Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live

Stamina aeleza kwanini remix ya ‘Number 1′ ilihit kuliko remix za nyimbo zingine za Bongo

$
0
0
Msanii wa Hip Hop kutoka Morogoro, Stamina ametoa sababu ya nyimbo nyingi za bongo zinazofanyiwa remix kutofanya vizuri hapa nyumbani.

Stamina aliitolea mfano remix ya ‘Number One’ ya Diamond na Davido kwa kudai kuwa msanii huyo alijua timing pamoja na thamani ya msanii aliyefanya naye.

“Diamond remix yake ilifanya vizuri kwasababu kwanza nyimbo ilikuwa hit, pili alijua kucheza na timing kitu ambacho ni cha umuhimu sana,” Stamina aliambia Bongo5. “Na tatu jinsi alivyopandisha thamani ya wimbo huo kwa kufanya kolabo na msanii mkubwa Africa kama Davido. Sasa kwanini isifanye vizuri? Kwahiyo timing, yaani muda wa kutoa hiyo remix. Kwasababu hauwezi kutoka remix kabla haijatoka original version. Unakuta original version imekufa wewe unadhani kufanya remix ndo utairudisha? Umefanya nyimbo ya masikitiko, nyimbo ya masikitiko unaifanyiaje remix, unataka usikitike nini zaidi? Remix nyingi zinakuwa ni nyimbo za party au nyimbo za umimi. Yaani zile nyimbo za kama kutuNishiana na kuoneshana nani zaidi. Kwahiyo tatizo kubwa wasanii wengi wanakosa kujua mambo kama hayo,” alisema Stamina.
-Bongo5

EPL: Matokeo ya Manchester United vs Everton Haya Hapa

$
0
0
Baada ya kukubali kunyanyashwa mara mbili mfululizo msimu uliopita na Everton, hatimaye leo Manchester United ilipata nafasi kufuta uteja wao kwa klabu hiyo ya Merseysed.
Katika mchezo uliomalizika hivi punde katika uwanja wa Old Trafford umemalizika kwa Man United kufuta uteja mbele ya Everton.
Kikosi cha Louis Van Gaal kimefanikiwa kupata ushindi wa 2-1.
Angel Di Maria alifungua akaunti ya magoli katika mchezo wa leo katika dakika ya 25 baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Juan Mata.
Dakika moja kabla ya mapumziko Leighton Baines alikosa mkwaju wa penati baada ya Luke Shaw kumkwatua mchezaji wa Everton.
Kipindi cha pili Everton walirudi vizuri na kufanikiwa kupata goli la kusawazisha kupitia Naismith.
Baada ya goli hilo Man United wakajipanga upya na alikuwa yule yule Angel Di Maria akatoa pasi nyingine ya mwisho kwa Falcao aliyefunga goli la ushindi.
United inabidi wamshukuru kipa David De Gea kwa kazi nzuri aliyoifanya kuokoa michomo ya magoli ya wazi na hatimaye wakafanikiwa kumaliza mchezo wakiwa na ushindi wa 2-1.

Matokeo ya Arsenal vs Chelsea Haya Hapa

$
0
0
Ile mechi ya kuamua nani mbabe wa jiji la London kati ya Chelsea dhidi ya Arsenal imemalizika muda mfupi uliopita.
Matokeo kwenye mchezo huo uliokuwa na kashi kashi nyingi ukiwemo ugomvi wa kushikana mashati wa Wenger dhidi ya Mourinho – ni ushindi wa 2-0 kwa Chelsea.
Eden Hazard alianza kuiadhibu Arsenal kipindi cha kwanza baada ya kufunga mkwaju wa penati baada ya kufanyiwa madhambi na Koscienly.
Kipindi cha pili katika dakika za mwishoni Diego Costa alipokea pasi nzuri kutoka kwa Cesc Fabregas na akaifungia Chelsea goli la pili na kuhitimisha ushindi huo dhidi ya Gunners.

Matokeo ya Yanga SC dhidi ya Wanajeshi JKT Ruvu Haya Hapa

$
0
0
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao lililofungwa na Kelvin Yondani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga Imeshinda katika Mchezo Huo

Wema Sepetu na Mwanamuziki Diamond Wazindua Gari Kwa Mahaba Mazito Huku Watu Wakishuhudia

$
0
0
Stori: Richard Bukos
Mahaba nimalize! Mastaa wapendanao, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wamesababisha tukio jipya kama kawaida yao, safari hii wameishtua kadamnasi kwa kuzindua gari jipya kwa mahaba mazito ndani yake, Ijumaa Wikienda lilinyaka mchongo mzima.

KAMA MUVI YA MAPENZI
Tukio hilo lililojiri kama muvi ya mapenzi (romantic movie) lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee uliopo Posta jijini Dar wakati Diamond alipokuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa na kujizawadia ndinga aina ya BMW X6 ambalo waliligeuza kuwa uwanja wa malovee wakati walipokwenda kukabidhiwa na menejimenti yake ya Wasafi.

SHEREHE ILIVYOANZA
Awali, waalikwa sambamba na mastaa mbalimbali wakusanyika kwenye ukumbi huo na ilipofika saa 5:00 usiku, Diamond akiwa ameambatana na ubavu wake, Wema sambamba na mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’, waliingia na sherehe kuanza.

TUKIO LA ZAWADI
Baada ya sherehe hiyo kupambwa na matukio mbalimbali zikiwemo bendi za asili na wasanii, ulifika wakati wa zawadi ndipo wageni waalikwa walipoanza kujinadi kupitia kipaza sauti na mwishoni ikawa ni zamu ya menejimenti ya Wasafi ambayo ilitamka kuwa inatoa gari hilo.

CHIEF KIUMBE NDANI
Pedeshee maarufu Bongo ambaye kwa sasa amemrudia Mungu na kuwa mtu wa ibada, Chief Kiumbe hakuwa nyuma katika eneo la zawadi, alifanya kufuru kwa kumrushia Diamond mabunda ya dola za Kimarekani.

BABU TALE SASA!
Baada ya kufuru ya kurushiwa ‘madolari’, funga kazi ya zawadi ilimaliziwa na meneja wa msanii huyo, Bab Tale aliyepanda jukwaani na kutangaza kuwa uongozi na familia ya mwanamuziki huyo wamemnunulia gari jipya aina ya BMW X6 na kumtaka ampeleke lilipoegeshwa amkabidhi.

WATU WASHUKA UKUMBINI
Kwa kuwa ukumbi huo upo ghorofani, waalikwa wote sambamba na ‘birthday boy’, Dangote au Chibu, walishuka kwa kutumia lifti za jengo hilo kwenda kuliona gari hilo lililokuwa limeegeshwa katika ‘parking’ maalum.
MAMA AKABIDHI
Mbwembwe na mikogo ya kimahaba kati ya Diamond na Wema iliendelea hadi pale mama Diamond, Sandra alipomkabidhi mwanaye huyo funguo za gari hilo, wakazama ndani.

MAHABA MAZITO
Kitendo cha wawili hao kuingia ndani ya gari hilo lenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 90 za Kitanzania na kufunga milango, kilikuwa ni mwanya mzuri kwao kuanza kuoneshana mahaba motomoto ambapo Diamond alimminia mtoto wa kike mabusu ya kumwaga kisha kugandana kama kumbikumbi.

WATUMIA DAKIKA 20
Wapendanao hao walionekana kuzidisha mahaba ambapo walijifungia ndani ya gari hilo kwa zaidi ya dakika 20 na kufanya yao huku watu wapenda ‘ubuyu’ wakiwachungulia kwa dirishani lakini wale waungwana waliamua kutazama pembeni wasione mambo ya chumbani hadharani.
Baada ya kushuka ndani ya gari hilo, wawili hao walikumbatiana tena na kurudi ukumbini ambapo burudani za kula na kunywa ziliendelea.

KUMBUKUMBU MUHIMU
Hivi karibuni ilifanyika bethidei ya Wema ambapo Diamond alimzawadia mpenzi wake huyo gari aina ya Nissan Murano lenye thamani ya Sh. milioni 36 za madafu huku meneja wa wema, Martin Kadinda akimpa BMW ambalo limeibua mjadala juu ya uhalali wa meneja huyo kuwa na uwezo wa kulinunua.

‘Batuli’ Azua Utata wa Aina Yake Kufuatia Kunaswa Akimpiga Busu Mzee Chilo

$
0
0
Stori: Gladness Mallya
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amezua utata wa aina yake kufuatia kunaswa akimpiga busu matata mkongwe, Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’.

Baada ya picha inayowaonyesha wawili hao wakiwa ‘very close’ wakifanya tendo hilo kunaswa na paparazi wetu, paparazi wetu alimtafuta Batuli na kumuuliza kulikoni?

“Aaah wewe acha mambo yako, busu la kawaida hilo bwana hakuna cha ziada, tulikuwa katika sherehe flani hivi Dodoma ndipo nikajikuta tu nimempiga busu,” alisema Batuli.

Tanzania Yang’ara Uzinduzi wa Big Brother Africa, Mtanzania Achaguliwa Kuwa Head Of House

$
0
0
Shindano linalopendwa  na wengi  barani Afrika, maarufu la Big Brother Afrika ambalo kwa mwaka huu ni la msimu wa 9 likijulikana kama Big Brother Hotshot lililoanza usiku wa kuamkia leo Tanzania imeng’ara hasa kwa washiriki wake kufanya vizuri katika muonekano wa awali sambamba na shoo iliyopigwa na mwanamuziki Nasseb Abdul ‘Diamond’ aliyeteka umati uliohudhuria uzinduzi huo.

Halfa hiyo ya masaa mawili ambayo imeweza kushuhudia washiriki  26,  imekuwa  gumzo pale washiriki wanaoiwakilisha Tanzania msimu huu wa 9, Laveda na Idriss wakifanya kweli katika utambulisho wao huku mwanamuziki Diamond akikonga vilivyo na wimbo wake wa ‘My Number One’.

Tanzania imekuwa na bahati ya kipekee kwa mshiriki wake huyo, Laveda ambapo aliteka umati mkubwa kwa kuonesha uhodari wake wa kupuliza “Saxophone”, hali iliyopelekea kupigiwa kura nyingi huku akishangiliwa kwa shangwe muda wote.

Kura hizo alizopigiwa Laveda na kuwa juu ya washiriki wote 26, pia zimemfanya awe Mkuu wa jumba hilo ‘Head of the House’ mpaka hapo itakapoamuliwa na Biggy. Kura alizopigiwa Laveda ni 85.0 huku mshiriki wa Kenya, Sabina akipata kura 78.3, ambaye yeye alionyesha uwezo wake wa kuchekesha kwa kutumia maneno.

Angalia Video zao Hapa Chini:

Tofauti na Ilivyofikiriwa Diamond Aonyesha Live Hadharani Kuwa Anamkubali Shem Wake Petit Man

$
0
0
Stori: Mayasa Mariwata
HESHIMA! Tofauti na ilivyokuwa ikifikiriwa na wengi kwamba hamkubali shemeji yake, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameonyesha kumkubali shemeji yake Ahmed Hashimu ‘Petit Man’ hadharani.

Hivi karibuni uvumi uliibuka kuwa Diamond hakufurahishwa na kitendo cha dada’ke kuolewa na Petit ndipo msanii huyo alipoamua kukata ‘vilimilimi’ kwa kusema uvumi huo hauna ukweli katika sherehe yake ya kuzaliwa iliyofanyika Oktoba 2, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee Tower, Posta jijini Dar.

“Kwa bahati mbaya dada yangu Esma anaumwa hajafika humu ndani, sasa kwa kuwa sasa hivi ameolewa na mtu ninayemkubali, namuita mumewe, shemeji yangu ninayemkubali, Petit Man aje kula keki badala yake,” alisikika Diamond.

Gari Aina ya Rav 4 Inauzwa Kwa Bei Nafuu Kabisa..Changamkia Kabla Halijanunuliwa na Mwingine

$
0
0
 Gari Aina ya Rav 4 Inauzwa Kwa Bei Nafuu Kabisa..Changamkia Kabla Halijanunuliwa na Mwingine..Gari ina Number ya CHY ,,Ipo Dar Es Salamaa na Ina Hali Nzuri Kama Unavyoona Kwenye Picha ....Piga Simu 0658139888



Hatimaye Diamond Ambwaga Davido Kwa Kishindo Kwenye Tuzo za World Music Awards

$
0
0
Diamond Platnumz amewabwaga Davido, Awilo Longomba, Willy Paul Msafi (Kenya) na Eddy Kenzo wa Uganda na kushinda kipengele cha ‘mtumbuizaji bora wa Afrika – Best African Entertainer kwenye tuzo za IRAWMA (International Reggae and World Music Awards).

It always seems impossible until it’s Done!…ningependa kuwataarifu Wadau wangu kwamba #MdogoMdodo ndio nyimbo bora yenye Mahadhi ya Kiafrika na Kijana wenu Diamond ndio M’burudishaji bora wa Mwaka kwenye tunzo hizi za #IRAWMA zilizofanyika nchini Marekani 04|10|2014….. Asanteni sana sana…hakika Umoja ni nguvu, tuhamieni kwenye nyingine sasa,” ameandika msanii huyo kwenye Instagram.

LAANA! Mwanaume Afunga Ndoa na Mama Yake wa Kambo

$
0
0
Mwanamke nchini Ufaransa, juzi amefunga ndoa na mwanae wa kambo baada ya kusuguana na mamlaka za nchini humo kuhusu haki yake ya kuolewa.

Elisabeth Lorentz, 48, amefunga ndoa na Eric Holder, kanisani kwenye kijiji kidogo Dabo huko Alsace-Lorraine, kaskazini mashariki mwa Ufaransa. Ms Lorentz alikutana na baba yake na Holder mwaka 1989, wakati huo akiwa na miaka 24.

Wawili hao walipata mtoto wa kike mwaka 1997 – ambaye ni dada yake na Holder lakini pia mtoto wake wa ubatizo.

Holder pia alikuwa na mtoto kipindi hicho. Ms Lorentz aliolewa na baba yake Holder mwaka 2003, lakini walitengena baada ya miaka mitatu.

Ms Lorentz ameviambia vyombo vya habari kuwa baada ya kuachana na mume wake, mwanae wa kike ambaye alikuwa  na  miaka 9 aliumizwa vibaya na alikuwa akilia kila siku. “Hapo ndipo Eric akawa msaada mkubwa kwetu na uhusiano ulizaliwa,” alisema.

Holder, ambaye anasema alijitahidi kumliwaza dada yake aliyekuwa pia mtoto wake wa kuzaliwa na sasa mwanae wa kambo, alisema: ‘Baada ya baba kumwacha mama, nilihisi kutengwa. Nilijua alivyojisikia.

Haikuchukua muda Holder akaamua kumwomba uchumba mama yake wa kambo. Hata hivyo walikumbana na kikwazo kwakuwa sheria za Ufaransa zinakataza ndoa ya watoto na wazazi wa kambo.

Utekaji wa Watoto Walitikisa jiji la Dar

$
0
0
Lile sakata la utekaji na upoteaji wa watoto ambao wengi ni wanafunzi wa shule za msingi katika Jiji la Dar na kudaiwa linafanywa na watu walio kwenye magari aina ya Toyota Noah limeingia katika sura nyingine.

Safari hii, gari moja lilitupiwa mawe na dereva nusura kuuawa kufuatia kufika katika Shule za Msingi za Kombo na Mtakuja zilizopo Vingunguti, Dar kwa lengo la kuzungumza na walimu kuhusu mikopo lakini likahofiwa lilikwenda kuteka watoto.

Tukio hilo lilijiri Ijumaa iliyopita na kusababisha vurugu kubwa kati ya wazazi na walimu hali iliyowafanya maafande wa Kituo cha Polisi Buguruni kuwasili katika eneo la tukio ili kutuliza ghasia na kwanusuru walimu.

Uwazi lilifika eneo la tukio muda mfupi na kuwakuta walimu wakiwa chini ya ulinzi wa polisi ili wasishambuliwe na wazazi ambao walivamia shule wakidai kwamba watoto watatu walitekwa na watu wenye Noah jeusi.

Vurugu hizo zilizoanza saa nne asubuhi siku hiyo zilitokea baada ya gari moja jeusi aina ya Toyota Noah kufika shuleni hapo na kushambuliwa na wananchi wakidai kwamba ndilo linalotumika kuwatekea watoto wao shuleni hapo.

Mmoja wa wazazi aliyejitambulisha kwa jina la Huma Selemani alisema Noah hilo la mikopo kwa walimu lililokuwa na vioo vyeusi lilihisiwa ni la utekaji baada ya jana yake (Alhamisi) ambapo gari kama hilo lilifika shuleni hapo na dereva kumuuliza mmoja wa wanafunzi sehemu hiyo inaitwaje ambapo mwanafunzi huyo alisema haijui.

Ilidaiwa kuwa, pamoja na denti huyo kusema haijui  sehemu hiyo walimchukua na kumuingiza ndani ya gari hilo ili kuondoka naye lakini mzazi mmoja aliona na kupiga kelele huku akilishambulia kwa mawe gari hilo hadi walipomshusha mwanafunzi huyo na wao kutimka.

Mayowe hayo yaliwafanya wazazi kuvamia shule hizo na kusababisha wanafunzi kutoka madarasani huku wengine wakiruka ukuta na kukimbilia majumbani na baadhi kwenda kusikojulikana.

Wazazi waliokuwa karibu na shule hizo walifika na kuwachukua watoto wao kisha kwenda nyumbani huku wengine wakitegemea msaada toka polisi ambao walipofika walifyatua risasi hewani kuwatawanya wananchi hao.

Hata hivyo, walimu wakuu wa shule hizo hawakupatikana mara moja lakini mwalimu mmoja ambaye hakupenda jina lake liandikwe  alisema hakuna utekaji wa watoto shuleni bali baadhi ya watu wamekuwa wakivumisha habari hizo na hivyo kuwatia hofu watoto.

Baadhi ya watu walioongea na Uwazi walisema kuwa, wana taarifa mbaya kwamba watekaji hao wakishawapata watoto huenda kuwaua ili kutwaa viungo vyao kwa ajili ya ushirikina wa kupata utajiri.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kombo, Jastin John Chiganga alipohojiwa alikiri kutokea kwa vurugu hizo hali iliyomfanya awaite polisi kutuliza ghasia lakini alisema kwa upande wa kutekwa watoto na gari aina ya Noah hajawahi kusikia.

“Shule ilibidi ifungwe, watoto waruhusiwe kutawanyika hadi hapo taarifa itakapotolewa. Hata hivyo, wazazi wameniomba kwamba kabla watoto wao hawajarejea shuleni hapo anatakiwa kiongozi wa juu, awe DC (mkuu wa wilaya) au yeyote afike kutoa tamko na kuweka mambo ili kuwatoa hofu wazazi na wanafunzi,” alisema mwenyekiti huyo.

Polisi wa Buguruni waliokuwepo kwenye tukio hilo walisema hawana taarifa ya watu waliojeruhiwa au  kukamatwa bali zoezi la kudhibiti amani lilifanyika kwa uangalifu wa hali ya juu.

Wakati huohuo, wazazi wa mwanafunzi Hadija Hansi (10) anayesoma darasa la nne Shule ya Msingi Magomeni, Dar wanahaha kumtafuta mtoto wao huyo ambaye alitoweka katika mazingira ya kutatanisha ikidaiwa alitekwa na Noah.

Akizungumza na Uwazi  wiki iliyopita, Zena Amour ambaye ni mama mzazi wa mtoto huyo alisema mwanaye alipotea katika mazingira ya kutatanisha Septemba 30, mwaka huu wakati akicheza na wenzake na ameshamtafuta katika vituo vya polisi jijini kikiwemo cha Tandale TAND/RB/1059/2014 na hospitali zote bila mafanikio.

Mama Amkata Mwanaye Paja Na Kuchoma mshikaki Kipande cha Nyama

$
0
0
Mwanamke mmoja Kilimanjaro amekamatwa na polisi akidaiwa kumkata mtoto wake mwenye umri wa miaka nane nyama ya paja na kuichoma mithili ya mshikaki.
Mwananmke huyo aliyetajwa kwa jina la Dafrosa Massawe anadaiwa kufanya unyama huo mwishoni mwa wiki na majirani wanasema mama huyo alifanya hivyo akiwa amelewa.
Kamanda wa Polisi Kilimanjaro Koka Moita alisema mwanamke huyo ataendelea kushikiliwa hadi uchunguzi wa tuhuma hizo utakapokamilika kabla ya kupelekwa mahakamani.
Akizungumza na Gazeti la MWANANCHI katika hospitali ya Kibosho mtoto huyo alisema hafahamu kosa alilofanya hadi mama yake ambaye ni mtengenezaji wa pombe za kienyeji kumfanyia kitendo hicho.
Alisema mama yake alirudi nyumbani usiku na kumkuta amekaa na kumsalimia kisha akamwomba chakula wakati akijua hakuna na baadae aliingia jikoni na kuchukua kisu kisha kumkata nyama kwenye paja lake baada ya kumwambia alishinda na njaa siku nzima.
Alisema baada ya kuikata aliichoma kama mshikaki na ilipoanza kufuka moshi na kutoa harufu aliitoa jikoni na kumwekea mtoto huyo puani ili avute harufu yake.

Wanaume Wafupi Ndio Waume Bora Kabisa Ndoa zao Zinadumu Kuliko Wale Warefu

$
0
0
Wanaume ambao ni wafupi kwa kimo mara nyingi wanasifika kuwa waume bora kuliko wanaume warefu.
Pia inaarifiwa huwa na busara zaidi kufidia kimo chao, amekiri Adam Gopnik, mwanamme mmoja wenye umbo dogo.
Wiki kadhaa zilizopita, wana soshologia wawili kutoka Chuo Kikuu cha New York, walichapisha waraka mrefu ulioangalizia maisha ya watu wafupi.
Utafiti wao ulizua mjadala mkali kutoka kwa kile kinachoweza kusemekana kuwa jamii ya wanaume wenye kimo kifupi.
Waandishi wa waraka huo wa maswala ya kijamii unaashiria kwamba wanaume wenye haiba ya kuvutia mara nyingi hupendelewa katika maisha yao hivyo wanaripotiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na zaidi ya mpenzi mmoja.
Hata hivyo, hitimisho la waraka huo, pindi mtu anapoupitia, unashangaza. Ni kwamba, watu wafupi wana ndoa za kudumu zaidi.

nafanya hayo, katika mazingira magumu wakiwa katika umri tofauti na kipato tofauti, na wanayafanya hayo wakiwa na wanawake wafupi ambao wanawaoa, na wakati mwengine na hata wanawake warefu wanaokutana nao.
Wanaume wafupi wanaoa kuchelewa, lakini pindi wanapooa, wanadumu katika ndoa kwa muda mrefu, na kwa kiwango cha sayansi ya kijamii, angalau wanakuwa na furaha.
Kuna sababu zinazoonyesha kwa nini wanaume wafupi wanadumu kwenye ndoa.
Nazo ni, wanaume wafupi wanaonyesha kukata tamaa. Wanaume wafupi wanaishi katika ulimwengu wa wanaume warefu na wanajua kila fursa inayopatikana, ni bora kuidhibiti.

Hali ya kukata tamaa ndio inayowafanya wanaume wafupi kuwa wanaume bora kwa wake zao. Watafiti hao pia walisema kuwa wanaume wafupi hukimbilia kufanya kila kitu kuwafurahisha wapendwa wao wakati wanume warefu hilo halliwajalishi.
Moja wapo ya ufumbuzi wa ripoti hiyo pia ni kwamba wanaume wafupi wanafanya kazi chache za nyumbani wanapokuwa kwenye ndoa kuliko wanaume warefu, ingawa utafiti pia unaonyesha kwa wanaume wenye kimo kirefu, aina ya kazi zao za nyumbani inatofautiana.
Kwa maana nyengine, wanaume wafupi hawafiki juu ya makabati. Wanaume wafupi hawadumu kwenye ndoa kwa sababu ya kutaka kuridhisha, bali wanadumu kwenye ndoa kwa sababu wanataka kuonekana.
Utafitio huu kama ulivyosoma hapo awali umeua mjadala mkali lakini pindi mtu anaposoma utafiti wao kinachojitokeza zaidi ni kuwa wanaume wafupi wanakuwa na ndoa za kudumu.
Hii ni licha ya mazingira magumu wanayokabiliwa nayo katika ndoa zao na hufanya hivyo na wake wafupi waliowaoa lakini pia na wanawake warefu wanaokuwa wamewaoa.

Utafiti huo unahitimika kwa kusema wanaume wafupi hawana kasi ya kuoa lakini wanapooa wao hudumu katika ndoa zao.

Mungu Mkubwa Wale Watoto Pacha Waliotenganishwa India Sasa Waanza Kutembea

$
0
0
Hali za watoto pacha waliozaliwa wakiwa wameungana, Eliud na Elikana wenye mwaka mmoja na miezi sita, zinazidi kuimarika tangu walipofanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya Julai mwaka huu.

Watoto hao, ambao mwaka jana walifanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha India, walilazwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya kufanyiwa matibabu ya marekebisho madogo ya kuziba njia za kutolea haja kubwa na kuwekewa njia ya kudumu.

Hata hivyo, kabla ya kufikishwa hospitalini hapo, Eliud alifanyiwa upasuaji wa aina hiyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dar es Salaam na alipopelekwa Mbeya alifanyiwa tena marekebisho.

Upasuaji huo ulifanywa na Daktari Bingwa wa Upasuaji, Kitengo cha watoto Muhimbili, Dk Zaituni Bokhary.

Wakizungumza nyumbani kwao katika Kijiji cha Kusumulu, Kyela juzi, wazazi wa watoto hao walisema afya za pacha hao zinaendelea kuimarika siku hadi siku, kwa kuwa vidonda vyao vimepona na wana furaha muda wote.

“Kwa kweli tunamshukuru Mungu, kama unavyowaona maendeleo yao ni mazuri, sasa Elikana ameanza kutembea kabisa na huyu mwenzake Eliud, bado ila ameanza kutambaa na hata uzito wanaongezeka.

“Elikana ameongezeka hadi kufikia kilo 13 kutoka kilo 10 alizokuwa nazo Agosti mwaka huu na Eliud amefikisha uzito wa kilo tisa kutoka kilo saba,” alisema mama yao mzazi, Grace.

Alisema kutokana na kuendelea vizuri kwa watoto wake, wanasubiri muda ufike wa kufanyiwa tena upasuaji mdogo wa njia ya mkojo.

Alisema waliambiwa na Dk Bokhary kwamba Mei mwakani watatakiwa kurudi India ili wakafanyiwe upasuaji tena.

“Wakati ule tukiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya, Dk Zaituni alituambia kwamba Desemba atarejea kutoka masomoni na Mei mwakani watatakiwa kwenda India kufanyiwa upasuaji wa njia ya mkojo na kuwekewa ya kudumu, hivyo tunamsikiliza yeye,” alisema.

Baba mzazi wa watoto hao, Erick Mwakyusa alisema wanaye wanamletea faraja kubwa kwani hata ile tabia ya kuchagua chakula walivyokuwa nayo awali, hawana tena na badala yake wanakula chakula chochote wanachopewa.

“Kutokana na uchumi wetu kutokuwa mzuri sana, hata chakula wanakula kile tunachokuwa tumepika siku hiyo na kwa bahati nzuri hata wao hawasumbui kama ilivyokuwa awali japo daktari wao alituhimiza zaidi kuwapatia maziwa na sisi tumekuwa tukifanya hivyo mara kwa mara,” alisema.

Aliishukuru Kampuni ya Mwananchi Communications Limited kwa kuwa karibu na familia yake kwa kipindi chote huku akibainisha kwamba imekuwa msaada mkubwa wa kufanikisha matibabu ya watoto wake.


“Bila ya ninyi waandishi wa Mwananchi, sijui hali yangu na watoto wangu ingekuwaje, msaada wenu ndiyo umenifanya niweze kukabiliana na hali halisi kwani ndiyo umenifanya nipate pikipiki ambayo kwa sasa ndiyo mkombozi wa familia yangu,” alisema.

Jaji Warioba: Siendi Ng'o Dodoma Kwenye Makabidhiano ya Katiba

$
0
0
Wakati Katiba inayopendekezwa ikikabidhiwa kesho kwa Rais Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema hata akialikwa katika sherehe hizo hatahudhuria kutokana na majukumu aliyonayo kwa sasa.

Jaji Warioba alisema angependa kuhudhuria sherehe hiyo ambayo pia itahudhuriwa na wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, wakuu wa mikoa, mabalozi na wageni mbalimbali, lakini kutokana na dharura aliyoipata haitawezekana.

Sherehe hiyo itafanyika mkoani Dodoma kesho na Mwenyekiti wa lililokuwa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta atakabidhi nakala ya Katiba inayopendekezwa kwa Rais Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein.

Katika hafla hiyo itakayofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, wajumbe wa Bunge hilo walioshiriki mchakato huo kuanzia mwanzo mpaka mwisho watapewa vyeti.

Breaking News: Halima Mdee na Wenzake Wapelekwa Segerea

$
0
0
Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee na wenzake tisa wamepelekwa katika Gereza la Segerea jijini Dar baada ya kushindwa kutimiza baadhi ya masharti ya dhamana yao.

Mdee na wenzake nane mapema leo walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar na kukana tuhuma zinazowakabili.

Mdee na wenzake hao wanashitakiwa kwa makosa mawili kototii amri za maofisa wa polisi na kufanya maandamano kinyume na sheria Jumamosi iliyopita ya Oktoba 4, mwaka huu.

Watapandishwa tena kizimbani hapo kesho saa 4 asubuhi.

(Habari na Deogratius Mongela/GPL)

Instagram Party Tanzania Tour 2014 Mwanza Waandika Historia Watu 5,000 Wajitokeza Jembe ni Jembe

$
0
0

Instagram Party Tanzania Tour 2014 juzi imeweka historia mpya ya Sherehe hizo zilizoanza mjini Dar Miezi 2 iliyopita baada ya watu Elfu Tano kufurika Ukumbi wa Jembeni Jembe wa Mjini Mwanza kusherehekea Sherehe hizo ambazo kwa mara ya kwanza zimetoka nje ya mkoa wa Dar kuanza na Mwanza juzi. Wakurugenzi wote 4 wa Instagram Party Tanzania Freddy + Gillsant + Bikira wa Kisukuma na Le Big Show wote walikuwepo kwenye sherehe hizo ambazo zilitumbuizwa na Ben Paul, Shilole, Jokate, pamoja na Wabiro. Sasa sherehe hizo zitakazozunguka Tanzania nzima zinahamia Mbeya. - Le Mutuz

Diamond ni Zawadi Kutoka kwa Mungu Kwa Watanzania..Ushahidi Huu Hapa

$
0
0
Jana nilijihakikishia jinsi gani Diamond yupo katika level yake ya kipekee huko juu....unajua ilikuwaje??

kwenye tamasha la fiesta la Dodoma ilipigwa nyimbo ya mdogomdogo bila Diamond kuwepo na ilipata shangwe zaidi ya wanamuziki wote waliokuwa wakipeform..

Zaidi hata ya Ally Kiba ambaye wanafki wachache wanafanya makusudi kumlinganisha na Diamiond...hebu fikiria mtu hayupo ila anakufunika je angekuwepo???!! ………………

Diamond ni zawadi kutoka kwa Mungu kama unampenda ally kiba, barnaba na wengineo poa tu lakini tambua Diamond yupo kule juu anawaangalia wale waliopo chini.

Eric Shigongo Hakusoma Sekondari Kabisa ila ni Moto wa Kuotea Mbali

$
0
0
Jamaa amekuwa inspirational kwa rika tofauti,mjasiriamali mwenye mafanikio ila historia ya elimu yake yakushangaza sana alifeli darasa la saba mara mbili na ajasoma secondary kabisa ila ni mwandishi wa hadithi na vitabu mzuri kabisa na Anajua Kingereza Vizuri, Kingereza Alijifunza Ukubwani baada ya Kuona Kina manufaa katika Biashara zake ..Kwa Walio Angalio Kipindi cha  Profesa Shaka Ssali wa VOA katika kipindi straight talk of Africa walishudia alivyofit ....Jamani kukosa Elimu isiwe Kikwazo ,U can still do mambo Makubwa Tusikate Tamaa

Viewing all 104712 articles
Browse latest View live




Latest Images