Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live

“Muna Unatembea na Uchebe wa Shilole?” – Nay wa Mitego

0
0
Msanii Nay Wa Mitego ameingilia kati sakata la Shilole kumbwatukia Muna Love kwa kujitokeza na kuongea mbele ya Waandishi wa Habari ikiwa ni siku chache tu baada ya Mtoto wake Patrick kufariki, tutakusomea yote aliyosema Nay wa Mitego ukibonyeza play  hapa chini: VIDEO:

"Maisha ya Mitandao Yanatesa Wengi" Rose Ndauka.

0
0

Mwanadada kutoka bong movies Rose Ndauka amefunguka na kusemakuwa maisha wanayoishi watu katika mitandao yanawapa matesi sana kutokana na ukweli kuwa wengi wao hawaishi yale maisha yao ya kiuhalisia na kuishia kuiga vitu ambavyo kwa namna moja ama nyingine sivyo walivyo.

Akitoa maoni yake kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii Rose Ndauka anasema ‘ maisha ya mitandao yanatesa wengi na wengine kusahau kabisa uhalisia watu na kupotea  na kujiona kuwa wao ndio wanahaki ya kila kitu.jamani tuwe makini na hii sehemu inayotukutanisha wengi , nadhani hata walioweka walikuwa na  nia nzuri”

Maneno ya Rose ndauka yanaweka ukweli uliopo bayana kabisa kwa maisha ya sasa ya mitandaoni ambapo watu wamekuwa wakijitahidi kuishi maisha yasiyo yao ilimradi tu kuwafurahisha au kuwaonyesha wengine wana uwezo wa kufanya kitu flani.

Tuhuma za Billnass Kuwa ni Marioo, Mwenyewe Afunguka Haya

0
0
Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko yake ya kurap, Billnas amefunguka na kukataa kata kata tuhuma alizorushiwa na Steve Nyerere kuwa ni mariooo.

Hivi karibuni Billnas na Steve Nyerere walijikuta katika vita kali ya maneno Kwenye mitandao ya kijamii baada ya Steve kumtuhumu Billnas baadhi ya mambo ikiwemo kuwa Marioo.

Billnas ameibuka na kukana taarifa hizo sio tu kwamba sio Marioo bali pia amemnyooshea kidole Steve na kudai inawezekana yeye ndio marioo maana anaonekana tu.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Billnas amemwagia povu hili Steve Nyerere:

Mimi siwezi kuwa marioo halafu ukishawahi kusikia msemo “Anayesifia mvua ujue imemnyeshea” basi ndiyo yule ukiona mtu amezidiwa anakimbilia umarioo basi ujue yeye ana fanya huo umarioo.

Kwanza sina hiyo lifestyle ya kimarioo na siwezi kuwa Marioo ndio maana nina vitu kama Tagi Ubavu kwaiyo asiongee kitu ambacho hakijui”.

Joh Makini Adai Haoni Tatizo Kwa Wasanii Wa Kiume Kuvaa Vikuku

0
0
Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa staili ya kuchana kutoka katika kundi la Weusi Joh Makini au Mwamba wa kaskazini amedai haoni tatizo kwa wasanii wa kiume kuvaa vikuku kama wanataka kufanya hivyo.

Joh Makini wameweka wazi kuwa wasanii wa kiume kuvaa vikuku miguuni sio kitu cha ajabu kama watu wengi wanavyodhani kwani anaamini ni fasheni kama fasheni nyingine.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, amesema kuwa wasanii ni watu ambao wanaishi na fasheni na style mbalimbali hivyo msanii kuvaa kikuku ni maamuzi yake na yeye anachukulia kawaida kabisa suala hilo;

Sijui kesho lakini mimi nachukulia kama style yake kama mimi nilivyoamua kuweka Rasta kuna wengine wameamua kuvaa vikuku wengine kutoboa pia na masikio lakini Sioni tatizo lolote kama mtu ameamua kuchagua aina ya maisha anayoishi”.

Wiki iliyopita msanii  wa muziki Diamond Platnumz aliposti picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akionekana mguuni akiwa amevalia cheni maarufu kwa jina la kikuku jambo ambalo lilisababisha ashambuliwe na mashabiki wake mitandaoni.

Tunatibu Na Kuponesha Kabisa Upugufu wa Nguvu za Kiume, Busha, Kisukari na Vidonda vya Tumbo

0
0
TUNATIBU NA KUPONESHA KABISA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME UUME MDOGO? BUSHA BILA KUPASUA KISUKALI NA VIDONDA VYA TUMBO? asilimia kubwa ya wanaume wanaupungufu wa nguvu za kiume NA maumbile madogo NI NINI KINACHOSABABISHA UUME KUZIDI KUWA MDOGO NA WEMBAMBA 1 kuugua chango LA uzazi 2 unene kupita kiasi 3 kuvaa nguo au chupi za kubana 4 kupiga punyeto kwa mda mrfu ,NI NINI TIBA YAKE MAKAKANUA MIX nidawa ya mitishamba iliyochanganywa NA mizizi kumi NA mbili urfusha NA kunenepesha UUME saizi upendayo ich 5,6,7, NA 8 kwa urfu NA sentimita 3,4, na 5 ipo dawa ya kunywa na kupaka NI NINI KINASABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME 1 kupungukiwa kwa homoni ya testerone 2 kuhudhurika kwa Neva au uti wa mgongo 3 utumiaji holela wa madawa ya kizungu 4 usongo wa mawazo na asira 5 utumiaji wa vyakula vya mafuta mengi NI NINI TIBA YAKE MAPRO POWER NO 2 NDIO tiba tosha kwa sasa kwani utibu matatizo matatu kwa pamoja 1 itakufanya uchelewe kufika kileleni dk 15 adi 20 ,2 itakufanya urudie tendo zaidi Mara tatu 3 uhimalisha uume uliolegea na kusinyaa OKOA NDOA YAKO SASA ujihepusha na lawama ndani ya ndoa yako au pale ukutanapo na mpezi dawa hii itamfanya mpenzi wako hakueshimu na hasitoke nnje ya ndoa na ata wazee wenye umri mkubwa wanapona zipo dawa za kupunguza kitambi,minyama uzembe, presha ,kisukar mvuto wa mpezi au biashara FIKA OFISINI KWETU MBAGALA ZAKHEMU na wateja wa kanda ya ziwa yupo wakala wetu mwanza mjini au piga simu 0752348593

DR MABULA na utaletewa popote ulipo uduma hizi

Nyimbo za Siku Hizi ni Bigijii- Master J

0
0
Nyimbo za Siku Hizi ni Bigijii- Master J
Muandaaji wa muziki nchini, Master J ameweka wazi kuwa anasikitishwa na baadhi ya wasanii kupenda kutengeneza kiki katika utoaji wa nyimbo zao na kupelekea kupoteza mvuto kwa wasikilizaji muda mfupi baada ya kutolewa na kuziona kama 'bigijii' ambazo hutafunwa kwa muda mfupi na kuisha utamu

Akizungumza na www.eatv.tv, Master J ameeleza kuwa chanzo cha yeye kulalamika juu ya wasanii hao  ni kwa sababu mtindo huo hauendelezi bali unaua muziki wa Tanzania, na kuongeza kuwa ni wazi jambo hilo limeshamiri kwa kiasi ambacho mara nyingine aonapo fujo za baadhi ya wasanii katika mitandao, yeye huwaelewa moja kwa moja kuwa wanampango wa kutoa wimbo.

"Hakuna kitu kinachoua muziki dunia nzima kama kiki, lakini ndiyo tulipo huko kwa sasa. Hili ni tatizo, na sio kwetu tu hata nchi za nje kama Marekani na Nigeria lipo. Licha ya kuwa hapo ndipo wasanii wanapotengenezea pesa zao, ila mwisho wake tutaujua tu. Mimi nalalamika sababu navyoona tunapoelekea siyo pazuri, sisi tulifanya kazi kubwa sana kujenga misingi ya muziki wetu", amesema Master J.

Pamoja na hayo, Master J ameendelea kwa kusema "haiwezekani mpaka mtu akae nusu utupu ndiyo iwe kiki ya kutoa wimbo wake. Mfano wiki hii nimeshaona wasanii wakubwa wakifanya fujo kwenye mitandao ya kijamii nikajua hawa wanataka kutoa wimbo, na cha ajabu wametoa kweli wimbo kupitia fujo zao mitandaoni".

Hata hivyo Master J ameeleza utofauti wa muziki uliokuwa unafanywa enzi za zamani kuwa ulikua na maudhui, yaani nyimbo ambazo mtu alikuwa na uwezo wa kuchambua mfano zile zilizokuwa zikiongelea masuala mbalimbali yanayoikumba jamii. Tofauti na baadhi ya muziki wa kileo ambapo hukosa maudhui hayo.

"Mfumo wa muziki umebadilika , zamani tulikua tukitengeneza muziki wenye maudhui tofauti na siku hizi mfano Muheshimiwa Sugu enzi hizo unaweza ukachambua baadhi ya nyimbo zake zikizungumzia vitu ambavyo vipo kabisa kwenye jamii mfano unyanyasaji wa raia unaofanywa na polisi, unyanyasaji wa wanawake na mengineyo. Yani kifupi ilihitaji ubunifu wakuzungumzia mambo huku ukiburudisha....

Wasanii wa siku hizi wanafanya muziki kama bigijii ambayo ukiweka mdomoni utatafuna na baada ya muda inaisha utamu, hivyo mtu akisikiliza atachoka tuu. Na sio tu wasanii watanzania wanafanya hivyo bali hata wamarekani na wanigeria. Kipindi hiko unakuta wasanii kama Ray C, Mr Paul, Juma Nature na wengineo hata wasipotoa wimbo mwaka mzima bado wakirudi ngoma huendelea na kasi ya utamu ule ule", amesisitiza Master J.

Msitumie Magari Kwenda kwa Michepuko Yenu- Waziri Ndalichako

0
0
Msitumie Magari Kwenda kwa Michepuko Yenu- Waziri Ndalichako
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako kwa niaba ya Serikali amekabidhi magari 47 kwa ofisi za uthibiti ubora wa shule za kanda na Wilaya pamoja na baraza la mitihani Tanzania kwajili ya kusaidia  kuongeza ubora wa elimu nchini.

Prof Ndalichako amesema…>>>“Haya ni magari kwa ajili ya ufuatiliaji wa elimu na ninaagiza kwamba yasitumike tofauti na masuala ya elimu, yeyote atakayeenda kinyume kibarua chake kimeota nyasi.”

“Madereva mtakaokabidhiwa haya magari ni moto msije mkacheza nayo, isiwe umetumwa kwenye kazi wewe unaenda kwa michepuko yako. Utakiona cha mtemakuni” –Prof Joyce Ndalichako

Trump Amualika Rais wa Urusi Washington

0
0
Trump Amualika Rais wa Urusi  Washington
Rais wa Marekani Donald Trump anakusudia kumwalika Washington, Rais wa Urusi Vladmir Putin baadaye mwaka huu, licha ya kuendelea kuwepo ukosoaji juu ya mkutano wao uliofanyika Jumatatu wiki hii katika mji mkuu wa Finland Helsinki.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Sara Sanders amesema majadiliano kuhusiana na ziara hiyo tayari yameanza.

Hata hivyo, Kiongozi wa maseneta kupitia chama cha Democrat nchini humo Chuck Schumer ameupinga mualiko huo mara moja kwa kusema kuwa Rais Trump hapaswi tena kukutana ana kwa ana na Rais Putin mpaka pale Wamarekani watakapojua nini kilitokea katika mkutano wa Helsinki.

Awali katika mkutano wake na kituo cha televisheni cha CNBC Rais Trump alitetea tena msimamo wake wa kuimarisha mahusiano na Urusi, lakini amesema kama jambo hilo halitafanikiwa, atakuwa adui na Rais huyo wa Urusi kushinda ilivyokuwa awali.

Wakati huohuo taarifa hizo za mualiko wa Rais Putin, zimeonekana kumshangaza Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa wa Marekani Dan Coats, ambaye aliambiwa jambo hilo katika mahojiano ya moja kwa moja wakati wa mkutano wa usalama uliofanika katika jimbo la Colorado.


Ameongeza kusema kuwa bado hajafahamu nini walichojadili Rais Putin na Trump katika mkutano wao, ambao ulihudhuriwa tu na watafsiri wao.

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo

Waziri Mkuu Ampongeza Balozi Mbelwa Kairuki

0
0
Waziri Mkuu Ampongeza Balozi Mbelwa Kairuki
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na Balozi wa Tanzania nchini China, Balozi Mbelwa Kairuki na amempongeza kwa kazi nzuri anayoifanya tangu aende huko.

Amekutana na Balozi Kairuki jana katika makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam, na amemtaka Balozi huyo ahakikishe anaboresha mahusiano kati ya Tanzania na China.

“Ni lazima nikupongeze kwa namna unavyoendelea kufanya kazi na unavyojitahidi kudumisha mahusiano na China. Tunashukuru kwamba wageni wanaokuja hapa nchini kutoka China wanatoa taarifa nzuri na jinsi unavyosaidia kuitangaza nchi yetu huko nje.”

“Umefanya kazi nzuri ya kuwaelekeza wawekezaji wa huko kwamba wakati tunaunda Serikali na kutengeneza mfumo wa utawala, tuliamua kujenga kwanza mifumo imara na kutambua fursa zetu tulizonazo ili baadaye Watanzania waweze kunufaika na hizo fursa.”

Amesema kupitia utaratibu huo, Serikali ilitaka Watanzania wamiliki ardhi ndipo mgeni apate, na kama kuna uzalishaji wowote unafanyika basi Mtanzania awe wa kwanza kunufaika, Serikali inufaike na mwekezaji naye anufaike.

“Tunakushukuru kwamba umesaidia kuwaambia wachina watulie wakati Serikali ikirekebisha mifumo yake. Na wao wameyaona mabadiliko hayo, kwani tumesimamia vita dhidi ya rushwa, na wao walikuwa ni waathirika wakubwa, lakini pia tumeongeza uwajibikaji. Watu wetu sasa wanawajibika kwenye viwanda na makampuni yao na Watanzania kwa ujumla, wametambua umuhimu wa kufanya kazi ili waweze kuishi,” amesema.

Waziri Mkuu amesema Serikali hivi sasa iko kwenye programu ya kutangaza utalii uliopo nchini hasa kwa kuamua kuagiza ndege kubwa zitakazobeba watalii na kuwaleta moja kwa moja hapa nchini.

“Sasa hivi tumepata wageni maarufu kutoka nje ya nchi akiwemo Rais mstaafu wa Marekani, Mheshimiwa Barack Obama na wachezaji maarufu duniani, kwa hiyo tunaendelea na mikakati yetu ya kutangaza utalii huko nje.”

Haji Manara Aguswa na Kichapo cha Yanga Awapa Pole Kiaina

0
0
Haji Manara Aguswa na Kichapo cha Yanga Awapa Pole Kiaina
Ofisa Habari wa klabu ya Simba amezungumzia kichapo walichokipata watani zao wa jadi katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC cha mabao 4-0.

Manara ambaye amekuwa akiwatania Yanga haswa kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii mara nyingi, amewapa pole akisema kuwa ni sehemu ya mchezo.

Mbali na pole hizo, Manara ameeleza kuwa wakati akihamasisha timu hizo zipeane uzalendo wakati Simba alipokuwa anajiandaa kushiriki mashindano ya Shirikisho Afrika, amesema Yanga walikataa ombi lake.

Manara amesema kitendo cha Yanga kupingana naye kilimfanya Manara kuendelea kuiombea mabaya Yanga na kipigo cha jana amekielezea kama faraja kwake huku akiwapa pole ya kiaina.

Yanga walikubali idaidi hiyo ya mabao juzi Jumatano huko Nairobi, Kenya na kujiwekea mazingira magumu ya kuendelea kusalia kunako mashindano hayo wakiwa wana alama moja pekee katika kundi D.

MC Alger ipo kileleni ikiwa na alama moja wakifuatia na Gor Mahia wenye alama 5 huku Rayon Sports ya Rwanda ikiwa na mbili na Yanga wakiwa na moja pekee.

Mapokezi na Huduma Nzuri Zamkosha Ronaldo Agawa Milioni 53 kwa Wahudumu Wake

0
0
Mapokezi na Huduma Nzuri Zamkosha Ronaldo Agawa Milioni 53 kwa Wahudumu Wake
MUDA mfupi baada ya kuanza maisha ya kuwa mchezaji wa Juventus, Cristiano Ronaldo ameonyesha kuwa yeye ni mtu wa watu.



Ronaldo, 33, alikuwa nchini Italia siku kadhaa zilizopita ili kukamilisha dili lake la kusajiliwa na Juventus, inaelezwa kuwa akiwa hotelini alipofi kia alifurahishwa na huduma aliyopatiwa kutoka kwa watoa huduma na ndipo akaaamua kuwapa fedha wagawane.



Akiwa hotelini hapo na baadhi ya memba wa familia yake, kabla ya kuondoka aliwaita wale wote waliokuwa wakiwahudumia na kuwapa pauni 17,850 (Sh milioni 53) kama zawadi ya huduma nzuri na kuwaambia wagawane.

Picha : Ndoa ya Zabibu Kiba na Abdu Banda Yaiva

0
0

Picha : Ndoa ya Zabibu Kiba na Abdu Banda Yaiva

Baada ya ndoa za kaka zake wawili kutikisa jiji, mwanadada Zabibu Kiba nae ameibuka na kukamilisha lile walilokuwa wamekamilisja ndugu zake hapo awali la kufunga ndoa na mpezni wake wa siku nyingi Abdul Banda ambae ni mchezaji mpira wa timu ya taifa.

Picha zilizosambaa katika mitandao ya kijamii znaonyesha maandalizi ya kwanza ya harusi hiyo.





Ridhiwani Afunguka Kifo cha Babu Yake Atoa Ratiba ya Mazishi

0
0
Ridhiwani Afunguka Kifo cha Babu Yake Atoa Ratiba ya Mazishi
KUFUATIA kifo cha Baba mzazi wa mke wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mzee Rashid Mkwachu aliyefariki dunia jana Alhamisi, Julai 19, 2018 majira ya saa tatu asubuhi, mjukuu wa marehemu, Ridhiwani Kikwete amezungumzia msiba huo na kusema kuwa tatizo kubwa lililokuwa likimsumbua babu yao ni moyo na hali ya uzee.



“Babu yetu alikuwa mzee sana, zamani utunzaji wa kumbukumbuku haukuwa mzuri, lakini anakadiria kuwa ameishi kwa miaka 104 au 107. Sisi hatuna kubwa la kusema lakini tunadhani tu kwamba umri wake ulikuwa umefika. Kuna wakati alikuwa anasumbuliwa na moyo kushindwa kusukuma damu vizuri, presha ya kupanda na ya kushuka.”



“Nitamkumbuka babu kwa kuwa alipenda sana kutupigisha stori hasa za mpira, simulizi na maisha yake ya kila siku, ni vitu vingi alikuwa akinishauri enzi za uhai wake, mengi yalikuwa ni kunitakia kheri kwa yale niliyokuwa nikiyafanya,” amesema Ridhiwani.



Kwa mujibu wa taarifa Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni msemaji wa familia, msiba huo upo nyumbani kwa Dkt. Jakaya Kikwete maeneo ya Msasani jijini Dar es Salaam na mazishi yatafanyika leo Ijumaa, Julai 20, 2018 katika Makaburi ya Kisutu majira ya saa 10:00 jioni.

Ratiba ya Mazishi

Ray C Amuunga Mkono Muna "Naamini Kuna Mzigo wa Maumivu Kutoka Moyoni Mwako Umeutua"

0
0
Ray C Amuunga Mkono Muna "Naamini Kuna Mzigo wa Maumivu Kutoka Moyoni Mwako Umeutua"
Baada ya muna kuongea yaliyopo moyoni mwake kuhusu swala la marehemu mtoto wake Patrick   kusema wazi juu ya baba wa mtoto wake kuna watu waliongea mengi kila mtu akim-judge  Muna kwa lake huku wengine wakisema kuwa ameyafanya mapema sana mambo hayo alitakiwa kusubiri mpaka 40 ya mtoto huyo  ipite ndio aongee hayo.

Lakini wapo waliomtetea na kumuona kama alichokifanya labda kinaweza kumsaidia kukaa kwa amani lakini pia labda kingeweza kufunga midomo ya baadhi ya watu waliokuwa wakimhukumu bila kujua kwa nini yalitokea yaliyotokea.

Ray c ameguswa na maamuzi ya Muna na hivyo aliamua kuongea kuhusu swala hilo la kumpongeza kwa kumwambia kuwa aloichokifanya kimeweza kumuondolea mzigo wa maumivu yake aliyokuwa nayo kuhusu mtoto wake.

"Una uhuru wa kuwa muwazi pale unapoona mambo fulani yamekuumiza au hayajakaa sawa,kuongea kuna kufanya nafsi yako inakaa sawa,safi muna ninaamini kuna kamzigi flani umekatua  kutoka kwenye moyo…good job.

Mwanamke Hawezi Kuchepuka na Akaendelea Kumpenda Mume wake Kwa Dhati

0
0

Mwanaume anaweza kuchepuka na bado akawa na upendo wa dhati kwa mke wake lakini mwanamke hawezi kuchepuka na akaendelea kumpenda mume wake kwa* dhati.

Nasema hivi kwasababu mwanaume hafanyi tendo la ndoa kwa hisia, mwanamke hawezi kufanya tendo la ndoa bila hisia mguso.Ndiyo maana wanaume wanahitaji mahali pa kufanya tendo la ndoa ila wanawake wanahitaji sababu ya kufanya tendo la ndoa.

Wanawake wengi wanaoenda mahakamani kudai talaka kwa waume zao ni wale wachepukaji,mwanamke asiyechepuka hawezi kwenda mahakamani kudai talaka isipokuwa kama mumewe atakuwa amezidisha unyanyasaji wa kimwili na kiakili kiwango cha kukaribia kumuua mkewe.

Wanaume hawawezi kubadili tendo la ndoa na upendo.Mwanaume anaweza kufanya tendo la ndoa na mwanamke lakini bado akawa hampendi-ndiyo maana wanawake wanaojikuta kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanaume waliooa *wanaowapenda* wake zao kwa dhati hupata tabu saana kupata kufurahia mahusiano hayo kwani huwa wanatumika tu na hao wanaume wenye ndoa zao. Lakini pindi tu mwanamke aliyeolewa anapolala na mchepuko wake huanza hata kusimulia habari za siri kuhusu mume wake na anaweza pia kusema ni kwa namna gani anamchukia mume wake;anaweza hata kukubali kuchukua sumu kwa mchepuko wake ili amwangamize mume wake.

Kwa *mwanaume tendo* la *ndoa* na *upendo* ni vitu viwili tofauti* kabisa,lakini kwa mwanamke tendo la ndoa na upendo ni vitu viwili vinavyoenda sambamba.Kwa mwanaume tendo la ndoa huja kwanza kabla ya upendo (matamanio) lakini kwa mwanamke upendo huja kwanza kabla ya tendo la ndoa (upendo wa dhati); kwahiyo pindi mkeo anapoanza kuchepuka upendo wake huhama kutoka kwako kwenda kwa mchepuko, anaweza hata kuanza kumpa chakula kizuri na mahaba ambavyo amekuwa akikupa wewe tu.

*Mwanaume* *kuchepuka* *haimaanishi* kuwa *ameacha* *kumpenda* *mkewe* la hasha!, ila siwezisema hivyo kwa upande wa mwanamke.Pindi mwanamke anapoanza kuchepuka anakuwa ametumbuki kimapenzi kwa mchepuko huo na maisha kwenye ndoa hayawezi kuwa sawa kamwe; na anaweza hata kumuua mmewe endapo tu atakuwa ameanza *kuchepuka.Mkeo akianza kuchepuka utakuwa mwanaume mwenye bahati sana endapo hautakufa ndani ya miaka 10 .

*B. Tafiti* . *zinaonesha* kuwa *95* % ya *wanawake* *wanaochepuka* *huwaombea* *waume* zao *wafe* haraka, ndiyo maana ni hatari sana kwa mwanaume kuendelea kuishi na mwanamke anaechepuka; vilevile ndiyo maana inashauriwa kila mahali hata kwenye Biblia kumtaliki mwanamke pindi tu anapogundulika kuwa amezini(amechepuka).

*Mwanamke* *anaechepuka* ni *hatari* kwa *uhai* wa *mume* wake kuliko hata wauwaji au silaha.Kuna wanawake wengi wachepukaji duniani hualika wauwaji usiku waje watoe uhai wa waume zao na askari hata ndugu wa mume hawawezi kugundua hilo kwani msibani huyo mwanamke atakuwa analia kwa uchungu wa kuigiza na kuficha maasi yake.Ndiyo maana wanasaikolojia hukataza sana mwanamke kuchepuka kuliko mwanaume.Wanawake hawawezi kuhimili mitafaruku ya kihisia itokanayo na kuchepuka; ndiyo sababu wanaume watafiti na wenye uelewa mkubwa watajua tu kuwa mkewe ameanza kuchepuka kwasababu huanza kumdharau mmewe na hujaribu hata kumnyima mumewe tendo la ndoa kwa visingizio lukuki.

*Tafiti* *zinaonesha* kuwa *90* % ya *wanawake* *wanaochepuka* *hawafurahii* *tendo* la *ndoa* na waume zao hapo mwanaume makini atagundua tu hasa tabia za mkewe zitakapobadilika kuhusiana na tendo la ndoa, lakini mwanaume zube hawezi kugundua hili ataendelea kuvumilia sababu dhaifu za kunyimwa unyumba mpaka atakapoondolewa duniani.

*Mwanamke* *hawezi* *kuchepuka* na *mtu* *ambae* *hampendi* , huwa wanaitoa mioyo yao kwa kila kitu, ndiyo maana huwezi kuamini maamuzi yao.Kichekesho kikitolewa wanawake wengi wanaocheka hawacheki eti kwa sababu kichekesho ni kizuri ila ni kwasababu huwapenda wale waliotoa vichekesho hivyo; na endapo hawakupendi hata kichekesho chako kingekuwa kizuri kwa kiasi gani hawatacheka, ila mwanaume akicheka kuhusu kichekesho fulani ni kwasababu kichekesho chenyewe ni kizuri lakini si kwasababu eti anampenda mchekeshaji hii ni kwasababu wanaume wana uwezo wa kukabili hisia.

ila ni vigumu kukuta ndoa imesimama na mambo yanaenda sawa huku mwanamke akiwa mchepukaji.Ninarudia, karibia 100% ya wanawake wanaochepuka huwaombea waume zao wafe haraka au hulazimisha talaka ili wawe na uhuru wa kufurahia penzi la kwenye mchepuko, ila wanaume wengi hawawezi kuruhusu wake zao wa ndoa wanyanyaswe ama kwa vitendo au kwa maneno na michepuko yao, siku zote wanaume husimama upande wa wake zao.Mwanaume anaweza kuchepuka na bado akampenda mkewe lakini mwanamke hawezi kuchepuka na bado akampenda mmewe.

*Pindi mkeo anapoanza kulala na mwanaume/wanaume wengine ujue kifo chako ki karibu.* "

Hukumu ya Kesi ya Wema Sepetu Kutolewa Leo

0
0
Hukumu ya Kesi ya Wema Sepetu Kutolewa Leo
Mahakama ya kisutu mjini Dar es Salaam inatarajiwa kutoa hukumu dhidi ya kesi ya umiliki wa bangi inayomkabili aliyekuwa mshindi wa shindano la malkia wa urembo nchini Tanzania Wema Sepetu.

Hakimu mkaazi Thomas Simba aliambia mahakama hiyo siku ya Jumatatu kwamba hukumu hiyo iliotarajiwa kutolewa siku ya Jumatatu sasa itatolewa Ijumaa baada ya kukamilika kwa maswala machache yaliokuwa yamesalia.

Wema Sepetu ambaye alishinda taji la malkia wa urembo nchini humo 2006 atahukumiwa pamoja na washtakiwa wengine wawili Angelina Msigwa na Matrida Seleman Abas .

Inadaiwa kwamba mnamo tarehe 4 mwezi Februari mwaka uliopoita , Wema na wenzake walipatikana wakimiliki misokoto ya bangi katika eneo la Kunduchi Ununio.

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Mafupi na Upungufu wa Nguvu za Kiume? Suluhisho Hili Hapa

0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WANA MAUMBILE MAFUPI NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME DR SITTA NDO SULULISHO LAKO tatiza, hili limekuwa likiwaasili watu wengi,sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine, kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo zipo , sababu nyingi zinazosababisha, tatizo hilo baadhi ni (i) upungufu wa vichocheo vya HORMONES ZA CETROGEN ambazo mwanaume, anapobarehe vichocheo hivi, HORMONES hizo, husaidia ukuaji wa uume

SUPER MIZIZI, ni dawa inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi utakayo na kuzibua mlija iliysinyaa,

NSHOLA ni dawa bora, ya kurudisha nguvu, za, kiume bari inatibu ,kabisa kutoa tatizo hilo, na kukupa , hamu ya , kurudia tendo, la ndoa zaidi, ya mala nne 4 ,bila kuchoka atakama unaumli ,wa mika 80,! pia ana ,dawa za ,kutibu, presha ya kupanda ,na kushuka, kisukari kuondoa, mafuta , mwilini ,na maumivu ya, mgogo kiuno, dawa zipo, matazo, ya hedhi, kwa ,wanawake hedhi, zisizokuwa na, mpangilio, na kasonono, pia , vidonda ,vya, tumbo ,(STOMACHI UCLENS) IHUSHI ndoji lako.

NKANYA ni dwa ya mvuto wa kimapenzi ,mchumba mpenzi ariyekuacha, mke mme, atakuludia kwa, mda, wa msaa3 tu , ukishaitumia atarudi ,mwenyewe bila ,ugovi tena, NKOMA ni dawa kuongeza HIPS na mguu wa bia kwa wadada .

HERBON, ni, dawa, ya kuongeza, CD4, NGAKAMA ,ni dawa ya kutibu ,miguu, kufaganzi, na ,kuwaka moto, huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa! DR SITTA, amebobea, kwa tiba asilia

DAR ANAPATIKANA MBAGALA, ZAKHEM, SONGEA BOMBAMBILI SHINYANGA, KAHAMA MJINI, KWA MAELEZO ZAIDI ,

PIGA SIMU 0763172670 au 0715172670

Watu Wanne Wanusurika Kuchomwa Moto Kisa Ushirikina

0
0
Watu wanne wanusurika kuchomwa moto kisa ushirikina
Watu wanne wamenusurika kuchomwa moto kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya ushirikina katika hifadhi ya msitu wa Isawima kijiji cha Mpanda Mlowoka wilayani Kaliua mkoani humo.

Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo kamanda wa polisi mkoa wa Tabora kamishna msaidizi EMMANUEL NLEY amesema tukio la mauaji lilitokea usiku wa July 14 ambapo marehemu alivamiwa na kuuawa kwa kukatwa shingo na kitu chenye ncha kali.

Kamanda NLEY anaendelea kuelezea tukio lingine la wakina mama wanne walionusurika kuchomwa moto

Katika tuki hilo jeshi la polisi limefanikiwa kukamata pikipiki mbili moja ikiwa ni mali ya Mtemi wa sungusungu wa eneo hilo pia kuwatia nguvuni watu kumi na sita.

Mbali na matuki hayo pia mnamo july 14 huko katika kata ya ipuli mjini Tabora mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la REGINA ATHUMANI aliuawa kwa kupigwa kisha kunyongwa na mumewe

Jeshi la pilisi mkoani Tabora limewataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheia mkononi

Bodi ya Ligi Yatoa Masharti kwa Klabu Zinazosajili Wachezaji wa Kigeni

0
0
Bodi ya Ligi Yatoa Masharti kwa Klabu Zinazosajili Wachezaji wa Kigeni
Wakati ukiwa umesalia mwezi mmoja pekee huu wa saba kuelekea msimu mpya wa Ligi kuu Bara 2018/19, Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, ametoa masharti kadhaa kwa klabu zinazosajili wachezaji wa kigeni.

Kwa mujibu wa Radio One, Wambura amesema kwa kila timu inayotaka kusajili mchezaji wa kigeni ni lazima ihakikishe ana ubora wa kutosha na si ilimradi awe anatoka nje ya Tanzania.

Mbali na ubora, Wambura ameeleza mchezaji yoyote wa kigeni anapaswa kucheza na si kukaa benchi ili kuonesha kweli kuwa yeye ni wa kimataifa halisi na si wale ambao wamekuwa wakiletwa kisha wanashindwa kucheza.

Vilevile Wambura amezitaka klabu zote endapo zinasajili wachezaji wa kigeni ziwe na uwezo wa kuwalipa mishahara yao vilivyo na isije ikatokea wanadai kwa maana watachukua hatua kwa wahusika.

"Tunataka klabu ikishasajili mchezaji wa kigeni ni lazima kwanza iwe na uwezo wa kumlipa stahiki zake zote ikiwemo mshahara, hatutaki kusika anadai, pia tunataka mchezaji huyo awe na uwezo unaoashiria kuwa ni wa kimataifa na si wa kukaa benchi" alisema Wambura.
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live




Latest Images