story zake zikiambatanishwa na caption za kimahaba... Alipo tafutwa meneja Timoth Conrad na Kuulizwa kuhusu tukio hilo la Ebitoke amefunguka kuwa ni Kweli Ebitoke anaolewa hivi karibuni na Kijana huyo, Akiwa Kama Meneja ameelezea furaha yake kuwa ni jambo la kheri kwani Ebitoke amemlea katika Nidhamu.
TOA MAONI YAKO HAPA

Kwa Wanaume tu: Wanawake wa Aina Hii ni Shida Usiwaguse Kabisa

$
0
0
Hakikisha unawakwepa aina hii ya wanawake ili usijiingize kwenye matatizo. Nitakwambia ni kwa nini…..

1.Demu wako wa zamani

Ni vizuri kutorudia mahusiano ya zamani na zaidi kama kwenye mahusiano yenu ya mwanzo mambo hayakuishia kwa uzuri. Sababu kuu ya msingi, kiukweli ni kwamba hakika mwanzoni mlikuwa hamuendani na ndio sababu ya iliyopelekea kuvunjika kwa mahusiano yenu, ndani ya hizo sababu kuna vitu vilivyopolekea kutokea kwa hayo, ukichunguza na kuziangalia kwa makini utagundua ni za asili na ambazo si rahisi kwa mmoja wenu kuzibadilisha sababu ni vitu au mambo ambayo yatakuwa ni ya damuni.

2.Dada wa rafiki yako kipenzi

Epukana na kujiingiza kwenye mahusiano na dada wa rafiki yako. Si tu kwamba utaweza kujiingiza kwenye uhasama na chuki kama mambo hayatakwenda sawa, ila pia utaweza kujiweka kwenye mazingira ya kujikuta siku moja unapigwa hata ngumi za uso sababu tu ulimuumiza dada yake. Pia, utaweza kumkosa mtu ambaye ndie alikuwa ni kimbilio lako kwa mambo mbalimbali pale ambapo itatokea wewe na dada yake mambo kutokwenda sawa, sababu hapo patakuwa na mgongano wa kimaslahi kwa huyo rafiki yako.

3.Wanawake wenye mambo mengi

Kiukweli, kutoka na watu kama hawa kinaweza kuwa ni kitu cha kufurahisha, ila mwisho wa siku itakuingiza kwenye matatizo. Mara zote kumbuka ni vyema kuwa salama kuliko kujuta. Usijiingize kwenye majaribu ambayo utakuja kuyajutia kwa maisha yako yote.

4.Wanawake wanaopenda hela kupitiliza (Wachunaji)

Kuwa mbali nao, labda kama unataka salio lako limalizike pasipo wewe kujifahamu. Naamini hili kila mmoja analifahamu na halihitaji darasa zaidi. 5.Demu wa zamani wa rafiki yako
Kama unathamini urafiki wako na mshikaji wako achana na habari ya kutoka na aliyekuwa demu wake. Mambo yanaweza kubadilika na kuwa kama au zaidi ya yaliyotokea kwa rafiki yako na ikaja kula kwako zaidi. Wakati mwengine inaweza tengeneza chuki kati yako na rafiki yako, huku akiamini kwamba ulikuwa unatoka au kumnyemelea demu wake toka zamani.

Wadau mademu wapo wengi sana, fanya kutafuta wengine nje ya hawa….. ni ushauri tu..

Kumenoga TAZARA, Tazama Hapa Picha Kuona Daraja la TAZARA- Dar es Salaam Lilivyo kwa Sasa

$
0
0

Daraja la juu llinalojengwa na serikali katika eneo la  TAZARA  jijini Dar es salaam likiwa katika hatua za Mwisho za ujenzi wake. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Tunatibu Na Kuponesha Kabisa Upugufu wa Nguvu za Kiume, Busha, Kisukari na Vidonda vya Tumbo

$
0
0
TUNATIBU NA KUPONESHA KABISA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME UUME MDOGO? BUSHA BILA KUPASUA KISUKALI NA VIDONDA VYA TUMBO? asilimia kubwa ya wanaume wanaupungufu wa nguvu za kiume NA maumbile madogo NI NINI KINACHOSABABISHA UUME KUZIDI KUWA MDOGO NA WEMBAMBA 1 kuugua chango LA uzazi 2 unene kupita kiasi 3 kuvaa nguo au chupi za kubana 4 kupiga punyeto kwa mda mrfu ,NI NINI TIBA YAKE MAKAKANUA MIX nidawa ya mitishamba iliyochanganywa NA mizizi kumi NA mbili urfusha NA kunenepesha UUME saizi upendayo ich 5,6,7, NA 8 kwa urfu NA sentimita 3,4, na 5 ipo dawa ya kunywa na kupaka NI NINI KINASABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME 1 kupungukiwa kwa homoni ya testerone 2 kuhudhurika kwa Neva au uti wa mgongo 3 utumiaji holela wa madawa ya kizungu 4 usongo wa mawazo na asira 5 utumiaji wa vyakula vya mafuta mengi NI NINI TIBA YAKE MAPRO POWER NO 2 NDIO tiba tosha kwa sasa kwani utibu matatizo matatu kwa pamoja 1 itakufanya uchelewe kufika kileleni dk 15 adi 20 ,2 itakufanya urudie tendo zaidi Mara tatu 3 uhimalisha uume uliolegea na kusinyaa OKOA NDOA YAKO SASA ujihepusha na lawama ndani ya ndoa yako au pale ukutanapo na mpezi dawa hii itamfanya mpenzi wako hakueshimu na hasitoke nnje ya ndoa na ata wazee wenye umri mkubwa wanapona zipo dawa za kupunguza kitambi,minyama uzembe, presha ,kisukar mvuto wa mpezi au biashara FIKA OFISINI KWETU MBAGALA ZAKHEMU na wateja wa kanda ya ziwa yupo wakala wetu mwanza mjini au piga simu 0752348593

DR MABULA na utaletewa popote ulipo uduma hizi

Mbunge wa CUF Ajivua Uanachama

$
0
0
Mbunge wa CUF Ajivua Uanachama
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum, Amina Mwidau Mkoa wa Tanga (CUF), amejivua uanachama wa chama hicho kwa madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa kisiasa wa chama hicho na kujiridhisha na utendaji wa serikali ya awamu ya Tano chini na Rais John Magufuli.

Aidha, Mwidau hajabainisha iwapo atajiunga na chama chochote cha siasa.

Viatu Virefu Vyamuumbua Wema Sepetu Morogoro

$
0
0
Viatu Virefu Vyamuumbua Wema Sepetu Morogoro
STAA wa filamu Bongo, Wema Sepetu ametengeneza kichwa cha habari mjini Morogoro baada ya juzikati kujikuta akiumbuka kufuatia viatu alivyokuwa amevaa kutaka kumng’oa meno alipokuwa akipanda jukwaani.



Kisanga hicho kilimpata Wema alipotinga kwenye mashindano ya Miss Morogoro 2018 ambapo alialikwa kama mmoja wa majaji. Awali saa 6 usiku wakati Wema akiingia katika Ukumbi wa

Hoteli ya Morogoro lilipofanyika shindano hilo alionekana akiwa amevalia gauni refu la rangi ya gold huku chini akiwa ametinga viatu virefu vilivyompa wakati mgumu kutembea kwa mikogo. Hata hivyo staa huyo alifanikiwa kufika kwenye meza iliyoandaliwa kwa ajili ya majaji na kukaa lakini shughuli ilikuwa pale ambapo alitakiwa kupanda jukwaa kutoa neno.



Wakati akielekea kwenye ngazi za kupandia jukwaani, Wema alionekana kuyumba na kutaka kupiga mwereka lakini mmoja wa watu waliokuwa karibu yake waliwahi kumzuia na ndipo aliposhikiliwa na kupandishwa. Hata hivyo, hali iliendelea kuwa tete baada ya staa huyo kufika ngazi ya pili ya jukwaa ambapo aliyumba tena na ndipo mtangazaji wa Redio Planet FM ya Moro, Warda Makongwa akaongeza nguvu na kumfikisha jukwaani salama.



Wakati wa kushuka ili kumuepushia aibu staa huyo, wadada wawili walionekana kumshika mikono na kushuka naye taratibu huku mtangazaji wa Redio Clouds FM, Gardner G Habash naye akiongeza nguvu. Mbali na viatu kumuumbua Wema, umbo lake namba nane lililokuwa limejengeka vilivyo kutokana na gauni alilokuwa amevaa lilikuwa gumzo na wengi waliibua gumzo kutokana na msambwanda wa mrembo huyo.

Twaweza Yaijibu Barua ya Serikali

$
0
0
Twaweza Yaijibu Barua ya Serikali
SHIRIKA lisilo la kiserikali la Twaweza, limejibu barua ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), iliyowataka kueleza taratibu walizotumia wakati wa kufanya utafiti wa umaarufu wa viongozi wa kisiasa nchini.

Akizunguma jana na Nipashe kwa njia ya simu, Ofisa Mawasiliano wa Twaweza, Annastazia Rugaba, alisema walijibu barua hiyo tangu Ijumaa iliyopita.

“Hatuwezi kueleza tulichowajibu kwa kuwa yalikuwa ni mawasiliano kati ya taasisi na taasisi, ila tumeshawajibu kabla ya muda wa siku saba waliotupa,” alifafanua baada ya kutakiwa kueleza majibu yao.

Nipashe iliwasiliana na Costech kutaka kujua ni lini uamuzi kuhusu shauri hilo utatolewa baada ya Twaweza kujieleza kutokana na kushindwa kufuata taratibu wakati wa kufanya utafiti wa umaarufu wa viongozi wa kisiasa, Kaimu Mkurugenzi wa Costech, Dk. Amos Nungu, alisema maamuzi yoyote yatakayotolewa dhidi Twaweza, hayatakuwa hadharani kwa kuwa yalikuwa mawasiliano ya ndani.

“Hatutarajii kutoa chochote kitakachojadiliwa nje kwa sababu siyo nia yetu, ilikuwa bahati mbaya kwamba ile barua ilikwenda kwenye mitandao, hivyo hata majibu yatakuwa ndani ya taasisi na taasisi,” alifafanua.

Aidha, alisema majibu ya barua kutoka Twaweza yalishapokelewa na yanafanyiwa kazi na Costech.

Wiki iliyopita, mkurugenzi huyo alisema “Tume inayo kamati maalum inayohusika na kusajili na kutoa vibali kwa tafiti mbalimbali zinazoendeshwa Tanzania. Maombi hupelekwa kwa wataalamu waliobobea katika nyanja husika kabla ya kuletwa kwenye kamati ili kujadiliwa.

Alisema Tume imekuwa ikiwasiliana na wadau pale wanapobaini utafiti kufanyika bila kusajiliwa ama kufuata taratibu na ndiyo maana iliwasiliana na Twaweza.

Dk. Nungu alisema siyo mara ya kwanza Costech kuwaandikia barua wadau wake na Twaweza siyo wa kwanza kuandikiwa barua ya namna hiyo.

Kocha Mkongomani wa Yanga Atimka Kimyakimya

$
0
0
Kocha Mkongomani wa Yanga Atimka Kimyakimya
IMEFAHAMIKA kuwa kocha msaidizi Mkongomani, Guy Bukasa, aliyetua nchini kwa ajili ya kuifundisha Yanga ametimka kimyakimya kwenye klabu hiyo na kurudi nyumbani kwao DR Congo.



Kocha huyo, alitua nchini wiki mbili zilizopita na kuanza kibarua cha kuki­noa kikosi hicho kwa ajili ya Kombe la Shirikisho Afrika akichukua nafasi ya aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa aliyemaliza mkataba wa kuifundisha timu hiyo mwishoni mwa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara.



Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezi­pata Championi Jumatano, kocha huyo aliondoka nchini baada ya kushindwa kufikia muafaka masuala ya kimkataba na viongozi wa Yanga kabla ya kubeba mabegi yake na kurudi kwao.



Mtoa taarifa huyo alisema, kocha huyo ana wiki mbili tangu ameondoka kwenye timu hiyo iliyokuwa inajifua kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es Salaam.



“Nashangaa kuona hadi sasa mme­kuwa kimya, kocha Mcongo aliyekuja kuwa msaidizi wa Zahera sasa ni wiki mbili hayupo hapa nchini.



“Hivyo, kocha Zahera hivi sasa yupo peke yake anakinoa kikosi hicho aki­shirikiana na kocha wa viungo Mwandila (Noel), baada ya kuondoka huyo mpya.



“Kikubwa kocha huyo alishindwa kufikia muafaka mzuri na mabosi wake hao ya kusaini mkataba wa kuifundisha Yanga,” alisema mtoa taarifa huyo.



Alipotafutwa Zahera kuzungumza ku­zungumzia hilo alisema kuwa :“Sifahamu taarifa za kuondoka Yanga kwa kocha huyo, nilikuwa naye kwa kipindi fulani, lakini siku za hivi karibuni sijamuona uwanjani.”

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo

$
0
0

Uturuki Yaondoa Hali ya Hatari Iliyoidhinishwa Baada ya Jaribo la Mapinduzi

$
0
0
Uturuki Yaondoa Hali ya Hatari Iliyoidhinishwa Baada ya Jaribo la Mapinduzi
Vyombo vya habari vya taifa nchini Uturuki vimetangaza kwamba serikali imeondoa hali ya hatari iliyowekwa nchini humo kufuatia mapinduzi yaliyoshindwa miaka miwili iliyopita.

Katika kipindi hicho makumi kwa maelfu ya watu walikamatwa na kushikiliwa bila ya kufunguliwa mashtaka chini ya agizo la Rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan.

Wanajeshi, Polisi, Raia, Waandishi wa Habarai na walimu ni miongoni mwa waliokamatwa.

Maelfu wengine ikiwemo majaji kadhaa waliachishwa kazi zao.

Reli mpya ya SGR nchini Kenya yasababisha hasara ya shilingi bilioni 10

Mfanyakazi azawadiwa gari na mwajiri wake baada ya kutembea umbali wa kilomita 32

Zawadi ya Magufuli kwa Obama na mambo mengine makuu

Shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International limesema kuondolewa kwa hali hiyo ya hatari pekee hakuwezi kbadili hatua kazli za kisiasa zilizochukuliwa ambazo ziliibadili nchi hiyo na kuifanya inayokandamiza haki za binadamu.

Mapema mwezi huu Rais Erdogan aliapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Gari la wagonjwa Lakutwa Limepakia Matairi Chakavu

$
0
0
Gari la wagonjwa Lakutwa Limepakia Matairi Chakavu
GARI la kubeba wagonjwa la Wilaya ya Itilima mkoani hapa limepata ajali, huku ndani likiwa na matairi chakavu tisa, siku chache baada ya serikali kupiga marufuku magari hayo kupakia kitu chochote zaidi ya wagonjwa.


Gari hilo lenye namba za usajili STK 6646, lilipata ajali hiyo majira ya saa 10 usiku kuamkia jana, katika eneo la Daraja la Mto Bariadi, katikati ya Mji wa Bariadi na chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika.

Serikali kupitia Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, hivi karibuni ilipiga marufuku magari ya wagonjwa kubeba kitu chochote zaidi ya wagonjwa.

Hatua ya kupiga marufuku hiyo inafuatia gari moja la wagonjwa kukutwa likiwa limepakia magunia ya dawa za kulevya aina ya mirungi, huku likiacha wagonjwa wakihangaika usafiri wa kuwawahisha hospitali kupata huduma.

Gari lililokutwa na matairi hayo chakavu ni lenye namba za usajili STK 6646.

Dereva wa gari hilo Ndekeja Makwenu, amelazwa katika hospitali teule ya Mkoa wa Simiyu baada ya kupata marejaha mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Paul Nyalaja, alisema gari hilo ni moja ya magari manne yaliyopelekwa mkoani Mwanza kwa ajili ya matengenezo ya kuondolewa matairi yaliyochakaa, Jumapili iliyopita.

Nyalaja alisema kuwa baada ya matengenezo hayo gari hilo lilibeba matairi yote ya magari manne, ambayo yalikuwa chakavu kwa ajili ya kuyarejesha ofisi za usafirishaji za halmashauri hiyo kama taratibu za manunuzi zinavyotaka.

“Gari lilifika Bariadi Jumatatu usiku na kuegeshwa katika kituo cha afya Muungano, kilichopo Mjini Bariadi, katika mazingira ya kutatanisha muda wa saa 10 usiku, gari liliondolewa kwenye kituo hicho kuelekea kusikojulikana,” alisema Nyalaja.

Alisema walishangaa kukuta gari hilo limepata ajali likiwa limebeba matairi hayo huku likionekana kuligonga tela la trekta lililokuwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara baada ya kuharibika.

Kaimu Mkurugenzi huyo alieleza kuwa bado wanachunguza ili kubaini chanzo cha ajali, ikiwa pamoja na sababu za gari hilo kuondolewa kwenye maegesho ya magari ya serikali nyakati za usiku.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya hiyo, Benson Kilangi, alisema hakuna kifo kilichotokea, lakini amesikitishwa na ajali hiyo.

Alisema kutokana na mazigira ya ajali hiyo kuwa tata, ameagiza kukamatwa Ofisa Usafirishaji wa Halmashauri hiyo, Oswini Mlelwa na kuwekwa ndani kwa ajili ya mahojiano zaidi ikiwa pamoja na kufanyika kwa uchunguzi.

Nisingefanana na Mwanangu Jadeni Ningepata Tabu Sana- Ray

$
0
0
Nisingefanana na Mwanangu Jadeni Ningepata Tabu Sana- Ray
LEGENDARI wa sinema za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ amefunguka kuwa asingefanana na mwanaye aitwaye Jaden, angetukanwa sana.Akizungumza na Amani juzikati, Ray alisema, anamshukuru Mungu kwa kupata mtoto wa kufanana naye kwani vinginevyo walimwengu wangemsumbua kwa maneno ya kejeli.

“Walimwengu bwana wanaongea sana. Ingetokea mtoto labda kafuata kwa mama kila kitu halafu kwangu hamna kitu, yangeibuka ya kuibuka hadi ungeshangaa, nashukuru sana Jaden amenifichia maneno kwa kufanana na mimi,” alisema Ray.

Haji Manara Amuomba Rais Aitumbue Yanga

$
0
0

"Mh Rais Magufuli wakati huu ukikimbizana na ujenzi wa viwanda nchini na kuinua uchumi wetu. Nakuomba pia utupie jicho na hukum kuna klabu kwa miaka yote imekuwa ikitumia hovyo fedha za kigeni na kulitia aibu Taifa letu. Wameifedhehesha nchi kwa kufungwa mabao nne".
Ujumbe kutoka Kwa Haji Manara (Utani wa Jadi).
.
Unahisi Manara anawalenga akina Nani???

Je Wajua Rais wa Croatia Mwanamama Kolinda Kitarovic ni Komando?

$
0
0

Rais wa Croatia, Mwanamama Kolinda Grabar Kitarovic ni Mwanajeshi "Commando" mstaafu ambaye ndiye mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Majeshi ya kujihami kwa nchi za Magharibi (NATO) anayeshughulikia masuala ya diplomasia.

Sababu Tatu Yanga Kupokea Kichapo cha Mbwa Mwizi Kenya

$
0
0

Tumeshuhudia Yanga ikipoteza mechi yake ya pili kati ya tatu ilizocheza kwenye kombe la shirikisho Afrika. Yanga imekubali kichapo cha magoli 4-0 ugenini dhidi ya Gor Mahia kwenye uwanja wa Kasarani Nairobi-Kenya.

Imefungwa idadi ya magoli manne ambayo ilifungwa kwenye mechi yake ya kwanza ilipocheza ugenini dhidi ya USM Ulger ya Algeria.

Kuna sababu nyingi kwa Yanga kupoteza mechi yao dhidi ya Gor Mahia lakini www.shaffihdauda.co.tz imeangazia maeneo matatu.

Kiufundi.

Kwa tulichokiona tunaweza kusema Yanga hwakujiandaa lakini Gor Mahia walijiandaa. Kwenye michezo haijalishi ni soka, masumbwi au kikapu, maandalizi ni kufanya majaribio uwanjani sio mazoezi tu bila mechi za kujipima.

Huwezi kuwa umejifungia unafanya mazoezi halafu ukasema unajiandaa, Gor Mahia walikuwa na faida zote, ligi ya Kenya inaendelea, wana kikosi kipana kwa sababu waliweza kukigawanya kuna kikosi kilikuja kwenye Kagame Cup kingine kilibaki Kenya.

Yanga walikaa karibu mwezi na nusu bila mechi za ushindani tangu walipotolewa kwenye michuano ya SportPesa nchini Kenya, kwa hiyo wavhezaji hawawezi kuwa katika hali ya ushindani.

Mechi ilikuwa kati ya timu iliyojiandaa dhidi ya timu ambayo haijajiandaa na kama Gor Mahia wangekuwa makini zaidi wangefunga magoli zaidi ya manne kwa sababu walikosa mabao ya wazi kama mawili au matatu.

Kisaikolojia

Hakuna asiyefahamu kwa sasa Yanga wanapitia kipindi kigumu kuna mambo mengi ambayo alizungumza ofisa habari wa timu Dismas Ten ambayo hayahitaji elimu kubwa kutambua kwamba ndani ya Yanga mambo hayapo sawa.

Kukosekana kwa wachezaji wenye ubora  na uzoefu.

Tambwe amekosekana kwenye kikosi cha kwanza kwa kipindi kirefu sana, Yanga imemkosa Kamusoko mwenye ubora kwa muda mrefu, wamempoteza Chirwa na Ngoma, Yondani, Kessy hawakuwepo.

Ukiangalia profile ya wachezaji ambao wamekosekana na ambao walicheza dhidi ya Gor Mahia unapata picha halisi ya matokeo waliyopata.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images